Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Shamba la Mahindi la Mh. Pinda lawavutia Wengi Mkoani Katavi

$
0
0
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda wakimuonyenyesha Mh. Dr Christian Mzindakaya shamba lao la mahindi lililopo katika kijiji cha kibaoni Mkoani Katavi,Wakati waliotembelea Shamba hilo.nyuma ya Mh. Mzindakaya ni mke wake,Mama Theresia Mzindakaya ambao walimtembelea Waziri Mkuu kijiji kwake kibaoni
Dr Christiani Mzindakaya akiangalia mahindi katika shamba la Waziri Mkuu na mahindi lililopo katika kijiji cha kibaoni Mkoani Katavi,Wakati waliotembelea Shamba hilo.Picha na Chris Mfinanga.

Michuzi Blog Exclusive: Mashua yazama jirani ya kisiwa cha chumbe leo

$
0
0
 Baadhi watu waliokuwemo kwenye mashua hiyo wakijaribu kutafuta uelekeo mara baada ya mashua hiyo kuanza kuzama kwa sababu ambazo bado hazijajulikana. Bahati njema  baadae abiria wote waliokolewa na boti. Ajali hiyo imetokea  leo jioni  maeneo ya Kisiwa cha Chumbe, kati ya Dar es salaam na Unguja ambako Globu ya Jamii ilipita na kukutana na ajali hii ambayo hadi tunaruka hewani hakukuwa na habari ya mtu aliyepoteza maisha.
  Baadhi ya abiria katika mashua hiyo wakiokolewa  baada ya mashua yao kupoteza muelekeo. Kwa habari zaidi tuvute subira kidogo. Tutawaletea taarifa kamili itakapopatikana

Jaji Warioba: Rais hakusema jipya kuhusu Katiba

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,Jaji Joseph Warioba (katikati) akiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume, Mbaraka Saleh, Ahmed Saadat na Kailima Kombwey.

Wapeleka watoto madrassa badala ya Shule kukwepa Rushwa ya Mkuu wa Shule Wilayani Mkuranga

$
0
0
Mkazi wa Kimanzichana Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Rajabu Juma Mkumba, akimuuliza maswali mbunge wa jimbo hilo Adam Malima (hayupo pichani) kuhusu kulipishwa mchango wa Shilingi elfu Ishirini ili kumuanzisha shule mtoto wa darasa la kwanza. Huku wakimtupia lawama mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kimanzichana kusini. Ambapo pia alimpa taarifa mbunge huyo kuwa wanawapeleka watotowao madrassa kwasababu adayao ni ndogo ukilinganisha na shule hiyo.
Mzee Said Hemedi Lihaku akimuuliza maswali Mbunge wa mkuranga kuhusu matibabu ya bure kwa wazee wenye umri wa miaka zaidi ya 60 kuwa wanaambiwa ni bure lakini mbona wanalipishwa wanapokwenda hospitali.
Wakazi wa Kimanzichana wakifurahi wakati mbunge wao alipokuwa akiulizwa maswali ya kumuudhi na na kusababisha kuzungumza kwa ukali kwenye mkutano huo.

KATIKA  hali isiyo ya kawaida mkazi mmoja wa kijiji cha Kimanzichana Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani Rajabu Juma Mkumba, amesema wananchi wa kijiji hicho wameacha kuwapeleka shule watoto wao na badalayake wanawapeleka  madrasa kutokana na gharama za madrassa hizo kuwa za bei ya chini kuliko Shule.
Akimuuliza swali mbunge wa jimbo hilo la Mkuranga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Adam Malima, alisema wanashangazwa na kitendo wanachofanyiwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kimanzichana Kusini cha kuwalipisha ada ya Shilingi Ishirini Elfu kwa motto mmoja anaetaka kuanza darasa la kwanza.
“Mheshimiwa mbunge Mkuu huyu wa shule anatoa wapi sharia ya kutuchangisha shilingi elfu ishirini (20,000) kwa kila mwanafunzi anaeanza darasa la kwanza? Wakazi wa hapa wengi wanaona bora watotowao wawapeleke madrassa kule kwasababu adayake ni ndogo,” Alihoji Mkumba.   
Lakini katika hali ya kushangaza mbunge huyo aligeuka mbogo na kuanza kuwafokea wananchi hao na kuwaambia hayo wamejitakia wenyewe kutokana na kutofanya juhudi ya kujenga shule nyingine kwani alishawaambia miaka miwili iliyopita kuwa watafute kiwanja ili ijengwe shule kwakua wao wanaongezeka sana.
“Nakumbuka miaka miwili iliyopita niliwaambia kwenye mkutano hapahapa kwamba kasi yetu ya kuongezeka  ni kubwa mno hivyo tujitahidi kutafuta kiwanja mapema ili tuwe na shule nyingine lakini hadi leohakuna kilichofanyika,” Alisema Malima.
Aidha mbunge huyo aliwaambia wananchi hao kama wanania ya kweli ya kutaka kutatua baadhi ya matatizo yao inawabidi wafanye ushirikiano wa dhati kwani wenzao wa kijiji Cha Mwalusembe walishirikiana nay eye wakaweza kujenga madarasa manne kwa siku 45 lakini kijiji hicho kinamiaka miwili hakijajenga hata darasa moja.
 
Mkutano huo ulikuwa ni wa ufunguzi wa kampeni ya uhamasishaji wa kujiunga kwenye mfuko wa afya ya jamii kwa wananchi kwenye Wilaya hiyo, ambapo wananchi wengi walionekana kuwa na maswali mengi yaliyokuwa nnje ya mada na maudhui ya mkutano huo hali iliyopandisha hasira za mbunge huyo na kuahidi atakwenda tena tarehe 17 mwezi huu kukutananao.

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0
Ngoma ya 'Asha' ya Tabora Jazz band miaka ya 70 ilikuwa haina mshindani

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

$
0
0
Ngoma ya 'Gere' ya The Kilimanjaro Band "Wana Njenje" si ya mchezo. Ikipigwa lazima utamuonea gere bibie Nyota akiwa Jukwaani, hasa anapoita kabila moja moja kuonesha umahiri wake wa kunanihiii kiuno

IN EVERLASTING MEMORY OF OUR BELOVED FATHER

$
0
0
LATE ROGATIAN M. SHIRIMA

DADDY WE MOURN AND GRIEF YOUR PASSING AWAY THREE YEARS AGO.

HOWEVER THE IDEAS, VALUES AND MORALS YOU LIVED FOR AND THE LEGACY YOU LEFT BEHIND WILL LIVE MANY YEARS TO COME THAN YOUR LIVES.

WE CHERISH YOUR GREAT LIVES WHILE THANKING GOD ALMIGHTY FOR THE GIFT OF YOUR LIVES ON US. YOU MADE US THE PERSONS WE ARE TODAY AND WE ARE PROUD OF YOU.

WE HUMBLYPRAY GOD TO REST YOUR SOULS IN ETERNAL PEACE TILL THAT DAY WHEN WE MEET AGAIN.

YOU ARE ALWAYS MISSED AND REMEMBERED BY YOUR LOVING WIFE FUDASIA, CHILDREN, INLAWS, GRAND CHILDREN, RELATIVES AND FRIENDS.

RAIS KIKWETE AWASILI SINGIDA KWA ZIARA YA KIKAZI


Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Mkoa wa Singida

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumia laptop yake kuwaonyesha viongozi mbali mbali wa Mkoa wa Singida masuala muhimu ya maendeleo nchini,wakati alipowasili mkoani humo jana Januari 5 kwa Ziara ya kikazi ya Siku Mbili.Picha na IKULU

MAPACHA WATATU KUFUNGUA MWAKA IJUMAA JANUARI 11

$
0
0
BENDI YA MAPACHA WATATU.(WAKALI WA TOWN) 
WANASHUKA NA ONESHO KABAMBEE LA FUNGUA MWAKA, NDANI YA  NEW MSASANI CLUB. IJUMAA HII YA TAREHE 11 MWEZI HUU JANUARI ,WAKISINDIKIZWA NA NYOTA WAZIRI NAKUNDI ZIMA LA MASHAUZI CLASSIC WATAKAOONGOZWA NA
 ISHA MASHAUZI
HAKIKA SI YAKUKOSA NI KWA KIINGILIO CHA ALFU 5,000 TU MLANGONI NA 15,000 KWA WATAOPENDA KAA VIP NA KUTRITIWA KVIP
KUBOOK MEZA YAKO PIGA NAMBA 
0713 701051, 0767 701051, 0786 701051 
....ULETEWE TIKETI
meza chacheee
2013 NI MWENDO WA BENDI....TUUENZI MUZIKI WETU... NJOO TUANZE NA
 MAPACHA WATATU.....WAKALI WA TOWN!!

Mtoto Samwel Mlope anahitaji msaada wa Matibabu

$
0
0
MTOTO SAMWEL MLOPE

Unaweza kujiuliza ni nini ambacho kimetokeza katika mgongo wa mtoto huyu?.Mtoto Samwel Mlope mwenye umri wa miaka kumi na moja(11) ambaye ni mkazi wa Mahenge ndani ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.Mtoto huyu alianza kuumwa mwaka 2001 ambapo alianza kusumbuliwa na tatizo la moyo kuwa na tundu.

Kwa mara ya kwanza kabisa alipoanza kusumbuliwa na tatizo hili mama yake mzazi ambaye ni Bi. Amina Ally alimpeleka katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma na baadae akaambiwa ampeleke mtoto huyo katika hospital ya Taifa Muhimbili na baada ya kufika muhumbili ndipo alipoambiwa kuwa mtoto Samwel anasumbuliwa na tatizo la kuwa na tundu kwenye moyo wake.
Afya ya mtoto Samwel wala hairidhishi kabisa,hali iliyompelekea kushidwa kabisa hata kupata masomo.
Na huyu ndiye mama mzazi wa mtoto Samwel Mrope,Bi. Amina Ally ambaye anajishughulisha na kazi za ndani ili aweze kujipatia pesa kwa ajili ya kujikimu kimaisha yeye pamoja na mwanae samwel. Alisema kuwa "baba wa mtoto Samwel aliondoka muda mrefu sana uliopita kuelekea machimbo kwa ajili ya kutafuta na mpaka hii leo hajarudi na hawafahamu yupo wapi.

Bi. Amina alisema kuwa "ninawaomba watanzania wote kwa ujumla waweze kunisaidia ili mwanangu Samwel aweze kupelekwa nchini India na kupata matibabu kwani mwanangu anapata shida sana"na hatimaye aliweza kuzitoa namba zake za simu kwa watu ambao watajitokeza kutoa msaada kwa mtoto Samwel ambazo ni 0752 732290.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWAJULIA HALI MAJARANI ZAKE KIJIJINI KWAO KIBAONI

$
0
0
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiwa katika mazungumzo majirani zake,Mzee Bernard Malyatabu Mayala (88) akiwa na mkewe Bi. Bernadetha Kabandime Msuluba (79) wakati alipowatembelea na kuwajualia hali na kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2013 kijijini kwao Kibaoni Mkoani Katavi.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda anaonekana akiulizia bei ya nyama ya mbuzi wakati akiwa katika kijiji cha Kibaoni,Mkoani Katavi.Picha na Chris Mfinanga.

TWANGA PEPETA FC YAIKACHA KIJITONYAMA VETERANS FC LEADERS LEO

$
0
0
 Kipa wa timu ya Kijitonyama Veterans, Abdallah Omary (kulia) akiokoa moja ya hatari iliyoelekezwa langoni kwake, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye uwanja wa Leaders Club Kinondoni, ikiwa ni badala ya mchezo kati ya Twanga Pepeta Fc na Kijitonyama, baada ya Twanga Pepeta kuingia mitini bila kutokea uwanjani hapo, leo.
 Kipute hicho kikiendelea...
 Mapacha Frki, Hamza na Kondo wakipozi kwa picha.
Kiungo mchezeshaji wa Kijitonyama Veterans, Isihaka Mussa, akiambaa na mpira wakati mchezo huo.Picha na  Sufiani Mafoto Blog.

Wafanyakazi wa Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania (TCAA) yasherehekea family day jijini dar

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),Charles Chacha (kulia) akimkabidhi kikombe cha ushindi kepteni wa timu ya Kombaini ya Makao Makuu ya TCAA,Maria Mamba ambaye ni mwanasheria wa mamalaka hiyo wakati wa familly day iliyofanyika Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA.),Charles Chacha (kushoto) akikabidhiwa zawadi na Kaimu Mkurugeni wa udhibiti wa usafiri wa anga Tanzania (TCAA),Makhiid Towillo. wakati wa familly day ILIYOWASHIRIKISHA WAFANYAKAZI WA TCAA.
Mshambuliaji wa timu ya JNIA ya wafanyakazi wa Mamkalaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Juma Hamis akifunga goli kwa njia ya Tiktaka.timu hiyo iliwafunga 2-0 Timu ya Makao Makuu ya TCAA.Wakati wa familly day iliyofanyika Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam leo.
Matilida Temba (kulia) ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Judo Tanzania akipambana na Richard Ndayulukiye ambaye ni mfanyakazi wa TCAA ikiwa ni sehemu ya shamra shamara za Familly day ya Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania.

Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania wakiwa katika hafla hiyo ya Familly day.
Watoto wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), walioshiriki katika Famillya Day wakishindana kukimbia na magunia wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika Kunduchi Beach,Jijinii Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi waTCAA wakicheza mpira wa mikono vollyball wakati wa Sherehe ya familly day iliyofanyika Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Wakishindana kuvuta kamba wakati wa sherehe ya familly day iliyofanyika Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA UCHIMBAJI MADINI WILAYANI SAME MKOA KILIMANJARO

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais,Sazi Salula akizungumza na Mkurugenzi wa Baraza la hifadhi na Usimamizi wa Mazingira {NEMC] Eng Benventure Baya na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makmu wa Rais Dk Julias Ningu na Ofisa Mwandamizi Bw Timotheo Mande mara baada ya kutembelea Uchimbaji wa Madini ya Bauxite yanayochimbwa kwenye kijiji cha Marieni Wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akionyeshwa-ex rey Mashine kwa ajili ya kupimia Bauxite na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kuchimba Madini ya bauxite ya kutengeneza Saruji Eng.Alumbwage Mhagama Katibu mkuu wakati alipofanya Ziara ya kikazi nakuona hali ya Mazingira kwenye Kijiji cha Marieni wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro,
  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akizungumza na wanakijiji cha Marieni Wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro alipokwenda kukagua Shughuli za Uchafudhi wa  Mazingira katika kjijihicho jana. 
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akiangalia Maadini Bauxite yanayochimbwa na kampuni ya Willy Enterprises alipokwenda kuangalia hali ya Uchafuzi wa Mazingira katika Kijiji cha Marieni Wilayani Same Mkoa waKilimanjaro.Picha na Ali Meja.

DKT. SHEIN AZINDUA BOHARI YA DAWA ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifungua rasmini Bohari ya dawa iliopo maruhubi mjini Unguja ikiwa ni shamra shamra ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akimuuliza swali msambazaji dawa na vifaa tiba Bi Husna Maulid huko katika Bohari kuu ya madawa maruhubi mjini Unguja ikiwa ni shamra shamra ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Hii ni moja ya sehemu ya ndani ya Bohari la dawa lililopo  maruhubi mjini Unguja lililozinduliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.
 Hili Ndio Bohari la madawa lililopo maruhubi mjini Unguja lililozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein . 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake ya uzinduzi wa Bohari la Madawa lililopo maruhubi mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mfamasia mkuu wa kwaza baada mapinduzi huko katika Bohari la madawa lililopo maruhubi mjini Zanzibar.Picha zote na Makame Mshenga - Maelezo Zanzibar.

MWANANCHI FC NA MICOVILLA FC NGOMA DROO ZATOKA SARE YA 2-2

$
0
0
 Beki wa Mwananchi Fc, Muhidin Sufiani 'Sufianimafoto'(kulia) akimtoka mchezaji wa Micovilla, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama Dar es Salaam leo asubuhi. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare kwa kufungana mabao 2-2.
 Beki wa Mwananchi Masua Mgumu (nyuma) akimdhibiti mchezaji wa Micovilla, wakati wa mchezo huo.
 Abdallah Masoud wa Mwananchi (mbele) akimhadaa beki wa Micovilla, wakati wa mchezo huo.
Nahodha wa Mwananchi, Majuto Omary akichuana na beki wa Micovilla kuwania mpira wakati wa mcheo huo.

RAIS AHUDHURIA SHEREHE ZA KUSIMIKWA WAKFU ASKOFU DKT ALEX SEIF MKUMBO WA KKKT DAYOSISI YA KATI, AANZA ZIARA YA SIKU NNE YA MKOA WA TABORA

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Kanisa la KKKT baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo (mwenye fimbo) pamoja na viongozi wa kanisa hilo wakiongozwa na Askofu Mkuu Dkt Alex Gehaz Malasusa (kulia kwa Rais), Msaidizi mpya wa Dayosisi hiyo Mchungaji Syprian Yohana Hilinti (wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Kone na viongozi wengine katika sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na  kiongozi wa kanisa la KKKT nchini  Dkt Alex Gehaz Malasusa baada ya kupokea kamba kama ishara ya kupokea zawadi ya ngombe toka kwa Dayosisi  hiyo huku  Askofu  mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo akishuhudia  katika sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipkea ripoti ya mkoa wa Tabora toka kwa Mkuu wa Mkoa Mhe Fatma Mwassa huo aliyosomewa mara baada ya kuwasili kuanza ziara ya kikazi ya siku nne
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na kiongozi wa kanisa la KKKT nchini  Dkt Alex Gehaz Malasusa na  Askofu  mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida leo Januari 6, 2013.PICHA NA IKULU

Article 4

MEYA WA KINONDONI,MH. YUSUF MWENDA AZINDUA UJENZI BARABARA YA MAKOKA,KATA YA MAKUBURI

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh. Yusuf Mwenda (mwenye shati la kitenge) hivi karibuni alifanya ziara katika Kata ya Makuburi,jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Makoka yenye urefu wa Kilometa 3.7. Barabara hiyo inajengwa na Manispaa hiyo kwa gharama ya shilingi milioni 300. Pichani ni sehemu ya ziara hiyo akiwa na viongozi mbalimbali wa Serijkali za Mitaa, Madiwani na Wahandisi wakikagua sehemu mbalimbali za barabara hiyo inayotarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni na Kampuni ya ukandarasi ya Gwema Decorator Co. Limited

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akimuuliza kijana aliekuwa akiuza nyama ya kuchoma aliekuwepo kwenye Kata hiyo ya Makuburi wakati alipokuwa katika ziara ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Makoka yenye urefu wa Kilometa 3.7 hivi karibuni.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kulia) akizungumza na Mmoja wa Waendesha boda boda aliekuwepo kwenye moja ya vituo vyao katika Kata ya Makuburi wakati alipokuwa katika ziara ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Makoka yenye urefu wa Kilometa 3.7 hivi karibuni.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kulia) akipewa maelezo na Diwani wa Kata ya Makuburi, William Mwangwa (kushoto) kuhusu ujenzi wa Barabara ya Makoka yenye urefu wa Kilometa 3.7 kwa gharama ya Sh milioni 300 wakati alipofanya ziara katika barabara hiyo, Dar es Salaam jana. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Abbas Tarimba (wa pili kushoto) na Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Gerald Urio. (Picha na Fadhili Akida).
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images