Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

Hivi ndivyo ilivyokuwa Safari ya Mwisho ya Marehemu Sajuki


SERENGETI FREIGHT YAIFYAGILIA KWA BODI YA UTALII TANZANIA

$
0
0

Salaam.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza bodi ya utalii kwa juhudi za hali ya juu walizozifanya kuitangaza nchi yetu kwenye ramani ya utralii duniani.
Mwaka jana mwezi November kulikuwa na maosnyesho ya kitalii ya dunia yaliyofanyika hapa UK na banda la Tanzania ndio lililovutia kuliko mabanda yote mia mbili yaliyokuwepo hapo kutoka nchi ozote duniani Kama unavyoona Tanzania ilifunika na sisi kama jina letu lilivyo la kizalendo(Serengeti) tulikuwa very proud na nchi yetu.

Kwa kuwaunga mkono, kampuni yetu itatengeneza vipeperushi(flyers ) ambavyo vitakuwa na matangazo ya vuvutio vya utalii wa tanzania na kuvisambaza UK yote, pia tutaangalia uwezekano wa kurusha haya matangazo kwenye television na redio za huku UK.
Haya tutayafanya kizalendo kama mchango wetu katika kuitangaza nchi yetu

Regards
CHRIS LUKOSI
DIRECTOR

HOJA YA HAJA YA MBUNGE WA KILWA KASKAZINI KUHUSU GESI ASILIA

$
0
0

Sekta ya gesi na mafuta ni moja kati ya sekta kubwa na ngeni kwa kiasi fulani hapa nchini.
Kwa kipindi cha miaka mingi na haswa miaka ya sabini na themanini Serikali ya awamu ya kwanza ilifanya kazi kubwa ya uwekezaji katika utafiti wa mafuta na gesi nchini  lakini bila ya mafanikio ya uwekezaji.

Hii inaweza kuwa ilichangiwa sana na siasa zilizokuwapo kwa wakati ule kwa maana ya umagharibi na umashariki na pengine imani ya wawekezaji kutokana na msimamo tuliokuwa nao kama nchi  katika suala la ukombozi wa bara la afrika dhidi ya ukoloni pia uduni wa hali ya teknologia ya wakati ule na ukweli kwamba eneo letu la nchi za mashariki mwa Afrika ilijulikana kuwa ni ukanda wa gesi asilia tu  na enzi zile gesi asilia ilikuwa haina thamani kuliko mafuta.

Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni , nchi yetu imefanikiwa sana kuwavuta wawekezaji katika sekta na nyanja tofauti  sana ikiwamo katika gesi na utafiti wa mafuta. Hii ni nafasi nzuri tuliyoikosa kwa miaka mingi kiasi cha kutuweka nyuma kimaendeleo ukilinganisha na nchi nyingi za afrika na dunia ya tatu.

Lakini sasa kiasi kikubwa tumeanza kuona manufaa ya uwekezaji ule japo kwa uchache na changamoto nyingi ndani yake.

Tumeanza mwaka 2012 na kumaliza na mfululizo wa matukio ya aina tofauti kwa waandishi kuandika makala na habari nyingi kuhusu shughuli na sekta nzima ya gesi nchini ,na mara ya mwisho kabisa kufuatia maandamano ya wanachi wa Mtwara ambao walitokea katika vyama  tofauti.

Sikuona tatizo la waandamanaji wale pamoja na ujumbe ulitolewa bali baadhi ya ujumbe  unaonyesha zipo tafsiri nyingi zaidi ya madai ya mahitajio ya manufaa ya mapato katika uwekezaji wa gesi na bomba la gesi.

Nilipata wasisiwasi mkubwa sana baada ya kuona wanaojua ukweli wa jinsi mambo yalivyo na wale wasiojua kuamua kwa dhati kabisa kuupotosha umma wa watanzania  na dunia kwa ujumla.


Murtaza Mangungu(MB)
Kilwa Kaskazini na mjumbe wa POAC


Mh. Zitto Kabwe amzungumzia Marehemu Sajuki

RAIS KIKWETE AONANA NA MSHAURI WA KIJESHI WA UMOJA WA MATAIFA IKULU DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja  na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto Mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Juma Maalim, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange, na wa pili kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na wengine ni maafisa waandamizi katika JWTZ na Umoja wa mataifa.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto Mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mahadhi Mahadhi Juma Maalim, akifuatiwa na Mkuu wa Majeshi Tanzania  Jenerali Davis Mwamunyange, na wa pili kulia ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na wengine ni maafisa waandamizi katika JWTZ na Umoja wa mataifa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na Mshauri Mkuu wa Kijeshi wa Umoja wa Mataifa Luteni Generali Babacar Gaye baada ya kuonana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.Kushoto ni  Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange. PICHA NA IKULU

Mti wapiga Mweleka Kutokana na Mvua iliyonyesha leo Jijini Dar

$
0
0
 Gari likipita kwa shida pembezoni mwa Barabara ya Pugu Road kutokana na Mti huu kupiga mweleka Mapema leo asubuhi kutokana na Mvua kubwa kiasi iliyonyesha.Hakuna madhara yeyote yaliyotokea wakati wa Kuanguka kwa mti huu.

"Mwanajeshi" Aliyepiga Picha na Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Godbless Lema Kwenye Mkutano wa Hadhara Akamatwa

$
0
0


 Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha kwenye mkutano wa Chadema Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni akiwa ndani ya gari ya jeshi baada ya kutiwa nguvuni, 
 
  Picha juu alipopiga picha na Viongozi mbalimbali wa Chadema
Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema, Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara hivi karibuni.
---
Yule mtu aliyedaiwa kuwa ni mwanajeshi wa JWTZ wa kikosi cha Monduli ametiwa mbaroni leo kwa ushirikiano wa jeshi la wananchi na Police.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kijana huyu hakuwa mwanajeshi wa JWTZ kama alivyojitambulisha kwa waandishi wa habari, ila aliwahi kuwa JKT na akaacha.  Imeelezwa kuwa amekuwa akivaa ngua hizo za jeshi kwa miaka mingi na wananchi wa Mererani wanamtambua kama mwanajeshi

DK. HARRISON MWAKYEMBE ATEMBELEA UWANJA WA NDEGE SONGWE MBEYA

$
0
0


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) Mhandisi Suleiman S. Suleiman akimwelezea Dk Harrison Mwakyembe jinsi uwanja wa ndege songwe unavyofanya kazi toka uzinduliwe mwezi wa 12 mwaka jana na kuwa sasa uwanja huo umebaki maendeo ya maegesho ya ndege kubwa kama boing 737 

Mmoja ya wahandisi wa ujenzi wa uwanja huo wa songwe akimwelezea waziri wa uchukuzi Dk Mwakyembe  akimwelezea hatuza za mwisho za ujenzi wa maegesho  ya ndege kubwa.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WAIFARIJI FAMILIA YA SAJUKI

$
0
0

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' nyumbani kwao wafiwa Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo Januari 4, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa nyumbani kwa msanii wa filamu Marehemu Juma Kilowoko ' Sajuki' Tabata Bima jijjini Dar es salaam leo ambako walienda kutoa pole leo Januari 4, 2013. Wa pili kulia ni mjane wa marehemu, Wastara. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0
Mida kama hii enzi hizo ngoma ya Boney M. wakishirikiana na THE ORIGINAL TRINIDAD STEEL BAND wa "Calendar Song" ulikuwa unatamba sana

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

$
0
0
Ngoma ya Isha Ramadhan "Mashauzi" wa 'Mama Nipe Radhi' alioimba na mama yake mzazi Rukia Juma ni moja ya ngoma kali sana za taarabu kupata kutokea karibuni

hepi besdei ya kuzaliwa mtoto Brayden leo

$
0
0
Familia ya  bwana  na bibi moses mwangende  wanafuraha ya kutimiza  mwaka mmoja  kwa mtoto wao  Brayden Moses Mwangende,(Nsajigwa) a.k.a B, tunamwombea MUNGU  ampe afya  tele na kumlinda, 

Balozi Seif Ali Iddi akabidhi msaada wa vitanda 24, magodoro na mashuka hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akiwaangalia watoto waliolazwa katika wodi ya watu wa ajali kwenye hospitali ya Mnazi Mmoja,Zanzibar kabla ya kukabidhi msaada kwa ajili ya wodi hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akizungumza wakati akimkabidhi Muuguzi Mkunga wa Wodi ya Watoto waliopata ajali Bibi Leluu Omar Said msaada wa vitanda 14, magodoro na mashuka yake kwa ajili ya wodi hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif akifuatana na Waziri wa Afya wa Zanzibar,Mh. Juma Duni Haji, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dr. Saleh Mohd Jidawi na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wananachi Kiuchumi na Ushirika,Mh. Haroun Ali Suleiman wakiangalia msaada wa vitanda, magodoro na mashuka yaliyotolewa na msamaria mwema katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na mmoja wa wagonjwa wa wodi ya Mifupa aliyelazwa kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vilivyotolewa na wasamaria wema,Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi Muuguzi dhama wa wodi ya Mifupa Bibi Afsa Abdulla msaada wa vitanda 24, magodoro na mashuka yake kwa ajili ya wodi hiyo.

NDEGE MEDICS YAKABIDHI AMBULANCES ZA KISASA KWA HOSPITALI YA AGA KHAN KWA AJILI YA MRADI WA KUBORESHA AFYA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO TANZANIA

$
0
0

Head of Primary Medical Centre Bwa. Siwawi Konteh (wa pili kulia) ambaye pia ni mratibu wa mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja ili kuokoa Afya ya Mama na Mtoto akizungumzia Malengo Makuu ya mradi huo kuwa ni kuongeza kiwango na matumizi ya Huduma ya Afya ya Mama Mjamzito na Watoto na kushirikiana na kujifunza kuhusu Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto. Kutoka kushoto ni Acting Medical Director wa Aga Khan Hospital Dr. Ambrose Chanji, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib, Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Dr. Sebastian Ndege na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu cha Hospitali hiyo Bw. Anis Nazrani.
Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi magari ya kubeba wagonjwa kwa hospitali ya Aga Khan ambapo amesema vifo kadhaa vinavyotokea katika hospitali nyingi kwa sasa vinawahusisha akinamama na watoto wasio na hatia ambao hukosa huduma za awali za haraka zikiwemo usafiri na hivyo katika kujali hilo wametoa magari hayo.
Aidha amesema Ndege Medics inashukuru kuwa sehemu ya mradi endelevu wa kujaribu kuokoa maisha ya akina mama na watoto ambao lengo lake ni kuchangia katika kuboresha afya ya uzazi wa mama na watoto wachanga katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mwanza, Mbeya na Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari ya kubeba wagonjwa kwa Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania
Wakipongezana baada ya makabidhiano hayo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Ndege Medics akionyesha baadhi ya vifaa vilivyomo ndani ya magari hayo ya kisasa.
Pichani Juu na Chini ni muonekano wa magari hayo ya kubebea wagonjwa kwa ndani yaliyotelwa kwa hospitali ya Aga Khan na NDEGE Medics kwa ajili ya mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania.
Pichani Juu na chini ni baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege Medics, Hospitali ya Aga Khan na waandishi wa habari walioshuhudia tukio la makabidhiano hayo.

Baadhi ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyokabidhiwa rasmi leo kwa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar ikiwa ni sehemu ya mradi Endelevu utakaohusisha Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Iringa, Mbeya na Morogoro kwa ajili ya kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto.

mansu-li kuzindua albam yake ya kina kirefu january 12


MVUA YALETA MAFURIKO MKOANI MTWARA

$
0
0
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika maeneo mengi ndani Ya Manispaa ya Mtwara/Mikindani Jana kufuatia Mvua kubwa iliyonyesha karibu kutwa nzima.Picha na na Abdulaziz Video,Mtwara

vikwangua anga vyaendelea kula mbavu za mbwa jijini Dar

$
0
0
Hapa ni maeneo ya Ubungo nyuma ya stendi ya mabasi yaendayo bara

RAIS KIKWETE KUZINDUA MIRADI MINNE YA UJENZI WA BARABARA NA DARAJA MKOANI TABORA

MKE WA MAKAMU WA RAIS, MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KIISLAMU WA SHULE YA SEKONDARI TAMBAZA

$
0
0
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Mama Asha amewahasa vijana hususan wanafunzi hao waliohitimu masomo kutokukubali kutumika na watu wenye maslahi binafsi na kujikuwa wakisababisha uvunjifu wa amani. Aidha amewataka kutojihusisha na makundi yanayochochea uvunjifu wa amani bila kujitambua wafanyalo, badala yake amewambo kuwa wakipima kila wanaloambiwa kuwa linamaslahi na dini yao ama maslahi kwa jamii na taifa kwa ujumla. Picha Zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Latifah Nuhu, wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. 
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Mwinga Gwao, wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi zawadi mhitimu wa Kidato cha Sita, Zuhura Azmin, kwa kuwa mmoja kati ya waliofanikisha sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya wahitimu wa kike wakiwa katika mahafali hayo leo.
 Baadhi ya wahitimu wa kiume, wakiwa katika mahafali hayo leo.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita, Khadija Hassan, wakati wa sherehe za mahafali ya Kidato cha Sita kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari ya Tambaza. Mahafali hayo yamefanyika leo, katika shule hiyo ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
 Dua baada ya shughuli hiyo kukamilika.
Mama Asha, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita, baada ya zoezi la kugawa vyeti kwa wahitimu. 

DKT. SHEIN AFANYA UFUNGUZI WA JENGO LA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA,TUNGUU ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja jana,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Utumumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma,(IPA) Harusi Masheko Ali,alipotembelea madarasa ya kusomea,baada ya ufunguzi rasmi wa Jengo la Chuo hicho uliofanyika jana Tunguu, Wilaya ya Unguja, katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akifuatana na Waziri wa Utumumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir,(kushoto) pamoja na Viongozi wengine baada ua kulifungua jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja jana,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akiwahutubia Wananchi, katika sherehe za ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja jana,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Maalim Abdalla Suleiman,(wa pili Kulia) na Waziri wa Utumumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir,(kushoto).

Baadhi ya walimu na wafanyakazi wa Chuo cha Utumishi wa Umma,wakiwa na nyuso za Furaha wakati wa sherehe za Ufunguzi wa Jengo la Chuo,uliofanyika jana Tunguu Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja,ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi na Wananchi walioalikwa katika sherehe za Ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma,zilizofayika jana huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja, wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Rais wa Zanzibar,alipokuwa akitoa hutuba yake katika kusherehekea shamra shamra za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images