Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110158 articles
Browse latest View live

Tawi la CCM UK lamshukuru Rais Kikwete


LOKASSA YA MBONGO ALONGA NA VIJIMAMBO

$
0
0

Hii ni sehemu ya kwanza ya Gwiji la ukung'utaji wa kitaa la kati kutoka DRC, Lokassa ya Mbongo Jina alilopewa naTabu Ley Rochereau wakati akiwa na miaka 16, Lokassa alonga na Vijimambo aelezea safari yake ndefu ya muziki yenye mabomde na milima inayosisimua, inayofundisha na usione mtu anakula raha, hujui mateso gani aliyopitia mpaka utakapo pata bahati akuhadithie. MSKILIZE.
Shukurani kwa Felix Muzungu mtafsili wetu wa kifaransa kwa kiingereza

BREAKING NYUZZZZZ.........: CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA CHAWAKA MOTO ASUBUHI HII

$
0
0
TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII TOKA MKOANI SHINYANGA HIVI SASA,INAELEZA KUWA MOTO UMETOKEA KATIKA HOSPITALI KUU YA MKOA WA SHINYANGA BAADA YA KUTOKEA HITILAFU YA UMEME KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI NDANI YA KUSPITALI HIYO NA KUPELEKEA KUTOKEA KWA HITILAFU.

JUHUDI ZA HARAKA ZILIWEZA CHUKULIWA KUWASILIANA NA WATU WA FAYA NA BAADA YA MUDA MFUPI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUUZIMA MOTO HUO.

HAKUNA MTU YEYOTE ALIEDHULIKA NA MOTO NA INASEMEKANA NDANI YA CHUMBA HICHO KULIKUWA NA MAITI MOJA TU YA MTOTO MDOGO AMBAYO ILIOKOLEWA PIA.

INAELEZWA KUWA TUKIO LA NAMNA HIYO SIO LA KWANZA KUTOKEA KATIKA CHUMBA HICHO,HIVYO JUHUDI ZA HARAKA ZINAFANYWA KUWASILIANA NA TANESCO ILI KUWEZA KUTATUA KABISA TATIZO HILO.

TUTAENDELEA KUJULISHANA KADRI TAARIFA ITAKAVYOKUWA IKITUFIKIA.

MKANDARASI WA BARABARA YA TUNDURU - SONGEA ATIMULIWA BAADA YA KUSHINDWA KAZI

$
0
0
Habari Kiongozi

Nimeona nikurushie taswira hizo za barabara ya Namtumbo - Tunduru ambayo Mkandalasi wa Kampuni ya Progressive amefungishwa virago baada ya kushindwa kuitengeneza. 

Hivi sasa hali ni mbaya, magari ya abiria na mizigo yamekwama na mengine yameharibika kabisa na kuna tishio kubwa kwamba barabara itajifunga sio muda mrefu kwa sababu mvua hasa bado hazijaanza.

Mkandalasi aliyekua akitengeneza alipewa ushindi wa vipande vitatu avitengeneze kwa kiwango cha lami na matokeo yake kashindwa, hadi anatangazwa rasmi kuondolewa Januari 08, 2013 ilikua tayari miaka miwili imepita tangu apewe kazi hiyo iliyopaswa kufanywa mwa muda wa miezi 28 na kazi aliyofanya haifiki hata asilimia 5.

So kutimuliwa hajaonewa.

Mdau RUVUMA
Hapa ni Baadhi ya abiria wa moja ya mabasi yanayotumia barabara hiyo wakiwa wamekaa chini ya kivuli cha mti wakisubiri basi lao lililokwama,ili litoke na waendelee na safari.
Hapa jamaa wamehangaina na basi lao mpaka wamechoka,hivyo wakaamua tu kuweka mapozi ili wajipatie picha za ukumbusho.
hivi ndivyo mambo yalivyo kwenye barabara hiyo.

Mipaka ndio chanzo kikubwa cha kuingia kwa bidhaa feki nchini - dkt. kigoda

$
0
0
Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara,Dr. Abdallah Kigoda (pichani) amesema kuwa mipaka ya nchi imekuwa chanzo cha uingizwaji wa bidhaa ambazo ziko chini ya viwango (feki) hali inayochangia kuleta athari kubwa kiuchumi na afya za watu wanaotumia bidhaa hizo.

Aidha waziri huyo ameeleza kuwa uingizaji wa bidhaa bandia nchini unatokana na taasisi zinazoshughulikia masuala ya viwango vya ubora kutoimarika kiutendaji.

Akizungumza katika ufunguzi wa Warsha iliyoandaliwa na shirika la dunia linalohusika na mambo ya kuandaa viwango (ISO) wakishirikiana na shirika linaloshughulikia viwango na ubora wa bidhaa nchini (TBS),warsha iliyokuwa ikijadili juu ya mfumo wa uzalishaji kuanzia malighafi, bidhaa, mtumiaji na taka inayotokana na bidhaa hiyo ilivyo na athari katika mazingira yaani (Life Cycle).

“Mkutano huu ni muhimu kwa nchi zinazoendelea kushiriki katika kuweka vigezo vya viwango vya ubora na kujiaandaa kuvitimiza ili kuweza kuuza bidhaa katika soko la dunia ili kuondokana na vikwazo katika uingizaji wa bidhaa zao kwenye soko hilo kutokana na bidhaa kutokizi ubora wa kimataifa na teknolojia dhaifu inayotumika kuanzia malighafi,bidhaa hadi usafirishaji” Waziri Kagoda.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TBS Bwana Leandri Kinabo amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwani unalenga kuweka mikakati ya viwango,na uzalishaji bora unaozingatia ubora ili kushiriki kikamilifu katika soko la dunia (WTO) ukizingatia kuwa Tanzania ni nchi mwanachama wa soko hilo.

Hivyo amewataka wazalishaji kuzingatia utunzaji wa mazingira katika mfumo mzima wa uzalishaji kuanzia malighafi, bidhaa, usafirishaji na utupaji wa taka inayotokana na bidhaa hiyo (Disposal).

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo ni kutoka nchi za Afrika Mashariki,Ukanda wa Kusini mwa Afrika (SADC) na pia unatarajia kuhudhuriwa na nchi za Malaysia, India, China na Uingereza.

WALIOFUZU SHINDANO LA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE WAKABIDHIWA HATI ZAO ZA KUSAFIRIA NA KUPOKEA MAELEKEZO YA SAFARI YA AFRIKA KUSINI.

$
0
0
 Wakiwa katika picha ya pamoja meneja wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi(katikati) na washiriki wa Guinness Football Challenge baada ya kupokea hati zao za kusafiria.


 Emmanuel Temu mmoja ya washiriki waliofuzu kuingia kwenye mashindano ya Guiness Football Challenge akipokea hati ya kusafiria kutoka kwa Meneja wa kinywaji cha Guiness Davis Kambi
 Mratibu wa safari Bi. Caroline akitoa maelekezo na taratibu za safari kwa washiriki waliofuzu kuingia katika mashindano ya Guinness Football Challenge wanaotarajiwa kusafiri karibuni.
Washiriki waliofuzu kuingia katika shindano la Guinness Football Challange wakisikiliza kwa makini maelekezo na taratibu za safari kutoka kwa mratibu wa safari na meneja wa kinywaji cha Guinness

LEPTIN - KAHAWA NA CHAI ZIPUNGUZAZO UZITO

$
0
0
KUTANA NA CHAI NA KAHAWA AMBAYO UKINYWA INAKUSAIDIA KUPUNGUZA MAFUTA NA KUPUNGUZA HAMU YA KULAKULA OVYO NA KUKUFANYA UONDOKANE NA NYAMA ZEMBE

LEPTIN NI NINI?!!
Ni hormone ambayo ndiyo yenye kazi ya kukufanya uhisi njaa. Kahawa ya leptin inafanya kazi haraka ya kuunguza mafuta na ina ufanisi mkubwa wa kupunguza uzito na haina athari yoyote. Unaweza kuona au kuhisi tofauti kipindi cha kuanzia wiki moja na kuendelea. Inapunguza hamu na kuchochea mwili kwa kuchoma mafuta, hivyo unaweza kupoteza uzito kwa haraka zaidi. Licha ya kupoteza uzito, Kahawa ya Leptin ina uwezo wa kupambana na kuzeeka, inasafisha utumbo, kuondoa sumu mwilini na ni nzuri kwa watu wenye matatizo ya ngozi kama acne.

WANAPATIKANA :: Morogoro,Samora Road & Ilala Shariff Shamba
WASILIANA NAO: 0786477776





Kali TV Online This Week..


RAIS KIKWETE AUNGURUMA NZEGA, AWASILI TABORA KUFUNGA MIRADI ZAIDI

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya ujenzi wa barabara ya Tabora-Ndono,kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Tanroads,Eng. Patrick Mfugale kabla hajazindua rasmi ujenzi wa barabara hiyo akiwa katika ziara yake ya siku nne ya mkoa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara  ya Tabora-Ndono akiwa katika ziara yake ya siku nne ya mkoa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisikilia maelezo ya Meneja wa TANESCO wa Nzega akielezea mikakati ya kuwapatia wakazi wa hapo nishati hiyo wakati wa mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Uyui toka kwa mkuu wa Wilaya hiyo,Mhe. Lucy Mayenga wakati Rais alipowasili Tabora mjini kuendelea na ziara yake ya siku nne ya mkoa huo wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo kwa Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Maji,Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Fedha,Dkt. William Mgimwa kabla hajahutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Tabora Mjini toka kwa mkuu wa Wilaya hiyo,Mhe.  Suleiman Kumchaya wakati Rais alipowasili Tabora mjini kuendelea na ziara yake ya siku nne ya mkoa huo ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mmoja wa wahandisi kutoka China waliopata kandarasi ya kujenga barabara baada ya kuzindua rasmi ujenzi wa barabara hiyo akiwa katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji. (PICHA NA IKULU)

MHE. MWANRI ZIARANI MKOANI RUKWA

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Aggrey Mwanri akikagua mradi wa maabara katika kituo cha afya cha Matai katika Wilaya mpya ya Kalambo leo. Naibu Waziri huyo amepiga marufuku miradi yote ya serikali hususani inayohusisha mbao kupigwa rangi na badala yake ipakwe vanish, hiyo ni kutokana na baadhi ya wakandarasi kutumia staili hiyo kuiibia Serikali kwa kuweka mbao za bei nafuu na kuzipiga rangi. Mhe. Mwanri yupo Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi ya siku saba ambapo ataembelea halmashauri zote za Mkoa wa Rukwa na kukagua miradi mbalimbali iliyopo chini ya Halmashauri hizo.
Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri (kulia) akikagua ujenzi wa banio la mradi wa umwagiliji katika kijiji cha Katuka katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Mhe Mwanri aligoma kuweka jiwe la msingi katika mradi huu kutokana na mkandarasi kujenga mradi huo chini ya kiwango kinyume na mchoro halisi wa mradi huo. Aliagiza mapungufu yarekebishwe ndipo Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a aweke jiwe hilo kwa niaba yake.
Kutoka kushoto ni Mama Mwanri mke wa Naibu Waziri, Mhe. Agrey Mwanri Naibu Waziri TAMISEMI, Mhe. Moshi Chang'a Mkuu wa Wilaya ya Kalmabo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Godfrey Schona wakiwa katika picha ya pamoja pembezoni mwa fukwe za Ziwa Tanganyika katika Hoteli ya Liemba Beach Resort walipotembelea ikiwa ni sehemu ya ziara yake Mkoani Rukwa.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiweka jiwe la msingi katika nyumba ya mganga wa kituo cha afya Matai mapema hii leo. Katika miradi miwili aliyotembelea Mhe. Mwanri aligoma kuweka mawe ya msingi hadi hapo marekebisho aliyoagiza yatakapofanyiwa kazi ndipo mawe hayo yawekwe kwa niaba yake. 
Naibu Waziri wa TAMISEMI Ndugu Agrey Mwanri akipanda kwa tahadhari kubwa katika daraja la Mto Momba linalounganisha wananchi wa Kilyamatundu Mkoani Rukwa na wale wa Kamsamba Mkaoni Mbeya. Daraja hili lililojengwa kwa kamba limekuwa halikidhi haja ya wananchi hao jambo wanaloomba Serikali kuwajengea daraja litakalowawezesha kuvuka na kuvusha mazao yao kirahisi. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

KUMBUKUMBU

$
0
0
MAREHEMU CASSIAN MALIMA

Leo ni miaka minne (4) kamili tangu ulipoitwa na Mwenyezi Mungu katika makao yake ya milele Januari 9, 2009 katika hospitali ya Aga Khan ya Dar es Salaam na kupumzishwa Januari 14, 2009 kule Musoma.

Ni vigumu kuamini lakini ukweli unabaki kama ulivyo, HAUPO NASI TENA CASSIAN! umeacha pengo katika familia, miongoni mwa rafiki zako na katika fani yako uliyoipenda sana ya Uandishi wa Habari.

Tunaamini uko mikononi mwa Bwana na tutaonana kwa mapenzi ya Mungu muda wetu utakapowadia.

Unakumbukwa daima na wanao, wapwa zako, dada zako, kaka zako, binadamu zako, wajomba, shangazi na hasa baba yako mzazi Mzee Flavian Kigeso Malima, marafiki na majirani zako.

Tunaendelea kukuombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kukupa raha ya milele na mwanga wa milele akuangazie upumzike kwa amani. Amina.

Kwa maana sisi wenyeji wetu uko mbinguni, kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi Bwana wetu Yesu Kristu atakayebadili mwili wetu wa unyonge upate kufanana na mwili wake wa utukufu kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake (Flp 3:20-21).

EXCLUSIVE VIDEO MPYA YA -"LINAH -USHAFAHAMU NAPENDA"

Tangazo la Ajira Umoja wa Mataifa

$
0
0
Ankali pole na  ziara, naomba uwatangazie wadau link hiyo hapo chini ambayo inaendeleza namna ya kuomba au kutafuta ajira katika Umoja wa Mataifa. miongoni mwa link hizo ipo ya kiswahili ambayo ni lugha yetu na itakuwa rahisi kwa wadau wengi kujifunza na kujielimisha namna ya kuomba kazi katika chombo hicho. Nawasilisha

 

In collaboration with the Department of Public Information, OHRM has prepared and broadcast radio spots in all official languages as well as Portuguese and Swahili on UN CAREERS. 

Please find the links below and feel free to circulate among your constituents.  


Dkt. Shein afanya uzinduzi wa barabara Mfenesini-Bumbwini Zanzibar

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B Unguja jana,ujenzi huo umejenga na Kampuni ya Mecco kwa umefadhiliwa na Benki ya Dunia na Serikali ya Mapinduzi,ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akizungumza na Wananchi na wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini Unguja,katika kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mwakilishi wa ADB Tanzania Toniya Kandiero,wakikata utepe kufungua Barabara ya Mfenesini-Bumbwini,iliyojengwa na Kampuni ya Mecco kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,ikiwa shamra shamra za kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) Mwakilishi wa ADB Tanzania Toniya Kandiero,(wa pili kulia) Naibu Waziri wa Mindombinu,Mawasiliano Issa Haji Gavu,(wa pili kulia) Katibu Mkuu wa Miundombinu ,Mawasiliano,Dk.Juma Malik Akili,(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kasakazini Unguja Pembe Juma,(kushoto) wakitembea katika Barabara ya Mfenesini-Bumbwini baada ya kufunguliwa Rasmi jana,ikiwa ni shamra shamra ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi ya Wananchi na wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza nao katika sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini Unguja,katika kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

KENYELA KUWA MGENI RASMI KATIKA MPAMBANO WA NDONDI UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

$
0
0
Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela (pichani) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la kutetea ubingwa Afrika mashariki na kati kati ya bondia Mtanzania Thomas Mashali na Bernad Mackoliech wa Kenya Jumamosi katika Ukumbi wa Friends Corner Manzese jijini Dar es salaam.

Mratibu wa pambano hilo Aisha Mbegu amesema wameamua kumualika kamanda Kenyela ili kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kutoa Elimu ya Ulinzi shirikishi na kwa kutambua mchango wa jeshi la polisi kudumisha amani katika michezo.

“ Jeshi la polisi ni wadau wetu wakubwa katika michezo hasa ngumi na mchango wao umekuwa ukionekana kwani sasa hakuna vurugu zinazojitokeza katika mapambano yeyote ya ngumi yanayofanyika tofauti na Miaka ya Nyuma ambapo Ngumi ilikuwa Watoto hawawezi kwenda kuangalia,”alisema Aisha.

Aisha alisema katika pambano la awali ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa Friend corner hakukuwa na vurugu na idadi ya watoto na wanawake kuangalia ngumi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na nhivyo kutoa hamasa kwa wazazi na watoto kupenda mchezo huo.

Mbali na Kenyela Mbunge wa Kinondoni Iddi Azan na Mbunge wa ubungo John Mnyika wamealikwa ili kushuhudia vipaji vya vijana wa kinondoni katika Ngumi.

Bondia Mackoliech anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari leo (Alhamisi) katika Uwanja wa Karume na Ijumaa wanatarajiwa kupima Uzito saa Nne asubuhi katika Ukumbi wa Friends Corner Manzese .

Waziri wa Uvuvi afanya ziara kwenye Machinjio ya Nyama jijini Arusha

$
0
0
Waziri wa Uvuvi na maendeleo ya mifugo Dr.Mathayo David Mathayo (katikati) akitembelea eneo la nje la machinjio ya nyama jijini Arusha wakati alipofanya ziara ya kutembelea machinjio hayo na kuona kazi zinavyofanywa.
Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo,Dk. David Mathayo David (kulia) akiangaliwa mandhali ya ndani kwenye ya machinjio ya nyama jijini Arusha wakati alipofanya ziara ya kutembelea machinjio hayo na kuona kazi zinavyofanywa,ambapo aliwaahidi wahusika wa machinjia hayo kuwa watazuia nyama zote zinazotoka nchi za nje ili soko la nyama hapa nchini likuwe.
Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo, Dk. David Mathayo David (wa pili kulia)  akisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja wa Machinjio ya nyama jijini Arusha,Fabian Kisingi wakati alipofanya ziara ya kutembelea machinjio hayo na kuona kazi zinazofanywa,ambapo aliwaahidi wahusika wa machinjia hayo kuwa watazuia nyama zote zinazotoka nchi za nje ili soko la nyama hapa nchini likuwe.Picha na Woinde Shizza,Globu ya Jamii-Arusha.

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakutana na Tume ya Katiba

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea katika mkutano na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) uliolenga kupata maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia kwa Jaji Warioba ni Bi. Ussu Mallya, Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo, Prof. Ruth Meena 9Mjumbe wa Bodi ya TGNP) na Mwenyekiti wa TGNP Bi. Mary Rusimbi.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi akiongea katika mkutano na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) uliolenga kupata maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Wajumbe wengine wa Tume Bi. Mary Kashonda na Bi. Salma Moulidi.
Mwananchama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Bi. Subira Kibiga akitoa maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Wengine ni wananchama wenzake Bi. Diana Mwiru (kushoto) na Bi. Asseny Muro.
Mwanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Bi. Asseny Muro akitoa maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TGNP Bi. Mary Rusimbi na Mjumbe wa Bodi ya mtandao huo Prof. Ruth Meena.
Baadhi ya Wajumbe ya Mabadiliko ya Katiba katika picha ya pamoja na Wanachama na viongozi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) mara baada ya mtandao huo kuwasilisha maoni yake kuhusu Katiba Mpya leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam).

Wanachuo Kipawa sasa kulipa ada kwa M-Pesa

$
0
0
Mkuu wa chuo cha VETA kipawa, Jijini Dar es Salaam, Eng. Lucius Luteganya, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa ulipaji ada kwa wanafunzi wa chuo hicho kupitia huduma ya M – Pesa. Kufuatia ushirikiano kati ya chuo hicho na Vodacom Tanzania. Kushoto ni Mkuu wa ukuzaji biashara – M - PESA Jackson Kiswaga.
Meneja mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa, akimuelezea jambo Mkuu wa Chuo cha Veta Kipawa, Eng. Lucius Lutenganya wakati wa uzinduzi wa ulipaji ada kupitia huduma ya M – pesa kwa wanafunzi wa chuo hicho. Katikati ni Mkuu wa Ukuzaji Biashara – M - PESA, Jackson Kiswaga.

Viewing all 110158 articles
Browse latest View live




Latest Images