Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1196 | 1197 | (Page 1198) | 1199 | 1200 | .... | 3272 | newer

  0 0
  0 0


  0 0


  Hatimaye Serikali ya Jamhuri ya Uganda imetangaza rasmi uamuzi wake wa kutumia Bandari ya Tanga nchini Tanzania kusafirishia mafuta ghafi yake. 
  Uamuzi huo umetangazwa na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda wakati wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini uliomalizika Jijini Kampala Uganda. 
  Ujumbe wa Tanzania ulio kamilisha mazungumzo hayo na hatimaye kushuhudia utangazwaji wa hatua hiyo uliongozwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa 
  Jopo la wataalamu kutoka Tanzania lililoongozwa na Mhe. Prof. Sospeter Muhongo bado wako jijini Kampala kukamilisha mpango huo wa Bomba la Mafuta Ghafi ambapo pia nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati zinatarajia kunufaika.

   

   
  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

  Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,

  Dar es Salaam

  23 Aprili, 2015
  0 0

   Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mkoani Arusha .

   Waziri Nape aliwaambia wadau na waigizaji wa Filamu waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha hilo kuwa hii ni moja ya hatua kubwa kwenye historia ya filamu nchini na kuahidi Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha haki za wasanii hazipotei wala haziliwi na wajanja.
   
   Mkurugenzi wa Tanzanite One ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha, Ndugu Faisal Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mjini Arusha kwenye hotel ya Mt. Meru
    Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifunua pazia kuashiria uzinduzi wa Tamasha la kimataifa la filamu la Tanzanite mjini Arusha.
    Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (mwenye kaunda suti ya kijivu) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Ntibenda  kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na wadhamini kwenye uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite.

  0 0  0 0


  CH10: PAC yaikomalia Lugumi, Aliyejilipa mishahara 17 afukuzwa, Serikali yaijibu Ukawa, Watumishi hewa tishio, Fuatilia magazeti ya leo.https://youtu.be/NUTtiRsQO9E
  MLIMANI TV: Ukawa yasema Magufuli anaihujumu, Jipu la watumishi hewa laiva, Ukawa wapondwa, RC apinga idadi ya watumishi hewa, kamati yaundwa kuichunguza Lugumi, Sukari yapaa. Pata uchambuzi wa kina wa magazeti ya leo.https://youtu.be/rX9olRoLLiI

  0 0

  Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi {CCM} na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete jana Aprili 23, 2016 alitembelea Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha jimbo la Fujian (Fujian Agriculture and Forest University-FAFU) kilichopo katika mji mkuu wake Fu Zhou.

  Mwenyekiti alikaribishwa chuoni hapo kuonyeshwa hatua ambazo jimbo hilo imepiga katika kuendeleza kilimo cha kisasa, teknolojia ya kuzalisha mbegu na teknolojia ya kupambana na magonjwa na wadudu waharibio mazao. Akiwa chuoni hapo, alikutana pia na wanafunzi wa kitanzania wanaosomea shahada za uzamivu kwa ufadhili wa serikali ya China.

  Katika mazungumzo yake na Mkuu wa Chuo hicho Profesa Lan Siren, Mhe Kikwete amependekeza kuanzishwa kwa mahusiano na ushirikiano baina ya Chuo Cha Kilimo SUA na Chuo hiko. Pia amependekeza wanafunzi na wakufunzi wa chuoni hapo kuja Tanzania kufanya mafunzo ya vitendo na tafiti zao.

  Kufuatia pendekezo hilo, Rais wa Chuo hicho ameelezea utayari wa Chuo hicho kushirikiana na SUA. Aidha, ameelezea kulipokea ombi la Mwenyekiti la kuongeza nafasi za masomo kwa vijana wa Tanzania na kuahidi kulifanyia kazi ombi hilo.

  Chuo Kikuu cha FUFA kina takribani wanafunzi elfu arobaini (40,000) ambapo wanafunzi kutoka Afrika ni takribani 120 kati yao watatu tu (3) wanatoka nchini Tanzania.

  Mhe Kikwete yuko nchini China kwa ziara ya kichama iliyotokana na mualiko rasmi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha China Mhe Xi Jinping.
  Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete akiwa pamoja na uongozi na wanafunzi wa Tanzania wanaosoma chuo cha Kilimo na Misitu FAFU.
  Dkt Kikwete akiwa katika chuo cha Kilimo FAFU ambapo alialikwa kutembea leo hii.

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa MWANZA John Mongella ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Ally Mkaripa,kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata kompyuta iliyo ibwa usiku wa kuamkia April 22,2016 kwenye chumba kinacho tumika na mifumo ya ukusanyaji mapato na uaandaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR)

  Mongella ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilicho fanyika katika ukumbi wa halmashauri,ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri.

  “OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana,amesema Mongella na kuongeza ,sisi tunajua Nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo komputa hiyo.

  Akizungumza kando ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri,kaimu mhazini wa halmashauri hiyo Baraka Munuo,alidai kupokea taarifa za kupotea kwa Komputa hiyo kutoka kwa afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe akimuelezea upotevu huo.

  Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa MWANZA, amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ukerewe,, kupitia mafaili na kubaini watumishi waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo ambalo mkuu wa mkoa amedai linachangiawatumishi kufanyakazi kwa mazoea,”Mkurugenzi nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika kituo hiki kwa muda mrefu, haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishirini na moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana, alisema Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama kuna mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.

  Awali akisoma taarifa ya wilaya hiyo, mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti,alimwambia mkuu wa mkoa kuwa hali ya ulinzi na usalama ni shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo huku akisema wilaya imefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu kilicho kuwa kimepiga kambi katika Wilaya hiyo kwa zaidi ya miezi 6.

  Mkuu wa mkoa wa yupo katika ziara yakujitambulisha na hii ikiwa ni wilaya yake ya saba,Mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi, Magu, Nyamagana, Ilemela na Kwimba na hii ya Ukerewe inakuwa wilaya ya saba huku akiwa amebakiza wilaya moja ya Sengerema yenye halmashauri za Buchosa na Sengerema yenyewe.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka wananchi wa wanaosafiri mara kwa mara  kwa ajili ya harakati zao za maisha kuchukua vyandarua na kuvitumia wanapokuwa safarini ili kujikinga na maradhi ya Malaria.

  Akizungumza katika Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika viwanja vya Maisara, Mjini Zanzibar, Balozi Seif alisema licha ya Zanzibar kuwa na kiwango cha chini ya asilimia moja cha Malaria, utafiti unaonyesha watu wanaogunduliwa kuugua maradhi hayo hivi sasa ni wale wenye utaratibu wa kusafiri nje ya Zanzibar.

  Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kwa dhati kuimarisha afya za wananchi na itaendelea kuboresha huduma za afya sehemu zote na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi hizo.

  Hata hivyo alisema wakati Zanzibar inajivunia mafanikio katika vita dhidi ya Malaria bado maradhi ya Kipindupindu yanaendelea kuwa tishio  kwa wananchi na kuwataka kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya.

  Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Afya Juma Malik Akili alisema katika kumaliza Malaria kuanzia tarehe 25 mwezi huu watatoa vyandarua  760,000 vilivyotiwa dawa bure kwa wananchi katika Wilaya zote za Zanzibar.

  Amewashauri wananchi kuvitumia vyandarua hivyo kikamilifu kwani inaonekana kuwa ndio njia kubwa inayosaidia kukinga Malaria.

  Katika maadhimisho hayo, wananchi na vikundi vya mazoezi wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais walifanya matembezi ya hiari yaliyoanza Mazizini, Wilaya ya Magharibi B na kumalizia viwanja vya Maisara, Mjini Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi (katikati) akiongoza Matembezi ya hiari ya kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika kuanzia mazizini na kumalizikia maisara mjini Unguja.kulia yake ni Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo na kushoto yake ni katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Juma Malik Akili.
  Vikundi vya mazoezi vikiwa katika matembezi ya hiari ya kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani ambayo yamefanyika kuanzia Mazizini Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia Maisara Mjini Unguja.
  Vikundi mbalimbali vya Mazoezi vikifanya mazoezi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Maisara katika maadhimisho ya Siku ya malaria Duniani ambayo yamefanyika Mjini Unguja.


  0 0

  Simu.tv: Mkuu wa wilaya ya Ilala awataka wafanyabiashara kote nchini kumuunga mkono jitihada za Rais Magufuli kwa kufanya usafi kwenye maeneo yao. https://youtu.be/txg9YC3vYoE
  Simu.tv: Rais mstaafu wa awamu ya pili mzee Ally Hassan Mwinyi awataka watanzania kutobaguana kwa misingi ya kidini na kisiasa ili kuendeleza upendo na mshikamano.https://youtu.be/3ABiWqV8Cmk
  Simu.tv: Serikali ya Uganda yaridhia ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta ghafi kutoka nchini humo hadi bandari ya Tanga Tanzania. https://youtu.be/EyI6WC9w-mE
  Simu.tv: Kituo cha afya cha Kambi ya Simba kilichiko wilayani Ngorogoro mkoani Arusha chaelezwa kukabiliwa na ukosefu wa vyumba vya upasuaji jambo linalo hatarisha maisha ya wajawazito na watoto. https://youtu.be/U6grVXkFvHI 
  Simu.tv: Serikali yaanza kupitia upya sera ya ardhi ya 1995 ili iweze kuendana na mabadiliko ya sasa na ipunguze au kumaliza kabisa migogoro ya wakulima katika maeneo mbalimbali nchini.https://youtu.be/zp5rZQHR0og 
  Simu.tv: Wakulima na wafabiashara wa vitunguu mkoani Singida walalamikia wakala wa vipimo mkoani humo kwa kushindwa kuweka bayana ujazo wa magunia ya vitunguu.https://youtu.be/kIhRWpVtxfE 
  Simu.tv: Wafanyabiashara katika soko la Nyamatare  wilayani Musoma waulalamikia uongozi wa halmashauri hiyo kuwaondoa katika eneo la soko hilo bila kuwaambia wapi pa kwenda.https://youtu.be/whD8Bfmewt8 
  Simu.tv: Wamiliki wa shule binafsi nchini wameunda chama chao kitakacho wafanya kuwa pamoja katika kushauriana na kutekeleza maagizo ya wizara ya elimu.https://youtu.be/Cr9X7pZ_5_o
  Simu.tv: Mkoa wa iringa umebaini ongezeko la watumishi hewa wengine 12 baada ya kurudia zoezi la uhakiki na kufanya jumla ya watumishi hewa mkoani humo kufikia 27https://youtu.be/duBwaqsxV6o
  Simu.tv: Watanzania wameshauriwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujenga mwili na kuepuka na magonjwa yanayoweza kuwapata. https://youtu.be/kMRXjLP07OU
  Simu.tv: Mbao Fc ya jijini Mwanza imefanikiwa kupanda ligi kuu ya Vodacom baada ya Geita FC na JKT Oljoro kupewa adhabu ya kushushwa daraja baada ya kukumbwa na tuhuma za upangaji matokeo https://youtu.be/2eMeQa0-UjM
    Simu.tv: ligi ya mabingwa wa mikoa Tanzania bara inatarajiwa kuanza mei kumi na nne ambapo mshindi wa ligi hiyo atapanda moja moja kucheza ligi daraja la kwanza.https://youtu.be/K5Nn2lWkLhM

  0 0


  Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na maafisa kutoka kampuni ya nchini Ufaransa ya Endel Engie mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wawekezaji hao walikuwa nchini kujifunza fursa za uwekezaji zinazopatikana. Kulia ni Bw. Jean Phillipe na Olivier Rousseau (wa pili kulia), wawekezaji kutoka kampuni hiyo.
  Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru (kushoto) akisisitiza jambo alipokuwa akiongea na maafisa kutoka kampuni ya nchini Ufaransa ya Endel Engie mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wawekezaji hao walikuwa nchini kujifunza fursa za uwekezaji zinazopatikana. Wengine ni Bw. Jean Phillipe (wa pili kulia) na Olivier Rousseau (wa pili kushoto), wawekezaji kutoka kampuni hiyo. Kulia ni Bw. Gaudence Kayombo, aliyefuatana na ugeni huo.


  Serikali imewataka wawekezaji wa ndani na nje kutumia fursa zilizopo Tanzania hasa katika eneo la kuongeza thamani ya malighafi mbalimbali.

  Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru alipokuwa akiongea na maafisa kutoka kampuni ya nchini Ufaransa ya Endel Engie mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

  Maafisa wa kampuni hiyo walikuwa nchini na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali waandamizi wa serikali kueleza nia yao ya kuwekeza Tanzania na kujua fursa zilizopo nchini.

  Endel moja ya makampuni ya Engie Group yenye mapato yanayofikia Euro milioni 700 kwa mwaka na waajiriwa 6,000 nchini Ufaransa.

  Baadhi ya shughuli za kampuni hiyo ni katika maeneo ya sayansi za anga, viwanda vya vyakula, reli, gesi, ujenzi wa meli, nishati ya nyuklia na viwanda vya chuma miongoni mwa vingine.

  Kwa bara la Afrika, kampuni hiyo inafanya kazi katika nchi za Afrika ya Kusini, Angola na Congo DRC.  0 0

  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza amesema amejipanga vilivyo kuhakikisha anawainua wanawake wa mkoa  huo, kiuchumi kwa kuwazesha kufanya ujasiriamali utakaowaingizia kipato.

  Shonza alitoa kauli hiyo jana  kwa  wajumbe wa Baraza la Wawanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Momba, alipokutana nao mjini Tunduma kwa lengo la kuwashukuru kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

  Shonza ambaye aliongozana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve, alisema  katika kuhakikisha adhima yake  ya kuwanua wanawake hao inatimia ameanzisha mfuko maalumu alioita ‘Songwe Women Foundation”   utakaolenga kuwasaidia wanawake wa umoja huo.
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (kulia) akimsisitiza jambo Mbunge mwenzie wa Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza jana wakati Shonza alipokutana na Wajumbe wa Baraza la Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Momba mjini Tunduma kwa lengo la kuwashukuru wajumbe hao kwa kumchagua kuwa mbunge wa viti maalum mkoani hapa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

  “Ninawaombeni sana undeni vikundi, hakikisheni mnavisajili na fedha ya kusajili vikundi vyenu nitatoa mimi, na nimeanzia mfuko maalum kwa ajili ya wanawake wote wa mkoa wa Songwe, na nimeweka Sh 20 milioni na kila kikundi kwenye kata zenu mtapewa Sh200,000 kwa ajili ya kuanzisha  mradi mtakaona unafaa. Niliwaahidi kuwainua nitafanye mtakavyotaka nyinyi.

  Kupitia mfuko huo, nitataka mniambie ni mradi gani mnataka kuufanya. Lakini mbali na kuwawezesha kifedha lakini kabla ya kuanza kuanzisha mradi huo kwanza nitawaletea wataalamu wa masomo ya ujasiriamali watawafundisha ili iwasaidie kuendesha mradi wenu,” alisema Shonza.

  Alisema kupitia mfuko huo, tayari ameanza kuzungumza na wadau mbalimbali watakaomsadia kuwawezesha wanawake wa mkoa wake kujikwamua kiuchumi huku akiwasisitizia kuchapa kazi bila kuchoka wala kubweteka kwa vile wanapata msaada kutoka kwake.
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza, akizungumza na wanawake, Wajumbe wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Momba Mkoa wa Songwe, jana alipokutana nao mjini Tunduma kwa lengo la kuwashukuru kwa kumchagua kwake katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Iringa, Tweve aliyemsindikiza Shonza kuzungumza na wanawake hao, aliwataka wanawake wa Songwe kujivunia mbunge wao (Shonza) kwani ni mchapa kazi na ni mtu mwenye mtandao npana ambao utawawezesha  kujikwamua kiuchumi.

  “kwanza ninawashukuru sana wanawake wa Momba, na Songwe kwa ujumla kumuamini motto wenu huyu Shonza, ni muda mfupi nimefahamiana naye. Na hii ni kutokana na uchapa kazi wake, ninaombe mtumieni vyema bila kusahau na nyinyi kufanya kazi bila kuchoka.” Alisema Tweve.

  Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Momba, Isavera Mwanisenga alisema CCM katika uchaguzi uliopita walipoteza majimbo yote mawili ya Momba na Tunduma hivyo lakini bado hawajafa moyo kwani bado wanaye mbunge Shonza anawapigania huku wakiendelea kujipanga kurudisha majimbo hayo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
  Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve (kulia) akimsisitiza jambo Mbunge mwenzie wa Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza jana wakati Shonza alipokutana na Wajumbe wa Baraza la Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Momba mjini Tunduma kwa lengo la kuwashukuru wajumbe hao kwa kumchagua kuwa mbunge wa viti maalum mkoani hapa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

  Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Songwe, Juliana Sonza (katikati) na Mbunge mwenzia wa Mkoa wa Iringa, Rose Tweve ( wa tatu kushoto) wakiserebuka na wajumbe wa Baraza la Wanawake wa CCM Wilaya ya Momba (UWT) Mkoa wa Songwe, jana walipokutana nao mjini Tunduma kwa lengo la kuwashukuru kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana kupitia UWT.

  0 0

  Wakazi wa Mlandizi mkoa wa pwani na vitongoji vyake,Wamerahisishiwa jinsi ya kupata huduma mbalimbali za huduma za mawasiliano kwa kuzinduliwa kwa duka jipya na la kisasa la Vodacom Tanzania lililozinduliwa leo ukiwa ni mkakati uliowekwa na kampuni hiyo kwa kusogeza huduma za mawasiliano karibu na wananchi nchini kote.Mwaka huu kampuni hiyo imedhamiria kufungua vituo vipatavyo 500 nchini kote. 
  Kituo hiki kipya kinatarajia kutoa huduma kwa wateja wa Vodacom wanaoishi Mlandizi na vitongoji jirani ambao walikuwa wanatembea  mwendo mrefu kufuata huduma pia kitahudumia wasafiri  mbalimbali wanaotumia barabara ya morogoro. 
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh amesema  kuwa mkakati huu wa kufungua vituo vya kutoa huduma za Vodacom umebuniwa ili kuwapunguza wateja adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma. 
  “Kwetu Vodacom wateja wetu ni wafalme na tunasikiliza ushauri wao,pamoja na kuwa na maduka sehemu mbalimbali lakini bado tumeona kuna haja ya kuwasogezea zaidi huduma wateja  wazipate popote pale walipo na kwa wakati wowote”.Alisema.
  Aliongeza kuwa  kupitia huduma hii ya  vituo vya mauzo kampuni itazidi kupanua wigo wa ajira nchini kwa kuwa watanzania zaidi ya 1000 watanufaika na mpango huu na  ni utekelezaji wa  moja ya malengo ya kampuni ambayo ni kufanya uwekezaji wenye mwelekeo wa kuwanufaisha watanzania. 
  Akifungua kituo hicho kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Pwani, Kaimu Katibu tawala wa Wilaya hiyo,Anathory Mhango aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kusambaza huduma zake karibu na wateja na aliwataka  wakazi wa Mlandizi kutumia huduma za mawasiliano kwa ajili ya kurahisisha maisha. 
  Mmoja wa wakazi wa Mlandizi Sheikh Daruwesh Mohamed Luhanjo akiongea kwa niaba ya wakazi wenzake alisema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo kutawapunguzia kero wakazi wa eneo hilo kutembea umbali mrefu kufuata huduma za Vodacom “Tunashakuru Vodacom kwa kutukumbuka wana Mlandizi”alisema
   Kaimu Katibu tawala wa Wilaya ya Kibaha,Anathory Mhango(watatu kushoto) kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo akikata utepe kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo Mlandizi Mkoa wa Pwani,Wengine kutoka kushoto Meneja wa duka hilo,Godfrey Lyimo,Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu,Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja Vodacom,Brigita Stephen na Meneja Mauzo wa kanda hiyo,James Kigodi.

   Kaimu Katibu tawala wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani,Anathory Mhango(wapili kushoto) kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo na Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja Vodacom Tanzania,Brigita Stephen(kushoto)wakimshuhudia Meneja Mauzo wa kanda hiyo,James Kigodi(kulia)akimsajilia namba za simu mteja wa kwanza Janeth Mnzava wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo”Service desk” lililopo Mlandizi.
   Kaimu Katibu tawala wa Wilaya ya Kibaha,Anathory Mhango(wapili kushoto) kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo akigonganisha glasi na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakati wa uzindua wa duka jipya la kampuni hiyo”Service desk” lililopo Mlandizi.
   Kaimu Katibu tawala wa Wilaya ya Kibaha,Anathory Mhango(wapili kushoto)kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo akikata keki kuashiria uzindua wa duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo Mlandizi Mkoa wa Pwani,Wengine kutoka kushoto Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu,Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja Vodacom,Brigita Stephen na Meneja Mauzo wa kanda hiyo,James Kigodi.

  Mkazi wa Mlandizi Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani,Darueshi Luwanja akilishwa keki na Kaimu Katibu tawala wa Wilaya hiyo,Anathory Mhango kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo,wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo Mlandizi,Wengine kutoka kushoto,Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu,Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja Vodacom,Brigita Stephen na Mkazi wa eneo hilo Abdallah Ahmed.


  0 0

  Mwenyekiti wa Mfuko wa mchezo wa Chess Tanzania (TCF) Bw. Vinay Choudary akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Ubingwa wa Afrika, Kanda ya 4.2 ya mchezo huo jana jijini Dar es Salaam. Kanda ya 4.2 inahusisha nTimu kutoka nchi za Misri, Ethiopia, Eritria, Sudan, Sudani Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia,Djibouti na wenyeji Tanzania.Mashindano hayo yameanza jana tarehe 23 April hadi April 31ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Chess Tanzania (TCA) Bw. Geofrey Mwanyika akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Ubingwa wa Afrika, Kanda ya 4.2 ya Mchezo huo jana jijini Dar es Salaam. Kanda ya 4.2 inahusisha Timu kutoka nchi za Misri, Ethiopia, Eritria, Sudan, Sudani Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia,Djibouti na wenyeji Tanzania.
  Rais wa Chama cha Mchezo wa Chess Malawi, ambaye pia ni ni Mbunge mstaafu wa wa Bunge La nchi hiyo Mhe. Kezzie Msukwa akizungumza namna Mhcezo huo Mchezo huo ulivyopiga hatua nchini Tanzania ukilinganisha na kwao jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Ubingwa wa Afrika, Kanda ya 4.2 ya Mchezo huo jana jijini Dar es Salaam. Kanda ya 4.2 inahusisha Timu kutoka nchi za Misri, Ethiopia, Eritria, Sudan, Sudani Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia,Djibouti na wenyeji Tanzania. Mbunge huyo wa zamani wa Malawi yupo nchini kama Mwamuzi katika mashindano hayo.

  Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya Ubingwa wa Chess Afrika, Kanda ya 4.2 kimchezo huo wakiendelea kuchuana jana jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yanendelea katika Ukumbu uliopo Hotel ya Peackok ambapo mshindi katika mashindano hayo atajinyakulia kitika cha Euro 3000.
  Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya Ubingwa wa Chess Afrika, Kanda ya 4.2 kimchezo huo wakiendelea kuchuana jana jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yanendelea katika Ukumbu uliopo Hotel ya Peackok ambapo mshindi katika mashindano hayo atajinyakulia kitika cha Euro 3000.

  0 0

  Mwanamuziki nguli wa Congo Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba maarufu kama Papa Wemba amefariki dunia huko Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia leo.
  Habari zilizotufikia hivi punde zinasema marehemu Papa Wemba amefia hospitali alikokimbizwa mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu wakati akiwa katika onesho jukwaani.
  Papa Wemba alizaliwa June 14, 1949 huko Lubefu katika wilaya ya Sankuru nchini Congo. Alijipatia umaarufu sana kwa sauti nyororo na midundo ya Soukous ulimwenguni kote, ikiwamo Tanzania ambako amezuru mara kadhaa na kujizolea mashabiki wengi.
   Papa Wemba akiwa jukwaani kwa mara ya mwisho jijini Abidjan, Ivory Coast, usiku wa kuamkia
   Papa Wemba aanguka na kupoteza fahamu katikati ya onesho
  Wafanyakazi wa huduma ya kwanza wamepanda jukwaani. Hali ilizidi kuwa mbaya wakamkibiza hospitali ambako alikata roho

  0 0


  0 0   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kati) akiwasili jijini Dar es salaam jioni hii, akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, alioongozana nao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akionyesha kwa wanahabari, mpango wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda mpaka Jijini Tanga, mara tu baada ya kuwasili nchini akitokea jijini Kampala. Mbali na kunufaika kwa Watanzania kupitia Mpango huo, pia utazinufaisha nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio walipokuwa wakimsubiria Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alierejea jijini Dar es salaam leo akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga. 


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Jerry Sabi akiongea na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TAHLISO Bw. Stanslaus Kadugalize.
  Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) kutoka Chuo Kikuu cha Bugando Bw. Elia Kandonga akiongea katika mkutano kati ya TAHLISO na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na kufanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya wahitimu bora wa vyuo vikuu mbalimbali wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandishi Stella Manyanya katika hafla iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) ili kuwapongeza na kufanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) kutoka vyuo mbalimbali nchini katika picha ya kumbukumbu na viongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) waliokutana katika Chuo Kikuu cha Mt. John mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

  Viongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) wamekutana mjini Dodoma mwishoni mwa wiki ili kubadilishana mawazo na kukubaliana kuendeleza ushirikiano ili kutatua kero za wanafunzi.

  Katika mkutano huo, uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu John, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TAHLISO kutoka taasisi za elimu ya juu nchini wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bw. Peter Kadugalize walikutana kwa siku nzima na viongozi wa HESLB walioongozwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Jerry Sabi na kujadiliana njia bora za kutatua kero za wanafunzi.


  0 0

  Mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Tovako Manongi akimkaribisha Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga nyumbani kwake siku ya Jumamosi April 23, 2016.Mkurugenzi huyo alitembelea nyumbani kwa Balozi jijini New York akiongozana na baadhi ya wafanyakzi wake ambao walikuja nchini Marekani kwa ajili ya tamasha la Radio lililofanyika jijini Las Vegas. Picha na Vijimambo New York.
  Mhe. Balozi Tuvako Manongi akiwatambulisha maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa kwa Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bwn, Joseph Kusaga (hayupo pichani) siku ya Jumamosi April 23, 2016.
  Mkurugenzi wa Clouds Media Group Bwn. Joseph Kusaga akitambulisha timu yake kwa Mhe. Balozi Tuvako Manongi.
  Mhe. Balozi Tuvako Manongi, mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bwn. Joseph Kusaga.
  Mkurugenzi wa Clouds Medea Group, Bwn. Joseph Kusaga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Tuvako Manongi na mkewe.
  Timu nzima ya Clouds Media Group iliyohudhuria Tamasha la Radio nchini Marekani ikiwa katika picha ya pamoja na Balozi Tuvako Manongi na mkewe.Kutoka kushoto ni Saleh Mohammed, Daudu Lembuya, Dj Venture, Mhe. Balozi Tuvako Manongi, Mkurugenzi Joseph Kusaga, Mama Manongi, Dj Peter Moe na Jackson Joseph.


  0 0


  Na Woinde Shizza,Arusha

  Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na michezo nchini,Nape Nnauye ametaja
  mambo manne ambayo ni vikwazo ndani ya sekta ya sanaa ya filamu nchini
  na kuyaita kwamba ni majipu huku akisisistiza kwamba serikali
  itakwenda kutunga sera ya sekta hiyo katika mwaka wa fedha 2016/17.

  Nape,aliyataja mambo hayo na kuyafananisha na majipu kuwa ni uporaji
  wa kazi za wasanii nchini,ujenzi duni wa miundombinu ya kazi za
  wasanii nchini,usimamizi mbovu wa bodi ya filamu nchini sanjari na
  tatizo la mfumo mbovu wa usambazaji wa kazi za wasanii nchini.

  Akizindua tamasha la filamu la Tanzanite International Film
  Festival(TIFF) jijini Arusha juzi ambao ulihudhuriwa na wasanii
  maarufu wa filamu nchini waziri huyo alisema kwamba jipu la kwanza
  ambalo atakwenda kulitumbua ni uporaji wa kazi za wasanii nchini.
  “Jipu la kwanza tutalitumbua kwenye bajeti yetu ya mwaka 2016/17 ni
  uporaji wa kazi za wasanii nchini wengi wananyonywa jasho lao”alisema
  Nape

  Hatahivyo,alisema kwamba jipu la pili ni ujenzi duni wa miundombinu ya
  kazi za wasanii za filamu nchini na kudai kwamba chini ya uongozi wake
  atahakikisha anaimarisha miundombinu bora kwa lengo la kuwasaidia
  wasanii hao pamoja na kulinda haki zao.

  Alisema ya kwamba mfumo wa kazi za usambazaji wa kazi za wasanii
  nchini pamoja na hakimiliki ni wa kinyonyaji huku akitolea mfano wa
  kazi za msanii maarufu wa sanaa hiyo nchini marehemu Stephen Kanumba
  na kusema kwamba familia yake hainufaiki na matunda ya kazi zake hadi
  sasa kutokana na mfumo mbovu wa usimamizi wa kazi za wasanii nchini.

  Alitaja takwimu kwamba mwaka 2011/12 jumla ya filamu 218
  zilitengenezwa nchini na mwaka 2014/15 kazi hizo ziliongezeka hadi
  kufikia 14,00 huku akidai hilo linadhihirisha kwamba sekta hiyo inakua
  kwa kasi nchini na kuongeza ajira .

  Hatahivyo,Rais wa shirikisho la wasanii wa filamu nchini(TAFF),Simon
  Mwakifamba aliwataka wasanii wa filamu nchini kujiandaa kisaikolojia
  kukabiliana na soko la ushindani wa filamu duniani kwa kuwa wabunifu.

  “Serikali tunaiomba iandae sera itakayoandaa mazingira mazuri kwa
  wasanii nchini kuhusu usalama wa kazi zao”alisema Mwakifamba

  Naye, muaandaji wa tamasha hilo,Said Sassi alisema kwamba tatizo la
  uharamia wa kazi za wasanii nchini limetanda na kuwaomba
  wafanyabiashara na makampuni kujitokeza kudhamini vipindi mbalimbali
  vya luninga kwa lengo la kuinua sekta hiyo.

  Mkurugenzi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya vito ya Tanzanite One
  Mining Ltd ambao ni miongoni mwa wafadhili wa tamasha hilo,Feisal
  Shabhai alisema lengo la kampuni yao kujitosa kufadhili tamasha hilo
  ni kutoa mchango wao katika kusaidia jamii kupitia faida wanayoipata
  ili kuinua sekta ya ajira nchini.

older | 1 | .... | 1196 | 1197 | (Page 1198) | 1199 | 1200 | .... | 3272 | newer