Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

IDADI YA WATUMISHI HEWA IRINGA YAONGEZEKA NJE YA ILE ALIYOPEWA RAIS MAGUFULI

$
0
0
 Mkuu  wa  mkoa wa  Iringa Mhe. Amina  Masenza  akizungumza na  wanahabari  mjini Iringa leo 
 
Ndugu Waandishi wa Habari,
Hadi kufikia tarehe 18/04/2016 Mkoa wa Iringa umefanya zoezi la uhakiki wa watumishi kwa awamu mbili awamu ya kwanza, uhakiki ulifanyika kuanzia tarehe 16/03/2016 na kukamilika tarehe 26/03/2016 ambapo jumla ya watumishi 15walibainika kuwa ni watumishi hewa katika Mkoa wa Iringa ambao waliisababishia Serikali hasara ya Shilingi 81,921,725.08. 
Katika uhakiki wa awali Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo haikuwahakiki watumishi 159 kutokana na kuwa masomoni. Halmashauri hiyo imekamilisha uhakiki huo ambapo imebainika watumishi wawili (2) ni watumishi hewa.
 
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ili kuhakikisha Mkoa unaondokana kabisa na tatizo la watumishi hewa, niliwaelekeza Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri kufanya zoezi hilo awamu ya pili. 
 Nimepokea taarifa kutoka kwa Wakuu wa Wilaya inayoonesha kuwapo kwa watumishi hewa kumi na mbili (12) hadi kufikia tarehe 18/04/2016. Watumishi hao wameisababishia Serikali hasara ya shilingi 155,205,681/=

Watumishi hao wapo katika mchanganuo ufuatao:
NA
HALMASHAURI
WATUMISHI HEWA WALIOBAINISHWA AWALI
WATUMISHI HEWA WALIOBAINISHWA SASA
JUMLA
1
H/W Iringa
2
7
9
2
H/W Kilolo
6
2
8
3
M/Mji Mafinga
3
0
3
4
H/W Mufindi
4
0
4
5
H/Manispaa
0
3
3
JUMLA
15
12
27
 Uhakiki uliofanywa na Mkuu wa Wilaya katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa umebainisha kuwapo kwa watumishi tisa (9) ambao ni watoro na mtumishi mmoja ambaye aliomba likizo bila malipo na kwenda kufundisha mahala pengine lakini akaendelea kulipwa mpaka kufikisha  kiasi cha Tsh. 25, 831,000/= lakini baada ya kufanya ufuatiliaji amerejesha kiasi cha Tsh. 18,604,679/= Mtumishu huyu ni mwalimu anaitwa Dinner J. Kissamo alikuwa mwalimu Manispaa ya Iringa.   
Aidha, Uhakiki pia ilibaini mwalimu mmoja (Ifunda) alikuwa na Check Na. 2 na zote alikuwa analipwa na halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika. 
Mtumishi Mwingine ni Khalid M. Meza Afisa kilimo Kilolo ni  mtoro wa muda mrefu mkurugenzi tayari ameshamfungulia mashtaka. Hii ni mifano tu ya watumishi hewa.
 
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ili kuendelea kujiridhisha  na kuondolewa kabisa watumishi hewa katika Mkoa wa Iringa, nimechukua hatua zifuatazo;

1.    Nimewaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kuwa, zoezi la uhakiki watumishi linakuwa endelevu na hatua zinachukuliwa ili kuwaondoa watumishi hewa wote           

TAARIFA YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA ND. DAVID MHINA UINGEREZA

$
0
0

Tunapenda kuwaarifu ndugu, Jamaa na Marafiki kuwa tutakuwa na kikao cha maombolezi ya msiba wa Ndugu yetu David Mhina aliyefariki ghafla hapa London. Kikao hicho kitafanyika siku ya leo tarehe 23/04/2016 kuanzia saa kumi jioni.

Adress ya makutano yetu ni,
15 Manse Close, Hillingdon, UB3 5ED.

Titashukuru Pia kwa msaada wa mchango wako 


ambao unaweza ukaweka kwenye account hii👇👇

METRO BANK,
Acc No. 10919417
Sort code 23-05-80.
Name- Michael Ananias Mwanga.

Tunashukuru Sana kwa ushirikiano wako na ni mategemeo yetu kuwa utajumuika nasi kwenye maombi ya ndugu yetu David Mhina

Namba ya dada wa mfiwa.
Mrs. RHODA FRANSIS MWANGA- 07974332047.
Ahsanteni Sana.

MBAO FC YAPANDA LIGI KUU

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitangaza klabu ya Mbao FC ya jijini Mwanza kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao kutoka katika kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza chini (StarTimes League).

TFF imeitangaza Mbao FC kfuatia maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF yaliyotolewa April, 2016 ya kuzishusha daraja timu nne kutoka kundi C baada ya kukutwa na hatia ya upangaji matokeo.

Mbao FC imeshika nafasi ya kwanza kundi C kwa kuwa na pointi 12 baada ya kufutwa kwa matokeo ya timu za Geita Gold, Polisi Tabora, JKT Oljoro na JKT Kanembwa zilizokumbwa na mkasa huo wa upangaji matokeo.

Timu ya Mbao FC inapanda ligi kuu (VPL) msimu ujao, sambamba na timu za African Lyon ya jijini Dar es salaam pamoja na Ruvu Shooting ya mkoa wa Pwani.

Wakati huo huo kikao cha Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF kinatarajiwa kukaa Jumamosi ijayo April, 30 jijini Dar es salaam kujadili rufaa mbalimbali ambazo zimekatwa na kutokana na maamuzi ya kamati ya Nidhamu ya TFF.

Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF itasikiliza rufaa za wafuatao waliokata rufaa

(i) Saleh Mang’ola,

(ii) Yusuph Kitumbo,

(iii) Amos Mwita,

(iv) Fateh Remtullah,

(v) Timu ya JKT Oljoro,

(vi) Timu ya Polisi Tabora.

Aidha Kamati ya Nidhamu ya TFF itakutana Jumapili Mei Mosi kupitia taarifa mbalimbali zilizowasiliswa katika kamati hiyo.

CDA,Uchukuzi SC zaendeleza ubabe Mei Mosi

$
0
0
Mshambuliaji Ramadhani Madebe wa Uchukuzi SC akikokota mpira katikati ya uwanja, huku Mohamed Salum wa GGM akimsogelea. Timu hizo zimetoka satre ya bao 1-1.
Issack Ibrahim (mwenye mpira) akimtoa Fernand Makanga wa GGM akimzuia asilete madhara. Timu zilitoka sare 1-1.
Mshambuliaji Oswald Binamungu wa GGM akitafuta mbinu za kumtoka Ally Poloto wa Uchukuzi SC. Timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI

MKUU WA MKOA WA DODOMA AKUTANA NA BALOZI WA USWISI HAPA NCHINI NA KUZUNGUMZIA SUALA LA AJIRA KWA VIJANA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely Mattli (kulia) na ujumbe alioambatana nao wakati walipo mtembelea Mkuu huyo wa Mkoa ofisini kwake mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely Mattli (wa pili toka kulia) na ujumbe alioambatana nao wakati walipo mtembelea Mkuu huyo wa Mkoa ofisini kwake mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana amemuomba balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli kusaidia kuunga Mkono jitihada za Serikali ya Mkoa wa Dodoma za kuongeza ajira kwa vijana kupitia shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma mbalimbali.

Mhe. Rugimbana alimweleza balozi wa uswisi hapa nchini kuwa moja kati ya vipaumbele vyake kwenye Mkoa wa Dodoma ni kuzalisha ajira kwa vijana kupitia uundaji wa makambi ya vijana ya uzalishaji mali na shughuli za kiuchumi kupitia sekta za kilimo, ufugaji na utoaji huduma mbalimbali, jambo ambalo hata viongozi wakuu wa kitaifa wamekuwa wakisisitiza.

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokutana na balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely Mattli na ujumbe wake wakati walipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo hapa Mkoani Dodoma na miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Uswisi

Katika kufanikisha azma hiyo Mhe. Rugimbana alisema kuwa serikali ya Mkoa wa Dodoma imejipanga kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa wadau mbalimbali wa maendeleo wanaofadhili miradi ya huduma za jamii na uzalishaji mali, na kuongeza kuwa kwa sasa serikali ya awamu ya tano imejikita katika kutaka wananchi kufanya kazi hususani vijana kuachana na mambo ambayo yanawapotezea muda bure kama michezo ya ‘pool’ badala yake wajikite kwenye shughuli za uzalishaji mali, lakini pia serikali inajukumu la kuwajengea vijana mazingira mazuri ya kuanzisha shughuli za uzalishaji mali.

Kwa upande wake balozi wa Uswisi hapa nchini Mhe. Florence Tinguely Mattli amemwambia Mhe. Rugimbana kuwa Nchi yake ya Uswisi na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa karibu wa muda mrefu na imekua ikifadhili miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma za jamii. Aliongeza kuwa katika ushirikiano huo Mkoa wa Dodoma ni moja kati ya Mikoa waliyoipa kipaumbele.

Alisema nchi yake inaunga Mkono jitihada za serikali za kuongeza ajira kwa vijana kupitia mradi wa Kuongeza Fursa za Ajira kwa Vijana kupitia shughuli za uzalishaji mali za kilimo, mifugo na usafi wa mazingira ambao unawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 30 ambao hawana ajira, wale ambao hawakupata nafasi za kupata elimu na wale walio vijijini na hususani wale wenye malengo ya kupata ajira au kujiajiri kupitia fursa mbalimbali zilizopo kwenye maeneo yao.

Mradi huu unafadhiliwa na kutekelezwa na shirika la maendeleo na ushirikiano la Uswisi (SDC) kwa kushirikisha wadau wengine wa maendeleo kama vile shirika la kimataifa la maendeleo la Uholanzi (SNV) ambapo awamu ya kwanza itaanza 2016 hadi 2018 na utajumuisha mikoa ya ukanda wa kati ikijumuisha Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga na pia Morogoro kwa mwaka wa 2016 pekee umetengewa jumla ya Euro 1.4 Milioni

Balozi Florence Tinguely Mattli aliongeza kuwa mradi huo utahusu kuwawezesha vijana eneo la utaalamu na mafunzo ya ufundi na stadi za maisha, na pia uwezeshaji wa uanzishaji miradi ya uzalishaji mali baada ya mafunzo. Alisema kupitia miradi ya uzalishaji kwenye kilimo, ufugaji nishati na usafi na utunzaji Mazingira, vijana wataboresha hali za maisha yao na kujipatia ajira na kipato.

Alisema changamoto inayoikabili sekta ya ajira kwa vijana ni pamoja na mtazamo hasi na imani haba juu ya uwezo na utaalamu wa vijana hasa upande wa waajiri wa sekta binafsi, lakini pia sekta za uzalishaji mali alizozitaja hapo juu bado hazijaweza kutoa mchango unaoridhisha kwa Taifa, wakati zinafursa nyingi za kuzalisha ajira kwa vijana na kuchangia pato la taifa.

WIZARA YA UJENZI ,UCHUKUZI NA MAWASILIANO YAENDELEA NA MCHAKATO WA UKUSANYAJI MAONI JUU YA UBORESHAJI SERA YA TAIFA YA (TEHAMA)MKOANI MBEYA

$
0
0

Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Simu katika Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera akizungumza na wanahabari katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu jijini Mbeya( TIA ) juu ya zoezi la uchukuaji maoni na ushauri kwa wadau katika kuboresha sera ya Taifa ya Habari ,Teknologia na Mawasiliano (TEHAMA). 
Mhandisi Enock Mpenzwa Idara Mawasiliano toka Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Forest jijini Mbeya waliofika kwa ajili ya zoezi la utoaji maoni na ushauri juu ya uboreshaji wa sera mpya ya Taifa ya TEHAMA katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu TIA jijini Mbeya April 22, 2015. 
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Forest jijini Mbeya wakiwa katika foleni ya kujiandikisha ili kutoa maoni yao na ushauri juu ya uboreshaji wa sera ya Taifa ya TEHAMA,zoezi ambalo limefanyika katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu Mbeya (TIA) April 22 ,2015.
Mwanafunzi shule ya sekondari Forest jijini Mbeya Mariam Jordan akijiandikisha kwa ajili ya kutoa maoni yake katika zoezi la uboreshaji wa sera ya Taifa ya TEHAMA zoezi ambalo limeratibiwa na Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ,katika viwanja vya Chuo Cha Uhasibu Jijini Mbeya (TIA).

BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI

Selous Game Reserve

$
0
0
Large numbers of cheetahs, African elephants, Masai lions, plus a variety kind of wild animals are found in this Game Reserve, one of the best fauna park in the world.


Tanzania has the best 7 World heritage sites recognized by UNESCO, which are Ngorongoro Conservation Area, Ruins of Kilwa Kisiwani and Ruins of Songa Mnara, Serengeti National Park, Kilimanjaro National Park, Stone Town of Zanzibar, Kondoa Rock-Art sites andSelous Game Reserve. The latter, which is 50,00 km2 size of many foreign countries, shows the unique features around the world. 
Jovago Tanzania, the hotel booking website has revealed that the property contains a variety of mammals than any other area; it contains a population of African Elephants (106,300), wild hunting dogs, the largest Hippopotamus and Buffaloes antelope, and more than 80,815 Nyasa wildebeest. 
However, amongst others, Selous Game Reserve Park has a lot of vegetation zones with the thickest wooded grassland. 
Miombo woodlands are the dominant vegetation of the reserve. Besides, you can visit the rocky acacia clad hills and ground water forests. 
“We receive a huge number of tourists in the most popular destinations like Kilimanjaro, Zanzibar and Serengeti National Park, but we guarantee Selous Game Reserve is one of the best destinations that you would never regret to spend your time with”. Andrea Guzzoni, Country Manager of Jovago Tanzania. 
There are comfortable accommodations around the park. The best luxurious tented camps and Lodges with the finest views are mainly concentrated on the northern and western Part of the park. They include Rufiji River Camp, Sable Mountain Lodge, Lake Manze camp, Ndovu camp and Selous Mbuyu Safari Camp. 

In Addition, It is easily accessible by Road, Flight or Railway. It is the largest game reserve in Africa, as you can depart from any regions in Tanzania between Morogoro, Coastal regions, Lindi, Mtwara, and Ruvuma. It's also easier to take a flight from Dar es Salaam, Arusha and Zanzibar.

Wahandisi Temesa watunukiwa vyeti

$
0
0
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme(TEMESA) Mhandisi Manase Ole Kujan, amewatunuku baadhi ya waandisi na mafundi  wakati  akifunga mafunzo ya umeme wa jua (Solar Photovoltaic Technology) kwa watumishi wa TEMESA.

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa wiki mbili, yametolewa kwa kushirikia na chuo kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Fizikia, kwa watumishi 20 wa TEMESA kupata mafunzo ya nadharia na vitendo.

Katika hotuba yake Mhandisi  Manase aliushukuru uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuendesha mafunzo hayo kwa wataalamu wa TEMESA, kwani yatawapa uwezo wahandisi na mafundi wa kuendana na mabadiliko ya sayansi na tekenolojia.

“Nishati ya umeme wa jua imeshika kasi kwa sasa na inatumiwa sana katika maeneo ambayo umeme wa kawaida haujafika hivyo basi kwa mafunzo haya wahandisi na mafundi wetu wataweza kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuandaa na kutekeleza miradi itakayosaidia kuondokana na tatizo la umeme nchini.” Alisema Mhandisi Manase.

Aidha, TEMESA inasimamia miradi mbali mbali ya teknolojia ya umeme wa jua nchini ikiwemo mfumo wa teknolojia ya umeme wa jua kwa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Songea, mfumo wa teknolojia ya umeme wa jua katika ofisi ya Rais Utumishi, kusimamia na kuhakiki mifumo ya  teknolojia ya umeme wa jua inayofungwa  vijijini katika mikoa ya Geita, Kigoma Ruvuma na Tabora iliyo chini ya REA, kusimamia matengenezo ya mifumo ya teknolojia ya umeme wa jua katika ofisi zote za TRA pamoja na miradi mbali mbali ya taa za kuongozea magari barabarani zinazotumia teknolojia ya umeme wa jua.
Dr. Brenda Kazimili kutoka kitengo cha Fizikia Chuo kikuu cha Dar es Salaam, akielezea umuhimu wa mafunzo ya teknolojia ya Umeme wa Jua(Solar Photovoltaic Technology) yaliyotolewa kwa Watumishi wa TEMESA wa tatu kulia ni Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan.
Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan akikabidhi cheti kwa Mhandisi Amani Mwanga baada ya kuhitimu mafunzo ya teknolojia ya umeme wa jua (Solar Photovoltaic Technology)
Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan akikabidhi cheti kwa Mhandisi Sara Moses baada ya kuhitimu Mafunzo ya teknolojia ya umeme wa jua (Solar Photovoltaic Technology).
Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Manase OleKujan ( wa sita kulia waliosimama) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa Mafunzo ya teknolojia ya umeme wa jua (Solar Photovoltaic Technology) kutoka TEMESA. (Picha Zote na Theresia Mwami wa TEMESA).

MIZANI YA WIKI NDANI YA AZAM TV 2 NA JAMALY HASHIM

$
0
0
 Usikose kuangali kipindi cha Mizani ya Wiki kesho Jumapili kuanzia  saa mbili na nusu kupitia AZAM two ambapo utamsikia Mhe.  Stephen Wassira aliyekuwa waziri wa kilimo na chakula katika serikali ya awamu ya Nnne na Profesa Mwesiga Baregu wakizungumzia mpango wa Taifa wa maendeleo kwa mwaka 2016 - 2020 uliowasishwa na waziri wa fedha na mipango dokta Philip Mpango.
Kwa mara ya kwanza utamsikiliza na kumuona Mze Stephen Wassira ndani ya Azam TV 2

MKUU WA MKOA WA MWANZA JOHN MONGELLA ATOA SAA 24 KOMPYUTA YA HALMASHAURI YA UKEREWE ILIYOIBWA IPATIKANE

$
0
0
Na Afisa habari RS MWANZA.

Mkuu wa mkoa wa MWANZA John Mongella (pichani) ametoa saa 24 kwa kamanda wa Polisi Wilaya ya Ukerewe Ally Mkaripa, kuhakikisha wanaitafuta hadi kuipata komputa iliyoibwa usiku wa kuamkia April 22, 2016 kwenye chumba kinachotumika na mifumo ya ukusanyaji mapato  na uaandaji wa malipo ya Halmashauri (EPICOR)

Mhe. Mongella ametoa agizo hilo wakati  akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri,ambapo taarifa za awali zilionesha kutokea kwa wizi wa komputa moja iliyofungwa kwenye chumba cha mifumo ya komputa ambayo ndio hutumika kuandaa malipo mbali mbali ya halmashauri.

“OCD kesho nitakwenda kanisani asubuhi, ikifika saa 8.00 mchana nataka taarifa niikute mezani kwangu, vinginevyo hatutaelewana", amesema Mongella na kuongeza sisi tunajua nini chakufanya kama kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa lakini na wewe tumia mbinu zako kuweza kubaini wapi ilipo kompyuta hiyo.

Akizungumza kando ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri, kaimu mhazini wa halmashauri hiyo Baraka Munuo, alidai kupokea taarifa za kupotea kwa Komputa hiyo kutoka kwa  afisa TEHAMA wa halmashauri ya Ukerewe akimuelezea upotevu huo.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa MWANZA, amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya  ukerewe,, kupitia mafaili na kubaini watumishi waliofanya kazi katika kituo hicho kwa muda mrefu, jambo ambalo mkuu wa mkoa amedai linachangia watumishi kufanyakazi kwa mazoea.
”Mkurugenzi nakuagiza pitia mafaili ya watumishi ili kubaini wote waliokaa katika kituo hiki kwa muda mrefu. Haiwezekani mtu amekaa hapa miaka ishirini na moja halafu uniambie kwamba atakuwa na maarifa mapya, hapana" alisema Mongella na kuongeza, Sasa nakuagiza pitia mafaili yao na kama kuna mtumishi aliye kaa kwa zaidi ya miaka kumi atafutiwe kituo kingine.

Awali akisoma taarifa ya wilaya hiyo, mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti,alimwambia mkuu wa mkoa kuwa hali ya ulinzi na usalama ni shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo huku akisema wilaya imefanikiwa kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu kilicho kuwa kimepiga kambi katika Wilaya hiyo kwa zaidi ya miezi 6.
Mkuu wa mkoa wa yupo katika ziara yakujitambulisha na hii ikiwa ni wilaya yake ya saba,Mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi, Magu, Nyamagana, Ilemela na Kwimba na hii ya Ukerewe inakuwa wilaya ya saba huku akiwa amebakiza wilaya moja ya Sengerema yenye halmashauri za Buchosa na Sengerema yenyewe.

WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI WAWAFAGILIA SAID SALIM BAKHRESA NA DKT. MENGI

$
0
0

 Mhandisi mitambo wa Azam TV, (kushoto), akiwapatia maelezo ya juu ya chumba cha uthibiti matangazo, (control room), wabunge wa EALA-Tanzania walipotembelea studio za Televisheni hiyo, Tabata jijini Dar es Salaam, Aprili 22, 2016.


NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WABUNGE wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka Tanzania, wamewafagilia wafanyabiashara wakubwa hapa nchini, Dkt. Reginald Mengi na Mzee Said Salim Bakhresa, kwa uthubutu wao wa kutambua na kuzitumia fursa zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwahimiza watanzania wengi kuiga mfano huo.
Pongezi hizo walizitoa Aprili 22, 2016 wakati walipotembelea studio za Azam Media, mwishoni mwa ziara yao ya kuvitembelea vyombo vya habari kwa lengo la kuhamasisha umma wa Watanzania kuchangamkia fursa kwenye Jumuiya hiyo ambayo mwenyekiti wa wabunge hao Mh. Charles Makongoro Nyerere ameiita kuwa ni jumuiya ya watu  wa Afrika Mashariki na sio ya viongozi.
“Napenda kumpongeza sana mzee Said Salim Bakhresa kwa kutambua fursa zilizopo kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo Azam TV inaonekana kwenye nchi kadhaa wanachama wa Jumuiya lakini pia bidhaa za Azam zimesambaa karibu Afrika Mashariki na Kati, na Mzee Mengi pia anastahili pongezi kwa utambuzi wao wa fursa zilizopo kwenye Jumuiya.” Alisema Mh. Shy-Rose Bhanji, ambaye alikuwa miongoni mwa wabunge hao.
Kuna haja ya watanzania kuondokana na dhana ya kujiona wanyonge kwenye Jumuiya hii kwani wanatakiwa kuchangamkia kila fursa iliopo, mfano mimi ni mwalimu wa hisabati, ukijumlisha na Kiswahili, unaweza kupata kazi huko Sudani Kusini na maeneo mengine ya Afrika Mashariki, kwani walimu wa Kiswahili wanahitajika sana, unachopaswa ni kujiongeza tu, unakuwa na kitu kingine cha ziada.” Alisema Mh. Nderaikindo Kessy.
Kwa upande wake, Mh. Abdulla Mwinyi, alisema, wabunge wa EALA kutoka Tanzania, wamefanya jitihada hizo za kutembelea vyombo vya habari kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na waandishi wa habari katika kuhabarisha umma na vyombo vya habari vinao mchango mkubwa wa kutangaza kwa kina fursa za kiuchumi kwenye Jumuiya.
Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kituo cha televisheni cha Azam TV, Mkurugenzi wa uendeshaji vipindi wa Azam TV,  Yahya Mohammed alisema, malengo ya Azam TV ni kufika kufanya kazi zake kwenye nchi zote za Afrika Mashariki, na Kati, ambapo kwa sasa wana soko zuri tu DRC, Rwanda, Uganda. Kenya na Burundi zinajikongoja lakini matumaini makubwa ya kulishika soko la nchi hizo yapo.


 Mh. Shy-Rose Bhanji, (kulia), na Mkuruenzi wa TV, Bi. Jane Shirima
 Mkuu wa chumba cha habari Azam TV, Bw. Hassan Mhelela, akizungumza wakati wabunge hao (hawapo pichani), walipotembelea chumba cha habari
Wabunge wa EALA-Tanzania, kutoka kushoto, Mh. Kessy, Mh. Mwinyi, Mh. Bhanji na Mhe. Makongoro.

TANZANIA YATIA SAHIHI MAKUBALIANO YA MABADILIKO YA TABIA NCHI, MSICHANA GETRUDE CLEMENT KUTOKA MWANZA ATIA FORA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, New York

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni   miongoni mwa  nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa 175 ambao wametia sahihi    kuhusu   Makubaliano ya Mabadiliko ya Tabia nchi ( Paris Agreement) yaliyofikiwa katika mkutano uliofanyika  Jijini Paris- Ufaransa mwezi Desemba 2015.

Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ndiyo aliyepewa dhamana ya kutia sahihi makubaliano hayo kwa niaba ya  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika hafla ya  kihistoria na ya aina yake iliyofanyika siku ya Ijumaa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban  Ki Moon, amesema haijawahi kutokea Mkataba au  Makubaliano ya  Kimataifa kutiwa sahihi na mataifa mengi katika siku ya kwanza  kama  ilivyokuwa  kwa Makubaliano ya Paris.

Mataifa makubwa  na ambayo yanachangia katika utoaji wa  gesi chafu ya ukaa( carbon dioxide) kama Marekani, China, Urusi, India , Ufaranza na mengineyo nayo yameweka sahihi zao.

Aidha, Getrude Clement(16)  kutoka  Mwanza -Tanzania  alizungumza katika hafla hiyo akiwakilisha ujumbe kutoka kwa vijana wenzie duniani kote.

Getrude alizungumza kwa umahiri wa hali ya juu, akianisha mambo kadha wa kadhaa ambayo vijana wa kizazi chake na kijacho wangependa kuona kizazi cha sasa kikiyatekeleza kupitia Makubaliano hayo ya Paris ili  nao  waje kuishi na kuifaidi  Sayari Dunia.

“Mabibi na Mabwana sasa nina mkaribisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa azungumze nanyi. Katibu Mkuu Karibu” akasema Getrude kauli iliyoufanya ukumbu mzima kumpigia makofi

Akizungumza baada ya  kutia sahihi, Balozi Tuvako Manongi, pamoja na  mambo mengine  amesema,  kwa Tanzania kutua sahihi Makubaliano nayo ni  hatua moja  kwenda hatua ya pili ya kuridhia.

Akasema, Tanzania inaserikali  makini na Bunge makini ambalo kwayo limeweka mbele na kutilia mkazo   suala  la utunzaji wa mazingira na kwa sababu hiyo hapana shaka haitachukua muda mrefu wa kuridhia Makubaliaano  hayo. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

 Getrude Clement(16)  kutoka  Mwanza -Tanzania  alizungumza katika hafla hiyo akiwakilisha ujumbe kutoka kwa vijana wenzie duniani kote.
 Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa akitia  sahihi makubaliano hayo kwa niaba ya  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika hafla ya  kihistoria na ya aina yake iliyofanyika siku ya Ijumaa.
 Getrude Clement akiwa na ujumba wa Tanzania  uliongozwa na  Balozi Tuvako Manongi wakati wa utiaji sahihi wa Makubaliano ya Tabia nchi. ( Getrude) ni mwanaharakati wa mazingira kwa kushirikina na UNICEF. 
 Getrude akizungumza kwa umahiri wa hali ya juu, akianisha mambo kadha wa kadhaa ambayo vijana wa kizazi chake na kijacho wangependa kuona kizazi cha sasa kikiyatekeleza kupitia Makubaliano hayo ya Paris ili  nao  waje kuishi na kuifaidi  Sayari Dunia.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliozungumza kabla ya utiaji sahihi wa  Makubaliano  ya Paris kutoka  kushoto ni  Hindou Oumarou Ibrah(Chad) aliwasilisha ujumbe wa asasi za kiraia,  Bw Leonardo Di Caprio mcheza senema maarufu na Mjumbe Maalum kuhusu amani , na  Getrude Clement ( Tanzania) aliyezungumza kwa niaba ya vijana. Msikilize Getrude akiongea umoja wa mataifa mbele ya viongozi wa dunia.

MKUTANO WA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM ZANZIBAR

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Naibu Katibu Mkuu wa CCM ZanzibarVuai Ali Vuai (kulia) na  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi wakiwa katika kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
 Baadhi ya wajumbe wa kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo, katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja wakipitia agenda  kabla ya kuanza kwa kikao hicho  katika ukumbi wa mkutano chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein 
 Baadhi ya wajumbe wa kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Naibu Katibu Mkuu wa CCM ZanzibarVuai Ali Vuai (kulia) na  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi wakiwa katika kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakipiga makofi ka kuimba wimbo wa Chama cha Mapinduzi wakati Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipoingia katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja kilimofanyika leo. Picha na IKULU

BALOZI WA MEXICO NCHINI INDIA ANAYETUMIA RASMI USAFIRI WA BAJAJI

NAIBU MEYA WA MANISPAA YA TEMEKE AFANYA ZIARA CHANG'OMBE JIJINI DAR.

$
0
0

 Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Feythar Salum akionyesha mtalo  kwa watendaji na baadhi ya Madiwani wa  Manispaa hiyo  katika ziara yake iliyofanyika Chang’ombe Polisi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Property Internationa, Abdul  Haleem (mwenye pama)akizungumza na Madiwani pamoja na watendaji wa  Manispaa ya Temeke juu ya kusaidia Manispaa hiyo katika sekta ya elimu kwa dhamira ya kumuunga mkono  Rais Dkt. John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam.

Video ya wimbo mpya wa lady jaydee "ndindindi"

MKUU MPYA WA WILAYA YA MUSOMA MHE HUMPHREY POLEPOLE AAPISHWA RASMI LEO

$
0
0
 Mkuu mpya wa Wilaya wa Musoma Mhe. Hamphrey Polepole  akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Magesa Mulongo tayari kwa kuanza kuitimikia nafasi hiyo.
 Mkuu mpya wa Wilaya wa Musoma Mhe  Hamphrey Polepole, akisaini hati ya kiapo.
Picha ya pamoja ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mara.

KUTOKA MAKTABA: HAYATI MWALIMU ALIKUWA MPENZI WA SOKA, LAKINI.....

$
0
0
 Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akikagua timu wanja wa Taifa miaka ya 1970. Alikuwa mpenzi sana wa mchezo huu hadi pale FAT walipomfedhehesha mbele ya mgeni wake Rais Nimeiry wa Sudan kwa kuleta timu ya Taifa Uwanjani wachezaji wakiwa tumbo wazi mwaka 1972. Toka siku hii hakukanyaga tena uwanja wa soka.
Siku ya Aibu kwa Taifa: Rais Jaafar Muhammad al-Nimeiry  wa Sudan akisalimiana na  Omary Zimbwe. Wengine kutoka kushoto ni Mohamed Chuma, nahodha Mohamed Abdurlahmani,  Kitwana Manara m na Abdallah Kibadeni 

Huu mchezo hauhitaji hasira...

$
0
0
Tawi la Magufuli Klabu ya soka ya Gor Mahia ya Kenya

TANZIA: NDUGU YETU DAVID MASASI WA SWANSEA, UINGEREZA, AFARIKI DUNIA

$
0
0
Ndugu zangu tunatangaza kifo cha ndugu yetu David Masasi (pichani)mkilichotokea jana mji wa  Swansea nchini Uingereza.Marehemu hana ndugu au jamaa wa karibu  mitaa ya Swansea na kwengineko UK.Kama utamaduni wetu tujitahidi kuona kwamba mwili wa marehemu unasafirishwa kwenda Dar es Salaam.Michango yenu ni muhimu sana kufaniksha zoezi hili.

ACCONT DETAILS :
M.UPETE
BACKLAYS BANK
SORT CODE:207103
ACCOUNT:43389219


Kwa tarifa zaidi wasiliana na  KAMATI MAALUM
MR MWAUPETE TEL 07404151936
MR KAPINGA KANGOMA TEL.07535210471
LEYBAB MDEGELA TEL 07545213515
AMRI DELLO

Ili mwana Adam aweze kuishi  maisha yenye maana hapa ulimwenguni na akhera hana budi kuwa na ujuzi wa yakini juu ya lengo,hadhi na dhima aliyonayo  hapa ulimwenguni.Please  kindly toa chochote ulichonacho Mungu atakulipa.Asante
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images