Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI


Tanzania kuwa mwenyeji mkutano wa wafanyabiashara wa Urusi na Afrika

$
0
0
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa kongamano la wafanyabiashara was Urusi la mwaka huu Russia-Africa Forum, mkutano uliopangwa kufanyika Dar es Salaam Jumatano, Waziri wa Biashara, Uwekezaji na Viwanda Charles Mwijage imethibitisha.
"Mipango inafanyika kwa ushirikiano na Serikali ya Urusi na taratibu za maandalizi maandalizi ipo katika hatua za mwisho," alisema waziri mjini Dodoma.

Mkutano huo wa siku mbili uliopangwa kufanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) utahusisha kundi kubwa la wawakirishi wa serikali ya Urusi, wenye viwanda na  wafanyabiashara wakubwa wenye dhamira ya kuboresha mazingira ya biashara.

Katika mkutano Waziri wa Viwanda na Biashara wa Urusi Denis Manturov na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Tanzania Charles Mwijage watatiana saini namna ya kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Mkutano utahusisha kufungua majadiliano juu ya ushirikiano wa makampuni ya Tanzania na Urusi na kutoa fursa kwa Wafanyabiashara wa Urusi, mamlaka za kifedha na serikali ili kupata uelewa mzuri wa uchumi wa Tanzania na kujenga ushirikiano wa pamoja.

"Makampuni ya Russia kuweka vituko juu ya kutumia RAF 2016 kama jukwaa kuchunguza fursa mpya za uwekezaji kama vile kuimarisha zaidi mahusiano ya kiuchumi na biashara na Tanzania," alisema Ekaterina Dyachenko, mkuu wa kamati ya maandalizi ya RAF .

Alisema lengo kuu la biashara lengo ni kuongeza uwepo juu ya soko la Tanzania na kuchunguza namna ya ushirikiano wa kijamii na kiuchumi katika maeneo kama vile kilimo, madini, mafuta na gesi, utalii, miundombinu ya kiuchumi, viwanda, uvuvi, benki na bima kama vile elimu na afya.
"Washa hii pia itatoa fursa za Biashara-kwa-Biashara, Serikali-kwa-Biashara na Serikali-kwa-Serikali. Kutakuwa na ziara katika viwanda vya ndani na wazalishaji kuongeza maarifa na uzoefu pamoja ya maendeleo ya biashara na uwekezaji. "mauzo kati ya Urusi na Tanzania mwaka 2014 yalifikia dola za Kimarekani  milioni 154, na takwimu ya robo ya kwanza ya 2015 ilikua asilimia 71 ya juu kuliko kipindi cha nyuma. 

RAF 2016 inaandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara ( Urusi), Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ( Tanzania), Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Sekta binafsi Tanzania (TPSF).

Wafanyabiashara wa Tanzania watapata fursa kutembelea Ekaterinburg tarehe 12 kwa 14 Julai 2016 wakati wa Maonyesho ya kila mwaka ya INNOPROM ambayo hukutanisha wageni zaidi ya 46 000 kutoka nchi 70 duniani kote.

MASAUNI ASISITIZA USAFI WA MAZINGIRA KIKWAJUNI ZANZIBAR

$
0
0
 WANANCHI wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar, wametakiwa kujenga tabia ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kuepuka maradhi ya kipindupindu yanayoathiri maeneo mbali mbali nchini.

Wito huo umetolewa kwa nyakati tofauti na Mbunge wa jimbo la Kikwajuni, Muandisi Hamad Yussuf Masauni alipokuwa akifanya usafi wa mazingira katika maeneo mbali mbali ya jimbo hilo Mjini hapa.

Alisema maeneo mengi ya jimbo hilo hasa katika Majumba ya Maendeleo ya Michenzani ni machafu sana  hali inayoweza kusababisha maradhi ya miripuko yakiwemo kipindupindu na kichocho.

Masauni ambaye pia ni Naibu Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, alieleza kuwa wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira na kupelekea uharibifu wa miundombinu ya kusafirisha maji taka ikiwemo mitaro kuziba.

“ Nachukua fursa hii kuwakumbusha wananchi wa kikwajuni kuwa suala la usafi wa mazingira halina itikadi za kisiasa ni lazima wananchi sote tuungane bila ya kujali tofauti za kisiasa.

Pia nakuombeni wananchi hasa mnaoishi katika majumba ya michenzani mbadilike kwa kujali mazingira yenu kwani mjue kuwa endapo eneo hili litapata maradhi ya mripuko kuna hatari ya wananchi wengi kupoteza maisha kwa maradhi ambayo tuna uwezo wa kuyazuia.”, alisema Masauni huku akisisitiza umuhimu wa kufanya usafi wa mara kwa mara katika maeneo hayo.

Alisema viongozi wa jimbo hilo kwa sasa wanapanga kuanzisha kikundi maalum cha vijana wa kufanya usafi katika maeneo ya jimbo hilo, ambapo kila kaya(nyumba) watakuwa wanachangia kiasi cha shilingi 200 kila siku ili fedha hizo ziweze kuwasaidia watu wanaofanya usafi huo.

 “Aibu kubwa kuona ndani ya jimbo la kikwajuni panaanza kupatikana wagonjwa wa maradhi ya kipindupindu kwani ni jimbo lenye sifa ya usafi na ukaribmu toka enzi na enzi tena lipo mjini, lazima tushirikiane kufanya usafi katika maeneo yetu.” Alisema Masauni.

Aidha aliishauri Manispaa ya Zanzibar kuanza mara moja utafti wa kubaini mifumo ya maji machafu na masafi inayoingiliana katika maeneo hayo ili kuifanyia matengenezo kwa haraka kabla hapajatokea maafa ya maradhi ya miripuko na kusababisha athari kwa wananchi wa maeneo hayo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salum Ali(Jazeera) aliwapongeza wananchi wa jimbo hilo waliojitokeza kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la kuweka maeneo yako katika hali ya usafi.

Jazeera alisema kwamba kinga ya maradhi ya mripuko hasa kipindupindu ni usafi wa mazingira hivyo kila mwananchi anatakiwa kutekeleza wajibu wake bila ya kulazishwa na mtu.

HARAMBEE KUBWA YAFANYIKA HOUSTON KWA AJILI YA MAREHEMU ANDREW SANGA

$
0
0
Marehemu Andrew Sanga enzi za uhai wake

Jumuiya ya Watanzania wanaoishi katika jiji la Houston, Texas na miji mingine ya jirani jana jioni  (Jumamosi tarehe 24/04/2016) katika ukumbi wa Sienna ulioko mitaa ya Bissonet ilifanya Harambee iliyovunja rekodi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuurudisha mwili wa ndugu ya kipenzi Andrew Nicky Sanga aka Drew. Katika Harambee hiyo jumla ya $52,511 zilikusanywa kutokana na fedha taslimu na minada ya vitu mbalimbali vilivyotolewa na wanajumuiya na marafiki wa Drew kutoka mataifa mbalimbali. Ama kweli Andrew aligusa mioyo ya watu wengi sana katika safari yake hapa duniani. Kamera yetu ilikuwepo ukumbini kukuletea  picha za tukio hilo .
Mchungaji akifungua Harambee kwa sala 
Wanajumuiya wa Houston
Emmy akiwa na Dada wa marehemu
Zoe (binti wa marehemu Drew) akiwa ameshikilia picha ya baba yake 
Wakina dada wa Drew wakiwa na Zoe na mama yake 
Emmy, Zoe na shangazi wa Marehemu Andrew
Julius Shayo wa North Carolina ( rafiki wa karibu wa Drew aliyempokea alipofika USA)
Wanajumuiya wakiwa na familia ya Andrew
Wanajumuiya wakifuatilia Fundraising

Wanajumuiya wa Houston




Emmy akiwa na Erasto Mvungi
Emmy akiwa na rafiki yake
Mrs.Khamsin
Wanajumuiya

Carl Louie, Rah P, Vernis na LBT
Marafiki wa Drew kutoka kushoto Dr.Jenga, John , Ephrahim na Aneth 

























































































































mama vicky Mtwenge aka Vicky Chungu ametoweka toka 2003, watoto wake wanamtafuta

$
0
0
 Mama Vicky Chungu  aka Vicky Mtwenge. 
Tunapata taarifa kuwa amewahi ishi Lushoto na Korogwe  mkoani  Tanga. Alitoweka 2003 mpaka leo hajaonekana.

Watoto wake Yussufu, Farida, Shabani, 
Glory wanamlilia saaana mama yao.
Yusuf Mtwenge +255 766 493 301

SERIKALI YAOMBWA KUTENGA FEDHA KILA MWAKA KWA AJILI YA UKARABATI WA SHULE KONGWE YA ILBORU

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha.
SERIKALI imeombwa kuendelea kutenga fedha za ukarabati kila mwaka kwa shule kongwe ya wanafunzi wenye vipaji maalum ya Ilboru ili walau kuzirudisha katika hali yake nzuri na kuzijengea mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundishia, ili zionekane tofauti na shule zingine hatimaye ziwafanye wanafunzi wajitume zaidi katika masomo.

Hayo yalisemwa jana na mkuu wa shule kongwe ya Ilboru sekondari Julius
Shulla alipokuwa akizungumza na wadau wa elimu na walezi katika mahafali ya 24 ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo.

Alisema kuwa shule hiyo kongwe na ambayo imekuwa ikitoa wataalamu mbali mbali imekuwa ina uhitaji wa kukarabatiwa na hivyo ili kuondokana na hali hiyo serikali inapaswa kutenga fedha kila mwaka ili kuweza kuirejesha shule hiyo katika mazingira mazuri yatakayowavutia wanafunzi.

Alileleza kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu mkubwa wa madarasa na nyumba za watumishi hali ambayo inasababisha mara nyingi wanafunzi kukosa mahala pazuri pa kujifunzia hivyo kuwakatisha tama kimasomo.

“tunaiomba na kuishauri serikali yetu sikivu iendelee kutenga fedha za
ukarabati kila mwaka kwa shule hizi kongwe ili kuzirudisha katika mazingira yake mazuri ikizingatiwa hii ni shule ya wanafunzi wenye vipaji maalum kiakili hali hii itawafnya wanafunzi wajitume zaidi katika masomo kwa kuwa na mazingi mazuri ya kujifunzia”aliongeza Shulla.

Aidha Shulla alitaja changamoto zingine zinazoikabili shule hiyo kongwe
kuwa ni pamoja na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi ambapo hali hiyo inatokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi ikilinganishwa na idadi ya walimu.

Alifafanua kuwa tatizo hilo husababisha shule hiyo kutafuta walimu wa muda wa masomo ya Fizikia,kemia ,na hisabati ambao malipo yao ni makubwa sana kwa mwezi ambapo shule haina uwezo wa kumudu gharama hizo kila mwezi.

Aliwataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata katika kutatua matatizo
yao na matatizo ya jamii yote kwa kufuata sheria na taratibu za nchi huku
wakijiepusha na uzembe ,ulevi,uvutaji bangi na matumiz ya madawa ya kulevya kwani hivyo vyote havina tija katika maendeleo.

DC HAPI ATEMBELEA UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE-MOROCCO LEO.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Salum Hapi leo ametembelea ujenzi unaoendelea wa upanuzi wa barabara ya Mwenge-Morocco kuona maendeleo yake. Barabara hiyo ambayo ilikua na kero kubwa ya foleni iliamriwa kupanuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli katika hatua yake ya kubana matumizi na kupeleka fedha katika shughuli za maendeleo. 

Katika ziara yake hiyo Mh. Hapi alitembea umbali wa mita 500 kwa miguu kukagua pia usafi wa mazingira ya kando ya barabara ambapo alipofika katila kituo cha mafuta cha Total, aliagiza uongozi wa kituo kufanya usafi wa mazingira yaliyo mbele ya kituo chao.

Aidha Mh. Mkuu wa Wilaya pia alizungumza na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam, Mkandarasi na wataalam wengine wa ujenzi na kujua maendeleo yao.

Meneja wa TANROADS na Mkandarasi walimueleza Mkuu wa wilaya kuwa tayari kazi imekamilika kwa asilimia 90 na kwa mbali wanatarajia kukabidhi mwezi June mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akikagua matengenezo ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi leo tarehe 25 Aprili 2016 jijini Dar es Salaam
Mkuu wa wilaya Kinondoni Ally Salum Hapi wa kwanza kulia akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa barabara ya Ali Hassani Mwinyi Halipo tembelea leo kuona maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akiwa na wafanyakazi wa MS ESTIM CONSTRUCTION CO.LTD
Mkuu wa wilaya Mhe.Ally Hapi akiongea na msimamizi wa ujenzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi kushoto akiwa na meneja wa Tanroad katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi leo tarehe 25 Aprili 2016
 

TAASISI YA UPASUJI MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI), KUENDESHA KAMBI YA UPASUAJI MOYO KUANZIA LEO JUMATATU APRILI 25

$
0
0
Taasisi ya Upasuaji Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) itaendesha kambi maalumu mbili za upasuaji moyo kwa kushirikiana na watalaam kutoka nje.
Kambi ya Kwanza: Itaanza leo Aprili 25 hadi 30, 2016. Na kufanya upasuaji wa wagonjwa 25 hadi 30. Kambi hii itashirikisha wataalam toka Australia kupitia Open Heart International.
Kambi ya Pili Itaanza Aprili 30 hadi Mei 7 ambayo itafanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 70. Kambi hii inashirikisha wataalam kutoka Saudi Arabia na London kupitia Al-Muntada Aid.
85%ya wagonjwa wote watakaofanyiwa upasuaji watakuwa watoto.


Article 20

HOSPITALI YA TENGERU INAKABIRIWA NA UHABA WA VITANDA

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

Hospitali ya wilaya ya Tengeru (Patandi) inakabiriwa na ukosefu wa vitanda ,hali inayopelekea baadhi ya wagonjwa kulala zaidi ya mmoja katika kitanda kimoja.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hii,Wagonjwa hao mara baada ya kupokea msaada wa vyandarua kutoka kwa wafanyakazi wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) tawi la Arusha, walisema kuwa wao kama wagonjwa wa hospitali hiyo wamekuwa wakipata tabu sana haswa wakati wakiandikiwa kulazwa,kwani wamekuwa wakibanana sana na wakati mwingine wamekuwa wakikosa kabisa vitanda.

Mmoja wa wagonjwa hao ambaye alijitambulisha kwa jina la Anna Akyoo alisema kuwa wamekuwa wakilala wagonjwa wawili hadi watatu hali ambayo imekuwa ikiwafanya wajisikie vibaya kwani wana banana sana katika vitanda hivyo vichache.
picha ikionyesha wafanyakazi wa NSSF pamoja na Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Tengeru katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi msaada wa vyandarua
wafanyakazi wa NSSF wakiwa wanabadilishana mawazo nje ya hospitali hiyo 
mmoja ya wagonjwa akiwa amekaa kitanda kimoja na watoto wawili wakiwa kila mmoja ana mama yake.
 

Wakazi Kata ya Kibamba wapiga kura kubaini majambazi

$
0
0
Wakazi wa Kata ya Kibamba wamepiga kura ya siri kuwabaini wahalifu wanaoishi katika maeneo yao kufuatia tukio la karibuni la uvamizi katika nyumba nne zilizopo Mtaa wa Muhongoni ambalo limesababisha kifo cha mkazi mmoja wa eneo hilo, aliyejulikana kwa jina la Upigaji kura huo ulifanyika katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na ofisi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo ambao ulifanyika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji wa Kata na kuhudhuriwa na Kamanda wa Polisi wa Kata ya Kibamba, Pius Lutumo.

Uamuzi wa kupiga kura hiyo umetokana na kuanza kuibuka kwa vitendo vya ujambazi unaofanywa majumbani na makundi ya vijana, uporaji wakati wa alfajiri na wizi wa mifugo hali ambayo imesababisha watu kadhaa kujeruhiwa na wengine kupoteza mali zao.

Katika mkutano huo, wakazi hao walikubaliana na kupiga kura za siri ambazo ziliwataja mara nyingi watuhumiwa wa uhalifu sugu wanne ambao Diwani wa Kata hiyo, alisema hata yeye majina yao ameyakuta ofisini kwake hivi karibuni alipoingia madarakani hivi karibuni.

Diwani wa kata hiyo, Ernest Mgawe aliwataka wakazi wa kata hiyo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na ofisi yake hasa pale yanapotokea matukio ya uhalifu nna kukamatwa kwa watuhumiwa ili lengo la kuifanya Kibamba kuwa sehemu salama ya kuishi liweze kufikiwa.

”Tunaomba ushirikiano wenu kwani kuna wakati watu walivamiwa na kujeruhiwa na mmoja kati ya watuhumiwa sugu ambaye pia leo ametajwa lakini hata hivyo wahanga walipotakiwa kwenda olisi kutoa maelezo ili mlenga afikishwe maakamanbi hawakuonekana” alisema.

Awali Kamanda wa polisi wilaya ya kipolisi ya ibamba aliwataka wananchi watambue kuwa suala la ulinzi na usalama ipo miononi mwao kutokana na hali halisi ilivyo hvi sasa na kuwataka waachane na nadhjaria kuwa polisi ndi walinzi wao na mali zao.

“Hilo mnapaswa kjulitambua na kulingana na sheria ndogo zilizotungwa katika manuspaa ya ionondoni suala la ulinzi shrikishi sio iyari hasa pa,e wananchi wanapokubaliana upitia mikutano yao halali kma huo” alisema.

Alibainisha kuwa kura za siri zilizopigwa zitafanyiwakazi na kila mkazi ni lazima ashiriki ulinzi huo iwe kwa yeye mwenyewe kutoka na kulinda au kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya uwezeshaji wa mpango huo na wale ambao watakaidi watafikishwa mahakamani kwani sheria ipo wazi.

Pia Diwani M,gawe amewapa siku 30 watu wanaomiliki maeneo katka kata hiyo ambayo hawajayaendeleza hivyo kuwa mapori ambayo sasa yanatumiwa kama maficho ya wahalifu na baada ya muda hup atawasilisha majina kwa mkuu wa mkoa kwa aili ya hatua zaidi.

Alisema kuna maeneo mengi eneo hilo ambayo wamiliki wake hawayaendelezi na yamegeuka mapori na ingawa wengine wana hati za kuyamiliki lakini wataomba msaada ofisi ya mkoa kwa hatua zaidi ili kuwanusuru wananchi na madhila ambayo wanayapata hivi sasa.

Prof. Mbarawa akagua vitengo vya mamlaka ya hali ya hewa (TMA)

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), kufanya tafiti na kuangalia fursa zitakazoiwezesha kupata mapato kutokana na kazi inazozifanya.

Amesema iwapo Mamlaka hiyo itafanya kazi kwa uadilifu na uaminifu itaongeza idadi ya watu inaowahudumia kwa mwaka nchini na hivyo kusaidia wadau mbalimbali wa sekta za Kilimo, Ujenzi, Afya, Uvuvi kufanya kazi kwa faida.

Prof. Mbarawa amekagua vitengo cha takwimu za hali ya hewa, hali ya hewa ya kilimo na Utabiri na kusisitiza kuwa ni wakati wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa teknolojia ya kisasa ili kuhudumia wadau wengi kwa wakati mmoja.

“Hakikisheni taarifa zenu zinawafikia watu wengi hususan wale wanaozihitaji taarifa hizi kwa kutekeleza shughuli zao kiuchumi”. Amesema Prof. Mbarawa.

Naye Mkurungenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa Mamlaka hiyo inafanya utabiri  kwa usahihi wa asilimia 80 na ni miongoni mwa Mamlaka inayofanya vizuri katika huduma za utabiri barani Afrika.

“Taarifa zetu ni sahihi na kila baada ya dakika 15 tunatoa taarifa zinazoonyesha hali ya hewa nchini”. Amesema Dkt. Kijazi.

Dkt. Kijazi amesema mamlaka hiyo imejipanga kuongeza uelewa wa watumiaji wa hali ya hewa hapa nchini ili kuwezesha wadau wa hali ya hewa kunufaika kikamilifu na utabiri unaotolewa na Mamlaka hiyo.

Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

Mtaalam wa kusoma utabiri wa hali ya hewa Hellen Msemo akimuonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano namna taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinavyorekodiwa na kutumwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisoma ramani ya utabiri wa hali ya hewa katika chumba maalum cha kusoma ramani wakati wa kukagua ofisi za Mamlaka ya hali ya hewa nchini.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Watatu kushoto) akifafanua jambo kwa wafanyakazi  wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (Hawapo pichani) huku Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agness Kijazi ( Watatu kulia) akifuatilia kwa makini.

 Mtaalamu wa maswala ya hali ya hewa nchini Didasian Kankesha akifuatilia utabiri kabla ya uhakiki na kuutangaza kwa wadau.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa viongozi wa TMA kuhusu namna ya kufanya kazi kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa ili kuhudumia wadau wengi kwa wakati.

Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Byakanwa akutana na wadau wa michezo wilayani mwake

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Byakanwa leo amekutana na wadau wa michezo katika harakati zake za kuandaa na kusimamia maendeleo ya michezo wilayani humo.

Renault Tanzania presented cricket kits and gears to Dar Raptors Cricket Club

$
0
0
As corporate social responsibility Luv Gadhvi Commercial Manager of Renault Tanzania presented cricket kits and gears to Osman Bairu (right) The Head Coach/ Owner of Dar Raptors Cricket Club. Osman who was the first local Tanzania to play for Tanzania Cricket National Team in 90s and now he teaches local kids at District levels. Boys and girls.

Kwaya ya Kinyakyusa ikiimba wimbo maarufu wa dini


20th ANNIVERSARY OF THE DEATH OF DR. FRANCIS MW. MSELLEMU

$
0
0
DR. FRANCIS MW. MSELLEMU 
1941- 1996

Baba, Ni Miaka 20 sasa tangu uondoke hata bila ya kutuambia neno la KWAHERI! 
Maisha yetu hayajawahi kuwa rahisi bila uwepo wako, Baba.

Japo watu wanatuona tukicheka , hawajui ni kiasi gani mioyo yetu inahuzunika kwa kukukosa malezi, mapenzi na uwepo wako  wewe.

Hata hivyo tunamshukuru Mungu kwa kuendelea kutulinda, kututunza na kutubariki. Ameedelea kuwa  kweli kwetu Mume wa Mjane na Baba wa Yatima.
Tunakuombea Pumziko la Milele, na tukiamini kwamba siku moja tutakutana na tutaimba Halleluya pamoja na wewe.

Unakumbukwa daima na Mke wako Mpendwa Kodawa Mikaline Msellemu - ‘Mama K’ kama ulivyo kuwa umezoea kumuita, Watoto, Wakwe zako, pamoja na Wajukuu. Ndugu , Jamaa na Marafiki nao hawajakusahau.

Pumzika kwa Amani DAD!

Kata ya Kibamba wapiga kura kubaini majambazi

$
0
0
Wakazi wa Kata ya Kibamba wamepiga kura ya siri kuwabaini wahalifu wanaoishi katika maeneo yao kufuatia tukio la karibuni la uvamizi katika nyumba nne zilizopo Mtaa wa Muhongoni ambalo limesababisha kifo cha mkazi mmoja wa eneo hilo, aliyejulikana kwa jina la Julius Msalangi.


Upigaji kura huo ulifanyika katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na ofisi ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo ambao ulifanyika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji wa Kata na kuhudhuriwa na Kamanda wa Polisi wa Kata ya Kibamba, Pius Lutumo.


Uamuzi wa kupiga kura hiyo umetokana na kuanza kuibuka kwa vitendo vya ujambazi unaofanywa majumbani na makundi ya vijana, uporaji wakati wa alfajiri na wizi wa mifugo hali ambayo imesababisha watu kadhaa kujeruhiwa na wengine kupoteza mali zao.


Katika mkutano huo, wakazi hao walikubaliana na kupiga kura za siri ambazo ziliwataja mara nyingi watuhumiwa wa uhalifu sugu wanne ambao Diwani wa Kata hiyo, alisema hata yeye majina yao ameyakuta ofisini kwake hivi karibuni alipoingia madarakani hivi karibuni.

Diwani wa kata hiyo, Ernest Mgawe aliwataka wakazi wa kata hiyo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na ofisi yake hasa pale yanapotokea matukio ya uhalifu nna kukamatwa kwa watuhumiwa ili lengo la kuifanya Kibamba kuwa sehemu salama ya kuishi liweze kufikiwa.


”Tunaomba ushirikiano wenu kwani kuna wakati watu walivamiwa na kujeruhiwa na mmoja kati ya watuhumiwa sugu ambaye pia leo ametajwa lakini hata hivyo wahanga walipotakiwa kwenda olisi kutoa maelezo ili mlenga afikishwe maakamanbi hawakuonekana” alisema.


Awali Kamanda wa polisi wilaya ya kipolisi ya Kibamba aliwataka wananchi watambue kuwa suala la ulinzi na usalama ipo miononi mwao kutokana na hali halisi ilivyo hvi sasa na kuwataka waachane na nadhjaria kuwa polisi ndi walinzi wao na mali zao.

“Hilo mnapaswa kjulitambua na kulingana na sheria ndogo zilizotungwa katika manuspaa ya ionondoni suala la ulinzi shrikishi sio iyari hasa pa,e wananchi wanapokubaliana upitia mikutano yao halali kma huo” alisema.

Alibainisha kuwa kura za siri zilizopigwa zitafanyiwakazi na kila mkazi ni lazima ashiriki ulinzi huo iwe kwa yeye mwenyewe kutoka na kulinda au kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya uwezeshaji wa mpango huo na wale ambao watakaidi watafikishwa mahakamani kwani sheria ipo wazi.

Pia Diwani Mgawe amewapa siku 30 watu wanaomiliki maeneo katka kata hiyo ambayo hawajayaendeleza hivyo kuwa mapori ambayo sasa yanatumiwa kama maficho ya wahalifu na baada ya muda hup atawasilisha majina kwa mkuu wa mkoa kwa aili ya hatua zaidi.


Alisema kuna maeneo mengi eneo hilo ambayo wamiliki wake hawayaendelezi na yamegeuka mapori na ingawa wengine wana hati za kuyamiliki lakini wataomba msaada ofisi ya mkoa kwa hatua zaidi ili kuwanusuru wananchi na madhila ambayo wanayapata hivi sasa.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akabidhi ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 bungeni

$
0
0
 Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad amekabidhi ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 bungeni leo ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.

Katika ripoti yake, CAG ametoa mapendekezo kadhaa ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kuboresha matumizi ya fedha za Serikali kwa malengo yanayokusudiwa.

Miongoni mwa maeneo ambayo CAG ametoa mapendeklezo ni Ofisi ya Masjili wa Vyama vya Siasa nchini ifuatilie suala la uwasilishaji wa taarifa za fedha kwa wakati kulingana na matakwa ya sheria.

Hatua hiyo ya CAG inafuatia ukaguzi uliofanywa kwenye vyama vya siasa nchini vyenye usajili wa kudumu ambavyo jumla yao ni vyama 22.

Prof. Assad alisema kuwa kati ya vyama hivyo vyenye usajili wa kudumu, ni chama kimoja ndicho kilichowasilisha hesabu zake kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Juni 2015 ambacho ni Chama cha Wananchi (CUF).

Vyama vingine 21 havikuwasilisha vitabu vya hesabu kwa ajili ya ukaguzi kinyume cha kifungu Na. 14 cha Sheria ya vyama vya siasa Na. 5 ya mwaka 1992.

 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akionesha ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.

 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mjini Dodoma juu ya ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.

 Waandishi wa habari wakipokea ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2015 ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka 2016/2017.
Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO


LIYUMBA AZIKWA KIJIJINI KWAO MAHENGE MKOANI MOROGORO

$
0
0
Watoto wa marehemu kwa umoja wao wakiweka shada la Maua kwenye kaburi la Baba yao.

Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Joachim Liyumba (68), aliyefariki Aprili 18 na umezikwa mwishoni mwa wiki kijijini kwao, Kwiro, Mahenge Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.Mwili ailaze roho ya Marehemu Mahali pema Peponi-Amin
Mazishi yalifanyika huku mvua kubwa ikinyesha
Pamoja na Mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha kijijini hapo,lakini Watu mbalimbali walishiriki kuupumzisha mwili wa Marehemu Liyumba katika nyumba yake milele
 Watoto wa Marehemu Liyumba wakiangua vilio wakati kaburi la Mpendwa baba yao likifukiwa.
Mwili wa marehemu wa Liyumba ukiwasili katika makaburi yaliyopo nje ya kanisani la Katoriki parokia ya Kwiro jimbo la Mahenge,tayari kwa kupumzishhwa kwenye nyumba yake ya milele.PICHA KWA HISANI YA http://shekidele.blogspot.com/

ankal uso kwa uso na magwiji wa ndondi nchini Habibu Kinyogoli na Emmanuel Mlundwa

$
0
0
Ankal akiwa na  furaha na heshima kukutana na magwiji wa ndondi nchini Tanzania leo. Habibu Kinyogoli "Master" (kati) na Emmanuel Mlundwa "Mzee wa Ulaya" jijini Dar es salaam leo. 
-----------------------
Kwa wasiowafahamu Mlundwa alikuwa kwenye timu ya Tanzania ya Olympic mwaka 1980 huko Moscow, Urusi (BOFYA HAPA) ambako alifanya vyema. Mlundwa pia ndiye muasisi wa ndondi za kulipwa nchini 

Kinyogoli alinyakua medali ya shaba katika Olympic mwaka 1972 uzito wa wa Unyoya ama Featherweight (BOFYA HAPA) Mjini Munich, Ujerumani

Kinyogoli ndiye aliyekuwa bondia wa pili wa Tanzania kuleta medali ya mashindano yanayoshirikisha nchi kutoka nje ya Afrika Mashariki wakati alipopata medali ya fedha katika Michezo ya Pili ya Afrika (2nd All African Games) iliyofanyika mjini Lagos, Nigeria mwaka 1973.  

Hadi wakati huo mwanamasumbwi aliyekuwa ameleta medali kutoka nje ya mipaka ya Afrika Mashariki alikuwa marehemu Titus Simba, ambaye alipata medali ya kwanza ya fedha kwa Tanzania katika Michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka 1970 huko Scotland. 
Miongoni mwa mabondia ambao ni matunda yake ni Majuto Mchevu, aliyemfundisha mwaka 1969  katika klabu ya Magomeni Community Centre, Zakaria Yombayomba, Habibu Mzungu, Bakari Selemani, Kweli Msigili, Abbas Pazi, Francis na nduguye Benedict Kakokele aliowafundisha mwaka 1971.
Mwaka 1973, aliweka historia nyingine kwa Tanzania baada ya kushiriki Michezo ya Pili ya Afrika nchini Nigeria. Katika robo fainali alimpiga bondia kutoka Madagascar na katika nusu fainali akamtwanga bondia kutoka Mali na kusonga mbele kwenye fainali kuwania ubingwa wa uzani wa Bantam, ambapo alikumbana na Omollo wa Uganda aliyemshinda Kinyogoli kwa pointi na hivyo Mtanzania huyo kuambulia medali ya fedha.

Katika klabu ya Urafiki mwaka 1973 aliwafundisha akina Charles Mhilu 'Spinks', Lazaro Makali, Salum Temianga, Herbert Sempoli na Mmasi, ambao walikuwa wakifanyia mazoezi Peninsula Hotel.

Baada ya kustaafu ndondi za ridhaa mwaka 1978 na kuanza kufundisha watoto ndipo alipopata nafasi ya kuwafundisha mabondia wengi zaidi. 
Mara tu baada ya kustaafu ndondi mwaka huo alianzisha klabu ya ndondi ya Simba na kwa kuanzia akawachukua watoto wa mzee Ally Matumla Namwera; akina Matumla, Haji, Rashid na Hassan, ambao hivi sasa wamekuwa maarufu katika mchezo huo duniani kote.

Baadaye akawachukua akina Mbwana, Karim na Mazimbo Matumla, Iraq Hudu, Joseph Marwa, Adeli Mkajanga, Oscar Manyuka, marehemu Steven Bicco, Patrick Kibona, Shabani Mhamila 'Star Boy' , Adam Abdulrahman, Maneno Oswald, Rajab Mhamila 'Super D' ambaye kwa sasa ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi na ni msaidizi wake katika kuwanoa vijana chipukizi kwa sasa, Abdallah Nyuni, Nassor Kondo, Rehema Matumla, Theresia Kapinga, na wengineo wengi.  

Enzi hizo mabondia nyota wa Afrika waliongozwa na Lottie Mwale na Francis Musankabala (Zambia), Steven Muchoki, David Attan, Michael Irungu, Robert Wangila, Isaya Ikonyi, na Modesti Napunyi (Kenya),


Wengine ni Emmanuel Mlundwa, Lucas Msomba, Ahmed Tesha, John Hugo, Clemence Chacha, Isangura, Nassor Michael, Joseph Marwa, Onesmo Ngowi, Gerald Isaac, Ali Muhamed, Emmanuel Kimaro, Rashid Matumla, Hamisi Kimanga na Koba Kimanga  (Tanzania), Ayub Kalule, John Mugabi, John Odhiambo, Boza Edward, John Byaruhanga,  Mustafa Waisaja  na Cuban Businge (Uganda).


Habibu Kinyogoli kulia aliyeshika kikombe na shingoni medali ya shaba akiwa na Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wakati huo Mhe. Rashid Mfaume Kawawa  baada ya kutoka katika mashindano ya All African Game 1973 akiwa na bingwa wa riasdha Filbert Bayi aliyeshinda medali ya dhahabu kwa kuibuka mshindi wa kwanza.

Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images