Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

MBUNGE HASNA MWILIMA ATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 6 NA TANI 17 ZA CHAKULA KWA WAHANGA WA MAFURIKO KIGOMA

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya Jamii, Kigoma

MBUNGE wa Jimbo la kigoma Kusini ,Hasna Mwilima amewakabidhi msaada wa shilingi milioni sita na laki tatu na tani kumi na saba za vyakula kwa wahanga wa mafuriko katika Kijiji cha Kirando kata ya Sunuka Wilayani Uvinza.

Akizungumza na Wananchi wa kijiji hicho wakati akikabidhi misaada hiyo iliyo tolewa na Halmashauri ya Uvinza na Mkoa wa Kigoma na wadau mbalimbali alisema serikali kwa kuwathamini wananchi imeamua kutoa misaada ilikuweza kuwasaidia wahanga waliopoteza mali zao wakati wa mafuliko.

Mwilima alisema anaupongeza uongozi wa Mkoa wa kigoma na halmashauri zote kwa kutoa msaada wa vyakula vitakazo wasaidia waathirika hao katika kipindi hika ambacho wanajipanga kurekebisha makazi yao.

Pia aliishukuru Halmashauri ya Uvinza kwa kuthamini Wananchi wake na kutoa msaada wa shilingi milioni tano na Mwenyekiti wa Halmashauli hiyo kuongezea laki mbili wameonesha jinsigani serikali ya awamu ya tano inavyo wathamini wananchi.

“mimi kama mbunge wenu nitatoa shilingi milioni moja nitaongezea katika mchango wa Viongozi wengine waliotoa tutahakikisha tunashirikiana katika wakati waraha, wakati washida na nyakati zote tupo pamoja nitawahudumia ipasavyo ndugu zangu “, alisema Hasna.

Hata hivyo alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuchangia Chakula tani saba kupitia michango iliyotolewa na Halmashauri zote za Mkoa ilikuweza kuwasaidia Wanakijiji waliokumbwa na mafuriko.

Rehema Hassani ni mmoja kati ya Wahanga wa mafuriko pia ni Mkazi wa Kirando alisema kwaniaba yawanakijiji wenzake wanaishukuru Serikali pamoja na Mbunge kwa kutoa misaada hiyo tunaimani itatusaidia na tutaweza kujipanga upya na kuziendesha familia zetu.

Aliiomba Serikali kuwapatia maeneo mengine waweze kujenga na kuondoka kuishi mabondeni ambapo mvua kubwa ikinyesha maji hujaa mtoni na kuingia ndani kupelekea mafuriko hivyo serikali igawe maeneo mengine yakuweka makazi.

Msaada uliotolewa ni maharage kilo218,mchere kilo1240, unga , mihogo,mahindi, mashuka kwaajili ya zahanati 218,na mafuta ya kupikia na chumvi na shilingi milioni sita na laki tatu watakazo gawiwa wahanga wa mafuriko hayo zilizo tolewa na serikali pamoja na wadau mbalimbali.

Mafuriko hayo yalitokea tarehe 13 mwezi wa pili mwaka huu kufuatia mvua kubwa iliyonyesha uharibifu mkubwa wa mali na kaya zipatazo 49 kukosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kusombwa na maji.
Mbunge wa jimbo la Kigoma kusini Husna Mwilima akimkabidhi fedha shilingi. Milioni sita na laki tatu mwenyekiti wa kijiji cha Kirando Athumani Chuma kwaajili ya wahanga wa mafuriko katika kijiji hicho.
Mhe. Hasna Mwilima akimkabidhi Bi rehema Issa mfuko wa sembe mmoja wa wahanga wa mafuriko katika kijiji cha kirando.
Mhe. Hasna akiteta jambo na muathirika wa mafuriko katika kijiji cha Kirando.
Sehemu ya chakula tani kumi na saba zilizokabidhiwa na mbunge wa jimbo la kigoma kusini Hasna Mwilima kwa wahanga wa mafuriko katika kijiji cha Kirando.
Baadhi ya makazi ya wanakijiji cha Kirando yaliyokumbwa na mafuriko

MAMA WA MHARIRI MTENDAJI WA THE NEW HABARI ABSALOM KIBANDA AZIKWA RUNGWE MBEYA

$
0
0

Familia ya wanahabari kutoka media mbalimbali pamoja na baadhi ya wahariri walioshiriki mazishi ya mama wa mhariri mtendaji wa The New Habari Absalom Norman Kibanda aliyesimama katikati mwenye miwani mara baada ya maziko yaliyofanyika Rungwe mission wilayani Rungwe mkoani Mbeya jana mchana.
Michuzi Media Group inakupa pole sana kwa msiba uliokupata mpiganaji Mwenzetu Absalom Kibanda,Tunaomba Mungu akupe uvumilivu wewe pamoja na ndugu wote katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wenu katika familia. Mungu alitoa na Mungu ametwaa jina la Bwana Lihimidiwe AMEN

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWASILI MKOANI MOROGORO KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Meneja Mkuu wa Uzalishaji katika kiwanda cha Ushoni wa Nguo za aina mbalimbali Mw. Ritesh Krishandev Beesony, wakati alipowasili katika kiwanda hicho leo April 16,2016 kwa ajili ya kutembelea na kuangalia utendajia kazi zinazofanywa kiwandani hapo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia nguo za aina mbalimbali zinazotengenezwa na kiwanda cha Ushoni cha Mazawa kiopo Msamvu Mkoani Morogoro wakati alipotembelea kiwanda hicho leo April 16,2016 kwa ajili ya kuangalia utendajia kazi zinazofanywa kiwandani hapo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha Ushoni wa Nguo cha Mazawa kiliopo Msamvu Mkoani Morogoro baada ya kukamilisha ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho leo April 16,2016 Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha Ushoni wa Nguo cha Mazawa kiliopo Msamvu Mkoani Morogoro baada ya kukamilisha ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho leo April 16,2016 Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

DARAJA LA KIGAMBONI KUFUNGULIWA RASMI JUMANNE APRILI 19, 2016

$
0
0

Viongozi Shrika la Taifa Hifadhi ya Jamii NSSF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakandarasi wa daraja la Kigamboni wakati lilipofunguliwa kwa ajili ya kupita magari kupita bure huku watembea kwa miguu na waendesha baiskeli wakipita bure. Daraja hilo litazinduliwa rasmi na Rais Dk. John Magufuli Jumanne tarehe 19.4.2016. 
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Karim Mataka akiwa katika eneo la daraja la Kigamboni mara baada ya kufunguliwa kwaajili ya kupita magari na waenda kwa miguu.
Muonekano wa daraja la Kigamboni baada ya magari kuanza kupita.
Eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi wakati wa uzinduzi rasmi.
Pikipiki na magari yakipita darajani.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MINING COMPANIES SIGNIFICANT CONTRIBUTORS TO ECONOMY, OPERATE TRANSPARENTLY.

$
0
0
Balozi Ami Mpungwe Balozi Ami Mpungwe

MINING COMPANIES SIGNIFICANT CONTRIBUTORS TO ECONOMY, OPERATE TRANSPARENTLY

TANZANIA CHAMBER OF MINERALS AND ENERGY PRESS STATEMENT
MINING COMPANIES SIGNIFICANT CONTRIBUTORS TO ECONOMY, OPERATE TRANSPARENTLY Recently, the mining sector has seen negative media reports in relation to the way in which it operates. The Tanzania Chamber of Minerals and Energy (TCME) represents member companies involved in the mining sector, from explorers to large scale producers as well as medium and small scale miners. 

Businesses that support the mining sector also form part of the membership. This sector is a significant contributor to Tanzania’s economy and the statistics below show the tangible fiscal and social benefits that accrue to the Tanzanian economy which in turn enables the Tanzanian Government to deliver on important development projects. 

  Mining Benefits to Tanzania Key statistics:  Investment into the mining sector from 1997 - 2015: USD 4.5 billion.  Revenue generated over the same period: USD 16.5 billion  GDP contribution: 3.3% (2013), Vs Vision 2025 of 10% contribution.  43% of total exports in 2013 (BOT Annual Report 2012/13).  48.2% Gross Value Added (% of revenue retained in country) i.e utilized for local procurement, taxes, training, infrastructure, local salaries and others.  Large Scale Mining employs directly 20,000 and another 200,000 induced (1:10) Chart showing distribution of revenue generated by member companies for the period 1997-2015 The revenue generated by our members amounted to USD 16,499,378,727 for the period 1997 to 2015 Description Amount spent (US$) % of Revenue Local Procurement 4,812,639,755 29.2 Community Spend 50,813,229 0.3 Training Spend 40,946,264 0.2 Local Salaries 1,146,813,407 7.0 Infrastructure Spend 58,095,698 0.4 Royalty & Other Taxes to Govt 1,827,814,617 11.1 TOTAL 7,937,122,971 48.2 The above chart and accompanying table indicates that the Gross Value Added (GVA) in the Tanzanian economy adds up to 48.1% (that is the amount of all payments made by the companies in-country as a percentage of revenue generated by the companies. The statistics provide to a large extent the vast tangible incremental fiscal and social benefits that accrue to the Tanzanian economy. The government benefits directly from royalty payments of 4% or 5% depending on minerals produced which is charged on gross turnover (not on profit).

 Local withholding taxes, corporation tax charged at 30% on profits, employment taxes and customs duties are other sources of Government revenue as shown on the chart. In addition to direct taxation, the development of the mining industry has had a massive impact on many other sectors. As a result of mines that were constructed, rural communities have had access to power and water supplies where there were none previously, thus enabling improvement of the quality of life of rural communities that prior to the arrival of the investors, might have seemed unattainable in rural Tanzania, mobile phone networks have reached communities previously isolated from modern communication. Other benefits include improvements and rehabilitation of local schools the equipping and supply of dispensaries and encouraging local businesses to flourish; these are all standard activities on the part of the mining companies in an effort to foster a positive relationship with the community around the mine area. 

It is noteworthy to point out that that these benefits flow to the communities without cost or charge, and are not a compulsory requirement of the Government but cost the companies millions of dollars. These costs cannot be reported as tax credits, but are funding tangible contributions to national development. In addition, railways have benefited by the freighting of supplies, trucking companies have expanded, to meet the demands of the mines, hotels in Dar es Salaam, Mwanza, Geita etc. have seen a significant increase in occupancy rates due to the mining employees and international visitors. Even tourism has reaped a benefit by the many mining related people visiting Tanzania’s world class national parks. New roads have been constructed or existing roads upgraded, not at the cost of the taxpayer, but the mining companies themselves.

MAONESHO YA KIMATAIFA YA MADIN I YA VITO ARUSHA TAREHE 19-21 APRILI, 2016

$
0
0

Wizara ya Nishati na Madini (MEM) kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA), wanawaalika wadau wote wa Sekta ya Madini na wamiliki wa Leseni ya Biashara za Madini, Masonara na Wachimbaji wa Madini ya Vito kushiriki kwenye Maonesho ya Tano ya Kimataifa ya Madini ya Vito Arusha (Arusha Gem Fair - AGF).

 Maonesho haya yatafanyika katika Hoteli ya Mount Meru ya Arusha, kuanzia tarehe 19 hadi 21 Aprili, 2016.

Maonesho ya AGF kwa mwaka 2016 yanalenga kuendeleza azma ya kuifanya Arusha kuwa kituo Kikubwa cha madini ya vito Afrika. Pia, maonesho haya yatawakutanisha washiriki (exhibitors) zaidi ya 100 kutoka nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini na wanunuzi wa kimataifa zaidi ya 500 pamoja na wadau mahiri wa tasnia ya vito. Maonesho pia  yanadhamiria kuendeleza biashara ya madini ya vito katika nchi za Mashariki, Kati na Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kutokana na hilo, Wizara ya Nishati na Madini haitatoa vibali vyovyote vya kusafirisha madini ya vito nje ya nchi kuanzia tarehe 5 hadi 28 Aprili, 2016. Ili kuhakikisha kuwa kunakuwepo na madini ya vito ya kutosha kwenye maonesho haya.

Vibali vitatolewa kwa Washiriki wa maonesho pekee kuanzia tarehe 19 Aprili, 2016 hadi maonesho yatakapokwisha. Lengo letu ni kuhakikisha maonesho haya yanafanikiwa na kuifanya Tanzania kuwa kituo kikubwa cha biashara ya madini ya vito barani Africa.

Mabanda ya maonesho yanapatikana kwa gharama za Dola za Marekani 1,000. Kamati ya Maonesho inasimamia ugawaji wa mabanda hayo kwa ushindani (first come-first be served).

Taarifa kuhusu usajili zinapatikana katika Ofisi za Madini za Kanda zilizo katika Miji ya Arusha, Mwanza, Dar es salaam, Mtwara, Mpanda, Shinyanga, Mbeya, Musoma, Songea na Singida au Ofisi za TAMIDA. 

Wanunuzi wanatakiwa kujisajili 
kupitia tovuti ya maonesho: www.arushagemshow.com; 
au kwa barua pepe ya maonesho: info@arushagemshow.com ; 
au kwa njia ya simu zifuatazo +255 784352299 or +225 767106773.


                                        Imetolewa na,


Katibu Mkuu

ADOLPH NDYEABURA NA DKT. GRACE MATASHA WAMEREMETA

$
0
0
 Wadau Adolph Ndyeabura na Dkt. Grace Matasha wakitoka nje ya Kanisa la Mtakatifu Gasper lililopo Mbezi Chini jijini Dar es salaam baada ya kufunga ndoa.
 Maharusi wakiwa na treni lao la wapambe baada ya kumeremeta
 Maharusi katika picha ya familia. Kulia ni mdau mwandamizi wa Globu ya Jamii wa UK Chris Lukosi ambaye bwana harusi ni mtoto wa dada yake
 Dkt. Grace na wapambe wake
Safari inaanza kuelekea katika ukumbi wa Target ulioko Mbezi kwa ajili ya mnuso wa nguvu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa aripoti kituoni na kuanza kazi kwa kasi

$
0
0
 Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa akila kiapo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mbele ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Meck Sadick mara tu baada ya kuripoti kituo chake cha kazi katikati ya wiki. Mhe. Byakanwa, ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa  alikuwa Katibu wa Rais Msaidizi Mwandamizi. amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Antony Mtaka aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
 Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa akiripoti ofisini kwake na kuanza kazi mara moja.
 Mkuu wa wilaya ya Hai mpya Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa akikagua maeneo ya soko la Kwa Sadala kwa kupita kila kona na kujionea hali ya uchafu mkubwa na kuamua kuuvalia njuga.
 Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa leo ameingia mitaani na kuanza kazi kwa kasi kwa kukagu usafi katika soko la Kwa Sadala ambako amekuta hali si nzuri na kutoa maagizo kwamba soko hilo liwe safi kila sehemu mara moja.
Mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa akifuatilia utekelezaji wa agizo lake la usafi katika soko la Kwa Sadala.

UCHUKUZI SC YATUA DODOMA NA KUANZA TIZI LA NGUVU TAYARI KWA MICHEZO YA MEI MOSI

$
0
0
TIMU ya Uchukuzi SC imesema haina wachezaji mamluki watakaowatumia katika mashindano ya Mei Mosi yatakayoanza Jumatatu (Aprili 18), kwenye viwanja vya Jamhuri mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Uchukuzi SC, Mohamed Ally, alisema jijini hapa kuwa hawawezi kutumia mamluki kwani ni moja ya masharti na kanuni ya mashindano hayo, kwani hairuhusiwi kutumia wachezaji ambao sio waajiriwa wa taasisi au wizara zinazoshiriki kwenye mashindano hayo.

“Tumekuwa tukishiriki haya mashindano na mengine mengi yanayoshirikisha taasisi za serikali na moja ya masharti makubwa ni kutotumia wachezaji wasiokuwa wafanyakazi halisi wanatambulika kama mamluki, hili tulisimamia kwa kuhakikisha wafanyakazi waajiriwa katika idara mbalimbali ndio wanaocheza katika mashindano haya” alisema Ally.

Ally alisema wanawachezaji wengi wenye viwango vya juu, ambao wanauhakika wa kufanya vizuri kwa kuchukua ubingwa katika michezo mbalimbali baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu.

“Tuliweka kambi kwa takribani miezi miwili huku tukifanya mazoezi kwenye viwanja vyetu vilivyopo kando kando ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na baadaye tukacheza mechi za kirafiki na timu mbalimbali za soka ikiwemo Amadori Boys ya Pugu Sekondari,” alisema Ally.

Naye kocha wa timu ya netiboli ya Uchukuzi SC, Judith Ilunda alisema hana hofu na wachezaji wake kutokana kufanya mazoezi ya kutosha kwa kucheza mechi tatu za kitafiki na timu za Uhamiaji na Cargo.

“Tunauhakika wa kutwaa kombe kwa sababu tumefanya maandalizi kabambe na tuna wachezaji wazoefu, wakiwemo waliowahi kuchezea timu ya taifa na wengine bado wapo katika timu hiyo ya taifa,” alisema Ilunda mchezaji wa zamani wa timu machachari ya Bandari na timu ya taifa.

Aliwataja baadhi ya wachezaji hao wazoefu ni pamoja na Matalena Mhagama, Mwadawa Hamisi, Subira Jumanne, Mary Kajigili na Sharifa Mustafa.

Meneja na kocha wa timu ya soka ya Uchukuzi SC, Robert Damiani alisema wapo tayari kwa mashindano kutokana na maandalizi kamambe waliyoyafanya wakiwa jijini Dar es Salaam.

Kocha wa timu ya riadha wa Uchukuzi SC, Kingsley Marwilo alisema atakuwa wachezaji watatu wa marathoni, ambao ni Scolastica Hasiri, Ramadhani Mwakilongo na Leonard Julius.

Timu ya Uchukuzi SC, ambayo inashiriki kwenye michezo ya soka, netiboli, riadha, baiskeli, kuvuta kamba, karata, bao na vishale, mwaka jana ilitwaa vikombe 13 kati ya hivyo vitano vilikuwa vya ubingwa wa kwanza, na vilivyosalia vilikuwa vya ushindi wa pili na tatu.

Timu kabambe ya  Uchukuzi Sport Club, tayari imeshafika mjini Dodoma kuanza mazoezi makali tayari kwa mashindano ya Mei Mosi ambayo yanaanza kesho Jumatatu na yatafunguliwa rasmi Jumatano  na mkuu wa Mkoa Mh. Richard Rugimbana.
 Wachezaji wa netball wa Uchukuzi SC mazoezini
Wachezaji wa netball wa Uchukuzi SC wakipanga mikakati baada ya mazoezi

Balozi Seif Ali Iddi akutana na Jaji wa Mahakama Kuu ya China Mheshimiwa Zhang Giannan

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kitendo cha Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuonyesha muelekeo wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar ni uthibitisho wake wa muendelezo wa uhusiano iliyokuwa nao kati yake na Zanzibar. 
Balozi Seif alisema hayo nyumbani kwake Kama nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akizungumza na Jaji wa Mahakama Kuu ya China Mheshimiwa Zhang Giannan aliyeuongoza ujumbe wa Viongozi sita wa Mahakamu Kuu ya China. 
Balozi Seif alisema China ni nchi ya kwanza iliyoamua kuiunga mkono Zanzibar mara tu baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa marejeo uliofanyika Tarehe 20 Machi mwaka huu katika hali ya amani na utulivu. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Nchi hiyo kubwa ya Bara la Asia kwa jitihada zake ilizochukuwa katika kuweka mfumo maalum wa utoaji wa mafunzo kwa watendaji wa Taasisi za Umma kwa nchi zinazoendelea kiuchumi ikiwemo Tanzania. Balozi Seif alisema utaratibu huo kwa kustawisha uwajibikaji na uchumi umesaidia zaidi watumishi wanaopata mafunzo nchini China kuwa na uwezo wa utekelezaji wa majukumu yao kitaaluma zaidi. 
“ Tumefarajika sana jinsi ya watendaji wa Baraza la Wawakilishi, Waheshimiwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanavyoitumia fursa hiyo ya mafunzo kwa kuwajibika kitaaluma wakati wa kuwatumikia wananchi ”. Alisema Balozi Seif. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimuhakikishia Jaji Mkuu huyo wa Mahakama Kuu ya China na Ujumbe wake kwamba uhusiano uliopo wa kihistoria katika ya pande hizo mbili utadumishwa zaidi kwa faida ya wananchi wake. 
Mapema Jaji wa Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Watu wa Chima Mheshimiwa Zhang Giannan akiambatana pia na Balozi Mdogo wa China aliyepo hapa Zanzibar Bwana Xie Yun Liang alisema wananchi wa taifa hilo la Bara la Asia wanafurahia kuona uhusiano wa Nchi hiyo na Zanzibar bado unaendelea kudumu. 
Jaji Giannan alieleza kwamba Mikakati ya China katika hatua yake ya baadaye imepanga kuimarisha zaidi uhusiano wake na Tanzania na Zanzibar kwa ujumla katika Sekta za Utamaduni, sanaa pamoja na Michezo. 
Alisema eneo hilo kwa sasa ni muhimu katika dhana ya kuwaunganisha Vijana ambao ndio kundi kubwa katika jamii kuelekeza nguvu zao katika sekta hizo zenye nafasi pana ya kutoa fursa za kujitegemea badala ya kusubiri Serikali ambazo tayari zimekuwa na ufinyu wa nafasi za ajira. 
Ujumbe huo wa Mahkama Kuu ya Jamuhuri ya Watu wa China upo Nchini kufanya ziara ya kutathmini maendeleo ya ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya nchi hiyo na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo pia Zanzibar.
 Jaji wa Mahakama Kuu ya China Mheshimiwa Zhang Giannan akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika nyumbani kwake kwa mazuungumzo ya kuimarisha uhusiano akiuongoza Ujumbe wa Majaji sita wa Mahakama Kuu ya China.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Jaji wa Mahakama Kuu ya China Mheshimiwa Zhang Giannan nyumbani kwake Kama nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China wakifuatilia mazungumzo kati ya Kiongozi wao Jaji  Zhang Giannan na Balozi Seif huko kama.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  akipokea zawadi maalum kutoka kwa Jaji wa Mahakama Kuu ya China Mheshimiwa Zhang Giannan mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Balozi Seif Kati kati aliyevaa suti nyeuzi akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Majaji wa Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Wat wa china uliopo nchini kwa ziara ya kutathmini uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na China.Kulia ya Balozi Seif ni Kiongozi wa Ujumbe huo Jaji wa Mahakama Kuu ya China Mheshimiwa Zhang Giannan na kushoto ya Balozi Seif ni Balozi Mdogo wa China aliyepo hapa Zanzibar Bwana Xie Yun Liang. Picha na – OMPR – ZNZ.

NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAISI MH.LUHAGA MPINA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KITAIFA MADALE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Jiwe la msingi lililozinduliwa na Mh.Naibu waziri wa Ofisi ya makamu wa raisi muungano na mazingira Mh.Luhaga Mpina kata ya Madale jijin Dar es salaam kuashiria uanzishwaji wa kampeni ya upandaji miti nchini kote,       
 
 Naibu Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa raisi muungano na mazingira Mh.Luhaga Mpina akizindua rasimi jiwe la msingi la kampeni ya Upandaji miti Kitaifa jijini Dar es salaam,        
 
 Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipanda mti katika kata ya Madale jijini Dar es salaam.   
 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa raisi Muungano na Mazingira akiongea na Waandishi wa Habari baada ya kushiriki zoezi la kupanda miti katika kata ya Madale jijini ikiwa ni sehemu ya kampeni kitaifa ya kupanda miti

MAANDALIZI YA MBIO ZA MWENGE MKOANI MOROGORO

$
0
0
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu kushoto akimpatia maelezo Wazairi wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu a Mh. Jenista Mhagama maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge unaotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu katikati, wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Steven Kebwe
Baadhi ya wasanii wakiwa katika maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge unaotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu kesho.
Maandalizi ya uzInduzi wa Mbio za Mwenge yakamilika mkoani Morogoro kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Mh. Steven Kebwe akiangali zoezi la matayarisho ya uzinduzi huo.
Maandalizi ya uzunduzi wa Mbio za Mwenge yakamilika mkoani Morogoro kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Mh. Steven Kebwe akiangali zoezi la matayarisho ya uzinduzi huo na kushoto ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama.
Baadhi ya watoto wa shule wakiwa katika maandalizi maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge unaotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu kushoto akimpatia maelezo Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu a Mh. Jenista Mhagama maendeleo ya maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge unaotarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu

WAZIRI MKUU MAJALIWA AMPA POLE MBOWE KWA KUFIWA NA KAKA YAKE

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe  wakati alipokwenda kumpa pole  kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha kaka yake   Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe   (kulia kwake) wakati alipokwenda kumpa pole  kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wanafamilia wakati alipokwenda  kumpa pole   Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe     kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwanasiasa mkongwe,Kingunge Ngombale- Mwiru  wakati alipokwenda  kumpa pole   Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe     kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI MOROGORO LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro leo April 17,2016, wakati alipowasili Hospitalini hapo kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolea kwa Jamii katika Hospitali hiyo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. kulia Daktari Mfawizi wa Hospitali hiyp Dr. Rita Lyamuya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Bibi Fausta Andreas na Mtoto wake Vayalet Michael (2) aliyelazwa katika Hospitali ya rufaa Mkoa Morogoro kwa matibabu wakati alipotembelea Hospitali hiyo leo April 17.2016 kwa ajili ya kuangalia utendaji na utoaji huduma kwa Jamii. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Mtoto Anisha Juma (2) mkazi wa Morogoro mjini aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kwa matibabu leo April 17.2016 Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ajili ya kuangalia utendaji kazi na utoaji huduma kwa Jamii.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Bidhaa za aina mbalimbali zinazotengenezwa katika kiwanda cha Mafundi Seremala cha (Kimasemo) kiliopo Sabasaba Mkoani Morogoro, wakati alipotembelea Kiwanda hicho leo April 17.2016 kwa ajili ya kukagua kazi zinazofanywa na kikundi hicho ambapo ameahidi kuchangia jumla ya Tshs 10 milioni kwa ajili ya kuendeleza utendaji wa kiwanda hicho. Makamu wa Rais yupo Mkoani Korogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
 

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA FLYOVER YA TAZARA DSM, 16 APRIL 2016


DARAJA LA KIGAMBONI LAWA KIVUTIO KIKUBWA KWA WATALII WA NDANI

$
0
0
 Ripota wa Globu ya Jamii Sultani Kipingo leo katembelea Daraja jipya la Kigamboni ambalo na kukuta limegeuka kivutio kikubwa cha watalii wa ndani, ambapo mamia ya wananchi kutoka sehemu mbalimbali za jiji na hata mikoani wamejazana darajani hapo kwa mamia kujionea suluhisho la tatizo la usafiri kwa wanaokwenda na kutoka wilaya mpya ya Kigamboni, mkoa wa Dar es salaam. 
Daraja hili lenye urefu wa mita 680 na amblo limeanza kujengwa mwaka 2012 linamilikiwa na mfuko wa jamii wa NSSF kwa asilimia 60 na Serikali asilimia 40. 
Ujenzi wake umeenda sambamba na ujenzi wa barabara ya kilomita 5.7  na gharama yake ni  kiasi cha Dola za Marekani 143.5, ambapo serikali imetoa asilimia 40, huku NSSF ikitoa asilimia 60 ya fedha zote. Designer wake ni Arab Consulting Engineers na wajenzi ni China Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd & China Major Bridge Engineering Company.
 Familia ikipita njia ya waendao kwa miguu katika daraja la Kigamboni leo
 Mamia ya watalii wa ndani wametembelea daraja hilo ambalo lilifunguliwa Jumamosi kuruhusu wananchi wajionee, kabla ya kuanza kazi baada ya kufunguliwa rasmi Jumanne hii
 Wananchi wakifurahia daraja la Kigamboni leo
Taswira ya daraja la Kigamboni kutoka angani. 

SOMO LA BURE LA USAFI WA MAZINGIRA NA UTII WA SHERIA BILA SHURUTI KUTOKA MJINI KIGALI, RWANDA

$
0
0
Moja ya changamoto kubwa zinazoikabili miji katika kanda ya Afrika Mashariki, ni uchafuzi wa mazingira, hasa kutokana kushindwa kusimamia kwa ufanisi suala zima la usafi. Kwa mujibu wa uchumbuzi wa DW, ukiacha mji wa Kigali, ambao kwa kiasi kikubwa umefanikiwa kudhibiti uchafuzi wa mazingira hasa utupaji hovyo wa takataka, miji mingine kama vile Dar es Salaam, Nairobi, na Kampala bado ina safari ndefu ya kufikia kiwango cha usafi. 
Kigali ni mji mkuu wa Rwanda na pia mji mkubwa kuliko mingine yote nchini humo. Iko karibu sana na mstari wa ikweta kwenye kimo cha 1400 - 1600 m juu ya UB. Hali ya hewa ni ya wastani hakuna baridi kali wala joto kali. 
Kigali ina wakazi 600,000. Kigali ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani mwaka 1907 kama kituo cha mwakilishi wa Afrika ya Masharikiy a Kijerumani Richard Kandt. Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilivamiwa na Wabelgiji ikawa sehemu ya eneo la kukabidhiwa la Rwanda-Urundi chini ya utawala wa Ubelgiji. 
 Baada ya kugawa kwa Rwanda-Urundi kuwa nchi mbili za Rwanda na Burundi Kgali ikawa mji mkuu wa Rwanda mwaka 1962. Mauaji ya Watutsi ya mwaka 1994 yalianza Kigali. Mji ulipungukiwa wakazi 100,000 wakati ule. Hivi sasa Kigali imebadilika na kuwa mojawapo ya miji misafi na yenye wananchi wanaotii sheria bila shuruti katika bara la Afrika.

Mji wa Kigali kama umepigwa deki. Mhe Paul Makonda na wakuu wa mikoa wengine wote na wakuu wa wilaya mpo hapo? Iko haja kwenda huko na kujifunza wenzetu wanatumia uchawi gani kufanikisha hayo...
Mitaa kama sebule ya hoteli
Utii wa sheria bila shuruti. Kwenye taa nyekundu hata bodaboda wanasimama
Hivi ndivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anavyotaka miji yake ionekane. Safi na watumia barabara watii sheria bila shuruti.
Katika kutii sheria bila shuruti huko ni pamoja na kila dereva wa bodaboda na abiria wake kuvaa kofia. Sheria kali ndogondogo zikiwekwa na kusimamiwa na kutekelezwa ipaswavyo  kama ilivyo katiia mji wa Kigali hili linawezekana kabisa!

Balozi Seif atembelea maeneo yaliyoathirika na mvua katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar

$
0
0
Mhandisi wa Baraza la Manispaa Mzee Juma Khamis wa kwanza kutoka kulia akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyefanya ziara kuangalia baadhi ya Mitaro iliyosababisha mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa nchini. Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed na Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Nd. Said Juma Ahmada.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili a Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Abdoud Mohammed akimueleza Balozi Seif hatua zilizokwisha chukuliwa na watendaji wa Kamati ya Maafa katika kunusuru maafa yaliyojitokeza ndani ya kipindi cha mvua zilizoleta athari kubwa.
Balozi Seif akiwafariji Baadhi ya Wananchi wa Mitaa ya Kwahani, Kwawazee na Sebleni ambao nyumba zao zimeathirika kwa mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia Jumapili.
Skuli ya Nyerere Sekondari ni miongoni mwa skuli zinazotoa huduma ya muda ya kuwahifadhi watu walioathirika na mvua kubwa za juzi ambapo Balozi Seif alipata wasaa wa kuwatembelea kwa kuwapa pole.

JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. MOHAMED CHANDE OTHMAN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JAJI WA MAHAKAMA KUU YA WATU WA CHINA MHE. ZHANG JIANNAN LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akiwa ameongozana na Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang Jiannan (kushoto) mara baada ya kumpokea katika viwanja vya Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam. Mhe. Zhang Jiannan pamoja na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi kwenye Mahakama ya Tanzania kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi na kuimarisha ushirikiano baina ya Mahakama ya Tanzania na China. 
  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China uliolenga kukuza ushirikiano na kubadilishana uzoefu wa utendaji wa Mahakama za Tanzania na China leo jijini Dar es salaam. 
 Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (wa pili kutoka kushoto mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman (katikati) na baadhi ya watendaji wa Mahakama ya Tanzania mbele ya Jengo la Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam.
 Picha/Aron Msigwa.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

WANAFUNZI 65 WA SHUE YA SEKONDARI CHALINZE WANUSURIKA KIFO BAADA YA BWENI LAO KUTEKETEA KWA MOTO.

$
0
0
VICTOR MASANGU,BAGAMOYO.
WANAFUNZI  65 wa shule ya sekondari chalinze iliyopo Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wamenusurika kupoteza maisha baada ya bweni moja la kulala  kuteketea  kwa moto wakati wao wakiwa darasani kwa ajili ya kujisomea masomo ya usiku.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga kuhusina na tukio hilo alisema kwamba limetokea jana majira ya saa 3:20 usiku wakati wanafunzi hao wakiwa madarasani wanajisomea.
 
Mkuu huyo alibainisha kwamba chanzo cha moto huo inadaiwa ni shoti ya umeme ambayo imesababisha moto huo kuteketeza vifaa vyote vikiwemo magodoro,vitanda,vitabu  vilivyokuwemo katika bweni hilo ambalo lilikuwa likilaliwa na wanafunzi wapatao 65 wa kiume.

“Taarifa za awali ambazo tumezipata chanzo cha kuungua kwa jengo hili ni umeme, lakini kwa kweli ni tukio la kusikitisha kwani vifaa vyote na mali za wanafunzi hao 65 ikiwemo magodoro,vitanda, madatfari yao yote yameteketea kwa moto huo,”alisema Mwanga.

Aidha Mwanga akizungumzia kuhusina na juhudi za serikali ambazo tayari wameshazichukua hadi sasa ikiwemo  kuwahifadhi wanafunzi hao  65 katika jengo lingine kwa  muda wakati wanaendelea na jitihada zingine za kuangalia ni namna gani ya kulijenga jengo linguine kwa haraka.

Alisema kuwa kwa sasa kutokana na tukio hilo la kuungua kwa shule hiyo amewaomba wadau mbali mbali wa maendeleo kujitoa kwa hali na mali kutoa michango yao kwa ajili ya kuwezesha ujenzi mwingine wa jengo hilo ikiwemo na mahitaji ya msingi wanayostaili kusaidiwa wanafunzi hao waliounguliwa na mali zao.

Katika hatua nyingine alisema  kwamba baada ya moto huo kutokea hakukuwa na msaada wowote wa gari ya zima moto hivyo kuliweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kushika kasi ya moto na kuteketeza vitu vyote katika jengo hilo, ambapo jitihada za kuuzima zilifanywa na jeshi la posili viongozi wa serikali pamoja na wananchi wenyewe.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo Chalinze Hussein Mramba amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kwamba mkakati waliyojiwekea ni kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kuweza kuhakikisha kwamba wanajenga jengo linguine ili wanafunzi waweze kupata sehemu ya kulala.

 SHULE hiyo ya sekondari Chalinze iliyopo wiayani bagamoyo Mkoa wa Pwani ina jumla ya idadi ya  wanafunzi 1151.ambapo kati yao 65 kwa sasa wameunguliwa na vitu vyao vyote hivyo kunahitajika juhudi za serikali katika kuhakikisha wanatoa msaada wa hali na mali ili waweze kuendelea  masomo yao.
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live




Latest Images