Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

BAMIZA TOP 20 CHART 16TH APRIL 2016 MAGIC FM

$
0
0
92.9Dar & Mtwara, 93.3Dodoma, 98.6Arusha, 101.7Mwanza &Tanga, 98.7Morogoro.

SONG

ARTIST

PRODUCER

PEAK/POS

20. Fundi

Mh Temba ft Malomboso & Jokate

Makochali

NEW

19. Kwetu

Raymond

Lizer


18. Walk it off

Fid Q ft Taz

Taz


17. Utanipenda

Diamond Platnumz

Tudy Thomas

2  WEEKS ON NO.1  

16. Nakuchana

Jux & Ben Pol

Manecke


15. One more night

Jux

Nahreel


14. Mabawa

Msami

Abidadi


13. Mama

Yamoto Band ft Zena

Shirko


12. Make me sing

Diamond & AKA

Tuddy Thomas


11. OG

G.Nako

Nahreel


10. Una Akili Wewe

Roma & Baghdad

ISSAM & GEOF MASTER.


  9. Mahaba niue

Mau Sama

Ema the Boy


  8. Kama utanipenda

Darasa ft Mavoko

Abba


  7. Mama kijacho

Tunda Man

Manecke


  6. Ahsanteni kwa kuja

Mwana F.A

Hermy B

2 WEEKS ON NO.1

  5. Kamatia chini

Navy Kenzo

Nahreel


  4. Siwezi

Baraka da Prince

Manecky


  3. Zigo rmx

Ay ft Diamond Platnumz

Nahreel,Hermy B,Marco Chali


  2. Sweeti sweetie

Chege ft Run Town&Uhuru

Uhuru

2 WEEKS ON NO.1

  1. Kwa hela

Linex

Tuddy Thomas

1ST  WEEK ON NO.1


serikali itashirikiana Millen Mageses katika kupambana na ugonjwa wa Endometriosis

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif afunga mafunzo ya Uongozi mdogo wa Polisi visiwani leo

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua gwaride la wahitimu wa mafunzo ya uongozi Mdogo wa Polisi katika ngazi ya Ukoplo, Sajenti na Stafu Sajent hapo chuo cha Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.
 Askari wa Kike wa Jeshi la Polisi ngazi ya Ukoplo, Sajenti na Stafu Sajenti wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mgeni rasmi wakati wakimaliza mafunzo yao ya wiki nane kwenye chuo cha Polisi Ziwani.
 Wahitimu wa mafunzo ya Uongozi mdogo wa Polisi ngazi ya Koplo, Sajenti na Stafu Sajenti wakifanya vitu vyao katika kuonyesha moja ya mafunzo waliyoyapata ya mapambano kwa singe kwenye hafla ya kumaliza mafunzo.
 Askari Godrey Kihimba Mjanja akivishwa cheo cha Koplo na Balozi Seif baada kumaliza mafunzo yake na kufanya kufanikiwa kuwa miongoni mwa askari Tisa waliofanya vyema katika mafunzo yao.
 Balozi Seif akimvisha cheo cha Sajenti Asha Hussein Magungu baada ya kumaliza mafunzo yake na kuwa miongozi mwa askari waliofanya vizuri katika mafunzo yao. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
 

RC DAR ES SALAAM NA KOREA KUSINI WAWEKA JIWE LA MSINGI LA HOSPITALI YA CHANIKA MANISPAA YA ILALA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda (kulia) na Makamu wa Rais wa Shirika la Koica la nchini Korea Kusini, Taemyon Kwon, wakiweka tofali kwa pamoja kuashiria uweka wa jiwe la msingi la Hospitali ya Chanika iliyopo Manispaa ya Ilala, inayojengwa kwa ufadhili wa nchi hiyo Dar es Salaam jana. Ujenzi huo hadi kukamilika utagharimu sh. bilioni 8.8  za Kitanzania.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mr Isaya (kulia), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Victriana Ludovic na Meneja wa Mradi wa ujenzi wa Hospitali hiyo Mr Kim wakiweka jiwe la msingi la Hospitali hiyo.
Meneja wa Mradi huo, Mr Kim akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na ujembe wake ramani ya majengo ya Hospitali hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' ASHINDA KWA POINT NCHINI PANAMA

$
0
0
 Ibrahimu Class 'King Class Mawe'
 Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akiwa na mpinzani wake Zapir Rasulov wa Russia baada ya kumshinda kwa point 
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akiwa na bondia Shane Mosley ambaye alishawai kucheza na Floyd Mayweather na kuonesha upinnzani mkubwa kushoto ni Rais wa ngumi za kulipwa nchini Emanuel Mlundwa hapa ni baada ya kushinda mpambano wake na Zapir Rasulov wa Russia kwa point.

 BONDIA Mtanzania Bingwa wa Afrika wa mikanda ya WPBF na U.B.O Afrika Ibrahimu Class 'King Class Mawe' april 15 mwezi huu amefanya maajabu baada ya kumtwanga bila huruma Bondia Zapir Rasulov wa Russia na kufanikiwa kumpiga kwa point katika mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Convenciones Vasco nchini Panama City, Panama 
Class anakuwa bondia wa kwanza kumpiga bondia huyo katika mapambano yake 30 aliyocheza ambapo kati ya hayo mapambano 27 ameshinda kwa K.O na matatu kashinda kwa point
Bondia huyo alikuwa na rekodi ya kutopigwa hata mpambano mmoja  aliyocheza katika michezo yake yote na sasa Class ameweka doa katika michezo yake na kuwa bondia wa kwanza kutoka Afrika kumpiga bondia huyo anaesifika ugaibuni 
Bondia King Class Mawe baada ya kuibuka na ushindi huo amesema ushindi ni wa watanzania wote kwani yeye amekuwa mtumishi wao tangia mpambano wake wa kwanza ambao ulikuwa wa ubingwa alipokwenda nchini Zambia na kufanikiwa kumdunda bondia Mwansa Kabinga katika mpambano uliofanyika Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia hii ilikuwa june 8 ,2014 na kushinda kwa TKO ya raundi ya tisa na kufanikiwa kurudi na mkanda wa WPBF Afrika
"Hivyo natarajia kuendeleza kuitumikia Tanzania na watu wake kupitia mchezo wa masumbwi nchini", amesema bondia huyo anaenolewa na jopo la makocha likiongozwa na kocha mkongwe kabisa Habibu Kinyogoli akisaidiwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye amekuwa akimshauri katika mapambano yake mblimbali nchini.
Bondia huyo anataraji kurudi nchini wakati wowote kwa ajili ya maandalizi ya mpambano mwingine wa masumbwi  hivi katibuni

YANGA YASHIKA USUKANI WA LIGI KUU, YAICHAPA MTIBWA SUGAR 1-0

$
0
0

 Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Mtibwa Sugar, Majaliwa Shaban katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijii Dar es Salaam. Yanga imeshinda 1-0 na kufikisha pointi 59 na kuongoza katika msimamo wa Ligi huku ikifuatiwa na Simba yenye Pointi 57. (Picha na Francis Dande)
 Mshambukiaji wa Yanga, Thaban Kamusoko akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar.
 Kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Donald Ngoma akipiga kwa kisigino huku akizongwa na beki wa Mtibwa Sugar, Andrew Vicenti. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

TAARIFA KWA UMMA - UPOTOSHWAJI WA GAZETI LA NIPASHE

$
0
0
Ofisi ya Bunge imebaini upotoshwaji mkubwa Katika habari iliyochapishwa na Gazeti la Nipashe toleo la leo Aprili 16, 2016 yenye kichwa cha habari kisemacho “ Bunge sasa laufyata mkataba wa Lugumi. Habari hiyo imeandikwa kufuatia ufafanuzi uliotolewa na Bunge jana kuhusu maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) dhidi ya utekelezaji wa mkataba wa Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd  kuhusu mradi wa utambuzi wa alama za vidole (AFIS) (Automated Fingerprint Identification System.

Ndani ya habari hiyo pia, Gazeti hilo limeeleza kuwa kamati ya PAC iliwahi kuliandikia Jeshi la Polisi kulitaka liwasilishe mkataba huo mbele ya Kamati, jambo ambalo si kweli bali ni upotoshwaji wa makusudi wenye lengo la kujenga hisia mbaya kuhusu mwenendo wa shughuli za Bunge mbele ya Umma.

Ukweli ni kwamba PAC haijawahi kuliandikia jeshi la Polisi kama inavyodaiwa na Gazeti hilo. Nukuu ya  maelezo ya PAC katika Hansard kwa Afisa Masuhuli kuhusu jambo hilo inasema kama ifuatavyo:

“Kamati inamuagiza Afisa Masuhuli kuwasilisha maelezo ya kina kuhusu utekelezaji wa Mkataba baina ya Jeshi la Polisi na  Kampuni ya Lugumi Enterprises  kuhusu mradi wa AFIS. Maelezo hayo yawasilishwe kwa Ofisi ya  Katibu wa Bunge kabla ya Jumatatu tarehe 11 Aprili, 2016”.

Katika agizo hilo PAC haikuwa imeandika kwa maandishi kuhusu agizo lake hilo hadi tarehe 12 Aprili, 2016 ilipo mweleza Katibu wa Bunge aweze kuwasilisha agizo hilo kwa maandishi ili liweze kupata Kinga chini ya Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge ambapo barua iliandikwa na kuwasilishwa kwa Afisa Masuhuli ili kupatiwa maelezo hayo kabla ya tarehe 18 Aprili, 2016.


Aidha, Mwandishi pia amelituhumu Bunge kuwa lina nia ya kuficha ukweli kuhusu jambo hili kwa kusema   taarifa ya ufafanuzi iliyotolewa na Bunge ni “kama kufunika kombe mwanaharamu apite kwa kujaribu kupotosha maagizo ya yaliyotolewa na kamati ya PAC ambayo inataka kuuona mkataba huo”


Ni vyema ikafahamika kuwa si jambo jema kwa mwandishi au chombo chochote cha habari kulituhumu Bunge linapotekeleza majukumu yake kwa kuwa Bunge linafanya kazi zake kwa kwa kuzingatia kanuni zake za Kudumu ikiwa ni pamoja na Sheria.  

Ofisi ya Bunge inalisihi Gazeti la Nipashe kuomba radhi kutokana na taarifa yake hiyo iliyojaa upotoshwaji mkubwa kwa uzito ule ule au kurekebisha taarifa yake kulingana na ukweli ulivyo haraka iwezekanavyo.


Imetolewa na;

Ofisi ya Bunge,

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,

S.L.P 9133,

DAR ES SALAAM.



16 Aprili, 216.


MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWASILI MKOANI MOROGORO KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU LEO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongozana na Meneja Mkuu wa Uzalishaji katika kiwanda cha Ushoni wa Nguo za aina mbalimbali Mw. Ritesh Krishandev Beesony, wakati alipowasili katika kiwanda hicho leo April 16,2016 kwa ajili ya kutembelea na kuangalia utendaji kazi zinazofanywa kiwandani hapo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia nguo za aina mbalimbali zinazotengenezwa na kiwanda cha Ushoni cha Mazawa kiopo Msamvu Mkoani Morogoro wakati alipotembelea  kiwanda hicho leo April 16,2016 kwa ajili ya kuangalia utendajia kazi zinazofanywa kiwandani hapo. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia nguo za aina mbalimbali zinazotengenezwa na kiwanda cha Ushoni cha Mazawa kiopo Msamvu Mkoani Morogoro wakati alipotembelea  kiwanda hicho leo April 16,2016 kwa ajili ya kuangalia utendajia kazi zinazofanywa kiwandani hapo. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia nguo za aina mbalimbali zinazotengenezwa na kiwanda cha Ushoni cha Mazawa kiopo Msamvu Mkoani Morogoro wakati alipotembelea  kiwanda hicho leo April 16,2016 kwa ajili ya kuangalia utendajia kazi zinazofanywa kiwandani hapo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongea na Viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha Ushoni wa Nguo cha Mazawa kiliopo Msamvu Mkoani Morogoro wakati wa  ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho leo April 16,2016. Picha na OMR

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA YA JUU (FLYOVER) MAKUTANO YA BARABARA YA MADELA NA NYERERE

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, eneo la Tazara Jijini Dar es salaam ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018. 
 Sherehe ya uzinduzi wa mradi huo imefanyika kando ya eneo la makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Mameya wa Jiji la Dar es salaam na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida. 
Barabara hiyo ya juu itakuwa ya kwanza kujengwa hapa nchini na ujenzi wake umepangwa kugharimu takribani shilingi Bilioni 100 ambapo kati ya fedha hizo shilingi Bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3. 
Barabara ya juu itakayojengwa itakuwa na njia nne na urefu wa mita 300 kutokea maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es salaam kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, na inatarajiwa kupunguza kero ya msongamano wa magari yaendayo na yatokayo Uwanja wa ndege na Bandari ya Dar es salaam. 
Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema barabara hiyo inajengwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya serikali yake ya kumaliza tatizo la msongamano wa magari Jijini Dar es salaam, ambao kwa mwaka 2013 pekee utafiti umeonesha ulisababisha upotevu wa shilingi Bilioni 411.55 
Rais Magufuli amebainisha juhudi nyingine za kukabiliana na msongamano wa magari Jijini Dar es salaam kuwa ni pamoja na kujenga barabara ya njia sita ya Dar es salaam hadi Chalinze ambayo itakuwa na Flyover tano, ujenzi wa barabara nyingine za juu katika makutano ya barabara za Nelson Mandela, Morogoro na Sam Nojuma eneo la Ubungo na ujenzi wa daraja jipya la Salander lenye urefu wa kilometa 6.23 kuanzia Coco Beach hadi hospitali ya Agha Khan. 
Juhudi nyingine ni ujenzi wa awamu ya pili wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara za Kilwa, Chang'ombe na Kawawa, na ujenzi wa awamu ya tatu wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka katika barabara za Nyerere - Gongo la Mboto na Uhuru - Azikiwe. 
Aidha, Rais Magufuli amezungumzia awamu ya kwanza ya mradi wa mabasi yaendayo haraka, kuwa serikali yake imelazimika kusimamisha kuanza kwa huduma hiyo baada ya kubaini dosari katika mkataba wa mradi ambazo zingesababisha serikali kupoteza fedha nyingi na wananchi kutwishwa mzigo mzito wa viwango vikubwa vya nauli, na amewahakikishia wananchi wa Dar es salaam kuwa mabasi hayo yataanza kutoa huduma hivi karibuni baada ya kurekebisha kasoro zilizobainika. 
Dkt. Magufuli pia amezungumzia usafi wa Jiji la Dar es salaam kwa kuwataka viongozi wa Manispaa zote za Jiji, kuhakikisha wanatafuta namna ya kudhibiti utupaji hovyo wa takataka ikiwemo kutoza faini kubwa kwa watakaokamatwa wakitupa takataka hovyo. 

Gerson Msigwa 
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, 
IKULU Dar es salaam 
16 Aprili, 2016







Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akifungua pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akifungua pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo ya namna mandhari itakavyokuwa baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Aprili 16, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipungia mkono wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya juu kwenye makutano ya barabara za Mandela na Nyerere maeneo ya Tazara Jijini Dar es Salaam.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Tanzanian doctors perform lifesaving heart Surgeries to Rwandan Children at King Faisal Hospital in Kigali

$
0
0
By Sultani Kipingo
The three doctors from the Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) at the Muhimbili National Hospital in Dar es Salaam who were sent to perform lifesaving heart Surgeries to Rwandan Children at King Faisal Hospital have arrived in Kigali and have today performed surgeries on four children. 
 The acting Executive Director of JKCI Professor Mohamed Janabi told this reporter that  the three Tanzanian Medical experts, who are working hand in hand with JKCI's International partner,  Open Heart International (OHI) Australia, have set up a nine-day surgical camp at the King Faisal Medical Central from 14th to 22nd April, 2016  during which time some 25 Rwandan Children are expected to get life saving heart operations. 
 The trio, Dr. Godwin Godfrey Sharau (team leader and Pediatric Cardiac Surgeon) , Dr, Naiz Majani (Pediatric Cardiologist) and Dr. Onesmo Mhewa (Pediatric Cardiac Anesthesiologist), left mid this week for Kigali. 
 “Since Rwanda has yet to have a standing cardiac program, the collaboration is aimed at addressing urgent surgical needs for the growing Rwanda waiting list as well as working with local health providers in training and development. 
“Moreover it is a welcome gesture from Tanzania to Rwandan children to having surgeries at the JKCI as part of the Tanzania-Rwanda and East Africa collaboration spirit”, Prof Janabi said. 
 He said though still at its infancy, JKCI has vastly grown its capacity in regard to open heart surgeries on children.
 “In 2015 for example, 207 children had their life saving surgeries at JKCI and many more continue to receive their treatment in this year. Some 300 more children are expected to be operated on at the Institute this year”, he said, adding that for this year already some 80 patients have already been operated one between January and March alone. 
 “The objective of JKCI remains to be a Center of Excellency in Heart Diseases in East Africa by 2020” recounted Prof Janabi. “For example in 2015 we operated on twins from DRC, patients from the Comoros and conducted procedures to a number of diplomats residing in Dar es Salaam - the future is bright...” he said.

 The three Tanzanian Medical experts: Centre is Dr. Godwin Godfrey Sharau (team leader and Pediatric Cardiac Surgeon), Right is Dr, Naiz Majani (Pediatric Cardiologist), left is  Dr. Onesmo Mhewa (Pediatric Cardiac Anesthesiologist) at the departure lounge of Julius Nyerere International Airport in Dar es salaam waiting for their flight to Kigali
 A quick selfie upon arrival at the King Faisal Hospital in Kigali ready for their nine-day life-saving camp
 One of the four procedures the trio conducted at the hospital today
 Part of the King Faisal Hospital in Kigali
King Faisal Hospital in Kigali

TAARIFA KWA UMMA kuhusu Bidhaa za IVORI CHOCOLATE

$
0
0
 Uongozi wa Kampuni ya IVORI IRINGA (I. F. B) Unapenda kuwataarifu Umma Hususani Walaji, Wauzaji wa Jumla na Reja Reja kuwa kumekuwepo na bidhaa  ya CHOCOLATE ambayo inatoka NJE YA NCHI ambayo imefananishwa jina la Nembo ya Bidhaa zetu za IVORI CHOCOLATE na hivyo kuwachanganya wateja wetu juu ya uwepo wa bidhaa yetu hiyo na kujiuliza maswali yafuatayo:
1-Je Tumebadilisha Jina la Kampuni yetu? 
2-Je Tumebadilisha Muonekano wa Bidhaa yetu ya CHOCOLATE? 
3-Je Tumebadilisha Bei ya Chocolate za Ivori?

Kutokana na maswali hayo yaliyojitokeza kwa Wateja wetu, Kampuni Ya IVORI IRINGA Inapenda kuutaarifu Umma yafuatayo
1-Kampuni ya IVORI-Iringa haijafanya mabadiliko yeyote juu ya muonekano wa bidhaa zake, Gharama yake  wala Nembo yake, haswa ya IVORI CHOCOLATE, Hivyo inawaomba wateja wake kuzingatia Yafuatayo
1-Kuhakikisha kila bidhaa unayonunua ya IVORI ina Nembo Halisi ya IVORI yenye Herufi I mwanzoni na herufi I  mwishoni. 
isomeke IVORI CHOCOLATE na Sio IVORY CHOCOLATE

2-Bidhaa zetu zote zinatengenezwa TANZANIA,Tunajivunia Uzalendo wetu na ndio maana bidhaa zetu zote ni MADE IN TANZANIA .
3-Hakikisha kila  Chocolate yetu unayoinunua ina Rangi ya kahawia ndani ya pakiti yake ikiwa na Ladha tamu ya maziwa ikitegenezewa na COCOA Halisi inayolimwa na Wakulima Nchini TANZANIA
4-Rangi ya kifungashio chakeni ya Njano iliyochanganywa na Rangi ya Zambarau.
5-Gharama zetu Elekezi ni Shilingi 1000 kwa Gram 40 na Shilingi 500 kwa Gram 20 na hatuna ujazo unaozid gram 40.
KUWA MJANJA USIDANGANYIKE KUNUNUA BIDHAA FEKI,NUNUA BIDHAA ORIJINO ZA IVORI IRINGA,  EPUKA KUTAPELIWA.
ZINGATIA-Iwapo kuna utofauti wa Bidhaa unayoiona na kuitilia shaka Tafadhari usisite kuwasiliana nasi.
       Imetolewa na
MKURUGENZI MKUU
I. F. B



RAIS WA VIKOBA NDANI YA KIPINDI CHA DANGACHEE

SIMU TV: UCHAMBUZI WA MAGAZETI APRIL 17, 2016

Kariakoo ya leo

$
0
0
Msitu wa majumba ya Kariakoo jijini Dar es salaam unavyoonekana kutoka jengo jipya la Mobile Plaza mtaa wa Uhuru.

Yale yale....Kumbe daraja la Kigamboni liko kwa watani wetu wa jadi

DIAMOND PLATINUM'S KAPAGAWISHA BONANZA LA VODACOM FUNGUA SEMESTER HATAREEEE-MABIBO HOSTEL

$
0
0
 Madansa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya bongo fleva, Diamond   Platinum’s wakifanya yao wakati wa bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania lililoshirikisha vyuo vikuu vyote vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Mabibo hosteli hapo jana.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya bongo fleva, Diamond   Platinum’s akiwapagawisha mashabiki wake kwenye bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania lililoshirikisha vyuo vikuu vyote vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Mabibo hosteli hapo jana.
 Diamond   Platinum’s akiwapagawisha mashabiki wake kwenye bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania lililoshirikisha vyuo vikuu vyote vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Mabibo hosteli hapo jana.
 Nyomi ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya jijini Dar es salaam na mashabiki wa msanii wa muziki wa kizazi kipya bongo fleva, Diamond   Platinum’s(hayupo pichani)wakipagawa naye wakati wa bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania lililoshirikisha vyuo vyote vikuu vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya  Mabibo hosteli hapo jana. 

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

VODACOM FUNGUA SEMESTER HATAREEEE MABIBO HOSTEL DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St.Joseph jijini Dar es Salaam,Aisha Ramadhan,akiumiliki mpira wakati timu yake ilipopambana na timu ya Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere Memorial hapo jana katika  bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania, lililoshirikisha vyuo vikuu vyote vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Mabibo hosteli hapo jana.
 Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya jijini Dar es Salaam,wakimkimbiza kuku wakati wa bonanza la Vodacom fungua semester lililoandaliwa na Vodacom Tanzania lililoshirikisha vyuo vikuu vyote vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Mabibo hosteli hapo jana.
John Mwakipesile ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam,akiruka juu kujaribu kumtoka beki wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) Abbakari Omary wakati timu hizo zilipomenyana hapo jana na kutoka suluhu ya bila kufungana katika  bonanza la Vodacom fungua semester  lililoandaliwa na Vodacom Tanzania,lililoshirikisha vyuo vikuu vyote vya jijini Dar es Salaam na kufanyika katika viwanja vya Mabibo hosteli hapo jana.

OLE SENDEKA ANOGESHA SHEREHE ZA DIWANI WA KATA YA ENGARENAIBOR LONGIDO MKOANI ARUSHA

$
0
0
 Msemaji wa CCM Ole Sendeka akiwa na wenyeji baada ya kuwasili Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani Arusha akiwa katika ziara ya kikazi jana.
 Wananchi wakiwa wamesheheni uwanjani wakati wa sherehe hizo za kumpongeza Diwani wa Kata ya Engarenaibor 
 Dada wa Kimasai akilia kutekeleza moja ya mila za kupokea mgeni muhimu, Msemaji wa CCM Ole Sendeka alipofika katika Kata ya Engarenaibor wilayani Longido akiwa katika ziara ya kikazi
 Wenyeji wa Jamii ya Kimasai wakiwa wamejipanga kumpokea Ole Sendeka kwenye eneo la sherehe katika kata ya Engarenaibor
 Msemaji wa CCM, Ole sendeka akisalimiana na baadhi ya viongozi alipowasili kwenye uwanja wa sherehe, katika Kata ya Engarenaibor wilayani Longodo mkoani arusha
 Ole sendeka akimtia baraka kimila mwari wa Kimasai alipowasili kwenye uwanja wa sherehe katika Kata ya Engarenaibor wilayani Longido mkoani Arusha.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images