Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110144 articles
Browse latest View live

WAZIRI UMMY ATEMBELEA -MNH- ARIDHISHWA NA UKARABATI WA MATERNITY BLOCK TWO.

$
0
0
  Waziri Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH  Profesa Lawrence Museru wakitoka ndani ya jengo hilo la wazazi “ Maternity Block Two” leo Apriil 18, 2016.
Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Lawrence Museru (kushoto) akimueleza jambo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mara baada ya kutembelea jengo hilo

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja nje ya jengo la Maternity Block Two  na baadhi ya Wakurugenzi wa idara wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, aliyesimama katikati kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MNH Profesa Lawrence Museru.



WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kukagua ukarabati wa jengo la wazazi- Maternity Block Two - ambao bado unaendelea.

Akizungumza mara baada ya kutembelea jengo hilo Waziri Ummy amesema anaridhishwa na zoezi hilo la ukarabati ambapo amesisitiza kuwa ni faraja sasa kuona hakuna mama mjamzito anayelala chini.

“ Kuwepo kwa jengo hili ni faraja kwa kina mama nafurahi kuona ukarabati unaendelea vizuri na upo katika hatua nzuri  kwakweli mnastahili pongezi kwani mnafanya kazi nzuri” amesema Waziri Ummy.
Maternity Block Two mpaka sasa kuna jumla ya vitanda 63 ambavyo vinatumika na wakina mama wanaendelea kupatiwa huduma.

MBUNGE WA KINONDONI, MAULID MTULIA ASISITIZA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo Kinondoni, Maulid Mtulia akizungumza na wananchi Jimboni kwake juu ya kuwasisitiza wananchi kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambayo kwasasa inapatikana Jimboni kwake kwa ada ya shilingi elfu 40,000 kwa mwaka mzima. mwananchi ukiwa na kadi hiyo utamuona Daktali utapa vipimo na kupatiawa dawa. bila kutoa gharama yoyote, katika mkutano huo ulifanyika  kwenye viwanja vya Magomeni jijini Dar es Salaam.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob kizungumza na wananchi wa Wilaya yake juu ya  kuwashawishi  Serikali iwalipe fidia waliobomolewa nyumba zao  lakini mbali na hayo mpaka sasa waathirika wote wameandaliwa mpango maalumu ili kunusuru Maisha yao.
Sehemu ya wananchi waliofika kwenye mkutano huo ulio fanyika kwenye viwanja vya Magomeni jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka ya Globu ya Jamii)

VIJANA KUNUFAIKA NA 'PROGRAM YA AJIRA YANGU' KWA KUANDIKA RASIMU YA WAZO.

$
0
0
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) jijini Daar es Salaam leo kuhusiana na Progrmu ya umoja wa mataifa kuhusu Ajira kwa vijana. Kushoto ni Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa Mtaifa,Anamarie Kiaga.
 Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa MtaifaAnamarie Kiaga akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari(Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo. kuhusiana na mawazo ya kibiashara yatakayoendeshwa na umoja wa mataifa. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa.
Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa Mtaifa,Anamarie Kiaga katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam l

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
VIJANA wametakiwa kuchangamkia fursa ya ajira kwa kuandika rasimu ya wazo la biashara katika eneo ambalo wanaweza kuendelea kiuchumi.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji la Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa amesema kuwa program ya hiyo ya ajira ni yangu linafanywa kati ya Baraza hilo na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ikiwa ni lengo kuwawezesha vijana katika mitaji ili waweze kuboresha biashara zao pamoja na kutengeneza ajira kwa wenyewe na kwa vijana wengine.

Amesema kuwa idadi ya vijana katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania inaendelea kukua kwa kasi na hivyo kuongezeka kwa vijana wengi wasio na ajira, hali dunia ya maisha ,ukosefu wa mitaji, ukosefu mbinu jumuishi pamoja na kukosa fursa za ajira.

Issa amesema kuwa program ya ajira yangu itahusisha vijana kuanzia miaka 18 hadi 35 kwa wale ambao wanataka kuanza biashara au wanaotaka kupanua na kuboresha biashara zao.

Amesema mchanganuo wa biashara katika mashindano hayo ni katika sekta za Kilimo,Usindikaji, viwanda, biashara inayohusu vyombo vya habari, masoko,mawasiliano, michezo, vifaa sanaa na Utamaduni, ,Utalii na Burdani, Biashara inayogusa mazingira na Utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na biashara za kijamii, Biashara ya Habari na Mawasiliano,Teknolojia ikiwa ni pamoja na ushindikaji biashara.

Amesema kuwa taratibu za uombaji utahusisha awamu tatu ya kwanza ni kujaza fomu ambazo zitapatikana katika tovuti za ILO pamoja na NEEC na maombi hayo yataanza kupokelewa kuanzia leo hadi mei 9 mwaka huu.

KIJANA YUNUS MTOPA AONDOKA NA KITITA CHA DOLA ELFU TANO ZA STATOIL TANZANIA

$
0
0
Mshindi wa Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, Yunus Omary Mtopa, akionekana ni mwenye furaha sana baada ya kujinyakulia kitita cha dola elfu 5, kwa kuonekana wazo lake la Biashara ya Miwa kuwa bora zaidi ya wenzake. Hafla ya shindano hilo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.

Mwaka huu shindano hili lilivutia vijana zaidi ya 400 ambao waliwasilisha mawazo ya biashara zao zinazolenga sekta mbalimbali za uchumi kama kilimo, ufugaji, mawasiliano, na biashara nyingine ndogondogo. Vijana waliruhusiwa kushiriki mmoja mmoja au hata kuunda vikundi vya watu wawili mpaka watatu.
Jaji Mkuu katika Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, Dkt. Neema Muro, akitoa maelezo mafupi ya washiriki wa shindano hilo kabla ya kumtangaza mshindi.
Sehemu ya Wageni mbali mbali waliohudhulia hafla hiyo, wakiwa makini kumsikiliza jina la Mshindi wa Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es salaam.
Mgeni rasmi katika Hafla ya kumtangaza Mshindi wa Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi Issa, akikabidhi mfano wa hundi kwa Mshindi wa Shindano hilo, Yunus Omary Mtopa.
Mgeni rasmi katika Hafla ya kumtangaza Mshindi wa Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bengi Issa (wa nne kulia), Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanna-Marie Kaarstad (wa pili kushoto), Meneja Mkazi wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Øystein Michelsen (shoto) wakiwa katika picha na washiriki wa shindano hilo.

MWONEKANO WA ENEO LILILOBOMOLEWA JIJINI DAR.

$
0
0
 
Mwonekano wa maeneo yaliyobomolewa kipindi cha bomoa bomoa. 

SERIKALI YALAANI TUKIO LA KUNAJISIWA NA KUUAWA KWA MTOTO WA UMRI WA MIAKA TISA (9) MKAZI WA KIJIJI CHA KAPANGA, WILAYANI SUMBAWANGA

$
0
0
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto inalaani vikali tukio La mauaji ya mtoto wa kike, umri miaka 9, ambaye alininajisiwa kwa zamu na watu wasiojulikana, na hatimaye kumkata mapanga yaliyosababisha kuuawa kwa mtoto huyo mdogo, katika kijiji cha Kapanga, wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Wizara imepokea kwa huzuni kubwa taarifa kuhusu mazingira ya mauaji ya mtoto huyo, ambaye alifanyiwa ukatili mkubwa yaliyosababisha kifo cha mtoto huyo katika umri mdogo.

Wizara inapongeza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima, ambaye amelitaka jeshi la polisi wilayani Sumbawanga kuhakikisha wanawasaka na kuwatia mbaroni watuhumiwa wa mauaji ya mtoto ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika, na hivyo kuwa fundisho kwa watu wengine.

Wizara inapongeza ushirikiano uliooneshwa na wakazi wa kijiji cha Kapanga wilayani Sumbawanga, katika kumtafuta mtoto toka mafichoni kwa ajili ya kuokoa uhai wake. Jitihada zilizofanywa na jamii ya Kapanga ni uthibitisho kuwa, ulinzi wa mtoto ni jukumu la wazazi, walezi na watu wote katika jamii.

Kwa niaba ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, tunatoa pole kwa marafiki wa mtoto, wazazi, ndugu na majirani na familia kwa ujumla, na tunawaomba kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki cha majonzi makubwa.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Erasto T. Ching’oro (Msemaji)
18/4/2016

MKATABA WA SOKO LA MACHINGA COMPLEX KUPITIWA UMPYA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar eS Salaam, Paul Makonda (mwenye tinted kushoto)  akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wakitembelea soko la machinga Complex leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar eS Salaam, Paul Makonda (mwenye suti mbele)  akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wakitembelea soko la machinga Complex leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wafanyabiashara  katika soko la machinga Complex leo mara baada ya kutembelea na Kamati ya Ulinzi na Usalama  jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema kuwa waliongia mkataba wa ujenzi wa soko la Machinga Complex unatatizo kutokana fedha nyingi kudaiwa  baada ujenzi sh.bilioni 36 huku ujenzi wa jengo hilo ni zaidi ya sh.bilioni 12.

Akizungumza leo baada ya kutembelea jengo hilo Mkuu wa Mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa, Makonda amesema kuwa kutokana hali hiyo anaunda kamati kuanzia kesho kuchambua mkataba huo kujua ni nani wamehusika na kwa nini waliingia au waliingia wakiwa wamekunywa pombe.

Amesema baada ya kuchambua wale waliohusika katika mazingira ya rushwa watachukuliwa hatua kutokana na kuiongezea mzigo serikali kwa masilahi yao.

Makonda amesema hata utaratibu wa ugawaji wa vizimba una matatizo kutokana baadhi ya watumishi wenye nafasi zao  kumiliki vizimba na kupangisha watu wafanyabiashara.

‘’Nitahakikisha mkataba wa machinga Complex una majibu ya kutosha juu ni nani waliohusika katika kubebesha mzigo serikali kwa wananchi wake’’ .amesema Makonda

Amesema katika mazingira hayo jengo hilo kwa fedha hiyo watu wafanyabiashara hawawezi kuilipa mpaka kuangaliwa uhalali wa mkataba wa ujenzi wa jengo hilo.

Aidha amesema kuwa wananchi wa Dar es Salaam lazima wachukie rushwa ili kuweza kupata huduma bora ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za rushwa na wanaotoa hata kama wanyonge hatua zitachukuliwa.

Amesema katika wafanyabiashara ndogo ndogo  wanaozungusha biashara zao katika mitaa waombe maeneo ya kufanyia kazi na kuweza serikali kupata kodi yake.

BREAKING: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi wa BOT, Amatus Liyumba afariki dunia

$
0
0
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania ( BOT), Amatus Liyumba amefariki dunia leo katika Hospitali ya Agha Khan alikokuwa akipatiwa matibabu, msiba uko nyumbani kwake maeneo ya Triple Seven, Mikocheni jijini Dar es salaam. Taarifa zaidi zitawajia baadae kidogo. 

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA AZINDUA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA 2D NHC MOROGORO

$
0
0

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya akifunua pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la jengo la biashara na Ofisi la 2D la mjini Morogoro lililojengwa kwa thamani ya Shilingi bilioni 4.3. Jengo hilo ni la ghorofa nne likiwa na eneo la chijni kwa ajili ya maegesho ya magari . Ni mradi wa kwanza kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu mara tuu baada ya kuwashwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Nyumba la Taifa, Felix Maagi ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa akiupokea kwenge mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.
Meneja wa Shirika la Taifa, Veneranda Seif akiupokea kwenge mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.

OPERESHENI YA KUONDOA OMBAOMBA YAGONGA MWAMBA, POLISI WAJIPANGA NA MKAKATI MPYA.

$
0
0
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,CP.Simon Sirro akionyesha silaha mbili  kwa waandishi wa habari walizokamata kwa jambazi Shaban Ramadhan baada kupewa taarifa na wananchi leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,CP.Simon Sirro akionyeshakwa waandishi wa habari mitambo ya kutengeneza pombe aina ya Gongo leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
OPERESHENI ya kuondoa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam limegonga mwamba kutokana na kukinzana na baadhi ya mamlaka katika kuwaondoa watu hao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam leo , Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP),Simon Sirro amesema kuwa operesheni ya kuondoa omba omba limeshindikana kutokana na baadhi ya mamlaka kushindwa kuhusishwa.

Amesema kuwa wanaendelea kujipanga kwa kuhusisha mamlaka zote ili kuweza kutekeleza operesheni hiyo kwa ufanisi.

Amesema kuwa kuna omba omba wengine wameweza kuondoka baada ya tangazo kutolewa hivyo waliobaki waondoke kutokana na operesheni itakayoanza hata angalia uso wa mtu.

Jeshi Polisi limeweza kukusanya zaidi ya sh. Milioni 911 zimekusanywa katika makosa mbalimbali ya magari  pamoja na pikipiki katika jiji la Dar es Salaam.

Kamanda Sirro amesema kuwa hawajisifii kukusanya fedha hizo nia yao ni kuona watu hawafanyi makosa ya usalama barabarani.

Wakati huo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata jambazi sugu, Shaban Ramadhan (35) ambaye alikuwa anamiliki bunduki mbili za kivita SMG na risasi nane.

Kamishina Sirro amesema kuwa walipata taarifa kutoka kwa watu juu ya mtu huyo kumiliki silaha ambapo alikutwa na silaha moja huko moja ikiwa kwa rafiki yake wa kike, Fatuma Salehe (20).
Aidha jeshi la polisi limeonya wananchi kununua gari katika sehemu zinazotambulika na zinalipa kodi kutokana na kuibuka uhalifu watu kuuza gari zisizo kuwa zao.

MABADILIKO YA MUDA WA MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI SIKU YA JUMANNE TAREHE 19 APRILI 2016

$
0
0
 Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya ufunguzi wa Daraja la Kigamboni kesho, Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016.

Kutokana na ufunguzi huo, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataarifu watumiaji barabara na Wananchi wote wanaotumia daraja hilo kuwa huduma ya magari kutumia daraja hilo itafungwa kwa muda kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana ili kuwezesha kufanyika kwa sherehe hiyo ya ufunguzi wa daraja. Aidha, huduma katika Daraja la Kigamboni itarejea kama kawaida kuanzia saa 8:00. 
Daraja la Kigamboni lililoanza kutumika tarehe 16 Aprili, 2016 lina urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5.  

Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu  (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
18 Aprili, 2016.

MH. RIDHIWANI KIKWETE ATEMBELEA ENEO LINALOFANYIKA UKARABATI WA BOMBA LA MAJI LILILOKATIKA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani, Mh. Ridhiwani Kikwete (mwenye fulana nyekundu) akiangalia maendeleo ya ukarabari wa Bomba kubwa la Maji lililokatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi hapa nchini, wakati alipotembelea eneo hilo lililopo katika Karavati bondeni Msata -Kihangaiko, Chalinze. Juhudi za ujenzi zimekuwa zikiendelea toka siku lilipobainika tatizo hilo na matarajio ni kumalizika jioni hii na maji kusukumwa kuanzia kesho.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani, Mh. Ridhiwani Kikwete, akipatiwa maelezo na mmoja wa mafundi wanaofanya ukarabari wa Bomba kubwa la Maji lililokatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi hapa nchini, lililopo katika Karavati bondeni Msata -Kihangaiko, Chalinze.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani, Mh. Ridhiwani Kikwete, akiendelea kuangalia maendeleo ya ukarabari wa Bomba kubwa la Maji lililokatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi hapa nchini, lililopo katika Karavati bondeni Msata -Kihangaiko, Chalinze.
Mafundi wakiendelea na kazi.

UFAFANUZI JUU YA UVUMI KUHUSU HALI YA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII (NSSF)

$
0
0
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zisizo rasmi kuhusu hali na mwenendo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Baadhi ya taarifa hizo zimekuwa zikieleza kwamba mali za Mfuko huo zimetumiwa vibaya na hivyo kuathiri mafao kwa wanachama.

Taarifa hizi zimesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wanachama wa NSSF na wadau wa Sekta ya Hifadhi ya jamii kwa ujumla kwa kuhofia usalama wa wa fedha na mafao yao.

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inapenda kuwaondoa hofu wanachama wote wa Mfuko wa NSSF na Wananchi kwa ujumla na kuwahakikishi kwamba Mfuko wa NSSF upo katika hali nzuri kifedha na unaendelea kulipa mafao ya wanachama kama kawaida.

Kama mnavyofahamu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko alikwishateuliwa na anaendelea na majukumu ya kusimamia shughuli zote za Mfuko.

Vilevile, taratibu za kupata Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko huo zipo katika hatua za mwisho.

Aidha, SSRA kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania kwa mamlaka waliyopewa chini ya Kifungu cha 6(2) (c) cha Sheria Na.8 ya mwaka 2008 ikisomwa pamoja na kifungu cha 40 na cha 48 wanaendelea kufanya kaguzi za Mifuko yote ukiwemo Mfuko wa NSSF kwa lengo la kuhakikisha kwamba muda wote Mifuko yote inakuwa katika hali nzuri kwa maslahi ya wanachama na taifa kwa ujumla.

Mwisho, Mamlaka inapenda kuwaondoa wasiwasi wanachama walioathirika na taarifa hizi pamoja na wanachama wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuwahakikishia kwamba fedha na mafao yao yapo salama na Mamlaka inazifanyia kazi kero zao kwa bidii kubwa.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar es Salaam

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI MOROGORO LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasha Mwenge wa Uhuru kuzindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2016 leo Aprili 18, 2016.  sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro. Kulia ni Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto - Zanzibar Mhe. Modelin Kastiko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016 George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Taifa kwenye Sherehe za uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa zilizofanyika leo april 18, 2016 katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
Vijana wa halaiki wakiwa Uwanjani, wakati wa Uzinduzi wa Mbio za Mwenge kwa Mwaka 2016.

Mkuu wa mkoa apapana na Sakata la kiwanja namba 28-A kilichopo katika eneo la Bugando jijini Mwanza

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ameuagiza uongozi wa Jiji la Mwanza kuhakikisha linakabidhi kiwanja namba 28-A kilichopo katika eneo la Bugando ifikapo Aprili 25, 2016 kwa mmiliki halali wa kiwanja hicho bwana Justine Eminoga ambacho amekuwa akikidai kutoka kwa mfanyabiashara wa Jijini humo kwa zaidi ya miaka sita sasa. 
Mhe. Mongella amefikia hatua hiyo mara baada yakupokea malalamiko kutoka kwa bwana Justine ambaye alifika katika Jiji la Mwanza kwa ajili kufatilia suala lake ambalo limedumu kwa zaidi ya miaka sita sasa. Akitoa malalamiko yake mbele ya mkuu huyo wa mkoa, bwana Justine alidai kuzulumiwa kiwanja hicho na mfanyabiashara aliye mtaja kwa jina Shanif Mansour ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kwimba. 
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ametoa siku saba kwa halmashauri za mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kuhakiki  watumishi, ili kubaini endapo kuna watumishi hewa waliosalia katika zoezi la awali, zoezi la sasa ambalo linasimamiwa na Ofisi ya katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza kwa kamati maalumu zilizo undwa na mkuu wa Mkoa huo. 
Akiwa katika ziara hiyo mkuu huyo wa mkoa aliagiza kukamatwa kwa Afisa Utumishi msaidizi wa jiji la Mwanza Henry Sedetale, ambaye alisaidia watumishi hewa watano kuchukua mikopo ya zaidi ya Mil.90 kutoka katika benki tofauti tofauti, hata hivyo taarifa kutoka  Taasisi yakupambana na kuzuia rushwa mkoani Mwanza  iliyotolewa wakati wa kikao hicho na mkuu wa Takukuru mkoani humo, ilisema mtuhumiwa huyo tayari alikuwa ametiwa nguvuni na taasisi hiyo kwa mahojiano zaidi.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza yupo katika ziara kujitambulisha katika mkoa huo na hii ikiwa ni Wilaya yake ya tatu mara baada yakutembelea wilaya za Misungwi na Magu hapo awali.

Imetolewa na


Atley J. Kuni

AFISA HABARI NA MAHUSIANO –RS

MWANZA.


18 Aprili, 2016


RAIS DKT. MAGUFULI ATINGA BENKI YA CRDB TAWI LA HOLLAND JIJINI DAR LEO

$
0
0
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezua taharuki mjini leo baada ya kufika katika Tawi la CRDB (Holland Branch), akiwa kwenye gari binafsi lenye namba T 182 DFQ huku likiwa halina nembo ya Adamu na Hawa wala bendera.

Tukio hilo lililodumu kwa  takribani dakika 25, limetokea majira ya saa nne asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam katika tawi la benki hiyo ambalo liko katika makutano ya Barabara ya Ohio na Samora bila kutarajiwa.

 Mara baada ya Rais Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo makutano ya barabara hizo yalifungwa huku ndipo rais aliposhuka kwenye gari  na kuingia ndani ya benki hiyo.

Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliokuwa wakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyo ilibidi wazuiwe kuingia huku huduma ikiendelea tu kwa wale ambao waliokwisha ingia.

Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais kuingia benki kwa staili ile kwani baadhi ya wananchi kudai kuwa hawajaona tukio kama lile kwa marais wote waliopita.

James Charles, ambaye ni dereva wa Texi, alisema baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimalishwa walishtuka huku wasijue ni nini kinaendelea, hadi pale walipomuona Rais Magufuli akishuka kwenye gari hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea ofisi yake ya zamani.

“Lakini kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja hata hivyo hatujui kama hiyo ilikuwa inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu haiwezekani aende akachukue fedha kwa utaratibu ule ngoja tusubiri tutasikia amefuata nini,” alisema Charles.

Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu, alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.

“Mimi wakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni nikisubiri huduma kwa ujumla kila mmoja wetu alishtuka lakini hatukujua kilichomleta,”alisema.


Baada ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka alitoka na kuingia kwenye gari huku akiwapungia mkono wananchi.
Muuza maji (kushoto) akishangaa gari alilopanda Rais Magufuli leo asubuhi wakati akitoka Benki ya CRDB tawi la Holland.
Gari alilokuwa amepanda Rais John Magufuli lenye namba za usaji T 182 DGQ likitoka katika benki ya CRDB tawi la Holland lililopo katika makutano ya barabara ya Samora na Ohio jijini Dar es Salaam.
Rais John Magufuli akiwa ndani ya gari lenye namba za usajili T182 DFQ huku akiwapungia mkono watu waliokuwa nje ya Benki ya CRDB tawi la Holland jijini Dar es Salaam jana, wakati akitoka katika benki hiyo. (Picha na Francis Dande)

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA NDG. ALLY SALUM HAPI KUWA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI

$
0
0
NDG. ALLY SALUM HAPI  MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MPYA

BREAKING NYUZZZZ.....HAMPHREY POLEPOLE ATEULIWA KUWA MKUU WA WILAYA YA MUSOMA

$
0
0
Hamphrey Polepole 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Hamphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara.

Bw. Hamphrey Polepole anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Musoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (Mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Uteuzi wa Bw. Hamphrey Polepole umeanza leo tarehe 18 Aprili, 2016

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
18 Aprili, 2016

SYMBION POWER-TANZANIA REACTS OVER DUBAI BASED FIRM, RENTAL SERVICES AND SOLUTION ON TAX CLAIMED

$
0
0

Paul Hinks, President Symbion Power Limited.
K-VIS MEDIA/Reporter

Symbion Power, today brushed off what it described as fraudulent and grossly exaggerated claims by a Dubai based firm, Rental Services and Solutions and it’s associated sub suppliers.
Speaking from Washington DC, Symbion Senior Vice President of Communications and Public Affairs Adi Raval said “ This is actually a tax matter. This company and it’s sub suppliers were working as a sub-contractor to Symbion for 3 years from 2011 to 2014. During that time none of them paid the Tanzania government a single dollar of tax, as they are required to by law”.
He continued “ This company maintained a presence in Tanzania and they had expatriate and local staff based in Arusha, Dodoma and Dar es Salaam. The law requires that they pay taxes and they have not done that. 
"We have withheld tax from payments to them and we have paid that money to the Tanzania Revenue Authority. When they produce a certificate that shows they have paid their taxes to the TRA we will release further payment to them”.

TIZA YA JOTO LA ASUBUBI YA RADIO EFM 93.7 APRILI 19, 2016

Viewing all 110144 articles
Browse latest View live




Latest Images