Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Wafanyabiashara kutoka nchini Oman wafanya ziara mkoani Tanga

$
0
0
                Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara za Vetenari Tanzania "TVLA" Dkt. Furaha Mramba akiwakaribisha baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini Oman waliopo nchini kwa ziara ya siku tatu (3) inayomalizika leo, ambao walitembelea katika Taasisi  ya utafiti na uchunguzi wa wadudu na magonjwa waenezayo "VVBDRI -TANGA" inayosimamiwa na wakala hiyo na kutembelea sekta ya mifugo ili kuweza kujionea fursa za uwekezaji kupitia miradi hiyo.
 Kiongozi wa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Oman Bw. Warith Al- Kharusi akieleza  malengo ya ziara yao Mkoani Tanga ambapo alieleza kuwa wamekuja kutembelea mradi wa shamba la mifugo ili waweze kujionea fursa za uwekezaji zinazoweza kupatikana kupitia mradi huo na miradi mingine watakayoitembelea.  
 Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Omani wakiongozwa na viongozi wakuu na maafisa  wa Taasisi za TVLA na VVBDRI-TANGA wakiwasili katika shamba la utafiti Mivumoni lililopo Wilayani Pangani Mkoani Tanga lenye ukubwa wa ekari 12789.6 ili kuweza kuona shughuli za ufugaji zinazofanyika katika shamba hilo

 Bw. Warith Al - Kharusi akijadili jambo na wafanyabiashara wenzie wakati walipokuwa wakitembelea shamba hilo linalofuga Ngo'mbe, mbuzi na Kondoo, ambapo mpaka sasa Taasisi ya VVBDRI - Tanga imeweza kutumia asilimia 20 ya shamba hilo kwaajili ya shughuli za ufugaji na sehemu inayobaki bado haitumiki.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NEWS ALERT: TAKUKURU KUKATA RUFAA DHIDI YA HUKUMU YA MHANDO NA WENZAKE

$
0
0
Kufuatia wadau wengi kuhitaji kujua hatua zitakazochukuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) dhidi ya hukumu ya kesi ya rushwa Na. 75/2014 iliyokuwa ikimkabili Bw. William Mhando aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wenzake watano.

TAKUKURU inapenda kuufahamisha umma kwamba inafanya taratibu za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iliyosomwa tarehe 14/4/2016 na Mhe. Hakimu Mkazi Hellen katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaniaba ya Hakimu Mkazi Mkuu Mhe. Kyey Rusema. Katika hukumu hiyo washtakiwa wote sita (6) waliachiwa huru.

Aidha, TAKUKURU inawataka wadau na wananchi kwa ujumla kutambua kwamba ni utaratibu wa kisheria kwamba upande usioridhika na hukumu iliyotolewa kukata rufaa katika Mahakama ya juu.

MHASIBU WA HALMASHAURI YA SINGIDA KIZIMBANI KWA WIZI WA MISHAHARA HEWA

$
0
0
Na Jumbe Ismailly, Singida.

MHASIBU wa Halmashauri ya wilaya ya Singida, Imani Abduli Nyamangaro (44) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida akikabiliwa na tuhuma za mashitaka 57 ya wizi wa mishahara hewa yenye jumla ya shilingi 29,418,642/=.

Mapema Mwendesha Mashtaka,Wakili wa serikali, Michael Lucas Ng’hoboko alidai kwamba kati ya apr, 29  mwaka 2013 na machi, 27 mwaka 2014 mshitakiwa Nyamangaro ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Utemini, mjini Singida kwa makusudi aliiba mishahara hewa ya zaidi ya shilingi milioni 29.4 huku akijua wazi kwamba kitendo hicho ni kinyume na sheria.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Joyce Minde, Ng’hoboko alidai kwamba mshitakiwa huyo alikuwa akijipatia mishahara hiyo ambayo wahusika waliisha staahafu kazi kwa kipindi cha muda mrefu, kupitia akaunti yake no. 50802503513 iliyopo katika Benki ya NMB Tawi la Singida.

Hata hivyo mshitakiwa Nyamangaro alikana kutenda makosa hayo  yote 57 na hivyo kesi yake imeahirishwa hadi apr, 27 mwaka huu itakapotajwa tena.

Hakimu wa Mahakama hiyo,Minde alisema dhamana ya mshitakiwa ipo wazi na kwamba atapaswa kutoa fedha taslimu shilingi 14,709,321/= Mahakamani au awe na mali isiyohamishika yenye thamani inayolingana na kiasi hicho cha fedha.

Hata hivyo hadi Mwandishi wa Habari hizi anaondoka katika Mahakama  hiyo,mshitakiwa alikuwa bado hajatekeleza masharti ya dhamana hiyo.

DKT. MWAKYEMBE AANZA ZIARA MIKOA YA MWANZA NA GEITA

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake Mkoani Mwanza. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Nd, Baraka Konisaga na kushoto ni Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Nd.Biswalo Mganga.

Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe ameanza ziara ya siku tatu katika mikoa ya Mwanza na Geita.

Lengo la ziara yake ni kukagua utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara yake na zile zote zinazohusika na utoaji wa haki kwa wananchi. Taasisi atakazozitembelea ni pamoja na RITA, Ofisi ya Kanda ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Mahakama Kuu na Jeshi la Magereza.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe akikabidhi Cheti cha Kuzaliwa kwa Mama wa mmoja wa watoto aliyesajiliwa katika Kituo cha Afya MakongoroJijini Mwanza. Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa katika Vituo vya Tiba inatekelezwa na RITA, Wizara ya Afya na UNICEF.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe akipewa maelezo ya jinsi motto anaposajiliwa na kupata Cheti cha Kuzaliwa.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dr. Harrison Mwakyembeakiangalia jinsi TEHAMA inavyotumika kutunza Kumbukumbu za Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano.

BIBI KIZEE ABAKWA MKOANI SINGIDA

$
0
0
Pichani ni Bibi kizee mwenye umri wa miaka 84 na mkazi wa Kijiji cha Chungu, tarafa ya Ihanja, wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida akiwa amebebwa na mmoja wa ndugu zake wakati akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mjini Singida kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili kijana mmoja mwenye umri wa miaka 32 (jina lake halikupatikana) anayetuhumiwa kumbaka bibi kizee huyo kwa mara ya tatu sasa ndipo walipofanikiwa kumkamata. (Picha Na Jumbe Ismailly)

BUNGE LATOA UFAFANUZI KUHUSU MKATABA WA LUGUMI

WAFANYAKAZI ‘WAUFAGILIA’ UJENZI DARAJA LA KIGAMBONI

$
0
0
Mmoja wa wataalamu wa kizalendo walioshiriki kwenye ujenzi wa Daraja la Kigamboni Muhandisi Jamal Mruma (kushoto) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) namna mradi huo ulivyowajengea uwezo kiutendaji wafanyakazi wazalendo. Kulia ni Meneja wa Mradi huo huo Bw. Zhang Bang Xu.

SIKU chache kabla ya uzinduzi wa daraja la kisasa la Kigamboni, wafanyakazi na wataalamu wazawa walioshiriki kwenye ujenzi wa daraja hilo wamesema kupitia mradi huo wamepata fursa ya kuongeza ujuzi unaowapa mwongozo katika kutekeleza kwa ufanisi miradi mikubwa inayofanana na huo.

Mradi huo uliogharimu Dola za Kimarekani milioni 135 umetekelezwa na kampuni ya China Railway Construction Engineering Group kwa ushirikiano na kampuni ya China Railway Major Bridge Group ya nchini China.

Wakizungumza kwenye eneo la ujenzi wa daraja hilo jijini Dar es Salaam jana baadhi wa wataalamu na wafanyakazi hao walisema kupitia mradi huo wameweza kujifunza mbinu na teknolojia za kisasa zaidi hatua inayowapa mwanga kuhusiana na utekelezaji wa miradi mikubwa na inayohusisha teknolojia ya kisasa kama huo.

“Mafunzo ambayo tungeweza kwenda kusomea nje ya nchi kwa gharama kubwa tumeweza kuyapata kupitia mradi huu tena kwa vitendo zaidi kwa kuwa tulikuwa tukishirikiana na wenzetu kutoka China bega kwa bega,’’ alibainisha mmoja wa wataalamu hao, Muhandisi Jamal Mruma.

Alitoa wito kwa Serikali na taasisi za elimu ya mafunzo ya ufundi stadi hapa nchini kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kutumia miradi mikubwa kama hiyo kuwajengea uwezo wanafunzi na wataalamu kutoka vyuo hivyo kupata mafunzo kwa vitendo.

“Tulipokea baadhi ya wanafunzi kutoka baadhi ya vyuo hapa nchini ikwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na vyuo vingine waliotembelea kuona mradi na mafunzo mafupi… nahisi tulitakiwa tungechamkia zaidi hii fursa ili waje wengi zaidi,’’ aliongezea

Nae Francis Mambo ambaye ni mkadiliaji ardhi kwenye mradi huo pamoja na kushukuru kwa ushirikiano walioupata kutoka kwa wenzao kutoka China, alitoa wito kwa serikali na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanawekeza nguvu nyingi kwenye kujifunza lugha ya kichina kutokana muingiliano wa kijamii na kiuchumi unaozidi kukua kila siku.

Kwa upande wake Meneja mradi kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group ambao wametekeleza mradi huo kwa ushirikiano na kampuni ya China Railway Major Bridge Group Bw. Zhang Bang Xu alisema mradi huo umehusisha ajira zaidi ya 5000 wakiwemo wataalamu na wafanyakazi huku akionyesha kuridhishwa na uwezo mkubwa wa kiutendaji ulioonyeshwa na wafanyakazi hao.

“Mbali na daraja hili la kisasa walipatata pia fursa ya kujifunza kutengeneza daraja la awali ambalo lilihusisha teknolojia ya kati ambalo ndio lilitumika katika ujenzi wa daraja hili kubwa,’’ alisema.

Alisema kuchelewa kukamilika kwa mradi huo kwa kiasi kikubwa kulisababishwa na changamoto zisizotarajiwa ambazo ziliukumba mradi ikiwemo kugundulika uwepo wa pango- hewa chini ya bahari na hivyo kusababisha wao kutumia zaidi miezi sita kujaza pango-hewa hilo.

“Pamoja na changamoto kadhaa tunashukuru tumekamilisha salama mradi huku kwa kiasi kikubwa tukiwa tumefanikiwa kutunza mazingira ikiwemo bahari yenyewe, uoto jirani na bahari pamoja na kubadili hali ya kiuchumi ya wafanyakazi na majirani wanaoishi jirani na mradi,’’ alishukuru.

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake leo (JUMAMOSI) wanatapa fursa ya kulitumia kwa mara ya kwanza Daraja hilo ili kutoa fursa kwa mkandarasi kuhakiki uwezo na ubora wa daraja hilo kabla halijazinduliwa na Rais Magufuli siku Jumanne.

RAIS WA SUDANI KUSINI SALVA KIIR ATIA SAINI MKATABA WA KUJIUNGA RASMI NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akipokea maua kutoka kwa mtoto Sharon Innocencia Shiyo mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu kwa ajili ya Utiaji saini wa Mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit akiwa amesimama na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.


DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI APRILI 15, 2015

Sababu za Rais Mstaafu JK Kupewa Tuzo ya White House ya Mapambano Dhidi ya Malaria Hizi Hapa

$
0
0
Ten years ago, malaria seemed invincible. Not anymore. As malaria leaders and champions gathered at Cipriani in New York on April 7th for a gala to celebrate the 10th anniversary of Malaria No More, this ancient disease felt like a weakened foe in retreat.

Of course the job is not finished, but the progress is staggering, and many of the people in the room played a direct role in driving it. More than six million people are alive today because bold leaders and strong partners came together across party lines, sectors and continents and said enough is enough: No child should die from a mosquito bite.

The evening highlighted the audacious goals and smart investments that led to a massive scale up of insecticide-treated bed nets, effective testing and treatments, and indoor spraying across Africa. Together, these interventions have slashed malaria deaths on the continent by 71 percent among children under five since 2000.

The gala was a time to reflect on the progress and galvanize champions for the final chapter of the fight. It was also a time to recognize leaders.

Malaria No More’s Board Co-Chair Peter Chernin presented the Inaugural White House Summit Award to Malaria No More founder Ray Chambers and former Tanzanian President Jakaya Kikwete, who founded the African Leaders Malaria Alliance. In a video tribute, President George Bush, President Bill Clinton, Chelsea Clinton, Bill Gates and U.N. Secretary-General Ban Ki-moon each praised the leaders for their roles in bringing people together and tackling malaria head on.
In a conversation moderated by CNN’s Wolf Blitzer, the two awardees shared their thoughts about the progress.

Chambers said “unprecedented partnership” was the key reason for success in the past decade. President Kikwete said the progress gave him the “audacity to say we can eliminate malaria.”

Our CEO, Martin Edlund, presented Malaria No More’s Corporate Leadership Award to Sumitomo Chemical, the leader in net technology and innovation as well as one of the biggest net suppliers in the world. Ray Nishimoto of Sumitomo Chemical, who also serves on the Board of Directors of Malaria No More, received the award and underscored the company’s commitment to continue developing innovative technologies for vector control.

Other longtime supporters and champions filled the room, including Admiral Tim Ziemer, who leads the President’s Malaria Initiative, Malaria No More board members, representatives from the Bill & Melinda Gates Foundation, the African Leaders Malaria Alliance, the Asia-Pacific Leaders Malaria Alliance, The UN Foundation’s Nothing But Nets campaign and many others.

We ended the evening with a video about Osas Ighodaro Ajibade, former Miss Black USA who lost her sister Joy to malaria 10 years ago. She traveled from Nigeria to share her tragic story and remind everyone of the very real and personal toll of the disease.

The next phase of the malaria fight won’t be easy. We need new tools, new money and smart approaches to ending the disease. But the steadfast commitment and energy in that room – and among partners around the world – convinces me that the end of this disease truly is within reach.

WANYAMA PORI WAVAMIA MASHAMBA YA WANANCHI NA KUMALIZA MAZAO YAO

$
0
0
Na Woinde Shizza,Karatu

Wananchi wa kata ya mbulumbulu walalamikia Mmalaka ya hifadhi ya Ngorongoro kushidwa kuzibiti wanyama pori kwani wanaharibu mazao yao.

Hayo waliyasema juzi wakati wa ziara ya mwenyekiti wa CCM mkoa Arusha, Lekule Laizer wakati alipotembelea katika kijiji cah losteti ikiwa ni ziara yake ya kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho.

Walisema kuwa mazao yao yamekuwa yakiaribiwa na wanyama wanaotoka katika hifadhi ya ngorongoro haswa nyakati za jioni na usiku na wametoa taarifa katika uongozi wa mamlaka hiyo lakini hamna hatua zozote ambazo wamezichukuwa.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Aron Saiteu alisema kuwa wanyama hao wamekuwa wanakuja katika mashamba yao ambayo wameotesha mahindi na maharage na kuingia na kula hali ambayo inawarudisha nyuma kimaendeleo na inawakosesha chakula.

Alisema kuwa wamepeleka taarifa za malalamiko katika kituo kidogo ambacho kipo katika eneo hilo lakini hadi sasa hamna kiongozi ambaye amechukuwa hatua .

“awali tulikuwa tunawafukuza wanyama hawa lakini mamlaka ikaja na kutunyima kufukuza wanyama lakini cha kushangaza mara baada ya kutuzuia kufukuza wakatuambia tukiona mnyama tupige simu tatizo lililokuja ukipiga simu unaambiwa na viongozi ambao wapo hapa katika kituo cha wanyama pori cha losteti wanasema hawana magari hivyo hawawezi kuja kufukuza wanyama na sisi wananchi tunashindwa tufanyaje unakuta tembo kaja au mbogo hivi unamfukuzaje jamani inabidi uache ale akitosheka aondoke “alisema Seuri lazier

SOMA ZAIDI HAPA

Wakurugenzi, Waganga Wakuu itangazeni NHIF - Waziri Jaffo

$
0
0
Na Grace Michael

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jaffo amewataka wakurugenzi wa Halmashauri na Waganga wa Wilaya kuhakikisha wanatoa elimu ya umuhimu na matumizi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa watumishi wengine ili waweze kunufaika na huduma hizo.

Mbali na hilo, ameupongeza Mfuko huo kwa jitihada ambazo umekuwa ukifanya katika kushughulikia changamoto mbalimbali hususan za huduma za matibabu katika maeneo yote wanapokutana nazo.

Hayo ameyasema wilayani Kisarawe wakati akipokea msaada wa magodoro 60 kutoka NHIF ambao ambao umekabidhiwa katika Hospitali ya Wilaya hiyo kwa lengo la kusambazwa katika vituo vya afya ambavyo vina uhitaji mkubwa.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jaffo akizungumza na uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa kupokea msaada wa Magodoro 60 kutoka NHIF.

“Katika hili NHIF mmefanya vizuri sana ….na sio hapa tu, nimekuwa nikipita katika maeneo mbalimbali na taarifa zenu nakutana nazo kuwa mmekuwa wepesi sana katika kushughulikia matatizo hasa ya uboreshaji wa huduma za afya pale mnapokutana nayo,”

“Mmeboresha sana huduma zenu kwa wanachama wenu hasa kwa kupanua wigo wa vituo vya kutolea huduma hatua inayowawezesha wanachama kupata huduma mahali popote wanapotaka wao…sasa naomba viongozi wa halmashauri hakikisheni mnawapa elimu watumishi na wananchi kwa ujumla juu ya huduma hizi za Mfuko,” alisisitiza Naibu Waziri Jaffo.

Akitoa maelekezo ya mgao wa magodoro hayo, alimtaka Mganga Mkuu kutoa kipaumbele katika Vituo vya Afya vya Mwanerumango, Masaki na Mzenga kwa kuwa vina uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Rehani Athumani akitoa maelezo ya awali juu ya misaada ambayo Mfuko umetoa katika maeneo mbalimbali.

Kwa upande wa NHIF, akikabidhi magodoro hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Rehani Athumani alisema kuwa Mfuko ulibaini changamoto ya ukosefu wa magodoro wilayani humo wakati ilipopita kwa ajili ya ugawaji mashuka hivyo Mfuko ulidhamiria kuondoa tatizo hilo.

“Tulipita katika vituo mbalimbali wilayani hapa wakati tunagawa mashuka siku ya sherehe za Uhuru ambapo Mfuko pia ulishiriki katika kufanya usafi katika vituo hivyo…baada ya kuona tatizo hilo Uongozi wa Mfuko uliona kuna haja kubwa ya kubana matumizi katika maeneo mengine kwa lengo la kuwasaidia wananchi,” alisema Bw. Rehani.
Naibu Waziri akipata maelezo wodini.

Alisema kuwa jitihada za kubana matumizi zimeuwezesha Mfuko kutoa misaada ya Magodoro 60 wilayani Kisarawe, mabati 400 katika zahanati ya Mpingi, Songea Vijijini, Vitanda 20 na magodoro 20 katika kituo cha afya cha Mjimwema mkoani Ruvuma pamoja na saruji tani tatu katika Shule ya Sekondari ya Kilangalanga.

“Mfuko huu ni wa Watanzania wote sisi tumepewa dhamana ya kuusimamia hivyo ni lazima twende na kasi ambayo Rais wetu anaitaka kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania na niseme tu kwamba Huduma bora za Afya Tanzania inawezekana.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dk. Elizabeth Omingo akiongozana na Naibu Waziri (TAMISEMI) Seleman Jaffo wakati wa kupokea msaada kutoka NHIF.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Waziri Nape adhamaria kurudisha heshima ya Tasnia ya Habari nchini

$
0
0
Na Daudi Manongi-WHUSM

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo amesema kuwa atahakikisha heshima ya tasnia ya habari inarudi baada ya kupitishwa kwa mswada wa sheria ya huduma za vyombo vya Habari.

Waziri Nape ameyasema hayo alipokuwa katika katika ziara mkoani Mara na Shinyanga na kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara hiyo na kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mikoa hiyo.

“Ule mswada utatoa tafsiri ya mwandishi wa habari,maana mwandishi wa habari lazma awe na sifa.Siku hizi anaweza kuwa mtu anauza ndizi alafu akajifunza kupiga picha akajiita na yeye mwandishi wa Habari.Ukifanya ivyo tasnia hii inakosa heshima,kwaiyo sheria ile itatafsiri nani mwandishi wa habari”Alisema Nape.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na wadau waliopo chiniya wizara yake pamoja na watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Mara wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mkoa huo. Wengine pichani ni Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw.Benedict Ole Kuyan(wa kwanza kulia),Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi.Anarose Nyamubi(wa tatu kulia) na Kaimu meya wa manispaa Bw.Wambura Kajala.

Aidha Waziri Nape alisema kuwa kwa kufanya hivi sheria hii itatibu tatizo la kulipwa vibaya na wamiliki wa vyombo vya habari maana mwandishi huyu atakuwa na elimu,maana kama hana elimu mmiliki ataajili mtu anaejua kusema wa kijuweni alafu ndo anamuajiri anakuwa mtangazaji wa radio yake kisa tu anajua kusema.

Pamoja na hayo waziri uyo mwenye dhamana ya wizara nyeti ya habari alisema kuwa sheria hiyo pia itazungumzia maslahi ya mwandishi wa habari,itawabana wamiliki na mswada huu ukipita utarudisha heshima ya tasnia hii ya habari katika nchi yetu.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi. Josephine Matiro akizungumza jambo wakati wa kumkaribisha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye baada ya kuwasili mkoani hapo ili kujua changamoto mbalimbali za watumishi walio chini ya wizara yake na kuongea na wadau wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.

Akizungumzia upande wa radio kujenga nchi waziri nape amewaasa waandishi wa habari na watangazaji wa radio kujenga amani ya nchi yetu kwa kuwaunganisha watanzania kupitia radio zao na si kuwatenganisha akitolea mfano wa yaliyotokea nchini Rwanda kwamba radio zilitumika kuhamasisha mauaji.

Mheshimiwa Nape pia amehaidi kuimarisha vitengo vya mawasiliano serikalini ikiwa ni pamoja na kuwapa maafisa hao vitendea kazi, pia ameliomba jeshi la polisi kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa na amehaidi kuzungumza na jeshi hilo ili waandishi hawa waweze kupata taarifa kirahisi.

Waziri uyo yupo katika ziara ya mikoa ya Kagera,Mara,Shinyanga,Tabora na Singida ikiwa na lengo kuu la kuileta Wizara ya habari,utamaduni,Sanaa na Michezo mikoani na wilayani karibu na wadau.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na katibu wa chama cha mapinduzi(CCM) mkoani Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe(mwenye kofia ya njano) kuhusu maendelezo ya uwanja wa kambarage ambao unamilikiwa na chama hicho mkoani hapo.Mhe.Nape amewaasa viongozi wa mkoa huo kutafta wadhamini ili kuuboresha uwanja huo.
Katibu Tawala mkoa wa Mara Bw.Benedict Ole Kuyan akizungumza na wadau mbali mbali wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo pamoja na watumishi wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye mkoani humo. serikali wa mkoa wa Mara leo hii wakati wa Ziara ya Waziri wa
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo mwandamizi wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bw.John Igomego jinsi mitambo yakurushia matangazo ya shirika hilo inavyofanya kazi mkoa wa Mara.

WABUNGE WATAKIWA KULIZUNGUMZIA SUALA LA ONGEZEKO LA KASI YA IDADI YA WATU NCHINI

WANAFUNZI WA KINYEREZI WAFURAHIA KUFUNDISHWA SOMO LA KOMPYUTA KWA VITENDO

$
0
0
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kinyerezi jijini Dar es salaam ambao mwaka jana walipatiwa msaada wa kompyuta 25, Televisheni yakufundishia pamoja na printa kutoka taasisi ya inayojishughulisha na jamii ya Vodacom Tanzania Foundation kupitia mradi wake wa Smart Schools wameeleza kuwa wanafurahia kujifunza somo la kompyuta kwa vitendo tofauti na ilivyokuwa hapo awali kabla ya kupatiwa msaada huo.

Wakieleza hisia zao baada ya ujumbe wa taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kutembelea shuleni hapo jana kujionea maendeleo ya wanafunzi hao tangu wapatiwe msaada huo walisema kuwa  hivi sasa ndoto zao za kutoachwa nyuma katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia zinaanza kutimia.

Akiongea kwa niaba ya wenzake,mwanafunzi Christina Salum anayesoma kidato cha nne shuleni hapo alisema kuwa tangu wapate msaada huo na kujifunza somo la kompyuta kwa nadharia na vitendo wanafunzi wengi wameanza kuelewa matumizi ya kompyuta tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali.

“Kwa sasa tukifundishwa kompyuta tunaweza kuelewa kwa haraka na mwamko wa wanafunzi kutaka kuelewa matumizi ya kompyuta umekuwa mkubwa na  woga wa kudhani kuwa teknolojia ya matumizi ya kompyuta ni ngumu umeondoka ,tunashukuru Vodacom Foundation kwa kutuwezesha kutobaki nyuma katika ulimwengu wa kisasa wa sayansi na teknolojia.

Naye mwalimu anayefundisha somo hilo shuleni hapo , Lupakisyo Igomole amesema japo wanafunzi wanaelewa na wanapenda sana somo hilo bado wanakabiliwa na changamoto  kubwa ya viti vya kukalia hali inayowalazimu  kuwafundisha wanafunzi hao wakiwa wamekaa chini sakafuni.

Mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza alisema kuwa  changamoto hiyo itafanyiwa kazi ili kuwawezesha wanafunzi hao kusoma somo hilo katika mazingira rafiki zaidi  wakiwa wamekaa kwenye viti .
Mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza (kulia)akiwafafanulia jambo baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Kinyerezi jijini Dar es Salaam kuhusiana na somo la kompyuta alipotembelea shuleni hapo kupata mrejesho wa maendeleo baada ya kutoa msaada wa kompyuta 25, Televisheni yakufundishia pamoja na printa kupitia mradi wa Smart Schools mwaka jana.
Mwalimu wa masomo ya sayansi wa shule ya sekondari Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Lupakisyo Igomole (kushoto) akiwafundisha kwa vitendo baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo kupitia kompyuta wakati walipotembelewa na oungozi wa taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation waliotoa msaada wa kompyuta hizo mwaka jana kupitia mradi wao wa Smart Schools.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Kinyerezi jijini Dar es Salaam,Wakijisome kupitia kompyuta wakati walipotembelewa na oungozi wa taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation waliotoa msaada wa kompyuta hizo mwaka jana kupitia mradi wao wa Smart School kutaka kujua maendeleo yao shuleni hapo.
Mwanafunzi wa kitado cha tatu katika shule ya sekondari Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Aurelia Kitenge (kushoto) akimwelezea jambo Mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza wakati alipotembelea shuleni hapo kwa ajili ya kujionea maendeleo ya mradi wao wa smart Schools ambao ulitoa msaada wa kompyuta hizo shuleni hapo.

MKE WA MTOTO WA MALKIA WA NORWAY AKUTANA NA VIJANA WALIOINGIA 5 BORA YA SHINDANO LA MASHUJAA WA KESHO LA STATOIL TANZANIA

$
0
0

Mke wa Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akifurahia jambo wakati alipokutana na kuzungumza na vijana watano waliongia katika hatua ya tano bora ya shindano la biashara la mashujaa wa kesho ambalo lina dhumuni la kuhamasisha ujasiriamali kwa mikoa ya kusini mwa Tanzania yaani Mtwara na Lindi, kwenye kambi yao iliyopo kwenye Jengo la Statoil ambao ndio wadhamini wa Shindano hilo, Masaki jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Genevieve Kasanga.

Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi kuwasilisha mawazo yao ya biashara ambayo baadae yalibadilishwa na kuwekwa kwenye andiko la biashara.

Mwaka huu shindano hili lilivutia vijana zaidi ya 400 ambao waliwasilisha mawazo ya biashara zao zinazolenga sekta mbalimbali za uchumi kama kilimo, ufugaji, mawasiliano, na biashara nyingine ndogondogo. Vijana waliruhusiwa kushiriki mmoja mmoja au hata kuunda vikundi vya watu wawili mpaka watatu.
Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akisikiliza kwa makini maeneo ya namna shindano hilo lilivyoendeshwa kutoka kwa Afisa wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Eric Mchome.
Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akipokea zawadi ya picha yenye mchoro wa wanyama aina ya Pundamilia, kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Genevieve Kasanga.
Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa shindano hilo.
 Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akiwa katika picha ya pamoja na Sehemu ya Washiriki hao.

HAFLA YA UTIAJI SAINI WA MKATABA WA SUDANI KUSINI KUJIUNGA NA EAC 15 APRIL 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA WADAU WA MRADI WA MABASI YAENDYO HARAKA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa Mradi wa mabasi yaendayo haraka UDA RT, ofisini kwake jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ZIKIWA zimebaki siku chache kabla ya mradi wa mabasi yaendayo kasi kuanza, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa taasisi zinazohusika na utekelezaji wa mradi huo kuhakikisha wanatoa elimu kwa umma ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.

“Katika kipindi hiki cha majaribio, ambacho madereva wameanza kutumia barabara za BRT, hakikisheni mnatoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu namna ya kuvuka barabara, kuzuia wenye bodaboda kutumia barabara hizo kuelezea na matumizi ya taa za barabarani kwa madereva wote,” amesema.

Ametoa agizo hilo jana usiku (Ijumaa, Aprili 15, 2016) wakati akizungumza na wakuu wa taaasisi, watendaji wakuu na wadau wa mradi huo kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu aliwataka watendaji wa wakuu wa taasisi wahakikishe wanapanua wigo na kutumia vyombo vya habari vingi kadri iwezekanavyo pamoja na mitandao ya kijamii katika kuelimisha raia juu ya zoezi hilo.

Akifafanua kuhusu hatua zilizofikiwa kwenye mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale alisema miundombinu kwa ajili ya mradi huo imekamilika na usafiri huo utaanza hivi karibuni.

Mhandisi huyo ametumia fursa huyo kutoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu ya barabara hizo kwa sababu imeigharimu Serikali fedha nyingi.

Naye Mrakibu wa Polisi (SP), John Shawa kutoka Makao Mkuu ya Trafiki alisema kuanzia kesho zoezi la majaribio kwa mabasi yaendayo haraka litaanza hivyo amewaomba wananchi kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani.


"Kuanzia kesho linapoanza zoezi la majaribio kwa mabasi yaendayo haraka ni vema watu wakatumia vizuri barabara hasa madereva wa bodaboda na madereva wengine watambue kuwa hawaruhusiwi kupita katika barabara hizo," alisema.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU AMFUTA MACHOZI MILLEN MAGESE MAPAMBANO DHIDI YA ENDOMETRIOSIS

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu amemfuta machozi Mwanadada, Happiness Millen Magese ambaye ni shujaa wa kipekee kutoka Afrika dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa Endometriosis.

Mama Samia amechukua hatua hiyo jioni ya 15 Aprili 2016 wakati wa hafla maalum ya kumkabidhi tuzo.

Katika kilio chake hicho, Millen kimemfanya Mama Samia kumfuta machozi na kumpa kitambaa, mwanamitindo huyo huku akimweleza kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana naye kwani tatizo hilo si la Millen pekee bali ni kwa wanawake wengi hapa Tanzania.

Mama Samia alimwambia kuwa, tatizo alilonalo la kuziba kwa mirija ya uzazi lipata ufumbuzi na kutaka asilie kwani Serikali inania njema kwa watu wake hivyo wataendeleza juhudi Zaidi huku akifungua milango na mwanadada huyo.
Mama Samia akimfuta machozi Millen ambapo alimwelezea kuwa kwa sasa asiie tena kwani Serikali itahakikisha inapambana na ugonjwa huo ilikusaidia wanawake wengi hapa nchini.

Suluhu alisema kuwa hata yeye tatizo kama hilo lipo katika familia yake, lakini ana amini kwa ushirikiano wa mwanamitindo huyo tatizo hilo linapewa uzito. Alisema kuwa ni kitu kilichokuwa kikimuumiza sana kichwa, ana amini kupitia Millen hata binti yake atapata nafuu.

"Nimefurahi kukutana nawe na Serikali haitakuangusha tutakuunga mkono katika kuhakikisha gonjwa hili linapata ufumbuzi na kutoa elimu kwa kila mtanzania kulitambua"alisema.
Mama Samia akieleza namna walivyopokea tatizo hilo la Millen ambapo amemweleza kuwa Serikali itaendelea kupambana nalo tatizo hilo hivyo kumuakikishia Millen na taasisi yake kumuunga mkono.

Akizungumza kwa upande wake Magese alisema amekuwa akifanya semina mbalimbali kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa, Muhimbili, kuwaelimisha wanawake kuhusu endometriosis.

Alisema Machi 30, mwaka huu Taasisi ya Millen Magese ilikusanya vijana (hususani wa kike) wapatao mia tano kutoka shule za Mugabe, Manzese, Salma Kikwete na Turiani, kuwafundisha, kuwatahadharisha na kuwatanabahi kuhusu Afya, Uenendo, Maisha yao ya kila siku na Changamoto zilizo mbele yao na hususani ikilenga zaidi watoto wa kike ambao wao ndio wahanga wa ugonjwa wa Endometriosis.

Usikose kutazama kipindi cha mizani ya wiki kupitia Azam TV

$
0
0
Usikose kutazama kipindi cha mizani ya wiki kupitia Azam TV na Jamaly Hashim ambapo utamsikia mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo pamoja na aliyekuwa Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali, Mh. Ludovick Utouh wakipongoza juhudi za serikali kutokana na kujenga nidhamu ya juu ya matumizi ya fedha za umma na hatua zinazochukuliwa.Kipindi hiki kitaruka hesho kuanzia mbili na nusu usiku. Usikose.

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images