Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

Ziara ya Mhe. Salva Kiir, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Tarehe 15 Aprili 2016

$
0
0

Mhe. Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini atafanya ziara ya kikazi ya siku moja nchini Tanzania tarehe 15 Aprili 2016. Rais Kiir anakuja nchini kusaini Mkataba wa kuwezesha Jamhuri ya Sudan Kusini kuwa Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo tangazo la kukubaliwa kuwa Mwanachama wa EAC lilitangazwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC uliofanyika jijini Arusha mwezi Machi 2016.
Rais Kiir atawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 3:00 asubuhi na baadaye ataelekea Ikulu na kupokelewa na Mwenyeji wake, Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli. Baada ya hapo, Viongozi hao watashiriki hafla ya uwekaji saini ya Mkataba huo iliyopangwa kuanza saa 5:00 asubuhi na kisha watapata fursa ya kutoa hotuba na kusaini Communique.
Rais wa Sudan Kusini atashiriki hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa heshima yake na Mwenyeji wake kabla ya kuondoka nchini baada ya hafla hiyo.
Sudan Kusini ni nchi ya sita kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo inaongeza fursa nyingi za kiuchumi ambazo zinaweza kuzifaidisha Nchi Wanachama ikiwemo Tanzania, endapo mipango madhubuti itawekwa kuzichangamkia. Fursa hizo ni pamoja na za kibiashara kwa kuwa bidhaa nyingi zinazotumika Sudan Kusini zinaagizwa kutoka Nje ya nchi. Hivyo, jamii ya wafanyabiashara wa Tanzania wanahimizwa kuchangamkia fursa zinazopatikana nchini humo na ndani ya Jumuiya kwa ujumla.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Dar es Salaam, 14 Aprili, 2016

TEASER JOTO LA ASUBUHI LA EFM 93.7 IJUMAA APRIL 15, 2016 KUANZIA SAA 12 ASUBUHI

MAMIA WAUAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA MWANAHABARI ABSALOM KIBANDA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mamia ya waombolezaji, wengi wao wakiwa wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, leo wamejitokeza kuuaga mwili wa mama mzazi wa Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Bw. Absalom Kibanda, leo  asubuhi  huko Masaki jijini Dar es Salaam.
Mama yake mzazi Kibanda, alifariki juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ambako alikuwa akitibiwa ugonjwa wa kiharusi. Mwili wa marehemu Marehemu Mama Gwaseko Kapyela (76)  baada ya kuagwa u mesafiriskwa kwa ndege kuelekea Tukuyu, wilayani Rungwe,  mkoani Mbeya kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi.
Waombolezaji wakimpa pole Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, na kaka yake wakati wa kuaga mwili wa mama yao mzazi marehemu Marehemu Gwaseko Kapyela Masaki jijini Dar es salaam 
Waombolezaji wakimpa pole Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, na kaka yake wakati wa kuaga mwili wa mama yao mzazi marehemu Marehemu Gwaseko Kapyela Masaki jijini Dar es salaam 
 Wanahabari nguli Neville Meena na Peter Nyanje wakiandaa shada la maua na msalaba kabla ya safari ya kwenda Tukuyu kuanza
 Safari ikianza
Waombolezaji wakipeleka jeneza lenye mwili wa mama mzazi wa  Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, baad ya hafla ya  kuaga mwili wa mama yao mzazi marehemu Marehemu Gwaseko Kapyela Masaki jijini Dar es salaam. Kwa picha zaidi ya hafla hii BOFYA HAPA

PROFESA ISSA SHIVJI AMZUNGUMZIA RAIS DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI

SIMU TV: MAPITIO YA MAGAZETI LEO

Waziri Nape afanya Ziara mkoani Kagera

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisalimiana na uongozi wa mkoa wa Kagera baada ya kuwasili mkoani hapo akiwa kwenye ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mkoa huo.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili mkoani Kagera kwa ajili ya kufanya ziara ya kutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara, kupokea taarifa ya mkoa na kuwapatia vitendea kazi maafisa mawasiliano wa mkoa huo.Wengine pichani ni Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw,Jackson Msome na Kaimu katibu tawala mkoa wa kagera Bw.Adam Mohamed Swai.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akikabidhi Tablet tano kwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya maafisa habari wa mkoa wa kagera.Bwana Msome alikuwa akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome ambaye anamwakilisha Mkuu wa mkoa wa kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wakati wa ziara ya waziri huyo katika mkoa wa kagera.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza jambo na waandishi wa habari wakati alipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Kaitaba.Uwanja huo umeshawekwa nyasi za bandia na maboresho mengine yanaendelea.

MLATA: SERIKALI NJOENI NA MKAKATI WA UZAZI WA MPANGO

MKUU WA MKOA WA MOROGORO AWATIA NDANI WACHINA WAWILI KWA KUKAIDI AGIZO LA SERIKALI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe, (katikati) pamoja na ujumbe wake wakifanya ukaguzi wa kushitukiza katika mgodi wa Kiwanda cha Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co Ltd , katika mgodi wa Kiwanda hicho uliopo eneo la Kitongoji cha Mazizi, Kijiji cha Maseyu, Kata ya Gwata, Tarafa ya Mikese, wilaya ya Morogoro, kiwanda hicho kinamilikiwa na wachina, uzalishaji wake ulizuiwa na Serikali kuu tangu mwaka 2010 hadi watakapokamilisha taratibu zote za kisheria zikiwemo na za kimazingira.
Mfanyakazi raia wa China, Wang Jun (33) ambaye ni mtunza stoo katika mgodi wa kutengeneza marumaru wa Kiwanda cha Tanzania Zhong Fa Construction Material Group Co Ltd ,kinachomilikiwa na Wachina akiwa chini ya ulinzi wa Polisi kufuatia ukaguzi wa ghafla wa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Steven Kebwe, Aprili 13,2016 akifuatana na ujumbe wa serikali ya mkoa na wilaya ya Morogoro katika mgodi wa Kiwanda hicho uliopo Kitongoji cha Mazizi, Kijiji cha Maseyu, Kata ya Gwata, Tarafa ya Mikese , ambapo walikutwa wakiendelea na uzalishaji licha kuzuiwa na Serikali kuu mwaka 2010 hadi watakapokuwa wamekamilisha taratibu zote za kisheria zikiwemo na za kimazingira.

Na John Nditi, Morogoro

RAIA  wawili wa China wametiwa nguvuni mkoani Morogoro kutokana na kuendelea kusimamia shughuli za uzalishaji wa marumaru katika mgodi wa mawe wa Kiwanda cha Zhong Fa Construction Material Group Co Ltd ,kinachomilikiwa na Wachina licha ya kuzuiwa na Serikali kuu tangu mwaka 2010.

Mbali na kuendelea na uzalishaji katika kipindi chote hicho, kampuni hiyo imekuwa ikifanya udangayifu  kuwa marumaru  zinazouzwa katika maduka yake zinaingizwa kutoka  nchini China , wakati bidhaa hiyo ikitengenezwa  kutoka Morogoro.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Steven Kebwe, aliamuru kukamatwa kwa raia hao  baada ya kufanya  ukaguzi wa kushitukiza   Aprili 13, 2016  akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa  pamoja na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro.


MBUNGE WA JIMBO LA MKURANGA MH.ABDALLAH ULEGA APOKEA MRADI WA MAJI MKAMBA NA KUKABIDHI KWA WANANCHI

$
0
0
ul14
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah ulega akifungua bomba la maji huku baadhi ya wananchi wakishuhudia katika kata ya Mkamba kijiji cha Tungi katika hafla fupi ya kukabidhi kisima cha Maji kilichochimbwa kwa ufadhiri wa Taasisi ya kimarekani ya African Reflections Foundatioan wiki hii, katika picha mwenye kofia anayeshuhudia ni Mama Maryborne Pool Mtekelezaji wa mradi kutoka taaisi ya Marekani kutoka African Reflections Foundatioan na kushoto ni Diwani Kata ya Mkamba Bw.Dunga Hassan (Picha zote na Raphael Malekela)
ul1
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah ulega akizungumza na baadhi ya wananchi wa kata ya Mkamba kijiji cha Tungi katia hafla fupi ya kukabidhi kisima cha Maji kilichochimbwa kwa ufadhiri wa Taasisi ya kimarekani ya African Reflectins Foundatioan, kulia ni Mama Caren kutoka Taasisi ya African Reflectins Foundatioan na kushoto ni Mama Maryborne Pool Mtekelezaji wa mradi huo.
ul4
Mama Maryborne Pool Mtekelezaji wa mradi kutoka taaisi ya Marekani kutoka African Reflections Foundatioan akizungumza jambo huku Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akifurahia wakati wa makabidhiano ya mradi wa maji katika kijiji cha Tungi wilaya ya Mkuranga.
ul8
Mama Maryborne Pool Mtekelezaji wa mradi kutoka taaisi ya Marekani kutoka African Reflections Foundatioan na mama Caren kutoka taasisi hiyo pia wakikabidhi madawa ya majikwa mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega.
ul12
Akina mama mbalimbali wakiwa katika makabidhiano ya mradi huo.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUHUSU MATUMIZI YA DARAJA LA KIGAMBONI

$
0
0
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Daraja la kigamboni litaanza kutumika siku ya Jumamosi tarehe 16, Aprili, 2016 kuanzia saa 12:00 asubuhi.

Katika siku za mwanzo, magari yatapita bila kulipia tozo hadi Serikali itakapokamilisha taratibu na kutangaza utaratibu wa kulipia.  Aidha, watembea kwa miguu na waendesha baiskeli watavuka bure katika Daraja la Kigamboni.  Hata hivyo maguta na mikokoteni haitaruhusiwa kutumia daraja hilo kutokana na sababu za kiusalama.

Magari yatakayoruhusiwa kupita katika Daraja la Kigamboni katika siku hizo za mwanzo ni yale yenye uzito usiozidi tani 10, hatua ambayo itasaidia kufuatilia mwenendo wa upitaji wa magari katika daraja, barabara za juu (Interchange) katika eneo la Kurasini, pamoja na kuhakikisha kwamba magari yanayotoka au kuingia katika daraja hayasababishi msongamano wa magari katika Barabara ya Nelson Mandela, Barabara ya Kilwa na maeneo mengine ya jiji.  Baada ya utaratibu kukamilika magari ya aina zote yenye uzito unaoruhusiwa kisheria yataruhusiwa kupita katika daraja.
Mambo muhimu ambayo madereva na watumiaji wengine wa barabara wanatakiwa kuzingatia ni:-
1)Kuzingatia sheria ya Usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na kufuata mwendo kasi unaotakiwa ili kuepuka ajali na kuepuka uharibifu miundombinu ya daraja
2)Kufuata alama za barabarani zilizowekwa katika ‘Interchange’ ya Kurasini ili kwenda kwenye uelekeo sahihi.
3)Kuzingatia alama zilizowekwa kwenye milango (Toll Gates) ya Kituo cha kulipia tozo (Toll Plaza) ili kuepuka uharibifu wa miundombinu ya kituo hicho.
4)Madereva na watumiaji wa barabara wengine watakaosababisha uharibifu wa aina yeyote wa miundombinu ya daraja watatozwa faini au kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.
5)Kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa takataka katika eneo la daraja.

Aidha, Wizaraya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inawataka madereva wa magari ya mizigo wanaoegesha katika barabara ya Nelson Mandela wakisubiri kuingia bandarini watafute eneo stahiki la maegesho na kuyaondoa magari hayo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoenda kinyume na agizo hili.

Msongamano wa magari hayo husababisha uharibifu wa barabara na usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara katika eneo hilo.

Imetolewa na;
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu  (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
14 Aprili, 2016

MAKAMPUNI BINAFSI HAYAHUSIKI ULINZI WA NDANI OFISI ZA BANDARI

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho -MAELEZO

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imesema kuwa makampuni binafsi ya ulinzi yanayofanya kazi bandarini hayahusiki na ulinzi wa sehemu nyeti za za Mamlaka hiyo.

Akitoa ufafanuzi huo leo jijini Dar es salaam, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Janeth Ruzangi amekiri kuwepo kwa makampuni yanayofanya kazi ya ulinzi bandarini na amefafanua kuwa hayahusiki kwa namna yoyote ile kulinda sehemu za ndani za ofisi zilizoko bandarini.

“Ninapenda kuwafahamisha wananchi kuwa Bandari inalindwa na walinzi wa aina tatu ; Jeshi la polisi, Polisi wasaidizi walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (Auxilliary Police) pamoja na walinzi wa Makampuni binafsi”

Ameongeza kuwa makampuni hayo yanalinda maeneo ya nje ya bandari yakiwemo maegesho ya magari ya watumishi wa mamlaka kama ilivyo kwenye ofisi nyingine.

Aidha,amefafanua kuwa Polisi wa bandari walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania wako kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na Bunge na wamepata baadhi ya mafunzo ya kipolisi.

Ikumbukwe kuwa agizo la kuwandoa walinzi wa makampuni binafsi kwenye maeneo nyeti ya bandari lilitolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mwezi Februari mwaka huu alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo.

RAIS WA SUDANI KUSINI, MHE. JENERALI SALVA KIIR MAYARDIT AWASILI NCHINI

$
0
0
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye kofia nyeusi) akishuka katika ndege ya Shirika la Kenya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (kushoto) akisalimiana na Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (mwenye fimbo) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Sudani Kusini, Mhe. Jenerali, Salva Kiir Mayardit (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja, 15 Aprili, 2016 Jijini Dar es Salaam.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Wakazi Dar ‘kuonja’ daraja la Kigamboni bure kesho

$
0
0
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake kesho  wanatapa fursa ya kulitumia kwa mara ya kwanza Daraja la Kigamboni linalotarijiwa kufunguliwa rasmi na Rais John Pombe Magufuli siku ya Jumanne ya wiki ijayo ili ‘kuonja’ na kujionea ubora wa daraja hilo kisasa.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam jana, Meneja mradi kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group ambao wametekeleza mradi huo kwa ushirikiano na kampuni ya China Railway Major Bridge Group Bw.Zhang Bangxu,  alisema  siku ya kesho, wataruhusu wakazi hao na magari kupita katika daraja hilo lililogarimu Dola za Kimarekani milioni 135 kujengwa.

“Kama wajenzi kesho tutaruhusu magari kupita kwenda upande wa Kurasini na upande wa Kigamboni siku ya Jumamosi tu kama ikiwa ni sehemu ya majaribio yetu kitaalamu ikiwa ni pamoja na kutumia fursa hiyo kufanya majaribio ya mitambo na mashine zote ambazo zitatumika katika kufanya tozo mbali mbali baada ya kuanza rasmi kwa mradi," alifafanua.

Kwa mujibu wa Bw. Bangxu, daraja la Kigamboni ndiyo daraja refu kuliko yote katika ukanda wa Afrika Mashariki lililotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya matumizi ya kamba (cable) kubeba uzito wa daraja, ambayo itaunganisha jiji la kibiashara la Dar es Salaam na eneo la Kigamboni na Kurasini. Ujenzi ulianza mnamo Tarehe moja Februari mwaka 2012.

“Pamoja na kujengwa katika ubora wa hali ya juu, daraja hili lina jumla ya njia sita yaani njia tatu kwa kila upande, pamoja na njia mahususi kwa ajili ya waenda kwa miguu na waendesha baiskeli ambayo ina upana wa mita 2 na nusu (2.5 meters) katika kila pande. Daraja hilo litaruhusu magari yenye uzito usiozidi tani 30 kupita.,’’ aliongeza
 
 Bw. Bangxu alisema kwamba kaskazini mwa daraja hilo, litaungana na barabara lenye urefu wa kilometa  moja ambayo inakatiza reli ya TAZARA kisha kuungana na barabara ya Mandela. Kwa upande wa Kigamboni, daraja litaungana na barabara lenye urefu wa Kilometa 1.5 ambayo inaungana na barabara ya Kigamboni Ferry - Kibada.

Aliongeza kwamba kukamilika kwa daraja hili ni ya maendeleo kwani inatarajiwa kuchochea kasi ya maendeleo ya mji wa kisasa wa Kigamboni (Kigambani satellite city), kutengeneza fursa za ajira katika sekta ya ujenzi wa maeneo ya makazi pamoja na sekta za huduma ambazo  zitastahimili ongezeko kubwa wa idadi ya wakazi wapya katika mji huo mpya.

Kukamilika kwa daraja hilo kunatajwa kuwa kutawapafusra wakazi wa Kigamboni na viunga vyake ikiwa ni kutoa njia mbadala ya kufikia makazi yao, biashara zao au shuguli zao za ujenzi wa taifa kwa njia ya barabara.
 
Maeneo ya Kigamboni na Kurasini kwa sasa hufikika kwa kutumia vivuko viwili vya MV Magogoni na MV Kigamboni ambazo kwa pamoja zinaumezo wa kubebe abiria 1000 na magari 78 kwa kila safari.

Mradi huo umedhaminiwa kwa kwa ubia kati ya Shirika la Hifadhi ya Jamii ya Taifa (NSSF) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UTAFITI WABAINI WATANZANIA HUTUMIA MUDA MWINGI KWENYE SHUGHULI ZISIZO ZA UZALISHAJI

$
0
0
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014/2015 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Uzinduzi huo umefanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Matokeo ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014/2015 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS). Uzinduzi huo umefanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akionyesha vitabu vya ripoti ya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa mwaka 2014/2015 wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee Hall Jijini Dar es Salaam.

MAMLAKAYA YA HIFADHI YA NGORONGORO YAINGIA MGOGORO NA WANANCHI

$
0
0
Na Woinde Shizza, Karatu

Wananchi wa kijiji cha Losteti kilichopo katika kata ya mbulumbulu wilayani karatu mkoani Arusha wamelalamika mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro kwa kitendo cha kuwanyanganya eneo lao la kuchungia mifugo lijulikanalo kwa jina la Olorieni lililopo ndani ya kijiji hicho.

Wananchi hao waliyasema hayo juzi wakati wakiongea na waandishi wa habari kijijini hapo na kusema kuwa mamlaka hiyo ya hifadhi ya ngorongoro wamewanyanganya eneo hilo ambalo walikuwa wanatumia kama eneo la malisho ya mifugo yao kwa kipindi cha muda mrefu kwani walianza kulitumia tangu enzi za mababu zao .

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Aron Saiteu Alisema kuwa eneo hilo la malisho ya mifugo ni lakwao kwa mdua mrefu lakini wanashangaa kuona hifadhi hiyo ya ngorongoro imekuja na kuwanyanganya hali ambayo inawafanya hata wao kukosa sehemu ya kufugia mifugo yao.

Walisema kuwa walishapeleka malalamiko mara kwa mara katika ofisi za viongozi wa serekali pamoja na ofisi za hifadhi hiyo lakini amna hatua yeyote ambayo imechukuliwa wala kupewa majibu ambayo yanawapa matumaini hali ambayo imepeleka wananchi hao kuumia na kukata tamaa ndani ya nchi yao.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

SIMBA KUSHIRIKI KOMBE LA NILE BASIN

$
0
0
Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es salaam imethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Nile Basin Club Championship, inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itakayoanza kutumia vumbi Mei 22, 2016 nchini Sudan.

Mashindano ya vilabu Kombe la Nile Basin huandailiwa na CECAFA kwa kushirikisha vilabu vilivyoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi kwa nchi wanachama wa CECAFA.

Bingwa michuano ya kombe hilo atajinyakulia zawadi ya dola za kimarekani U$30,000, mshindi wa pili dola U$20,000, huku mshindi wa tatu akipata kitita cha dola za kimarekani U$10,000.

Nile Basin inashirikisha vilabu kutoka katika nchi wanachama wa CECAFA ambazo ni Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania na Zanzibar.

Vitoria University kutoka Uganda ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo baada ya kuifunga AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika mwaka 2014.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII

SIMU TV: UJIO WA RAIS WA SUDANI KUSINI MH.SALVA KIIR NCHINI TANZANIA

$
0
0
SIMU.TV: Rais Magufuli ampokea rais wa Sudani Kusini  Salva Kiir Ikulu jijini Dar es salaam baada ya kuwasili leo asubuhi;  https://youtu.be/G3-SOq8b23A 
SIMU.TV: Katibu mkuu wa EAC anayemaliza muda wake Dkt. Richard Seziberi  akimuelezea rais Salva mafanikio nchi yake itakayoyapata EAC; https://youtu.be/BWlLpTRAmLY  
SIMU.TV: Mh.Mahinga  akieleze utekelezaji  wa  makubaliano ya mikataba ya amani pamoja na masuala ya wakimbizi  nchi za Afrika Mahsariki; https://youtu.be/KKqrdy25qvI  
SIMU.TV: Rais Magufuli asimamia utiaji saini wa mkataba wa Sudan kusini kujiunga na jumuiya ya afrika mashariki baada ya kukidhi vigezo; https://youtu.be/vX6Fax0b90o
 SIMU.TV: Rais Kiir akielezea matarajio ya nchi yake katika kurejesha amani katika nchi yake pamoja na ubalozi mpya wa Sudani hapa nchini; https://youtu.be/zZkQctfb7XA  
SIMU.TV: Rais Magufuli aelezea umuhimu wa nchi ya Sudani Kusini kukubaliwa kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki;  https://youtu.be/pxc2D7TSRxA
 SIMU.TV: Rais Magufuli na mgeni wake rais Salva Kirr wakisaini fomu maalum kwaajili ya kuhifadhi katika kumbukumbu ya tukio la utiaji saini lililofanyika leo; https://youtu.be/S2Ljeb-BN0M  

WABUNGE WAPONGEZA KUANZISHWA KWA TADB

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka (Kulia) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Dkt. Anaclet Kashuriza (Aliyesimama) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakifurahia jambo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi (Kulia) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
 

MABADILIKO YA URUSHWAJI WA VIKAO VYA BUNGE KUPITIA REDIO NA TELEVISHENI

Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images