Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1184 | 1185 | (Page 1186) | 1187 | 1188 | .... | 3348 | newer

  0 0  0 0

  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kutaarifu Umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya juu(Flyover) katika makutano ya TAZARA na ufunguzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

  Siku ya Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais ataweka jiwe na msingi la ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya barabara Nyerere na Mandela (Flyover ya TAZARA).

  Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais atafungua rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5. Ujenzi huu umefanywa na Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni ya China Bridge Engineering Group.

  Aidha wakati tunasubiri uzinduzi rasmi, Wananchi na magari yenye uzito usiozidi tani 10 yataruhusiwa kutumia Daraja la Kigamboni kuanzia Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 ili kuwawezesha kuelewa vizuri miundombinu na matumizi ya daraja.

  Utekelezaji wa miradi hii ni mojawapo ya jitihada za Serikali za kuboresha miundomninu na kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam.

  Imetolewa na;

  Eng. Joseph M. Nyamhanga
  Katibu Mkuu (Ujenzi)
  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  14 Aprili, 2016

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  akizungumza na  Makamo wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini "KOICA GLOBAL" Bw.Kwon  Taemyon akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo pamoja na mwenyeji wa Ujumbe huo Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed(hayupo pichani)
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)  akizungumza na  Makamo wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini "KOICA GLOBAL" Bw.Kwon  Taemyon (wa pili kushoto) akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo pamoja na mwenyeji wa Ujumbe huo Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed(wa pili kulia) akiwepo Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini "KOICA GLOBAL" Bw.Kwon  Taemyon akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo pamoja na mwenyeji wa Ujumbe huo Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed(hayupo pichani)

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  akiagana na   Makamo wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Korea Kusini "KOICA GLOBAL" Bw.Kwon  Taemyon baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ukumbi wa  Ikulu Mjini Zanzibar leo (katikati) Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed,[Picha na Ikulu.]

  0 0

  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rusha Mkoani Mwanza (Pichani) Mhandisi Ernest Makale, leo ametoa taarifa ya Utendaji kazi wa taasisi hiyo mbele ya Wanahabari katika kipindi cha robo mwaka (Januari hadi Machi) mwaka huu.

  Katika taarifa hiyo, Mhandisi Makale amebainisha kuwa Takukuru imepokea jumla ya malalamiko 45 yanayohusiana na vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi ambapo katika malalamiko hayo, 27 yameelekezwa kwa watumishi wa idara za Serikali za Mitaa TAMISEMI hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 60. Kati ya malalamiko hayo 27, malalamiko 13 yameelekezwa katika idara ya ardhi.

  Zaidi Bonyeza HAPA

  0 0

  Wafanyakazi wa Airtel katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya na Morogoro leo wameingia katika mitaa mbalimbali katika mikoa yao kuitambulisha huduma mpya ya Airtel Jipimie Yatosha yako kwa wateja na kutoa elimu jinsi ya kufurahia uhuru wa kutengeneza vifurushi vinavyokidhi mahitaji yao

  Zoezi hili limefanyika jana katika mkoa wa Dar es salaam ambapo wafanyakazi wa Airtel Makao makuu waliweza kutembelia maeneo mbalimbali na kutoa elimu hiyo, halikadhalika timu ya Airtel imefikia wateja wake kupitia vyombo vya habari mbalimbali ikiwemo radio, Tv na mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwahabarisha wateja na watanzania kwa ujumla juu ya huduma hiii ya kipekee, kibunifu na ya kwanza nchini Tanzania inayomuwezesha wateja kununua kifurushi cha muda wa maongezi tu, au kuchanganya kifurushi cha muda wa maongezi na MB za intaneti au Muda wa Maongezi na SMS lakini pia bado wanaweza kupata vifurushi vyote yaani muda wa maongezi zaidi, SMS zaidi na MB zaidi. Vifurushi hivi vinapatikana kwa siku, wiki au mwezi

  Ili kujiunga na kufurushi cha Airtel jipimie yatosha yako mteja anatakiwa kupiga *149*99# kisha kufata maelekezo.
  Wafanyakazi wa Airtel Mkoani Mwanza wakitoa elimu kwa wakazi Mwanza mjini na wafanyabiasharaa waendesha Bodaboda kuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake. 
  Wafanyakazi wa Airtel Mkoani Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuingia mtaani kukutana na wateja na kuitambulisha huduma mpya ya kibunifu ya Airtel jipimie yatosha yako itakayowawezesha wateja kujitengenezea vifurushi vya yatosha wanavyovitaka
  Wafanyakazi wa Airtel Mkoani Morogoro wakishuka kutoka kwenye basi kwenda kukutana na wateja katika maeneo yao ya kazi ili kutambulisha huduma mpya ya kibunifu ya Airtel jipimie yatosha yako itakayowawezesha wateja kutengeneza vifurushi vya yatosha wanavyovitaka
  Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akifanya mahojiano na Jembe radio mkoani Mwanza na kutoa elimu kwa wasikilizaji wa vipindi vyake juu ya huduma mpya ya kibunifu ya Airtel jipimie yatosha yako itakayowawezesha wateja kutengeneza vifurushi vya yatosha wanavyovitaka
  Wafanyakazi wa Airtel mkoani Arusha wakiongea na wateja sokoni na kutoa elimu jkuhusu huduma mpya ya kifurushi cha Airtel Yatosha kijulikanacho kama “Jipimie Yatosha Yako” kitakachompatia uhuru mteja kutengeneza na kununua kifurushi kinachokidhi mahitaji yake.


  0 0

  NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla amekutana na Afisa miradi anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika kutoka wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon Haile katika mazungumzo yaliyofanyika leo asubuhi Aprili 14.2016, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
   
  Katika mazungumzo hayo, Dk. Kigwangalla ameomba Tanzania ipatiwe kibali cha kununua mashine mpya ya kutibu saratani (LINAC) Sambamba na sehemu ya msaada iliyoahidiwa na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Bw.Yukiko Amano mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Mizengo Kayanda Pinda miaka mitatu iliyopita.

  Tanzania tayari imetenga kiasi cha Euro 1.65 Milioni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya mchango wake kwa asilimia 50 kama mradi ulivyokuwa awali.Mh. Kigwangalla alisema: “Bahati mbaya sana kutokana na ucheleweshwaji, Bajeti ya msaada huo kutoka IAEA ilipitwa na wakati na kusababisha Tanzania kukosa fursa hiyo. Malengo ya Tanzania ni kununua mashine hizo mbili kwa ajili ya kuboresha huduma za tiba ya Mionzi nchini”.

  Ujenzi wa jengo kwa ajili ya kufunga mashine hizo mbili umesha kamilika na mashine moja itakamilika mwaka huu na ya pili mwakani ili kuboresha huduma za Saratani nchini.

  Katika mazungumzo hayo, Maafisa waandamizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Woto walishiriki, akiwemo Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba anayeshughulikia magonjwa yasiyo ambukiza, Profesa Ayoub Magimba, Mratibu wa Magonjwa ya Saratani Kitaifa pamoja na magonjwa yasiyoambukiza kwa watu wazima, Dk. Sara Maongezi pamoja na Kaimu Mkurugenzi taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaiselage.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla (wa pili kushoto) akisikiliza kwa makini mazungumzo na Afisa miradi anayesimamia miradi ya mionzi barani Afrika kutoka wakala wa Kimataifa wa nguvu za Atomiki (IAEA), Bw. Solomon Haile (wa kwanza kulia). Wengine ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Tiba anayeshughulikia magonjwa yasiyo ambukiza, Profesa Ayoub Magimba (katikati), akifutiwa na Mkurugenzi taasisi ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaisalage na kushoto Mratibu wa Magonjwa ya Saratani Kitaifa pamoja na magonjwa yasiyoambukiza kwa watu wazima, Dk. Sara Maongezi.

  0 0

  Waziri afya ,maendeleo ya jamii,jinsia ,wazee na watoto Ummy Mwalimu akiongea na wajumbe wa baraza jipya la usajili wa wataalam wa afya ya mazingira nchini(hawapo pichani) kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof: Bakari Mohammad
  Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo pamoja na maofisa mazingira wakifuatilia hotuba ya Mh. Waziri Ummy Mwalimu
  Mwenyekiti mpya wa baraza la usajili wa wataalam wa afya ya mazingira nchini Bartholomayo Ngaeje(katikati) akitoa neon la shukrani kwa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto(hayupo pichani) mara baada ya kuzinduliwa kwa baraza hilo,kulia ni msajili wa baraza hilo Iddy Hoyange na kulia ni njumbe wa baraza hilo toka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa wizara hiyo
  Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akimkabidi cheti cha Uongozi kwa kuthamini mchango wake kwa baraza hilo aliyekuwa mwenyekiti wa awamu ya pili Bi.Mary Swai

  0 0

  Kushoto ni mmiliki wa ukumbi wa ZANCINEMA Mohammed Bajbeir, akiwa pamoja na Andy Jones, raia wa Uingereza, mtengenezaji wa filamu za ‘As Old sa My Tongue’ na ‘I shot Bi. Kidude’, zinazoonesha historia ya maisha hadi kufa kwa msanii mkongwe marehemu Fatma Baraka ‘Bi. Kidude’, wakizungumza na waandishi wa habari juu ya kumbukumbu ya msanii huyo aliyefariki dunia Aprili 17, 2013. (Picha na Yussuf Simai-MAELEZO, ZANZIBAR.

  Na Salum Vuai, MAELEZO
  KATIKA kuadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa tatu tangu kufariki kwa msanii mkongwe aliyeitangaza sana Zanzibar duniani Fatma Baraka ‘Bi. Kidude’, filamu mbili zinazohusu maisha na kifo chake zitaoneshwa mjini Zanzibar.

  Mohammed Bajbeir, mmiliki na Mkurugenzi wa ukumbi wa sinema uliopo mjini Zanzibar, ZANCINEMA, amewaambia waandishi wa habari jana, kwamba maonesho ya filamu hizo yanalenga kuwapa fursa Wazanzibari na wageni, kumjua kwa undani nyakanga huyo wa sanaa ya uimbaji na unyago.

  Marehemu Bi. Kidude, alifariki dunia Aprili 17, 2013 baada ya kuugua maradhi ya kisukari yaliyochangiwa na umri mkubwa, na kuzikwa kijijini kwao Kwambani katika mazishi yaliyoweka rekodi miongoni mwa wasanii kwa kuhudhuriwa na watu wengi wakiwemo viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

  Bajbeir amezitaja filamu hizo kuwa ni ‘As old as my tongue’ inayoelezea kwa urefu maisha ya msanii huyo katika tasnia ya muziki, pamoja na ‘I shot Bi. Kidude’ (Kifo cha Bi. Kidude), ambayo inaelezea kuumwa kwake hadi pumzi zake za mwisho.

  Filamu hizo zimeandaliwa na kutengenezwa na Andy Jones, raia wa Uingereza, ambaye alikuwa akimsoma na kumfuatilia marehemu Bi, Kidude kwa miaka kadhaa hadi akamudu kuandika filamu hizo zinazogusa mtima wa kila anayeziangalia.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa ZANCINEMA ulioko Funguni mjini Zanzibar kuelekea siku ya kumbukumbu ya Bi, Kidude, Jones alisema Wazanzibari wana kila sababu ya kumuenzi gwiji huyo wa sanaa ambaye amefanya kazi kubwa kuitangaza nchi yake ulimweguni, kisanii na kiutamaduni.

  Aidha, alieleza kwamba, kwa namna Bi. Kidude alivyokuwa mtu wa watu wa kila rika, mcheshi, na mwenye imani asiyeangalia kipato, anastahili kukumbukwa kwa namna ya pekee. 

  “Wapo watu wa mataifa ya nje ambao hawakuwa wakimfahamu, lakini waliposikia kazi zake, walisafiri hadi Zanzibar kwa ajili ya kumjua na kumshuhudia jukwaani akionesha uwezo wake,” alisema Muingereza huyo.

  Alifahamisha kuwa tayari filamu hizo zimeshaoneshwa katika nchi mbalimbali duniani, lakini maonesho ya Zanzibar yatakuwa ya kipekee.

  Aidha, alisema zimewahi kuoneshwa katika matamasha ya Zanzibar, Sauti za Busara na lile la filamu (ZIFF), ambapo watu wengi walivutiwa nazo.

  Andy Jones, alifika Zanzibar kwa mara ya kwanza mwaka 2000, na kuendelea kuja kila mwaka hadi 2006 alipokamilisha filamu ya kwanza, ‘As old as my tongue’ kuhusu historia ya Bi. Kidude.

  Alieleza kuwa, alitumia pauni 15,000 za Kiingereza (sawa n ash. 51,000,000 kwa thamani ya sasa), kutengeneza filamu ya ‘Kifo cha Bi. Kidude’ (I shot Bi, Kidude), iliyochukua miaka miwili na nusu hadi kukamilika.

  Jones alisema, wakati wa uhai wake, marehemu Bi, Kidude alikuwa akilipwa asilimia kumi ya mauzo kila ilipouzwa, na sasa fedha hizo ameamua kuzigawa kwa Akademi ya Muziki wa Nchi za Jahazi (DCMA) ya Zanzibar kwa ajili ya kuwaendeleza wasanii wa kike wanaochipukia.

  0 0

  Baraza la Michezo Taifa(BMT) kwa kushirikiana na wadau wa ngumi za kulipwa wameunda kamati ya muda kwa ajili ya kuratibu na kusimamia maendeleo ya mchezo huo ndani na nje ya Nchi.

  Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja amesema kuwa wameamua kuunda kamati ya muda ya mchezo huo itakayoongozwa na Katibu Mkuu Yassin Ustaadh kutoka TPBO na Makamu katibu Mkuu Chaulembo Palasa kutoka Chama cha Ngumi za kulipwa Tanzania(TPBC) kwa sababu hakukuwa na chombo kimoja kinachoratibu Ngumi za kulipwa nchini.

  “Tuliamua kukutana na wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa mapema mwezi huu wakiwamo TPBO, TPBC,TPBC Limited , PST na KBF ili tuweze kupata chombo kimoja imara cha kuratibu mchezo wa ngumi za kulipwa nchini” alisema Bw. Kiganja.

  Aidha Bw. Kiganja ameongeza kuwa viongozi waliochaguliwa wafanye kazi kwa bidii na sio kuongea sana ikiwemo kuwasilisha katiba ya kamati hiyo ndani ya siku 90 ili kuweza kuufikisha mbali mchezo huo na kuiletea sifa na heshima Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

  “ Natoa wito kwa viongozi wa kamati hii wasifanye mzaha katika suala hili ikiwa kama mwanakamati hawezi kufanya kazi aseme mapema ili achaguliwe mwengine kwa manufaa ya Taifa” aliongeza Bw. Kiganja.

  Kwa upande wa Katibu Mkuu wa kamati hiyo Bw. Yassin Ustaadh amesema kuwa wapo tayari kufanya kazi na kuufikisha mchezo huo mbali katika Nyanja za kimataifa na kuwataka mashabiki wakae mkao wa kula.

  Mbali na hayo Bw. Ustaadh amewataka waandaaji wa mapambano hayo ambao hawana sifa na vigezo kukaa mbali na shughuli hiyo kwani hawahitaji ubabaishaji katika tasnia hiyo vinginevyo watatumbuliwa.

  Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa(BMT) Bw. Mohamed Kiganja wa kwanza kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani leo jijini Dar es salaam kuhusu viongozi waliochaguliwa wa kamati ya muda ya mchezo wa Ngumi za kulipwa , kulia ni Katibu Mkuu wa kamati hiyo Bw. Yassin Ustaadh.
  Katibu Mkuu mpya wa Kamati ya Muda ya Mchezo wa Ngumi za kulipwa Bw. Yassin Ustaadh akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani baada ya kukabidhiwa kamati hiyo leo jijini Dar es salaam.
  Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa(BMT) Bw. Mohamed Kiganja hayupo pichani alipotambulisha viongozi waliochaguliwa wa kamati ya muda ya mchezo wa Ngumi za kulipwa , kulia ni Katibu Mkuu wa kamati.

  0 0

  Na Al-Hassan Michuzi,Globu ya Jamii.

  Serikali imezindua utafiti wa Ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, (NBS) ya Watu wenye uwezo wa kufanya kazi leo jijini Dar Es Salaam ,katika uzinduzi huo imeelezwa kuwa utafiti huo utasaidia kufuatilia na kutathmini katika kufanya mipango ya maendeleo.

  Akizungumza katika Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge,Kazi, Walemavu, Jenister Mhagama, amesema kuwa matokeo ya utafiti yatasaidia kupata ufahamu wa hali halisi ya soko la ajira katika kuingia katika uchumi wa pato la kati 2020-2025.

  Waziri Jenister amesema kuwa utafiti huo utasaidia kutengeneza Sera,mpango wa kupambana na kupunguza Umasikini nchini (Mkukuta) na mpango wa maendeleo wa miaka mitano katika kupata suluhisho la tatizo la ajira.

  Amesema nguvu kazi ya vijana kati ya miaka 15 hadi 35 sawa na milioni 15.1 na asilimia 68, hivyo utafiti huo utatibu swali vijana la ukosefu wa ajira.Jenister amesema fursa zitakazotolewa ziweze kutatua changamoto zilizopo kwa vijana na lazima zitoe tija, na Tanzania kuwa ya kwanza duniani katika uongezaji wa ajira kutokana fursa ambazo serikali itatekeleza.

  Amesema sekta ya kilimo ndio inaweza ikifanya vizuri katika kutoa ajira kwa vijana kama sekta kiongozi.Amesema asilimia 35 ya sekta binafsi ndio yenye ajira kubwa kuliko ya sekta ya umma hivyo utafiti lazima utumike katika kufanya mipango.Kiwango cha upungufu wa ajira kwa wanaume ni asilimia 8.4 na wanawake ni asilimia 12.4 hivyo ukosefu wa ajira kwa wanawake uko juu kuliko wanaume..
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista Mhagama,akizungumza katika katika uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014. Uzinduzi huo ulifanyika katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam, jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu nchini,Dk.Albina Chuwa.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista Mhagama,akizindua ripoti ya matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014 katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam, jana. Wengine wanaoshuhudia ni kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu nchini,Dk.Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani,Marry Kawar.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista Mhagama,akionesha ripoti ya matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014 katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam, jana. Wengine wanaoshuhudia ni kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu nchini,Dk.Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani,Marry Kawar.


  0 0

  Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani,
  Suzan Rymond.
  Na Victor Masangu, Pwani.

  TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani Pwani imezitaja taasisi na idara zipatazo 11 ambazo zimelalamikiwa  kuhusika katika  matukio mbali mbali  ya vitendo vya kupokea rushwa kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi.

  Akizungumza katika mkutano na  waandishi wa habari ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi januari hadi machi mwaka huu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzan Rymond  alisema  kuwa wale waliohusika watapeekwa katika vyombo vya sheria.

  Susan alisema kwamba kwa sasa wamepokea jumla ya malalamiko 49 yanayohusina na vitendo vya rushwa  baada ya kufanya uchunguzi waa wa wameweza kubaini idara inayoongoza kwa malalaamiko hayo kwa Mkoa  mzima wa Pwani  ni  serikali za mitaa ambayo  ina jumla ya malalamiko 18.

  Kamanda huyo alifafafnua kuwa idara  nyingine iliyoshika nafasi ya pili ilikuwa ni afya ambayo ilipata malalamiko 8,polisi 4,mahakama 3 ardhi 3 sekta binafsi 3 elimu 2 tanesco 2 fedha 1 vipimo 1 pamoja na maji 1.

  “Ndugu zangu waandishi wa habari leo tumewaita ili kuwapa taarifa ua utekelezaji wa majukumu yetu kwa kipindi cha kuanzia mwezi januari hadi kufikia mwezi machi, na katika miezi hiyo tumepata malalamiko mengi yanayohusina na vitendo vya rushwa katika mkoa wetu wa Pwani.

  Aidha Kamanda huyo alisema malalamiko ambayo wameshayapokea katika ofisi yaa ni 64 ambapo kati yao 49 ndio yanahusina na  malalamiko ya vitendo vya upokeajiwa  rushwa katika idara za serikali pamoja na taasisi mbali mbali.
  Pia Suzan alisema kwamba kwa sasa katika kuhakikisha wanakomesha vitendo vya kupokea na kutoa rushwa wataendelea kufanya uchunguzi wa kina katika maeneo mbali mbali ili pindi watakapowabaini wahusika waweze kuwachukulia kali na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

  Kamanda huyo alisema hadi sasa tayari kuna jumla ya kesi  22 zinazohusiana na vitendo vya rushwa  ambazo zimeshafikishwa  mahakamani,na pia bado kuna baadhi ya kesi nyingine bado zinafanyiwa uchunguzi zaidi.

  Katika hatua nyingine Kamanda huyu aliwaomba wananchi wote wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha wanatoa taarifa katika vyombo vinavyohusika endapo wakibaini kuna daily zoozte za mtu kutoa au kupokea rushwa ili sheria iweze kufuata mkondo wake wa kuwakamata wahusika ambao wamekuwa na tabia kama hiyo.

  0 0

  Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha (Mb) anatarajia kufanya ziara ya kikazi Gereza Kwamugumi, Korogwe Mkoani Tanga, kesho Aprili, 15 2016.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja inaeleza kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kujionea maendeleo ya mradi wa mabwawa ya samaki yaliyopo gerezani hapo ambayo hadi sasa yamepandwa vifaranga wa samaki 18,800 tangu tarehe 16/12/2015.

  Kabla ya kutembelea eneo la mradi wa mabwawa ya samaki, Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha atapokea taarifa fupi ya maendeleo ya mradi wa uzalishaji samaki Gereza Kwamugumi, Korogwe.

  Miradi ya ufugaji samaki ipo katika Magereza ya Karanga, Njombe, Masasi, Tukuyu ambapo nia ya Uongozi wa Jeshi la Magereza ni kuieneza katika Magereza mbalimbali yenye fursa za kuendesha mradi huo.

  Mradi wa uzalishaji samaki katika Gereza Kwamugumi ni mojawapo ya miradi mbalimbali ya uzalishaji mali iliyoanzishwa na Uongozi wa Jeshi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi la Magereza, hususan katika kuipunguzia Serikali gharama za kuhudumia Magereza na kuongeza pato la kodi kwa Taifa.

  0 0  0 0


  0 0

  Kwa kutambua mchango wa wajasiliamali katika maendeleo ya nchi, Taasisi ya CITI iliyo chini ya benki ya Citi, imeandaa shindano litakalowahusisha wajasiriamali wadogo wadogo kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao watapata nafasi ya kushiriki na kushirikisha washiriki katika vipengele mbalimbali.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Uhusiano wa benki ya Citi, Frank Kallaghe, amesema thumuni la kuandaa shindano hilo ni kuangalia jinsi gani benki hiyo itaweza kuwatambua wajasiriamali nchini na hivyo wakaamua kuandaa shindano hilo ambalo mbali na washindi kupewa pesa pia watapatiwa tuzo na vyeti.

  Amesema shindano hilo ni mara ya kwanza kufanyika nchini na litahusisha wajasiliamali ambao kupitia biashara wanazofanya kumeleta mabadiliko katika maisha yao, familia, jamii na pia biashara ambayo imeweza kutoa nafasi ya ajiraa kwa wengine.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Citi, Joseph Carasso akizungumzia Taasisi ya CITI na shindano hilo.

  “Tuliamua kuanzisha tuzo hizi baada ya kuangalia jinsi gani tutawatambua wajasiliamali wa Tanzania na katika tuzo hizo tunataraji kushirikisha wajasiliamali ambao biashara yao ipo tofauti kwa kuwasaidia kupata maendeleo,” amesema Kallaghe.

  Aidha Kallaghe ameongeza kuwa kwa kufanikisha shindano hilo kikamilifu wameshirikiana na Mtandao wa Asasi zinazotoa Huduma za Kifedha kwa Wajasiliamali Wadogo Wadogo TAMFI ili waweze kuwasaidia kuwatafuta wajasiliamali walio na vigezo vya kushiriki shindano hilo ambalo linatarajiwa kumalizika mwezi Juni mwaka huu.

  Nae Katibu Mtendaji wa TAMFI, Winnie Terry amesema mbali ya kuangalia jinsi biashara imebadilisha maisha ya mshiriki pia anatakiwa awe amekopa katika taasisi ambazo zinatoa mikopo ya kifedha na jinsi gani anautumia mkopo huo ili kuzidi kuikuza biashara yake.

  Bi. Terry ameongeza kuwa  wanataraji kuendesha shindano hilo kwa kutumia majaji, maofisa wa Wizara ya Fedha na watu kutoka Taasisi mbalimbali za wajasiliamali ili kuhakikisha wanapata mshindi aliye na sifa za kutosha.
  Afisa Uhusiano wa benki ya Citi, Frank Kallaghe akizungumzia shindano hilo.

  “Tutakuwa na watu ambao watakuwa wakipita kwa kila mjasiriamali kuona anafanya vipi biashara na kuangalia biashara hiyo imeboresha vipi maisha yake,” amesema Bi. Terry.

  Amesema shindano hilo litahusisha washiriki kutoka Dar es Salaam na Pwani na mbali na shindano la mjasiliamali bora pia kutakuwa na shindano la mjasiliamali mwanamke, mjasiliamali kijana na mjasiliamali mlemavu.

  “Mshindi wa kwanza atapata Dola 7,500 (Mil. 15), mshindi wa pili Dola 6,000 ( Mil. 12), watatu Dola 4,000 (Mil. 8), mshindi wa shindano mama, kijana na walemavu kila mmoja atapata Dola 2,000 (Tsh. Mil. 4), wajasiliamali 10 kila mmoja Dola 1,000 (Mil. 2), Taasisi ya wajasiliamali Dola 2,500 (Mil. 5) na Afisa Mkopo ambaye anamsimamia mshindi wa mjasiliamali bora atapata Dola 1,500 (Mil. 3) ambapo kwa ujumla itatumika Dola 37,500 (Mil. 70),” amesema Bi. Terry.
  Katibu Mtendaji wa TAMFI, Winnie Terry akizungumzia jinsi washindi watapatikana.

  Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Citi, Joseph Carasso amesema kuwa waliamua kuanzisha Taasisi ya CITI ili kuweza kusaidia jamii katika mambo mbalimbali na kupitia shindano hilo wataweza kuwasaidia wajasiriamali mbalimbali nchini ili waweze kukuza biashara zao.

  0 0

  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akutana na Wamiliki wa Mabenki Nchini ili kuzitambua Hati Miliki za Ardhi za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwasisitiza Wamiliki wa Mabenki Nchini kuzitambua Hati Miliki za Ardhi za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali, kushoto ni Bibi Medelina Kiwayo Meneja Usimamizi wa Taasisi za Fedha-Benki Kuu na Tuse Joune Kaimu Mkurugenzi Mkuu Chama cha Wenye Mabenki Tanzania (TBA).

  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwasisitiza Wamiliki wa Mabenki Nchini kuzitambua Hati Miliki za Ardhi za Kimila katika kutoa mikopo kwa Wakulima, wajenzi na Wajasiliamali alipo kutana nao leo jijini Dar es salaam.

  0 0

  Benki ya NMB leo imesaini makubaliano na shirika lisilo la kiserikali la STICHTING MEDICAL CREDIT FUND (MCF) la nchini Uholanzi kwaajili ya kutoa fursa za mikopo nafuu kwa hospitali, vituo vya Afya na maduka ya dawa nchini kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma bora na nafuu za afya nchini.

  Mkopo huu utatolewa kwa hospitali za binafsi (zisizo za serikali) ambapo hospitali na vituo vya afya vitaweza kukopa kuanzia shilingi milioni 30 mpaka bilioni 2.

  NMB inategemea kuwa fedha hizo zitasaidia kuboresha huduma za afya kwenye maeneo mengi zaidi nchini tofauti na sasa ambapo hospitali nzuri zinazotoa huduma bora zinapatikana sehemu chache. NMB itatoa mikopo kwaajili ya uwekezaji zaidi kwenye sekta ya afya huku MCF watatoa elimu juu ya usimamizi wa utoaji huduma na upatikanaji wa vifaa bora katika sekta ya Afya.

  NMB inakuwa benki ya kwanza nchini kuingia ubia na MCF taasisi ambayo tayari inafanya kazi zake nchini Kenya, Nigeria na Ghana.

  MCF wamechagua kufanya kazi na NMB kutokana na ukweli kwamba benki hiyo ina mtandao mpana wa matawi nchi nzima kuliko benki yoyote hivyo kurahisisha utoaji wa huduma kwenye maeneo mengi zaidi hata vijijini.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Medical Credit Fund (MCF)- Bi Monique Dolfing-Vogelenzang (kushoto) na Mkurungenzi Mtendaji wa NMB - Bi Ineke Bussemaker wakisaini makubaliano yatakayowezesha sekta ya afya kupata mikopo nafuu kutoka NMB. Nje ya mikopo, MCF itasaidia kutoa elimu juu ya usimamizi wa utoaji huduma na upatikanaji wa vifaa bora katika sekta ya Afya.
  Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo Abdulmajid Nsekela akiongea na waandishi wa habari juu ya makubaliano yaliyoingiwa kati ya NMB NA MCF kwaajili ya utoaji wa mikopo nafuu kwenye sekta ya afya hususani hospitali, vituo vya afya na maduka ya dawa ya binafsi.

  0 0

  Mpendwa Meryciana, 
  Hakika umekuwa mwema, mkarimu, mwenye nidhamu na mwenye upendo kwa kila mtu, dada zako wapendwa na wadogo zako, mama, ndugu na jamaa wote.

  Hakika wote tunakupenda na zaidi ya yote tunakutakia maisha marefu na yenye baraka tele. Ukafanikiwe yale yote ambayo ndio haja ya moyo wako, Mungu na akafungue milango yote ya baraka na akufanye uwe mwenye furaha katika maisha yako yote ya apa dunia na ata baadae.

   UWE NA MAISHA MAREFU SIKU ZOTE!!!!
  KR na FAMILIA

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Mhe George Simbachawene akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe.  Paul Makonda  nyaraka za jengo la Machinga Complex (pichani juu) baada ya kuvunja bodi  ya jengo hilo mapema leo kwa kushindwa kazi, na kutangaza kuwa amelikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa  leo jijini Dar es Salaam. Jengo hilo lilijengwa mahususi kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) ili kuwaondoa mabarabarani na kupunguza msongamano wa Wamachinga mitaani, lengo ambalo Bodi iliyovunjwa imeelezwa kuwa ilishindwa kutimiza.

  0 0


older | 1 | .... | 1184 | 1185 | (Page 1186) | 1187 | 1188 | .... | 3348 | newer