Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1183 | 1184 | (Page 1185) | 1186 | 1187 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Na Elias Malima , NEC

  Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala imeipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kufanikisha kuendesha Uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 vizuri na kuiacha nchi ikiwa na Amani, utulivu na Usalama.

  Hayo yalisemwa jijini Dar ess Salaam jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Najma Murtaza Giga walipokutana na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere convention Center katika kikao mahsusi cha Kupitia Bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya mwaka wa fedha wa 2016/2017.

  Aidha, pongezi hizo kwa NEC zilitolewa na wajumbe wa pande zote mbili yaani wa Chama tawala na wale wa upinzani wa kamati hiyo kwa nyakati tofauti. Baadhi ya wabunge hao ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa Najma Murtaza Giga(CCM), Twahir Awesu Mohammed (CUF) na Nassor Suleiman Omar (CUF).

  Alisema ni jambo la heri sana pale ambapo taasisi ama mtu anafanya kazi ya kutukuka kupewa sifa yake na kupewa moyo ili aendelee na moyo wa kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi si tu kwa manufaa ya taasisi yake bali hata kwa Taifa.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhan aliiambia kamati hiyo kwamba haikuwa kazi rahisi kuendesha na kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na Nchi ikaendelea kuwa na amani na utulivu kwani ushindani wa kisiasa ulikuwa mkubwa kiasi cha kutishia maisha ya watanzania.

  “Tulijitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kufuata Sheria Kanuni na taratibu za kusimamia Uchaguzi pamoja na kwamba Bajeti ilikua haitoshi hasa wakati tunaanza zoezi la Uandikishaji wa Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia ya BVR ambapo tulilazimika kuandikisha wapiga Kura kwa kuhamahama” Alisema Kailima.

  Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge Jenista Mhagama aliwashukuru wabunge kwa niaba ya Serikali kwa jinsi walivyothamini na kutambua Kazi kubwa iliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuahidi kufikisha Serikalini mawazo ya kuitafutia Tume fedha kwaajili ya Tume kuzipatia Asasi za Kiraia zinazotoa Elimu ya Mpiga Kura kwani lilijitokeza suala la Ukosefu wa Fedha za Kuendeshea Elimu hiyo.

  Bajeti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 ni jumla ya Tsh4,830,537.167/= ikiwa ni fedha za matumizi ya kawaida OC Miradi ya Maendeleo pamoja na Mishahara ya watumishi.

  Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ulifanyika tarehe 25 Oktoba ambapo aliyekua Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mh.Dkt John Pombe Magufuli aliibuka Mshindi.

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, January Makamba akifungua warsha ya wadau wa Mazingira wa ndani na nje ya Nchi iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais juu ya kujadili jinsi Wafadhili wanavyoweza kusaidia Ofisi katika kuimarisha mambo mbalimbali ya mazingira.
    Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo wanaojihusisha na Mazingira hapa Nchini  Mh. Egon Kochanke akiongea wakati wa warsha hiyo.
    Sehemu ya Wahudhuriaji wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba(hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha hiyo.

  0 0

   Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akitoa heshima zake za mwisho mapema leo kabla ya mazishi, kwa aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lisu,Wilayani Ikungi mkoani Singida.
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida,Bi Martha Mlata akitoaa heshima zake za mwisho mapema leo kabla ya mazishi, kwa aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lissu,Wilayani Ikungi mkoani Singida. 
  Msemaji wa chama cha CCM,Ole Sendeka, Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba wakimpa pole Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA),Mh Tundu Lissu,ambao waliwasili wilayani Ikungi mkoani Singida kushiriki Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lissu.
   Msemaji wa chama cha CCM,Ole Sendeka akimpa pole Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA),Mh Tundu Lissu kwa kufiwa na dada yake
   Msemaji wa chama cha CCM,Ole Sendeka akitoa neno la pole kwa Wafiwa,ndugu,jamaa na marafiki kabla ya kufanya maziko, kwa aliyekuwa Mbunge wa CHADEMA (Viti maalum),Marehemu Christina Lissu,Wilayani Ikungi mkoani Singida.


  0 0
 • 04/13/16--07:14: AJALI KAZINI
 • Mwendesha baiskeli akihangaina kuinyanyua baiskeli yake baada ya kupiga mweleka mchana huu, katika Barabara ya Chang'ombe jijini Dar.
  Msamalia akisaidia kuinyanyua Baiskeli hiyo.

  0 0

   Wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania wanafuatilia kwa ukaribu na umakini sana sakata la upangaji matokeo kwa timu nne za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambazo zimeshushwa daraja na tuhuma za viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu kujihusisha na suala hilo.

  Ufuatiliaji huu wa Vodacom umeanza siku moja baada ya kuwepo taarifa kuwa Kampuni ya Geita Gold Minning imevunja mkataba wa kuidhamini timu ya Geita Sports wenye thamani ya sh. milioni 300 kutokana na kukutwa na hatia kuhusishwa na upangaji matokeo katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya JKT Kanembwa ambapo Geita ilishinda bao 8-0.

  Akiongea na mtandao huu kuhusiana na sakata hilo Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema kuwa wameamua kulifuatilia kwa makini suala hili kwa kuwa ligi hiyo ndio inatoa timu tatu bora zinazopanda daraja na kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ambao wanaidhamini.

  " Tunadhamini Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa lengo la kukuza mchezo wa soka nchini,Tunapenda kuona malengo yetu ya kukuza soka hapa nchini yakilandana na  kufuatwa kwa sheria zote za mchezo huu ili tuendeleze mchezo huu nchini na ngazi ya kimataifa na kuboresha maisha ya wachezaji pia mchezo kuchangia pato la serikali kupitia kodi. Napenda kuwasihi viongozi wa soka wanaohusika na masula ya mchezo huu kuzingatia sheria kwa umakini ili malengo haya yaliyokusudiwa yaweze kufikiwa " Alisema Nkurlu.

  Timu nyingine zilizoshushwa daraja katika uamuzi wa  Kamati ya Nidhamu ya TFF ambayo ilibainisha kuwa baadhi ya viongozi wa soka wameshiriki kwenye sakata hilo  ni Polisi Tabora na JKT Oljoro ambazo zilicheza na Polisi kushinda mabao 7-0.

  Uamuzi huo ulitolewa baada ya kamati hiyo kukaa vikao vitatu na kuwahoji viongozi wa timu, wachezaji, makocha pamoja na waamuzi na makamisaa wa mechi hizo.

  Polisi Tabora na JKT Oljoro  zimeshushwa mpaka Ligi Daraja la Pili (SDL) sanjari na Geita huku JKT Kanembwa ikishushwa hadi ligi ya mkoa.

  Waliofungiwa kuhusika na masuala ya soka maisha yao yote ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora, Yusuph Kitumbo, Mwenyekiti wa JKT Oljoro Amos Mwita, Kocha Msaidizi wa Tabora, Katibu wa chama cha mchezo huo Tabora, Fateh Remtullah, kocha msaidizi wa Geita, Choki Abeid na Katibu wa Polisi Tabora, Alex Kataya, mwamuzi na kamisaa wa mchezo wa JKT Kanembwa na Geita Gold Sport.

   Waliofungiwa kujihusisha na soka kwa miaka 10 na faini ya Sh 10 milioni ni mlinda wa Geita Denis Richard ambaye alikuwa anachezea kwa mkopo timu hiyo akitumia timu ya vijana ya  Simba na mwamuzi Hamis Mchunde, refa Masoud Mkelemi, kipa wa JKT Kanembwa, Mohamed Mohamed aliyekiri kupokea sh 300,000.

  0 0

   TIMU ya soka ya Uchukuzi Sports Club mwishoni mwa wiki ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Amadori Boys ya Pugu Sekondari katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

  Uchukuzi Sports Club inajiandaa kwa mashindano ya Mei Mosi yatakayoanza Aprili 16 mkoani Dodoma, ambapo mechi hiyo ni ya pili ya majaribio baada ya ile ya kwanza iliyofanyika hivi karibuni.

  Katika mchezo huo, Uchukuzi SC ndio walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Isack Ibrahim katika dakika ya saba kabla ya Christian Moyo hajasawazisha mwanzoni mwa kipindi cha pili.
  Hatahivyo, Ibrahim alikosa magoli kadhaa ya wazi, baada ya walinzi wa Amadory Boys kumkaba baada ya kuona ni tishio langoni mwao.

  Meneja wa Uchukuzi SC, Robert Damian aliyewahi kuichezea Simba ya Jijini Dar es Salaam, alisema kuwa mechi hizo za kirafiki zinawasaidia makocha wa timu yao kujua makosa ya wachezaji wao na kuyarekebisha kabla ya kwenda kwenye kituo cha mashindano, ili waweze kufanya vizuri.

  Alitamba kuwa timu yao ya soka pamoja na nyingine za netiboli, kuvuta kamba, riadha, bao, drafti na vishale zitafanya vizuri katika mashindano hayo ya Mei Mosi kwani zimejiandaa vizuri, kwa kupata mechi kadhaa za kirafiki.
  Aidha, timu ya netiboli ya Uchukuzi SC juzi ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Bandari Kurasini huku ikiwa na wachezaji wake wakongwe kama akina Matalena Mhagama, Subira Jumanne, Fanuna na wengineo, ambao wanaipa nguvu timu hiyo chini ya kocha wao mzoefu Judith Ilunda.

  Timu ya Uchukuzi SC katika mashindano yaliyopita ya Mei Mosi yaliyofanyika jijini Mwanza, iliweza kutwaa makombe 13, kati ya hayo matano ni ya ubingwa katika michezo ya kuvuta kamba, baiskeli, bao, karata na riadha kwa upande wa wanawake na wanaume, wakati yaliyosalia ilishika nafasi ya pili na tatu.

  0 0

  MKE wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa amewaomba wananchi wa wilaya ya Ruangwa kuwaombea dua viongozi wa taifa, Rais Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili waweze kufanya kazi zao kikamilifu.

  Amesema kazi nzito inayofanywa na viongozi hao ya kuhakikisha nchi inakuwa salama na inasonga mbele kimaendeleo ni shughuli ngumu na inahitaji nguvu ya Mungu, hivyo ni vema wananchi wakawaombea dua ili kazi hiyo iweze kuwa na tija kwao na taifa kwa ujumla.

  Mke wa Waziri Mkuu ameyasema hayo jana alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Chinongwe wilayani Ruangwa, ambapo amewaomba mwananchi hao wajitahidi kuwaombea dua viongozi hao ili malengo yao ya kuwaletea maendeleo yatimie.

  Mary ambaye ameongozana na Waziri Mkuu Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa, katika ziara yake ya kuwashukuru wananchi waliomchagua kwa nafasi ya ubunge na kisha  Rais Dk Magufuli kumteua kuwa kushika wadhifa huo.

  "Nawashukuru sana wananchi kwa kuwa kura zenu ndiyo zilizosababisha Mheshimiwa Majaliwa ambaye ni mbunge wetu kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, hivyo nawaahidi kuwa tutaendelea kushirikiana,” amesema mke wa Waziri Mkuu.

  Amesema licha ya kuongezewa majukumu atahakikisha anaendelea kushirikiana na wanaruangwa ili waweze kuendeleza shughuli za maendeleo katika wilaya hiyo na kwamba wasiwe na wasiwasi kwani hata wasahau kwa kuwa anawapenda na kuwaheshimu.

  Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0

  Na Zawadi Msalla.
  WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amekifunga mara moja kiwanda kilicho kuwa kikiendeshwa kwa njia zisizo halali na  Wakandarasi wa  Uwanja wa Taifa,  Kampuni ya BFG kutoka nchini China.

   Nape amefanya zoezi hilo leo  baada ya kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya Uwanja wa Uhuru na kubaini kuwepo kwa kiwanda hicho ambacho ni kinyume na taratibu na mkataba wa kisheria walio ingia baina ya Serikali na Kampuni yao ambao unahusu ujenzi wa miudombinu ya michezo pekee ikiwemo  Uwanja wa Taifa na Uhuru.

  Kabla ya kukifungia kiwanda hicho Waziri Nape aliomba maelezo ya kina juu ya uhalali wa uwepo wake na namna uendeshwaji wake unavyofanyika ili kujiridhisha ndipo alipofikia uamuzi huo wa kukifungia baada ya kujiridhisha kuwa kinaendeshwa kinyume na utaratibu.

  “Ninataka kujua kwa undani zaidi uhalali wa kiwanda hiki cha useremala kama kipo ndani ya mkataba wa ujenzi wa Uwanja wa Taifa na eneo changamani la michezo”. Alisisitiza Nnauye
  Uwepo wa kiwanja hicho kunapelekea ucheleweshwaji wa kukamilika kwa maboresho na ujenzi wa Uwanja wa Uhuru.

  Aidha Waziri Nape amemuagiza Meneja wa Uwanja wa Taifa Rishe Urio kutoa maelezo ya kina juu ya uwepo wa Kiwanda hicho katika eneo la ndani ya masaa 24 ni kwanini akutoa taarifa juu ya uwepo wa shughuli za Kiwanda hicho katika eneo hilo ila hali yeye ndiye msimamizi mkuu wa Uwanja huo.

  Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya BFG Cheng Longhai amekiri kuwa Kiwand hicho kinaendeshwa kinyemela kwakuwa hakihusiani na mkataba wa kampuni hiyo.
  Wakatihuohuo Nape ameuagiza uongozi wa Selcom Tz kuhakikisha inakimilisha mfumo wa Tiketi za Kielekroniki na kukabidhi kwa Serikali ndani ya siku 30 kuanzia sasa.

  Agizo hilo ni muendelezo wa kutekeleza maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim wakati akiongea na wadau wa sekta ya michezo kwa mara ya kwanza toka kuteuliwa kwake kuwa Waziri Mkuu.

  0 0


  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Umoja wa Switch, Danford Mbilinyi akizungumza na waandishi wa habari juu ya utoaji wa huduma za kifedha katika benki leo jijini Dar es Salaam.

  UMOJA wa Switch imetimiza miaka 10 katika utoaji wa huduma za kibenki katika kufanya malipo.

  Akizungumza leo na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Umoja wa Switch, Danford Mbilinyi amesema kuwa kati benki 54 wamefikia benki 27 ambazo zinafanya huduma mijini na vijijini.

  Amesema kuwa katika utoaji huduma ya umoja switch wameshaweza kuunganisha na kampuni za simu katika utoaji wa huduma kifedha.

  Mbilinyi amesema kuwa katika kuongeza huduma ya umoja Switch watu wa  Afrika Mashariki wanaweza kupata huduma za kifedha katika kila nchi.

  Aidha amesema kwa mfumo wa malipo ya kidijitali dunia sasa ndio inakwenda huko hivyo itafika wakati kila mtu hatakuwa na fedha za kutembea nazo kutokana  mifumo ya kidijitali kuimarika.

  Aidha amesema kuwa umoja switch itazidi kujiimarisha katika utoaji huduma za kifedha katika benki.

  0 0

   Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji francis S. K Mutungi pamoja na Maaafisa Wandamizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa nje ya ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam Leo kabla ya kuanza kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
   Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakifuatilia kwa makini mawasilisho ya bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam.
   Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini,  Jaji Francis S.K Mutungi akitoa ufafanuzi wa hoja za wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti yam waka 2016/2017 ya  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika  Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam. Kushoto ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Manaibu waziri ,Mhe Antony P. Mavunde na Mhe. Dkt Abdallah Possi.

  WAJUMBE wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Sheria wamepewa rai ya kushikamana na Serikali katika kuhakikisha kuwa maboresho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka1992 na Sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 yanafanyika ili kuondoa utata na migongano ya utekelezaji wa masuala ya siasa nchini.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama wakati akijibu swali kutoka kwa wajumbe kwenye kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kilichofanyika  Leo katika ukumbi wa Saadan wa Mwalimu Nyerere Jijini dar es salaam ambao walihoji uhalisia wa utekelezaji wa sheria zililizopo sasa.

  Wajumbe hao walihoji utitiri wa vyama vingi nchini ambavyo miaka nenda rudi havina madiwani wala wabunge na vingine kutoshiriki katika chaguzi . Wajumbe pia walihoji gharama ndogo za usajili wa vyama vya siasa ukilinganisha na hali ya maisha iliyopo kwa sasa.
  Jambo lingine ambalo wajumbe wamehoji ni nafasi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika kushughulikia migogoro ya kisiasa ndani na nje ya Vyama vya Siasa na ushirikishwaji wa wanawake katika maamuzi ndani ya vyama vya siasa.

  Akijibu hoja hizo Mhe Mhagama amesisitiza kuwa maboresho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Gharama za uchaguzi ndio njia pekee itakayompa meno Msajili wa Vyama vya Siasa nchini katika kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

   “Sheria tulizonayo ndio inatoa mwanya wa haya yote haya na ndio maana Serikali kwa sasa inaendelea na taratibu za kuboresha sheria hizi, tayari Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ameshawasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Vyama vya Sasa na Sheria ya gharama za uchaguzi na sisi tumeridhia , tunasubiri tu bunge kujadili ili ziweze kutumika”alisisitiza mhe Mhagama.

  0 0

  Wabunge wa bunge la Arika Mashariki, (EALA), kutokaTanzania, wameendelea na ziara yao ya kutembelea vyombovya habari hapa nchini, ikiwa ni mkakati wa Jumuiya hiyo, kushirikisha vyombo vya habari ili kuwafahamishawananchi wa nchi hizo manufaa ya jumuiya hiyo kwao. LeoAprili 13, 2016, wabunge hao wakiongiozwa na Mwenyekiti wao Mh. Makongoro Nyerere, wametembelea kampuni ya The Guardian, wachapishaji wa magazeti ya The Guardian, Nipashe na Lete Raha, na kupata fursa ya kuelezwa shughuli zifanywazo na waandishi wa habarikwenye kampuni hiyo ambapo walitembelea kitengo cha habari mtandao, (E-NEWS), kitengo cha usanifu gazeti na kumalizia kwa mkutano wa kubadilishana mawazobaina ya wabunge hao na uongozi wa chumba cha habari cha The Guardian. Pichani, msanifu wa gazeti la The Guardian, Ben Mgana (aliyekaa), akiwaonyesha jinsi gazeti hilo linavyoandaliwa kabla ya kuchapishwa. Wakwanza kushoto ni Mhari Mtendaji wa gazeti hilo, Wallace Maugo, Mkuu wa chumba cha Habari cha The Guardian, Jesse Kwayu, (wapili kushoto) na wabunge wa hilo wakiongozwa na wmenyekiti wao Mh. Makongoro Nyerere (watatu kulia).NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
   MhaririMtendaji wa The Guardian, Wallace Mauggo, (watatu kushoto) na Mhariri Mkuu wa Chumba cha Habari cha The Guardian Limited, Bw. Jesse Kwayu) wakiwaonyesha wabunge hao baadhi ya magazeti yanayochapishwa na kampuni hiyo
   Mwenyekiti wa wabunge wa EALA-Tanzania, Mh. Makongoro Nyerere, 9wapili kulia), akisalimianana Mkuu wa kitengo cha habari mtandao (E-NEWS), cha The Guardian Limited, Mashaka Mgeta, wakati wabunge hao walipotembelea chumba cha Habari cha The Guardian Mikocheni jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Vijana watano kutoka Tanzania ni miongoni mwa vijana 30 wanaoshiriki katika mafunzo ya wawezeshaji wa ujasiliamali unaozingatia mazingira yanayofanyika jijini Beja, nchini Ureno.

  Mafunzo hao ambayo yanafanyika kwa muda wa siku saba yanalenga kuwajengea uwezo vijana hao kuendesha mafunzo kwa vijana wenzao katika nchi wanakotoka ili kusaidia kupunguza tatizo la ajira na uharibifu wa mazingira.

  Nchi zinazoshiriki mafunzo hayo na majina ya taasisi zinazoshiriki kwenye mabano ni pamoja na wenyeji Ureno (Check In), Italia (Cesie), Argentina (Subiral Sur), Slovenia (Pina), Nepal (CNN) na Tanzania (TYCEN) ambapo kila nchini imewakilishwa na vijana watano chini ya mradi wa ujasiliamali wa kujali mazingira ‘Green Entrepreneurship’.
  Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea kiwanda cha kuchakata taka cha Resialentejo, wakiongozwa na Injinia wa kiwanda hicho Pedro Sobral.
  Wahsiriki wakiwa katika picha ya pamoja walipotembelea Halimashauri ya Manispaa ya Jiji la Beja ambao walipokelewa na Sonia Calvario Mshauri wa Meya wa Manispaa hiyo
  Mkurugenzi wa TYCEN, Chris Ndalo kutoka Tanzania akitoa mada wakati mafunzo hayo

  0 0


  Na Rabi Hume.  Katika kuhakikisha watu wanaoishi na UKIMWI wanaishi kwa furaha bila kunyanyapaliwa na watu wanaowazunguka, jamii imetakiwa kuwa na mtazamo tofauti kwa watu wanaoishi na ugonjwa huo.

  Hayo yalisemwa na mke wa mtoto wa mfalme wa Norway, Mette-Marit ambaye pia ni balozi kimataifa wa Shirika la Umoja la kupambana na HIV na UKIMWI (UNAIDS) wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kazi anazozifanya kwa UNAIDS kama balozi ambaye anazunguka maeneo mbalimbali duniani ili kuelimisha jamii kuhusu UKIMWI.

  Mette-Marrit alisema kuwa watu wenye UKIMWI ni kama watu wengine hivyo wana haki ya kupata huduma bila kunyanyapaliwa ili waweze kuishi kwa uhuru kama watu wengine na ili kufanikisha hilo ni wajibu wa kila mtu kuwasaidia waathirika.

  “Watu kuwa na UKIMWI sio mwisho wa maisha inatakiwa kwanza jami kuwa na mtazamo tofauti na inatakiwa kila mtu kusaidia mapambano ya UKIMWI sio jambo la mtu mmoja mmoja,” alisema Mette-Marit.
  Balozi wa Kimataifa wa UNAIDS, Mette-Marit akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kazi anazofanya kama balozi wa UNAIDS kwa kipindi cha miaka 10 tangu aanze kazi hiyo. (Picha zote na Rabi Hume)

  Nae Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho alisema Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili kupambana na UKIMWI lakini pia ili kufanikisha mapambano hayo wanahitaji kushirikiana na taasisi ambazo zitawasaidia katika mapambano hayo.

  Lakini pia Dkt. Mrisho amezitaka serikali za mitaa kuacha kusubiri mpaka serikali imepeleke pesa ndiyo wawasaidie watu wanaoishi na UKIMWI na hivyo waweke utaratibu wa kutumia sehemu ya mapato yao ili kusaidia mapambano hayo.


  “Serikali haijalala katika mapambano tunahitaji kushirikiana na taasisi ambazo zinatusaidia kupunguza maambukizi mapya na tunaona Mette-Marit amekuwa akifanya jambo zuri anazunguka sehemu nyingi ili kusaidia kupunguza maamukizi mapya ya UKIMWI,” alisema Dkt. Mrisho.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho akizungumzia kuhusu juhudi zinazofanywa na serikali katika mapambano ya UKIMWI.
  Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi, UNAIDS nchini Tanzania, Warren Naamara akizungumzia ugonjwa wa UKIMWI.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed (kulia)  akikabidhiana Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini leo katika ukumbi wa Tume ya Mipango Vuga Mjimkongwe wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
  Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wa tume ya mipango wakati wa makabidhiano ya Ofisi na  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed katika ukumbi wa Tume ya Mipango Vuga Mji Mkonge wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
  Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini akiagana na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed baada ya makabidhiano ya Ofisi katika viwanja vya Ofisi ya Tume ya Mipango leo Vuga Mji Mkongwe wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
  .[Picha na Ikulu.]

  0 0

  Na Raymond Mushumbusi


  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saeed Kubenea kifungo cha nje cha miezi mitatu kutokana kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  Akisoma hukumu hiyo leo Jijini Dar es Salaam Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Thomas Simba amesema kuwa mahakama imeamua kumpa mshitakiwa adhabu ya kifungo hicho kwa kuwa ndilo kosa lake la kwanza, hivyo Mshatakiwa anastahili kupata adhabu ya huruma.
  Chini ya adhabu hiyo iliyotolewa chini ya kifungu No. 89 kifungo kidogo cha kwanza Kubenea hatakiwi kufanya kosa la aina yoyote ambalo litamsababisha arudishwe tena mahakamani na endapo itatokea akafanya hivyo mahakama itampa adhabu ya kifungo cha kwenda jela.


  Awali kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo mshtakiwa Said Kubenea mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba alipewa nafasi ya kujitetea ni kwanini asipewe adhabu kali kwa kosa alilolitenda ambapo alieleza Mahakama hiyo kuwa hakuwa na nia mbaya ya kwenda kufanya fujo eneo la tukio ambapo kulikuwa na mgomo wa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha TOOKU cha jijini Dar es salaam bali alikwenda kwa lengo la kutafuta suluhu ya mgomo huo akiwa kama mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Ubungo. 

  Ikumbukwe kuwa Jalada la kesi hiyo na 320 lilifunguliwa na Jamhuri dhidi ya Said Kubenea kwa kosa la kutumia lugha ya matusi kwa aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda
  Upande wa washtakiwa wameonyesha kutoridhishwa na hukumu hiyo na wameomba kukata rufaa.

  0 0

  Gari lililobeba sanduku lenye mwili wa marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo, likiwasili kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar leo jioni tayari kwa mazishi.
  Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akiweka shada la Maua kwenye kaburi la Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo, wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar jioni ya leo.
  Sanduku lenye mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo,likishushwa kwenye nyumba yake ya Milele,makaburi ya Kinondoni jijini Dar leo jioni.
  Mama wa Marehem Ndanda Kosovo akimshukuru Waziri Nape Nnauye pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubali mtoto wake kuzikwa katika ardhi ya Tanzania.
  Baadhi ya Wafiwa wakiwa Makaburini tayari kushirik mazishi ya mpendwa wao Ndanda Kosovo.
  Taratibu za Maziko zikiendelea makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
  Hapa ndipo mahala alipohifadhiwa Mwanamuziki Mkongwe wa Dansi hapa nchini, Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo,amezikwa leo jioni katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar,ambapo Waziri mazishi hayo yameongozwa na Wazir Nape Nnauye,Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,Wanamuziki,wasanii wa filamu,ndugu jamaa na marafiki kutoka sehemu mbalimbali.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Czech hapa nchini  Pavel Rezac, tukio hilo lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa nchi ya Jamhuri ya Sudani Kusini Mariano Deng Ngor aliyefika Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha hati yake za utambulisho.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa Brazil hapa nchini Carlos Alfonso Iglesias Ikulu jijini Dar es Salaam.
  PICHA NA IKULU.

  0 0

  The Jakaya Kikwete Cardiac Institute at the Muhimbili National Hospital in Dar es salaam is dispatching  a team of three doctors to perform life-saving heart surgeries to Rwandan Children at the King Faisal Hospital in Kigali.

  According to the Acting Executive Director of JKCI Prof Mohamed Janabi (pictured right), the three Tanzanian Medical experts will work hand in hand with their international partner,  Open Heart International (OHI) of Australia that has a five year Memorandum of Understanding with JKCI in regard to developing Pediatric Cardiac Services in Tanzania. 
  Prof Janabi named the trio who are pictured below as taem leader Dr. Godwin Godfrey Sharau (Pediatric Cardiac Surgeon),  Dr, Naiz Majani Pediatric (Cardiologist)  and Dr. Onesmo Mhewa (Pediatric Cardiac Anesthesiologist)
  The three Tanzanian medical experts will set up a surgical camp at the  King Faisal Medical Central from 14th to 22nd April, 2016 where some 25 Rwandan Children are expected to get their life-saving heart operations.  
  Since Rwanda has yet to have a standing cardiac program, the collaboration is aimed at addressing urgent surgical needs for the growing neighboring country's long waiting list of patients as well as working with Rwandese health providers in training and development.
  This is a welcome gesture from Tanzania to Rwandan children to have their surgeries at JKCI as part of Tanzania – Rwanda and East Africa collaboration spirit.  
  The JKCI, though still at its infancy, has vastly grown its capacity in as far as  open heart surgeries on children is concerned.
  In 2015,  for instance, some  207 children had their life-saving surgeries at JKCI, and many more continue to receive treatment  this year. 
  Over 300 more children are expected to be operated on at the Institute this year, whereby already some 80 patients have already been operated on from January to March alone.  


  The trip comes only a few days after President Dr. John Pombe Joseph Magufuli's  visit of   Rwanda during his maiden trip abroad. 
  " The objective of JKCI remains to being  a to Center of Excellency in Heart Diseases in East Africa by 2020", said  Prof Janabi, adding that in 2015 the center successfully  operated on twins from the DRC, patients from the Comoros islands and procedures have been conducted on a number of  diplomats residing in Dar es Salaam.
  "All i can say at the moment is that  the future of JKCI  is bright",  said the soft-spoken Prof. Janabi

  0 0

  RAIS wa zamani wa Klabuya Simba ya Dar es Salaam, Alhaj Ismail Aden Rage, (kushoto), akipokea kadi yake ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSS, kutoka kwa Meneja Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa PSPF, Bi.Costantina Martin, makao makuu ya PSPF, katikati ya jiji la Dar es Salaam, Aprili 14, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
  Alhaj Rage akionyesha kadi hiyo

  NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

  RAIS wa zamani wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Alhaj Ismael Aden Rage, amejiunga na mpangowa uchangiaji wa Hiari (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Aprili 14, 2016.

  Rage ambaye pia ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Tabora mjini, kufuatia kujiunga huko, amefaidika kuingizwa kwenye fao la huduma ya afya litolewalo na Mfuko huo kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF ambao una ushirikiano wa kutoa huduma za afya kwa wanachama wa PSPF wanaotaka kufaidikana huduma hiyo.

  “Nitoe wito kwa wanamichezo wakiwemo wa mpira wa miguu, kuchangamkia fursa hiyo kwani mambo sasa yamebadilia kujiunga na PSPF kupitia mpango huu wa hiari ambao unamruhusu mtu binafsi au vikundi kujiunga na uanachama, lakini pia kutokana na kupanda kwa huduma za afya, ukiwa mwanachama wa PSPF unaweza kupata huduma ya afya wewe na familia yako, hii ni faida kubwa.” Alisema Rage wakati akikabidhiwa kadi yake ya uanachama na Meneja Masoko, Mawasiliano na Uenezi wa PSPF, Bi. Costantina Martn.

  Rage alisema, yeye kama mwanamichezo atahamasisha wanamichezo hususan wacheza mpira kujiunga na mpango huu kwani maisha ya sasa yanahitaji kwenda kisasa, na jambo muhimu ni kuwa na afya bora, na afya bora utaipata kama unapata huduma bora, nimeambiwa kupitia mpango huu ninaweza kupata matibabu kwenye hospitali yoyote nchini na wakati wowote, Alisema.

  Awali Rage alijaza fomu za kujiunga na uanachama ambapo alipokewa na Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, PSS, wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe. Ambaye alimshukuru Rage kwa kuwa mwanachama wa Mfuko huo.
  Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mwanjaa Sembe, (kushoto), akipokea fomu za kujiunga na uanachama kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Klabu ya soka ya Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, makao makuu ya PSPF, katikati ya jiji la Dar es Salaam, Aprili 14, 2016
  Alhaj Rage, (kushoto), akiweka dole gumba kwenye fomu yake ya uanachama huku akisaidiwa na Bi. Mwanjaa Sembe, (kulia) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw.Abdul Njaidi.
   

older | 1 | .... | 1183 | 1184 | (Page 1185) | 1186 | 1187 | .... | 3286 | newer