Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1179 | 1180 | (Page 1181) | 1182 | 1183 | .... | 3283 | newer

  0 0  0 0

  Globu ya jamii imepokea taarifa za Mwanamuziki mkongwe aliyewahi kujizolea sifa kem kem katika miondoko ya dansi hapa  nchini wakati akiwa na bendi ya FM miaka ya nyuma kabla ya kujiengua na kuunda kundi lake lililojulikana kwa jina la Stono Musica a.k.a Wajela Jela Gwaa, Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ amefariki Dunia leo asubuhi,baada ya kuugua kwa siku chache

  Taarifa kutoka kwa mtu wake wa Karibu ambaye pia ni Mwanamuziki wa dansi,Kardinal Gento amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na ameongeza kuwa Ndanda Kosovo amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa tangu juzi kutokana na matatizo ya tumbo.
  *Tutazidi kupeana taarifa zaidi hapa hapa kadiri zitakavyokuwa zikiingia*
  Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-AMIN.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  ALIYEKUWA mgombea ubunge jimbo la Vunjo (CCM),  Innocent Melleck Shirima, amelitaka Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro kuchukua hatua za haraka kuhusu uchunguzi wa mauaji ya mlinzi wa nyumba yake iliyopo Marangu ambaye aliuawa kwa kuchomwa visu na watu wasiojulika.

  Mauaji hayo ya kikatili ambayo haijajulikana chanzo chake, yalitokea wiki hii nyumbani kwa  Melleck ambaye ni kada wa CCM.

  Melleck alipeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, katika Vunjo mkoani Kiliamnjaro.

  Akizungumza na Mtandao huu, Melleck alisema, kwa sasa anaishi kwa hofu kubwa kutokana na mauaji hayo ya kinyama kwa kuwa hajui yalimlenga huyo mlinzi pekee ama alikuwa anatafutwa yeye.

  Alisema wasiwasi unakuwa mkubwa kwa kuwa wauaji hayo hao baada ya kukamilisha unyama huo hawakuchukua kitu chochote nyumbani kwake.

  Akisimlia mkasa huo, Melleck alisea siku ya tukio hilo, ilikuwa awasili nyumbani kwake akitokea Dar es Salaam, lakini bahati nzuria akawa amepata dharura na hivyo akaahirisha safari yake.
  "Kutokea mauaji hayo kumenipa hofu kubwa pamoja na familia yangu yote kwa sasa inaishi kwa hofu," alisema

  Alisema siku ya tukio alikuwa akipokea simu za watu wengi kutoka jimbo la Vunjo ambako aligombea ubunge, zikimuuliza anatarajia kufika Marangu muda gani

  Melleck alisema baada ya kupokea simu hizo aliwajibu watu hao kuwa alikuwa njiani kuelekea huko, ingawa ukweli ni kwamba wakati huo bado alikuwa Dar es Salaam.

  Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema, jeshi la polisi linaendelea kuwasaka wauaji hao ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua mashine ya MRI katika hospitali ya Benjamin Mkapa kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma wakati alipoitembela Aprili 9, 2016. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, , Dkt. Hamis Kigwangala.
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Khamis Kigwangala wakikagua mashine ya Mobile Digital xray wakati walipotembelea hospitali ya Benjamin Mkapa kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma Aprili 9, 2016.Kulia ni Kaimu Mkuu wa Hospitali hiyo ProfesaGesai. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront Leo April 09,2016. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wa tatu kushoto Mwenyekiti wa Kampuni Uwekezaji ya Group 6 Jonson Huang wa pili kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Geoge Simbachawene, na Waziri Biasha na Uwekezaji Mhe. Chales Mwinjage.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Pazia kuzindua rasmi Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village Msasani Beach Waterfront Leo April 09,2016. Kulia Afisa Muandamizi Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wa tatu kushoto Mwenyekiti wa Kampuni Uwekezaji ya Group 6 Jonson Huang.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront, Leo Aapril 09,2016.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Afisa Muandamizi wa Ubalozi wa China Hapa Nchini Guo Haodong, wakati wa ghafla ya uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Villege unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Gropu 6 ya China zinazojengwa Msasani Beach Waterfront.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China. Mradi huo unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront unategemewa kutoa ajira jumla ya watu 2000 utakapokamilika. Kuli Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Jonson Huang, Leo Aapril 2016.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Palm Village unaodhaminiwa na kujengwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Group 6 ya China. Mradi huo unaojengwa katika eneo la Msasani Beach Waterfront unategemewa kutoa ajira jumla ya watu 2000 utakapokamilika. Leo Aapril 09,2016.(Picha na OMR).

  0 0

  Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira, Mh luhaga Mpina , kushoto Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesera Kulia Naibu Meya wa mji wa Iringa Bw. Joseph Liata ambae pia ni diwani (Chadema) kwa pamoja wakifanya usafi katika soko la mji wa Iringa.
  Kushoto Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesera kulia Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina wakimwaga maji wakati wakifanya usafi sokoni Mkoani Iringa Leo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, Akiuandaa mche wa mti kabla kuupanda katika eneo la chanzo cha maji cha chemchem cha Kitwiru, Leo Mkoani Iringa.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina Akimwagilia maji mara baada ya kupanda mti , katika eneo la chanzo cha maji cha Kitwiru Mkoani Iringa.
  Kulia Mganga Mkuu mfawidhi wa hospitali ya Rufaa Iringa dkt Robert Salim, akitoa maelezo ya uteketezaji wa taka katika hospatali ya Rufaa kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina na Ujumbe wake walipokagua mazingira ya hosptali hiyo leo.

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa, Mkoani Iringa Kulitaftia ufumbuzi suala la uteketezaji wa taka ngumu katika hospitali hiyo.

  Mh. Mpina ametoa maagizo hayo leo alipotembelea Hosptali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa katika ziara yake ya kukagua usafi wa mazingira na utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa maziringa katika viwanda vya mkoa wa Iringa.

  Imeelezwa kuwa uteketezaji wa tanga hatarishi katika hosptali hiyo ya mkoa umekumbana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa kifaa cha kuteketeza taka hospitalini hapo kwa muda mrefu bila matengezo yeyote uliosababishwa na taratibu za utekelezaji manunuzi serikalini.

  Kwa Upande wake mganga mkuu mfawidhi wa hospital hiyo dkt Robert Salim Amemueleza Naibu waziri Mpina kuwa taka zizalishwazo katika hosptali hiyo zimekuwa zikitupwa katika Dampo la mkoani hapo na hata hivyo..hosptali imekuwa na wakati mgumu sana katika kuteketeza taka hatarishi kama vile za sindano, gloves, nyembe na bandeji mana haziozi ardhini kirahisi.

  Akitolea ufafanunuzi sualala za uteketezaji wa taka hatarishi hospitalini hapo, mratibu wa kanda ya nyanda za juu kusini wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) bw. Godlove Mwamsojo..ameleeza kuwa baraza limewahi kushauri uongozi wa hosptali hiyo kuteketeza taka hizo kwa kusaidiwa na kiwanda cha mbao cha Sao hill kilichopo wilayani Mufindi kwa kuwa kiwanda hicho kina vifaa vya kutosha, bila mafanikio kutokana na sababu kwamba hospital hiyo huzalisha taka nyingi kuzidi uwezo wa kiwanda cha Sao Hill kusaidia kuziharibu.

  Wakati huo huo, Naibu Waziri Mpina alikagua mazingira ya soko la Mjini Iringa na kushiriki katika usafi wa mazingira pamoja na kupanda miti, ambapo Mh. Mpina,alipanda mti katika kata ya Kitwivu na kuwaasa wakazi wa Iringa kuwa walinzi wa misitu na kutoa taarifa za wizi na uhujumu wa magogo ili sheria ichukue mkondo wake na kuwaasa watunze vyanzo vya maji kama walivyotunza vizuri chanzo cha maji ya chemchem cha Kitwivu.

  “Taifa lazima lipande miti ili kuhepukana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi tunazokumbana nazo.” Alisisitiza. Aidha Mh Mpina aliiongeza Wilaya ya Mufindi kwa kupitiliza lengo la kupanda miti milioni moja na laki tano kila mwaka katika kila wilaya na kupanda miti milioni thelathini na tano kwa mwaka.

  0 0

  Na Raymond Mushumbusi MAELEZO

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Uratibu,Ajira,kazi na watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama amewatembelea wananchi waliopatwa na majanga ya kuangukiwa na kifusi eneo la Kawe na kuwapa mkono wa pole.

  Akiongea na moja ya familia zilizopatwa na maafa hayo Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya tukio hilo na kwa vifo vilivyojitokeza na kuahidi kutoa ushirikiano kwa familia ya wafiwa na waathirika wa tukio hilo.

  “Ndugu zangu tumekuja kushirikiana nayi kwenye msiba huu mzito, ambao wenzetu wamepoteza karibu familia nzima kutokana na haya maafa, poleni sana kwa msiba na Serikali ipo pamoja nayi katika kipindi hiki kigumu.” Alisema Mhe Jenista.
  `
  Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wakati Serikali inapokuja kwa ajili ya kujadili jinsi ya kutatua mambo yanayowezesha kuhatarisha maisha yao hasa, tatizo la makazi yaliyopo mabondeni kwa ajili ya usalama wao na familia zao katika kuzingatia suala la mipango miji ili kuepukana na majanga kama haya.

  Aidha kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Raymond Mushi amesema kwa upande wake amesikitishwa na tukio hilo na kuongeza kuwa Wilaya imejipanga kwa kushirikiana na kamati ya maafa ya Wilaya na Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuendelea kuangalia ni kwa namna gani wataweza kuwasaidia wananchi waliobaki katika maeneo hayo.

  Akitoa shukrani kwa niaba ya familia ya wafiwa Bi Gaudencia Deogratius ambaye amepoteza mume na watoto wawili ameishukuru Serikali kwa faraja aliyopata kutoka kwa Waziri na hakutegemea kupata ugeni huo na ameiomba Serikali kuwasaidia wale waliopo mabondeni ili kuepusha majanga mengine zaidi kutokea.

  Tukio la hili la nyumba kuangiwa na kifusi katika eneo la kawe Jijini Dar es Salaam lilitokea April 7 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagamaakitoa ubani kwa Gaudensia Deogratius aliyefiwa na watoto wawili na mume baada ya kufunikwa na kifusi Kawe Ukwamani Dar Es Salaam Aprili 9, 2016
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa mkono wa pole kwa mama wa marehemu Ephrahim Mangule (aliyefariki kwa kuangukiwa na kifusi Kawe) wakati wa msiba huo Kinondoni Dar es Salaam tarehe 9 Aprili, 2016
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagamaakitoa salamu za pole kwa wafiwa waliopotelewa na ndugu 3 baada ya mvua zilizonyesha Aprili 7, 2016 na kuangukiwa na nyumba Kawe Dar es Salaam kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Raymond Mushi
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Raymond Mushi akizungumza na moja ya familia ya wafiwa walioangukiwa na kifusi Kawe Dar es Salaam wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipowatembelea tarehe 9, Aprili, 2016
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiangalia chumba kilichoangukiwa na kifusi baada ya mvua kubwa zilizonyesha Aprili 7, 2016 na kuua watu 5 wa familia moja Kawe Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema mtambo mpya wa kisasa wa kupima mafuta yanayoingia nchini flow meter unaojengwa Kigamboni jijini Dar es salaam uko katika hatua za mwisho za kukamilika kwake na utaanza kazi rasmi mapema mwezi ujao.

  Prof. Mbarawa amesema hayo wakati alipokagua mtambo huo unaosimamiwa na Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) na kuhimiza waendeshaji wa mtambo huo wawe watu wenye uadilifu wa hali ya juu na elimu ya kutosha ili kuulinda na kuwezesha kufanyakazi inavyostahili.

  “Hakikisheni mnawasiliana na Wakala wa Vipimo nchini (WMA), ili wahakikishe mtambo huu unaviwango vinavyotakiwa vitakavyowawezesha wafanyabiashara wa mafuta kuridhika na ufanyakazi wa mtambo huu ili kuondoa malalamiko”, amesema Prof. Mbarawa.

  Zaidi ya shilingi bilioni 12 zimetumika katika ujenzi wa mtambo huo ambao utawezesha Serikali kupata mapato stahiki na wafanyabishara kupata mafuta sahihi kwa mujibu wa mahitaji yao.

  Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni na kuwataka wananchi kuhakikisha wanalitumia daraja hilo kwa usahihi na kuepuka vitendo vyote vya hujuma.

  Amesema daraja hilo lililojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 214 linatarajiwa kufunguliwa rasmi Aprili 16 na litakuwa na njia sita za magari na mbili za watembea kwa miguu.

  “Nawataka wananchi na watumiaji wote wa daraja hili kuhakikisha kuwa miundombinu ya daraja haihujumiwi na watu wenye nia mbaya kwani vitendo vya aina hiyo licha ya kuharibu daraja vitahatarisha usalama wa watumiaji”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

  Naye Msimamizi wa Daraja hilo kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eng. Karim Mataka amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa Daraja la Kigamboni umekamilika katika hatua zote na kinachosubitriwa na ufunguzi na kuanza kutumika.

  Amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya daraja hilo kwa madereva na watembea kwa miguu ili kuepuka usumbufu siku za mwanzoni.

  Daraja hilo litakalofunguliwa rasmi Aprili 16 litapunguza msongamano wa usafiri kwa wakazi wa kigamboni na maeneo ya katikati ya jiji la Dar es salaam.
  Meneja wa mradi wa Ujenzi wa Flow Meter ya Kigamboni Eng. Mary Mhayaya akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alipokagua maendeleo ya ujenzi huo.
  Muonekano wa Flow Meter mpya ya Kigamboni katika hatua za mwisho za ujenzi wake.
  Muonekano wa Daraja la Kigamboni mara baada ya ujenzi wake kukamilika.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kivuko cha Magogoni (kushoto) na Nahodha wa kivuko hicho (kulia) wakati alipokikagua.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelekezo kwa Mkurugenzi Msaidizi Barabara za Mijini Eng. Hussein Mativila (kushoto) alipokagua Daraja la Kigamboni.

  0 0

  Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wametakiwa kuwa wabunifu katika sehemu zao za kazi ili kuongeza ufanisi katika majukumu yao ya kila siku.

  Akitoa wito huo wakati akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge, Ajira,Kazi na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema watumishi wanatakiwa kutumia rasilimali walizonazo kuonesha ubunifu wao katika idara na vitengo walivyopo ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.

  “Ofisi ya Waziri Mkuu ni mratibu na msimamizi wa shughuli za kila siku za Serikali hivyo basi naomba tuwe wabunifu katika sehemu zetu za kazi ili tumsaidie Mhe. Waziri Mkuu kutelekeza majukumu haya kwa kasi na ufanisi unaotakiwa.” Alisema Mhe. Jenista.

  Mhe. Jenista Mhagama ametoa wito kwa wakuu wa Idara na Vitengo kushirikiana na watumishi katika ofisi zao ili kuongeza ufanisi wa kazi za kila siku katika idara na Vitengo mbalimbali.

  Akizungumza mara baada ya kikao Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu Dkt Hamis Mwinyimvua amesema kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi ni fursa muhimu kwa wafanyakazi kukutana na kujadili masuala mbalimbali ili kupata mbinu za kupambana na changamoto zinazokabili Idara na vitengo mbalimbali.

  Kwa mujibu wa Waraka wa Rais Namba 1 wa Mwaka 1970, moja ya madhumuni ya kuanzishwa kwa Mabaraza ya Wafanyakazi ni kuongeza ufanisi na tija katika sehemu za kazi na kupitia Mabaraza haya, wafanyakazi pamoja na waajiri hupata fursa ya kubadilishana mawazo na kubuni mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto katika sehemu zao za kazi.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akitoa ufafanuzi wa masuala ya wafanyakazi wa Ofisi hiyo wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 9, 20 katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hoja za Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani)) wakati wa mkutano wa baraza hilo tarehe 9 Aprili, 2016 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamis Mwinyimvua akizungumza wakati wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu, Aprili 9, 2016 Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi hiyo mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo Aprili 9, 2016.(Picha Zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   

  0 0

  Na.catherine Sungura,Kyela 

  Wananchi wa wilaya ya kyela wametakiwa kuachana na mila potofu na kupelekea kufanya mauaji ya watu kwa kuhusisha ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa unaoletwa kwa imani ya kishirikina

  Hayo yamesemwa leo na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu,wakati alipofanya ziara katika wilaya hii na kuongea na watendaji wa halmashauri.

  Mh.Ummy alisema ameshangazwa na baadhi ya wananchi katika kijiji cha unyakyusa kujichukulia sheria mkononi na kuwauwa wanawake watatu kwa madai ndio wanaoneza ugonjwa huo.

  Naye mkuu wa wilaya ya kyela dkt. Thea Ntara alisema kamati yake ya ulinzi na usalama imeshawakamata watuhumiwa wawili wa tukio hilo na kuwafikisha mahakamani ingawa bado mtuhumiwa mmoja aliyekimbilia nchi jirani ya malawi anatafutwa.

  Matukio hayo yametokea mwezi februari na machi mwaka huu.
  Wilaya ya kyela ilipokea mgonjwa wa kipindupindu novemba 2015 na hadi kufikia machi 2016 jumla ya wagonjwa 405 waliugua ambapo vifo vilikua 8. Kwa sasa wilaya hii haina mgonjwa wa kipindupindu

  Hali ya kipindupindu nchini imekua ni tatizo kubwa nchini,takribani mikoa yote tanzania bara imekubwa na ugonjwa huu tangu ulipotiwe mwezi agosti mwaka jana,isipokuwa kwa mkoa wa Ruvuma na Njombe ambapo hawajaripoti mgonjwa wowote hadi Sasa

  Ripoti ya wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto ya tarehe 4 machi mwaka huu inaonesha jumla ya wagonjwa 20,294 wametolewa taarifa na kati ya hao 320 wamepoteza maisha.Kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka,mwenendo wa kipindupindu unaashiria idadi ya wagonjwa nchini inaongezeka

  0 0

  Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma akichuana vikali na Mabeki wa timu ya Al Ahly ya Misri, wakati wa mtanange wa Mashindano ya kuwania Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka suluhu ya kufungana bao 1-1.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI-MMG.
  Salum Telela wa Yanga, akiichachafya ngome ya Al Alhy, katika mtanange wa Mashindano ya kuwania Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka suluhu ya kufungana bao 1-1.
  Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amisi Tambwe akiondoka na mpira huku Mabeki wa timu ya Al Ahly ya Misri wakimfata bila kujua la kufanya, wakati wa mtanange wa Mashindano ya kuwania Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka suluhu ya kufungana bao 1-1.
  Kiungo Mkabaji wa Timu ya Yanga, Salum Telela, akiwania mpira wa juu na Abdallah Said wa Al Ahly, wakati wa mtanange wa Mashindano ya kuwania Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka suluhu ya kufungana bao 1-1.
  Mchezaji wa Yanga, Deus Kaseke, akiichambua kama karanga, ngome ya Al Ahly, wakati wa mtanange wa Mashindano ya kuwania Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka suluhu ya kufungana bao 1-1.
  Wachezaji wa Timu ya Al Ahly, wakishangilia baada ya kupata bao la kuongoza mnamo dakika ya 10 ya mchezo, dhidi ya Timu ya Yanga, iliwa ni mchezo wa kuwania Kombe la Klabu Bingwa Afrika, uliopigwa jioni ya leo katika dimba la Taifa, Jijini Dar es salaam. Timu hizo zimetoka suluhu ya kufungana bao 1-1.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Unesco National Commission for Tanzania, organised a women empowerment workshop, titled "UNESCO Cultivating Women Empowerment".The workshop took place on Friday, the 8th of April 2016 at British council in Dar es salaam.

  The workshop was organised in an effort to implement the United Nations 17 global goals for sustainable development that put women at the forefront of development, specifically sustainable development goal no.5 that seeks to achieve gender equality and empower all women and girls in the effort to attain planet 50-50 by 2030.

  Cultivating Women Empowerment workshop was set to equip young women with the required skills to professionally grow and develop skills which include, Corporate Protocol and Communication Etiquette, Emotional Intelligence, Leadership and Negotiations skills together with Venture Capital and Entrepreneurship. The workshop involved presentation, discussions, sharing experience and Networking among participants and Speakers

  UNESCO National Commission invited speakers who delivered presentation on different topics the speakers include, Dr. Vicensia Shule from the University of Dar es Salaam, Doris Mollel from Doris Mollel Foundation, Anna Mtembei from DICE Micro finance and Judith Mwaya from Unesco National Commission.

  The Workshop gave women a platform to discuss and share issues that aim at achieving Sustainable development.
  A group photo of the speakers and the participants of the workshop. From the left its Judith Mwaya from Unesco national commission, Doris Mollel from Doris Mollel Foundation, Simba Mwinyi from Unesco National Commission and Rehema Horera from the Unesco National commission.
  Doris Mollel a guest speaker from the Doris Mollel Foundation speaking on Leadership and Negotiations.
  Judith Mwaya a speaker from Unesco National Commission speaking on emotional intelligence.


  0 0

  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein.

  0 0
  SIMU.TV:  Mh.Samia Suluhu azindua mradi wa makazi ya Palm Village unaoendeshwa na serikali ya China kusaidia wananchi wa kawaida;  https://youtu.be/BViIIRwWCjg

  SIMU.TV:   Jeshi la polisi lafyeka mashamba ya bangi na kuteketeza tani 2 za bangi katika wilaya ya Bariadi; https://youtu.be/XQM08T9YGr4

  SIMU.TV:  Wazee wanaolelewa katika kambi ya Kolandota Shinyanga walazimika kujihifadhi kwenye madarasa ya shule kufuatia ubovu wa majengo ya kituo hicho; https://youtu.be/RKm_VArWZ1Y

  SIMU.TV:  Naibu waziri Ruhanga Mpina atoa agizo kali kwa hospitali ya rufaa Iringa na kutaka agizo hilo litekelezwe ndani ya mwezi mmoja; https://youtu.be/gfEQYIdbi3I

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

   Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  akiweka udongo kwenye kaburi la kaka yake, Selemani Selemani katika mazishi yaliyofanyika  kwenye kijiji cha Narung'ombe wilayani Ruangwa Aprili 9, 2016. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0  0 0

   Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu (kulia), akiwaelekeza jinsi ya kucheza mpira wachezaji wa Timu ya vijana waliochini ya miaka 20 ya Sunderland alipotembelea Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park kilichopo Kidongo Chekundu Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana. Kanu yupo nchini kwa ziara ya siku tano kwa mwaliko wa Kampuni ya StarTimes Tanzania ambapo jana alitoa msaada wa vyakula, magodoro, sabuni na vyombo vya matumizi ya jikoni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi ya Majimatitu ya Mbagala wilayani Temeke.
   Kanu akielekeza namna bora ya kucheza mpira.
   Kanu akizungumza na watoto wanaopata mafunzo ya soka katika kituo hicho.
  Kanu akikagua timu ya watoto hao.  0 0


  0 0


  0 0

  Kituo cha EFM redio kwa mara nyingine tena kimeibuka na shindano lake la shika ndinga kwa mashabiki wake wa jiji la Dar na Pwani. Pamoja na kufanyika kwa shindano hilo lililozua msisimko mkubwa miongoni mwa wilaya ya Temeke,EFM Radiao pia waliwatangaza watangazaji wao Wapya watatu waliokuwa Clouds FM,Watangazaji hao ni Abel Onesmo,Paul James na Gerald Hando.Shindano hilo Kwa mwaka huu ,limezinduliwa rasmi jana April 9/2016 kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke  jijini Dar.

  Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Sebo alisema kuwa shindano hilo litaendelea pia kwa wilaya ya Ilala, Kinondoni, Bagamoyo, na Kibaha na hatimae kilele chake kufanyika katika uwanja wa Sinza TP.


  Sebo alisema kuwa Shindano hilo litaanza na washiriki 60 kwenye kila wilaya na washiriki 10 kati yao wanawake watano na wanaume watano ambao wataingia kwenye fainali ya kujinyakulia gari ambao wamepata nafasi ya kushiriki kwa njia ya kupiga simu na kujibu kiufasaha swali husika ili kupata nafasi ya kushiriki shindano la shika ndinga.
  Alisema kuwa shindano hilo mwaka huu limeboreshwa zaidi kwa kutoa zawadi za pikipiki kwenye ngazi ya wilaya na magari kwenye ngazi ya fainali.Lengo ni kuwawezesha wasikilizaji wake kwa namna moja ama nyingine katika kuongeza na kukuza kipato kitakacho changia kuimarisha maisha yao kupitia zawadi watakazoibuka nazo.
  Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, DenisSebo akiwatambulisha watangazaji wapya wa kituo cha redio cha Efm,Abel Onesmo,Paul James na Gerald Hando kwa wananchi jana katika shindano la shika ndinga kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam.
  Watangazani wapya Paul James na Gerald Hando na ,Abel Onesmo akielekea jukwaani kutangazwa rasmi kwa wakazi wa Temeke,jijini Dar.
  Watu wa huduma ya kwanza wakiwahudumia washiriki wa Shindano hilo waliokuwa wamezimia kutokana na mshtuko alioupata kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam.
  Mshindi wa shindano la shika ndinga alieshinda pikipiki Salehe Maga akizungumza na waandi wa habari (hawapo picha) juu ya kuushukuru uongozi wa Efm kwa kuanzaisha shindano hilo.
  Mshindi wa shindano la shika ndinga alieshinda pikipiki Philipina Mshanga akizungumza na waandi wa habari (hawapo picha) juu ya kuushukuru uongozi wa Efm kwa kuanzaisha shindano hilo , na kuwaomba wakina wanawake wajitokeze kwa wingi kwenye mashindano hayo.
  Ndinga na pikipiki zikiwa juu ya jukwaa kwenye uwanja wa zakhiem- Temeke jijini Dar es salaam.
   

older | 1 | .... | 1179 | 1180 | (Page 1181) | 1182 | 1183 | .... | 3283 | newer