Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LIMEFANIKIWA KUWAKAMATA WATU 63 WANAOZANIWA KUWA MAJAMBAZI.

$
0
0
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro kizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limekamata majambazi sitini na tatu (63) wa matukio ya unyang'anyi wa kutumia silaha katika oparesheni maalum iliyoendeshwa kwa wiki nzima na Jumla ya silaha sita, (6) ikiwemo SMG 1, SHORTGUN PUMP ACTION 3 na RIFLE 2. 
 Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro akionesha silaha huizo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakimsiliza Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata watu 63 wanaozaniwa kuwa  majambazi wa kutumia silaha katika operesheni endelevu ya kuwasaka majambazi wanaofanya matukio mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kamishna wa Polisi kanda maalumu Simon Sirro aamesema, miongoni mwa majambazi waliokamatwa ni Ibrahim Juma(31) mkazi wa Kiwalani Kigilagila, Samweli Mbonea (40) Fundi gereji Mkazi wa Kiwalani pamoja na Anthony Kanywenywe (60) Mwindaji na mkazi wa Kiwalani.

Amesema majambazi hao walikutwa na taa kubwa nne za magari, pawa windo moja na nati za magari na watuhumiwa sita  kati ya waliokamatwa wamekiri kushiriki katika matukio ya unyanganyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali likiwemo la Riki Hill Hotel katikati ya jiji na Lake oil Buguruni.

Katika tukio jingine  kikosi maalumu cha kupambana na majambazi kimefanikiwa kukamata silaha sita  aina ya SMG  moja ,Short gun pump action tatu na Rifle mbili katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

amesema silaha aina ya SMG iliyokatwa kitako ilipatikana baada ya askari kuwafyatulia risasi majambazi hao waliokuwa eneo la vingunguti ndipo walipoitupa silaha hiyo ikiwa kwenye mfuko mweusi wa plastiki na wao kukimbia katika bonde la Mto Msimbazi.

“Tunaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao na upelelezi unaendelea ili kubaini mmiliki halali wa silaha hiyo hatupotayari kuendelea kuona maovu yakiendelea kufanya jeshi lipo imara na tutapambana nao,” alisema Sirro.

Ameongeza kuwa jeshi hilo pia lilifanikiwa kukamata silaha Rifle mbili katika eneo la Masaki ambazo zilikuwa zimeficha na kufunikwa kwa taulo zikiwa na maandishi ya Collessium Fitness Club  moja ikiwa na namba A 6777013 iliyosajiliwa nchini kwa namba TZCAR 58596, na nyingine ikiwa na namba L 691848176 iliyosajiliwa kwa namba TZCAR 75062.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Kanda maalum Dar es salaam limefanikiwa kukamata jumla ya risasi 15 za silaha ndogo aina ya bastola zikiwa kwenye magazine, Risasi hizo alikutwa nazo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mamboleo Willium (41) Mfanyabiashara mkazi wa Mikocheni.
Katika mahojiano mtuhumiwa huyo alikiri kuwa na risasi hizo kinyume na sheria na kushindwa kueleza mahali alipozipata, mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa  na uchunguzi unaendelea kufanyika 

TFF YAZITAKIA KILA LA KHERI AZAM, YANGA

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri klabu za Azam FC na Young Africans ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa itayochezwa wikiendi hii.

TFF imevitaka vilabu hivyo kupambana katika michezo inayowakabili na kuweza kufanya vizuri kwa kupata ushindi, ili kutengeneza mazingira mazuri katika michezo ya marudaino itakayochezwa Aprili 19-20 mwaka huu.

Young Africans wanaochezwa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Afria (CAF CL) watashuka dimbani kesho Jumamosi uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki, kucheza dhidi ya Al Ahly katika mchezo namba 89 wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CAF CL).

Mchezo huo utachezeshwa na Dennis Dembele, akisaidiwa na Marius Donatien, Moussa Bayere, mwamuzi wa akiba Tangba Kambou wote kutoka nchini Ivory Coast, huku kamisaa wa mchezo huo akiwa Celestin Ntangungira kutoka nchini Rwanda.

Jumapili katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi saa 9 kamili alasiri, Azam FC watwakua wenyeji wa Esperance Sportive de Tunis (EST) ya Tunisa katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) hatua ya 16 bora.

Waamuzi wa mchezo huo namba 75 ni Daniel Frazer Bennet, akisaidiwa na Zakhele Siwela, Thembisile Theophilus, mwamuzi wa akiba Mbongiseni Fakudze wote kutoka nchini Afrika Kusini, huku kamisaa wa mchezo akiwani Joseph Nkole kutoka nchini Zambia.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTNO WA ALAT.

$
0
0
 Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Edwin  Rutageruka wakati alipotembelea abanda la maonyesho  la TANTRADE kabla ya kufungua Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Tawala  za Mitaa (ALAT) kwetuo cha Mikutano cha Dodoma  Aprili  8, 2016.
 Wasanii wa kikundi cha Nyota cha Dodoma  wakitumbuiza katika Mkutano Mkuu Malum wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma  mjini Dodoma Aprili  8,2016. 
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa  Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma Aprili 8, 2016. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

HOSPITALI YAKABILIWA NA UHABA WA VYUMBA VYA KUHUDUMIA WAGONJWA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda akizungumza na Wagonjwa katika Hospitali ya Ngarenaro, jijini Arusha. hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa pamoja na gari la wagonjwa

Na Woinde Shizza, Arusha.

Hospitali ya Ngarenaro inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya kuhudumia wagonjwa pamoja na kukosekana kwa miundombinu imara ya maji katika chumba cha upasuaji hivyo kuhitaji upanuzi pamoja na ukarabati wa hospitali hiyo ambayo inahudumia zaidi ya Wakazi 74000 wa kata ya Ngarenaro jijini Arusha.

Akizungumzia changamoto hizo Daktari Mfawidhi wa Hospitali hiyo Josephat Kivuyo katika taarifa yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ,Kivuyo amesema kuwa hospitali hiyo inahitaji upanuzi na ukarabati ili kuweza kuboresha huduma za afya ambazo zinahitajika na wananchi wengi.

Daktari huyo Mfawidhi alisema kuwa changamoto nyingine ni uhaba wa magari ya wagonjwa maarufu kama Ambulance kwani gari lililopo ni la zamani na haliwezi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kama inavyotarajiwa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amewataka wananchi na wadau mbalimbali kuunganisha nguvu katika kuboresha huduma kwa kufanya ukarabati ambao tayari umeshaanza ili kuboresha mazingira bora kwa wananchi na wahudumu wa afya.

Pia Amewataka Wahudumu wa Afya kuepuka kutoa lugha mbaya kwa wagonjwa na kuwahudumia vizuri ili kupunguza malalamiko katika sekta ya afya ambayo inahudumia watanzania wengi.

Alisema Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ngarenaro unaendelea na tayari hivyo nguvu ya serikali n wadau wa maendeleo inahitajika katika kuhakikisha kuwa vituo hivi vinakuwa katika mazingira rafiki ya utoaji huduma za afya.

WIZARA YA ARDHI YAWASILISHA HOTUBA YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2015/16

$
0
0
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb), akitoa hotuba ya utekelezaji wa bajeti ya wizara kwa mwaka 2015/16 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2016/17 kwenye Kamati ya kudumu ya Bunge ya ardhi, Maliasili na Utalii.
 Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, wakifuatilia Hotuba ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2015/16 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2016/17 iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe. Lukuvi.  
Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara mbalimbali wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifuatilia Hotuba ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2015/16 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2016/17 iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe. Lukuvi.  

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA DUKA LA DAWA LA MSD KANDA YA MBEYA.

$
0
0
Na Rabi Hume.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amefanya uzinduzi wa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa Kanda ya Mbeya.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema uzinduzi wa duka hilo ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais Magufuli kuwatia wananchi huduma bora na kwa gharama nafuu.

“Neema hii imekuja kwa kipindi cha Rais Magufuli, sasa amekidhi matakwa na shauku ya wananchi wa Mbeya kwa kuwapa duka la dawa.

“Sera ya huduma ya afya inataka wananchi wachangie isipokuwa wazee, watoto na wajawazito na kupitia duka hili wananchi wataweza kupata dawa kwa gharama nafuu,” amesema Mhe. Mwalimu.

Duka hilo la dawa la Kanda ya Mbeya limetumia Shilingi Milioni 13 kwa ukarabati wa jingo na vifaa vyake.
Mfamasia wa Duka la Dawa, Cornel Mkeng'e akitoa maelezo kwa Ummy Mwalimu mara baada ya kuzindua duka hilo
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu akiangalia jinsi ya ufungashaji wa dawa kwenye ghala jipya la Kanda ya Mbeya.ghala hilo limelozinduliwa leo jijini Mbeya.

KESI YA BOSS WA ZAMANI WA TRA YASIKILIZWA TENA LEO

$
0
0
Kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya, akipunga mkono kwa baadhi ya wanahabari waliokuwepo kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam leo, mara baada ya kusikilizwa kwa kesi inayowakabili yeye na wenzake wawili ambao ni waliokuwa Maafisa Waandamizi wa Benki ya Stanibic Tanzania, Shose Sinare pamoja na Sioi Solomoni waliofikishwa kwenye mahakama hiyo kwa makosa manane likiwamo la kutakatisha fedha kiasi cha Dola milioni sita za Marekani.

Kesi hiyo imesikilizwa tena leo Mahakamani hapo, ambapo baada ya kusikilizwa kwa muda wa takribani masaa matatu, kesi hiyo imeahirishwa mpaka Aprili 22 itakapotajwa tena na watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
Mmoja wa watuhumiwa katika kesi ya kutakatisha fedha kiasi cha Dola milioni sita za Marekani, Shose Sinare akisindikizwa na Askari wa Jeshi la Magereza kwenda kwenye gari maalum, tayari kwa safari ya kurudishwa rumande baada ya kesho yao kusogezwa mbele.
Sioi Solomoni akijiangaa kupanga Gari hilo.

CAG aikana ‘ripoti’  ya NSSF, Asema ripoti  itatolewa na Bunge April 25

$
0
0
Na  Mwandishi Wetu

OFISI ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imekana taarifa inayosambazwa kwenye vyombo vya habari na kuonyesha kuna ufisadi mkubwa kwenye miradi mbalimbali ya Shirika la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF).

Taarifa ya kuaminika iliyopatikana ndani ya ofisi hiyo na mmoja wa viongozi wa ofisi hiyo, wameeleza kuwa taarifa kamili kuhusiana na NSSF itatolewa na bunge April 25, mwaka huu na wanashangazwa na mambo yanayoenezwa kwenye vyombo vya habari.

Kiongozi huyo mwandamizi huku akikataa kuandikwa kwa jina lake alisema hata magazeti hayo yanayoandika uvumi huo, hakuna hata moja linaloeleza kwa ufasaha kuhusiana na ripoti ya CAG.

Ilisema watanzania wanapaswa kutulia na kusubiri taarifa rasmi itakayopelekwa bungeni, kwa kuwa imeeleza kila kitu na sio hicho ambacho kinaonekana kama kinakolezwa na watu wenye maslahi nayo.

"Hata sisi tunashangazwa kumekuwa na msukumo mkubwa na hatujui dhamira yake ni nini, ila tunachoamini tusubiri tu taarifa rasmi ya ripoti itakayopelekwa bungeni,''alisema mtoa taarifa wetu.

Akizungumza na Wabunge wajumbe wa Kamati za Bunge za usimamizi wa fedha, LAAC na PAC, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Mussa Assad kwenye semina ya mafunzo aliwaeleza wabunge kuwa Ripoti ya CAG anayo yeye na Rais Magufuli tu na anashangazwa na wanaosambaza kinachoitwa taarifa ya CAG wanapata wapi nguvu ya kufanya hivyo.

Profesa Assad alikuwa anajibu maswali ya wabunge ambapo mmoja wa Wabunge kutoka Kambi ya Upinzani alitaka maelezo ya CAG kuhusu kinachoitwa ufisadi katika NSSF.

“taratibu za ukaguzi zinajulikana. Baada ya mkaguzi kuandaa taarifa ya awali hutoa kwa mkaguliwa kujibu hoja za ukaguzi. Kisha Mkaguzi huweza kuziondoa hoja zenye majibu aliyoridhika nayo na baada ya hapo huitwa kikao kinachoitwa ‘exit meeting’ na kukubaliana masuala ya ukaguzi”. Alifafanua.

Profesa Assad kwa wabunge wajumbe wa PAC,LAAC na Kamati ya Bajeti. Aliwaeleza wabunge kuwa inawezekana kinachosambazwa ni taarifa ya awali kwa malengo mahususi ambayo yeye kama CAG hawezi kuyajua na kuwataka wabunge wasubiri taarifa yake rasmi itakayowasilishwa Bungeni kabla ya tarehe 25 Aprili 2016.

Kumekuwepo na taarifa mbalimbali, ambazo nyingi zinaonekana zinamtuhumu aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau aliyeliendesha shirika hilo kwa mafanikio makubwa kuhusishwa na vitendo vya ufisadi wa miradi mbalimbali.

Baadhi ya wachunguzi wa mambo wanasema nguvu inayosukumwa kuichafua NSSF ina lengo la kufifisha nyota ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo kabla ya uzinduzi wa daraja la Kigamboni mnamo tarehe 16 Aprili 2016.

SPAIN ACCREDITS ENVOY TO EAC BLOC

$
0
0
East African Community Headquarters, Arusha, 8th April , 2016: The government of Spain has accredited its Ambassador to the United Republic of Tanzania, Mr. Felix Costales Artieda, to also serve as Ambassador to the East African Community. His Excellency Felix Costales Artieda today presented accreditation letter to the Secretary General of the East African Community, Amb. Dr. Richard Sezibera.

Amb. Felix Artieda informed the Secretary General that his government attaches great importance to regional economic groupings such as the EAC and congratulated the EAC Secretary General for the wonderful regional initiative. “Count on Spain’s support because the goals of the Community are excellent for the prosperity of the people in the region”, asserted the Spain Envoy, adding that “regional integration initiatives take time but you need to continue so as to build a strong and powerful bloc”.

While receiving the Spain Envoy, the Secretary General of the East African Community, Amb. Dr. Richard Sezibera hailed the existing cordial relations between the EAC and Spain. The Secretary General welcomed the support from Spain Government geared towards enabling the Community to achieve its ambitious agenda.

Dr Sezibera briefed him on the progress being registered by the Community so far that include implementation of Protocols on the Customs Union, Common Market and East African Monetary Union .

Meanwhile, earlier today, the EAC Secretary General met the Ambassador of the People’s Republic of China, H.E Mr. Lv Youqing for bilateral discussion. The two parties deliberated on a number of areas that offer the potential for collaboration between EAC and China including the cooperation in aviation and trade sectors.

The EAC Secretary General appreciated the Chinese for their role in infrastructure development in the EAC Partner States and specifically for their support to the Secretariat.

In his part the Chinese Ambassador Extra-ordinary and Plenipotentiary to Tanzania, commended the Secretariat for a role playing in promoting regional cooperation and integration.
Dr Sezibera briefs Spain Amb. Mr. Felix Costales Artieda on the progress being registered by the Community.
Secretary General of the East African Community, Amb. Dr. Richard Sezibera receives letter of accreditation from Spain Ambassador Mr. Felix Costales Artieda.
Ambassador of the People’s Republic of China, H.E Mr. Lv Youqing and the Secretary General of the East African Community, Amb. Dr. Richard Sezibera shake hands after the successful bilateral discussion.

INTRODUCING NEW SONG: FOREVER BYA CHEMICAL

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI WASHIRIKI KUTOA MADA KATIKA MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA (ALAT) UNAOFANYIKA DODOMA.

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu  wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, WCF,  Bw. Masha Mshomba, (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Juu ya Huduma na Mafao yatakayotolewa na Mfuko hususani fidia ya muda mfupi na fidia ya kudumu kwa Wanyakazi wa Sekta Binafsi na Umma watakaopata ajali na kuumia, kuugua ama kufariki kutoka na kazi. Awali Bw. Mshomba  alipata fursa ya kutoa mada kwa wajumbe wa ALAT, kutoka mikoa mbalimbali kuhusu huduma za Mfuko huo. Katikati ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (TAMISEMI), Suleiman Jaffo.

 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba akiwasilisha mada.
 Baadhi ya wajumbe wa ALAT na wageni waalikwa.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Serikali yaitaka Yanga kufanya uchaguzi haraka iwezekanavyo

$
0
0
WIZARI ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imeandikia barua klabu ya Yanga kuiagiza iwe imekwishafanya uchaguzi wake hadi kufika Aprili 15, mwaka huu. Yanga imekwishapokea barua hiyo kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wakisistizwa hilo ni agizo la Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye.

Pamoja na kwamba wapo kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kesho dhidi ya Al Ahly, lakini tayari Yanga wameanza kulifanyia kazi agizo la Serikali na wakati wowote wanaweza kutangaza uchaguzi.

Lakini kuna wasiwasi kama uchaguzi unaweza kuwa umefanyika hadi Aprili 15, kwa sababu muda waliopewa ni mfupi mno kukamilisha taratibu.

Yanga inapaswa kuutangaza japo kwa wiki moja uchaguzi, kugawa fomu kwa wagombea japo kwa wiki moja pia, na baada ya hapo ipatikane angalau wiki moja nyingine kwa ajili ya usaili, mapingamizi kabla ya kupiga kura kuchagua viongozi.

Yanga kwa sasa ipo chini ya uongozi ambao umekwishamaliza muda wake, chini ya Mwenyekiti Yussuf Manji na Makamu, Clement Sanga. Manji na Sanga waliingia madarakani Julai 15, mwaka 2012 katika uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi za viongozi waliojiuzulu akiwemo Mwenyekiti Wakili Lloyd Nchunga na Makamu wake, Davis Mosha.

Walichaguliwa pamoja na Wajumbe Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na Geroge Manyama ambao waliungana na Wajumbe waliobaki, akiwemo Salum Rupia na Mohammed Binda. Hata hivyo, baada ya uongozi huo kumaliza muda wake mwaka 2014, Manji akaunda Kamati ya Muda, yeye na Sanga wakiendelea na nyadhifa zao.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

Jeshi la wananchi watanzania JWTZ kwa kushirikiana na umoja wa mataifa limesema litafanya uchunguzi dhidi ya wanajeshi wa Tanzania wanaodaiwa kufanya vitendo vya unyanyasaji nchini Congo. https://youtu.be/kndyFLxcAVE
Polisi kanda maalum ya Dar es salaam yawakata watuhumiwa 63 wa ujambazi na silaha 6. https://youtu.be/cM2nxpweQF4

Serikali imetenga kiasi cha zaidi ya shilingi trilioni moja kwa ajili ya kuongeza kasi ya uboreshaji wa sekta ya usafiri wa reli na anga katika juhudi za kukuza uchumi wa nchi.https://youtu.be/_3LKRnzdAos

Waziri wa nishati na madini Prof. Muhongo atoa agizo kwaa wafanyakazi wote wa wizara ya nishati na madini walio na vitalu vya madini kuchagua moja kati  ya kuendelea kuajiriwa na kuacha vitalu vya madini au waache kazi waendelee na vitalu vya madini. https://youtu.be/vWLL61BECXY

Wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na vitendo yasema itaendelea kutekeleza agizo la Rais Magufuli la kufungua maduka ya dawa katika kila makao makuu ya mkoa ili kurahisha upatikanaji wa dawa kwa wananchi katika hospitali mbalimbali. https://youtu.be/qRfuWiwHGKI

Moto mkubwa wateketeza mabweni ya shule ya sekondari Soni Day wilayani Lushoto na kusababisha hasara ya takribani milioni 167. https://youtu.be/26_sGAvrZXo

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam yawatia mbaroni watuhumiwa 63 wa ujambazi huku pia likikamata silaha 6 katika msako maalum.https://youtu.be/6GbQSYE_Tgs

Waziri mkuu Kassim Majaliwa azitaka jumiya za serikali za mitaa nchini ALAT kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kupambana na rushwa na uvujaji wa mapato. https://youtu.be/K_g7rz1YacY

Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania JWTZ, laeza kushitushwa na taarifa za kulituhumu jeshi hilo juu ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wananchi wa Congo huku liki ahidi kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kali. https://youtu.be/tC8hmY2qW_0

Nyumba zaidi ya 12 zimeanguka kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Tabora na kusababisha kaya kadhaa kukosa makazi. https://youtu.be/kqql6EYVt3c

Serikali yasema bajeti ya dawa kwa mwaka ujao wa fedha 2016/2017 itakuwa ni zaidi ya mara 3 ya bajeti ya mwaka uliopita ili kuondoa tatizo la dawa na vifaa tiba katika hospitali, vituo vya afya na zahanati nchini. https://youtu.be/Dn--9A4BWXQ 

Hatimae ofisi ya madini ya mkoa wa Geita yaufungua mgodi wa Mgusu baada kufungwa hapo awali kwa takribani mwezi 1 kufuatia vifo vya watu 5.https://youtu.be/apX7zOr80PI

MCHEZAJI KANU WA NIGERIA AMBAYE NI BALOZI WA KAMPUNI YA STARTIMES ATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WA SHULE YA MSINGI YA MAJI MATITU MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maji Matitu Bw.  Abdul Mgomi akimkaribisha mchezaji huyo shuleni hapo. Kutoka kulia ni Mwalimu Shabani Msabaha wa shule hiyo, Mchezaji Kanu na Makamu Rais wa Kampuni ya StarTimes, Zuhura Hanif.
Mchezaji Kanu akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kukabidhi msaada huo.
Hapa Kanu akimkabidhi msaada wa sabuni ya unga Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi.
Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Kanu akitoa msaada wa magodoro.

DIRA YA DUNIA IJUMAA 8/4/16


EAC TO SUPPORT LIQUID TELECOM GROUP INITIATIVE

$
0
0
The Secretary General of the East African Community; Amb. Dr. Richard Sezibera today received Mr. Sam Nkusi; Group Executive of Liquid Telecom; the leading independent data, voice and IP provider in Eastern, Central and Southern Africa. The Secretary General, who was accompanied by Eng. Robert Achieng; EAC Senior Engineer in charge of Planning and Communications, warmly welcomed the Liquid Telecom Group Executive to the EAC Headquarters. 
Mr. Nkusi briefed Amb. Sezibera on the operations of Liquid Telecom and said the company was embarking on a project to build a new submarine cable infrastructure that will provide a cost-effective and reliable link for landlocked, southern, central and east African countries to the Internet and to the world. 
“Leveraging Liquid Telecom's 20,000km-long fibre optic terrestrial network, this pan-African private sector project will support fast growing needs for Internet connectivity and help Africa’s Information Communication Technology (ICT) sector leapfrog towards achieving its Sustainable Development Goals” noted the Liquid Telecom CEO.

Mr. Nkusi reiterated that the cable, running along the East coast of Africa and into the Red Sea, will take a less congested route to Europe, and will interconnect with all existing networks and with other international submarine cables. According to Liquid Telecom, this will also address the need for mobile operators to increase internet speed delivered over their mobile broadband networks. 
He said the project was a major step towards fulfilling EAC’s mission to widen and deepen Economic, Political, Social and Cultural integration in order to improve the quality of life of the people of East Africa. 
The Secretary General hailed the private sector-led initiative and affirmed the Secretariat and the Community’s support to the project and urged Partner States to support the project. He noted that the biggest support EAC could provide towards the overall implementation of the project would be to provide a Cross-Border Inter-Connectivity Regulatory Framework in order to guide and facilitate inter-connections across borders within the EAC, and could .possibly be shared with other regional economic blocks in Africa.


NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: Si ulinikataa - Q chief

FOR SALE Jipatie Tyre Changer, Wheel Balancer na Compressor kwa bei nafuu

$
0
0

 TSH 6.5 MILLION kwa full set. used kutoka UK lakini vipo katika hali nzuri. vipo Dar es Salaam. Tunazo rangi tofauti jipatiye kabla hazijaisha.

Mawasiliano: +255788741125
                      +255718030320
                      +255717669548



WAZIRI UMMY MWALIMU ALIPOKUTANA NA WADAU WA AFYA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA

$
0
0
Na Catherine Sungura, Mbeya

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mhe. Ummy Mwalimu amefanya ziara katika hospitali zilizopo Mbeya na kuzitaka hospitali zinazotumia mfumo wa ukusanyaji mapato wa kieletroniki wasibweteke na mapato wanayoyakusanya kila siku.

Rai hiyo imetolewa na aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali ya rufaa ya kanda ya mjini Mbeya.

Ummy alisema ukusanyaji wa mapato kwa mfumo huu unasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo ununuzi wa dawa, vifaa na vifaa tiba pamoja na utoaji wa motisha kwa watumishi.

"Bado tunatambua hali ya uhaba wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kuanzia ngazi zote, tukiweza kusimamia vizuri hili tutafanikiwa," alisema.

Aidha alisema wanatarajia katika serikali ya awamu hii bajeti ya dawa itaongezeka zaidi ya mara tatu kulinganisha na bajeti za nyuma, hivyo wameishauri Bohari Kuu ya Dawa (MSD) wanunue dawa toka kwa wawekezaji wa hapa nchini ambapo itakua na bei nafuu na itaongeza tija na upatikanaji wa dawa kwa haraka.

Waziri Ummy Mwalimu aliutaka Mkoa kufuatilia, kuwafichua na kuwachukulia hatua wale wote watakaojihusisha na wizi wa dawa.

"Tunao watumishi wachache wa afya ambao wanahujumu na kuiba dawa na kuzipeleka kwenye maduka ya dawa binafsi, hao hatutowafumbia macho na kuwapeleka mahakamani"

Kuhusu upungufu wa watumishi wa kada ya afya nchini, Waziri wa afya alisema, nchi ina upungufu wa asilimia 52, hivyo serikali inatarajia kuajiri watumishi takribani elfu kumi hivi karibuni ambao watatawanywa nchi nzima ikiwemo mikoa iliyo pembezoni.

Katika hospitali ya uzazi ya Meta, waziri huyo ameguswa na ufinyu wa wodi za wazazi na kupelekea mama wajawazito na waliojifungua kulala chini na wawili wawili kwenye kitanda kimoja na hivyo kuwataka kufanya haraka ujenzi wa jengo jipya litakaloondoa mrundikano wa mama wajawazito na watoto njiti.

Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya inakusanya kwa mwezi kiasi cha shilingi Milioni mia tano na pia inahudumia mikoa saba nchini na kuhudumia zaidi ya watu milioni mbili.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisalimia na watumishi mara alipofika kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mbeya.
Waziri Ummy akimsalimia mtoto Jenifer Joel (9) mkazi wa Chunya aliyelazwa hospitalini hapo.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA TRA YAENDELEZA ZOEZI LA KUBOMOA MTANDAO WA WAFANYA BIASHARA YA MAGENDO UKANDA WA KUSINI MWA PWANI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu-Kilwa.

Siku ya tarehe 6/4/2016 maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kikosi cha (FAST)  wakiwa na maofisa wa Polisi walifanya upekuzi kwa lengo la kutafuta magendo kwenye nyumba ya mfanyabiashara Yusuf Barkat Sareh.

Upekuzi huo ulifanyika baada ya kupata taarifa za kiintelijensia zilizofanyiwa kazi muda mrefu.

Bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi zilikamatwa kama zifuatazo
Sukari ya India kilo 50 jumla mifuko762Sukari ya nje iliyokamatwa kwenye mifuko ya viwanda vya hapa nchini kilo 25 jumla mifuko 135,Mafuta ya kula lita ishirini (20) aina mbalimbali kutoka nje jumla madumu 49,Betri aina ya tigger katoni 223,Amira katoni 135,Sabuni za kufulia katoni 48

Vitu mbalimbali vilivyokamatwa kama ushahidi wa biashara haramu ya magendo ya sukari.Mashine mbili (2) za kushonea kwenye mifuko ya iliyowekwa sukari inatoka nje ya nchi na kuwekwa kwenye mifuko ya viwanda vya nchini nya sukari vya Kilombero,TPC na Mtibwa Sugar.
Mifuko mitupu mipya ya sukari kilo 25 toka India  2000
Mifuko iliyotumika ya kilo 50 mitupu ya sukari36,000
mifuko ya sukari iliyotumika ya Viwanda vya Tanzania ya kilo25 kiasi cha 1150
Madumu mafuta ya nje mchanganyiko ya kula lita 20 kiasi cha 609
Madumu matupu ya lita 10 ya nje kiasi cha 310.
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayomboakionesha ndoo zinazotarajiwa kuwekwa mafuta.
Sukari na viroba vya kuweka kwa matayarisho ya kuingizwa sokoni.
Hii ni Sukari iliyomwangwa chini kabla ya kuwekwa kwenye viroba
Askari wakisimamia zoezi la kuvunja mlango
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Richard Kayombo akizungumza na waandishi.

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images