Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1177 | 1178 | (Page 1179) | 1180 | 1181 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiweka shada la mauwa katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume baada ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli,kuweka Shada la mauwa katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume baada  ya kumalizika kisomo cha Hitma na dua ya kumuombea, iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli,(wa pili kulia) pamoja na Viongozi mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa.
  Viongozi mbali mbali wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa.
  Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanawema Shein (kushoto) Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume,Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Mama Shadya Karume,Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi pamoja wake wa Viongozi wakiitikia dua iliyoombwa baada hitma na uwekaji wa mashada ya mauwa leo katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume pembeni kwa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipozikwa.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (katikati) akikagua mikondo mikubwa inayotiririsha maji ya mvua kwa wingi kwenye miundombinu ya reli eneo la Gulwe na kusababisha eneo hilo kushindwa kupitika na Treni baada ya kufukiwa na udongo Jana, Mkuu wa Mkoa na timu aliyoambatana nayo walibaini uchimbavu wa mabwawa makubwa ya uvunaji maji ya mvua utasaidia kuondoa athari hizo za mvua.
  Mikondo mikubwa inayotiririsha maji ya mvua kwa wingi kwenye miundombinu ya reli eneo la Gulwe na kusababisha eneo hilo kushindwa kupitika na Treni baada ya kufukiwa na udongo jana.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (katikati) akikagua miundombinu ya reli eneo la Gulwe iliyofunikwa na udongo ulioletwa na mafuriko na kusababisha eneo hilo kushindwa kupitika na Treni, Tayari mafundi wa TRL wameanza kazi ya kufukua njia hiyo ya Reli.
  Mafundi wa TRL wakitoa udongo kwenye miundombinu ya reli eneo la Gulwe iliyofunikwa na udongo ulioletwa na mafuriko na kusababisha eneo hilo kushindwa kupitika na Treni.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (katikati) akifanya majumuisho ya ziara yake ya kukagua miundombinu ya reli eneo la Gulwe iliyofunikwa na udongo ulioletwa na mafuriko na kusababisha eneo hilo kushindwa kupitika na Treni, Tayari mafundi wa TRL wameanza kazi ya kufukua njia hiyo ya Reli.

  0 0


  Mchezaji nguli wa kikosi cha Nigeria au Super Eagles na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu (kulia),akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la Kampuni ya StarTimes lililopo jengo la Mkuki Mall Barabara ya Nyerere Dar es Salaam leo mchana. Mchezaji huyo yupo nchini kwa ziara ya siku tano. Kulia kwake ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao.

  Na Dotto Mwaibale

  Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles) na Arsenal ya Uingereza, Nwankwo Kanu ameshiriki katika uzinduzi wa duka jipya la kampuni ya StarTimes Tanzania lililopo katika jengo la Mkuki Mall jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mchezaji Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika ambapo inafanya shughuli zake katika nchi zaidi ya 10 amesema kuwa anajisikia mwenye furaha kuwepo nchini na atashiriki shughuli mbalimbali za kampuni pamoja na za kijamii.

  “Ni mara ya kwanza mimi kuwepo nchini Tanzania, nashukuru nimefika salama na kupokelewa kwa ukarimu mkubwa, kwa kweli sikutarajia. Uwepo wangu hapa ninaiwakalisha kampuni ya StarTimes barani Afrika kama balozi wao na kama balozi ninao wajibu wa kufika kila nchi ambayo kampuni hii ipo. Kwa namna nilivyopokelewa ninaamini kuwa kweli StarTimes ni kampuni kubwa, inapendwa na kujulikana miongoni mwa watanzania wote.” Alielezea Bw. Kanu

  “StarTimes wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kuwa wateja wake wote wanafurahia huduma za matangazo ya dijitali kwa ubora wa hali ya juu na gharama nafuu. Na hii ni kutokana na falsafa iliyojiwekea kampuni ya kutaka kuhakikisha kuwa kila nyumba ya muafrika inafikiwa na matangazo hayo. Changamoto ni nyingi katika uendeshaji na utoaji huduma za kidijitali lakini kampuni imejizatiti kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika uboreshaji wa vipindi na chaneli zake. Kwa mfano kwa sasa kama mnavyoweza kushuhudia kuwa ligi kubwa barani Ulaya za Bundesliga na Serie A za nchini Ujerumani na Italia zinaonyeshwa moja kwa moja kupitia StarTimes Pekee.” Aliongezea Kanu.

  “Michezo na burudani ni maudhui muhimu sana ambayo lazima yawekewe mkazo kwani ndivyo vitu vinavyopendwa na kuwavutia wateja wengi hivyo haina budi kuweka mkazo. Ninaamini kuwa uwepo wangu nchini Tanzania utasaidia kwa kukaa chini na uongozi wa kampuni nchini na kuweza kuona wanawaongezea na kuwapatia nini wateja wao. Ninatumaini ninacho cha kuongezea kwa nilichojifunza kutoka nchi kama za Uganda na Kenya ambazo nimetokea huko pia,” alisema na kumalizia Kanu kuwa, “Nashukuru kuwepo Tanzania na ninaamini nitajifunza na kushirikiana kwa mengi kwa kipindi nitakachokuwepo mpaka kuondoka kwangu.”

  Naye kwa upande wake akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya ambalo litakuwa ni la saba kwa mkoa wa Dar es Salaam pekee, Mkurugenzi wa Uendeshaji (Operesheni) wa StarTimes Tanzania, Bw. Carter amebainisha kuwa duka hilo jipya litawarahishia wateja wote wanao kama maeneo ya jirani kama vile Tandika, Mbagala, Temeke, Kurasini, Yombo, Kiwalani, Vingunguti na kwengineko kujipatia huduma na bidhaa kwa urahisi zaidi.

  “Leo tunayo furaha kubwa kufungua duka hili jipya ambalo katika kumbukumbu litakuwa limezinduliwa na balozi wetu barani Afrika, Nwanko Kanu. Duka hili litakuwa msaada mkubwa kwa wateja walio maeneo ya jirani na kwingineko na ningependa kuwatoa wasiwasi kuwa litakuwa linatoa huduma zenye ubora sawa na maduka yetu yote hivyo wasiwe na wasiwasi. Ninawaomba wateja wetu watembelee hapa kujipatia huduma kama vile kununua visimbuzi, antena na kebo, vocha za malipo ya mwezi pamoja na huduma kwa wateja.” Alimalizia Bw. Carter.

  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame wakiwasili katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 22 ya mauaji hayo yaliyotokea mwaka 1994 ambapo watu takribani milioni 1,000,000 waliuawa.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishuhudia  wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame pamoja na binti yao wakiweka shada la maua katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Rais Paul Kagame kwa pamoja wakiwasha "Urumuri Rutazima" (Mwenge/mwali wa Matumaini)  katika maadhimisho Kumbukumbu ya miaka  22 ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange huku Inspekta jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu akisubiri zamu yake  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Msajili wa vyama vya Siasa Mhe Jaji Francis Mutungi mara baada ya kutua  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea nchini Rwanda alikokuwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili leo Alhamisi April 7, 2016. 

  0 0

  Naibu Waziri Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura (kulia) akipokea moja ya kazi ya Kikundi cha Albino Revolution Culture Troup kutoka kwa Mkurugenzi wa kikundi hicho Bw. Titto Mtanga wakati walipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili walemavu katika kutekeleza majukumu yao ya kisanaa.
  Naibu Waziri Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura (kulia) akiongea na wasanii wa kikundi cha sanaa na utamaduni cha Albino Revolution Troup kutoka Wilayani Temeke walipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili walemavu katika kutekeleza majukumu yao ya kisanaa, kulia kwa naibu waziri ni Mkurugenzi wa kikundi hicho Bw. Titto Mtanga.

  0 0

  Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati) akipiga picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF ( Universal Communications Services Access Funds ) na kushirikisha wasichana 240 hapa nchini, na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu, Airtel ni mdhamini wa mashindano hayo . Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam
  Mwanafunzi Elisia Yohana (kulia) wa shule ya sekondari Nyankumbu iliyopo Geita akielezea jinsi program ya kikundi chao jinsi itakavyokuwa inafanyakazi katika mashindano ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF ( Universal Communications Services Access Funds ) na kushirikisha wasichana 240 hapa nchini na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu, Airtel ni mdhamini wa mashindano hayo. Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam.
  Afisa Mtendaji mkuu wa mfuko wa Mawasiliano kwa wote (Universal Communications Services Access Funds) UCAF, Eng. Peter Ulanga (aliyesimama) akiongea na wanafunzi katika mashindano ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF na kudhaminiwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel na kushirikisha wasichana 240 hapa nchini na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu. Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam.
  Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia wizara ya elimu, sayansi, teknolojia na ufundi, Prof. Evelyne Mbede (kushoto) akiongea na wanafunzi wa kidato cha tatu katika mashindano ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF ( Universal Communications Services Access Funds ) na kushirikisha wasichana 240 hapa nchini na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu, Airtel ni mdhamini wa mashindano hayo . Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam.
  Mkurugenzi wa Elimu ya sekondari, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali- Zanzibar bi Asya Iddi (kushoto) akikabidi cheti kwa Aines Mtani (wa tatu kulia) kama mmoja wa washiriki katika mashindano ya ya ICT kwa wasichana wa kidato cha tatu hapa nchini yaliyoandaliwa na UCAF ( Universal Communications Services Access Funds ) na kushirikisha wasichana 240 hapa nchini na kupata washindi sita watakaoenda kushiriki nchini Ethiopia mwishoni mwa mwezi huu, Airtel ni mdhamini wa mashindano hayo . Hafla hiyo ya kupata washindi hao sita ilifanyika hapo jana katika ukumbi wa Buni Innovation Hub uliopo katika ofisi za COSTECH, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam

  0 0
 • 04/08/16--01:58: BEI YA MADAFU LEO.


 • 0 0

  Mratibu wa tamasha la Pop Up Bongo, Natasha Stambuli (kulia) akinunua bidhaa za duka la Chasing Faboulous wakati wa tamasha hilo, anaemuuzia ni Groria Mwakasole na wa katikati ni Victoria Martin wamiliki wa duka hilo.
  Mmiliki wa duka beauty heaven Tanzania Winfrida Mgongolwa (kulia) akiwaonesha wateja waliotembelea eneop la duka lake katika tanmasha la biashara la Pop Up Bongo lililofanyika Masaki juzi katika mgahawa wa Tuk Tuk Thai.
   Bidhaa kama hizi zilizotengenezwa kwa mbao zilikuwapo pia 

  Na Mwandishi Wetu 
  MAMIA ya vijana walijitokeza juzi katika tamasha la biashara lililohusisha burudani ya muziki la Pop Up Bongo na kununua bidhaa mbalimbali.


  Tamasha hilo la saba kufanyika kwa mwaka huu limefanyikia katika mgahawa wa Tuk Tuk Thai uliopo Masaki na kupambwa na burudani kutoka kwa Dj D Ommy.

  Akizungumzia tamasha hilo, mratibu wake, Natasha Stambuli alisema kuwa wabunifu wa ndani wengi wamejitokesha kushiriki tamasha hilo.  Alisema kuwa vijana wengi wamekuwa na hamasa ya kubuni bidhaa zao wenyewe na kuziuza hasa wakihusisha zaidi nakshi za kiasili katika kupendezesha bidhaa hizo.

  Alisema kuwa kutokana na mwamko huo tamasha hilo limewakutanisha wajasiriamali hao pamoja na wanunuzi kwa maana ya wateja ili wawaunge mkono.

  Alisema kuwa bidhaa kama vile nguo, viatu vidani na bidha nyingine vimeuzwa katika tamasha hilo.
  Alisema “kwa awamu hii ambayo ni ya saba tukiwa bado na mdhamini wetu kinywaji cha Smirnoff watu wengi wamejitokeza na kupata huduma kadhaa ambapo wamekuwa wakinunua bidhaa huku wakipata burudani ya muziki”.

  Kwa upande wake Meneja wa vinywaji vikali kutokea, Serengeti Breweries Limited (SBL) Shomari Shija alisema kuwa kampuni hiyo kupitia kinywaji chake cha Smirnoff imeamua kudhamini tamasha hilo kwa kuwa inatambua mchango wa ujasiriamali katika maendeoleo.

  Mmoja kati ya wajasiliamali walioshiriki katika tamasha hilo, Sackry Papillon wa huduma ya mwili, The Ryb Spa iliyopo Kijitonyama alisema kuwa tanmasha hilo limemkutanisha na wadau mbalimbali hasa vijana wanaopenda huduma hiyo.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhungo akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini na kufungua baraza la wafanyakazi wa wizara yake katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
  Mwenyekiti wa Baraza la wafanyazaki wa wizara ya Nishati na Madini, Selina Msumbushi akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini na kusoma mapendekezo ya wafanyakazi hao leo katika mkutano wa kufungua baraza la wafanyakazi uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa wizara ya Nishati na Madini wakiimba wimbo wa Solidarity leo katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo wakati wa ufungunzi wa Baraza la wafanyakazi jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  WAZIRI wa Nishati na Madini, Mhe. Sospeter Muhongo amelishauri Baraza la Wafanyakazi wa Nishati na Madini kujikita katika kujadili mwelekeo wa mapinduzi ya kiuchumi kwa kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye viwanda.

  Mhe. Muhongo ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, ambapo baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni masuala ya usafiri kwa wafanyakazi wa wizara hiyo, upandishwaji vyeo kwa wafanyakazi, mafunzo pamoja na uhaba wa nafasi wa ofisi kwa wafanyakazi.

  Kuhusu suala la upandishwaji vyeo, Mhe. Muhongo amesema kuwa tayari yeye kama Waziri alishafanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ili kuona namna gani wafanyakazi wanapandishwa vyeo kulingana na elimu pamoja uwezo wao kikazi ambapo alipendekeza kubadili mtindo wa upandishwaji vyeo uliopo sasa kwani ni wa zamani.

  ‘’Sifa za upandishaji vyeo kwa wafanyakzi ni vema ukabadilika pamoja na muda wa utoaji vyeo, hivyo napenda kuwasisitiza kuwaangalia vijana tulio nao kwani pale Wizarani tuna vijana wengi wazuri wenye uwezo mkubwa katika kufanya kazi. Katika kikao hiki ni vema mkajadili namna gani mnawapa kipaumbele vijana katika kuwapandisha vyeo vijana hawa,’’ alisema Muhongo.

  Kuhusiana na uhaba wa nafasi za ofisi, Mhe. Muhongo alifafanua kuwa, ofisi nyingi za Serikali ziko katika mfumo wa zamani, hivyo amelishauri Baraza hilo kuona namna gani watabadilisha muundo wa ofisi ili watu wakae pamoja katika eneo moja lililo wazi na kufanya kazi kuliko kila mtu kuwa na sehemu yake ya kufanyia kazi hali inayosababisha ufinyu wa eneo na uvivu.

  Aidha, Amewataka wajumbe wa Baraza hilo kujadili ni namna gani wanaweza kubadilisha hali ya kiuchumi toka asilimia 7% hadi kufikia asilimia 8% mpaka 10% ili kukuza uchumi wa nchi na kutokomeza umasikini.

  ‘’Jukumu kubwa la Wizara ya Nishati na Madini ni kuhakikisha kuwa tunakuza uchumi wa nchi kwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na umeme mwingi wa bei nafuu na wa uhakika, na kazi tuliyonayo hapa ni kuongeza uzalishaji wa umeme toka Megawati 1400 hadi kufikia Megawati 5,000 mpaka 10,000 na ikiwezekana hadi 15,000 baada ya miaka 10 ijayo’’, aliongeza Mhe. Mhongo.

  Kuhusu suala la Mafunzo kwa wafanyakazi hao, Mhe. Muhongo amesisitiza kuwa hakuna mtu anayekatazwa kupatiwa mafunzo kwa maana ya kuongeza elimu juu ya jambo fulani, isipokuwa kuna utaratibu wa kwenda kusoma, ambapo panapotokea umuhimu wa wafanyakazi kwenda kusomea mambo muhimu yenye manufaa kwa umma nafasi hizo ni vema zikatolewa ili nchi iwe na wataalam mbalimbali katika nyanja mbalimbali.

  ‘’Hii Wizara inahitaji watu wasome na waelimike, hivyo tunahitaji watu wasome na wawe wataalam katika maeneo mbalimbali ya kazi lengo likiwa ni kuleta maendeleo ya nchi’’, Alisema Mhe. Muhongo.


  Amegusia masuala ya Bajeti katika Wizara yake ambapo amefafanua kuwa zaidi ya asilimia 89.5/% ya bajeti itatumika katika kufanya shughuli za maendeleo ya nchi.

  0 0


  Mbunge wa jimbo la Nyamagama,jijini Mwanza pichani akifurahia mara baada ya kutangazwa mshindi wa jimbo hilo na Mahakama kuu ya jijini Mwanza dhidi ya aliyekuwa Mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha CHADEMA,Mh.Ezekiel Wenje.

  Kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Nyamagana iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje (CHADEMA) dhidi ya Mbunge wa sasa wa Nyamagana Stanslaus Mabula (CCM) ilikuwa ikiendelea katika mahakama Kuu Mwanza ambapo Ezekiel Wenje alifungua kesi hiyo akipinga matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yakimpa ushindi Mbunge wa sasa, Stanslaus Mabula. 

  Leo April 8 2016, maamuzi ya kesi hiyo yametangazwa rasmi ambapo Mbunge Stanslaus Mabula ameshinda kesi hiyo, baada ya kubainika upande wa madai hauna ushahidi unaokidhi, kuithibitishia mahakama.

  Sikiliza Sauti ya Mbunge wa Nyamagana  Mh.Stanslaus Mabula akizungumza na Wanannchi mara baada ya Uamuzi wa Mahakama kutolewa leo,ambapo yeye ameibuka mshindi dhidi ya aliyekuwa Mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha CHADEMA,Mh.Ezekiel Wenje. 


   Wananchi wakifurahia ushindi wa Mbunge wa CCM Mh .Mh.Stanslaus Mabula.


  0 0

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha Mauzo  
  na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh 

  Watanzania zaidi ya 1,000 mwaka huu  wanategemea kujipatia ajira kupitia kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kuanzia mwezi huu  itakapoanza kufungua vituo vidogo vya kutoa huduma zake mbalimbali muhimu vipatavyo 500 nchini kote ambako vituo 200 vitafunguliwa kati ya mwezi huu hadi mwezi Juni.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha Mauzo  na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh amesema  kuwa mkakati huu wa kufungua vituo kwa kila umbali wa kilometa 10 kwenye maeneo yenye wakazi wengi kama vile kwenye miji midogo wilayani na kwenye makambi ya jeshi kwa ajili ya kutoa huduma za Vodacom umebuniwa ili kuwapunguzia wateja adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kuzipata.
  Baadhi ya sehemu ambazo vituo hivyo vitafunguliwa alivitaja kuwa ni Mbaba Bay mkoani Ruvuma,Inyonga wilayani Mpanda,Pemba,Handeni,Uvinza,Karagwe,Tarime na  wilayani Chunya mkoani Mbeya.
   “Kwetu Vodacom wateja wetu ni wafalme na tunasikiliza ushauri wao,pamoja na kuwa na maduka sehemu mbalimbali lakini bado tumeona kuna haja ya kuwasogezea zaidi huduma wateja  popote pale walipo na kwa wakati wowote”.Alisema.
   Aliongeza kuwa  kupitia huduma hii ya  vituo vya mauzo kampuni itazidi kupanua wigo wa ajira nchini kwa kuwa  vitahitaji wafanyakazi wa kuviendesha na watanzania zaidi ya 1,000 watanufaika na mpango huu .
   alizitaja baadhi ya huduma mbalimbali zitakazotolewa  katika vituo hivyo ni kuwaunganisha wateja na mtandao wa Vodacom,M-Pesa,kuuza simu, “Wateja wetu pia watapata fursa ya kupata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni kupitia kwenye vituo hivi”.Alisema
  Alitoa wito kwa  wateja wa Vodacom  na wananchi kwa ujumla kutumia huduma hizi ili waondokane na usumbufu na kuongeza kuwa  kampuni ya Vodacom itazidi kubuni huduma mbalimbali za kuboresha maisha ya wananchi na kuwarahisishia kupata mawasiliano.

  “Vodacom imedhamiria kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa teknolojia na kuwawezesha kupata mawasiliano kwa urahisi na kuanzishwa kwa huduma hii ni ushuhuda kuwa sasa huduma zake zinazidi kuwafuata wananchi popote walipo”.

  0 0


  IDARA ya Uhandisi ya Shirika la Ndege la Etihad itakuwa mwenyeji na mdhamini wa mkutano ujao wa uhandisi na ukarabati wa ndege wa mtandao wa MRO uliopo Mashariki ya Kati, Mkutano huo unaotazamiwa kufanyika mjini Abu Dhabi mwezi Aprili 26-27, 2016. Mjadala mkuu utakuwa juu ya ukuaji wa mtandao wa  MRO wenye historia isiyopungua miaka 20, wenye wadau katika sekta za – Ndege, MROs, OEMS na Wauzaji – kuwaleta pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya kimasoko.


  Mada mbalimbali kama maendeleo katika masoko ya usafiri wa anga huko mashariki ya  Kati, sekta ya utabiri wa masoko ya MRO pamoja na jinsi mashirika ya ndege yanajenga mahusiano na wadau wengine wa MRO.

  Miongoni mwa wazungumzaji sekta inayoongoza ni Jeff Wilkinson, Makamu wa Rais shirika la ndege la Etihad kwa upande wa Ufundi alisema: " Ni furaha yetu kuwa mwenyeji wa wajumbe wa uhandisi na ukarabati wa ndege hapa mjini Abu Dhabi – kitovu kipya cha masuala ya teknolojia ya anga na usafiri kanda ya mashariki ya Kati”

  Ikiwa ni mwaka mmoja tangu kufanikisha maonyesho mengine kama haya, idara ya uhandisi ya Shirika la ndege la Etihad kwa mara nyingine tena itatoa ziara ya kituo chake kwa wajumbe baada ya kuhitimisha mkutano huo, hivyo kuwapa fursa wajumbe kukutana na timu ya uongozi ya idara ya uhandisi  pamoja na kutoa fursa ya kutembelea karakana  na warsha mbalimbali ndani ya kituo .

  "Tumeandaa ziara ya kituo cha kisasa kabisa cha idara ya uhandisi ya shirika la ndege la Etihad, karakana zake  pamoja na warsha zitakazo fanyika katika kituo hicho kikubwa kuliko vyote katika mtandao wa MRO kanda ya mashariki ya kati. Hii ni pamoja na karakana sita (6) zenye uwezo wakuhifadhi hadi ndege kubwa tatu (3)  aina ya A380 kwa wakati mmoja. "

  0 0


  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kushuka kwa mfumuko wa bei kwa Machi mwaka huu. Kulia ni Meneja wa Ajira na Bei wa NBS, Ruth Minja.
  Kulia ni Meneja wa Ajira na Bei wa NBS, Ruth Minja akiwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo jijini Dar es Salaam leo.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  MFUMUKO wa Bei kwa Machi 2016 umepungua hadi asilimia 5.4 kutoka asilimia 5.6 ya Februari.

  Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kuwa upandaji wa bei za bidhaa kwa mwaka ulioshia kwa Machi , 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioshia Februari mwaka huu.

  Amesema Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 101.93 mwenzi Machi, 2016 kutoka 96.69 mwezi Machi 2015.

  Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mweziMachi, 2016 umepungua hadi asilimia 8.5 kutoka 9.5 iliyokuwa kwa Februari, 2016.

  Amesema kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Machi, 2016 kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Machi 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Machi 2015.

  Kwesigabo amesema mwenendo wa bei za bidhaa zisizo za vyakula zinaonyeshwa kupungua kwa mwezi Machi 2016 ikilinganishwa na mwezi Machi 2015 bidhaa hizo ni Gesi asilimia 10, Diseli 5.8, Mafuta 1.0.

  Mfumko wa bei unafanana nchi za Afrika Mashariki , kwa mwezi Machi nchi ya Kenya Mfumuko umepungua hadi asilimia 6.45 kutoka asilimia 6.8 kwa Februari, Uganda mfumuko wa bei umepungua hadi asilimia 6.2 kwa Machi 2016 kutoka asilimia 7.0 kwa Februari 2016.

  0 0

  Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akisisitiza jambo mbele ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Jaffery Ind. Saini Ltd inayofunga Meza na Viti katika Ukumbi wa Bunge Ndg. Vishal Singh Sain baada ya kampuni hiyo kukamilisha zoezi la kufunga meza mpya 404 na viti vipya 94 na kurejeshea viti vya awali katika meza mpya zilizofungwa katika ukumbi huo.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Jaffery Ind. Saini Ltd inayofunga Meza na Viti katika Ukumbi wa Bunge Ndg. Vishal Singh Sain akimuonesha Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah jinsi ubora wa Meza Mpya katika Ukumbi wa Bunge na jinsi Kampuni hiyo ilivyofanikisha kurejeshea vipaza sauti katika Meza hizo.
  Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akimuonyesha eneo la paa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jaffery Ind. Saini Ltd Ndg. Vishal Singh Sain wakati wa ukaguzi huo.


  0 0
 • 04/08/16--04:51: TAARIFA KUTOKA JWTZ
 • Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa kwa taarifa zinazo lituhumu JWTZ kuhusu unyanyasaji wa kijinsia unaodaiwa kufanywa na Wanajeshi wetu kwa Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

  JWTZ chini ya Umoja wa Mataifa (MUNUSCO) limekuwa likitekeleza majukumu ya Ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo takribani miaka mitatu sasa.Katika muda ambao JWTZ limekuwa nchini Congo hapakuwepo na tuhuma kama hizo.

  Aidha, JWTZ limetekeleza na limeendelea kutekeleza majukumu kama hayo katika nchi mbalimbali duniani kama vile Msumbiji, Liberia, Visiwa vya Comoro (Anjouan), Lebanon, Sudan katika jimbo la Darfur na sehemu nyingi kama hizo.Katika kutekeleza majukumu hayo JWTZ limeyatekeleza kwa nidhamu na weledi wa hali ya juu.JWTZ limekuwa moja ya majeshi mengi yanayofanya vizuri na kutoa mchango mkubwa katika Ulinzi wa amani katika nchi ambazo limetekeleza majukumu hayo.

  Hivi karibuni kumezuka tuhuma nchini Congo kuhusu Wanajeshi wa JWTZ kuwanyayasa kijinsia wananchi wa Congo. Kimsingi JWTZ haliwezi kupuuzia taarifa hizo, hivyo limeanza kuchukuwa hatua za kiuchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo ingawa rekodi za majukumu ya ulinzi wa amani zilizokwisha fanywa na JWTZ sehemu mbalimbali zinaonesha kuwa hakukuwa na tuhuma kama hizo.

  Kufuatia tuhuma hizo, JWTZ kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa unafanya uchunguzi wa kina ili kujiridhisha na ukweli wake. JWTZ halitasita kuchukua hatua kali kwa watakaobainika katika tuhuma hizo. JWTZ bado lipo imara na linaendelea kutekeleza majukumu yake nchini Congo kwa kufuata sheria na taratibu za Umoja wa Mataifa. 

  Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
  S.L.P 9203, Simu: 0784-477638/0756-716085
  Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gelasius Gaspar Byakanwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.

  Taarifa iliyotolewa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 08 April, 2016. Bw. Byakanwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Antony Mtaka aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

  Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Byakanwa alikuwa Katibu wa Rais Msaidizi Mwandamizi.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es Salaam
  08 Aprili, 2016

  0 0

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amelihasa jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) kujenga uzalendo ndani ya jeshi letu kupitia michezo mbalimbali ya ndani.

  Waziri Nape ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya Ulingo wa Kisasa wa Ngumi kwa Jeshi hilo ili wautumie kwa ajili ya maandalizi mbalimbali ya mchezo wa ngumi kwani Serikali imeona ni sehemu salama Zaidi na nidhamu ya kuutunza ipo na hata pale utapoitajika kutumika kwingine uchukuliwe na kurudishwa jeshini hapo kwani jeshi hilo limeleta heshima kubwa ya michezo nchini na kulifanya baraza la michezo ya majeshi (BAMMATA) kuimarika zaidi.

  “Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa na mchango mkubwa sana katika michezo hapa nchini na limetuletea sifa kubwa sana kwetu na hivyo hatukuwa na shaka tulipoletewa ombi la ulingo huu.Ulingo huu utumike vyema na ulete heshima hapa nchini”Alisema Nape.

  Aidha Waziri nape alitoa rai kwa jeshi hilo kurudisha michezo jeshini kwani inajenga uzalendo na kuimarisha umoja,undugu na urafiki.

  Waziri huyo pia alikazia kuwa wizara yake itaendelea Kwa upande wake Meja Jenerali Issa Nassor ambaye ni mkuu wa mafunzo na Operesheni Jeshini alimshukuru Waziri Nape na Wizara yake kwa kuwapa ulingo huo na kuwa utawasaidia “Ulingo huo utatumika kwa mabondia wote Tanzania kwani utajenga Umoja na Kufahamiana na kukuza michezo na pia tutashirikisha askari wote kwani michezo ni sehemu ya kazi pia”.

  Alisema Aidha alisema kuwa Msaada wa Ulingo huo ni chachu ya mazoezi na itawajengea wana mchezo huo chachu ya ushindi na kuwataka wadau mbalimbali wa michezo kuunga mkono jitihada za Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo imetoa ulingo huo kwa jeshi hilo baada ya kupewa msaada na serikali ya watu wa china mwaka jana ikiwa ni jitihada za kuboresha jeshi hilo.

  kushirikiana na jeshi hilo katika michezo mbalimbali nchini. sana katika suala la mazoezi na hata mashindano mbalimbali. Meja Jenerali Issa. jeshi hilo kwani wana nia ya wazi ya kuwa kituo cha ubora. michezo nchini.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(wa pili kushoto) akiwa na Mkuu wa Mafunzo na Operesheni jeshi la wananchi Tanzania Meja Jenerali Issa S. Nassoro(wa kwanza kushoto) wakati wa makabidhiano ya Ulingo wa Ngumi uliotelewa na Wizara hiyo kwa jeshi la wananchi Tanzania(JWTZ).Wengine pichani ni Brigedia Jenerali Martin Busungu ambaye ni mkurugenzi wa michezo jeshini (wa pili kulia) na Kaimu mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Alex Nkenyenge.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimvisha medali bondia wa jeshi kama moja ya ishara ya ufunguzi wa ulingo wa ngumi waliopewa na wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ili kuimarisha mchezo wa ngumi jeshini na nchini kwa ujumla kwani ulingo huo utatumiwa na baraza la Michezo ya majeshi kujiimarisha katika mchezo huo.Wengine pichani ni Mkuu wa Mafunzo na Operesheni JWTZ Meja Jenerali Issa S. Nassoro(wa kwanza kushoto).
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akimkabidhi Mkuu wa Mafunzo na Operesheni JWTZ Meja Jenerali Issa S. Nassoro ulingo wa Ngumi wa kisasa ambao wizara ilipewa na Serikali ya China kwa ajili ya maendeleo ya ngumi nchini.Wizara imeamua kuwapa jeshi kwakuwa ni sehemu salama na watakuwa na nidhamu ya kuutunza na pia ulingo huo utaimarisha Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania(BAMMATA). Wengine pichani ni Brigedia Jenerali Martin Busungu ambaye ni mkurugenzi wa michezo jeshini (wa kwanza kushoto) na Kaimu mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Alex Nkenyenge(wa kwanza kulia).
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akipiga gitaa pamoja na bendi ya jeshi la wananchi Tanzania(JWTZ) wakati wa makabidhiano ya Ulingo wa Ngumi uliotelewa na Wizara hiyo kwa jeshi hilo leo jijini Dar es Salaam.Picha na Daudi Manongi-(WHUSM).

  0 0

  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na sababu za kiufundi na usalama , umeamua kuahirisha safari ya treni ya abiria leo Ijumaa Aprili 08, 2016 hadi kesho Jumamosi Aprili 09, 2016 saa 11 jioni.

  Wakati huo huo taarifa imefafanua kuwa treni ya abiria ya Deluxe kwenda Kigoma iliyopangwa kuondoka Jumapili Aprili 10, 2016 saa 2 asubuhi imesogezwa mbele muda wa kuondoka hadi saa 2 usiku.

  Tokea Jumanne wiki hii eneo la stesheni ya Gulwe mkoani Dodoma limekumbwa na mafuriko ambayo huleta mchanga na udongo na kufunika tuta la reli.

  Hata hivyo kwa vile kujaa kwa maji hutokea takriban kila siku kazi ya kusafisha eneo hilo kunakofanywa na Mafundi wa TRL imekuwa ni endelevu kuhahakisha njia ya reli inapitika.

  Taarifa imeainisha kuwa kama kutatokea mabadiliko yeyote katika eneo la Gulwe kabla muda wa safari uliotangazwa taarifa ya ufafanuzi itatolewa.

  Aidha Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

  Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya Kaimu Mkurugenzi
  Mtendaji wa TRL Nd. Masanja Kungu Kadogosa
  Dar es Salaam
  Aprili 08, 2016

older | 1 | .... | 1177 | 1178 | (Page 1179) | 1180 | 1181 | .... | 3285 | newer