Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1180 | 1181 | (Page 1182) | 1183 | 1184 | .... | 3285 | newer

  0 0


  0 0

  Na kitengo cha Sheria na Mahusiano, 
  Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)

  TIMU ya Uchukuzi Sports Club imepania kufanya vyema kwenye  mashindano ya Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) yatakayofanyika mjini Dodoma kuanzia Aprili 16 mwaka huu.

  Mwenyekiti wa timu hiyo inayoundwa na wafanyakazi wa taasisi zinazounda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mohamed Ally alisema kuwa timu yake itafanya vizuri katika mashindano hayo, kutokana na maandalizi kabambe waliyofanya. 
  Ally alisema kuwa kwa sasa wako katika mazoezi makali kujiandaa na mashindano hayo, ambayo yatafikia kilele siku ya Mei Mosi mjini Dodoma.

  Ally alisema Uchukuzi Sports Club inaundwa na timu za michezo ya soka, netiboli, kuvuta kamba, bao, karata, riadha, baiskeli na vishale. 
  Alisema kuwa wana uhakika timu yao kufanya vizuri katika mashindano hayo, kutokana na kufanya mazoezi kwa muda mrefu chini ya makocha wazoefu wa michezo hiyo.

  Ally aliwataja baadhi ya makocha hao kwa upande wa soka kuwa ni pamoja na Kenny Mwaisabula, Robert Damian, Terry, Kingsley Malwilo na Abunu Issa, ambao wameifanya timu yao kuwa tishio kwa timu zingine, wakati netiboli inafundishwa na mchezaji mkongwe Judith Ilunda.

   Alisema kuwa timu zao hizo zimekuwa zikicheza mechi za kirafiki na timu mbalimbali, ili kuwawezesha makocha kubaini makosa na kufanya marekebisho ya mwisho kabla timu hiyo haijaondoka kwenda Dodoma.
  Naye Meneja wa Uchukuzi Sports Club, Robert Damiani alisema kuwa timu yao inatarajia kwenda Dodoma Aprili 14 tayari kwa mashindano hayo. 
  Damiani alisema wanauhakika wa kufanya vizuri na kuvunja rekodi ya mwaka jana ya kutwaa vikombe 13, kati ya hivyo vitano vikiwa ni vya ushindi wa kwanza, wakati vilivyosalia walishika nafasi ya pili na tatu.


   Timu ya soka ya Uchukuzi Sports Club iliyopo chini ya Wizara ya Ujezi, Uchukuzi na Mawasiliano ikifanya mazoezi wakijiandaa kwa mashindano ya Mei Mosi 
   Makipa wakila tizi maalumu
   Kikosi kabambe cha timu ya soka ya Uchukuzi kikiwa pamoja na kocha na meneja wa timu hiyo Robert Damiani (kushoto).
   Wachezaji wa timu ya wanawake ya kuvuta kamba ikiwa kwenye mazoezi katika viwanja vya JNIA.

  Kikosi kabambe cha wanawake cha klabu ya Uchukuzi wakifanya mazoezi kabla ya kuvuta kamba.

  0 0

   Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
  RAIS wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara 13 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mawaziri wasiokuwa na Wizara Maalum ambao pia ni Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi. 
  Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa vyama na Serikali pamoja na wananchi kadhaa ambapo miongoni mwa waliohudhuria ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid. 
  Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji na Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis. Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib pamoja na viongozi wa vikosi vya Ulinzi. 
  Walioapishwa katika hafla hiyo ni Waziri, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji  Ussi Gavu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora  Mhe. Haroun Ali Suleiman. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ   Mhe. Haji Omar Kheri, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud Mohammed.   
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed, Waziri wa Afya Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma pamoja na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mhe. Moudline Castico. 
  Wengine ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Balozi Ali Abeid A. Karume. Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohammed. Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Rashid Ali Juma na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Salama Aboud Talib. 
  Kwa upande wa Manaibu Waziri ni Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Khamis Juma Maalim. Naibu Waziri wa Afya Mhe. Harusi Said Suleiman na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri.


  Wengine ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mhe. Mohammed Ahmed Salum. Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo nan Uvuvi Mhe. Lulu Msham Abdulla, Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Bibi Choum Kombo Khamis na Naibu Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mhe. Juma Makungu Juma.

           

  Aidha, Dk. Shein amewaapisha Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum akiwemo Mhe. Said Soud Said kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum pamoja na Mhe. Juma Ali Khatib Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum. 
  Kwa uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42, 43,44 na 47 vya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk. Shein ameunda Wizara 13 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuwateua Mawaziri na Manaibu Mawaziri wa Wizara hizo pamoja na Mawaziri Wasiokuwa na Wizara Maalum na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi.

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Mawaziri wa Wizara mbali mbali (waliosimama) pamoja na Viongozi Wakuu baada ya kuwaapisha Wajumbe wapya wa Baraza la Mawaziri kwa kipicha pili cha Uongozi wake   katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Manaibu Mawaziri wa Wizara mbali mbali (waliosimama) pamoja na Viongozi Wakuu baada ya kuwaapisha Wajumbe wapya wa Baraza la Mawaziri kwa kipicha pili cha Uongozi wake   katika hafla ya kuapisha Baraza jipya la Mawaziri iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu

  0 0


  0 0  0 0

  WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Kassim Majaliwa amesema Mkurugezi yeyote wa Halmashauri nchini atakayeshindwa kutenga asilimia 10 ya mapato kwa ajili ya wanawake na vijana ataondolewa.

  Amesema suala la kila Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi ni la lazima na si hiari.Waziri Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo leo (10 Aprili, 2016) alipokuwa anazungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Kitandi, Mtimbo, Likunja, Nkowe na Namahema ambako lifanya mikutano ya hadhara.

  “Halmashauri ambayo itashindwa kutenga asilimia 10 kwa maana asilimia tano kwa ajili ya vijana na tano kwa ajili ya akinamama Mkurugenzi wake atakuwa anatafuta safariiri,” amesema Waziri Mkuu, Majaliwa.

  Waziri Mkuu, Majaliwa yupo wilayani Ruangwa, Lindi kwa ajili ya ziara ya kikazi inayolenga kukagua shughuli za maendeleo, ambapo amewasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutimiza wajibu wao na serikali haitamvumilia yeyote atakayeshindwa.

  Pia Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka wananchi hao kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali ili zitakapofika sh milioni 50 za kila kijiji zilizoahidiwa na Rais, Dk. John Magufuli waweze kunufaika.Amesema fedha hizo ambazo zitatolewa kuanzia mwezi Julai mwaka huu zitagawiwa katika vikundi mbalimbali vilivyosajiliwa na si kwa mtu mmoja mmoja hivyo amewataka watendaji wa kata na vijiji kuwahamasisha wananchi kujiunga katika vikundi.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu, Majaliwa amesema serikali imefuta tozo tano kati ya tisa za zao la korosho zilizokuwa kero ya muda mrefu na kufanya wakulima wachukie mfumo wa Stakabadhi ghalani.

  Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwendesha pikipiki maarufu na hodari, Zaina Amour wa kijiji cha Nandagara wilayani Ruangwa Aprili 10, 2016.

  WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa amesema serikali inatarajia kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Nanganga, Ruangwa hadi Nachingwea.

  Hatua hiyo itawezesha kutatuliwa kwa kero ya changamoto ya miundombinu ya barabara inayowakabili wananchi wa wilaya za Ruangwa na Nachingwea kwa muda mrefu.Waziri Mkuu, Majaliwa amesema barabara hiyo ambayo kwa sasa haipo katika hali nzuri itajengwa kwa kiwango cha lami, ambapo serikali inatarajia kuanza kuifanyia upembuzi yakinifu katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

  Hayo yamesemwa jana jioni (10 Aprili, 2016) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Likunja, Nkowe na Namahema katika mikutano ya hadhara aliyoifanya wilayani Ruangwa wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi.

  Amesema serikali imejipanga katika kuboresha miundombinu ya barabara kwenye maeneo mbalimbali nchini na kwamba mara baada ya kumalizika kwa upembuzi yakinifu ujenzi wa barabara hiyo utaanza, hivyo amewataka wananchi kuwa na subira.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka wananchi wa vijiji hivyo kushirikiana katika shughuli za maendeleo na kuweka kando itikadi zao za kisiasa kwa sababu uchaguzi ulishamalizika tangu Oktoba 25 mwaka jana.

  “Mimi nitaendelea kuwaheshimu, kuwasikiliza na kuwahudumia, nawaomba tushirikiane na tuweke kando masuala ya itikadi za vyama, sasa ni wakati wa kazi, hivyo ni bora tukashirikiana kufanya kazi kwa maendeleo ya Ruangwa jambo ambalo linawezekana.

  Hata kama wewe ambaye najua ulinichukia mimi nimekusamehe kutoka moyoni, wewe ni wangu hata kama hukunichagua nitakuhudumia na kukutumikia kwa sababu mimi ndiye mbunge wako hivyo naomba tushirikiane,” amesema.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Rashid Nakumbya aliomba wakazi wa wilaya hiyo kushirikiana kwa pamoja kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya wilaya yao na hatimaye iweze kupiga hatua.

  0 0

  Na Shamimu Nyaki, WHUSM.

  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura amemuagiza Meneja wa Miradi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC ) Bw. Mackselin Chota kuhakikisha kiwanja Na.1 Kitalu “B” kilichopo eneo la Kimani wilaya ya Kisarawe kinapatiwa Hati Miliki ili kuepusha kuvamiwa pamoja na migogoro inayoweza kutokea.

  Agizo hilo amelitoa jumamosi wakati alipotembelea kiwanja hicho na kueleza kuwa kiwanja hicho ni lazima kiendelezwe kwa ajili ya kuwasaidia wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambapo kiwanja hicho kilitafutwa kwa dhumuni hilo.“Naishukuru Halmashauri kwa kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo,hivyo natoa siku saba kwa idara ya Miradi ya TBC kushirikiana na Halmashauri kuhakikisha kiwanja hicho kinapatiwa Hati”.Alisema Mhe.Annastazia.

  Aidha amewataka kuwasilisha gharama zilizotumika katika ujenzi wa nyumba zilizopo katika eneo hilo na wapi zimetoka na sababu zilizosababisha ujenzi huo kukwama kwa zaidi ya miaka mitatu.

  Akitoa maelezo kuhusu Kiwanja hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Bi Mwanamvua Mrindoko amesema kuwa kiwanja hicho kilipimwa na ramani yake ya upimaji ilipata kibali cha Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kusajiliwa kwa namba 68480,ramani namba E 292/83 ya tarehe 22 februari, 2012.

  “Taratibu za umilikishwaji zilifanyika kwa kuandaliwa gharama za kulipia kabla hati haijaandaliwa,malipo hayo yalifanywa na TBC kupitia NMB na kuwasilisha fomu ya malipo hayo(Bank pay in slip)”.Alisema Bi Mwanamvua.

  Naye Meneja wa Miradi wa Shirika la Utangazaji Tanzania Bw.Mackselin Chota amesema kuwa Shirika hilo lina jumla ya viwanja 55 nchi nzima,ambavyo 19 kati ya hivyo vina Hati miliki ambapo katika mkoa wa Pwani kuna kiwanja kimoja, Dar es Salaam viwanja vitano ambavyo viko Pugu Road,Kunduchi, na TAZARA, Mikocheni na Sinza.a

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Basila Mwanukuzi (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation) yenye lengo la kusaidia wanawake kuinua uwezo wao wa kibunifu ili kujiinua kiuchumi  hasa Mama Lishe kwa kushirikiana na wadau mbali mbali. Uzinduzi huo umefakika leo Aprili 11, 2016 kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Basila Mwanukuzi (kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia, Timoth Mgonja pamoja na Mwakilishi wa Mama Lishe, Bi. Grace Foya.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu, akitoa hotuba yake wakati wa Uzinduzi wa Taasisi ya Basila Mwanukuzi (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation), uliofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam leo Aprili 11, 2016.
   Mwanzilishi wa Taasisi ya Basila Mwanukuzi (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation), Basila Manukuzi, akizungumza machache wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi yake hiyo yenye lengo la kusaidia wanawake kuinua uwezo wao wa kibunifu ili kujiinua kiuchumi  hasa Mama Lishe uliofakika leo Aprili 11, 2016 kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam.
  Picha ya pamoja na baadhi wa Wageni wa waalikwa pamoja na Kina Mama Lishe.


  0 0
 • 04/11/16--03:46: In Loving Memory


 • 0 0

  Kampuni ya Statoil Tanzania ina furaha kutangaza majina ya vijana watano waliongia fainali za shindano la biashara la mashujaa wa kesho ambalo lina dhumuni la kuhamasisha ujasiriamali kwa mikoa ya kusini mwa Tanzania yaani Mtwara na Lindi.

  Akitoa taarifa hii meneja wa shindano hilo kutoka Statoil, Erick Mchome amewataja washindi hao kuwa ni Razaki Kaondo, Edward Timamu and Sifael Nkiliye (walioshiriki kama timu moja), Saleh Rashid Kisunga, Azizi Doa, na Yunus Mtopa.

  Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi kuwasilisha mawazo yao ya biashara ambayo baadae yalibadilishwa na kuwekwa kwenye andiko la biashara.

  Mwaka huu shindano hili lilivutia vijana zaidi ya 400 ambao waliwasilisha mawazo ya biashara zao zinazolenga sekta mbalimbali za uchumi kama kilimo, ufugaji, mawasiliano, na biashara nyingine ndogondogo. Vijana waliruhusiwa kushiriki mmoja mmoja au hata kuunda vikundi vya watu wawili mpaka watatu.
  IMG-20160411-WA0001
  Mwazo bora yaliyopatikana kati ya 400 yalikuwa 60 na wamiliki wa mawazo hayo ambao ni zaidi ya vijana 80 kutoka Lindi na Mtwara walipewa mafunzo maalum ya kuandaa andiko la biashara ambapo yalishindanishwa tena na kupatikana vijana kumi bora waliopelekwa mbele ya majaji ambao wiki hii walichagua maandiko matano bora kati ya kumi waliyopokea.

  “Vijana hawa watano watawasili jijini Dar es Salaam wiki ijayo ili kuja kutetea maandiko yao ya biashara mbele ya jopo la majaji ambao mwisho wake wataamua nani anafaa kuwa mshindi wa shindano letu,” alisema Bwana Mchome.

  Mshindi wa shindano hili atatangazwa siku ya Ijumaa tarehe 15 Aprili jijini Dar es Salaam katika hafla maalum iliyoandaliwa na Statoil ili kumpongeza mshindi huyo na wenzake wanne ambao wamefanikiwa kuingia fainali. Mshindi huyo atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani 5,000 wakati washindi wanne waliobakia watapata dola 1,500 kila mmoja. Washindi wengine watano waliofanikiwa kuingia kumi bora watapata dola 1,000.

  “Statoil inaamini katika kuwawezesha vijana wenye vipaji katika maeneo yote ambayo tunafanya shughuli zetu na kwa kufanya hivi tunachochea maendeleo katika maeneo hayo ambayo nasi ni sehemu yake kwani tunafanya shughuli zetu za uendelezaji wa nishati kama gesi na mafuta.,” amesema Meneja Mkazi wa Statoil Tanzania, Øystein Michelsen.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa STAMICO Bi. Zena Kongoi ameupongeza mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo uliopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera kwa kuendelea kuwa mfano wa mgodi pekee hapa nchini unaomilikiwa na serikali kwa 100% na kuzalisha dhahabu chini ya Wataalam wa Kitanzania pekee.

  Pongezi hizo zilitolewa wakati wa ziara yake hapa mgodini mwishoni mwa juma iliyolenga kuzungumza na Wafanyakazi na kuelezea dhamira kuu ya STAMICO ya kuhakikisha mgodi huu unasonga mbele pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazoukabili mgodi hususani suala la ufinyu wa mtaji na kuahidi kuwa Shirika limepanga kwa mwaka huu wa 2016 fursa zote zinazohusu madini zinaunufaisha mgodi wa STAMIGOLD.
  “ Ningependa kuchukua fursa hii kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya pamoja na uwepo wa changamoto nyingi na hasa ya ufinyu wa mtaji lakini bado mnaendelea kutumia ubunifu na uzalendo wenu kuendesha mgodi na kuzalisha dhahabu hivyo kwa niaba ya STAMICO tunawapongeza sana na tunatambua kazi yenu nzuri mnayofanya ukizingatia kuwa moja ya malengo ya serikali ya sasa ni kuhakikisha uchumi wa madini unarudi kwa Watanzania na kwa kupitia mgodi huu mmeweza kuonyesha kuwa hilo linawezekana” Alisema Bi. Kongoi.


  0 0

  Droo ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup), inatarajiwa kufanyika kesho Jumanne saa 3 usiku moja kwa moja (live) kupitia kituo cha luninga cha AzamTwo.

  Hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) itafanyika live katika kituo cha AzamTwo, ambao kupitia Azamtv ndio wadhamini wa wakuu wa michuano hiyo iliyoibua msisimiko wa mpira wa miguu na kushirikisha timu nyingi zaidi nchini.

  Baada ya timu za Azam FC, Mwadui FC, na Yanga SC kukata tiketi ya kucheza Nusu Fainali, mshindi wa mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Coastal Union utakaochezwa leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam atungana na timu hizo tatu kwenye droo ya kesho.

  Michuano ya Kombe la Shirikisho iliyoanza kwa kushirikisha timu 64 mwishoni mwa mwaka jana, imefikia hatua hatua ya nusu fainali, baada ya Azam FC kuindoa Prisons (3-1), Mwadui FC kuiondosha Geita Gold (3-0) na Yanga SC kuwaondoa Ndanda FC kwa mabao (2-1).

  Mshindi wa Kombe la Shirikisho (ASFC) msimu huu, ataiwakilisha Tanzania mwaka 2017 katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC).

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea soko kuu la wilaya ya Ruangwa na kukagua hali ya upatikanaji na bei za vyakula akiwa katika jimbo lake la uchaguzi Aprili 11, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Mkewe Mary wakikabidhi baiskeli kwa walemavu Kanisia Ndaka (wapili kulia) Rehema Mtachi (wapili kushoto) kwenye uwanja wa michezo wa mjini Ruangwa Aprili 11, 2016.
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (wapilinkulia) akitoa msaada wa shuka na mito kwa wazazi wote waliojifungua na waliokuwa wakisubiri kujifungua kwenye wodi ya wazazi ya hospitali ya wilaya ya Ruangwa Aprili 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  WABUNGE wa Jumuiya la Afrika Mashariki kuanza kuhamasisha jamii ili kujua fursa za Kibiashara zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Ameyasema hayo leo Mbunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa wataanza kuhamasisha jamii katika soko la Kariakoo na Soko la Samaki la Feri jijini Dar es Salaam pamoja na vyombo vya habari mbalimbali.

  Makongo amesema kusudi la kuelimisha jamii ili wafanyabishara waweze kufanya biashara katika nchi za Afrika Mashari kama Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashari Makongoro Nyerere akizungumza na waandishi wa habari(Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na wabunge wa bunge la Afrika Mashariki kuanza kuhamasisha jamii kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji, Miriam Yahaya Usi, Ndarakilo Kessy na Dk.Twaha Tasilima wakiwa katika mkutano huo leo.


  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi (Katikati)akifafanua jambo katika mkutano wa waandishi wa habari na wabunge wa bunge la Afrika Mashariki leo jijini Dar es Salaam.
  Mbune wa Bunge la Afrika Mashariki, Nderakilo Kessy (aliyesimama )akizungumza na waandhishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na wabunge hao kuanza kuhamasisha jamii juu ya Fursa zilizopo katika jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Banji akizungumza kuhusiana na Fursa zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashari.

  Amesema kuwa frusa zilizopo kwa waalimu wa Lugha ya Kiswahili wanaweza kwenda kufundisha Kiswahili kwenye Nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni Kenya Uganda, Rwanda, Burundi na Afrika ya kati ipo mbioni kujiunga na Umoja huo.

  Amesema Lugha ya Kiswahili kwa sasa imeanza kushika karibu nchi zote za Afrika Mashariki na hii ndio fursa Kubwa tuliyo nayo.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

  Wananchi wa Kijiji cha Olbili kilichopo kitongoji cha Tilili,kata ya Shambarai wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wakibeba mabango kupinga kunyang`anywa ardhi ya waliyokua wakiitumia kwa kilimo na kubadilishwa kuwa ya malisho ya mifugo,kijiji hicho kinakabiliwa na tatizo la ukosefuchakula cha miongoni mwa familia nyingi hali inayochangia kuzorota kwa hali ya lishe na shughuli za kijamii pamoja na za kiuchumi.

  Na Woinde Shizza,Simanjiro.
  KIJIJI cha Olbili kilichopo kitongoji cha Tilili,kata ya Shambarai 
  wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kinakabiliwa na tatizo la ukosefu
  chakula cha miongoni mwa familia nyingi hali inayochangia kuzorota 
  kwa hali ya lishe na shughuli za kijamii pamoja na za kiuchumi.

  Wananchi wa kijiji hicho Zuhura Salim na Anna Lazaro wamesema kuwa 
  uhaba huo wa chakula unatokana na kunyang`anywa maeneo waliyokua 
  wanatumia kwa kilimo na kutumika kama ardhi ya malisho.

  Wananchi hao waliandamana na mabango yao kuzunguka eneo la shamba hilo 
  wameiomba serikali kupitia wizara ya ardhi na wizara ya kilimo 
  kuingilia kati mgogoro huo baina yao na wafugaji wanaogombea eneo hilo 
  ambalo kwa zaidi ya miaka 24 tangu mwaka 1992 hadi mwaka 2013 ambapo 
  walizuiwa kutumia maeneo hayo ambayo walikua wakiyatumia kwa 
  shughuli za kilimo cha kujikimu.

  Eliud Jackson ni Mwanakijiji wa Olbili amesema kuwa licha ya kunyimwa
  maeneo ya kulima pia mwaka huu hawakupata chakula cha msaada kama kata 
  nyingine zilizopata mgao huo hivyo kuteseka na njaa wao na watoto wao 
  ,wamemuomba Rais Magufuli kutazama suala hilo na kulipatia ufumbuzi.

  Mwenyekiti wa Kitongoji cha Tilili Kingi Lomayani Laizer amesema kuwa 
  baada ya kuzuiliwa kulima na Mtendaji wa Kata na Diwani aliyekua 
  madarakani walifika katika ngazi za wilaya bila mafanikio hivyo 
   wanamuomba Mkuu wa Mkoa wa Manyara afike kutatua mgogoro huo ili 
  kuwanusuru na baa la njaa.

  “Nimefuatilia suala hili kwa Mwenyekiti,Mtendaji wa kata na Diwani
  aliyemaliza muda wake bila mafanikio kwani wao ndio walitoa zuio la
   kutuzuia kulima katika maeneo haya ,inaonekana jambo hili 
  linashikiliwa na wafugaji wenye fedha wanatumia fedha zao kuwanyanyasa 
  wakulima” Alisema Laizer

  Aliiomba serikali kupitia wizara ya kilimo,ardhi kufika katika kijiji
  hicho na kutatua kero hiyo ya muda mrefu kwani wamekua wakishindwa 
  kuendesha familia zao kutokana na kutegemea kilimo kama shughuli ya 
  kuwapatia chakula na kipato.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA), Ludovick Utouh akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) jijini Dar es Salaam. 
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA), Ludovick Utouh  wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) jijini Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja  katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. 
  Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango amesema kukosekana kwa uwajibikaji na utawala bora  kunafanya mfumo wa maisha ya wananchi kuharibika.

  Dk.Mpango ameyasema hayo leo katika ufunguzi wa Kongamano la  Kimataifa linalojadili juu ya Uwajibikaji katika Sekta ya ya Gesi na Mafuta lililoandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA) ,amesema katika kuweza kufikia uchumi wakati lazima lipewe kipaumbele katika uwekezaji wa Gesi na Mafuta.

  Amesema jamii inayoamini uwajibikaji na utawala bora inafanya jamii hiyo kuwajibika kwa pamoja katika maendeleo ya kiuchumi.

  Dk.Mpango amesema akiwa Waziri mwenye dhamana ni kuangalia uwajibikaji kwa raia katika nchi na bila kuangalia uwajibikaji na utawala bora  mfumo wa maisha ya wananchi unaharibika.

  Amesema taasisi ya wajibu ni moja ya taasisi ambayo itasaidia juu ya kutafsiri wa uwajibikaji kwa wananchi kwa lugha inayofahamika na kueleweka.

  Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwajibikaji Tanzania (WIPA), Ludovick Utouh amesema nia ya kongamano hilo ni kutafuta mawazo ya watu wengine katika uwajibikaji wa katika sekta ya Gesi na Mafuta.

  Utouh amesema kuwa kutokana na rasilimali hiyo kugundulika wameona kuna umuhimu wa kushirikisha watu wengine ambao walipata rasilimali hiyo lakini hakuweza kuwasaidia ambapo hata Tanzania tunaweza kuangukia huko.

  Mkutano huo umeshirikisha watu waliobobea katika sekta ya Gesi na Mafuta katika kutoa mawazo yao juu ya Tanzania inavyoweza kufanya  katika sekta hiyo.

  0 0

  Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amewataka wawekezaji nchini kujiamini na kuwekeza katika sekta za Nishati na Madini ili sekta hizo zitoe mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

  Profesa Muhongo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika kikao chake na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania, Mhandisi Ray Ywa Seng’enge aliyeambatana na ujumbe wake. Kikao hicho kilishirikisha watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

  Profesa Muhongo alisema kuwa umefika wakati wa watanzania wenye uwezo katika uwekezaji hususan katika uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini kujitokeza na kuomba kazi kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kufanya kazi kwa ufanisi kwani uwezo wanao.

  Alisema kuwa wawekezaji wengi wamekuwa na mtizamo hasi kuwa makampuni ya kigeni pekee ndiyo yenye uwezo wa kuzalisha na kusambaza umeme vijijini.

  “Nataka niwahakikishie kuwa kampuni za kitanzania zina uwezo mkubwa katika uzalishaji na usambazaji wa umeme vijijini, na kama Serikali tupo tayari kuwasaidia ili kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi zaidi,” alisema Profesa Muhongo.

  Aliendelea kusema kuwa katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ya REA awamu ya pili, zipo kampuni za kitanzania zilizoonesha uwezo katika miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme vijijini.

  Akielekea mikakati ya Serikali ya kuwajengea uwezo wawekezaji wadogo wazawa Profesa Muhongo alieleza kuwa kampuni za kitanzania zimeonekana kujifunza kutokana na ushirikiano kati yao na kampuni za kigeni kwenye miradi ya umeme.

  Awali akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania, Mhandisi Ray Ywa Seng’enge alimpongeza Profesa Muhongo na kuelezea shughuli zinazofanywa na chama hicho.

  Akielezea mafanikio ya chama hicho Seng’enge alisema kuwa chama kimekuwa kikitoa huduma Serikalini na makampuni binafsi ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo yanayohusiana na masuala ya uhandisi.

  Alisema kuwa wakiwa na kampuni ya ushauri katika masuala ya uhandisi, wamekuwa wakishirikiana na makampuni mengine yaliyopo nje ya nchi.

  Akielezea changamoto katika utendaji wa kampuni hiyo Seng’enge alisema kuwa kampuni yao imekuwa ikitumiwa zaidi na makampuni yaliyopo nje ya nchi katika utoaji wa huduma na kuiomba Serikali kuwasaidia na kuahidi kutoa ushirikiano ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania, Mhandisi Ray Ywa Seng’enge (kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kuanza kwa kikao hicho.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akifafanua jambo kwa ujumbe kutoka Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania ofisini kwake mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania uliomtembelea ofisini kwake.

  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Baadhi ya walimu wa jiji la Arusha wamelalamikia utaratibu uliotumika wa upandishwaji wa madaraja na kusema kuwa utaratibu huo ni ujawatendea haki walimu waliofanya kazi kwa kipindi kirefu pamoja na wale ambao wamestaafu
  .

  Walimu hao walisema kuwa utaratibu uliotumika wa kuwachanganya walimu waliofanya kazi kwa kipindi cha mda mrefu zaidi ya miaka 20 pamoja na walimu wageni ambao wengine hawana mda mrefu kazini kwani wamefanya kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi miaka mitatu ni mbovu na unawakatisha tama ya kufanya kazi kwa umakini.

  Mmoja wa walimu hao aliyejitambulisha kwa jina la Mark Mbwabwo alisema kuwa mfumo huo wa upandishwaji wa madaraja haukuwatendea haki kabisa walimu ambao wamefanya kazi kwa kipindi cha mda mrefu kwani katika swala la ulipwaji mshahara mnakuta mwalimu aliefanya kazi kwa kipindi cha miaka 20 analipwa sawa na mwalimu ambaye amefanya kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja au mitatu.

  Gazeti hili lilitembelea ofisi ya chama cha walimu (CWT) mkoa wa Arusha ili kujua kama wamepata malamiko hayo ambayo yalitolewa na baadhi ya walimu ambao wamepandishwa madaraja na kukutana na katibu wa chama cha walimu Halmashauri ya jiji la Arusha Magreth Hovokela ambapo alitolea ufafanuzi tuhuma hizo na hatua ambazo wao kama chama cha walimu wamezifikia.

  Katika ufafanuzi wake alisema kuwa swala la upandishwaji wa madaraja kwa walimu waliogota ni la mda mrefu kwani wao kama CWT walipeleka pendekezo hilo tangu December 17 mwa ka 2014 na serekali ikakubali kupandisha walimu waliogota kwa kipind cha muda mrefu , serekali ilisema kuwa walimu hao wanaopandishwa madaraja wapandishwe kutokana na muundo wa zamani ambapo ilipitishwa walimu wapandishwe kuanzia mapema July 1 ,2015 lakini swala hilo halikutekelezeka.

  Aidha aliongeza kuwa swala hilo alikutekelezwa kwa kipindi hicho na lilianza kutekelezwa rasmi January 1 hadi machi mwaka huu na kila halmashauri imeshaanza kutekeleza swala hilo kutokana na ilivyojipanga pamoja na bajeti yake na katika barua ambazo walimu wamepewa za kupandishwa madaraja zinaainisha kuwa walimu hao wamepanda madaraja kuanzia January 1 mwaka huu badala ya July 7,2015 kama vile waraka unavyoelekeza.

  HABARI ZAIDI  BOFYA HAPA

  0 0

  Mwenyekiti wa Soko la Kisutu Tamimu Chande akizungumza katika Kampeni ya Kuongeza uelewa wa kupinga ukatili wa Kijinsia katika Soko la Kisutu Dar es Salaam leo asubuhi. Kampeni hiyo inaendeshwa na Shirika la Eqiuality for Growth (EfG).
  Mmoja wa kiongozi wa Soko la Kisutu akifungua mkutano wa kampeni hiyo.
  Igizo la kupinga ukatili wa kijinsia kutoka kundi la machozi likifanyika.

older | 1 | .... | 1180 | 1181 | (Page 1182) | 1183 | 1184 | .... | 3285 | newer