Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 116 | 117 | (Page 118) | 119 | 120 | .... | 3278 | newer

  0 0  0 0

  Tanzania will host the next Smart Partnership Dialogue. The Host and Patron Advisor for the 2013 Smart Partnership Dialogue, His Excellency Jakaya Mrisho Kikwete, and President of the United Republic of Tanzania officially launched preparations for the 2013 Dialogue in 29th May, 2012. 
  He also introduced the theme of Global 2013 SPD as Leveraging Technology for Africa’s Socio – economic Development and announced the dates for the dialogue to be 28th June - 1st July, 2013 to be held at Julius Nyerere Convention Center, Dar es Salaam. 
  The decision of His Excellency President Jakaya Kikwete to host the Global 2013 SPD and the choice of the theme for the dialogue were anchored on the realization and conviction that these dialogues provide a unique forum for interaction and equal opportunities for all participants.

  0 0

   JAJI ROBERT MAKARAMBA (WA TATU KUSHOTO WALIOKAA) KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA KIMATAIFA YA USULUHISHI. MAFUNZO HAYO YANAFANYIKA SHULE YA SHERIA KWA VITENDO

  MGENI RASMI WAKATI WA UFUNGUZI WA MAFUNZO YA USULUHISHI WA KIMATAIFA JAJI ROBERT MAKARAMBA AKIBADILISHANA MAWAZO NA MKUFUNZI KUTOKA DLA PIPER. KATIKATI NI MKUU WA CHUO CHA SHERIA KWA VITENDO DKT. JAJI GERALD NDIKA

  0 0

  Kocha wa Azam FC, Stewart Hall akizungumza na Florian Kaijage Mratibu wa klabu katika mashindano ya Afrika, baada ya kuwasili Cassablanca leo


  Na Mahmoud Zubeiry, Rabat
  AZAM FC imewasili salama nchinio Morocco tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji, FAR Rabat, Raundi ya Tatu ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumamosi wiki hii.  
  Azam, imewasili Cassablanca, majira ya saa 9:15 za huku Alasiri, sawa na saa 10:15 za Afrika Mashariki na kusafiri kwa basi kwa saa mbili kwenda Rabat, mji ambao mechi itachezwa.
  Azam imetua Morocco ikitokea Dubai, UAE ambako ilifika usiku jana saa 6:00 kwa saa za huko sawa na saa 5:00 kwa saa za Afrika Mashariki, ikitokea Dar es Salaam.
  Msafara huo unaouhusisha wachezaji na benchi la Ufundi, baada ya awali viongozi na wapenzi kadhaa kutangulia nchini humo, ili kuweka mazingira sawa, uliondoka Dar es Salaam kwa ndege ya shirika la Emirates, wadhamini wa Arsenal ya England saa 11:00 jioni kwa saa za Tanzania.
  Ni safari ndefu iliyohusisha mabara mawili, kutoka Afrika, Tanzania kupitia Asia Dubai na kurudi Afrika nchini Morocco.
  Azam walilala katika hoteli ya nyota tano ya Copthorne Dubai kabla ya kuunganisha ndege saa 7:35 asubuhi ya leo kuja Morocco kesho.
  Wachezaji wanawasili Morocco

  Azam imefikia katika hoteli ya Golden Tulip, maeneo ya Rabat, kaskazini mwa Cassablanca,  kilomita 120 kutoka Uwanja wa Ndege wa Cassablanca, umbali wa takriban saaa mbili.
  Azam itaanza rasmi mazoezi kesho kujiandaa na mchezo huo, ambao wanatakiwa kutoa sare ya mabao au kushinda ili kusonga mbele, baada ya awali katika mchezo wa kwanza kulazimishwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wiki iliyopita.
  Japokuwa hilo linachukuliwa kama jambo gumu mbele ya wengi, lakini rekodi ya timu hiyo, mali ya bilionea Alhaj Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake inaonyesha linawezekana.
  Wachezaji wanatua Morocco

  Azam imekuwa ikicheza vizuri na kupata matokeo mazuri katika mechi za ugenini kwenye michuano hii, kuliko nyumbani na hata kufuzu kwake hadi hatua hii zaidi kulitokana na matokeo ya mechi za ugenini.
  Raundi ya kwanza, Azam ilianza kwa kushinda kwa taabu 3-1 Dar es Salaam dhidi ya Al Nasir Juba ya Sudan Kusini, sehemu kubwa ya mchezo huo matokeo yakiwa 1-1 kabla ya mabao ya dakika za jioni ya Kipre Tchetche kutengeneza ushindi huo.
  Mchezo wa marudiano, Azam ilishinda 5-0 ugenini na kufanya ushindi wa jumla wa 8-1, ikisonga mbele kibabe.
  Raundi ya Pili, ilianza kwa ushindi wa 2-1 ugenini, Liberia dhidi ya wenyeji, Barack Young Controllers II, lakini katika mchezo wa marudiano ilibanwa kwa sare ya 0-0.
  Kocha Muingereza Stewart Hall hakuipa umuhimu mechi ya Ligi Kuu Ijumaa dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga iliyoisha kwa sare ya 1-1 akiwapumzisha wachezaji wake kadhaa wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya mechi na FAR Rabat.
  Wakati mabeki Waziri Salum, Joackins Atudo, viungo Khamis Mcha ‘Vialli’, Kipre Balou na mshambuliaji Kipre Tchetche hawakukanyaga kabisa nyasi za Uwanja wa Mkwakwani Ijumaa, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ alicheza kwa dakika 15 tu za mwisho- ili kuhakikisha wanakuwa vizuri Jumapili mjini Rabat.
  Kutoka kikosi cha kwanza cha sasa cha Azam waliocheza dakika zote juzi ni kipa Mwadini Ally, kiungo aliyehamishiwa beki ya kulia, Himid Mao, beki David Mwantika, kiungo Humphrey Mieno na washambuliaji Brian Umony na John Bocco ‘Adebayor’.
  Azam, itakuwa Rabat kwa wiki nzima hadi Jumamosi itakapocheza mechi na imejipanga vema kuhakikisha inavuka hatua hii.

  0 0

  Tume ya Mabadiliko ya Katiba imesema imejipanga kuandaa rasimu ya katiba itakayoweka mbele maslahi ya taifa na kuwaomba wananchi waijadili na kutoa maoni yao katika mabaraza ya katiba yatakayokutana kuanzia mwezi Juni mwaka huu (2013). 
   Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jospeh Warioba amesema leo (Jumatatu, Aprili 29, 2013) jijini Dar es Salaam kuwa katika kuandaa rasimu hiyo, Tume yake haitapokea shinikizo kutoka taasisi, asasi, makundi au vyama vya siasa.
   “Tume haitengenezi katiba ya vikundi au vyama, tunaandaa katiba ya nchi,” amesema Jaji Warioba katika mkutano wake na waandishi wa habari katika ofisi za Tume.
  Amefafanua kuwa Tume inazingatia uzito wa hoja zilizotolewa na wananchi na sio idadi ya watu waliotoa maoni. Jaji Warioba amewataka wananchi kutokubali kutumiwa na makundi, asasi, taasisi na vyama wakati wa kujadili na kutoa maoni katika mabaraza ya katiba ya wilaya.

  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu, Aprili 29, 2013). Kulia ni Katibu wa Tume, Bw. Assaa Rashid.

  Mwenyekiti wa kamati ya uwasilishaji wa mapendekezo ya muundo wa mabaraza ya Katiba kwa jamii ya watu wenye ulemavu, Bw. David Nyendo (kushoto) akiwasilisha maoni yake ya kamati hiyo kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao uliofanyika  ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Feb mwaka huu (2013). Kulia ni Mjumbe wa Tume, Dkt. Salim Ahmed Salim. (Picha na Tume ya Katiba)  0 0


   Wateja waBenki ya NMB wakipata maelekezo ya huduma za JISEVIE kutoka kwa Ofisa wa NMB tawi la NMB House  Edith Mavura.Huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB waliojisajili kutumia NMB Mobile, huduma inayomuwezesha mteja kupata huduma za kibenki mahala popote bila kufikakwenyetawi la NMB
   Wateja wa Benkiya NMB wakipata maelekezo yanayohusu maboresho ya huduma ijulikanayo kama JISEVIE kutoka kwa Ofisa wa NMB tawi la Bank House, Salvatory Mushi .Jisevie inamsaidia mteja wa NMB kupata huduma za kibenki sehemu yoyote atakapokua bila kufika kwenye tawi la NMB.Mteja ataweza kutumia simu yake ya kiganjani na kutembelea Mashine za kutoa fedha ili Kujisevia.
   Ofisa wa NMB tawi la Bank House, Salvatory Mushi akimwelekeza mteja wa NMB jinsi ya kujiungana NMB Mobile ili KUJISEVIA huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB waliojisajili kutumia NMB Mobile .Huduma inayomuwezesha mteja kupata huduma za kibenki mahala popote bila kufika kwenye tawi la NMB

  Ofisa wa  NMB tawi la Loliondo, Lembris Lesion akimwelekeza Mchungaji mstaafu, Ambelikile Mwaisapile jinsi ya kujiungana NMB Mobile ili KUJISEVIA huduma zitolewazo kwa wateja wa NMB waliojisajili kutumia NMB Mobile .Huduma inayomuwezesha mteja kupata huduma za kibenki mahala popote bila kufika kwenye tawi la NMB.

  Na Mwandishi Wetu

  NMB imeendelea kuboresha huduma zake kwa kuzindua bidhaa na huduma mbali mbali ili kuwawezesha wateja kupata huduma za kibenki kwa urahisi na unafuu zaidi.
  Ili kukuwezesha kupata huduma za kibenki haraka na kwa wakati wowote, Benki ya NMB imeendelea kuelemisha wateja wake aina mbalimbali ya huduma za kibenki wanazoweza kuzipata bila ya kwenda katika tawi la NMB kupitia kampeni yake maalum iitwayo JISEVIE.
  Huduma zilizojumuishwa katika mpango huu maalum wa Jisevie ni pamoja na Huduma ya NMB mobile, Huduma ya NMB PesaFasta, Huduma ya NMB ATM na huduma ya kuweka na kutoa fedha kupitia Vodacom Mpesa.
  “ Mpango huu wa kuelemisha wateja juu ya huduma mbali mbali wanazoweza kuzipata bila ya kupitia benki, yaani Jisevie unalenga katika kuendelea kutoa huduma bora zaidi , kuvutia na za haraka zaidi wakati wowote mteja anapohitaji huduma za kibenki”, alisema bwana Arjan Molenkamp, Afisa Mkuu wa Biashara ya Wateja Binafsi.
  Wateja ambao wataweza kutumia moja ya huduma hizi zilizoainishwa katika mpango huu wa Jisevie watapata faida mbalimbali ikiwemo; kutokutumia fedha taslimu kulipia huduma mbali mbali, kuweka au kutoa fedha mahali popote kwa kutumia huduma ya Vodacom Mpesa, Kutuma fedha kwa mtu yeyote asiye na akaunti wala kadi ya ATM ya NMB kwa kutumia NMB PesaFasta na kutohitaji kutembelea tawi lolote la benki ya NMB ili kuweka fedha kwenye akaunti yako.
  Wateja wa NMB sasa wanaweza kupata huduma za kibenki popote walipo bila kutembelea tawi la NMB. Haya yote yametokana  NMB Jisavie ambayo itamwezesha mteja wa NMB  kuwa na  NMB Mobile,NMB Pesa Fasta ,POS,NMB ATM,Huduma ya kuweka na kutoa fedha  kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda M-Pesa na M-Pesa kwenda Akaunti ya NMB,Zaidi ya hayo yote NMB inalenga kumuwezesha Mteja wake aweze kujihudumia mwenyewe bila kufika kwenye tawi la NMB.
  Faida nyingine anazoweza kupata Mteja wa NMB kwa kupitia mpango huu wa Jisevie ni pamoja na kuangalia salio la akaunti yako, kupata taarifa fupi ya matumizi ya akaunti yako, kununua Luku,Kulipa ankra ya Maji-DAWASCO, kulipia bili ya King’amuzi ya DStv, Kulipia kodi za Mapato na kununua muda wa hewani.

  0 0
 • 04/29/13--12:34: Article 19


 • 0 0
 • 04/29/13--12:41: Article 18

 • Kumekucha....Redds Miss Nyamagana 2013 mchakato umeanza...shindano kufanyika Jumamosi ya tarehe...11/05/2013 JB Belmont Hotel Mwanza..Show nzima Itasimamiwa na mchekeshaji Zembwela..huku burudani ikikamilishwa na Recho kutoka THT.....Warembo Zaidi ya 20 watapanda jukwaani...wakiwa na hamu sio tu kulichukua taji la Miss Nyamagana lakini pia Taji la Miss Tanzania 2013/14. 
  Tiketi zitauzwa mapema, wahi tiketi yako..kwani ni chache mno!! Karibu....


  0 0

  NEEMA HERBALIST & NUTRTITIONAL FOODS CLINIC ni wauzaji wa dawa mbalimbali za asili. Tunayo dawa nzuri na ya asili ya KUONDOA KITAMBI. Dawa hii ni ya asili “ pure herbal “, haijachanganywa na kemikali yoyote, haina side effect kwa mtumiaji na inaondoa kitambi ndani ya siku kumi na nne tu. Bei yake ni Shilingi Elfu Arobaini Tu ( Tsh 40,000/=)

  Tunapatikana jijini Dar Es salaam, katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU. Vile vile tunafanya ‘delivery’ kwa wateja wasio weza kufika ofisini kwetu, na kwa wateja wa mikoani tunawatumia kwa njia ya mabasi, wateja waliopo Zanzibar tunawatumia dawa kwa njia ya meli na kwa wateja waliopo nje ya nchi tunawatumia kwa magari, DHL, ama posta kulingana na nchi waliyopo.

  PIA tunayo dawa ya asili iitwayo JIKO ambayo hutibu tatizo la ukosefu na upungufu wa nguvu za kiume.

  Wasiliana Nasi kwa Simu : 0767010756 au 0766538384. 
  Website http://www.neemaherbalist.blogspot.com


  0 0

  Hatimaye Mshindi wa Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela amepatikana ikishuhudia Mwanafunzi chuo cha Ualimu cha Mkoani Kigoma Bw.Valelian Nickodemus(22) akiibuka mshindi kupitia droo kubwa iliyochezeshwa leo jumatatu. 
   Mshindi huyo amepatikana miongoni mwa mamilioni ya washiriki walioshiriki kucheza katika promosheni hiyo, Katika mahojiano yaliyofanyika kwa njia ya simu Mshindi huyo ameishukuru kampuni ya Vodacom kwa kumuwezesha kushinda kiasi hiko kwani hayakuwa mategemeo yake katika maisha yake.
   "Watu wengi hawakuwa wanaamini kuwa Promosheni hizi ni za kweli, Sikuwa na pesa ya kucheza moja kwa moja katika Promosheni hii ila nilipotumiwa pesa ya matumizi na mzee niliamua kuweka na kushiriki katika Promosheni hii, Hakika nimefurahi sana na ninawashukuru Vodacom, alisema Nickodemus. 
   Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amewapongeza Wateja wa mtandao huo kwa kushiriki katika promosheni hiyo na kumpongeza kwa upekee mshindi wa Promosheni hiyo na kujinasibu kuwa anajivunia mafanikio ambayo Promosheni hiyo imeyapata kwa kufanikiwa kubadili maisha ya mamia ya Watanzania.
   "Sisi kama Vodacom tumefurahi kwa kumpata mshindi wetu wa mwisho ambaye ameibuka kidedea kati ya Mamilioni ya Watanzania lazima tukiri kuwa ni bahati kubwa na tunatoa pongezi za kipekee kwa mshindi wetu, alisema Twissa na kuongeza kuwa 
  "Zaidi ya yote tunajivunia kwa upekee kabisa namna ambavyo promosheni hii imebadilisha mamia ya maisha ya Watanzania, Tumepata washindi kutoka katika Nyanja mbalimbali wakiwemo wakulima, wafanya biashara ndogondogo wanafunzi pamoja na wastaafu wengi ambao nao wameendelea kuboresha maisha yao. 
   Tangu Promosheni ya MAHELA kuzinduliwa tarehe 24 Mwezi wa kwanza na washindi 333 wamepatikana na kushuhudia kiasi cha Shilingi milioni 480 zikitolewa hadi sasa.
  Kutoka kushoto,Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bw.Mrisho Milau,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu,pamoja na Meneja wa Huduma za ziada wa kampuni hiyo, Bw. Benjamin Michael,wakichezesha droo ya mwisho ya "MAHELA"ambapo Bw.Valelian Nickodemus(22)Mwanafunzi wa Chuo cha uwalimu Mkoani Kigoma alijishindia kitita cha shilingi Milioni 100,kupitia promosheni hiyo
  Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Kelvin Twissa(katikati)akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kumpata mshindi wa Droo ya mwishi ya "MAHELA "Bw.Valelian Nickodemus(22) wa Mkoa wa Kigoma aliyejishindia shilingi Milioni 100.kushoto ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Bw.Mrisho Mlau  na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa Vodacom Tanzania,Bw. Benjamin Michael.

  0 0

  Na Profesa Mbele

  Nimerejea jioni kutoka Montana, ambako nilikwenda jana, kuonana na Mzee Patrick Hemingway (akiwa nami pichani), mtu maarufu sana. Ni yeye pekee ndiye bado hai kati ya watoto wa mwandishi maarufu Ernest Hemingway (BOFYA HAPA).

  Mwandishi Hemingway, ambaye alizaliwa mwaka 1899 jirani na Chicago na kufariki 1962, ni maarufu duniani kote. Kwa miaka yapata kumi, nimevutiwa na jinsi alivyoandika kuhusu Afrika, kutokana na kutembelea na kuishi Afrika Mashariki, mwaka 1933-34, na mwaka 1953-54. Ninasoma na kufundisha maandishi ya Hemingway, kama nilivyoandika hapa, na hapa.

  Kwa muda mrefu nilitaka niwasiliane na Mzee Patrick Hemingway, ambaye ni mtoto pekee wa Hemingway aliyebaki. Nilifahamu kuwa aliishi Tanzania miaka yapata 25. Moja ya shughuli alizofanya ni kufundisha katika chuo cha Mweka. Nilisoma sana maandishi yake na kusikiliza mazungumzo yake ambayo yako mtandaoni.

  Nilijua kuwa huyu ni hazina kubwa kwa yeyote anayefuatilia maandishi na maisha ya Ernest Hemingway. Siku moja, miaka yapata miwili iliyopita, nilijipa moyo nikampigia simu. Nilifurahi jinsi alivyonifanyia ukarimu, tukaongea sana. Kuanzia hapo, nimeongea naye mara kwa mara.

  Hatimaye, jana nilisafiri hadi Montana, ambako tumepata fursa ya kuongea kwa masaa mengi, jana na leo. Nimefurahi kwa namna ambayo siwezi hata kuelezea. Nategemea kuandika taarifa mbali mbali za ziara hii siku zijazo.  0 0
 • 04/29/13--20:00: ngoma azipendazo ankal

 • Mb Dogg alitoka na ngoma yake ya 'Latifah'

  0 0

   Mashindano ya kwanza ya ulimbwende nchini yalifanyika mwaka 1967 katika hoteli ya Kilimanjaro ambapo mshindi aliibuka mrembo Theresia Shayo (namba 5) kabla ya kupigwa marufuku kwa kile kilichosemekana wakati huo kukosa maadili
   Miss Tanzania wa kwanza Theresia Shayo akipita pembeni mwa bwawa la kuogelea
  Huko Zanzibar nako mashindano ya ulimbwende yalifanyika kwa mara ya kwanza (na ya mwisho, kwani hayajafanyika tena hadi leo) na mshimdi alikuwa Bi Hediye Khamis Mussa (katikati) hii ilikuwa Januari 13, 1968
   Mwaka 1994 Miss Tanzania ikaibuka tena na mshindi alikuwa Aina Maeda
  Miss Tanzania 1994 Aina Maeda akiwa na mshindi wa pili Lucy Ngongoseke Kihwele (shoto) na wa tatu alikuwa Dotto Abuu.

  0 0
 • 04/29/13--20:03: KUMBUKUMBU
 • MIKAH GODWIN KOBOLE (1970 - 2012)

  Leo tarehe 30/04/2013 - Ni mwaka mmoja tangu Ndugu yetu mpendwa ulipotangulia mbele ya haki katika Hospitali ya Hindu Mandal - DSM. Mnamo saa 4 za asubuhi.

  Hakika tulikupenda sana kwa uwazi, ushirikiano na ukweli wako kwetu sote. Tulikupenda sana lakini Mungu alikupenda zaidi. Tutaendelea kukuenzi kwa kukumbuka mawaidha yako mazuri sana kwetu.

  Unakumbukwa sana na Mama yako (Agnes Mgaya) ,Mkeo (Hawa) ,Wanao (Agnes na Patrick), Dada zako (Martha, Jane na Gloria), Baba zako wadogo, Shangazi zako bila kusahau wafanyakazi wenzako, marafiki na majirani wote.

  Bwana ametoa, Bwana ametwaa
  Jina la Bwana lihimidiwe

  0 0
 • 04/29/13--22:39: KIJIWE CHA UGHAIBUNI

 • 0 0

  Washiriki wakichukua taarifa muhimu wakati wa mkutano kuhusu Mchango wa Utumishi wa Umma katika Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano uliofanyika tarehe 29-30 Aprili,2013 Dar es Salaam Serena Hotel.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (MB) akiongea na vyombo vya habari baada ya kufungua mkutano kuhusu Mchango wa Utumishi katika Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano uliofanyika tarehe 29-30 Aprili,2013 Dar es Salaam Serena Hotel.
  Katibu Wakuu Viongozi wastaafu Bw.P.Luhanjo (kushoto) na Dokta.M.Lumbanga (kulia), katikati ni Katibu Mkuu-utumishi mstaafu Bw.J.Ruguyamheto wakisikiliza mada wakati wa mkutano kuhusu Mchango wa Utumishi katika Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano uliofanyika tarehe 29-30 Aprili,2013 Dar es Salaam Serena Hotel.
  Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Dokta.M.Lumbanga na Katibu Mkuu-Utumishi mstaafu Bw. J.Rugumyamheto wakibadilisha mawazo na Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw. HAB Mkwizu, pamoja na wajumbe wengine wakati wa mkutano kuhusu Mchango wa Utumishi katika Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano uliofanyika tarehe 29-30 Aprili,2013 Dar es Salaam Serena Hotel.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (MB) mstari wa kwanza katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano kuhusu Mchango wa Utumishi katika Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano uliofanyika tarehe 29-30 Aprili,2013 Dar es Salaam Serena Hotel.

  0 0

  Adolph, Brian au Thadeo Lwakajende Enzi ya uhai wake

  TUNAPENDA KUWATAARIFU KUWA MAZISHI YA MPENDWA WETU MAZISHI YATAKAYOFANYIKA JUMATANO MAY 1, 2013

        RATIBA YA MAZISHI MAY 1, 2013 NI KAMA IFUATAVYO

       VIEWING:            LEE.O.WOOD FUNERAL HOME
                                        23 EAST 2ND STREET
                                       MT.VERNON,NY,10552   
                                      TIME:  10:00 AM/ 4 ASUBUHI

       MAZISHI :                  MT.PLEASANT CEMETERY 
                                        80 COMMERCE STREET
                                         HAWTHORNE,NY,10532 
                                         TIME: 1:00PM/7 MCHANA


  BAADA YA MAZISHI TUTAELEKEA


  374 HAWTHORNE TERRACE
  MT.VERNON,NY,10552
  KWA CHAKULA

    KWA MAELEKEZO ZAIDI WASILIANA NA:

     RAHMA ADAM.........617 818 7657
    PETER LUANGISA...917 681 6971
    RASHIDI KAMUGISHA...973 703 4596
    BERNARD KIVUGO.......973 580 7166
    WILLIAM VEDASTO......973 551 2916

  TAFADHALI MTAARIFU MTANZANIA MENZAKO UKIPATA UJUMBE HUU.  

  0 0


  Barabara hii ni ya kutoka Singida kuelekea Shelui mpaka Igunga Mkoani Tabora,na hapa ni katika kijiji cha Ntondo kilichopo Mkoani Singida.Shukrani kwa wadau wote waliojaribu kujibu Chemsha Bongo hii ambayo haikuwa na Zawadi.

  0 0

  Kamishna wa Maadili,Jaji mstaafu Salome Kaganda (aliesimama mbele kushoto) akisoma utangulizi wakati wa Semina ya maadili ya viongozi wa serikali inayoendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala bora) Mh. George Mkuchika akifungua Semina ya maadili ya viongozi wa serikali inayoendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Blue Peal,Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam..

  0 0


older | 1 | .... | 116 | 117 | (Page 118) | 119 | 120 | .... | 3278 | newer