Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 117 | 118 | (Page 119) | 120 | 121 | .... | 3285 | newer

  0 0
 • 04/30/13--01:14: kumbukumbu

 • DR. FRANCIS MW. MSELLEMU


  Baba, ni miaka 17 sasa tangu ulipotuacha!

  Haijawahi kuwa rahisi kwetu, kwani kila iitwapo leo machungu na majonzi yetu ni kama jana.


  Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia nafasi ya kuwa na Baba kama wewe, na nafasi ya kuishi nawe kwani kwetu  ulikuwa Rafiki na  Mwalimu.


  Kwa Mapenzi  ya Mwenyezi Mungu,  tunaendelea kukua kiimani tukiamini kwamba ipo siku moja tutakutana nawe tena.


  Pumzika kwa Amani Baba!


  0 0


  0 0

  Queen Beatrix of the Netherlands has handed the throne to her son Prince Willem-Alexander.

  Queen Beatrix, 75, signed the instrument of abdication in Amsterdam after 33 years on the throne.

  Willem-Alexander has now become the country's first king since 1890.

  Willem-Alexander is now king, and will later be officially sworn at the Nieuwe Kerk, before a joint session of the Dutch parliament.

  His wife Máxima, a 41-year-old Argentine-born investment banker, will become queen consort.

  0 0
 • 04/30/13--02:15: Article 2


 • 0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza kuwa Skauti Mkuu nchini.

  Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue  amesema uteuzi wa Mheshimiwa Mahiza umeanza tangu tarehe 19 Aprili, 2013.

  Mheshimiwa Mahiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu ambaye amemaliza muda wake.

  Imetolewa na:

  KAIMU KATIBU MKUU
  WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

  0 0
 • 04/30/13--02:30: TAARIFA KUTOKA TFF LEO

 • 0 0
  Wakati Serikali ikipoteza mabilioni ya Pesa kwa utengenezaji na ukarabati wa barabara kila kona ya nchi, baadhi ya wananchi wachache wa Maeneo ya Kitunda Relini Kona ya Kizuiani kama inavyoonekana katika picha wamekutwa leo wakikata rami na kuaribu barabara na miundombinu kwa ajili ya kupitisha bomba la maji la mtu binafsi.

  Swali la kujiuliza Mbunge, diwani, wajumbe na wawakilishi wa Serikali za mitaa mpo wapi?? Nani ameruhusu uharibifu wa miundombinu ya maeneo haya na kwa misingi ipi??

  Muheshimiwa Magufuli na wizara yako husika tunaomba ufuatilie ili swala na wanaohusika ktk uharibifu huu wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

  0 0

   Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa KFC-Tanzania,Bwa.Simon Schaffer akizungumza na Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kuhusiana na uzinduzi wa tawi lao lilipopo Mikocheni karibia na shule ya Feza jijini Dar,Tanzania.Bwa.Simon alisema kuwa wazo la kufungua mgahawa huo nchini Tanzania,ni wazo ambalo limechukua muda wa miaka 3 kutimiza,amesema kuwa KFC itahakikisha viambata vinavyotumika kuandaa vyakula vinapatikana kutoka kwa wasambazaji waliokidhi vigezo vya viwango na ubora,aidha alibainisha kuwa Wafanyakazi wa mgahawa huo (ambao kwa asilimia kubwa ni Watanzania),walipata mafundisho ya miezi 6 kwa malengo ya kuboresha uwezo wao katika kuhudumia wateja kwenye sekta ya vyakula.

  "Nasubiri sana kwa hamu kuona jinsi Watanzania watakavyo furahia chakula na huduma za KFC,huduma zetu zimeandaliwa kwa kuzingatia jinsi ya kuwapa wateja huduma kwa haraka na ubora,tunafurahia sana kwa kuanza kuhudumia soko la Tanzania na kuleta huduma tofauti na iliyo bora zaidi",alisema Bwa.Simon.KFC ina migahawa zaidi ya 17,000 duniani historia yake ikianzia huko Kentuky nchini Marekani.
  Mmoja wa Wafanyakazi wa mgahawa wa KFC,Faraja Kilongole akifafanua  jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani), namna walivyopata mafunzo jinsi ya kuwahudumia wateja kupitia mgahawa huo,ambao ndio mara ya kwanza kufunguliwa nchini Tanzania.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgahawa wa KFC,wakishangilia jambo mara baada kuzinduliwa rasmi na kuanza kuwa tayari kuanza kuwahudumia wateja mbalimbali watakaokuwa wakiwasili kwenye mgahawa huo.

  0 0

  Urban Pulse Creative inakuletea taswira kutoka Westminister Abbey jijini London katika misa maalum ya kuombea amani nchi yetu ya Tanzania siku ya muungano iliyofanyika ijumaa tarehe 26.4.13.

  Balozi wetu Mh Peter Kallaghe, maofisa kutoka ubalozini na baadhi ya watanzania waishio nchini Uingereza walijumuika pamoja kuhudhuria ibada hii maalum na raia wengine kutoka nchi mbalimbali. Ibada ilianza kwa jumuiya ya Abbey kuwaombea watanzania wote, viongozi pamoja na wanadiplomasia wote waliopo duniani na kwa ajili ya kazi maalum ya Ubalozi wetu hapa nchini Uingereza.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA

  Asanteni,

  Urban Pulse Creative
  Mh Balozi Kallaghe akisalimia na Kiongozi wa kanisa baada ya ibada.
  Bendera yetu ikipepea.
  Kanisa la Westminister Abbey London.
  Kutoka kushoto Abu Faraji, Caroline Chipeta, Mirium Mungula na mdau baada ya ibada.
  Wazee wa kazi.
  Picha ya Pamoja.

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akifungua maonyesho ya nne ya biashara na huduma katika viwanja vya Amaan, ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, “May day”.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa maonyesho ya nne ya biashara na huduma katika viwanja vya Amaan, ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, “May day”.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikagua bidhaa mbali mbali katika maonyesho ya nne ya biashara na huduma katika viwanja vya Amaan, ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, “May day”.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikagua bidhaa mbali mbali katika maonyesho ya nne ya biashara na huduma katika viwanja vya Amaan, ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, “May day”.

  0 0

  Katibu Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (kulia) akiangalia picha ya nembo ya chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria aliyopewa na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanajeshi 22 kutoka chuo hicho wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano.
  Katibu Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (kulia) akimkabidhi picha ya wamasai Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John (kushoto) wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
  Kanali Anderson Msuya (kushoto) kutoka Jeshi la Wananchi la wa Tanzania (JWTZ) akiongea jambo na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Mchezo leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakimsikiliza Katibu Mkuu kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (hayupo pichani) wakati walipomtembea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza Joyce Fisoo akielezea kuhusu kazi za bodi hiyo kwa wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Joyce Hagu ambaye ni Kaimu Mkurugenzi msaidizi Idara ya utamaduni.
  Wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati walipoitembelea wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano. Picha na Anna Nkinda – Maelezo.

  0 0

  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkaribisha Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman alipofika kumtembelea Ofisini kwake Dodoma leo na kufanya nae mazungumzo.
  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman alipofika kumtembelea Ofisini kwake Dodoma.
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake wakimsikiliza Spika wa Bunge Ofisi Kwake leo. Jaji Mkuu na Ujumbe wake walimtembelea Mhe. Spika na kufanya nae Mazungumzo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Mbunge wa Maswa (CHADEMA) Mhe. John Shibuda akimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman kuelekea Ofisi ya Spika alipofika viwanja vya Bunge leo. Jaji Mkuu na Ujumbe wake walimtembelea Mhe. Spika na kufanya nae Mazungumzo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde akieleza jambo kwa hisia Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman katika viwanja vya Bunge leo.
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman akisalimiana na Mhe. Ngeleja Bungeni leo. PICHA ZOTE NA OWEN MWANDUMBYA WA BUNGE

  0 0

   Maeneo mbali mbali ya jiji la Dar siku ya leo yalikuwa hayapitiki kabisa kutoka na foleni kubwa ambayo haikufahamika ilianzia wapi,maana si njia za barabarani wala za mitaani zilizokuwa zikipitika.kila mahala kulikuwa na msongamano wa magari.zifuatazo ni picha za hali ilivyokuwa maeneo mbali mbali ya jiji la Dar mchana wa leo.

  0 0


   Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa Tawi la CCM Mzuri wilaya ya Kusini Unguja,alipofanya ziara ya kuimarisha Chama leo.
   Vijana wa CCM katika Kijiji cha Bwejuu,wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,alipotembelea katika Tawi la CCM la Kijiji hicho akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja leo.
   Baadhi ya wananchi na wanachama wa Tawi la CCM Bwejuu kaskazi wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza wakati alipotembelea Tawi lao akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama katika Mkoa wa Kusini Unguja leo.
   Wanachama wapya wa CCM wakilakiapo cha Utii kwa Chama cha Mapinduzi baada ya kukabidhiwa kadi zao za Chama na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,alipofanya ziara ya kuimarisha Chama katika Wilaya ya Kusini Unguja leo.
  Baadhi ya wananchi na wanachama wa Tawi la CCM Bwejuu kaskazi wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza wakati alipotembelea Tawi lao akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama katika Mkoa wa Kusini Unguja leo. [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0


  Salam,
  Urban Pulse wanakuletea music video ya msanii Mish Da Fyah Sis inayokwenda kwa jina la Roll Like Dem ikiwa ni single ya kwanza ya album yake itakayo kuja hivi karibuni.

  Urban Pulse Creative is proud to share exclusive access to the behind the scene of the Music video for their Upcoming artist Mish Da Fyah Sis featuring Pascal titled BAD GYAL. The track was produced by Furious T, shot and directed By Frank for Urban Pulse Creative Media.
  Take a peek  Behind the Scene of Bad Gyal Music Video

  0 0
 • 04/30/13--20:00: Ngoma azipendazo ankal

 • Ngoma ya 'Mume Bwege' ya Bushoke sio tu ilifurahisha bali pia ilikuna vichwa na kumtoa kijana huyu

  0 0

  Mnara wa Askari jijini Dar es salaam enzi hizi na hizi sasa.
  Hii  ni kumbukumbu ya askari jeshi waliopigana katika vita ya kwanza ya dunia inayosimama kuangalia bandari ya jiji hilo. 
  Ilizinduliwa mwaka 1927. Sanamu hiyo ya askari wa British Carrier Corps iliundwa Uingereza na mchonga sanamu Mwingrereza aitwaye James Alexander Stevenson ambaye katika sanamu hii katumia jina lake la kufikirika la “Myrander”. 
  Kabla ya kupelekwa Dar es salaam sanamu hii ya Askairi ilioneshwa kwa muda jijini London katka Royal Academy. Kabla ya kuwekwa sanamu ya askari, mahali hapa palikuwa na sanamu ya Meja Herman von Wissman, gavana wa wakati huo wa German East Africa, iliyozinduliwa mwaka 1911. Waingereza walipoingia Dar es salaam mwaka 1916, waliibomoa sanamu ya gavana wa Kijerumani pamoja na zingine za Karl Peter na Otto vo Bismarck zilizokuwa hapo. Sanamu ya askari ya Dar es salaam ni moja kati ya tatu zilizozinduliwa wakati mmoja kati ya tatu zilizoweka katika mwaka huo wa 1927 sehemu za koloni ya Uingereza ya Afrika Mashariki (British East Africa). Zingine mbili zilikuwa Mombada na Nairobi.  0 0
 • 04/30/13--20:06: kumbukumbu

 • Bwana na Bibi Kanza.

  Wapendwa wetu, ilikuwa siku, wiki, mwezi na hatimaye tarehe 01/05/2013 mmetimiza miaka minne (4) toka mtutoke kwa ajali ya gari katika hii dunia. Tunafarijika kwa sababu tuna Imani mpo pamoja nasi Kiroho siku zote.

  Hakuna siku ipitayo kwetu bila kuwakumbuka kwa UPENDO, UKARIMU, USHAURI MWEMA, MSIMAMO BORA NA BUSARA ZENU. Hakika BUSARA ZENU zimekuwa dira na nuru katika maisha yetu. Tunaendelea kuwaombea na tutaendeleza yale yote mema mliyotuachia.

  Daima mnakumbukwa na watoto wenu, Bright Kanza na Alvin Kanza, Mr & Mrs T. Kweka, Mr & Mrs G. Kanza, wadogo zenu wote, wajomba, shangazi, ndugu, jamaa na marafiki. Daima tutawakumbuka Milele.

  Sisi tuliwapenda sana, lakini Mungu Baba wa Mbinguni aliwapenda nyinyi zaidi. Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe. Amen!!

  0 0

  Habari na Picha na 
  Ramadhan K. Namkoveka
  Timu ya Tanzania ya kuogelea imerudi jjumatatu saa 1.30 usiku ikitokea Lusaka, Zambia, baada ya kushiriki mashindano ya CANA kanda ya tatu na nne yaliyoshirikisha nchi 10 za Afrika mashariki, kati na kusini. Mashindano hayo yalifanyika kuanzia tarehe 25 hadi April 28 katika maeneo ya kituo cha maendeleo ya olimpiki. 
  Timu ya Tanzania ilikuwa na wachezaji 18, hata hivyo haikuweza kupata medali tofauti na ilivyotarajiwa. Hata hivyo waliiweza kuimarisha muda wao ambayo inaonyesha kwa kuogelea Tanzania inakuwa siku hadi siku. 
  Sonia Tumiotto alitokeza wa nne kwa kutumia muda wa 3.17.75 katika mtindo wa Breaststroke. Shamrad Magesvaran kwenye mita 50 backstroke aliweza kutumia muda wa sekunde 36.13 ambapo mshindi alikuwa ni Luan Grobbelaar kutoka Afrika Kusini. 
  Muda wa kufuzu mashindano ya dunia yatakayofanyika Barcelona mwezi Julai mwaka huu ni sekunde 23.11 kwa muda B ambapo Hilal alitumia sekunde 25.36. Hii inaonyesha kuwa karibuni tu mchezo utatoa matunda mazuri.
   Licha ya kuwa mashindano yalikuwa ni magumu lakini tulifarijika wakati balozi wa Tanzania nchini Zambia mheshimiwa Grace Joan Mujuma alipoweza kuhudhuria mashindano hayo ya siku nne jukwaani pamoja na viongozi waliombatana na timu hiyo ikiongozwa na Ramadjhan Namkoveka na pia baada ya mashindano aliialika timu imtembelee ofisini kwake. 
   Hilal Hilal akiruka ktk 100 freestyle

   Shamrad Magesvaran akiogelea 200 freestyle
   Sonia Tumiotto akiogelea mita 400 freestyle
   Balozi Grace Mujuma (tshet nyekundu) akiwa na timu ya Tanzania katika  mashindano ya kuogelea jijini Lusaka
   Balozi Grace Mujuma(kushoto) akiwa jukwaani akiangangalia mashindano ya kuogelea
  Tanzania ya kuogelea imerudi jijini Dar es salaam ikitokea Lusaka,
  Viongozi wa timu ya kuogelea Tantzania walipoenda kumsalimia ofisin kwake Balozi wa Tanzania nchini Zambia

  0 0  Mchora vibonzo Nathan Mpangala aka Kijasti, (wa pili kulia) akishiriki mafunzo ya utengenezaji video fupifupi zihusuzo migogoro isiyo na mapigano iliyofanyika mwezi uliopita nchini Mexico. Mafunzo hayo yaliyoshirikisha washiriki 80 kutoka nchi mbalimbali yalitolewa na School of Authentic Journalism ya nchini humo. Baada ya darasa huko Mexico, Kijasti alipata nafasi ya kutalii jijini New York. Kumuona huko BOFYA HAPA


older | 1 | .... | 117 | 118 | (Page 119) | 120 | 121 | .... | 3285 | newer