Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

MABONDIA WANNE WAPIGWA PINI.

$
0
0
MABONDIA WANNE WAPIGWA PINI AKIWEMO THOMAS MASHALI, FRANSIC MIYEYUSHO, NASSIB RAMADHANI NA RAMADHANI SHAULI KUCHEZA NA MABONDIA KUTOKA NJE MEI 14 DAR ES SALAAM.

Bondia THomasi Mashali katikati akisaini mkataba mbele ya katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa PST Anton Ruta kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa wa Dunia na muirani Sajjad Mehrabi utakaofanyika mei 14 katika uwanja wa ndani wa taifa kushoto ni bondia Fransic Miyeyusho.
Bondia Ramadhani Shauli kushoto akisaini mkataba wa kuzipiga Mei 14 na bondia Salim Salim kutoka Malawi katikati ni katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa PST Anton Ruta na kocha wa bondia huyo Cristopher Mzazi.
Bondia Nassibu Ramadhani akisaini mkataba wa kuzipiga na bondia kutoka nje ya nchi mbele ya katibu mkuu wa chama cha gumi za kulipwa PST Anton Ruta kulia na kocha wa bondia huyo Cristopher Mzazi.
Bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' kushoto akisaini mkataba wa kuzipiga na bondia kutoka nje siku ya mei 14 katika uwanja wa ndani wa tasifa kushoto ni kulia ni katibu mkuu wa PST Anton Ruta katikati ni bondia Thomas Mashali .
Picha na SUPER D BOXING NEWS

SHULE ZA MSINGI WINGWI ZAPATIWA VITENDEA KAZI

$
0
0

Na Waandishi wetu, Pemba
Shule za msingi Mtemani, Wingwi msingi na Simai zote za Wingwi, wilaya ya micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, zimepatiwa msaada wa vifaa vya kisasa vya kutendea kazi kwa ajili ya kuleta ufanisi kazini.
Msaada huo uliotolewa na mhadhiri kutoka chuo kikuu cha SOAS, London, nchini Uingereza Mwalimu Yussuf Shoka Hamad, ulijumuisha mashine ya kompyuta za dawatini, mashine ya kutolea fotokopi, kupigia skani na kuchapishia barua na hati mbali za kiofisi.
Katika hafla fupi iliyoandaliwa na shule hizo jana (Jumatatu) mchana, Bwana Yussuf alisema kuwa lengo na nia yake ni kuzisaidia shule zote za Wingwi kwa kuzipatia vitendea kazi vya kisasa ili kukuza ufanisi na kuendana na maendelea ya sasa ya dunia ya sayansi na teknolojia.
‘Lengo langu si kujijenga kisiasa. Mimi si mwanasiasa, naruadia kusema hivi na naisitiza tena kwamba sitoi misaada hii kwa madhumuni ya kisiasa. Mimi ni mzaliwa wa Wingwi na ari ya uzawa na mchango nilioupata kwa jamii yangu ya Wingwi ni miongoni mwa misukumo inayonipelekea kutoa misaada hii bila kuchoka na bila kujali thamani, ukubwa au udogo wa vitu hivyo ninavyotowa’.

Bwana Yussuf pia aliongezea kwa kusema nia yake hasa ni kuzibadilisha shule zote za Wingwi na kuzifikisha katika kiwango cha ubora wa shule za kisasa kivitendea kazi ifikapo mwaka 2020. Moja kati ya mikakati yake ya kufikia lengo hilo ni kuhakikisha kila shule inapata mashine za kutolea kopi (photokopi) zenye uwezo wa kuchapisha mitihani ya ndani ya wanafunzi, kujenga maktaba za ndani ya shule hizo na kuzipa uwezo wa vifaa vya asili na vile vya kisasa ili kukuza kiwango cha elimu nchini.
Katika hafla hiyo, Bwana Yussuf aliahidi kuzipatia shule hizo mashine za kutolea photokopi (kubwa) ifikapo mwakani ambapo kila shule itaweza kujitegemea kwa vitendea kazi vyenye uwezo na ubora wa kisasa.Wakitoa shukrani zao kwa Mwalimu huyo, Walimu wakuu wa shule hizo walimpongeza Mwalimu Yussuf kwa uzalendo na moyo wake wa kujitolea na hasa katika kusaidia sekta ya elimu ya shule hizo za Wingwi.
 
‘Kwa kweli msaada huu ni mkubwa kwetu kiasi ambacho hatujui jinsi gani tufikishe shukrani zitakazofikia thamani ya msaada huu. Tunashukuru sana na tunakutakia heri na fanaka katika kazi zako ili uweze kusaidia zaidi katika sekta hii ya Elimu ya shule zako za Wingwi.’ Aliema Mwalimu Mohammed Hamad wa Shule ya Msingi Simai.
Naye Mwalimu mkuu msaidizi wa Shule ya msingi Wingwi, Bwana Khamis Rashid alimshukuru na kumpongeza Bwana Yussuf Shoka kwa hatua yake hiyo ya kukumbuka kusaidia shule za Wingwi ambako yeye (Yussuf) alisomea hapo.

Msaada huu wa zawadi uliotolewa ni moja ya sehemu za ahadi alizitowa Bwana Yussuf wakati wa hafla ya kuwazawadia wanafunzi waliofaulu mitihani yao ya darasa la saba mwaka jana ambapo kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule hizo kimeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Mwalimu Yussuf Shoka Hamad akikabidhi vifaa kwa Mwalimu mkuu shule ya msingi Simai, Wingwi, Mw. Muhammed Hamad.

Mwalimu Yussuf Shoka Hamad akikabidhi vifaa kwa Mwalimu Khamis Rashid wa Shule ya Msingi Wingwi 

MESSAGE ON THE INTERNATIONAL DAY OF REFLECTION ON THE GENOCIDE IN RWANDA

$
0
0
U N I T E D   N A T I O N S                                   N A T I O N S   U N I E S

THE SECRETARY-GENERAL

In 1994, more than 800,000 people were systematically murdered throughout Rwanda. The vast majority were Tutsi, but moderate Hutu, Twa and others were also targeted. On this Day, we remember all who perished in the genocide and renew our resolve to prevent such atrocities from ever being repeated, anywhere in the world.

We should all be inspired by the survivors’ courage in showing that reconciliation is possible even after such a tragedy. With the Great Lakes region still facing serious threats to peace and security, healing and reconstruction remain essential.

Honouring the victims of the genocide in Rwanda also means working for justice and accountability. I commend United Nations Member States in the region and beyond for their continued efforts to arrest and hand over remaining fugitives and end impunity. The best way to ensure that genocide and other egregious violations of human rights and international law can never occur again is to acknowledge shared responsibility and commit to shared action to protect those at risk.

Genocide is not a single event. It is a process that takes time and preparation. History has repeatedly demonstrated that no part of the world is immune. One of the key warning signs is the spread of hate speech in public discourse and the media that targets particular communities.

The theme of this year’s observance is “Fighting Genocide Ideology”. It is essential that Governments, the judiciary and civil society stand firm against hate speech and those who incite division and violence. We must promote inclusion, dialogue and the rule of law to establish peaceful and just societies.

The history of Rwanda teaches us an essential lesson. While the capacity for the deepest evil resides in all societies, so too do the qualities of understanding, generosity and reconciliation. Let us nurture these hallmarks of our common humanity to help build a life of dignity and security for

KAMPUNI YA MAFUTA YA TOTAL YAWAKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA SHINDANO LA "START UPPER OF THE YEAR BY TOTAL CHALLENGE"

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya TOTAL Tanzania, Tarik Moufaddal akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la wajasialiamali hapa nchini ambapo washindi watatu bora wajasiliamali walikabidhiwa zawadi zao na kampuni ya TOTAL katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni thelathini na tano Mshindi wa Kwanza, Iddi Kalembowa pili kutoka kuliakatika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya TOTAL Tanzania na washindi wa shindano la wajasiliamali mara baada ya wajasiliamali hao kukabidhiwa zawadi zao katika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa shindano la wajasiliamali la kampuni ya Mafuta ya TOTAL iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

MKUU WA WILAYA YA BABATI AIFUNGA SHULE KUFUATIA KUHARIBIKA KWA VYOO.

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela
Na Woinde Shizza,Manyara

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Crispin Meela ameifunga shule ya msingi Matufa kwa muda usiojulikana baada ya kutitia kwa matundu ya vyoo vya wanafunzi na walimu kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazonyesha.

Akizungumza baada ya kuitembelea shule hiyo, Meela alisema kutokana na matundu  24 ya vyoo vya shule hiyo kuharibika inabidi shule hiyo ifungwe kwani hakuna vyoo vingine vya kutumiwa kwa wanafunzi na walimu. Hata hivyo, kaya 64 zilizokuwa zinaishi kwenye shule hiyo ya Matufa kwa kukosa makazi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizonyesha siku mbili hivi sasa wamepatiwa hifadhi kwa kuwekwa kambini.

Alisema kutokana na maafa hayo hana budi kuifunga shule hiyo kwa muda usiojulikana na anatarajia watahakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi kwa muda mfupi kupitia ushirikiano wa viongozi wa wilaya na mkoa huo. “Namuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Babati vijijini Dominick Kweka, kuhakikisha shule hiyo inajengewa vyoo mara baada ya wiki moja kupita ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao,” alisema Meela.

Kwa upande wake, mbunge wa jimbo la Babati vijijini Vrajlal Jitu Soni aliwapa pole wakazi wa vijiji vya Magugu na Matufa vilivyopo kwenye tarafa ya Mbugwe ambao wameathirika kutokana na mafuriko hayo. Jitu Soni alisema hivi sasa wanafanya tathmini ya mafuriko hayo ili kamati ya maafa kupitia ofisi ya Waziri Mkuu waweze kuwapatia msaada wananchi hao ambao nyumba na mazao yao yamechukuliwa na mafuriko hayo.

TPDC yachangia madawati 500 Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

$
0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara imepokea jumla ya madawati  500 kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Akiongea wakati wa kupokea madawati hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego alisema msaada huu unamaliza kabisa tatizo la madawati kwa kata zote za kijiji cha Madimba na Msimbati. Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alisema kwamba TPDC itaendelea kutoa misaada katika maeneo ambayo inafanya shughuli zake lengo likiwa ni kuboresha maisha wa wananchi wa maeneo hayo na kufaidika na shughuli za utafiti na uendelezaji wa gesi na mafuta.  
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio akikabidhi rasmi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego.
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego na Mbunge wa Mtwara Vijijini. Mhe. Hawa Ghasia wakifurahia kwa pamoja baada ya TPDC kukabidhi madawati kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Madimba wakiwa wamekaa katika madawati waliyopokea kutoka TPDC.

MIUNDOMBINU INAYOLETA MAJI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM YAENDELEA KUJENGWA

$
0
0
Msimamizi wa ujenzi wa Mradi wa bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 40 ambalo liko katika hatua  za mwisho  za ujenzi kutoka DAWASA Mhandisi Christian Gava akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiufundi kuhusu mradi huo.

Moja ya daraja linapopitisha bomba hilo kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 40linavyoonekana mara baada ya kukamilika eneo la Kibamba.

 Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Jamii wa DAWASA Bi. Neli Msuya akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa bomba hilo.
 Wataalam wa ujenzi kutoka DAWASA na kampuni ya Megha Engineering & International Ltd inayojenga bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es salaam India wakiangaliamoja ya matoleo 12 yanayopita chini ya barabara kuu ya Morogoro eneo la kimara.

UMOJA WA ULAYA(EU) WAZINDUA PROGRAMU WA KUZISAIDIA ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI HAPA NCHINI.

$
0
0
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer kizungumza jambo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa programu ya kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika jana. Picha na Geofrey Adroph
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya(EU) kutoka Brussels, Bi Rosario Bento Pais akizungumzia masuala ya kuzisaidia asasi zisizo za kiserikali ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa maana hizo zinawalenga watu katika jamii husika.
Mwakilishi wa asasi za kiraia, Bw. Francis Kiwanga akizungumza juu ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya(EU) ulivyoamua kuzisaidia asasi zisizo za kiserikali za Tanzania Bara pamoja na Zanzibar. Maeneo ambayo Umoja wa Ulaya inajikita nayo katika asasi zisizo za kiserikari ni tatu amabazo ni kuweka mazingira bora kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kufanya kazi katika mazingira bora hapa nchini, pili ni kuyajengea uwezo mashirika hayo na mwisho nikufanya kazi katika Sere pamoja na sheria ili kuwa na sheria bora na nzuri kwa maendelea ya nchi yetu.

Picha ya Pamoja.

The Goats are Back! Dar es Salaam Charity Goat Races will take place from noon, on Saturday, 10 September at The Green on Kenyatta Drive

$
0
0

DAR ES SALAAM, Thursday, 7 April 2016 –  Since the first race was held in 2001, the Dar es Salaam Charity Goat Races have raised over 1 billion shillings for local charities, and in their 16thyear are on track to continue raising funds. 
The 2016 Dar es Salaam Charity Goat Races will take place from noon, on Saturday, 10 September at The Green on Kenyatta Drive. 
Dar es Salaam Charity Goat Races Committee Co-Chair, Rachel Carlin, says the continued support the Goat Races receives from the community is invaluable. 
„Each year we are able to put on this event because of the support from a number of sponsors and of course the people who attend the event,‟ she said. 
„And with the date set, we are encoring people and organisations to become a goat owner for the day. 
„Owning a goat is a lot of fun, especially if it wins; but it is also a good way to get behind the races and help us raise money,‟ Ms Carlin added. 
With goat numbers limited, prospective owners are encouraged to visit the website and download a form to avoid disappointment. 
For those wanting to don a costume and try their luck in the fancy dress parade, the theme for this year‟s Goat Races – A Day At The Races – provides plenty of inspiration. The theme is open to various interpretations which promises it to be a fun and colourful event

 „While it is all a bit of fun, the reason we organise this event each year is to raise funds for local charities, so I also request any registered Tanzanian charity to visit our website and download an application form,‟ Janine Deetlefs Committee Co-Chair said. 
Help2kids is an NGO that focuses on vulnerable children’s educational needs, providing them with the necessary resources to continue their primary and secondary education. 
“The Dar es Salaam Charity Goat Races enabled help2kids to finally complete their goal of creating a sanitation block at our partnered Primary school,” remarked Justine LeDonne, Field Manager at Help2kids. 
“The Goat Race charity provides both small and large organizations like ours to improve upon current projects in Dar es Salaam. With every-day running costs a priority in the efficiency of small NGOs, making large improvements on current projects can get pushed aside for years without the proper funding. The Goat Races enables those ideas and projects to come to light,” she further remarked. 
A volunteer committee organizes the Dar es Salaam Charity Goat Races, and many other volunteers lend a hand on the day.  
„At the end of the day, the goat races wouldn‟t happen if it wasn‟t for the sponsors, and as always a large number of organizations have come out to support the races in 2016.

 „I would particularly like to acknowledge the support of our race sponsors: Southern Sun Hotel, Tanzanian Breweries Limited, Coca-Cola (Kwanza), Tigo, Stanbic Bann, Toyota Tanzania and Regent Tanzania Limited as well as SWISS and Continental Outdoor.‟ Ms Deetlefs concluded.  

Those interested in buying a goat, or helping out on the day are encouraged to contact the Dar es Salaam Charity Goat Races. 

LULU DIVA: KUOLEWA NA WIZIKID?

Kamati ya PIC Yaitaka Serikali Kuisaidia TTCL Ijiendeshe Kibiashara.

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam.Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (hayupo pichani) katika mkutano na wanahabari leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (hayupo pichani) katika mkutano na wanahabari leo jijini Dar es Salaam.Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akipitia nakala ya taarifa ya Kampuni ya Simu nchini (TTCL) jujiridhisha na takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akipitia nakala ya taarifa ya Kampuni ya Simu nchini (TTCL) jujiridhisha na takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.

KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imeitaka Serikali kutekeleza kwa vitendo ahadi zake za kuiwezesha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kujiendesha kibiashara. Akitoa maazimio ya Kamati ya PIC leo Dar es Salaam baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini TTCL, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya PIC, Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) alisema, ili TTCL iweze kutekeleza jukumu lake kwa Taifa, Serikali iharakishe utekelezaji wa ahadi zake kwa Kampuni hiyo Kongwe ya Mawasiliano nchini. "Serikali ikamilishe kwa haraka mchakato wa kuondoka kwa Kampuni ya Bharti Airtel ndani ya TTCL, mchakato huu umechukua muda mrefu sana, ni vyema sasa ukatekelezwa sambamba na kuisaidia TTCL kupata malipo yake inayodai kutoka kwa Wateja wake zikiwemo taasisi za Serikali," alisema Bi. Bukwimba.

 Aidha Mhe Bukwimba aliongeza kuwa, Kamati ya PIC inaiagiza Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuharakisha mchakato wa kukabidhi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa TTCL ili utumike kibiashara na kwa ufanisi zaidi kuliko hivi sasa ambapo umiliki wake haupo bayana.Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam.[/caption] Alisema kwa kipindi cha miaka 15 hivi sasa Serikali haijafanya uwekezaji wa aina yoyote ndani ya TTCL hivyo kuitaka kuwekeza ili kampuni iweze kusonga mbele kibiashara. "...Kwasababu huwezi kutegemea kupata mapato mazuri bila kuwekeza uwekezaji wa aina yoyote...miaka kumi na tano ni mingi mi nauhakika wakiwekeza fedha wataweza kuisaidia kampuni kuiuwisha na kuweza kufanya shughuli zake vizuri kama taasisi zingine.

." Agizo jingine la PIC kwa Serikali ni kuiongezea TTCL wigo wa kutumia rasilimali zake kama dhamana ili kupata mitaji kutoka taasisi za fedha na kufanikisha mpango wa kampuni hiyo wa kufanya mageuzi ya kibiashara. Awali, Wabunge waliochangia hoja katika kikao hicho, waliitaka Bodi na Menejimenti ya TTCL kusimamia kikamilifu mipango mizuri ya kibiashara iliyowasilishwa mbele ya Kamati. Wabunge Esther Matiko (Tarime Mjini), Steven Ngonyani (Korogwe) Riziki Lulida (Viti Maalum), Sabrina Sungura (Viti Maalum), na Frank Mwakajoka (Tunduma) wamesema, Seriki inao wajibu mkubwa wa kuisaidia TTCL ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa ikipitia kipindi kigumu hasa kutokana na uwekezaji usio na tija uliofanywa ndani ya Kampuni hiyo.

MIUNDOMBINU YA KULETA MAJI JIJINI DAR ES SALAAM YAENDELEA KUJENGWA.

$
0
0
 Msimamizi wa ujenzi wa Mradi wa bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 40 ambalo liko katika hatua  za mwisho  za ujenzi kutoka DAWASA Mhandisi Christian Gava akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiufundi kuhusu mradi huo. Kushoto ni Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Jamii wa DAWASA Neli Msuya.
 Wataalam wa ujenzi kutoka DAWASA na kampuni ya Megha Engineering & International Ltd inayojenga bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es salaam India wakiangalia moja ya matoleo 12 yanayopita chini ya barabara kuu ya Morogoro eneo la kimara.
 Moja ya daraja linapopitisha bomba hilo kutoka Ruvu Juu Mlandizi hadi Dar es salaam lenye urefu wa km 40 linavyoonekana mara baada ya kukamilika eneo la Kibamba. 
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.

Na.Aron Msigwa - MAELEZO.
MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam ( DAWASA) imesema kuwa wakazi zaidi wa jiji la Dar es salaam na Kibaha mkoani Pwani wanatarajia  kunufaika na huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama ifikapo Juni mwaka huu kufuatia mradi wa ujenzi wa bomba jipya la maji kutoka Ruvu Juu Mlandizi, Kibaha hadi jijini Dar es salaam kuwa katika hatua  za mwisho za ujenzi.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Jamii wa DAWASA Neli Msuya ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam mara baada ya kutembelea eneo Kimara na Kibamba ambako mafundi wa Kampuni inayojenga mradi huo ya Megha Engineering & International Ltd kutoka India wanaendelea na kazi ya ujenzi wa madaraja na matoleo ambayo bomba hilo linapitia katika barabara ya Morogoro.

Amesema hadi kukamilika kwake mradi huo utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni 59.3 na utawezesha kiasi cha Lita milioni 196 za maji kusafirishwa kwa siku ambazo zitaongezwa kwenye lita milioni 270 zinazozalishwa kwa siku na Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini ulioko Bagamoyo mkoani Pwani.

Ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaondoa kabisa tatizo la uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ambayo yameunganishwa na mtandao wa mabomba ya DAWASCO ambayo yalikua hayapati maji kwa muda mrefu au kupata kwa mgawo kufikia mwezi Juni, 2016. 

Bi. Neli amesema kuwa ili kuhakikisha mradi huo unakamilika katika kipindi kilichopangwa na kuanza kuwanufaisha wananchi, ujenzi wake unakwenda sambamba na umaliziaji wa tenki jipya la kuhifadhia maji lililoko eneo la Kibamba lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 10 ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98.

 Aidha, amesema kuwa kazi ya ukarabati wa matenki ya zamani yaliyoko eneo la Kimara jijini Dar es salaam inaendelea sambamba na ubadilishaji wa mifumo ya mabomba ya zamani ambayo sasa ni chakavu ili iweze kuhimili wingi wa maji uliopo.

" DAWASA tumeshaingia mkataba na Mkandarasi kwa ajili kulaza upya mabomba ya maji kwa wananchi wasiounganishwa na maji ili waweze kuingia kwenye mtandao wa mabomba yetu, kazi hii inaendelea katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kimara, Mlandizi,Kibaha, Kwembe, Segerea, Changanyikeni, Mbezi na Makuburi" Amesema.

Bi. Neli ameongeza kuwa baadhi ya maeneo yataanza kupata mabadiliko ya huduma ya maji kuanzia mwezi Mei kufuatia maji yatakayosukumwa kutoka Ruvu, Mlandizi kuanza kutoka katika kituo cha kwanza kwenye tenki la maji la Kibamba.

“Tunatarajia wananchi waliounganishwa na mtandao wataanza kuona mabadiliko kuanzia mwezi Mei, japo sasa kuna maeneo yana mgawo wa Dawasco,lakini baada ya maji haya kufika na kuanza kutoka kwenye kituo cha tenki la Kibamba wananchi watakua na maji ya kutosha" Amesisitiza.

Kwa upande wake Msimamizi wa ujenzi wa Mradi huo kutoka DAWASA Mhandisi Christian Gava akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiufundi kuhusu mradi huo amesema kuwa ili kukamilisha ujenzi wa mradi huo imewalazimu kujenga maungio 15 ambayo bomba hilo linavuka mito na matoleo 12 yanayopita chini ya barabara kuu ya Morogoro.

Amesema kazi ya wekaji wa miundombinu ya kulifanya bomba lipite juu ya mto kupitia madaraja yaliyojengwa imefanyika kwa umakini mkubwa ili kuepuka kuathiri uasili wa mito husika.

Aidha, amesema kuwa ili kulinda bomba hilo na athari za mafuriko katika mito hiyo ulifanyika utafiti maalum ukihusisha upimaji wa kimaabara wa udongo ili kubaini namna udongo huo unavyoweza kubeba nguzo kubwa zilizoshika bomba hilo.

Mhandisi Gava ameongeza kuwa ujenzi wa tenki la maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 10 umekamilikia kwa 98 na kubainisha kuwa kilichobakia ni umaliziaji wa kazi ndogondogo.

“Ujenzi wa Tenki umekamilika, hatua inayofuata ni kukamilisha kazi ndogondogo kisha kulijaza maji kama sehemu ya uangalizi na taratibu za kiufundi, Tunatarajia wiki ijayo tutajaza maji" Amesisitiza Mhandisi Gava.

KITWANGA ATAKA MADAKTARI, WAUGUZI WANAOJIHUSISHA NA RUSHWA WACHUKULIWE HATUA KALI JIMBONI KWAKE.

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (aliyevaa koti) akicheza ngoma ya asili na wananchi wa Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi mara baada ya kuwasili katika eneo hilo kwa ajili ya kufungua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi hao. Waziri Kitwanga amemaliza ziara jimboni kwake leo na kuwaonya madaktari na wauguzi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaomba rushwa wananchi. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi. Katika hotuba yake, Kitwanga aliwataka wananchi wa jimbo lake washirikiane ili kuliletea maendeleo jimbo hilo na kuwaonya madaktari na wauguzi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaomba rushwa wananchi. Kitwanga amemaliza ziara jimboni kwake leo.  
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (katikati meza kuu) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihelele wilayani Misungwi. Katika hotuba yake, Kitwanga aliwataka wananchi wa jimbo lake washirikiane ili kuliletea maendeleo jimbo hilo na aliwaonya madaktari na wauguzi wilayani humo kuacha tabia ya kuwaomba rushwa wananchi. Kitwanga amemaliza ziara jimboni kwake leo.  Picha zote na Felix Mwagara.
Picha na Felix Mwagara.

Na Felix Mwagara, Misungwi
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga amemtaka Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Misungwi kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwafukuza kazi wauguzi na madaktari watakaokuwa wanawaomba rushwa wananchi jimboni kwake.

Kitwanga alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kwa muda mrefu kuwa rushwa imekithiri katika hospitali ya Wilaya jimboni humo na kuwakatisha tamaa wananchi wanaoenda kupata huduma hospitalini hapo.

Akizungumza huku akishangiliwa na mamia ya wananchi wa mjini Misungwi, Kitwanga alisema hali sasa imekuwa tete hivyo lazima tuchukue hatua kali kwa wale watumishi wachache ambao hawafuati sheria na kuweka mbele rushwa kwa wananchi.

“Ndugu wananchi madaktari na wauguzi ni watu muhimu sana katika jamii kwani wanatupa huduma nzuri kabisa, ila wataalamu hawa wanachafuliwa majina yao kwa watumishi wachache mno, sasa tunataka kuwaondoa wale wachache ili tubaki na wengi ambao wanaipenda kazi yao, nawaonya wale wachache wenye tabia hiyo waiache haraka iwezekanavyo,” alisema Kitwanga.

Alifafanua kuwa ni kosa kwa daktari au muuguzi kumuomba rushwa mgonjwa au ndugu wa mgonjwa, kufanya hivyo ni hatari ni sawa na kuua, hivyo lazima sheria ifuate mkondo wake ili kulimaliza tatizo hilo sugu ndani ya Hospitali ya Wilaya pamoja na Misungwi kiujumla.

“Ndugu wananchi msiwe na wasiwasi kabisa, nina aapa sitalivumilia tatizo hilo, na Mkurugenzi yupo hapa analisikia hili, hivyo lazima alifanyie kazi kwa kuwasimamisha kazi wauguzi au madaktari watakaotuhumiwa kuomba au kupokea rushwa,“ a;lisema Kitwanga huku akishangiliwa na wananchi jimboni humo.   

Wakati huohuo, Kitwanga aliwataka wananchi hao kuanzisha vikundi ili waweze kupewa mikopo kupitia fedha alizoziahidi Rais John Magufuli kuwa atatoa kwa kila kijiji shilingi milioni hamsini.
“Fedha zipo jirani kuja, hivyo anzisheni vikundi ili muweze kukopeshwa fedha hizo na muweze kufanya mambo ya maendeleo, fedha hizo ni kwa ajili ya mikopo hivyo tumieni fursa hiyo kwa kuanzisha vikundi vyenu ili muweze kuzipata fedha hizo kwa uharaka zaidi,” alisema Kitwanga.

Hata hivyo, Waziri Kitwanga aliwahakikishia wananchi wa jimbo hilo wawe watulivu na wasubiri maendeleo, na pia waendelea kuchangia maendeleo ya jimbo lao ikiwemo uchangiaji wa madawati katika shule zao. Kuhusu barabara Kitwanga alisema barabara zote ambazo hazipitiki zitatengenezwa hivi karibuni na tatizo la maji litakuwa historia kwani mipango ya upatikanaji wa maji hayo ilishakamilika.

Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara yapokea tozo ya kwanza ya gesi

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (mwenye miwani ya jua) akikabidhi mfano wa hundi ya Tsh. 150,000,000/ kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego , Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi. Fatma Ally, Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia na viongozi wengine wa Halmashauri wa Wilaya ya Mtwara.
---------------------------------
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limelipa tozo ya kwanza ya huduma (Service Levy) inayotokana na shughuli za kuzalisha, kuchakata na kusafirisha gesi asilia kutoka Madimba hadi Dar es Salaam. 
TPDC imelipa kiasi cha Tshs. 150,000,000 ikiwa ni tozo ya huduma kwa shughuli za kuzalisha, kuchakata na kusafirisha gesi kuanzia mwezi Oktoba 2015 hadi Machi 2016 (miezi sita). Kiasi hiki kinajumuisha pia fedha kutoka Kampuni ya Maurel and Prom Tanzania Ltd ambayo ni wazalishaji wa gesi katika kitalu cha Mnazi Bay kilichopo kijiji cha Msimbati, Mtwara.
Akiongea wakati wa kukabidhi mfano wa hundi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio alisema malipo ya tozo ya huduma yatakua yakifanywa kwa kipindi cha miezi mitatu mitatu ili kuwezesha Halmashauri kutekeleza mipango yao ya maendeleo bila kukwama.

ABIRIA WALIOKWAMA KILOSA KUONDOKEA DODOMA KWA DELUXE LEO ALHAMIS APRILI 07, 2016

$
0
0


 KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)


 

Abiria 775 wa treni waliokwama Kilosa baada ya stesheni ya Gulwe kukumbwa na mafuriko wamefanyiwa utaratibu na Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuendelea na safari yao kwa treni ya deluxe wakianzia Dodoma leo saa 2 usiku.Wakati taarifa hii inatolewa na Uongozi wa TRL treni iliokwama Kilosa iko njiani kurejea Morogoro ambapo mabasi yapatayo 12 yatawasafirisha hadi Dodoma ambapo watasafiri na deluxe kuelekea Tabora, Kigoma na Mwanza.

Hadi jana asubuhi treni 2 za abiria zilikuwa zimekwama katika stesheni za Dodoma ( treni ya Deluxe iliokuwa inateremka kuja Dar) na Kidete mkoani Morogro ( ilikuwa inapandisha kwenda bara).Abiria 219 wa treni ya Dodoma walipatiwa usafiri mbadala wa mabasi kuja Dar es Salaam lakini hawa wa Kidete ilitarajiwa mafuriko Gulwe yangepungua na kuiwezesha treni kupita salama.

Taarifa za kiufndi Alafjiri ya leo zilithibitisha kuwa mafuriko bado yanaongekeza na hivyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kadogosa aliyekuwepo katika tukio alirejea Kilosa asubuhi leo kutoka Gulwe na kujiunga na abiria wa treni hadi Morogoro . Basi la kwanza linatarajiwa kuwasili Dodoma saa 10 jioni.

Katika taarifa hiyo ya Uongozi umeomba radhi kuwa usumbufu uliojitokeza kwa abiria na jamaa zao waliokuwa wakiwasubiri kuwapokea katika vituo mbali mbali vya treni nchini.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Aprili 07, 2016
DAR ES SALAAM

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE KUMBUKUMBU YA KARUME ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi wa ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo  inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akijiandaa kuweka Shada la Maua kwenye Kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo  inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar, ambapo  Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli ambaye yuko nje ya nchi kikazi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa pili kulia, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kulia na Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Dua ya pamoja mbele ya Kaburi la Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar,Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli ambaye yuko safarini nchini Rwanda.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa pili kulia Mama Mwanamwema Shein kulia Mama Asha Ali Iddi wa pili kushoto na Mama Zakia Bilal kushoto, wakiwa katika Dua ya pamoja kwa ajili ya kumuombea Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo  inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar, Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli ambaye yuko safarini nchini Rwanda
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa katika Dua ya pamoja na Viongozi mbalimbali na Wananchi wa Bara na Visiwani katika Dua ya pamoja kwa ajili ya kumuombea Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume baada ya dua ya pamoja na Viongozi mbalimbali na Wananchi wa Bara na Visiwani katika Dua ya pamoja kwa ajili ya kumuombea Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Muasisi ASP Hayati Sheikh Abeid Amani Karume wakati wa Dua maalum ya kumbukumbu ya kifo cha Muasisi huyo inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo April 07, Kisiwandui Zanzibar.

RAIS DKT. MAGUFULI AUNGANA NA WANANCHI WA RWANDA KUADHIMISHA KUMBUKUMBU YA MIAKA 22 TANGU KUTOKEA KWA MAUAJI YA KIMBARI.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiweka shada la maua wakishuhudiwa na  wenyeji wao Rais Paul Kagame na Mama Janeth Kagame wakiweka shada la maua katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo.

Top 40 African visionaries 2016

$
0
0
Dr.Kwame Nkuruma Osagyefo and Mwalimu Julius Kambarage Nyerere both had a vision for a united Africa, which has been the subject of discussion since 1963. It has led to the African Union (formerly Organization of African Unity- OAU) coming up with Africa Agenda 2063, which is an ambitious vision for Africa. 

In it, as narrated by outgoing AU chair Dr. Nkosazana Dlamini Zuma, is an Africa that is leading in Trade, e-commerce, innovation, space exploration, technology, Education, Quality infrastructure connecting the whole of Africa, one currency, one leader and a united people without borders or barriers, borderless Africa among many other progressive visions. 

Thomas Sankara of the Bukinabbe had a vision for an Africa infested with upright men, before the enemies of progress cut his life short just like they did to Patrice Emery Lumumba of the Du-Congo. But Africa has never been short of Visionary young men and women,Africa has a crop of quick growing leaders,entrepreneurs and innovators. 

They are taking charge of their destiny, transforming the continent and rewriting is future. They are living the African dream and solving critical socio-economic problems like poverty, disease, unemployment, corruption, illiteracy among many other problems. 

From the election of no non sense, action on President in Tanzania, to a young lady making bicycles using bamboo in Ghana, we bring to you a list of 40 promising African visionaries in different fields and professions and their stories as of March 2016.Tanzania's President elect John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, October 30, 2015. Tanzania's ruling party candidate, John Magufuli, was declared winner on Thursday of a presidential election, after the national electoral body dismissed opposition complaints about the process and a demand for a recount. The election has been the most hotly contested race in the more than half a century of rule by the Chama Cha Mapinduzi Party, which fielded Magufuli, 56, a minister for public works. REUTERS/Sadi Said Tanzania's President e John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM).

1. PRESIDENT DR. JOHN POMBE MAGUFULI Since his election and swearing in in November 2015, he has sent shockwaves across Africa by his actions, in his first week in office, pundits say that he did something his predecessor had not done in 10years, he went on a surprise visit to Muhimbili Hospital which is the biggest public hospital in Tanzania and the state of the hospital was pathetic and wanting, within a week of his visit, the top management of the hospital was sent home and the hospital got a totally new face. 

His anti-corruption war, and visionary style of leadership has seen him quickly rise to be a role model and an admiration in Africa and the whole world. If he keeps up with that spirit, Tanzania willbe the talk of Africa and Africa Agenda 2063 and vision 2030 will be realized sooner than expected. We wish him well and encourage him to keep up the good fight, he is a pillar and a beacon of Africa rising. 

  2. JOE KARIUKI (KENYAN)
keter-pic 
Co-Founder: African women and Beyond (AFWAB), Joe Kariuki (Kenyan).

Joe is a successful businessman, entrepreneur, philanthropist and a co-founder of AFWAB, which he co-founded with Martin Kappel who is also a renowned community empowerment champion and has been helping different communities in Africa through projects and initiatives. AFWAB is an initiativethrough which they have empowered over 100,000 women from different parts of Africa by giving them capital to start their businesses, mentorship training, market access and bringing them together to network and do business. He is intending to empower over 1 million women to start businesses, connect those in business to help them network so as to open market access for their merchandise to all parts of the world. 

TANZIA: Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Mh. Christina Lissu Mughwai afariki dunia

$
0
0
Taarifa iliyotufikia hivi punde, inaeleza kuwa, Mbunge wetu wa Viti Maalum na Dada wa Mh. Tundu Lissu, Mh. Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Kansa tangu mwaka jana. 

Mungu aiweke roho Marehemu Mahala pema peponi 

Amin.

TIZA YA JOTO LA ASUBUHI IJUMAA APRIL 8

Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images