Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

Afya Sports Bara Yatamba Nyumbani Yaifunga Afya Sports Zanzibar 3-0

$
0
0
Timu ya  Afya Sports Bara imeifunga timu ya Afya Sports Zanzibar  mabao 3-0 katika mchezo uliyofanyika leo katika kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
Bao la kwanza limefungwa dakika ya 12 kipindi cha kwanza na mchezaji machachari kutoka Afya Bara, Ali magoma.
Katika kipindi cha pili  Muhaji Kampala alitikisa nyavu na kufunga bao  la pili, huku  bao la tatu likiwekwa kimiani  na Ali Magoma. 
Katika mchezo huo wachezaji wa Bara walionekana kuwa makini kulinda lango lao, huku morali ya wachezaji hao ikiwa juu katika kuhakikisha timu yao inaibuka na ushindi.
Kwa matokeo hayo timu ya Afya Sports Bara imeibuka kidedea ambapo mechi nyingine inatarajiwa kuchezwa Jumatatu.
Mchezo huo ni Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka kati ya Watumishi wa Sekta ya Afya Zanzibar na Watumishi wa Sekta ya Afya Bara kwa lengo la kuendeleza undugu na ushirikiano uliopo.
 Mchezaji wa Afya Sports Zanzibar, Abdulheri Thani ( mwenye jezi namba tatu) akijaribu kufunga bao mbele ya kipa wa Afya Sports Bara, Salumu Saidi katika mchezo wa tamasha la pasaka. Mchezo huo umefanyika leo kwenye Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
 Kipa wa Afya Sports Bara, Salumu Saidi akidaka mpira ili kuokoa hatari langoni mwake leo.
Mchezaji wa timu ya Afya Sports Bara, Robert Ndimbe (kulia) Bara akiwania mpira na Saidi Bundara Zanzibar (kushoto) kutoka Afya Sports ya Zanzibar. Mchezo huo umefanyika leo kwenye Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam. Afya Sports Bara 3-0 Afya Sports Zanzibar.
Picha zote na John Stephen, 
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)

Taarifa ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)

$
0
0
KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ilikutana hivi karibuni na kujadili masuala mbalimbali.
 
A; Mafunzo
TASWA imepata wadau watakaosaidia kudhamini mafunzo kwa waandishi wa habari za michezo 60 chipukizi na wale wa kada ya kati.
Mada mbalimbali zitatolewa zikihusisha wataalamu wa uandishi wa habari za michezo, wahariri wazoefu na baadhi ya wataalamu wa michezo mbalimbali.
Pia itatolewa mada ya masuala ya ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano na namna ya kuripoti habari za michezo.
Mafunzo haya yatafanyika Mei 21-23 mwaka huu jijini Dar es Salaam, ambapo TASWA inaendelea na juhudi za kusaka wadau wengine ili mafunzo hayo yatatanguliwe na mkutano wa siku moja kwa wahariri wa habari za michezo na baadhi ya waandishi wazoefu wa habari za michezo.
Utaratibu wa kupata washiriki hao utafanyika kwa kutumia wahariri wa habari za michezo wa vyombo mbalimbali kwa kadri mahitaji yatakavyoruhusu.
TASWA inawashukuru wadau hao ambao tutawatangaza baada ya taratibu za udhamini wao kukamilika na tunaomba wengine waendelee kutuunga mkono katika hili.
B: Media Day
Kwa miaka miwili sasa, bonanza la wanahabari ‘Media Day’ limeshindwa kufanyika kutokana na sababu mbalimbali, hivyo imeundwa kamati ndogo kwa ajili ya jambo hilo na inaendelea vyema na maandalizi na muda si mrefu majibu mazuri yatatangazwa.
C: Vitambulisho
Tulisitisha kwa muda kutoa vitambulisho kwa wanachama ili kuboresha utaratibu na kutoa vyenye ubora zaidi, hilo tayari limekamilika na mtatangaziwa utaratibu mzuri na wale wote ambao hawana watapata vitambulisho vyao.
 
Nawasilisha,
 Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
26/03/2016

KUANGALIA MECHI YA TAIFA STARS NA CHAD BUKU TANO TU

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kundi G siku ya Jumatatu kati ya Tanzania dhidi ya Chad, bei ya chini ikiwa ni shilingi elfu tano (5,000) tu. 
Viingilio vya mchezo huo vimegawanyika katika makundi matatu, ambapo kiingilio cha juu kitakua shilingi elfu ishirini na tano (25,000) kwa VIP A, na shilingi elfu ishirini (20,000) kwa VIP B, na kwa viti vya rangi ya bluu, kijani na orange itakua shiligi elfu tano (5,000). 
Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa kesho Jumapili saa 2 asubuhi katika vituo vinne ambavyo ni kituo cha mafuta Buguruni (Buguruni), Ubungo Oilcom (Ubungo) na Dar Live (Mbagala), na Jumatatu tiketi zitauzwa katika viunga vya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 
Wakati huo huo Rais wa TFF, Jamal Malinzi amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa kwa kubali kuwa mgeni rasmi katika mchezo kati ya Tanzania v Chad utakaochezwa siku ya Jumatatu jijini Dar es salaam. 
TFF pia inamshukuru Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa kufanikisha ujio wa Waziri Mkuu kwa kufuatilia kwa karibu maombi ya TFF ya tarehe 21/03/2016 ya kumuomba Waziri Mkuu awe mgeni rasmi katika mchezo huo. 
Kwa upande wa Taifa Stars iliyoweka kambi katika hoteli ya Urban Rose inaendelea na mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Chad. 
Waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Djibouti wanatarajiwa kuwaisli leo jioni ambao ni mwamuzi wa kati Djamel Aden Abdi, Abdilahi Mahamoud, Farhan Bogoreh Salim, Farah Aden Ali, huku kamisaa wa mchezo akiwa Andrea Abdallah Dimbiti kutoka nchini Sudani Kusini.

TFF yaomboleza kifo cha gwiji wa soka duniani Johan Cruff

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeomboleza kifo cha gwiji wa soka duniani Johan Cruff aliyefariki hivi karibuni kwa ugonjwa wa Saratani. 
Katika taarifa aliyoituma kwa Rais wa Chama cha Soka cha Uholanzi, Rais wa TFF Jamal Malinzi amemwelezea Marehemu Cruyff kama gwiji aliyetoa mchango mkubwa kama mchezaji na kocha katika timu ya Taifa ya nchi yake na klabu za Barcelona, Ajax, Lavanet mwaka 1964 – 1977. 
Tanzania tulikuwa na bahati ya kutembelewa na Cruyff ikiwa ni sehemu ya kuitangaza klabu yake ya Barcelona na kuendeleza mpira wa Vijana na maendeleo ya walimu wa soka nchini. 
TFF inaungana nawe, familia ya marehemu na wapenda soka ndani ya Uholanzi na duniani kote katika kuomboleza na kusheherekea maisha ya Marehemu Johann Cruyff. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Amen. 
Johann Cruyff alizaliwa Uholanzi tarehe 25 Aprili, 1947 na kuchezea klabu za Ajax, Feyenoord, Lavante, Los Angeles, Washington Diplomats na timu ya Taifa ya Uholanzi kati ya mwaka 1966 - 1977 na baadae alizifundisha kalbu za Ajax, Barcelona na Catalonia.

NGUMI KUPIGWA KESHO UWANJA WA NDANI WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mabondia Abdalla Pazi 'Dulac Mbabe' kushoto akitambiana na Mada Maugo baada ya kumaliza kupima uzito kwaajili ya mpambano wao wa ubingwa wa UBO Afrika utakaofanyika jumapili ya pasaka march 27 kesho katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.


Abdalla Pazzi na Mada Maugo

TAARIFA YA SERIKALI YA MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0
                                              JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU


TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

Ndugu Wanahabari, tukiwa tunaelekea sikukuu ya pasaka, Serikali ya Mkoa wa Dodoma imeona ni vyema ikakutana na wawakilishi wa vyombo vya habari hapa Mkoani Dodoma, ili kupitia vyombo vya habari, tupate fursa ya kuweka wazi kwa wananchi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla masuala ya msingi ambayo yamejiri hapa Mkoani Dodoma.
Awali, usiku wa kuamkia jana kuna tukio tunaloweza kuita la ujambazi lilitokea kama majira ya saa 8 usiku ambapo kundi la watu takribani saba (7) ambao bado hawajafahamika walivamia ofisi za Halotel Mkoani Dodoma kwa lengo la kutaka kufanya uhalifu ambapo waliwavamia askari wawili waliokuwa wakilinda Ofisi hiyo, ambapo pamoja na athari nyingine zilizojitokeza; walipora silaha aina ya SMG na kumjeruhi askari mmoja ambaye alilazwa kwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kuruhusiwa jana hiyohiyo.


Hadi hivi sasa Jeshi la polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea kulifanyia kazi suala hilo ambapo hadi tunavyozungumza sasa tayari silaha hiyo iliyoporwa imeshapatikana, uchunguzi zaidi wa suala hilo unaendelea kubaini watu wote waliohusika. Kufuatia suala hilo, Serikali ya Mkoa wa Dodoma, kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana anapenda kutoa tamko lifuatalo: 
·        Kwanza kabisa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana analaani vikali tukio hilo la uhalifu na kuwa halivumiliki na halikubaliki katika Mkoa wa Dodoma na Mikoa mingine hapa nchini na amewataka wananchi wema kutoa ushirikiano kwa vyombo vya Dola ili kuwabaini wahusika na kukomesha matukio kama hayo.

·        Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana analiagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanafanya uchunguzi na kuwabaini wale wote waliohusika katika tukio hilo la uhalifu,ili kuwatia mbaroni na kuwachukulia hatua kali za kisheria. Aidha amelitaka jeshi la polisi kujipanga vizuri na kuhakikisha kuwa tukio hili ni la mwisho na halijitokezi tukio jingine la aina hii.

·        Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanafanya uchunguzi wa kina ili kubaini kama kuna dalili zozote za kuwepo kwa uzembe wa aina yoyote kwa askari hao waliokuwa wanalinda Ofisi hiyo, na endapo itabainika kulikuwa na uzembe basi Jeshi la polisi lichukue hatua kali kwa askari hao waliohusika.


RIP JOHAN CRYUFF

Kuibuka kwa mtoto aliyekufa miaka 2 iliyopita mkoani simiyu


NYOTA MPYA WA SOKA MTANZANIA ANAYEKIPIGA UINGEREZA AJIUNGA TAIFA STARS

MKUU WA WILAYA YA GEITA AWATAKA WANANCHI WA MKOA HUO KUMRUDIA MUNGU NA KUACHA MAUAJI YA ALBINO NA VIKONGWE

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie, ambaye 
ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika tamasha la pasaka,baada ya kukaribishwa jukwaani,alizungumza na mashabiki wa muziki wa injili waliohudhuria katika tamasha hilo,alisema kuwa ujio wa tamasha hilo ni fursa pekee kwa Wananchi wa mkoa wa Geita kumrudia Mungu na kutubu ili kuacha tabia mbaya inayoupaka matope mkoa huo kwa mauaji ya walemavu wa ngozi Albino pamoja na Vikongwe.

"Hii ni fursa ya kipekee kwetu sisi Wana Geita ya kuwa na hofu ya Mungu,kuepuka kutenda maovu na badala yake tumrudie Mungu wetu,tutendeane mema,kwa sababu Wanadamu wengi wa leo wamekosa hofu ya Mungu',alisema Mh.Mangachie huku akiishukuru kampuni ya Msama Promotion na Mkurugenzi wake Bw. Alex Msama kwa kuandaa tamasha hilo .

Waimbaji mbalimbali wameshiriki katika tamasha hilo ambao ni Upendo Nkone, Bonny Mwaiteje, Joshua Mlelwa, Martha Baraka, Jesca BM, Jennifer Mgendi, Mwimbaji kutoka Zambia Ephraim Sekereti, Waimbaji kutoka Nchini Kenya Solomon Mukubwa , na Mtanzania Faustine Munishi pamoja naye Christopher Muhangila.

Matamasha hayo yataendelea kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na keshokutwa litafanyika tamasha lingine kama hilo mjini Kahama mkoani Shinyanga.

Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion chini ya mkurugenzi wake Bw. Alex Msama kwa udhamini wa magazeti ya Dira, Dira TV na Dira FM na linafanyika kila mwaka katika kipindi cha sikukuu za Pasaka (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-GEITA)
20
mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangachie akitoa salamu zake za shukurani kwa kampuni ya Msama Promotion kwa kuandaa tamasha la pasaka katika mkoa wa Geita wilaya ya Geita kwa ni jambo jema kuwahubiria amani wananchi wa Geita ili wamrudie Mungu na kuacha mauaji ya Albino na Vikongwe.
21
Waimbaji Solomon Mukubwa kulia , Bonny Mwaiteje kushoto wakimpiga tafu Mwimbaji mwenzao Christopher Muhangila katikati wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani.
1
Mmoja wa Mashabiki wa Tamasha la Pasaka pamojana mashabiki wengine waliohudhuria katika Tamasha la Pasaka lililofanyika mjini Geita Mkoani Geita kwenye ukumbi wa Desire wakiimba kwa kuzinguka ukumbi huo wakati mwimbaji Upendo Nkone alipokuwa akifanya vitu vyake jukwaani na kuwafanya wavutiwe na tamasha hilo kiasi cha kushindwa kukaa kwenye viti wakizunguka huku na kule huku baadhi wakiwa wamebeba viti juu juu.

MBIO ZA MAGARI ZA VAISAKH RALLY 2016 ZINAFANYIKA JUMAPILI HII VIWANJA VYA KIA,KILIMANJARO

$
0
0
Gurjit Dhan Dereva anayepewa nafasi kubwa ya kufanya vyema katika mashindano hayo.
Dereva Larry Horn anaingia katika mashindano hayo akiwa na gari aina ya Porche.
Baadhi ya magari yanayoshiriki mashindano hayo yanayofanyika Jumapili hii katika viwanja vya KIA. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

SHUKRANI WADAU ; MTOTO EBENEZA PEMBE AMEANZA MATIBABU YA SARATANI YA NGOZI HOSPITALI YA MUHIMBILI

$
0
0
Mtoto EBENEZA PEMBE
........................................
                                    NDUGU ZANGU HABARI ZA WAKATI HUU;
SIKU CHACHE ZILIZOPITA TULILETA TANGAZO,  OMBI LA MSAADA WA MATIBABU KWA MTOTO EBENEZA PEMBE ANAYESUMBULIWA NA SARATANI YA NGOZI.
NAWASHUKURU SANA RAFIKI ZANGU MLIOGUSWA NA KUTOA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI, LEO KUPITIA ACCOUNT YA MTOTO EBENEZA  TUMEKABIDHI KIASI CHA SHILINGI MILIONI MOJA LAKI SITA NA ELFU SITINI NA NANE (1,668,000/-) MLIZOCHANGA KWA UPENDO WENU MKUBWA.


EBENEZA NA MAMA YAKE WAPO HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI WAKIENDELEA NA MATIBABU, NA TAARIFA NJEMA TULIYONAYO NI KWAMBA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA NHIF, BAADA YA KUONA TANGAZO LILE WAMEMWANDIKISHA EBENEZA KWENYE FAO LA TOTO CARD HIVYO ATATIBIWA KWA GHARAMA ZA MFUKO HUO.
EBENEZA NA MAMA YAKE WANAWASHUKURU SANA KWA MOYO WENU WA KUMSAIDIA NA TUWANAWAOMBEA BARAKA TELE KWA MWENYEZI MUNGU.
 SISI PIA KWA UPANDE WETU TUNAPENDA KUWASHUKURU NYOOTE MLIOJITOA KWA HALI NA MALI KUFANIKISHA SUALA LA KUMSAIDIA MTOTO EBENEZA.

TUNAWASILISHA ; SALUM MWINYIMKUU NA 
                       SILVANUS KIGOMBA 

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: k.sher feat squezer - uvumilivu

Ngoma Africa Band Yawatakieni Heri ya Sikukuu ya Pasaka!

$
0
0

Bendi yako maarufu ya muziki wa dansi “Ngoma Africa Band” aka FFU yenye makao yake nchini Ujerumani, Inawatakieni wadau wote popote pale mlipo KILA LA HERI NA FANAKA katika sikukuu ya msimu wa Pasaka. bendi yenu “Ngoma Africa band” inawaombea amani na baraka. Pia msikose kupata burudani kamili ya Pasaka kwa kusikiliza nyimbo aka (Virungu vya FFU) at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com,
mawasiliano at contact@ngoma-africa.com.
 Gwaride kali
 FFU Ughaibuni kazini
 Hapa kazi tu!
Kikosi kazi
Nyomi

SIMU TV: MAPITIO YA MAGAZETI LEO


SERIKALI YA TANZANIA HAINA MPANGO KWA KUTEKETEZA MENO YA TEMBO YALIYOHIFADHIWA

$
0
0
Serikali ya Tanzania imetoa tamko kuwa kwa sasa haina mpango wowote wa kuteketeza meno ya tembo yaliyohifadhiwa ambayo yametokana na vitendo vya ujangili na vifo asilia vya tembo.

Tamko hilo limetolewa hivi karibuni na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark Childress alipotembelewa na balozi huyo ofisini kwake kujadili maendeleo ya sekta ya Maliasili mchini.


Prof. Maghembe alisema hayo baada Balozi huyo wa Marekani hapa nchini kutoa pendekezo kwa Serikali ya Tanzania kuchoma sehemu meno ya tembo yaliyohifadhiwa ili kutoa ujumbe mzito duniani juu ya dhamira ya Serikali kukomesha biashara hiyo haramu.


"Naomba niweke wazi kuwa kwa sasa hatupo tayari kuteketeza meno haya, tunaweza kuyatumia kwenye tafiti za kisayansi au vielelezo kwa ajili ya kesi za ujangili ambazo zipo mahakamani na nyingine ambazo bado zinafanyiwa uchunguzi" Alisema Prof. Maghembe.


Zipo nchi mbalimbali duniani ambazo zimechukua hatua ya kuteketeza meno yake ya tembo yaliyohifadhiwa ikiwemo nchi jirani ya Kenya na Malawi ambapo inaaminika kuwa kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kushawishi Ulimwengu kukomesha biashara hii haramu ya meno ya tembo.


Nchi nyingine ni Chad, Ubelgiji, Ufaransa, China, India, Marekani na Ureno. Kwa upande wa nchi ambazo zina msimamo sawa na Tanzania katika kuendelea kuhifadhi meno yake ya Tembo ni pamoja na Afrika ya Kusini, Botswana na Zimbabwe.


Akizungumzia kuhusu kuendeleza sekta ya Maliasili nchini, Prof.Maghembe amemuomba Balozi wa Marekani Bw. Mark Childress kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukuza sekta hiyo kwa kuleta wawekezaji mbalimbali kutoka Marekani kuja kuwekeza Tanzania pamoja na kusaidia kwenye mapambano dhidi ya Ujangili.


Aliongeza kuwa Tanzania ina fursa nyingi ambazo zinahitaji uwekezaji mkubwa ikiwemo hoteli za kitalii, fukwe za kisasa na kuendeleza vivutio mbalimbali vilivyomo hapa nchini.


Prof. Maghembe amemshukuru balozi huyo kwa misaada mbalimbali kutoka Serikali ya Marekani ya kuendeleza sekta ya Maliasili nchini ukiwemo wa hivi karibuni wa mbwa maalum (Snifer Dogs) kwa ajili ya kusaidia utambuzi wa rasilimali za Maliasili zinazoweza kutoroshwa nje ya nchi kupitia bandari na viwanja vya ndege.


Katika taarifa iliyowasilishwa kwenye kikao baina ya Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark Childress imeonesha kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Serikali ya Marekani imetoa misaada mbalimbali ambayo jumla yake ni dola za kimarekani Milioni 41.35 katika kusaidia eneo la uhifadhi hapa nchini.




Akizungumzia mahusiano baina ya Tanzania na Marekani Balozi Mark Childress alimueleza Prof. maghembe kuwa Serikali ya Marekani itaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi hizi mbili ambapo pia ofisi yake ya ubalozi imeshatafuta wadau mbalimbali ambao wapo tayari kusaidia fedha, vifaa na mafunzo kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi na mapambano dhidi ya ujangili. 

(Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)

ZUBEIR MAULID ACHUKUA FOMU YA KUWANIA USPIKA BARAZA LA WAWAKILISHI, ZANZIBAR

$
0
0
KATIBU wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dk. Yahya Khamis Hamad (kushoto) akimkabidhi fomu ya kugombea uspika, mgombea wa nafasi hiyo kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Zubeir Ali Maulid , ambapo uchaguzi wa spika unatarajiwa kufanyika tarehe Machi 30 , 2016, fomu hiyo alikabidhiwa katika ofisi ya katibu wa baraza ziliopo Mbweni Wilaya ya Magharib ‘B’.
KATIBU wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dk. Yahya Khamis Hamad (kushoto) akisalimiana na mgombea wa nafasi ya Uspika wa Baraza hilo kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Zubeir Ali Maulid wakati alipofika kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo katika ofisi ya katibu wa baraza ziliopo Mbweni Wilaya ya Magharib ‘B’.
MGOMBEA wa Nafasi ya Uspika kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) Zubeir Ali Maulid akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uspika wa Baraza la Wawakilishi katika ofisi za Baraza hilo ziliopo Mbweni Wilaya ya Magharib ‘B’.Picha na Haroub Hussein

STARS KUWAVAA CHAD KESHO TAIFA

$
0
0
Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kesho inashuka dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakabili Chad katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2017.

Taifa Stars itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0 ilioupata katikati ya wiki jijini N’Djamena katika uwanja wa Idriss Mahamat Ouya, bao lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta dakika ya 30 ya mchezo.

Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema maandalizi kwa kikosi chake yamekalimika, vijana wote wapo katika hali nzuri ya kusaka ushindi ushindi kesho, kikubwa amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Taifa kujwa kuwapa sapoti vijana watakapokuwa wakiwakilisha Tanzania.

Kuelekea katika mchezo huo, tiketi za mchezo zimeanza kuuzwa leo katika vituo vya Ubungo Oilcom, Buguruni kituo cha mafuta, Mbagala Darlive na Karume ofisi za TFF. Viingilio vya mchezo huo ni Shilingi 25,000 kwa VIP A, Shilingi 20,000 kwa VIP B na Shilingi 5,000 kwa viti vya rangi ya Blu, Kijani na rangi ya Machungwa.

Embarking on information technology can reduce congestion and air pollution in our cities.

$
0
0

By Abdalah Kileo

Many jobs, businesses and other activities are drawn into city centers, you can find shops, restaurants, financial services, Government ministries, libraries, colleges, open spaces and other facilities all concentrated in a city centers. 
Since very few people lives in the city center, most of those surrounding the city centers have to access the city through walking, bicycles, motorcycles, public and private cars for their daily activities. This has led to sometimes intolerable levels of traffic congestion on urban streets as well as the main road accessing the city, causing delays and severely effect on productivity of business, their ability to innovate and business access to new markets and resources. 
The problem of congestion span from the business to people who live in our city, they finds themselves stuck in traffic when they should be at work or school and sometimes frustrated at the time wasted in trying to get from point A to point B. 
The problem go far where it increases oil consumption  and CO2 emissions as well as noise emission from transport, with people living along congested routes and very busy towns like Dar Es Salaam they suffer from poorer air quality for most of their life. 

NAVY KENZO WATUA BUKOBA TAYARI KWA SHOW YAO USIKU HUU LINA'S NIGHT CLUB

$
0
0
Wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo, Nahreel na Aika leo wametua Bukoba ikiwa ni mwendelezo wao wa "Kamatia Chini lights up Tour" ambapo usiku huu watashusha show yao ya Nguvu kwenye Ukumbi wa Burudani wa Lina's Night uliopo Bukoba Mjini. Wasanii hao wanaletwa hapa Mjini Bukoba kupitia kampuni ya Sleek Events ya Jijini Mwanza.
Msanii Aika akishuka kwenye ndege leo hii kwenye Uwanja wa Ndege Mjini Bukoba




Wadau wakipata picha ya pamoja na wasanii wa Kundi la Navy Kenzo

Kushoto ni Mr. Tega JassonMkurugenzi wa Sleek Events akitokelezea kwenye picha ya pamoja na msanii Aika, Faustine Ruta wa Bukobasports.com na kulia ni Bwogi.

Viewing all 110021 articles
Browse latest View live




Latest Images