Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

BASI LAPARAMIA KITUO CHA MABASI YAENDAYO KASI ENEO LA KIMARA JIJINI DAR USIKU HUU

0
0
Basi la Abiria mali ya Kampuni ya Princess Muro, limeparamia Kibanda cha Kituo cha Mabasi yaendayo kasi eneo la Kimara Jijini Dar usiku hii wakati likiingia kutoka Mkoani. Chanzo chake bado hakijafahamika mpaka sasa.


NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: Pressure - Banana Zoro fet Hafsa

Dondoo za magazeti leo Machi 26, 2016

WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KATIKA KITUO CHA KULEA YATIMA CHA CHAKUWAMA WAPATA MSAADA WA VYAKULA KWA AJILI YAKUSHEREHEKEA SIKUKUU YA PASAKA

0
0

Meneja Mkuu wa Maduka ya nguo ya Woolworths Tanzania, Joehans Bushir (Kushoto) akiongea na mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto Yatima wanaoishi katika mazingira magumu cha Chakuwama, kilichopo Sinza jijini Dar es Salaa, wakati kampuni hiyo ilipopeleka misaada mbalimbali ya vyakula ,ikiwemo mchele,mafuta na sabuni, ili watoto wakituo hicho waweze kusherehekea sikukuu ya pasaka kwa furaha.
Meneja Mkuu wa Maduka ya nguo ya Woolworths Tanzania, Joehans Bushir (Kushoto) akimkabidhi msaada wa ndoo ya mafuta ya kupikia Jesca John ambaye ni miongoni mwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto Yatima wanaoishi katika mazingira magumu cha Chakuwama, kilichopo Sinza jijini Dar es Salaa, kampuni hiyo ilipopeleka misaada mbalimbali ya vyakula ,ikiwemo mchele,mafuta na sabuni, ili watoto wakituo hicho waweze kusherehekea sikukuu ya pasaka kwa furaha.
Wafanyakazi wa maduka ya kuuza nguo ya Woolworths Tanzania, Joehans Bushir (Kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto Yatima wanaoishi katika mazingira magumu cha Chakuwama, kilichopo Sinza jijini Dar es Salaa, mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vyakula mbalimbali , ikiwemo mchele, mafuta yabkula na sabuni,ili watoto wakituo hicho waweze kusherehekea sikukuu ya pasaka kwa furaha. 
Meneja Mkuu wa Maduka ya nguo ya Woolworths Tanzania, Joehans Bushir (Kushoto) akimsikiliza kwa makini mlezi na mmiliki wa kituo cha kulea watoto Yatima wanaoishi katika mazingira magumu cha Chakuwama, kilichopo Sinza jijini Dar es Salaa, Saida Hassan , wakati kampuni hiyo ilipopeleka misaada mbalimbali wa vyakula ,ikiwemo mchele,mafuta na sabuni, ili watoto wakituo hicho waweze kusherehekea sikukuu ya pasaka kwa furaha.

VIJANA WA KKKT IRINGA MJINI WAKIINGIZA IGIZO LA MATESO YA YESU KRISTO

0
0
Kijana  wa kwaya  ya  vijana   katika  kanisa la Kiinjili la  Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika  wa Iringa mjini Bw   Ezekiel Mbyopyo akiwa ametundikwa Msalabani   wakati  akiigiza  igizo la Mateso ya  Yesu  Kristo  igizo lililofanyika Ijumaa kuu wakati  wa tamasha  la maneno Saba ya Yesu Msalabani.
Vijana   walioigiza kama wayahudi  Brown  Mwaipopo (kushoto) na Eston Mgaya  wa  kanisa la  Kiinjili la Kilutheri  Tanzania (KKKT) usharika  wa  Iringa mjini wakimuwamba Msalabani  kijana  mwenzao Ezekiel Mbyopyo  wakati  wa Igizo la mateso ya  Yesu  Kristo  siku ya  Ijumaa kuu.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

USIKU WA MCHIRIKU NA TAARABU KUFANYIKA KESHO PASAKA DAR LIVE

Dar es salaam by night today

0
0
Courtesy of ZAP Photography

DAWASCO YABAINI WIZI MKUBWA WA MAJI MITAA YA TANDALE, DAR ES SALAAM

0
0
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) limebaini wizi mkubwa wa Maji ujulikanao kwa jina maarufuu kamaa wizi wa nyoka kwenye mitaa ya chama pamoja na Mkundunge Sinza Tandale Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye tukio hilo wakati wa operesheni maalum ya kubaini wizi wa Maji meneja wa Dawasco Magomeni Mhandisi Pascal Fumbuka amesema kuwa wamebaini wizi mkubwa wa Maji ujulikanao kwa jina la wizi wa nyoka ambapo wananchi wamejitengenezea laini za Maji kinyemela kwa kutumia mipira yakawaida na kutoa maji kutoka umbali mrefu nakuzipitisha kwenye nyumba zao au kuunganisha kwenye tenki za Maji nakuuza bila kibali kutoka Dawasco.

“Leo tumebaini wizi mkubwa wa Maji ujulikanao kama wizi wa nyoka kwenye mitaa  ya Sinza tandale ambapo wananchi wamekuwa wakijunganishia laini za Maji kwa kutumia mipira ya kawaida kutoka umbali mrefu nakupitisha kwenye maeneo ya makazi kinyemela bila kupata kibali kutoka Dawasco”, alisema Fumbuka.

Pia Mhandisi Fumbuka amesema wamechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuondoa laini zote za Maji kwa sababu za kiafya ,kutoa elimu kwa wakazi hao yakuwa hawaruusiwi kujiunganishia wenyewe bali wafike kwenye Ofisi za Dawasco kuomba huduma hiyo na waweze kuwekewa kihalali kwani kuna  ongezo  kubwa la Maji jijini hivyo hamna haja ya kuiba Maji ila pia hatua nyingine ni pamoja na kuwawekea kizimba (kioski) cha Maji ilikuwezesha wakazi hao kuendelea kupata huduma ya Maji.

“Baada ya kubaini wizi wa Maji kwenye mitaa ya Sinza Tandale tumechukua  hatua kadha ikiwemo kuondoa laini zote zilizounganishiwa kinyemela kwa sababu za kiafya kwani laini nyingine zimepita kwenye bomba za Majitaka , kutoa elimu kwa wakazi kuwa kuna ongezeko la Maji hivyo mtu yeyote anayehitaji huduma ya Maji afike kwenye  ofisi zetu za Dawasco tuweze kumuunganishia kihalali pia tumeweka kizimba cha Maji kitakacho toa huduma ya Majisafi ilikuwezesha wakazi waendelee kupata huduma ya Maji kama kawaida”,alisema Fumbuka.

Kwa upande wawakazi wa Sinza Tandale akiwemo Mzee Seif Shabani Mohamed amekiri kuwepo kwa wizi mkubwa wa Maji kwenye mitaa hiyo nakusema kuwa unatokana na gharama kuwa kubwa za kuunganishiwa huduma ya Maji pamoja na ubabaishaji kuwa mkubwa  ukiomba huduma hiyo hivyo ameiomba Dawasco kupunguza gharama za kuunganishiwa Maji ilikufanya wakazi wenye kipato cha  cha chini kumudu gharama itasaidia kupunguza tatizo la wizi wa Maji kwani wananchi wengi watajiunganishia kihalali.

“Kweli mitaa mingi hapa Tandale kuna tatizo la wizi wa Maji ila inatokana na gharama kubwa ya ada ya kuunganishiwa huduma ya Maji na pia ukiomba kuunganishiwa mchakato unakuwa una ubabaishaji mrefu hivyo kufanya wananchi wenye kipato cha chini kutoweza kumudu gharama pamoja na kukata tama kutokana ubaishaji ila gharama zikipunguzwa itasaidia kupunguza tatizo la wizi wa Maji”, alisema Mzee Seif.

Dawasco inaendelea kuwasihi  wakazi wote wa Jiji la Dar es salaam kuepuka kujiunganishia huduma ya Maji kinyemela  kwani operesheni ya kubaini wezi wa Maji kwenye maeneo mbalimbali ya jiji ni endelevu na pia ni agizo kutoka kwa waziri wa Maji na umwagiliaji Mh Gerson Lwenge pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda  ambao waliagiza Dawasco kuwabaini wezi wa Maji   hivyo wale wote waliojiunganishia bila kibali kutoka Dawasco wajisalimishe iliwaweze kupewa kibali halali kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika akitumia huduma ya Maji kwa wizi.


Meneja wa Shirika la Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam (Dawasco) Mhandisi Pascal Fumbuka akionyesha moja ya laini ya Maji iliyounganishwa kiholela (wizi wa nyoka) ambapo iliunganishiwa kwenye tenki la kuhifadhi Maji kwa ajili ya kuuza kwa wananchi kwenye eneo la mtaa wa mkundunge Sinza Tandale Jijini Dar es salaam.


Samsung Tanzania yazindua Simu mpya aina ya Galaxy S7

0
0
KAMPUNI ya Samsung nchini Tanzania imezindua simu mpya ya Samsung Galaxy S7 Mlimani City jijini Dar es Salam.

Akizungumza na waandishi wa habari Meneja mafunzo wa bidhaa za Samsung, Julius Giabe mara baada ya uzinduzi alisema simu ya Samsung Galaxy S7 ni toleo jipya ambalo kwa sasa inapatikana madukani kote nchini.

Amewaomba watanzania wajitokeze kununu simu hiyo yenye ubora wa hali ya juu kwani imeboreshwa zaidi kulingana na tekinolojia ya sasa.

Alisema Julius Samsung Galaxy S7 imeboreshwa zaidi kwenye upande wa Camera kwani ina Mega Pixel 12 zilizoboreshwa zaidi kiasi ambacho unaweza kupata picha au Video nzuri zaidi.

Kioo chake kizuri cha kuvutia na inazuia vumbi na Maji kwa muda wa dakika 30 ndani y maji.

Julius alisema, Samsung Galaxy S7 inakaa na chaji kwa muda mrefu sana na hata ikiisha chaji inauwezo wa kuichaji bila kuchomeka kwenye Umeme(Wireless charging).

Julius alimaliza kwa kuwaomba watanzania tusikose kumiliki simu ya Samsung Galaxy S7 ukakosa mambo mazuri katika teknolojia hii ya kisasa ambayo Dunia yote iko Kiganjani mwako.

Kwa wakazi wa Dar es Salaam tutembelee Mlimani City ambapo promosheni ya Samsung Galaxy S7 inaendelea,upate kwa undani ubora wa simu hiyo.“Kuwa wa kwanza kumiliki simu ya Samsung Galaxy S7”.
Balozi wa Samsung Tanzania,Aisha Saki(katikati) akiwaelezea jambo wateja waliotembelea uzinduzi wa simu ya Samsung Galaxy S7 Mlimani City jijini Dar es Salaam.Kulia ni mabalozi wenzake.
Balozi wa Samsung Tanzania,Rhoda Iddy(kulia) akimkabidhi mteja simu ya Samsung Galaxy S7 baada ya kuinunua mara baada ya uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam. 

Tractor hizi zinauzwa zipo katika hali nzuri karibuni sana

0
0
                                       MASSEY FERGUSON 178 bei ni milioni 19.5 tsh

FORD 4000 bei ni milion 17.5 tsh.
zipo Mbweni, Daresalaam
mawasiliano zaidi 0714242879


East Africa's leading female artist Vanessa Mdee 'Vee Money' brings you new heat with Niroge

0
0
Tanzania's dynamite is back at it again with her brand new single 'Niroge' off of her upcoming debut album Money Mondays. Niroge which is Swahili for compel me or bewitch me, is a coming of age love song about a love so strong that one would assume she was under a spell. 
It depicts what is also known as Ride or Die love. Written by Vanessa Mdee and Barnaba (who also wrote Vanessa's 2015 AFRIMA Award Afro Pop song of the year Hawajui) and Produced by Tanzania's Award winning Producer Nahreel at The Industry – Tanzania. 
This smash hit is a clear indication of Vee Money, Nahreel and Barnaba's undeniable chemistry. This melodic Swahili tune will have you spellbound accompanied by visuals shot in Johannesburg, South Africa by Justin Campos. 
Vanessa Mdee is a multi time Kilimanjaro Tanzania Music Award winner and recipient of the All African Music Awards - AFRIMA Best East African Female Artist in 2014 and recently won an AFRIMA Best African Pop Award for her song Hawajui. She has also been nominated for the 2015 MTV MAMAS Best Female Award and is currently in the running for Best Female East Africa at the KORA Awards 2016.

Mgombea uwakilishi Marekani William Jawando ahojiwa Kilimanjaro Studio, azungumza na Diaspora

0
0
Mgombea uwakilishi katika Bunge la Marekani William Jawando, amehojiwa katika studio za Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland nchini Marekani ambapo alizungumzia kuhusu mikakati yake katika kuisaidia Diaspora ya Afrika katika eneo lake na Marekani kwa ujumla.
Will, ambaye akishinda atakuwa ni mtu wa pili aliyezaliwa na Baba aliyetoka Afrika kuingia bungeni humo (baada ya Rais Obama) ameeleza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna ambavyo uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni muhimu Zaidi nchini Marekani, na hasa kwa wakazi wenye asili ya Afrika waishio vitongoji vya Washington DC.
Ikumbukwe kwamba, inakadiriwa kuwa mmoja kati ya wazaliwa kumi wa Afrika walipo nchini Marekani, anaishi eneo hili, na nusu yao, wameingia nchini baada ya mwaka 2000. Hivyo amefafanua namna ambavyo kuwa na mtu mwenye kuelewa na kuwakilisha vema jamii hiyo, ni muhimu kwa jamii hiyo.
Aligusia pia namna ambavyo asili yake na makuzi yake yamechangia yeye kuingia katika kazi za kuihudumia jamii, akaeleza vipaumbele vyake kwenye uongozi wake ujao na pia wito alionao kwa jamii ya waAfrika walioko Marekani.
Uchaguzi wa kuteuliwa kugombea kupitia chama cha Democrat utafanyika Aprili 26, lakini kura za mapema zitapigwa kati ya Aprili 14 na 21.
Kujua mengi kuhusu Will Jawando, maisha yake, kampeni na mipango yake, tembelea willjawando.com
Anagombea kiti kilichoachwa wazi na mwakilishi Chris Van Hollen ambaye ameamua kugombea kiti cha Seneti kinachoachwa wazi na Seneta Barbara Mikulski anayestaafu
Mahojiano kamili na Will Jawando yatakujia hivi karibuni
Baada ya mahojiano, Will alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wanaDiaspora wa Afrika waliokuwa ndani ya jengo ilipo studio.
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akipata picha na Mubelwa Bandio baada ya mahojiano
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando
Mgombea uwakilishi kutoka jimbo la Maryland, Will Jawando akizungumza na baadhi ya waAfrika waliohudhuria "Meet & Greet". 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Dk. Rajab Rutengwe amemuomba msamaha Rais Dr. Magufuli kwa kushindwa kuendana na kasi yake

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyemaliza muda wake, Dk. Rajab Rutengwe amemuomba msamaha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. John Pombe Magufuli kwa kushindwa kuendana na kasi ya "HAPA KAZI TU" hali iliyopelekea kuwekwa pembeni na nafasi yake kuchukuliwa na Dk. Kebwe Kebwe, ambapo amemuomba amfikirie upya kutokana na kutokujua pa kushika baada ya kuwekwa kando.

Dk. Rutengwe Aliyasema hayo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi ofisi kwa Mkuu mpya wa mkoa huo, Dk Kebwe S. Kebwe.

Mh. Luhaga Mpina aongoza zoezi la kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi

0
0
Aliyevaa shati ya blue Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira mh Luhaga Mpina akiweka taka katika gari la kuzolea taka katika mtaa wa TPDC Mikocheni JIjini Dar es salaam leo, Jumamosi ya mwisho wa Mwezi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali la usafi wa Mazingira
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina, akifanya usafi katika mtaro wa maji machafu katika mtaa wa TPDC, maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa siku ya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Picha na Evelyn Mkokoi wa Ofisi wa Makamu wa Rais

MWANASHERIA MKUU ZANZIBAR AAPISHWA RASMI LEO

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Bwana Said Hassan Said, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyeikiti wa Baraza la Mapinduzi alimteua Bwana Said Hassan jana kushika wadhifa huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 55 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. 
 Hafla ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu huyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
 Miongoni mwao ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis. 
 Wengine ni Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib,Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.








Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar.
Viongozi mbali mbali na watendaji waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.ALi Mohamed Shein akiwa katika picha na Said Hassan Said Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar na familia yake baada ya kumuapisha rasmi leo katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.


SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA BUNGE LA ISRAEL

0
0
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na  Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Mhe. Ronen Plot (kushoto) aliyemtembelea Ofisini kwake leo tarehe 26 Machi, 2016,Jijini Dar es Salaam.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Mhe. Ronen Plot  aliyemtembelea Ofisini.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Mhe. Ronen Plot  aliyemtembelea Ofisini.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Mhe. Ronen Plot  na viongozi wengine waliombatana na ujumbe huo.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Mzee Ibarahim Kaduma ambaye ni Mweyekiti wa Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT). Mzee Kaduma aliambatana na Ujumbe wa Israel uliomtembelea Spika ambao ndio wafadhili wa KLNT. Picha na Ofisi ya Bunge.

KITUO CHA KULEA WATOTO YATIMA CHA JANGO ZAIDA ORPHANAGE CENTRE CHAPATIWA MSAAADA

0
0
 Watoto Wanaoishi kwenye Kituo cha Jango zaidi Orphanage Sinza jijini Dar es salaam wakiwa kituoni hapo leo walipotembelewa na Wadau waliosoma Pamoja Shule ya Sekondari Bwawani.
 Baadhi ya Vitu mbalimbali vilivyotolewa.
 Wadau waliosoma Shule ya Sekondari Bwawani wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Mama Mlezi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Jango Zaida Orphanage centre  walipokitembelea kituo hicho na Kutoa Msaada ya Vitu MBalimbali kwajili ya Kusaidia Kutatua Changamoto Mbalimbali zinazokikabili kituo hicho.

Picha ya Pamoja na watoto wanaoishi katika Kituo Hicho

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

0
0

SIMU.TV:  Wavuvi ziwa Nyasa waililia bunge kutathmini na kuifanyia marekebisho  sheria mpya ya tozo za leseni ya uvuvi; https://youtu.be/6KzY5Be6n7E
 SIMU.TV:  Wakazi wa Magu wametakiwa kukamilisha malipo ya zaidi ya hati 800 za mashamba ili kurasimisha rasilimali ardhi; https://youtu.be/R_pW6KXSKaE
 SIMU.TV:  Mahakama kuu yaitupilia mbali zuio lililowekwa na mbunge wa Temeke dhidi ya aliyekuwa mbunge wa Temeke Abas Mtemvu; https://youtu.be/4-AHGCpqIsU
  SIMU.TV:  Wajumbe wa baraza la wawakilishi CCM wamefanya uchaguzi wa kumpata mjumbe atakayewakilisha CCM katika kuwania nafasi ya uspika;https://youtu.be/3qfw3IZZurw
 SIMU.TV:  Mabondia Said Mbelwa na Ibrahim Tamba kuchuana vikali leo hii katika pambano la masumbwi  ndani ya ukumbi wa Travelntine;https://youtu.be/vpZ72Ymsf_w 
 SIMU.TV:  Shirikisho la mchezo wa kikapu Dar es Salaam BD linatarajia uanzisha ligi ya vijana wa shule za sekondari ili kuimarisha vipaji; https://youtu.be/u3YaE2t7IH8 
 SIMU.TV:  Mahakama Zanzibar yajipanga kukusanya mapato zaidi ya MIL.200 kupitia benki ya Zanzibar kwa mwaka 2016-2017; https://youtu.be/4_eL_ecE54I

MAJAMBAZI YAUA NA KUJERUHI JIJINI MWANZA

0
0
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, SACP Justus Mamugisha, akitoa taarifa kwa wanahabari kwamba Watu wawili wameuawa Jijini Mwanza kwa kupigwa risasi na Majambazi, huku Wengine saba wakijeruhiwa katika tukio la uvamizi wa duka lililokuwa likitoa huduma mbalimbali za kifedha.
Habari Zaidi BONYEZA HAPA.

WIZARAYA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI YATEMBELEWA NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA

0
0
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelline Mabula (Mb), akisisitiza jambo kwa ujumbe kutoka Benki ya Dunia walipofika ofisini kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb) kufanya  mazungumzo mbalimbali katika Sekta ya ardhi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Willium Lukuvi (Mb), na Naibu wake kushoto kwake; Angelline Mabula (Mb), wakiwa na ujumbe kutoka Benki ya Dunia walipofika Wizarani hapo kufanya  mazungumzo mbalimbali katika Sekta ya ardhi. 
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images