Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1164 | 1165 | (Page 1166) | 1167 | 1168 | .... | 3348 | newer

  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiwasilisha mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, taarifa yake kuhusu ziara yake aliyoifanya hivi karibuni nchi Burundi. Katika taarifa yake ameelezea kutiwa matumaini na uteuzi wa Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa kuwa Mwezeshaji wa majadiliano ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi.
  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza kwa niaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokutana Ijumaa uliojadili kuhusu Burundi. Aliyeketi nyuma ya Balozi, ni Bw. Khamis Abdallah Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Burundi, Bw. Alain Amic Nyamitwe naye akielezea hali ya mambo na jitihada mbalimbali ambazo serikali ya Burudi imekuwa ikichukua katika kurejesha hali ya amani na utulivu.
  Wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, katika mkutano wao wa Ijumaa ambapo baada ya kupokea taarifa kuhusu Burundi, waliendelea na kikao chao cha ndani.

  Na Mwandishi Maalum, New York

  Wakati Mwezeshaji wa majadiliano kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa ameanza mchakato wa kukutana na viongozi na wadau mbalimbali. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema, uteuzi wa Benjamin Mkapa unatia matumaini.

  Ban Ki Moon ametoa kauli hiyo jana Ijumaa, wakati alipokuwa akiwasilisha mbele ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, taarifa kuhusu ziara yake aliyoifanya nchini Burundi mwezi uliopitia.

  “ Uteuzi uliofanywa na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa kumteua Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa kuwa mwezeshaji wa majadiliano kuhusu Burundi ni maendeleo yanayotia moyo”. Amesema Ban Ki Moon.


  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wamiliki wote wa silaha jijini hapa kuwasilisha taarifa ya uhalali wa silaha zao na kusajiliwa upya kwa wakuu wa polisi wa Wilaya (OCD). 

   Aidha amewataka watu wote wanao miliki silaha hizo kinyume cha sheria kuzisalimisha kabla ya kuanza kwa Oparesheni ya ukaguzi jijini hapa Julai mosi mwaka huu. Akizungumza Dar es Salaam jana wakati alipotembelea katika Kanda Maalum jijini hapa, Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama jijini hapa, wamiliki hao wafike katika ofisi za wakuu wa polisi wa wilaya kuanzia April mosi mwaka huu hadi julai mosi mwaka huu itakapo anza oparesheni hiyo. 

  Alisema lengo la hatua hiyo ni kujihakikisha na kujua idadi ya silaha zinazotumika na kuzisajili upya. "Hivyo kwa yule ambaye hakutumia siku hizo katika kuwasilisha taarifa au kusalimisha silaha tutaona kwamba anatumia silaha hiyo kinyume na kile ambacho kilikusudiwa kwa utoaji wa silaha," alisema. 

   Hata hivyo alisema kwa wale ambao hawana nyaraka nao katika kipindihicho wasalimishe silaha hizo na kwamba mtu huyo hata chukuliwa hatua na kwamba silaha hiyo itachukuliwa na kuwekwa kwenye utaratibu unaostahili. 

   Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa jiji linaloongoza kwa utulivu pamoja na kusitisha matukio ya ujambazi ya kutumia silaha, au pikipiki wala kusikia milio ya silaha na badala yake ni kuona jiji lina kuwa la amani na utulivu. 

   Makonda alitumia nafasi hiyo kulipongeza jeshi hilo na kuwatangazia utaratibu mpya wa kutoa tuzo kwa askari watakao pambana na ujambazi jijini hapa ambao wanawafanya watanzania wanaishi na hosfu katika kila kipindi cha miezi mitatu. 

   Alisema hatua hiyo ambapo skari bora atakao fanya vizuri katika pambana na ujambazi watapewa sh.milioni moja na mkuu wa mkoa huo ikiwa ni shemeu ya motisha na kuwatia moya katika kutimiza majukumu yao na katika hatua ya kupambana na ujambazi.  

  "Askari wanafanya kazi katika mazingira magumu katika kupambana na uhalifu hivyo kama mkuu wao wa mkoa hawezi kukaa kimya na kuona ni vyema kuweka fumo huo wa kuwaongezea motisha kwani hiyo ni kazi ngumu inayohitaji kutiwa moyo licha ya kwamba ni sehemu ya majukumu yao," alisema. 

   Kwa upande wake Kamanda Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema kuna kila sababu ya kuhakiki silaha zote kwani matukio mengi yanayofanyika wakikamatwa watuhumiwa wanakutwa na silaha zinazokamatwa ni zile ambazo zilitolewa kwa umiliki kwa lengo zuri lakini inakuwa tofauti. 

   Hivyo baada ya miezi mitatu tutaanza oparesheni kubwa ya kuwakamata kwani tunataarifa za watu wote wanaomiliki silaha na kuwaomba Watanzania kujitokeza na si kusubiri kukamatwa lakini kama anaamini anatumia silaha hiyo inatumiwa kihalali ni vema kuiwasilisha na taarifa zake.

   "Hivyo ni vema kuziwasilisha kwani hakuna haja ya kusubiri kukamatwa kwani mwishowake ni kufikisha mahakamani hivyo ni bora wafike katika sehemu elekezi kwaajili kuwasilisha taarifa zao na matumizi na kama umetumia risasi kumi ueleze katika hali gani," alisema.

  0 0  0 0


  0 0

  Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala Mbunge wa Jimbo la Nkenge akiweka jiwe la Msingi kuzindua Ujenzi wa chumba cha darasa kinachojengwa Shule ya Msingi Kikukwe Kanyigo. Chumba hicho kinajengwa kwa michango ya Wanakikukwe waliosoma katika shule hiyo. Balozi Kamala ametoa mifuko ishirini ya saruji kuunga mkono jitihada hizo.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon (katikati) akiwa na wenyeviti- wenza wa Jopo a ngazi ya juu kuhusu uwezeshaji wa wanawake kiuchumi pamoja na baadhi ya wajumbe wa Jopo siku ya uzinduzi wa Jopo hilo uliofanyika sambamba na mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake (CSW) unaoendelea hapa Umoja wa Mataifa
  Wenyeviti -Wenza wa Jopo la Ngazi ya Juu kuhusu Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, Rais wa Costa Rica, Mhe. Luis Guillerma Solis na Mkurugenzi Mtendaji wa IKEA Switzerland Bi. Simona Scarpaleggia wakibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi, mara baada ya kundi hilo kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, mapema wiki hii. Mmoja wa wajumbe wa Jopo ambao idadi yao ni 21 ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu. Ban Ki Moon ameunda Jopo hilo ili limpatie maoni na mapendekezo kuhusu uwezeshwaji wa mwanamke kupitia utekelezaji wa Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu.

  Na Mwandishi Maalum, New York

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amezindua Jopo la Nganzi ya Juu ambalo ameliunda kusaidia kufanya uchambuzi na kutoa mapendekeo ya namna ya kuchagiza kasi ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.

  Jopo hilo ambalo linaundwa na viongozi na wataalamu wa kada mbalimbali linaongozwa na WenyeViti -Wenza ambao ni Rais wa Costa Rika, Mhe. Luis Guillerma Solis na Bi. Simona Scarpaleggia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa IKEA Switzerland.

  Wajumbe wa Jopo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu, Mkuu wa Banki ya Dunia, Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Fedha ( IMF) Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Mkurugenzi Mtendaji wa UN- WOMEN, wapo pia Maprofessa na wataalamu wa uchumi, watafiti, viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wawakilishi kutoka serikalini, wataalamu wa masuala ya jinsia na fursa sawa na wafanyabiashara. Kwa pamoja jopo hilo linakuwa na wajumbe 21.


  0 0
 • 03/19/16--01:46: NEC yakigomea chama cha CUF
 • Na Clarence Nanyaro- NEC

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema haitambui kujitoa kwa Chama cha Wananchi (CUF), katika uchaguzi wa Mbunge Jimbo la Kijitoupele hapa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Jumapili licha ya kuwa Tume imepokea barua rasmi toka kwa uongozi wa Chama hicho.

  Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume ya Taifa Bw. Kailima Ramadhani amesema Tume imefikia maamuzi hayo kutokana na ukweli kuwa barua hiyo ya CUF  imechelewa huku maandalizi ya uchaguzi huo yakiwa yamekamilika na ni Wananchi tu kwa sasa Wanasubiriwa kwenda kupiga kura.

  Aidha, Bw. Kailima ameeleza kuwa, kwakuwa karatasi za kupigia kura zilishachapishwa na kuwasili hapa nchini tayari kwa uchaguzi huo, zitaendelea kuwa na picha za Wagombea wa CUF hata kama wamejitoa katika uchaguzi huo.

  Awali,wajumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji mstaafu Hamid Mahamood Hamid walitembelea katika vituo mbalimbali vya kupigia kura katika Jimbo la Kijitoupele ili kujiridhisha na maandalizi ya uchaguzi huo kabla ya uchaguzi kufanyika jumapili.

  Tume ilibaini kuwepo kwa baadhi ya kasoro ndogo ndogo katika baadhi ya vituo vya kupigia kura ikiwa ni pamoja na kubanduliwa kwa karatasi zenye majina ya wapiga kura, mfano katika kituo cha Skuli ya sekondari Kinuni.

  Jimbo la Kijitoupele lina jumla ya Wapiga kura wapatao 17,274 na vituo vipatavyo 53 vitatumiwa na wapiga kura ili kumchagua mbunge waJimbo la Kijitoupele siku ya Jumapili.

  Sambamba na Uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Kijitoupele, marudio ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar Oktoba 25,2015 ambayo matokeo yake yalifutwa uatafanyika Jumapili hiyo pia.

  Uchaguzi katika jimbo la Kijitoupele uliahirishwa mwaka jana kutokana na hitilafu ndogo ndogo zilizojitokeza katika karatasi za kupigia kura, kabla ya kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, 2015.

  0 0

  MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Hashim Kambona amewataka wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ili wapate matibabu pindi wakiugua .

  Akizungumza kwenye uzinduzi wa uhamasishaji wa kujiunga na CHF uliofanyika mji mdogo wa Mirerani, Kambona alisema kaya nyingi zinatakiwa kujiunga na mfuko huo kwani unalipa sh10,000 na kutibiwa kwa mwaka mmoja. 

  Alisema wilaya ya Simanjiro ina utajiri wa kutosha ikiwemo madini, mifugo na ardhi nzuri yenye rutuba inayofaa kwa kilimo na kupitia rasilimali hizo jamii hiyo inapaswa kujiunga na mfuko huo ambao utawasaidia kujitibu pindi wakiugua.

  “Pamoja na hayo japokuwa wilaya yetu ni tajiri kuliko wilaya nyingine kwa hapa nchini, lakini wananchi wetu maisha yao wanayoishi ni ya hali ya chini,hivyo msaada pekee wa matibabu ni kujiunga kwa wingi na CHF,” alisema Kambona.

  Alisema kaya nyingi zikijiunga na mpango huo zitasababisha hata dawa kupatikana kwa wingi kwenye vituo vya afya na zahanati zilizopo maeneo mbalimbali kutoka bohari kuu ya dawa (MSD) hivyo wajiunge kwa wingi.

  Mkurugenzi wa uendeshaji wa (NHIF) Raphael Mwamoto alisema CHF ni utaratibu unaoilenga jamii kwenye maeneo ya halmashauri na wanachotakiwa ni kuchangia kati ya sh5,000 au sh10,000 au sh15,000 kiwango kinachopangwa na wilaya husika.

  “Mfano hapa Simanjiro kaya huchangia sh10,00 na baada ya  kutoa fedha hizo, serikali nayo inaongeza malipo yanayoitwa tele kwa tele kwa kiasi hicho cha sh10,00 kwa kila kaya, kwa ajili ya kupata tiba,” alisema Mwamoto.

  Alisema kinachotakiwa hivi sasa ni halmashauri husika kuweka miundombinu vizuri na kuboresha huduma za afya ikiwemo dawa na vifaa tiba, ili jamii ihamasike kuchangia mfuko huo kwa kuona inanufaika na mfuko huo.
  Mkurugenzi uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Raphael Mwamoto akizungumza kwenye uhamasishaji wa wananchi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa kaya ya watu sita kuchangia shilingi 10,000 na kupata matibabu kwa mwaka mmoja.
  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Hashim Kambona akizungumza na wananchi wa Mji mdogo wa Mirerani, juu ya kujiunga kwa wingi na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa kila kaya kulipa shilingi 10,000.
  Baadhi ya wakazi wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakijiung ana mfuko wa afya ya Jamii (CHF) ambapo kaya yenye watu sita yaani baba, mama na watoto wane wanajiunga kwa shilingi 10,000 na kupata matibabu kwa mwaka mmoja.

  0 0

   
   Dkt. Ayoub Rioba ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

  Prof. Godius Kahyarara ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).

  0 0

  By Sultani Kipingo
  Tanzanians are happy with the implementation speed of the proposed construction of the Tanzania-Uganda crude oil pipeline which is expected to start in August this year, and will be completed in 2019. 
  Many of those interviewed expressed gratitude to President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda and his Tanzanian counterpart Dr. John Pombe Joseph Magufuli for initiating the 4-billion-U.S. dollar oil pipeline project that is expected to hasten socio-economic development between the two nations.
  “We are overwhelmed by the rapidity of the project considering only two weeks have  passed since  Presidents Museveni and Dr. Magufuli  jointly approved the project when they met in Arusha. 
  “It is unbelievable to note that officials from both sides have this week signed the agreement and come August the construction work takes off”, said Ms Natala Kimaro of Moshi. 
  Amani Abdallah of Tanga  said that the 1,403-kilometer pipeline that will link oil fields in Uganda’s Lake Albert, Hoima region to Tanga port in Tanzania is testimony to true East African integration spirit, hoping more such projects would be initiated. 
  The construction of the crude oil pipeline will be carried out by three oil firms–UK’s Tullow Oil PLC, France’s Total E&P and China’s Cnooc. Once completed, the pipeline is expected to transport up to 200,000 barrels per day passing through a number of Tanzanian regions from the Indian Ocean port of Tanga to Uganda. 
  The construction will lead to installations of 200km of permanent new roads and corresponding bridges, and upgrades to 150km of existing roads, opening up regional integration in the energy sub-sector. 
   Tanzanians are also happy that that the crude oil pipeline project will also increase foreign Direct Investment  by more than 50 percent per annum, let alone creating over 15,000 jobs.
  Tanzania President Dr. John Pombe Joseph Magufuli announces the crude oil pipeline project to reporters after his meeting with President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda on March 1, 2013 in Arusha in the sidelines of the  The 17th Ordinary East African Community (EAC) Heads of State Summit 
  "The project will be implemented at Dr. Magufuli's  speed" jokes President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda when confirming  the project to reporters after talks with his host President Dr. John Pombe Joseph Magufuli on March 1, 2013 in Arusha in the sidelines of the  The 17th Ordinary East African Community (EAC) Heads of State Summit. 
  Tanzania's Minister for Energy and Minerals  Prof. Sospeter Muhongo (second left) and Uganda's Minister for Energy and Minerals Development Engineer  Irene Muloni ( wa tatu right), with the Managing Director of the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) Dr. James Mataragio  (left) and the General Manager of  Total E&P Uganda, Mr Adewale Fayemi (second right) sign the crude oil pipeline project implementation plan in Arusha on March 17, 2016. Seated extreme right is Permanent Secretary Ministry of  Energy and Minerals Development of Uganda Dkt. Kabagambe Kaliisa 
  Map of the proposed crude oil pipeline project

  0 0


  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefafanua kwamba uchunguzi wao umeonyesha kwamba Mke wa Rais, Mama Janet Magufuli hana akaunti ya Facebook na tovuti inayohamasisha watu kuomba mikopo ya vikundi vya Vicoba.

  Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dr Ally Simba amesema Dar Es Salaam Jumamosi Machi 19 kwamba akaunti ya face book ambayo iliyodaiwa kuwa ni ya Mama Janet ilianzishwa na matapeli wa mtandao.

  Dr. Simba alisema TCRA imeshafungia akaunti hiyo ya Facebook na tovuti ya www.focusvikoba.wapka.mobi ambayo ilikuwa ina tarifa za kutaka wananchi kutuma pesa za kiingilio kwa Vicoba ili wapate mikopo.

  Dr. Simba alisema ingawaje kumekuwepo na maendeleo na mabadiliko makubwa katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watoa huduma za mawasiliano, idadi ya watumiaji na aina ya huduma zinazotolewa kuna watumiaji wachache wanaotumia huduma hivyo kutenda uhalifu kupitia simu za mkononi na kwenye intaneti kwa kuanzisha tovuti za kihalifu na kupitia mitandao ya kijamii kama vile face book.

  Alisema hivi karibuni kumekuwa na matukio ya wahalifu hawa wa mtandao kuanzisha tovuti na blogu na pia kurasa za facebook kwa kutumia majina ya viongozi wakuu wa nchi, wabunge na watu wengine maarufu.

  Wahalifu hawa wanawadanganya wananchi kwamba kuna fursa za kupata mikopo au misaada kupitia vikundi vya kusaidiana, maarufu kama VICCOBA na kuwataka wananchi watume fedha za kujiunga na huduma hizo kwa njia za simu za mkononi.

  Alisema pamoja na kuzifungia akaunti hizo za facebook na tovuti, Mamlaka inashirikiana na Polisi kuchunguza matukio hayo na tayari hatua kubwa imefikiwa katika kuwakamata na kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria. Mkurugenzi Mkuu alisema kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 15 (1) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015, mtu yeyote haruhusiwi, kwa kutumia kompyuta, kujifanya yeye ni mtu mwingine15. 

  Adhabu kwa kutenda kosa hili imeainishwa kwenye kifungu cha 15 (2) ambacho kinasema mtu akipatikana na hatia anaweza kutozwa faini ya isiyopungua shilingi milioni TANO au mara tatu ya thamani ya kile ambacho amekipata kupitia ulaghai huo, au kiasi ambacho ni kikubwa kati ya faini na mara tatu ya alichokipata. Vilevile anaweza kufungwa kifungo kisichopungua miaka SABA au vyote.

  Uchapishaji wa taarifa za uwongo ni kosa chini ya Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015. Kwa mujibu wa kifungu hicho, mtu yeyote ambaye anachapisha taarifa kwa kutumia mfumo wa kompyuta akijua kwamba taarifa alizochapisha sio za kweli, ni za udanganyifu na sio sahihi na kwa lengo ka kukashifu, kutishia, kutukana,kudanganya na kuptosha umma anatenda kosa ambalo adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni TANO au kifungo miaka mitatu au vyote.

  Dr. Simba aliwaomba wananchi kwa ujumla na hasa watumiaji wa huduma za mawasiliano kuzingatia sheria wanapotumia huduma za mawasiliano. 
  Aidha aliwataka Watanzania kuwa macho dhidi ya utapeli kupitia mitandao ya kijamii, tovuti na blogu ambazo zinawataka kutuma fedha au kuchangia kitu chochote ili wapewe mikopo au misaada. Wananchi wakiona matangazo ambayo wanayatia shaka, wawasiliane na Mamlaka ya Mawasiliano kwa taarifa zaidi.

  Kuhusu maendeleo ya sekta, alisema hadi Desemba 2015, idadi ya laini za simu za mkononi ilikuwa 39,808,419 ukilinganisha na 2,963,737 mwaka 2005. Watumiaji wa intaneti walifikia 17,263,523 Desemba 2015 ukilinganisha na 1,013,104 mwaka 2005.

  0 0  Kama umekua nje ya Jiji la Dar es Salaam kwa muda mrefu, ni wazi kwamba ukija utahitaji kupata maelekezo ya mambo kadha wa kadha ili kurahisisha maisha na shughuli zako kwani kuna mabadiliko ya vitu vingi. 
  Pamoja na badiliko kubwa la UTUMBUAJI MAJIPU ambalo liko kinywani mwa kila mtu unayekutana naye, kuna mabadiliko ya matumizi ya barabara hasa zile ambazo zinatarajiwa kutumika kwa mabasi yaliyolenga kuboresha usafiri wa umma. Barabara hizi (hasa Morogoro na Kawawa) zimekua safi zaidi; zimekua nyembamba ukilinganisha na awali; zimeongezwa taa za kuongoza magari; na zina alama mpya/za ziada. 
  Kama vile haitoshi, maboresho ya barabara hizi yamebadili mwelekeo wa baadhi ya safari kwani kuna maeneo huruhusiwi tena kukata kulia au kushoto; kuna maeneo huwezi kuingi kwenye barabara za pembeni; na kwingine unalazimika kuchepuka na kupita njia za pembeni ili kupata barabara kuu. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Mgeni Rasmi katika maadhimisho Mkuu wa mkoa wa dar-es-salaam Mhe. Paul makonda akihutubia waumini waliojitokeza changia damu
   Wageni waalikwa katika maadhimisho hayo kutoka kushoto Meneja damu salama kanda ya Mashariki Dr Aveline Mgasa,  Mganga mkuu mkoa wa Dar , Dr Grace magembe, Mhe. Paul Makonda, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr Mpoki Ulisubya.
  Baadhi ya waumini wakichangia damu kwa hiari

  Mpango wa Taifa wa Damu salama kwa kushirikiana na waumini wa dhehebu la sabato wameendesha zoezi la kuchangia damu katika mikoa mbalimbali hapa nchini, mikoa hiyo ni Mara, Kigoma, Dar-es-salaam, Dodoma, Mwanza, Kilimanjaro,Tabora, Morogoro, Mbeya na Iringa.

  Siku ya matendo ya huruma hufanyika jumamosi ya tatu ya mwezi wa tatu kila mwaka, ambapo waumini hushiriki katika huduma mbalimbali za jamii. Lengo ni kukusanya chupa za damu 3000 kutoka katika mikoa hiyo ambazo zitasambazwa Hospitali mbali mbali kuokoa maisha ya wahitaji

  0 0

  Kushoto ni Bwana Harusi JOHN SAMWEL CHACHA akiwa pamoja na Bibi Harusi Milika Daniel Binagi, katika hafla ya harusi yao iliyofanyika Juzi Alhamisi Machi 17,2016 Rebu, Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
  Picha Zaidi BONYEZA HAPA

  0 0  0 0

   Beki wa Timu ya Yanga, Haji Mwinyi akimtoka Mchezaji wa timu ya APR ya nchini Rwanda, katika Mchezo wa marudiani wa Klabu Bingwa barani Afrika, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa timu zote kufungana bao 1-1, na kuifanya timu ya Yanga kuendelea na mbio za mashindano hayo, huku timu ya APR ikiyaaga baada ya   kukubali kipigo cha bao 2-1 katika mchezo wa awali uliopigwa nchini Rwanda.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI - MMG
   Kiungo wa Timu ya APR, Yannick Mukunzi akiruka juu na kupiga mpira wa kichwa kwa ustadi mkubwa, lakini haukuza matunda baada ya beki wa Yanga, Vicent Bossou kuuzuia, katika Mchezo wa marudiani wa Klabu Bingwa barani Afrika, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa timu zote kufungana bao 1-1.
   Nahodha wa Timu ya APR, Iranzi Jean Claude, akichuana vikali kuwania mpira na Mshambuliaji wa Pembeni wa Yanga, Deus Kaseke, katika Mchezo wa marudiani wa Klabu Bingwa barani Afrika, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa timu zote kufungana bao 1-1.
   Mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe, akionyesha umahiri wake wa kuwachambua mabeki wa Timu ya APR, katika Mchezo wa marudiani wa Klabu Bingwa barani Afrika, uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Mchezo huo umemalizika kwa timu zote kufungana bao 1-1.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 03/19/16--10:09: Article 18


 • 0 0


  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda, akizungumza na wenyeviti na maofisa watendaji wa jiji la Dar es Salaam leo kuhusu mambo mbalimbali haswa suala la usafi wa mazingira.
   Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Theresia Mmbando akiongoza mkutano huo.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala,  Mhe. Raymond Mushi akizungumza katika mkutano huo.
   Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema akizungumza katika mkutano huo.
   Mwakilishi wa Taasisi ya Wakala wa Upimaji Ardhi Tanzania Bw. Linus Kinyondo akizungumzia suala zima la ujenzi wa nyumba kwa kuzingatia mipango miji ili kutunza mazingira.
   Wenyeviti na maofisa watendaji wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (hayupo pichani)Picha na Dotto Mwaibale


older | 1 | .... | 1164 | 1165 | (Page 1166) | 1167 | 1168 | .... | 3348 | newer