Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

SIMUTV: MAPITIO YA MAGAZETI LEO


IN LOVING MEMORY OF LATE DR L. OLE LENGINE

$
0
0
THE LATE DR L. OLE LENGINE 
(10/12/1949 -28/03/2014)

Two years has passed since your loss. You were a dad who was so special; and who was loved very much and brought so much happiness to the many hearts you have touched.

‘’Work hard and always work as team”

That was your favourite quote; and we promise to live with it.

We miss you so incredibly much, and wish you were here to see everything we are doing, but we are trying to be strong as we know that’s what you would always have wanted.

You are remembered by your lovely wife Mrs Endesh Ole Lengine , your mother,your children Peter, Esther ,Dr Emmanuel, and Martin,your grandchildren, your sisters & brothers ,relatives, inlaws friends and the whole staff team of EKENYWA E.N.T HOSPITAL.

Isaiah 41:10  “So do not fear, for I am with you; do not be dismayed, for I am your God.  I will strengthen you and help you; I will uphold you with my righteous right hand.”

MAY OUR ALMIGHTY GOD REST YOUR SOUL IN PEACE.AMEN.

UBALOZI WA TANZANIA CANADA WAWA MWENYEJI WA KIKAO CHA MABALOZI WA NCHI ZA SADC

$
0
0
Ubalozi wa Tanzania nchini Canada ulikuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mabalozi wa nchi wanachama wa SADC ambao wana ofisi za Ubalozi mjini Ottawa, Canada. Mkutano huo ambao umehudhuriwa na mabalozi wote wanane wanaowakilisha nchi zao Canada ulifanyika katika makaazi rasmi ya Balozi wa Tanzania hapa Ottawa, nchini Canada tarehe tarehe 15 Machi, 2016. 

Nchi zilizowakilishwa ni Zimbabwe, Madagascar, Angola, Congo -DRC, Lesotho, Afrika ya Kusini, Zambia na Tanzania. Mbali na maswala mengine muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano huo mfupi wa siku moja agenda kubwa ya mkutano ilikuwa ni kuimarisha mshikamano wa kufanya kazi kwa pamoja ili kuziletea maendeleo nchi wanachama. 

 Aidha wanachama wa mkutanano hupata fursa ya kubadilishana taarifa za mambo mbalimbali yanayoendelea katika nchi zao. Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka aliwaeleza Mabalozi wenzake juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano za kuinua hali za maisha ya watanzania hasa wenye hali ya chini kupitia kauli mbiu ya “ Hapa Kazi Tu”.
Balozi wa Zimbabwe nchini Canada ambaye ni Mwenyekiti wa Mabalozi wa SADC, Ottawa, Mhe. Florence Zano Chideya, akiweka saini katika kitabu cha wageni, mara baada ya kuwasili katika makaazi rasmi ya Balozi wa Tanzania, Ottawa, Canada.
Mabalozi wawakilishi wa SADC Ottawa, Canada wakiwa katika chumba cha mkutano, Tanzania House.
Balozi wa Tanzania nchini Canada, Mhe. Jack Mugendi zoka (kulia) akiwakaribisha rasmi mabalozi wenzake wa nchi za SADC, Tanzania House wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Kushoto ni Balozi wa Zimbabwe nchini Canada ambaye ni Mwenyekiti wa Mabalozi wa SADC, Ottawa, Mhe. Florence Zano Chideya.
Sekretarieti ya Mkutano wa SADC uliofanyika Tanzania House. Wa kwanza kutoka kulia ni Bw. Admire Hwata Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Zimbabwe, Wa katikati ni Bw. Leonce E. M. Bilauri, Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania, akifuatiwa na Bw. Liteboho K. Mahlakeng, Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Lesotho.
Pichani ya pamoja, Mbele wa kwanza kutoka kulia ni Mhe. Simon Constant Horace, Balozi wa Madagascar, Kulia kwake ni Mhe. Dr Mathabo Theresia Tsepa, Balozi wa Lesotho akifuatiwa na Mhe. Florence Zano Chideya, Balozi wa Zimbabwe nchini Canada ambaye ni mwenyekiti wa Mabalozi wa nchi za SADC. Aliyesimama kushoto mstari wa mbele ni Bw. Evaristo Kasunga, Kaimu Balozi wa Zambia. Balozi wa Tanzania Mhe. Jack Mugendi Zoka ambaye amesimama nyuma akiwa amevalia Tai ya bendera ya Taifa amepakana kulia kwake na Balozi wa Afrika ya Kusini Mhe.Membathisi Shepherd Mdladlana ambaye mbele yake ni Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Bw. Kalelwa Kalimasi. Aliyesimama nyumba kabisa ya picha ni Mhe. Edgar Augusto Martins, Balozi wa Angola.

WAZIRI KITWANGA ATEMBEA MITAANI AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA PEMBA, ATEMBELEA MSITU WA NGEZI NA KUGUNDUA HAKUNA WAKIMBIZI WOWOTE

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wa pili kulia) akitembea mitaani eneo la Chake Chake Pemba, Zanzibar kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu usalama wao katika kipindi cha uchaguzi kisiwani humo. Waziri Kitwanga ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdullah (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman (wapili kushoto aliyevaa kaunda suti) na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kusini Pemba, Ahmed Khalid Abdulla (kushoto, aliyevaa tai. Kitwanga aliridhishwa na juhudi za kuimarisha ulinzi katika kisiwa hicho.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuuzunguka msitu wa Taifa wa Ngezi, uliopo Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba ambao baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar walisambaza taarifa za uongo kuwa kuna wakimbizi wamejificha katika msitu huo baada ya kukimbia vurugu kisiwani humo. Hata hivyo hakuna mkimbizi yeyote aliyekuwepo katika msitu huo na wananchi wapo katika makazi yao wakiendelea na shughuli zao za kujitafutia kipato. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nasri.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na wauza nguo wa Soko Kuu la mjini Chake Chake, Pemba. Wananchi hao walikuwa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida bila wasiwasi wowote. Waziri Kitwanga pia alisikiliza maoni ya wananchi hao kuhusu uchaguzi mkuu na kuridhishwa na juhudi za kuimarisha ulinzi katika kisiwa hicho.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, mjini Chake Chake, Pemba, kuhusu masuala mbalimbali ya uimarishaji ulinzi katika kipindi cha uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Machi 20, 2016. Kushoto meza kuu ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mwanajuma Majid Abdullah na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omari Khamis Othman.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

TASAF yapatiwa Dola milioni 665 kunusuru kaya masikini

$
0
0


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akiongea na wadau wa maendeleo mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 zilizotolewa na Wadau wa Maendeleo ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wake wa Kunusuru Kaya Masikini nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akibadilishana mkataba wa makubaliano na Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird (kushoto) mara baada ya kusaini makubaliano ya jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 zilizotolewa na Wadau hao ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akisaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Dola za Kimarekani milioni 665 zilizotolewa na Wadau wa Maendeleo nchini ili kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini nchini.
Wadau wa Maendeleo wakimskiliza Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo nchini ambaye pia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird wakati wa mkutano jijini Dar es salaam.

TAARIFA YA MSIBA WA MZEE MATHEW CHANDO

$
0
0
Familia ya Bwana Mathew Chando wa Mikocheni Regent Dar es salaam inasikitika kutangaza kifo cha Baba yao mpendwa mzee Mathew Chando kilichotokea tarehe 15/03/2016 huko  Regent Estate mtaa wa Chato  Dar es salaam.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 19/03/2016 saa 9 alasiri katika makaburi ya Kinondoni Dar es salaam na yatatanguliwa na ibada ya mazishi itakayofanyika katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Msasani Dar es salaam kuanzia saa 7 mchana.

Habari ziwafikie ukoo wote wa Mathew Chando,ndugu,jamaa na marafiki popote pale walipo. msiba uko nyumbani kwa marehemu Regent estate mtaa wa chato dar es salaam.

"Yesu akwambia,mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi,ajapokufa,atakua anaishi". Yohana 11:25.

SPIKA NDUGAI ATEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT

$
0
0
Mkurugenzi wa Hospitali ya Walemavu CCBRT, Bi. Brenda Msangi akimueleza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) kuhusu namna ya utendaji kazi hospitalini hapo. Spika alitembelea hospitali hiyo kuangalia utendaji kazi kama mlezi wao.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (mwenye tai nyekundu) akipokea machapisho yanayohusu masuala ya walemavu kutoka kwa Afisa Mtetezi CCBRT wa masuala ya walemavu, Bw. Fredrick Msigala wakati alipotembelea hospitali hiyo kwa mara ya kwanza akiwa ni Mlezi wa Hospitali hiyo.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akipata maelekezo juu ya namna ya wagonjwa wa macho wanavyowekewa macho bandia (artificial eyes) wakati alipotembelea hospitali hiyo kwa mara ya kwanza akiwa ni Mlezi wa Hospitali hiyo. Kulia ni ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mpoki Ulisubisya.

G4S NA BPF WAPANDA MITI SHULE YA MSINGI HANANASIF, WAENDESHA MAFUNZO YA MCHEZO WA RAGA

$
0
0
Meneja wa taasisi ya Bhubesi ya nchini Uingereza, (BPF), ambayo kwa sasa inaendesha mafunzo ya kuunyanyua mchezo wa Raga (Rugby), sambamba na kusaidia jamii pamoja na maendeleo mashuleni na kwenye vituo vya kijamii, Mark Cole, (kushoto), akinyunyuzia maji kwenye mti alioupanda kwenye shule ya msingi Hananasif ya jijini Dar es Salaam, Machi 18, 2016. BPF kwa kushirikiana na kampuni ya ulinzi ya kimataifa ya G4S ya jijini Dar es Salaam, wameendesha mafunzo hayo kwa muda wa siku tano kwa shule sita za jijini na Jumamosi hii Machi 19, 2016 wanafunzi walioshiriki kwenye mafunzo hayo watashindana katika bonanza kubwa litakalofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mapambano, Sinza jijini. Anayeshuhudia mwenye kapelo, ni Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko cha G4S, Alfred Elia. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
Wanafunzi wa shule ya msingi Hananasif wakiwa kwenye mafunzo ya mchezo wa raga, Machi 18, 2016.
Wanafunzi wa shule ya msingi Hananasif wakiwa kwenye mafunzo ya mchezo wa raga, Machi 18, 2016.

Wanafunzi wa shule ya msingi Hananasif wakiwa kwenye mafunzo ya mchezo wa raga, Machi 18, 2016.


SIMU TV: Polisi Zanzibar Waaswa

KAMPUNI YA HUSEA YASHEREKEA KUTIMIZA MWAKA MMOJA NA AKINAMAMA WALIOJIFUNGUA LEO KATIKA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA.

$
0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya HUSEA imeadhimisha mwaka mmoja tangu kuazishwa kwake Machi mwaka huu kwa kutoa msaada wa vifaa vya hospitali na kuwapa zawadi akinamama waliojifungua leo katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wandishi wetu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUSEA , Pamela Maro amesema kuwa Kampuni hiyo inajishughulisha na Mipango miji, utoaji ushauri bure kuhusiana na Ardhi, Upimaji wa Ardhi pamoja na uchoraji ramani za nyumba, pia amesema kuwa ofisi za Kampuni ya kampuni ya Husea zipo Sinza Palestina kwa yeyote anayetaka ushauri kuhusiana na ardhi anaweza kufika maeneo hayo kujipatia ushauri bila malipo.

Pia Pamela amewaasa wanawake waliotoka kujifungua leo na wanawake wote wanaopenda kumiliki ardhi kisheria waende katika ofisi zao ili waweze kupata ushauri wa bure kuhusiana na maswala ya ardhi.

Kwa upande wa Daktari Mkuu wa Hospitali ya Palestina Sinza, Wandi Kariame amewapongeza wafanyakazi wa  kampuni ya HUSEA kwa kuadhimisha mwaka mmoja leo.

Pia amewashukuru kwa  kuona mahitaji ya Hospitali hiyo na kuwapongeza wanawake waliojifungua leo kwa kuwapa zawadi ikiwa ni kuadhimisha siku iliyofunguliwa ofisi hiyo kwa kufikisha mwaka mmoja wa kampuni hiyo kwani wangeweza kwenda  katika hospitali nyingine au kwenda kilabu cha  pombe (Bar) kwenda kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni yao kwa kunjwa na kula vitu wanavyovitaka au kunywa pombe tuu lakini wamewaona wao.
Mratibu Huduma Tiba katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Palestina Sinza, Faith Mdee akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Husea inayojishughulisha na utoaji ushauri, upimaji wa viwanja, uchoraji ramani za nyumba pamoja na mipango miji.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUSEA , Pamela Maro akimkabidhi Daktari Mkuu wa Hospitali ya Palestina Sinza, Dkt. Wandi Kariame aadhi ya vifaa vinavyotumika katika uzalishaji katika wodi la wazazi katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Muuguzi katika wodi ya wazazi katika hospitali Palestina Sinza.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUSEA , Pamela Maro  pamoja na madaktari wa hospitali ya Palestina Sinza wakimkabidhi baadhi ya zawadi zilizotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Husea, mama aliyotoka kujifungua katika hospitali hiyo, Bahati Ramadhani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUSEA , Pamela Maro(Kushoto) akiwa na baaadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya hiyo katika picha ya pamoja mara baada ya kutoa zawadi kwa watoto walipozaliwa leo katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni hiyo tangu kuanzishwa.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

IKULU YAKABIDHI GARI JIPYA LA WAGONJWA KWA HOSPITALI YA WILAYA YA CHALINZE

$
0
0
Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo akimkabidhi funguo za gari jipya la wagonjwa Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya shughuli ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze. Tukio hilo lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akishukuru mara baada ya kukabidhiwa gari la kubebea Wagonjwa na Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwasha gari jipya la Wagonjwa lililotolewa na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiendesha gari hilo la wagonjwa lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI



Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amekabidhi  gari la kubebea wagonjwa kwa hosipitali ya wilaya ya Chalinze, Ikiwa ni utekelezaji wa ilani na  ahadi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa wananchi ikiwa ni pamoja na wa jimbo la Chalinze.

Gari hilo la kubebea wagonjwa limekabidhiwa kwa niaba ya Rais, na Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo kwa  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hilo, Katibu Mkuu Ikulu Ndugu Peter Ilomo amesema gari hilo limetolewa na Mheshimiwa Rais kwa hosipitali hiyo ikiwa ni kuitikia wito na utekelezaji wa ilani na ahadi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wake kote nchini.

Aidha, Ndugu Ilomo amewaomba viongozi wa jimbo la Chalinze kulitumia gari hilo kwa matumizi yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi wa eneo hilo.

Akipokea gari hilo kwa niaba ya wananchi wa jimbo na  Wilaya ya Chalinze, Mbunge wa jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amemshukuru Mheshimiwa Rais    Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada huo na kuahidi kulitumia gari hilo kwa malengo yaliyokusudiwa, na kusema kuwa, utendaji kazi wa Rais Magufuli umekuwa ukiungwa mkono na wananchi wa kada mbalimbali na kuwaomba watanzania kuzidi kumuombea kwa Mungu.

Kwa upande wake Dakta Nasoro Ally Matuzya, amesema gari hilo limekuja kwa wakati muafaka kwa kuwa umezingatia utekelezaji wa malengo ya Milenia hususan lengo namba nne  linalosisitiza kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano

Naye Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Chalinze Ndugu Saidi Omar Zikatimu amesema gari hilo la kubebea wagonjwa litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo la Chalinze hususan katika kusaidia kutoa wagonjwa ambao wako katika maeneo ya vijijini wilayani humo na kuwafikisha katika hospitali ya Chalinze na hivyo kunusuru maisha yao kwa kupata huduma za afya kwa haraka.

Mbali na Wilaya ya Chalinze kupata msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa, tayari magari mengine mawili ya kubebea wagonjwa yameshakabidhiwa katika vituo vya afya vya Kiroka na Kisemu mkoani Morogoro.

Hospitali mpya ya Wilaya ya Chalinze imepanda hadhi kutoka kituo cha Msoga ambayo ilikuwa haina gari la kubebea wagonjwa na hivyo kufanya usafirishaji wa wagonjwa kutoka hospitali hiyo hadi hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi au kutoka maeneo ya vijijini kuwa mgumu.

Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais 
Ikulu

18 Machi 2016.

WAANDISHI WA HABARI KUTOKA NCHINI FINLAND WATEMBELEA TAASISI YA UONGOZI.

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja (wapili kutoka kushoto) akizungumza na kundi la waandishi wa habari kutoka nchini Finland (hawapo pichani) mapema leo walipotembelea taasisi hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Milma Kuttenen, Mshauri wa masuala ya Ushirikiano kutoka Taasisi ya UONGOZI Bi. Liisa Tervo na Mkuu wa Utafiti na Sera kutoka Taasisi ya UONGOZI Bw. Dennis Rweyemamu. 

 Kundi la waandishi wa habari 15 kutoka nchini Finland waliotembelea Taasisi ya UONGOZI mapema leo ikiwa ni moja kati ya mafunzo yao katika programu maalum ya maendeleo na sera inayoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland. Waandishi hao ambao wapo nchini kwa muda wa siku tano pia walisindikizwa na watumishi wawili kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Finlan.

Mkuu wa Idara ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Milma Kuttenen (kushoto) akitoa neno lake la shukrani kwa niaba ya waandishi wa habari na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, walipotembelea Taasisi ya UONGOZI kufahamu shughuli zake mapema leo.  

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA NHC.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda (kushoto kwake), wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara kwenye miradi miwili ya Shirika la Nyumba la Taifa ya NHC Mwongozo na NHC Eco Residence uliopo Kinondoni Hananasif. Kwa ujumla Kamati ya Bunge imeridhishwa sana na utendaji mzuri wa Shirika la Nyumba la Taifa na imeahidi kuyavalia njuga masuala ya Double Taxation kwa serikali ili lifanyiwe kazi na Watanzania wengi zaidi wapate nyumba za kuishi na suala la Mamlaka husika kufikisha huduma za kijamii katika nyumba za NHC zinakojengwa kama za Maji, Umeme na Barabara. Picha Zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii cha NHC.
Mh. Wilfred Lwakatare akiongozana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Sixtus Mapunda na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Angelina Mabula wakiwasili kwenye eneo la mradi wakati Kamati hiyo ya Bunge ilipofanya ziara katika mradi wa nyumba za gharama nafuu wa NHC Mwongozo.

UMOJA WA VYAMA VYA SIASA VISIVYO NA UWAKILISHI BUNGENI VYATOA TAMKO LA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA MAREJEO ZANZIBAR.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Makatibu wa  Umoja wa Vyama visivyo na uwakilishi Bungeni, ambae pia ni Katibu wa Chama cha SAU, Ali Kaniki  akizungumza na wandishi wa Habari katika ukumbi wa Studio ya kurikodia Rahaleo kuhusu kushiriki uchaguzi wa marejeo wa Zanzibar tarehe 20 mwezi huu.
Mmoja wa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha TLP Bwana. Hafidh Hassan Suleiman akithibitika wa kugombea na kuwataka wananchi kumpikia kura yeye. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

Na waandishi wetu.   Maelezo Zanzibar.
Umoja wa vyama  vya siasa ambavyo havina  uwakilishi Bungeni wametoa tamko rasmi la kushiriki uchaguzi  wa marejeo tarehe 20 mwezi huu na wamewataka wazanzibar kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi huo.

Hayo yamezungumzwa na makatibu wakuu wa vyama hivyo wakati walipokuwa wakizungumzwa na waandishi wa habari  katika ukumbi wa studio za Rahaleo  mjini Zanzibar.

Wamesema Chama chochote cha siasa kazi yake ni kushiriki uchaguzi na sio kususia kwani kufanya hivyo kutakoseshawananchi  haki yao ya msingi na  kurudisha nyuma shughuli za maendeleo.

Aidha  wameamua kurejea uchaguzi huo kutokana na kasoro zilizojitokeza uchaguzi wa mwanzo  ambapo  mambo mengi   yalionesha dhahiri  ulikuwa na kasoro za wazi wazi.

 Makatibu hao wamesema kurejewa uchaguzi sio jambo geni duniani  na yapo mataifa mengi yamewahi kurejea uchaguzi kutokana na kasoro mbali mbali zilizojitokeza katika chaguzi zao.

Viongozi wa Umoja huo wamesema  pamoja na kushiriki uchaguzi pia wamesimamisha  wagombea  12 ambao wamo katika ngazi zote ikiwemo rais, wawakilishi na madiwani.

Mwenyekiti wa umoja huo Ali Kaniki amewataka wazanzibari  kujitambua  na kufikra kwani wakiweza kujitambua wataweza kutoa maamuzi yaliyo sahihi.

“Wazanzibar tujitambue kifikra kwani tukiwa tunajitambua tutaweza kutoa maamuzi yalio sahihi, alisema  Kaniki”
Kwa Upande wake  mjumbe wa umoja huo Abdul Mhuya amesema  khatma ya wazanzibar imo mikononi mwa wazanzibar wenyewe  na Tanzania kwa ujumla hivyo wazanzibar wasikubali kuuipoteza thamani yaoya kushiriki kupiga kura kwa kupata viongozi wawatakao.

Vyama vitakavyoshiriki katika marudiao ya uchaguzi huo ni DP,CCK, AFP, DEMOKRASIA MAKINI , SAU, TLP, UPDP, UMD, ADC, NRA, TADEA NA CHAUMMA.

WACHINA WALIOKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA

$
0
0
 Raia wa Kichina kutoka kulia ni na Xu Fujie na  Huang Jing  ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela au kulipa faini ya shilingi bilioni 54 leo katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
 Raia wa kichina wakisindikizwa na Askari Magereza mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela leo katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Raia wa China wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 au kulipa zaidi ya sh.bilioni 54 kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya makosa mawili.

Washitakiwa hao katika kosa la kwanza ni kukutwa ni kuwa na nyara ya serikali ya vipande vya meno ya tembo 706 yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni tano na kosa la pili kushawishi kutoa rushwa kwa askari sh.milioni 30.

Washitakiwa hao ni Huang Jing pamoja na Xu Fujie wameanza kutumikia kifungo hicho leo baada ya kushindwa kutoa faini hiyo.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu         Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Sprian Mkeya amesema kuwa kutokana na kupata maelezo katika pande zote mbili pamoja na kuisababishia hasara serikali washitakiwa adhabu yao ni miaka 30 au kulipa  ya zaidi ya bilioni tano (5).

Hakimu Mkeya amesema washitakiwa hao wanaweza kukata rufaa makahakama kuu kutokana na hukumu iliyotoka.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliomba mahakama iwape adhabu kali kutokana na kosa waliolifanya na kudai kuwa kutokana na kukamatwa kwao vitendo vya uhalifu kwa wanyamapori vimepungua
Kwa upande wa Wakili upande wa washitakiwa Nehemia Mkoko aliomba mahakama kuwaonea huruma kwa adhabu wataoipata ili waweze kutoka na kuweza kujumuika na familia zao. Washitakiwa hao walikamatwa 2010 katika eneo la mikocheni mwaka huu.

IDARA YA UHAMIAJI YAFANYA MABADILIKO KWA WAFANYAKAZI 200 KATIKA VITUO VYA KAZI.

$
0
0
Kaimu Kamishina wa Fedha na Utawala, Abbas Irovya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
IDARA ya Uhamiaji imefanya mabadiliko ya wafanyakazi katika vituo vya kazi ikiwa ni kuongeza ufanisi wa kazi wa idara hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamishina wa Fedha na Utawala, Abbas Irovya amesema mabadiliko hayo ni kuongeza ufanisi kazi na tija.

Mabadiliko hayo ni DCI.Faustine Nyaki Mkoa wa Iringa anahamia Mkoa Mwanza, na aliyekuwa Mwanza,DCI.Remigius Ibrahim Pesambilia anahamia kwenda kwa Mfwadhi wa Ofisi ya uhamiaji uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere , DCI.Rose Mhagama (Njombe) amehamia Mtwara,DCI.Chale,s Habe (Geita) anahamia Njombe.

Amesema kuwa mabadiliko hayo kwa wafanyakazi katika idara hiyo ni 200 ambapo inatokana agizo la Waziri mwenye dhamana hiyo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA DUKA LA MSD WILAYANI CHATO

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD),  Laurean Bwanakunu (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya Waziri Mkuu hajafungua duka la dawa la MSD Wilayani Chato juzi.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim M. Majaliwa (wa tatu kushoto), akizungumza wakati akifungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), Wilayani Chato.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amefungua duka la Bohari ya Dawa (MSD), la Wilayani Chato duka litakalotoa huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa duka hilo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu alisema duka hilo ni mfano kwa Wilaya nyingine na mikoa,ambapo tayari Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa(Tamisemi) mikoa na Wilaya kuanzisha maduka hayo,na kisha MSD itatoa ushauri wa kitaalam.

Bwanakunu alisema kwa kuanza,duka la dawa la Halmashauri ya Chato linaendeshwa na MSD,lakini baada ya muda watalikabidhi kwa Halmashauri ya Chato. 

MWENYEKITI UWT MKOA WA DAR ES SALAAM AWANYOSHEA KIDOLE WALIOKISALITI CHAMA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Masaburi amesema wanachama wa chama hicho waliokiuchumu wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wasitegemee kupata uongozi wowote ndani ya chama hicho.

Masaburi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo mchana katika mkutano wa kuwashukuru kwa kukichagua chama hicho na kukipa ushindi ambapo kimeunda Serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.

"Kunawenzetu walitusaliti wakati wa uchaguzi mkuu na kuchangia mkoa wa Dar es Salaam kushindwa kufanya vizuri hali iliyosababisha kuwepo na changamoto hata ya kumpata Meya wenzetu hao tunawafahama na hawatapata nafasi ya kupata nafasi ya uongozi ndani ya chama chetu" alisema Massaburi.

Massaburi alisema ni heri kubakiwa na wanachama wachache waadilifu ndani ya chama kuliko kuwa wengi ambao ni wasaliti na katika jambo hilo ataendelea kulisimamia na kupigania maslahi ya chama ambacho anakitumikia.

Katika hatua nyingine Massaburi aliwataka wana umoja huo kushikamana na kushirikiana na kuhakikisha nguvu yao inaendelea kukipa ushindi chama hicho wa kushika dola kwani jambo hilo linawezekana kwa asilimia 100.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Massaburi, akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam leo mchana, katika mkutano wa kuwashukuru kwa kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth Massaburi (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Joel Kafuge, Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala, Apruna Humba na Katibu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Tatu Maliaga.
 Wanawake wa CCM Wilaya ya Ilala wakiwa kwenyev mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

Polisi kanda maalum ya Dar es salaam kwa kushirikiana na polisi mkoani Pwani wamefanikiwa kukamata watuhumiwa wa ujambazi 120 katika operesheni maalum iliyofanyika katika mapori yaliyoko mkoani Pwani. https://youtu.be/HfukSrwN9F0
 Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, kimelaani vikali agizo la mkurugenzi wa jiji kukitaka chama hicho kushiriki uchaguzi wa Meya wa jiji kikiwa na wajumbe tu bila ya kuwepo wafuasi wake. https://youtu.be/LWm-eyfAI2E
 Mamlaka ya mapato nchini TRA kwa kushirikiana na umoja wa mataifa kitengo cha kudhibiti uhalifu wasaini makubaliano ya kushirikiana katika udhibiti wa makontena yanayoingiza mizigo hatarishi nchini. https://youtu.be/v368pPGTYOo
Mtu mmoja afariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akiendesha baiskeli mkoani Tabora huku wananchi wakitishia kufunga barabara hiyo.https://youtu.be/MJ3_u1h3KfA
 Wakazi wa jiji la Dar es salaam wanaomiliki silaha kihalali wametakiwa kwenda vituo vya polisi kwa ajili ya uhakiki na ukaguzi wa silaha zao ndani ya siku 90 huku wale wanaomiliki silaha hizo bila kibali kuzisalimisha kabla ya operesheni maalum ya kusaka silaha hizo kuanza. https://youtu.be/wn3aAp6aoRk
 Waziri wa mambo ya nje kikanda na ushirikiano wa Afrika mashariki awataka maafisa na wanataaluma wa ustawi wa jamii Afrika Mshariki kupaza sauti zao kwa ajili makundi yenye mahitaji maalum. https://youtu.be/XOouWgz-CEo
Rais Magufuli akabidhi msaada wa gari la wagonjwa kwa hospitali ya wilaya ya Chalinze ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM kwa wananchi. https://youtu.be/6hzv15_FdpU
 Polisi wa Misenyi mkoani Kagera wanawashikilia watumishi 4 wa serikali kwa tuhuma za kuhusika na hujuma dhidi ya Ranchi ya Misenyi. https://youtu.be/77RQZPkZ-_I
 Spika wa bunge la Tanzania Job Ndugai aipongeza hospitali ya CCBRT kwa huduma inazotoa huku akibainisha kwamba serikali itaendelea kuunga mkono jitihada za sekta binafsi katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini. https://youtu.be/ueusTdbIiqM
 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Mkonda aahidi kutoa motisha ya shilingi milioni moja kwa askari yeyote atakaye pambana na ujambazi. https://youtu.be/vVkvd1bb46E
 Naibu waziri ofisi ya makamo wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina atoa miezi mitatu kwa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh kutengeneza mfumo wa kutibu majitaka kufuatia uharibifu mkubwa wa mazingira. https://youtu.be/QAQNlhK0QfM
 Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam imewahukumu raia wawili wa China kulipa faini ya shilingi bilioni 54 kila mmoja kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali za meno ya Tembo vipande 728 ambavyo ni sawa na tembo hai 226.https://youtu.be/H3JBHQ67rUI
 Ukiwa umebaki muda mfupi kabla ya uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar, tume ya uchaguzi visiwani humo ZEC yasema maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika.https://youtu.be/P1MhiiRal-c

TANGAZO kwa waliosoma Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibosho

$
0
0
 Kamati ya maandalizi ya waliosoma Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibosho inayo furaha kuwaalika wakina Mama na  Dada wote ambao wamesoma shule hiyo enzi za uhai wa Sister/Mother Consolatha Shayo, katika kikao cha  kuandaa re-union, kitakachowashirikisha wanafunzi wote waliosoma sekondari ya Wasichana Kibosho.  
Kikao hicho cha maandalizi kitafanyika siku ya  jumamosi ya tarehe 02.04.2016, kuanzia saa kumi kamili alasiri katika Hotel ya Mikocheni Resort Centre (MRC), iliyopo nyuma ya Shoppers Plaza ya Mikocheni.  Usikiapo taarifa hizi tafadhali mjulishe na mwingine.  Karibuni wote tushikiriane.

MUNGU IBARIKI SHULE YA KIBOSHO

KUJUA, KUPENDA, KUTENDA NDIO NGAO KUU, TUIDUMISHE


Mawasiliano:


Anna Mihambo:                    0784 291 094

Sauda Sinare:                                    0753 991 281

Magreth Adhero:                  0713 248 192

Hanifa Kachicky Mponji:    0713 473 762

Caroline John Hans:             0718 802 332


Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images