Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 17.03.2016


Balozi Seif Ali akutana na Viongozi wa Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania

$
0
0
Viongozi wa Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania umewaomba Wazanzibari kwenda kukamilisha haki yao ya kidemokrasia ya kupiga kura kwa kuwachagua Viongozi wanaowataka kuwaletea maendeleo kwenye uchaguzi Mkuu wa marejeo wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyia Jumapili ya Tarehe 20 mwezi huu.

Kauli hiyo imetolewa na Ujumbe wa Viongozi saba wanaotoka vyama vidogo vidogo vya Kisasa Nchini Tanzania vilivyokuwa havimo kwenye Umoja wa Ukawa ukiongozwa na Mheshimiwa John Shibuda wakati walipokutana kwa mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Bwana Shibuda alisema kinachohitajika wakati huu kwa Taifa ni kuona watanzania wanaendelea kuishi kwa amani na ushirikiano utakaotoa nafasi pana kwa Wananchi wake kujikita zaidi katika uzalishaji mali badala ya kuhubiri Siasa. Aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vikosi vyake vya ulinzi kwa kulinda amani ya Zanzibar.

Bwana Shibuda aliwataka Wanachama wa vyama vya siasa, Viongozi pamoja na Wananchi kukamilisha zoezi la kupiga kura kwa amani na usalama ili lengo la kurejewa uchaguzi huo likamilike na kuleta mafanikio makubwa.

Alitahadharisha kwamba si vyema wakati wa uchaguzi wakajitokea baadhi ya watu kutaka kuchezea matokeo ya kura jambo ambalo ni hatari na matokeo yake ni kwamba gharama za kuja kulinda vurugu ni ndogo.

Naye Mjumbe wa Umoja huo wa Rufaa za Wananchi Tanzania Bwana John Momos Cheo alisema upigaji kura ya marejeo Jumapili ijayo ndio njia pekee itakayotoa mwanga kwa Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar kuamua wapi wanataka kuelekea katika mustakabali wa maisha yao ya baadaye.

Akitoa shukrani zake kwa Ujumbe huo wa Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Tume huru ya Uchaguzi Zanzibar { ZEC } haikufanya makosa kufuta uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Tarehe 25 Oktoba mwaka 2015.

Balozi Seif alisema yapo mambo tisa yaliyoainishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Bwana Jecha Salum Jecha ambayo yalichangia kuvuruga zoezi zima la uchaguzi na kufikia hatua ya kufuta uchjaguzi pamoja na matokeo yake yote.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Ujumbe wa Viongozi hao wa Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania kwamba Serikali itaendelea kusimamia amani ili kuona zoezi hilo la uchaguzi linakamilika kwa utulivu.

Balozi Seif alisema jukumu hilo la Serikali limelenga kuona Maisha ya kila siku yanatoa nafasi kwa Wananchi waendelee kufanya shughuli zao za kimaisha kama kawaida.

Ujumbe huo wa Umoja wa Rufaa za Wananchi uliofanya ziara ya siku mbili Zanzibar umejumuisha Viongozi wa Kisiasa wa vyama visivyokuwa ndani ya Ukawa vya UPDP, SAU, UDP na ADATADEA.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania Ukiongozwa na Bwana John Shibuda.
Balozi Seif akifafanua jambo mbele ya Mwenyekiti wa Umoja wa Rufaa za Wananchi wa Tanzania Bwana John Shibuda aliyeuongoza ujumbe wa Umoja huo kufanya ziara ya siku mbili Zanzibar.
Mjuumbe wa Umoja wa Rufaa za Wananchi Tanzania kutoka Chama cha UDP Bwana John Momos Cheyo wa kwanza kutoka kulia akielezea malengo la Umoja huo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif. Picha na – OMPR – ZNZ.

ZIARA YA WAZIRI MKUU CHATO NA KATORO MKOANI GEITA.

$
0
0
 Waizri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mtambo wa kukamu mafuta ya alizeti  wanaushirika wa Chato akiwa katika ziara ya mkoa wa Geita Machi 17, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa  Ushirika huo Elias Kaswahili. 

 Wasani wa Katoro Geita wakicheza ngoma ya Kisukuma mara baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo  Machi 17, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara katika mji wa Katoro , Geita Machi 17, 2016. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

TEASER YA JOTO LA ASUBUHI IJUMAA MARCH 18

IYK-Columbus, Ohio | Karibuni Ibada ya Kiswahili Jumapili ya Mitende 20 Machi 2016 Kuanzia saa Kumi kamili hadi Kumi na mbili jioni

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete azuru hospitali ya moyo ya Wolfson nchini Israel

$
0
0
Katika kudumisha urafiki mwema  kati ya  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  (JKCI)  na Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko  jijini Tel Aviv, Israel, Kaimu Mkurugenzi wa JKCI  Profesa Mohamed Janabi amefanya ziara kutembelea hospitali hiyo na kuonana na madaktari bingwa wa moyo pamoja na watoto wa Kitanzania kadhaa waliopewa rufaa kwenda kupata matibabu hapo.

Profesa Janabi ameiambia Globu ya Jamii kwa njia ya simu kutoka Tel Aviv kuwa Serikali ya Israel kupitia mpango wake wa Save a Child's Heart  (Okoa moyo wa mtoto) ni moja ya washirika wakubwa wa JKCA katika kubadilishana utaalamu na vifaa.

 “Washirika wetu wengine ni Open Heart international ya Australia, Mending Kids Heart ya California, Madaktari Africa ya South Carolina, Almutada ya Saudi Arabia, Sharjah International ya UAE na Madras Medical mission and BLK  ya India.

“Hawa wote kwa muda mbalimbali huw wanakuja JKCI na mpaka sasa  katika mwaka huu wa 2016 wamekuja BLK, Madaktari Africa na lsrael” alisema, na kuongezea kuwa “Kwenye hospital ya moyo ya Wolfson tunayoshirikiana nayo JKCI. Nimeona watoto wetu 11 tuliowaleta huku wakiwa na complicated cases. Tisa wamekwisha fanyiwa upasuaji bado wawili na wote wanatokea Zanzibar.

Profesa Janabi ameongozana na manesi watatu na daktari mmoja.


  Kaimu Mkurugenzi wa JKCI  Profesa Mohamed Janabi baadhi ya wenyeji wake katika Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko  jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake
 Kaimu Mkurugenzi wa JKCI  Profesa Mohamed Janabi akiwa na madaktari bingwa wa moyo katika Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko  jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake
 Kaimu Mkurugenzi wa JKCI  Profesa Mohamed Janabi akiongea na Mkuu wa Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko  jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake
 Kaimu Mkurugenzi wa JKCI  Profesa Mohamed Janabi akiwa ametoka kusaidia upasuaji na madaktari bingwa wa moyo katika Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko  jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake
Kaimu Mkurugenzi wa JKCI  Profesa Mohamed Janabi akiwa na baadhi ya wagonjwa na walezi wao waliofanyiwa upasuaji  katika Hospitali ya Moyo ya Wolfson iliyoko  jijini Tel Aviv, Israel, wakati wa ziara yake. Bango aliloshika linaonesha majina ya wagonjwa kutoka Tanzania waliofanyiwa upasuaji

Solidstar - Wait [Official Video] ft. Davido

$
0
0

Here's another one from Achievas Entertainmentsigned artiste, Solidstar and he titles this one "Wait". He features HKN's CEO, Davido, and they both did justice to this video.
The video is about the readiness of a man to wait patiently for his woman until she is ready to take the plunge with him.
Directed by Avalon Okpe.

Tanzania na Uganda yafikia hatua nyingine kubwa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanga

$
0
0
Hatua nyingine kubwa imefikiwa leo hii katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda kupitia Kaskazini mwa Tanzania hadi bandari ya Tanga. 
Katika kikao kazi kilichofanyika jijini Arusha, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini-Uganda, Mhandisi Irene Muloni, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt. James Mataragio na Meneja Mkuu wa Total E&P Uganda, Ndugu Adewale Fayemi wametia saini mpango wa pamoja wa utekelezaji wa mradi huo (Project Implementation Plan). 
Hatua hii imekuja ikiwa ni wiki mbili tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kutoa tamko la pamoja la utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda kupitia mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma hadi bandari ya Tanga. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (wa kwanza kushoto), Waziri wa Nishati na Madini-Tanzania, Prof. Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kushoto), Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini-Uganda, Mhandisi Irene Muloni ( wa tatu kutoka kushoto), Meneja Mkuu wa Total E&P Uganda, Adewale Fayemi (wa nne kutoka kushoto) wakitia saini mpango wa pamoja wa utekelezaji wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga. Kulia kabisa ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Nishati na Madini-Uganda, Dkt. Kabagambe Kaliisa
 
 Waziri wa Nishati na Madini-Tanzania, Prof. Sospeter Muhongo na Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini-Uganda, Mhandisi Irene Muloni wakibadilishana nyaraka baada ya kutia saini kwa pamoja
Waziri wa Nishati na Madini-Tanzania, Prof. Sospeter Muhongo na Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini-Uganda, Mhandisi Irene Muloni wakionesha nyaraka zenye mpango kazi wa pamoja kati ya Tanzania, Uganda na Kampuni ya Total na TPDC juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga. 

KAMATI YA BUNGE YA MAENDELEO YA JAMII YATEMBELEA MFUKO WA BIMA YA AFYA (NHIF)

$
0
0
01
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni akisaini kitabu cha wageni mara baada ya wajumbe wa kamati hiyo kuwasili katika ofisi za Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa jijini Dar es salaam ambapo kamati hiyo imekutana na uongozi wa mfuko huo ili kusikiliza mipango yao ya baadae na changamoto mbalimbali zinazoikabili taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na mafanikio na kuangalia mambo kadhaa yanayokwamisha shughuli za mfuko huo ili hatua za kurekebisha zichukuliwe na kwa ajili ya kufanya mfuko huo kusaidia jamii katika suala zima la afya , Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando.
2
Mbunge wa Busega na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya jamii Mh. Raphael Chegeni pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakiendelea na utaratibu wa kusaini kitabu cha wageni.
3
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wakielekea mwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kupewa taarifa na Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo Bw. Michael Muhando wa kwanza kulia.

SERIKALI KUENDELEA KUWAWEZESHA WANAWAKE - UMMY MWALIMU

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, New  York

 Wajumbe wa  Mkutano wa 60 wa Kamisheni  kuhusu hali ya wanawake,  wanaendelea na majadilino juu ya   dhima ya  uwezeshwaji wa wanawake na uhusiano wake katika  utekelezaji wa Malengo  ya Maendeleo Endelevu ( Agenda 2030).

Akichangia   majadiliano hayo,Waziri wa Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ( Mb) anasema  Tanzania  inatambua kwamba uwezeshwaji wa mwanamke na mtoto wa kike ni muhimu sana katika kufanikisha utekelezaji wa   Agenda 2030.

Na kwamba ili  kufanikisha  hilo, Serikali  inaendelea na  jukumu la  kuhusisha na kuingiza   Ajenda 2030  katika  mifumo   iliyopo ya  kisera, mipango na mikakati ya kitaifa ya maendeleo.



Waziri Ummy Mwalimu anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu, amebainisha  pia kwamba  Serikali inapitia kwa makini  lengo namba tano la agenda 2030 ambalo linazungumzia umuhimu wa kufanikisha  usawa wa kijinsi na  uwezeshaji wa wanawake wote na wasichana.



Akaeleza zaidi kwamba uamuzi wa serikali kufanya marejeo ya mikakati  Na mipango ya kitaifa  inalenga kuhakikisha kwamba  usawa wa  jinsia  na uwezeshwaji wa wanawake unaendelea kuwa kipaumbele cha nchi.

Vilevile  amesema,  ushiriki  jumuishi umefanyika katika  kubuni viashiria ambavyo vinaendana na mahitaji ya nchi na vinaweza kutumika  mpaka ngani za chini katika  upimaji wa utekelezaji wa Agenda 2030.



Katika kuelezea  zaidi uzoefu wa Tanzania katika uwezeshwaji wa  mwanamke na msichana wa  kitanzania. 

Waziri pia alianisha sheria mbalimbali zinazolimda mwanamke na mtoto wa kike dhidi ya  ukatili au ubaguzi wa aina yoyote ile ,  kuanzishwa kwa mifuko na Banki za kuwawezesha wanawake kujipatia mikopo kwa riba nafuu, uboreshwaji wa huduma za afya hususani  afya ya mama na mtoto pamoja na  fursa sawa za ajira zenye staha na fursa za kujiajiri.



Pamoja na kueleza  namna  Serikali inavyoendelea kujipanga katika utekelezaji wa  Agenda 2030,  Waziri Mwalimu amesema ili  utekelezaji huo uwe na  mafanikio  tarajiwa,  ushirikiano na wadau  mbalimbali wa maendeleo pamoja sekta binafsi  utahitajika sana. 
Na akatumia  nafasi hiyo kuwashukuru wadau hao ambao wamekuwa wakishirikiana na  Serikali   katika maeneo mbalimbali


Baadhi ya  changamoto ambazo amesema Tanzania inakumbana nazo katika   jukumu hilo la uwezeshwaji wa wanawake na wasichana pamoja na vikwazo vya kimila na kitamadani anavyokumbana navyo mwanamke na  mtazamo hasi dhidi ya wanawake. 

Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.)wakati akitoa taarifa ya nchi katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake Duniani (CSW).
Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb.) akiwa Ubalozini New York na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Peter Serukamba (kushoto na Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Mhe. Tuvako Manongi baada ya kuwasilisha taarifa ya nchi katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake Duniani (CSW).
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu ( Mb) akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu dhima ya  uwezeshwaji wa wanawake na uhusiano wake na utekelezaji wa Agenda 2030. katika mchango wake  Waziri anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano  huu wa Kamisheni  ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake amesema Serikali inatambua umuhimu wa mwanamke katika utekelezaji wa ajenda mpya ya maendeleo endelevu ( Agenda 2030) na kwamba itaendelea kumwezesha

DIRA YA DUNIA ALHAMISI 17.03.2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0

Simu.tv:  Watu 2 wapoteza maisha na wengine 12 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Ndenjela kugonga gari dogo aina Hiace mkoani Mbeya.https://youtu.be/LmppVsMtlq4
 Simu.tv:  Mamia ya wananchi katika mkoa wa Kilimnjaro wanatarajia kunufaika na miradi mipya ya maji inayotekelezwa katika vijiji mbalimbali vilivyoko katika wilaya ya Siha. https://youtu.be/MNAhIdInOc4
 Simu.tv:  Waziri mkuu awataka wahamiaji haramu walioingia nchini bila kuwa na vibali maalum kuondoka nchini mara moja kwa hiari yao wenyewe kabla ya msako wa kuwasaka kwa nguvu haujaanza. https://youtu.be/x1hh2vso5i4
 Simu.tv:  Serikali kupitia wizara ya Afya yaagiza wamiliki wa maduka ya dawa yasiyo na vibali kufunga maduka hayo mara moja. https://youtu.be/eBmM-5O1I0I
 Simu.tv:  Taharuki yawakumba wakazi wa Manispaa ya Musoma kufuatia watu wanaodhaniwa kuwa majambazi kuwaua watu wawili kinyama na kisha kufanya uporaji. https://youtu.be/RmZDi1eGmK4
 Simu.tv:  TAKUKURU mkoani Mara inamshikilia mhasibu wa mfuko wa bima ya Afya mkoani humo kwa tuhuma za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.https://youtu.be/tBrmYA2WwcM
 Simu.tv:  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awataka watanzania kutunza na kulinda rasilimali za nchi ili vizazi vijavyo viweze kunufaika na rasilimali hizo.https://youtu.be/ZB4xy_F7c-Q
 Simu.tv:  Maduka 432 ya dawa muhimu yamefungwa baada ya kubainika kuwa hayakidhi matakwa ya kutoa huduma hiyo kisheria pamoja na kukutwa na dawa za serikali kinyume cha sheria. https://youtu.be/Q2YD-F6A02s
 Simu.tv:  Katibu wa wizara ya mali asili na utalii Meja Generali Gaudence Milanzi asema serikali inaangalia namna ya kufanya ukaguzi wa meno ya tembo yaliko nchini ili kubaini idadi iliyopo hivi sasa. https://youtu.be/ePH0nsWm_D8
 Simu.tv:  Katibu wa Bunge Dr. Thomas Kashilila azungumzia ukarabati unaoendelea katika ukumbi wa bunge mkoani Dodoma na kusema unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika kabala ya vikao vya bunge mwezi ujao. https://youtu.be/9Vh7va-JopU
 Simu.tv:  Waziri wa nchi ofisi ya Rais utumishi na utawala bora Angella Kairuki asisitiza kuwa watu wanaotumia fedha za mfuko wamaendeleo ya jamii TASAF kinyume na malengo yaliyowekwa watachukuliwa hatua za kisheria.https://youtu.be/zCSZoZL_xMA

3 Days To Go #LadyJayDeeOfficialCountDown

MGOMBEA URAIS ZANZIBAR KUPITIA CHAMA CHA ADC Mhe. Hamad Rashid Mohamed akutana na wapiga kura wake PEMBA

$
0
0
 Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha ADC Mhe.  Hamad Rashid Mohamed akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa chama hicho katia ya 13, kwenye kutano uliofanyika Chuo cha Amali Vitongoji Chakechake Pemba
 Mlezi wa chama cha ADC Pemba, Shoka Khamis, akizungumza kwenye mkutano wa wanachama, wagombea na mawakala wa chama hicho, uliofanyika Chuo cha Amali Vitongoji Chakechake Pemba, na kuhutubiwa na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho Mhe. Hamad Rashid Mohamed
 Wanachama wa chama cha ADC, pamoja na wagombea na mawakala wao, wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha Amali Vitongoji Chakechake Pemba, mkutano huo ulihutubiwa na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho, Mhe. Hamad Rashid Mohamed
 Kaimu Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama cha ADC Tanzania Omar Constantine Wilbert, akizungumza kwenye mkutano wa wanachama, wagombea na mawakala wa chama hicho, uliofanyika Chuo cha Amali Vitongoji Chakechake Pemba
 Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya ADC Hamad Rashid Mohamed, akizungumza na wanachama, wagombea na mawakala wa chama hicho, kwenye kutano wa hadhara, uliofanyika chuo cha Amali Vitongoji Chakechake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

wito kwa wafanyabiashara tamasha la dini la upendo music festival

$
0
0

Kampuni ya Legendary Music Entertainment and Promotions Company Limited inatoa wito kwa wafanyabiashara wote kujitokeza kufanya Biashara katika Tamasha la Dini La Upendo Music Festival.
Tamasha la Upendo Music Litakalofanyika siku ya PASAKA, Tarehe 27/03/2016. Katika viwanja vya LEADERS Kinondoni, Kuanzia Saa 4:00 Asubuhi Hadi Saa 10:00Usiku, Litakalojumuisha Waimbaji binafsi na Kwaya mbali mbali, pia Litajumuisha Bonanza la Michezo, Michezo ya Watoto na Uuzaji wa Biashara mbali mbali.
Hivyo basi kwa wafanyabiashara Wakubwa na Wadogo wenye lengo la kujitokeza kufanya Biashara kama UUZAJI WA CHAKULA NA VINYWAJI na Biashara nyinginezo, kwa bei nafuu sana Mnakaribishwa.
...

MAKALLA ATAKA SUALA LA UGONJWA WA KIPINDUPINDU LIWE HISTORIA MKOANI MBEYA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mstaafu Abbasi Kandoro (kulia) akimkabidhi rasmi ofisi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Machi 17 mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na watumishi  waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Abaas Kandoro Machi 17 mwaka huu .

Baadhi ya watumishi wa ofisi ya mkoa wa mbeya wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa huo Amos Makalla wakati akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya ofisi na Mkuu wa Mkoa mstaafu Abasi Kandoro Machi 17 mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa Mstaafu Abbas Kandoro akizungumza na watumishi na baadhi ya viongozi (hawapo pichani)waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ofsini na Mkuu wa Mkoa mpya Amosi Makalla Machi 17 mwaka huu.

Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya  wakiwa makini kumsikiliza Mkuu wa Mkoa mstaafu Abbas Kandoro wakati awaaga rasmi mara baada ya kustaafu rasmi nafasi hiyo.
Na Emanuel Madafa, Mbeya.
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala,  amewaagiza watendaji wote wenye dhamana ya kulinda afya na usalama wa wananchi kuhakikisha kuwa ugonjwa wa kipindipindu unakuwa historia mkoani Mbeya kwa kusimamia usafi katika ngazi zote za kijamii.
Mbali na agizo hilo , pia Makala amewaagiza Wakuu wote wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani humo kuandaa madawati ya malalamiko katika kila siku za Alhamisi  kuanzia ili kusikiliza malalamiko ya wananchi kuhusu kero mbalimbali zinazojitokeza kwenye maeneo yao.
Mkuu huyo mpya wa Mkoa wa Mbeya  ametoa maagizo hayo katika hafla fupi ya kukabidhiwa ofisi ya mkoa wa Mbeya na mtangulizi wake, Abbas kandoro, ambaye amestaafu utumishi wa umma baada ya kufanya kazi kwa miaka 40 kuanzia mwaka 1976.
Amesema suala la ugonjwa kipindupindu hatopenda kulisikia katika uongozi wake hivyo amezitaka mamlaka husika kuwajibika ipasavyo ili kudhibiti kabisa ugonjwa huo hatari.
Wakati huo Makala amepiga marufuku matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watumishi wa umma mkoani humo, wakati wa saa za kazi ili kutoa fursa kwa watumishi hao kutimiza vyema majukumu yao kazini.
Ameonya kuwa  hatamvumilia mtumishi yeyote atakayebainika kupoteza muda mwingi kwenye mitandao hiyo huku akishindwa kutimiza majukumu yake katika kuwatumikia wananchi.
 Hata hivyo, Makala alitahadharisha kuwa haitaji majungu ya aina yoyote kutoka kwa watumishi wa sekta wala wanannchi mbalimbali mkoani hapa ili kuhakikisha kuwa kila mtu anatimiza majukumu yake na si kukwamishana katika  utendaji wa kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Mstaafu Abaas Kandoro amewashukuru watumishi na viongozi mbalimbali kwa ushirikiano waliompa wakati wa utumishi wake na kuahidi kutoa ushirikiano kwa mkuu wa mkoa huo Amosi Makala  .




JUST IN: KIWANDA CHA RHINO CEMENT CHA TANGA CHAFUNGIWA KWA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (MB) amekifungia kiwanda cha kuzalisha cement na chokaa kilichopo jijini Tanga cha Rhino Cement, leo jioni kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni uharibifu na uchafuzi wa mazingira na kuvunja sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.

Mh. Mpina amechukua uamuzi huo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata ya maweni kupitia diwani wa kata hiyo Bw. Joseph Colvas na kujionea mwenyewe namna ambavyo kiwanda hicho kinavyo achilia moshi mzito kwenda angani, pamoja na vumbi lisilovumilika kusambaa katika maeneo ya makazi ya wanachi wa kata hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaa katika maeneo ya shule ya sekondari ya Don Bosco ambapo, Mh. Mpina ameelezwa kuwa athari zitokanazo na uachiachi wa hewa hiyo chafu angani si tu kwa watoto wa shule zinazozunguka kata hiyo bali pia ni kwa viumbe hai na mazingira.


“Hawa jamaa wamekuwa wakiachilia vumbi jingi na moshi mzito kutoka katika kiwanda hiki mara kwa mara, hivi tangu jana wamezima mitambo yao wakijua kabisa kuwa kuna ugeni wa Naibu Waziri kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Alisisitiza Bw. Joseph.”

Kwa upande wake Afisa Afya wa jiji la tanga aliyejulikana kwa jina moja la bwana Kizito alimuelezea Naibu Waziri Mpina kuwa ni kweli kiwanda hicho kimekuwa kikifanya uchafuzi huo wa mazingira, na Afisa uendeshaji kutoka Baraza la Taifa na HIfadhi ya Mazingira NEMC Bw. Novatus Mushi ameeleza kuwa kiwanda hicho kimeshawahi kutozwa faini ya shilingi milioni kumi na saba (17) kwa kosa la kuchelewa kulipa ada ya mwaka ya mazingira pamoja na uharibifu wa mazingira uliokuwa ukifanywa na kiwanda hicho kwa upande wa kuzalisha chokaa.

Mh. Mpina ameelekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) kukifunga kiwanda hicho kisiendelee na uzalishaji kwa muda usiopungua miezi mitatu, na kulitaka baraza hilo lijiridhishe na kufuatilia namna kiwanda hicho kinavyotakiwa kutekeleza sheria ya mazingira kwa kujenga mfumo wa kisasa wa kutoa taka zitokanazo na uzalishaji kiwandani hapo pamoja, na kupima vumbi na moshi utokao kiwandani hapo kama hautakuwa na madhara na athari kwa mazingira na viumbe hai. Kinyume na hapo kiwanda hicho kitafungiwa moja kwa moja.

Aidha, akitolea mfano wa kiwanda cha bonite bottles cha mjini moshi kwa kuwa kinara katika upandaji miti na utunzaji wa mazingira, mh Mpina alivitaka viwanda vingine viige mfano wa kiwanda hicho cha coke cola.

Ziara ya Mh. Mpina Jijini Tanga ilihusisha pia kuangalia namna ukuta wa fukwe ya Pangani uliojengwa enzi za mkoloni, ulivyo athirika na madhara yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kusema kuwa, ukuta huo huko kwenye mchakato wa kujengwa na kuboreshwa upya, ifikapo mwezi wa  nne mwaka huu mradi wa ujenzi wa ukuta huo utaanza kutekelezeka kwa kuwa tenda imeshatangazwa na jumla ya kiasi cha fedha za kimarekani dola milioni 1,400 zimepatikana kupitia mfuko wa nchi maskini zaidi duniani (LDCf).

Mh. Mpina aliwaasa wakazi wa mji wa Tanga na viunga vyake kutunza mazingira kwa kupanda miti na kufanya usafi kama ilivyoagizwa na serikali, ili kuhepukana na nchi kuwa janga na magonjwa yatokanayo na uchafu.


Waziri Mpina Pia alitembelea kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh na kiwanda cha Tanga Cement na kuridhirishwa na namna ambayo wanatekeleza sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.


NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: Regina

TAARIFA YA MSIBA YA MAREHEMU MZEE MATHEW CHANDO

NAIBU WAZIRI MPINA AFANYA ZIARA JIJINI TANGA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mh Luhaga Mpina akitolea ufafanuzi namna ambayo fukwe ya Pangani imeathirika na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
 kushoto meneja mkuu wa kiwanda cha maziwa cha tanga fresh Bw. Michael Kalata, akimuonyesha mh Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, moja nya bidhaa ya maziwa inayozaliswa katika kiwanda hicho. mh Mpina alitembelea baadhi ya viwanda jijini tanga kujionea namna ambavyo vinatekeleza sheria ya mazingira ya 2004 na kanuni zake. 
 Pichani Namna ambavyo fukwe ya Pangani Jijini Tanga ilivyoliwa na maji ya bahari, kutokana na kuongezeka kwa kina cha bahari ikiwa ni athari zitokanano na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi. na baaadhi ya visiwa nchini viko hatarini kumezwa na bahari.

Mh Luhaga Mpina Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira aliyea nguo nyeusi akipata maelezo toka kwa mtaalam katika kiwanda cha Twiga cement alipokitembelea leo jijini tanga kuona namna ambavyo kiwanda hicho kinatekeleza sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake. (Picha zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais)
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images