Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1165 | 1166 | (Page 1167) | 1168 | 1169 | .... | 3278 | newer

  0 0  0 0


  0 0
  0 0


  0 0

  Padri Honest Munishi akiongoza misa ya kumbukumbu ya marehemu James Luhanga Jr iliyofanyika siku ya Jumamosi March 19, 2016 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani. Marehemu James Luhanga Jr alifariki Februari 3, 2016 mkoani Iringa. Picha na Vijimambo Blog/ kwanza Production.
  Ndugu wa marehemu wakipeleka matoleo ya sadaka ya misa ya kumbukumbu ya mpendwa wao James Luhanga Jr.
  Wanafamilia wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya mpendwa wao marehemu James Luhanga Jr. iliyofanyika siku ya Jumamosi March 19, 2016 Baltimore, Maryland nchini Marekani.
  Wanafamilia wakifuatilia misa ya kumbukumbu ya mpendwa wao marehemu James Luhanga Jr. iliyofanyika siku ya Jumamosi March 19, 2016 Baltimore, Maryland nchini Marekani.
   
  Pamela (kushoto) na Eliza Madada wa marehemu James Luhanga Jr. wakiwa katika picha ya pamoja kama kumbukumbu ya misa ya kumkumbuka mdogo wao aliyefariki Februari 3, 2016 mkoni Iringa. 
  Wakati wa kupata chakula.
  Katika picha toka kushoto ni Pamela Luhanga, James Luhanga Sr na Eliza Luhanga.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  Dk. Mehul A. Shah, Mtaalamu wa magonjwa ya figo kwa watoto kutoka Hospitali za Apollo; Hyderabad


  Siku ya Figo duniani, ni tukio la kimaarifa na la kuleta mwangaza duniani linaloadhimishwa mwezi Machi. Kila mwaka, kumekuwepo na shughuli mbalimbali kitaifa na kimataifa zinazofanywa na mashirika mbalimbali ya Figo, mahospitali, wataalamu wa afya na watu binafsi wanaotaka kuleta mabadiliko duniani dhidi ya ugonjwa wa figo. 

  Ni muhimu kuhimiza elimu, vipimo vya awali, na mtindo mzuri wa maisha ili kuruhusu Jamii itambue magonjwa ya Figo yanayoathiri watu milioni duniani ikiwemo watoto ambao wapo katika hatari ya kuugua katika umri mdogo. Kampeni ya mwaka 2016 ina lengo mahususi kwa magonjwa ya Figo na watoto.

  Matatizo ya figo kwa watoto yajulikanayo kitaalamu kama (Paediatric Nephology aliments) yanahusiana na magonjwa ya Figo kwa watoto wachanga na watoto wadogo mpaka miaka kumi na nane. Kwa mujibu wa Dk. Mehul A. Shah, Mtaalamu wa magonjwa ya figo kwa watoto kutoka Hospitali za Apollo; Hyderabad Magonjwa ya Figo kwa watoto yanaweza tokea Sababu ya mapungufu katika ukuaji au maumbile (yanayotokea wakati wa kujifungua), kurithi (katika familia) au mabadiliko katika mazingira/ kinga mwilini au madawa. Matatizo Kama hayo yakitambulika mapema huweza zuia uharibifu wa Figo.

  Dk. Shah anawahimiza watanzania kufwata mbinu za kuzuia matatizo ya Figo kwa watoto ambazo zitasaidia kujenga Tanzania isio na magonjwa ya Figo. Mbinu izi ni kama Kupima mkojo kwa watoto wadogo chini ya umri wa miaka miwili wenye homa kali, kuhimiza watoto wasiozidi miaka mitatu kukojo kwa wakati (wasibane mkojo), ulaji wa matunda na mbogamboga, chumvi ya kiasi na nyama katika milo ya familia.

  Kupunguza muda unaotumika na watoto katika televesheni na kompyuta na kuongeza shughuli nyingi Zaidi zenye kupunguza ongezeko la uzito, kuepuka dawa za kupunguza maumivu kama Nimesulide, Ibuprofen n.k. pamoja na madawa ya Ayurvedic/Unani, matumizi ya Crocin/ Calpol/ Paracetamol, kupima presha angalau mara moja kwa mwaka kwa watoto wenye Zaidi ya miaka mitatu, kufanya uchunguzi wa  ugonjwa wa Figo kwa mtoto mwenye matatizo katika ukuaji, anemia, shinikizo la damu, damu katika mkojo, kuvimba kwa mwili au maambukizi ya mkojo ya mara kwa mara. Mbinu hizi pia zimetajwa na Dk. Shah kama njia za kuepuka magonjwa ya Figo kwa Watoto.

  Matatizo ya Figo yanaweza tokea kwa watoto kutokana na matatizo katika maumbile au yanayotokea baada ya kuzaliwa. Wataalamu wa magonjwa ya figo kwa watoto kutoka  Hospitali za Apollo wanahimiza upimaji wa mara kwa mara ili kufahamu kama mtoto wako ana matatizo ya figo.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein akipiga kura katika uchaguzi wa marudio  kituo namba 1cha kupiga kura namba 1 Skuli ya   msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo,Wananchi wa Zanzibar leo wanapiga kura katika uchanguzi wa marudio baada ya kufutwa kwa uchanguzi uliofanyika October 25,2025 kutokana na kasoro zilizojitokeza.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitimiza haki  yake ya kupiga kura katika kituo Namba 11 Shule ya Sekondari Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Unguja kwa ajili ya Uchaguzi wa marudio unaofanyika leo March 20,2016 Visiwani Zanzibar. 
   Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akiwa katika maandalizi ya kupiga kura katika uchaguzi wa marudio kituo cha Skuli ya Kitope, Wilaya ya Kaskazini B , Mkoa wa Kaskazini. 
    Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akipiga kura katika uchaguzi wa marudio katika kituo cha Skuli ya Kitope, Wilaya ya Kaskazini B , Mkoa wa Kaskazini. 
    Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari mara baada ya kupiga kura katika uchaguzi wa marudio kwenye kituo cha Skuli ya Kitope, Wilaya ya Kaskazini B , Mkoa wa Kaskazini. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.January Makamba akizungumza na Waandishi wa habari akielezea hali halisi ya mwenendo wa upigaji kura katika uchaguzi wa marudio  kituo namba 1cha kupiga kura namba 1 Skuli ya   msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo.
   Mkazi wa chake chake akizungumza.na  wanahabari ( hawapo pichani) mara baada ya kutoka kupiga kura
  Baadhi ya Wakazi wa Madungu wakiangalia majina yao kwenye kituo cha kupigia kura
  kituo cha kupigia kura cha skuli ya Madungu chake chake Pemba.
  Baadhi ya wananchi wakihakiki majina yao kabla ya kuingia kupiga kura katika kituo cha skuli ya Raha Leo.

  0 0


  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York

  Miaka 15  tangu kupitishwa kwa Azimio la Durban na Mpango wa Utekelezaji kuhusu ubaguzi wa rangi na vitendo vingine vya aina hiyo. Kadhia   ubaguzi wa rangi na asili ya mtu anakotoa bado inaendelea na kuongezeka

  Mwishoni mwa Wiki hapa  Umoja wa Mataifa palifanyika maadhimiyo ya  siku ya Kimataifa ya  kutokomeza  vitendo vya   kibaguzi: Changamoto na  Mafanikio  la Azimio la Durban.

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  alikuwa mmoja wa  viongozi waliozungumza wakati wa adhimisho hilo,  ambapo Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika  katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika

  Kwa ujumla viongozi wote waliozungumza walieleza kwamba pamekuwapo  na mafaniko na changamato za  utekelezaji wa Azimio la Durban na  Mpango wa Utekelezaji miaka  kumi na tano tangu kupitishwa kwake.

  Baadhi ya mafanikio hayo kama ilivyoelezwa na Katibu Mkuu  Ban Ki Moon, ni pamoja na Nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Mataifa  ama wametunga au kuboresha sharia zinazopinga vitendo vya  ubaguzi, ukiwamo ubaguzi wa radi,  Imani ya dini au asili ya mtu anakotoka.

  Mafanikio mengine ameyataja  kuwa ni yale  ya Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana  kutangaza Muongo wa Kimataifa wa Watu wenye asili ya Afrika ambao utaendelea hadi mwaka 2014 ikiwa ni sehemu ya kuenzi asili ya mtu mweusi, mila, tamaduni zake, ustawi na maendeleo yake.


  Hata  hivyo  pamoja na  juhudi zote hizo na safari ndefu ambayo  jumuiya ya kimataifa imepitia tangu kupitishwa wa Azimio na Durban .Ban Ki Moon  anasema  vitendo vya ubaguzi ukiwao ubaguzi wa rangi, dini au  asili ya mtu vinazidi kuongezea jambo  ambalo anasema linampa wasi wasi.

  “ Naingiwa na wasiwasi sana  namna wimbi la ubaguzi wa rangi,  Imani ya  mtu, au asili ya mtu linavyoongezeka.  Kumekuwapo na ongezeko la maoni ya kibaguzi,  vurugu na chuki duniano kote na vujo na vurungi dhidi ya kundi. Hii  inaashiria kwamba bado  hatujafanya vya kutosha na tuna safari ndefu.

  Akabainisha  pia kwamba  mihemuko ya kisiasa na siasa za mrengo wa kulia navyo vinachangia kuondoa dhana ya  kuvumiliana,  lakini pia matatizo ya  kiuchumi na ugumu wa maisha , wimbi la wakimbizi na changanoto wanazokumbana nao na kauli  za kichochezi dhidi ya dini nyingine ni viashiria vingine vya dalili  ya kuipeleka pabaya dunia.

  Kwa upande wake  Balozi Tuvako Manongi  pamoja na  kuungana na  wazungumzaji wengine katika maadhimisho hayo kwamba Jumuiya ya Kimataifa   imepiga hatua  katika kujaribu kutokomeza ubaguzi  na ubaguzi wa rangi bado watu wenye asili ya afrika wanaendelea kukabiliana na  changamoto hiyo.

  “Afrika inatambua  ukoloni, ubaguzi wa rangi na dhuluma  za  kisiasa umesababisha ubaguzi wa kila aina  na  tabia ya kutovumiliana.   Hadi leo hii Waafrika  na Watu wenye asili ya Afrika na  Watu wenye Asili  bado wanaendelea kuwa waathirika dhuluma hii ya ubaguzi  unao unakwenda sawia na  ukosefu wa fursa za kiuchumi.u. Akasema Balozi Manongi.

  Pamoja na  changamaoto hizo  kuendelea kuwapo  miongoni mwa watu wa asili ya Afrika,   amesema  Kundi la nchi  za African  linashukuru kwa  kupitishwa na  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2015   Muongo wa Watu wenye asili ya Afrika:  kwa lengo   la kutambua haki, maendeleo , kukuza heshima, ulinzi na haki zote za binadamu na misingi ya  uhuru wa  watu  asili ya Afrika.

  Akaongeza  Umoja wa Afrika unatambua  na kuheshimu  haki na uhuru wa kujieleza wa vyombo vya habari na mifumo mengine ya teknolojia ya mawasiliano yakiwamo mawasiliano  ya  internent   na namna  inavyoweza  kusaidia juhudi za kukabiliana na vitendo vya ubaguzi wa rangi na vitendo vingine vya aina hiyo.

  Hata hivyo  akasema Afrika  inahofu  juu ya matumizi mabaya ya teknolojia mpya za mawasiliano, kama jukwaa la  kuhubiri na kusambaza  tabia ya  kutokuvumiliana na  vilevile kutumika  kueneza namna mbalimbali za utumwa na  biashara  haramu ya usafirishaji  binadamu.

  Balozi Manongi, akaongeza kuwa Afrika  inatoa wito kwa wamiliki  na waendeshaji wa teknolojia ya mawasiliano kuweka sheria zitakazowabana watumiaji wanaokwenda kinyume na malengo mazuri ya matumizi  ya  teknolojia  ya mawasiliano.

   Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi, akizungumza  kwa  niaba ya  Nchi za kundi la Afrika katika Umoja wa Mataifa wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa kuhusu  ubaguzi wa rangi  miaka kumi  na tano tangu kupitishwa  kwa Azimio la Durban na Mapango wa Utekelezaji. Azimio hilo lilitokana na   Mauaji yaliyotokea  huko Sharpeville, Afrika ya Kusini mwaka 1960.
  Mwakilishi wa Kudumu wa Antigua and  Barbuda, Balozi Walton Alfonso Webson ambaye ni  mlemavu wa  kutoona,. akizungumza kwa niaba ya Kundi  la Nchi za Latini ya Amerika na Visiwa vya Caribbian wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kutokomeza aina zote za kibaguzi ukiwamo ubaguzi wa rangi, dini au asili anayotoka mtu. Maadhimisho hayo yamefanyika mwisho mwa wiki. 
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiwa na Rais wa Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa,  Bw. Mogens Lykketoft wakati wa  maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi

  0 0

  Mhe. JPM awali ya yote napenda kukupongeza kwa kwa kazi nzuri ya kusafisha uchafu ndani ya nchi almaarufu  kutumbua majipu. Kero za wananchi zipo katika ngazi mbalimbali na wewe mwenyewe ulizianisha kwa kina katika kampeni zako wakati ukitafuta nafasi ya kuliogoza taifa hili. Wakati wewe umekuwa muwazi katika  kuondoa kero kwa wananchi, nichelee kusema watendaji wengi  wa serikali za mitaa (sio wote) maisha yao  yamekuwa yakineemeka kwa kuongeza  kero kwa wananchi, hasa wa kipato cha chini. 
  Wamekuwa wakiongeza kero kwa wananchi wanyonge ili waendelee kuwanyonya kwa kwa njia moja au nyingine. Hili kwa kiwango kikubwa liko kwenye  Serikali za  mitaa  na mabaraza ya ushauri ya kata, mengi yao ni kero kubwa sana na yanalalamikiwa na wananchi wazi wazi au chini chini kwa kuogopa manyanyaso kutoka kwa wakubwa hao. 
  Ingawa nafasi nyingi za uongozi katika  ngazi hizo ni za kujitolea  watu wamefanya kazi hizo ni  za kudumu(full time) kwa ajili ya  kujineemesha. Watu wanyonge wasio na kitu wengi wao hawapati haki kabisa au zinacheleweshwa. Kwani hili shauri lako lisikilizwe na wajumbe waje kwenye eneo la tukio kwa ajili ya ushauri lazima ulipe posho za wajumbe? Wajumbe wa mabaraza ya kata na mitaa wamekuwa Miungu watu.
  Baadhi ya wajumbe wa mabaraza ya mitaa na kata wamekuwa watendaji wa kudumu  na wanashinda katika ofisi hizo  siku nzima wakifanya ndio eneo lao la ajira la kupatia kipato, na  kutumia mbinu mbali mbali ambazo zinaongeza  kero kwa wananchi wanyonge(hilo liko zaidi kwenye  mitaa na vitongoji vya mijini). Nashukukuru  Waziri Simbachawene alilwahi kuzungumzia  hili katika ziara yake  mkoani Morogoro.
  Ngoja nitoe mifano michache; Hivi karibuni nimeshuhudia watu wawili wameziba kwa ukuta njia ya kwenda kwenye makaburi ya waislamu katika mtaa wa Boko Dovya, eneo la Somji Dar es salaam, serikali ya mtaa inafahamu, serikali ya kata inafahamu, lakini kwa kuzibwa midomo kwa njia ambazo hazieleweki, wanyonge wamenyimwa haki yao ya kutumia njia ya kwenda makaburini kwa miaka zaidi ya mitatu hivi. Mpaka sasa walioziba njia hiyo ambao kati yao ni wafanyakazi  wa serikali  ya JPM  bado wameendelea kuwa na kiburi na kupingana kwa vitendo na  nia ya dhati ya serikali ya JPM ya kuwaondolea wananchi wanyonge kero.
  Siku moja nilitembelea ofisi ya  mtaa mmoja nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Nilishtushwa na maneno ya baadhi ya wajumbe  katika ofisi ile.  Kulikuwa na mwananchi mmoja alikuwa anakuja kwa mbali kuja kupata huduma katika ofisi  hiyo, wajumbe wakamuona, na wakaanza kuambiana angalia yule jamaa anakuja, hana hela achana naye. Nilishtuka sana, na kujiuliza hawa ndio wawakilishi wa wananchi au wachuuzi katika ofisi ya serikali? Lakini Nikaa kimya, baada ya muda nikaanzisha mazungumzo kuhusu serikali ya JPM na utumbuaji majipu, mjumbe mmoja mwanamama akanishangaza tena kwa maneno yake, akasema majipu wanatumbua huko juu  huku chini  hawawezi kutufikia tutaendelea kula tu.
  Baada ya  kusikia maneno hayo nikaishiwa nguvu na kujiambia mwenyewe kuwa serikali ya JPM ina kazi kwelikweli. Lakini Mhe.  JPM napenda kukuhakikishia kuwa tupo nyuma yako,  kuna watu wako  tayari kufanya kazi na wewe iwe jua au mvua, ili mradi Tanzania irudi  kwenye mstari na wananchi wanyonge  wapate haki zao. Tunawaomba wakuu wa wilaya watembelee kata zote katika wilaya zao  waongee na wananchi na  ikiwezekana wawe na simu  ofisini kwao kwa ajili kupokea ujumbe wa kero za wananchi, wananchi wapewe namba ya simu hiyo. Mkuu wa wilaya awe anapata majumiisho ya kero za wananchi kila siku/au kila wiki na kuzitolea maagizo/maamuzi. Maafisa tarafa kwa sehemu za vijijini nao wawe na utaratibu wa kupokea  taarifa za wananchi na kuzifanyia kazi kwa niaba ya mkuu wa wilaya.
  Serikali za  mitaa na vitongoji ambazo zitaonekana zinalalamikiwa sana na wananchi  basi mtendaji  hasimamishwe kazi na serikali ya mtaa ivunjwe kwa kufuata taratibu , sheria na mamlaka  aliyopewa waziri mwenye dhamana.  Mtendaji wa kata na afisa tarafa wawajibike kwa kushindwa kutatua kero za wananchi katika maeneo yao.
  Wananchi wamechoshwa na kero ambazo zinasababishwa na viongozi serikali za mitaa na vitongoji ambao wengi wao wamegeuza  matatizo ya wananchi kuwa miradi yao ya kujineemesha. Ni vyema  utumbuaji majibu unaoendelea katika ngazi za juu uende sambamba na utumbuaji majibu katika ngazi za serikali ya mitaa na vitongoji ambako watanzania wengi  ndiko waliko.
   Mungu ibariki Tanzania
   Mdau

  0 0

  Chama cha Mapinduzi CCM leo kimemtangaza Christopher Ole Sendeka kuwa msemaji mpya wa CCM kuanzia leo.Sendeka ametangazwa rasmi na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar.Pichani Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kushoto ni aliyekuwa Katibu Mwenezi wa chama hicho Ndugu Nape Nnauye ambapo kwa sasa Olesendeka pichani kati ndiye ameishika nafasi hiyo.

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtangaza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Christopher Ole Sendeka kuwa Msemaji Rasmi wa CCM leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
  Ole Sendeka akizungumza baada ya kuteuliwa. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Picha: Bashir Nkoromo)  TAARIFA ILIYOSOMWA NA OLE SENDEKA BAADA YA KUTAMBULISHWA KWA WAANDISHI WA HABARI LEO.

  Machi 15, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwaapisha Wakuu wapya wa mikoa, aliagiza pamoja na mambo mengine, viongozi katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanasimamia nguvu kazi ya vijana katika maeneo yao ili waache kukaa kijiweni.

  Agizo hilo lililenga utekelezaji wa vitendo wa matumizi bora ya rasilimali watu nchini wakiwemo vijana ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, kujengewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali.Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa agizo lake hilo lenye lengo muhimu la kuwafanya watanzania kwa pamoja kuwajibika.

  CCM inampongeza Rais Magufuli kwani kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa wapiga kura walio wengi walifanya uamuzi sahihi kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya Tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

  CCM kama chama anachotoka Rais Magufuli na ambacho ndicho Ilani yake inatekelezwa na serikali kwa kupindi cha 2015/2020, ina kila sababu ya kumpongeza kwa kuanza vizuri katika uongozi wake wa miaka mitano na tunaamini kuwa katika kipindi hicho, “Tanzania Tunayoitaka” itafika mbali kimaendeleo kwenye kila ngazi.
    

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Kigambon, Dkt Faustine Ndugulile, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Kamati ya Ushauri ya masuala ya UKIMWI, Afya ya kina mama na Watoto ya Taasisi ya Mabunge Duniani (IPU).

  Dkt. Ndugulile amechaguliwa katika mkutano wa 134 wa Mabunge duniani unaoendelea mjini Lusaka, Zambia. Mkutano huu ulioanza tarehe 17 Machi unatarajia kuisha tarehe 23 Machi. Kabila ya kuchaguliwa kwake Dkt Ndugulile alikuwa ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hii.

  Kamati hii inajumuisha wabunge wasiozidi kumi na mbili (12) ambao huteuliwa na Rais wa IPU kutokana umahiri na mchango wao katika masuala ya UKIMWI na masuala ya Afya ya Mama na Watoto. Wajumbe wengine wa kamati hii wanatoka nchi za Armenia, India, Bangladesh, Afrika Kusini, Rwanda, Italia, Ubelgiji, Austria, Sweden, Dominica na Marekani.

  Majukumu ya Kamati hii n kushauri, kujengea uwezo na kuhamasisha Mabunge Duniani kuhusiana na na njia bora za kuboresha huduma za UKIMWI pamoja na Afya za kina mama na watoto.

  Dkt Ndugulile ni daktari na mbobezi kwenye magonjwa ya maambukizi na pia kwenye Afya ya jamii. Pamoja na majukumu haya mapya, Dkt Ndugulile ni mwakilishi wa bara la Afrika katika Taasisi ya Kimataifa ya UKIMWI (International AIDS Society), mjumbe wa kamati ya wabunge duniani kuhusu masuala ya TB (Global TB Caucus) na Mwakilishi WA Bunge la Tanzania kwenye Bunge la Afrika (Pan African Parliament).

  0 0

  Timua ya MAJIMAJI – WANALIZOMBE  imeendeleza ushindi kwa kuichapa  MBEYA CITY ya jijini MBEYA magoli matatu kwa moja. MAJIMAJI ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la MBEYA CITY  dakika ya 14 kipindi cha kwanza DANNY MRUANDA akapacha goli wavuni. MBEYA CITY nao katika dakika ya 33 ya mchezo ikapata goli la kusawazisha kupitia

  mchezaji wake ABDALA JUMA.Mpaka mapumziko MAJIMAJI moja na MBEYA CITY moja.


  Kipindi cha pili katika dakika 64 ya mchezo, mchezaji wa MBEYA CITY akafanya makosa, ndipo MAJIMAJI ikapewa penati, walioyoitumia vema, na kupitia mchezaji  DANNY MRUANDA akaipatia timu yake goli la pili, dakika ya 78 ya mchezo MAJIMAJI ikapata goli la tatu kupitia mchezaji wake MASSELE BONIVENTURE. Mpaka mpira unamalizika MAJIMAJI WANALIZOMBE ikawa imefunga magoli matatu
  na MBEYA CITY imefunga goli moja.

  0 0

  Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) limewapiga faini ya shilingi milioni 17 raia wa China wanaofanya kazi kwenye wizara ya afya (Chinese medical team) baada yakubaini wizi mkubwa wa Maji kwenye nyumba wanayoishi iliyopo mtaa wa Mtwara Oysterbay Jijini Dar es salaam.

  Akizungumza kwenye eneo la tukio Meneja wa Dawasco Kinondoni, Bi Judith Singinika alieleza kuwa waliwabaini baada ya kufanya operesheni maalum kwenye mtaa huo ya kubaini wizi wa Maji ndipo walipofanikiwa kunasa nyumba hiyo ikiwa imeunganishiwa Maji pasipo mita na kukuta imefungwa pampu kubwa ya kuvuta Maji kutoka kwenye laini ya bomba kubwa la Maji.

  “Dawasco tumewapiga faini raia wa China kiasi cha shilingi milioni 17 baada yakuwanasa wamejiunganishia huduma ya Maji kinyume na utaratibu na laini inayopeleka Maji ndani haina Mita na imefungwa pampu kubwa yakuvuta Maji wakati sio utaratibu hivyo tumeng’oa pampu na nakuwapiga faini ambapo wanatakiwa wailipe ndani ya miezi 24 hivyo watatakiwa walipe kiasi cha shilingi laki 7 kila mwezi”,alisema Singinika.

  Hata hivyo meneja wa Dawasco amesisitiza kuwa operesheni hiyo yakukamata wezi wa Maji kwenye maeneo tofauti ya Jijini Dar es salaam niendelevu na inatokana na agizo la Waziri wa Maji na umwagiliaji Mh Gerson Lwenge ambapo alilitaka shirika hilo kukagua majengo yote makubwa pamoja na viwanda nakujiridhisha matumizi yake ya Maji.

  Hivyo Dawasco inaendelea kuwasihi watu wote waliojiunganishia huduma ya Maji kiholela kinyume cha utaratibu kwenye nyumba za makazi, majengo makubwa pamoja na viwanda kujisalimisha nakutambuliwa kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa endapo wakibainika kwani ndio wanaolikosesha Shirika mapato.
  Pampu iliyokamatwa na mafundi wa Shirika la Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam (Dawasco) iliyokuwa ikivuta Maji kutoka kwenye laini ya bomba kubwa la Maji kupeleka kwenye laini ndogo ambayo ilikuwa imeunganishwa kiholela pasipo mita kwenye nyumba wanayoishi raia wa China ambao wanafanyakazi wizara ya Afya (Chinese medical team) eneo la mtaa wa Mtwara Oysterbay Jijini Dar es Saalam.

  0 0

  Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya ameshiriki Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa  Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman. Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler.
  Katika Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameelezea dhamira ya Umoja wa Afrika kuona kuwa mgogoro wa Libya unapatiwa suluhisho la kudumu. Amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa jawabu la matatizo ya Libya ya hali ya usalama na changamoto zake liko mikononi mwao. Amewakumbusha dhamana kubwa iliyo juu yao na matarajio ya wananchi wa Libya kwa wajumbe hao kupawapatia Katiba ambayo itatoa majawabu kwa changamoto za Libya na kulinda haki na usawa kwa makundi yote. 
  Rais Mstaafu Kikwete pia amepongeza jitihada za Umoja wa Mataifa chini ya Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler za kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Libya kupitia Mkataba wa Amani wa Libya (Libya Political Agreement) uliotiwa saini tarehe 17 Desemba, 2015 huko Shkirat, Morocco. Amehimiza wadau wa pande zote za siasa nchini Libya kutekeleza makubaliano hayo ikiwemo kuundwa kwa serikali na kusimikwa kwa serikali hiyo yalipo makao makuu ya nchi hiyo mjini Tripoli mapema iwezekanavyo.
  Mwakilishi huyo wa Umoja wa Afrika amewahakikishia wajumbe hao utayari wa Umoja wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Falme za Kiarabu (Arab League)  na wadau wengine wote kusaidia jitihada za wananchi wa Libya kurejesha hali ya usalama, amani na utulivu nchini Libya.
   Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya akiongea katika Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa  Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman. Pamoja naye ni  Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler.
  Picha ya pamoja  ya Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa  Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman. 

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Barcelona striker Lionel Messi takes a selfie on top of the roof of Africa in a commercial shoot

  0 0    
  Na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa  kisiwani Zanzibar baada ya watu kujitokeza kuchagua viongozi wao. https://youtu.be/yXTsjsqR0-s
   Zoezi la upigaji kura kisiwani Pemba laelezwa kuendelea vizuri katika maeneo mbalimbali huku baadhi ya vituo vikiwa na watu wengi na vingine wachache.https://youtu.be/TSlXL6UOFkI
   Hivi ndivyo Watu walivyojitokeza kupiga kura kuchagua viongozi wao ili kuweza kuunda serikali wanayotaka. https://youtu.be/ZlhDytKEBAg


older | 1 | .... | 1165 | 1166 | (Page 1167) | 1168 | 1169 | .... | 3278 | newer