Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1161 | 1162 | (Page 1163) | 1164 | 1165 | .... | 3353 | newer

  0 0

  JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
  KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO.

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya uvumi ulioenea katika mitandao ya kijamii kuwa, limepeleka Wanajeshi wengi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kudhibiti Usalama wakati wa kipindi hiki cha uchaguzi marudio unaotarajia kufanyika tarehe 20 Machi, 2016

  Habari hizo siyo za kweli na zina lengo la kupotosha Umma. Kimsingi JWTZ linao Wanajeshi visiwani Zanzibar wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa nchi yetu. Hivyo hakuna Mwanajeshi yeyote aliyeongezwa zaidi ya wale waliopo visiwani humo tangu awali. Taarifa hizo zipuuzwe,zisipewe nafasi yoyote ya kujenga hofu kwa Wananchi.  JWTZ linapenda kwa mara nyingine tena kuwahakikishia Wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi wowote kuhusu ulinzi na usalama wa nchi yetu, kwani wakati wote Jeshi lao lipo imara kuwalinda.

  Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano

  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

  S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

  Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638.

  0 0


  0 0


  Na  Bashir  Yakub.
  Mara  kadhaa  tumeeleza  mambo  mbalimbali  ya kisheria kuhusu  mikopo , waomba mikopo  na  watoa  mikopo.  Haki  na  wajibu  ni  vitu  ambavyo  mara  nyingi  vimeguswa. Hii  ni  kwasababu  eneo  hili  ni  katika  maeneo  tata. 

  Ni tata kwa  pande  zote  yaani taasisi  za  fedha halikadhalika  wachukua  mikopo.  Iko  sintofahamu  nyingi  hasa  kwa  wachukua  mikopo. Mara  nyingi  hawa  hujikuta  katika  matatizo   na  wakati  huo  eti  ndio  hufahamu  haki   na  wajibu  wao.
  Baada  ya  tatizo  kutokea  ndipo  hujua  walitakiwa  kufanya nini  huko  nyuma. Bahati  mbaya muda  huo huwa  wamechelewa  tayari. 

  1.SUALA  NA  KUWA  NA  MKE/MME WAKATI  WA  KUCHUKUA  MKOPO.
  Wakati  wa  kuchukua  mkopo  ni  wakati  ambao  taasisi  inayotoa  mkopo  humtahini ( interview)  mchukua  mkopo. Kila  taasisi  yaweza  kuwa  na  maswali  ambayo  yana tofauti  na  taasisi  nyingine. Maswali hutokana na   na taarifa ambazo  taasisi ingependa  kujua  kutoka  kwa  mchukua  mkopo. 

  Hata  hivyo  pamoja  na  utofauti  huo bado   yapo  maswali  ya  msingi ambayo  kila  taasisi  utakayoenda  kuchukua  mkopo  ni  lazima  utaulizwa.  Haya  ni  yale  yatokanayo  na  sheria zinazohusu  masuala  ya  mikopo.  Ni maswali  yanayofanana( common  questions).

  Moja  ya  maswali  haya  ni  swali  hili   la  kutaka  kujua  kama  muomba  mkopo  ana  mwenza kwa  maana  ya  mke  au  mme.  Hili  ni  swali  la  kisheria  ambalo   lina  athari  na  matokeo  ya  kisheria  kama  tutakavyoona  hapa . 

  2.UPI  UMUHIMU  WA  KUJUA IWAPO MWOMBA  MKOPO  ANA  MME/MKE.

  Hii  ni  kwasababu  unapochukua  mkopo   mara  nyingi  hutakiwa  kuweka  rehani.  Na  rehani  inayokubalika  huwa  ni  mali  isiyohamishika  ambayo  ni  nyumba au  kiwanja. Na  mara  nyingi nyumba  au  kiwanja  ni  mali  ambazo  huhesabika  zinamilikiwa  kwa pamoja kati ya  mme  na  mke  ikiwa  wameoana. 

  Kwa  maana  si  ruhusa  kwa  mmoja  wa wanandoa  hao  kuweka  rehani  mali  hizo  bila  mwingine kuridhia. Na  ikitokea  kuwa mmoja  hakuridhia  basi  hupata  haki  ya kusitisha  mali  hiyo  kuhusishwa  katika  mkopo.

  Hatua  hiyo  inaweza  kuwa  hasara  kwa  mtoa  mkopo. Basi  kutokana  na  hilo huibuka  umuhimu mkubwa  wa  kujua  iwapo  mwomba  mkopo   ana  mke/mme.

  KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com

  0 0

  Zimamoto wameiokoa !
  Moto ambao hakuleta madhara makubwa!
  Habari ambazo zilikuwa zimefichwa lakini ! tumezinyaka
  Kuwa jengo linalotumiwa kufanyia mazoezi na bendi maarufu ya muziki wa dandi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni limeshika moto ghafla na kuokolewa na kikosi cha zimamoto huko ujerumani.

  Wadakuzi wa mambo walimtafuta mkuu wa bendi hiyo bila mafanikio
  kamanda ras makunja kazima simu. tukampata mmoja wa wanamuziki
  wa bendi hiyo ambaye alisema kweli kambi ilishika moto lakini moto huo
  haUkufika katika ukumbi wa mazoezi,kwani ukumbi wa mazoezi upo chini
  under ground ambako si rahisi kufika.
   
  jengo hilo pia ni kituo cha vijana
  na ofisi za tasisi mbali mbali zinazoshughulika na mambo ya utamaduni.
  chanzo cha moto huo mpaka sasa hakijajulikana, lakini inaonyesha ulianzia katika papipa ya taka yaliyowekwa karibu na mlango.

   

  0 0

  Wavaaji nguo za mitindo wakipata picha ya pamoja na mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
  Mama mitindo Asya Idarous Khamsini (kati) akiwa katika picha ya pamoja na mashabiki wake wa mitindo kwenye usiku wa Tanzania Red Carpet uliofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 mjini Seattle jimbo la Washington na kuhudhuriwa na Watanzania wanaoishi jimbo hilo na marafiki zao.
  Mama mitindo Asya Idarous Khamsini akipata ukodak moment.

  0 0

   Mhe. Waziri wa Afya.Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumzia uzefu wa Tanzania katika kukabiliana na tatizo la  ukeketaji akiwa na wazungumzaji wengine katika Meza Kuu, kutoka kushoto ni Mke wa  Rais wa Burkina Faso Bi. Sika Bella Kabore,  Bw. Benoit Kalasi (UNFPA), Bi.Emma Bonino Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Italia.
    Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mhe. Peter Serukamba akifuatilia majadiliano kuhusu tatizo la  ukeketaji  na  adhari zake wa afya na maendeleo ya mtoto wa kike na mwanamke.
   Wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi nao wakifuatilia majadiliano  yaliyovutia washiriki wengi kuhusu madhara  yatokanayo  na ukeketaji na namna gani  jamii inatakiwa kushirikiana kutokoza tatizo hilo. 
  Sehemu ya washiriki wa Mkutano na majadiliano  kuhusu utokomezaji wa vitendo vya ukeketaji na uhusiano wake na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Mkutano huu  uliandaliwa kwa pamoja na Wakilishi za  Kudumu za Tanzania, Burkina Faso, Italy, Iran, UNFPA na UNCEF.


  Na Mwandishi Maalum, New York
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ( Mb)  amesisitiza   kuwa ni  kwa ushirikiano baina ya Serikali  na  jamii ndipo tatizo la ukeketaji  kwa watoto wa kike na wanawake litakapoweza kutokomezwa.

  Akaongeza kwamba, serikali  inaweza kutunga sheria nyingi  za kukabiliana na tatizo hilo  lakini kama jamii yenyewe  kuanzia ngazi  ya familia isipotoa ushuriano wa dhani itachukua muda mrefu kwa tatizo hilo kutokomezwa. Alikuwa akizungumza wakati wa majadiliano ya mkutano wa  kuhusu  utokomezwaji  vitendo vya ukeketaji kama sehemu  muhimu ya utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( Agenda 2030.

  Waziri Ummy Mwalimu alikuwa mmoja wa  wazungumzaji wakuu  katika  mkutano  huo  uliowahusisha  Mke wa Rais wa  Burkina Faso, Bibi. Sika Bella Kabore, Mawaziri na  Asasi za Kiraia na uliandaliwa kwa pamoja  na Wakilishi za kudumu za Tanzania,  Italy, Iran, Burkina Faso,UNFPA na UNICEF, ikiwa ni sehemu ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni  ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake.

  Na kwa sababu hiyo, Waziri  Ummy Mwalimu, amerejea kutoa wito kwa watanzania wote kwa  katika ujumla wao   wakiwamo wazee wa kimila, viongozi wa dini na vijana wakiume    kutoa ushirikiano kwa  serikali na wadau wengine ili hatimaye tatizo hilo ambalo   linaelezwa  kuwa  siyo tu lina madhara makubwa kiafya na kisaikolojia lakini pia ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

  “Tunatakiwa kufanya kazi kwa  pamoja na katika umoja  wetu, serikali peke yake haitaweza kulimaliza tatizo hili, ambalo  imefikia mahali  sasa  wazazi kwa kuongopa mkono wa sharia wanaamua kuwafanyia ukeketeji watoto wa kike katika umri  mdogo sana” Akaeleza Waziri.Akasema  , Tanzania  imebaini  uelimishwaji na  majadiliano  yanayohusisha familia na vijana wakiume ni muhumu katika kuchangiza juhudi za serikali katika  kukabili ukeketaji.
  0 0

  ·         Aagiza TAKUKURU na Polisi kuanza uchunguzi mara moja

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa tuhuma za ubadhirifu, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

  Watumishi hao ni Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika, Bw. Mwita Mirumbe Waryuba pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya, Bw. Dioniz Mutayoba. Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana usiku (Jumatano, Machi 16, 2016) alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara zote na taasisi zilizomo kwenye wilaya ya Chato katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mshikamano SACCOS wilayani humo.

  Afisa Kilimo na Ushirika anadaiwa kuchangisha kiasi cha sh. milioni 20 kutoka kwa watumishi wa Halmashauri hiyo kwa ajili ya kuanzisha SACCOS tangu mwaka 2013 lakini hadi sasa SACCOS haijaanzishwa na wala fedha hizo hazijarejeshwa. Fedha hizo zinadaiwa kuliwa na watumishi watatu (majina yamehifadhiwa). Aidha, Bw. Waryuba anadaiwa kutumia lugha chafu na za vitisho kwa watumishi walio chini yake ikiwa ni pamoja na kuomba na kupokea rushwa, na kunyanyasa na kudhalilisha kijinsia baadhi ya watumishi wa kike.

  Inadaiwa pia Bw. Waryuba alikopa bila kufuata taratibu za mikopo wilayani Chato ambapo alikopa sh. milioni 15 kutoka Mwambao SACCOS na sh. milioni 15 nyingine kutoka Chato Teachers’ SACCOS tangu mwaka 2015 na tangu wakati huo hajazirejesha hali ambayo imeleta manung’uniko kutoka kwa viongozi na wananchama wa SACCOS husika.

  “Malalamiko ya watumishi na wananchi dhidi ya huyu bwana yamefikishwa kwa Kaimu Mkurugenzi lakini hajachukua hatua kwa sababu ni rafiki yake,” alisema Waziri Mkuu. Kaimu Mkurugenzi huyo ni Mhandisi Joel Baha ambaye hakuwepo ukumbini hapo kwa sababu yuko kwenye ziara ya mafunzo huko Japan. Kwa upande wake, Bw. Mutayoba ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo anadaiwa kuzembea kusimamia mradi wa kufyatua matofali ya gharama nafuu (interlocking bricks) zilizogawiwa kwa vikundi vinne vya vijana wa wilaya hiyo.

  “Mwaka 2013 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilitoa mashine nne za kufyatulia matofali ya bei nafuu kwa ajili ya vikundi vinne vya vijana wilayani Chato. Mashine hizo ziligawiwa kupitia kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya, Bw. Dioniz Mutayoba na kila kikundi kilipewa sh. 500,000 ili waanze kazi ya kufyatua matofali na kuyauza kwa bei nafuu katika maeneo waliyopo lakini hadi leo hakuna kitu kilichofanyika,” inasema sehemu ya taarifa.

  Afisa huyo anadaiwa kugawa mashine mbili kwa kila kata katika kata za Muganza na Buseresere lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika kwani vikundi hivyo havikuzalisha kitu chochote tangu wakati huo. Aidha, Bw. Mutayoba anatuhumiwa kudai na kupokea rushwa kwa wanachama wa vikundi vya ujasiriamali ili aweze kuvisaidia kupata mikopo. “Yaani watu wanakuja kukopa sh. milioni mbili halafu unawadai kitu kidogo cha sh. 300,000. Sasa mradi waliotaka kufanya wataweza kuukamilisha kweli?,” alihoji Waziri Mkuu.

  “Huyu bwana amelalamikiwa lakini Mkurugenzi aliyepita lakini naye anadaiwa kumlinda kwa sababu ni rafiki yake,” alisema Waziri Mkuu na kuibua minong’ono ndani ya ukumbi huo. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato, Bw. Clement Berege hivi sasa amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.

  “Katika Serikali hii tunataka tuwe na Halmashauri zilizo safi. Lakini pia Serikali hii ina mkakati wa kuimarisha ushirika na tunataka kuinua kilimo. Kwa hiyo basi, TAKUKURU na polisi wachunguzeni hawa watu wawili kwa maana ya Afisa Ushirika na Afisa Maendeleo ya Jamii na nipewe taarifa uchunguzi utakapokamilika,” alisema Waziri Mkuu.

  Mapema, akizungumza na watumishi hao, Waziri Mkuu ambaye amewasili mkoani Geita kwa ziara ya siku mbili akitokea mkoani Kagera, alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi hao aliwakumbusha wajibu wao wa kuwahudumia Watanzania bila kujali hali zao na akasisitiza kuwa Serikali haitamuonea mtumishi yeyote ambaye anatimiza wajibu wake.

  “Napenda kusisitiza kuwa malengo ya Serikali ni kuimarisha utendaji wa watumishi lakini pia Serikali hii haitamvumilia mtu mdanganyifu, mzembe, asiye mwadilifu na mla rushwa. Ukiharibu kazi hapa Chato mwwisho wako ni hapa hapa tu. Usitarajie kupelekwa Bunda au kwingine ili ukaharibu na huko,” aliongeza.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  ALHAMISI, MACHI 17, 2016.

  0 0
 • 03/16/16--23:13: DONDOO ZA MAGAZETI

 • 0 0
 • 03/16/16--23:18: Article 12


 • 0 0

  MWENYEKITI wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama amekoshwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka litakalofanyika Mwanza Machi 27 na kueleza kwamba ni faraja kwao.

  Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema Nape ni mmoja wa walezi wa tamasha hilo ambalo mwaka huu linatarajia kuanzia Geita Machi 26 na kumalizikia Kahama Machi 28.

  “Maandalizi kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri Nape, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa muziki wa Injili,” alisema Msama  na kuongeza.

  “Tunafurahishwa na Waziri Nape kukubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka, kwa sababu ni mmoja wa wanaoweza kusaidia mipangilio ya Matamasha yanayoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions kama ilivyokuwa Tamasha la Krismasi lililofanyika mwaka jana,” alisema Msama.  
    
  Aidha Msama anatumia fursa hiyo kuwaweka bayana waimbaji waliothibitisha kushiriki  Tamasha la Pasaka ambao ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Sifael Mwabuka, Jenipher Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro ya Mwanza na Kwaya ya Wakorintho wa pili kutoka Njombe.

  Anavitaja viingilio katika tamasha hilo litakalofanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa ni Sh. 5,000 kwa wakubwa na kwa watoto Sh 2,000. Msama alisema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vema na kutoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi.

  0 0


  0 0
 • 03/16/16--23:42: What is Emerald Gemstone?
 •  Rough Emerald                                             
  Cut and Polished Emerald

  By Eng.Gilay Shamika
  Senior Engineer and Gemologist at TMAA

  Emerald name comes from Greek word meaning green. Before, Greeks called all gemstones with green color Emeralds until when gemological knowledge categorized other green colored gemstones according to their refractive index.
  Emerald being among the ‘big four’ gemstones which are Ruby, Sapphire, Tourmaline and Emerald itself, it assumes higher price as well. However, compared to other big four gemstones, Emeralds are the gemstones which are rarely found without inclusion and fractures. Most of Emeralds are found with fractures and inclusions. Therefore, there is tolerance in the market for Emeralds grades, that is fracture filling and inclusions into Emeralds are factors which are normal but not tolerable into other gemstones.

  This means, don’t be surprised when you mine Emeralds and you find all times you don’t get emeralds with no fractures and inclusion free. It is the gem with the most cracks and inclusions; three and two-phase inclusions, fingerprint inclusions, liquid filled inclusions, tube and needle like inclusions, calcite inclusions, angular growth zoning and minerals/crystals inclusions.


  In Tanzania Emeralds deposits are available in different places including Manyara: Mbulu Kagera: Karagwe –kyerwa .Morogoro: Mt. Nguru. Rukwa: Sumbawanga-Mpanda.

  The international Market receives great majority of Emeralds from Colombia, Zambia, Brazil and Zimbabwe. Other countries which supply emeralds but not in consistent volume to the international market include Tanzania, Russia, Pakistan, Australia, India, Afghanistan and Madagascar.


  Geology

  Emeralds are formed in either metamorphic rock or sedimentary rock. However, mostly emeralds are formed in regions with metamorphic rock environments, where pegmatite intersects with schists. Emeralds form when beryllium, aluminum, silicon, oxygen and one or more of trace elements like chromium, vanadium and iron that cause its characteristic green color come together in the correct geological environment.

  Color Ranges: Emerald has only green color; it is a beryl with green color.

  Variety: Emerald belongs to beryl group which has two varieties – Emerald and Aquamarine. Aquamarine is a blue beryl while Emerald is a green beryl.

  Emeralds’ Imitations are: Green glass, Synthetic spinel triplet

  Synthetic Emeralds: Flux Emeralds and hydrothermal Emeralds

  Buyers have alternatives for Emeralds and sometime confuse with: Demantoid garnet, Tourmaline, Diopside, Jadeite, Peridot, Zircon, Tsavorite garnet, Alexandrite.


  Gemological properties of Emerald


  Gemological Properties of Emerald

  Unit of Measure

  Gem group

  Beryl

  Refractive Index (RI)

   1.577 to 1.583

  Specific gravity

  2.72

  Hardness (Mohs Scale)

  7.5 to 8


  Treatment and Grading of Emerald

  Fracture filling: filling surface-reaching fractures with colorless oils or resins. Almost 95% of Emeralds are fracture filled because the occurrence of emerald is associated with fractures and inclusions.

                                                               

  Emerald Grading

  Explanation

  A

  Vivid Pure Green

  B

  Deep Green Colour

  C

  Green Color  with zoning, window and impurities

  Traditional Grading


  Gem quality

  A

  Near Gem

  B

  Industrial/Low quality

  C

  0 0


  ·         Ni Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Chato
  ·         Pampu yadaiwa kupelekwa Morogoro, yeye asema iko kijijini

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Chato, Bw. Peter Ngunura kwa kosa la kumdanganya mbele za watu na kumpa taarifa za uongo juu ya pampu ya maji iliyodaiwa kupelekwa Morogoro.

  Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Machi 16, 2016) alipokuwa akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Chato waliojitokeza kumsikiliza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo wilayani Chato, mkoani Geita.

  Waziri Mkuu ambaye amewasili mkoani Geita kwa ziara ya siku mbili akitokea mkoani Kagera, alisimamishwa na wakazi wa kijiji cha Kalebezo, kata ya Nyamirembe, wilayani Chato na kukuta mabango yaliyokuwa yakidai maji safi na kuelezea uharibifu wa pampu ya maji.

  Katika maelezo yao, wakazi hao walimweleza Waziri Mkuu kwamba mradi wa maji kwenye kata hiyo ulishakamilika lakini pampu yao imechukuliwa na kupelekwa Morogoro jambo lililosababisha wakose maji kwa muda mrefu.

  Kwa sababu alikuwa hajafika Chato mjini na hakuwa na taarifa sahihi za mradi huo wa maji, Waziri Mkuu aliwaeleza wakazi hao kwamba analibeba jambo hilo na atafuatilia hadi aelezwe ni kwa nini pampu hiyo imepelekwa Morogoro. Akiwa kwenye mkutano wa hadhara, ndipo suala la maji likaibuka tena na Waziri Mkuu kuamua kuchukua hatua hiyo.

  “It’s unethical (ni kinyume cha maadili) kumdanganya kiongozi wako. Nimekuuliza mara mbili mbili kama una uhakika kuwa pampu hiyo ipo ukasema una uhakika kuwa ipo. Nimemtuma diwani na vijana wangu wakacheki wakasema hakuna pampu,” alisema Waziri Mkuu na kumwita Diwani huyo jukwaani ili atoe majibu.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Joyce Thobias na mwanae Jonathan Mbarak ambaye amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Chato akimuuguza mwanae majeraha ya moto Machi 16,2916. mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Geita.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha gari la wagonjwa likiwa ni moja kati ya mawili yaliyotolewa msaada na Bibi Merete Trolle wa Denmark akisaidiwa kulisafilisha hadi hapa nchini na Mgodi wa Geita Gold Mine. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye hospitali ya wilaya ya Chato Machi 16, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua duka la dawa la MSD baada ya kulizindua kwenye hospitali ya wilaya ya Chato Machi 16, 2016. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD, Profesa Mtulia.
  Waziri Mkuu, Kasim Majaliiwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Chato , Machi 16, 2016.

  0 0

  Mkurugenzi Idara ya Habari- MAELEZO Bw.Assa Mwambene(wa tatu kushoto) akikabidhi madawati kwa watoto wa shule ya msingi Tindiga wakati maafisa habari na mawasiliano wa serikali walipotembelea shule hiyo kugawa madawati na kufanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji wilayani kilosa.Wengine pichani ni Mkuu wa wilaya ya kilosa Bw.John Henjewele(wa pili kulia).
  Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kilosa wakati alipokuwa akiongea nao walipotembelea shule ya palakuyo kutoa vifaa vya kusomea masomo ya Sayansi na kufanya kampeni ya kuhamasisha kuacha mauaji baina ya wakulima na wafugaji.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akitoa mada kuhusu huduma mbalimbali za TeknolojiA ya mawasiliano kwa njia ya mitandano  kwenye kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano serikalini katika ukumbi wa VETA mkoani Morogoro leo Machi 17, 2016
  Afisa kutoka kampuni ya Push Mobile Bi. Patricia Michael akitoa mada kuhusu huduma mpya ya upashaji habari kwa njia ya simu za mkononi iitwayo SIMU TV kwenye kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano serikalini katika ukumbi wa VETA mkoani Morogoro leo Machi 17, 2016
  Meneja wa mawasiliano na uhusiano wa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bi. Gaudensia Simwanza    akipokea  zawadi baada ya kufaulu maswali kutoka kwa Mwezeshaji kutoka Uongozi Institute, Bi Joy Nyabongo katika kikao kazi cha maafisa Habari na Mawasiliano  Serikalini ukumnbi wa VETA mjini Morogoro
  Afisa kutoka kampuni ya Push Mobile Bw. Abdi Zagar  akitoa mada kuhusu huduma mpya ya upashaji habari kwa njia ya simu za mkononi iitwayo SIMU TV kwenye kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano serikalini katika ukumbi wa VETA mkoani Morogoro leo Machi 17, 2016
  Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Sarah Kibonde akitoa mada kuhusu mamlaka hiyo kwenye kikao kazi cha maafisa habari na mawasiliano serikalini katika ukumbi wa VETA mkoani Morogoro leo Machi 17, 2016
  0 0

  The East African Legislative Assembly has proposed enactment of an omnibus law to harmonize national laws appertaining to the Community and to institute an administration law for the Common Market Protocol. 

  The Assembly is of the view such a move shall cure, existing challenges of harmonisation of Partner State laws appertaining to the Community. At the same time, the Assembly wants the Council of Ministers to direct the Sectoral Council on Legal and Judicial Affairs to hold regular meetings and to prioritize harmonization of laws for EAC in order facilitate integration within the set time frames. 

  In order to meaningfully facilitate co-operation in legal and judicial affairs as provided for under Article 126 of the Treaty, EALA urges EAC Council of Ministers to expedite implementation of the entire Article which obliges Partner States to harmonize legal training and certification; encourage standardization of judgments of courts within the Community as well as in establishing common syllabus for the training of lawyers.
  Hon Dora Byamukama refers to the EAC Treaty. The legislator presented the report of the Committee on Legal Rules and Privileges on the oversight activity on the harmonisation of national laws in the EAC context.

  Late yesterday, EALA approved the Report of the Committee on Legal Rules and Privileges on the oversight activity on the harmonisation of national laws in the EAC context. The Report presented to the House by Hon Dora Byamukama on behalf of the Chair of the Committee, Hon Peter Mathuki, follows an oversight activity carried out by the Committee in February 22- 26, 2016.


  Chapter 24 of the Treaty provides for co-operation in Legal and Judicial Affairs. Specifically, Article 126 (2) (b) of the Treaty provides that “Partner States shall through their appropriate national institutions take all necessary steps to harmonize all their national laws appertaining to the Community”. 
  Hon Martin Ngoga gestures as he makes a point during the debate earlier today.

  In line with that Treaty provision, EAC Partner States established a sub-committee on the approximation of national laws in the EAC context.


  0 0

   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili jijini hapo jana akitokea mkoani  Kagera kwa ziara ya kikazi.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akisaini katika kitabu mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Mwanza,mara baada ya kuwasili jijini hapo  jana akitokea Kagera kwa ziara ya kikazi.
   Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,ACP Japhet Lusingu(kushoto), akitoa taarifa ya hali ya usalama katika mkoa wa Mwanza kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(katikati) mara baada ya Naibu Waziri kuwasili jijini Mwanza jana akitokea mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.Kulia ni Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai mkoa wa Mwanza,SSP Augustine Senga.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili jijini hapo jana akitokea Kagera kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi) .Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

   Mkurugenzi wa kampuni ya Jaffery Industry Saini LTD Ndg. Vinshal Singh Saini akitoa maelezo juu ya hatua iliyofikiwa katika ufugaji meza mpya katika ukumbi wa Bunge kwa Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah (mwenye miwani) alipotembelea kujionea hatua ya ukarabati wa Jengo la Bunge ilipofikiwa.
     Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akijaribisha kukaa katika moja wapo ya kiti kilichofungwa katika meza mpya kwenye ukumbi wa Bunge. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa kampuni ya Jaffery Industry Saini LTD Ndg. Vinshal Singh Saini akimpa maelezo juu ya namna viti na meza hizo vitakavyokuwa vinatumika baada ya kukamilika.
   Mwonekano wa Meza Mpya zilizofungwa katika Ukumbi wa Bunge
  Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Jaffery Industry Saini LTD Ndg. Vinshal Singh Saini mara inayofunga meza mpya katika ukumbi wa Bunge maada ya kukagua ukarabati wa Jengo la Bunge.Picha na Ofisi ya Bunge


  0 0

  Ajali iliyohusisha Basi la Kampuniya Ndenjela na basi ndogo aina ya Toyota Hiace, imetokea mapema leo asubuhi katika eneo la St Agrey Uyole, Jijini Mbeya na kupelekea watu kadhaa kujeruhiwa, huku wengine wakidhaniwa kupoteza maisha. Chanzo cha ajali hiyo, inaelezwa kwamba ni basi hilo dogo kuingia barabara kubwa bila ya tahadhali, hali iliyopelekea kugongwa na Basi hilo la Ndenjela lililokuwa safarini kuelekea Jijini Dar es salaam.Picha na Fadhil Atick MR PENDO, GLOBU YA JAMII, MBEYA

older | 1 | .... | 1161 | 1162 | (Page 1163) | 1164 | 1165 | .... | 3353 | newer