Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1160 | 1161 | (Page 1162) | 1163 | 1164 | .... | 3348 | newer

  0 0

  ASSALAAM ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATU
  Al Madrasat Rahman iliyopo Segerea mwisho,Dar-es-Salaam
  .
  INAWAALIKA KATIKA SHUGHULI YA MAWLID YA KUMSIFU
  MTUME WETU MUHAMMAD (S.A.W) siku ya jumamosi 19/03/2016 Jitokezi kwa wingi!

  Ndugu zetu watukufu wa kiislam Uongozi wa Al Masjid Qubbah na  Madrasat Rahman ya Tabata Segerea Mwisho,Dar-es-salam inawaalika waislamu wote waume kwa wanawake,Masheikh,na Madrasat mbalimbali kuwa siku ya jumamosi ya tarehe 19/3/2016 kutakua na Maulid ya kumsifu bwana Mtume Muhammad (S.A.W) katika viwanja vya madrasat Rahman segerea mwisho. 

  Kama ilivyoada kuanzia saa nne asubuhi kutakua na maulid ya kina mama mpaka saa kumi alasiri, na baada ya swalatul inshai kutakua na maulid ya jumuiya waume kwa wanawake.Jitokezeni kwa wingi katika shughuli hii,tuuzaje uwanja wa shughuli hii ,kushiriki kwenu ndio mafanikio na baraka ya shughuli hii ya Maulid ya Mtume Muhammad(S.W.A)
   Karibuni sana.INSHAALLAH

  WABILLAH TAUFIQIH mawasiliano Simu 0777 000036, au 0712 840 960


  0 0


  9222e2ae-9627-4a09-abd3-72692b57d550Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu akiwa katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Tanzania wa Kudumu Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manong.
  Ummy Mwalimu
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu ( Mb) ametoa hutuba kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Mkutano huu wa wiki mbili .

  unawakusanya wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia ambapo hujadiliana na kubalishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua mbalimbali ambazo serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya mwanamke na mtoto wa kike.

  Wakati mamia ya wanawake kutoka serikalini na Asasi za Kiraia wakiwa wanakutana hapa Umoja wa Mataifa kwa mkutano wao unaojadili hali yao katika maeneo mbalimbali. Mamia mengine ya wanawake hususani wale wa Afrika wanaendelea kukumbana na changamoto lukuki zinazowarudisha nyuma kimaendeleo.

  Ni wanawake hao wanaoishi katika nchi zenye migogoro, vita visivyokwisha, wenye kukabiliwa na uhaba na ukosefu mkubwa wa chakula, maji safi na salama, matatizo yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, ndio ambao Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu(Mb) ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya ushirikiano ili malengo mapya ya maendeleo endelevu (Agenda 2030) yaweze kuwafikia.


  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema daraja la Kigamboni litafunguliwa rasmi Aprili, 16 mwaka huu.
  Amesema kazi inayoendelea sasa hivi ni kupitisha magari maalum kwa ajili ya kupima ubora wa daraja hilo ili kujiridhisha kabla ya kukabidhiwa rasmi Serikalini.
  Amewataka watumiaji wa daraja hilo kuwa waangalifu, kulinda miundombinu na kuepuka vitendo vya hujuma  ili lidumu kwa muda mrefu.“Daraja hili lina urefu wa mita 640, barabara sita, tatu zinapanda na tatu zinashuka, hivyo tunawaomba wananchi watakaovuka kuzingatia usafi na ustaarabu”, amesema Profesa Mbarawa.
  Amebainisha kuwa Serikali itaweka sheria kali kwa wote watakaokiuka matumizi sahihi ya daraja hilo na kusisitiza umuhimu wa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani wanapovuka katika daraja hilo.
  Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja hilo Eng. Karim Mattaka amesema wataalam wanaendelea na taratibu za kulipima daraja hilo ili kujiridhisha kama linamudu kupitisha uzito uliokusudiwa kabla ya kulikabidhi kwa Serikali mapema mwezi ujao.
  Amesema awamu ya kwanza ya kulipima daraja hilo imekamilika na sasa wanaendelea na awamu ya pili hadi watakapomaliza awamu nne ili kujiridhisha kabla ya kuanza kutumika.
  Takribani shilingi bilioni 216 zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo linalotazamiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa abiria na magari katika kivuko cha Magogoni na Kigamboni.
  IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akipata maelezo kutoka kwa Meneja Msimamizi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni Eng. Karim Mattaka alipokagua daraja hilo leo jijini Dar es salaam.
   Mwonekano wa daraja la Kigamboni ambalo litafunguliwa rasmi mwezi ujao.
  Barabara za maingilio (inter change) ya Daraja la Kigamboni upande wa Kurasini.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja miradi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Eng. John Msemo wakati alipotembelea daraja la Kigamboni kuangalia ujenzi wa daraja la Kigamboni leo jijini Dar es salaam.

  0 0
 • 03/15/16--23:05: DONDOO ZA MAGAZETI LEO

 • 0 0


  0 0

  Mtu mmoja mkazi wa Mbangala – Chapwa wilaya ya Momba aliyefahamika kwa jina la Erasto Vickson [17] alifariki Dunia baada ya gari yenye namba za usajili T.806 ABY aina ya mitsubishi Fuso lori lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Masoud Wilson Nzowa kushindwa kupanda mlima na kisha kurudi nyuma.

  Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 15.03.2016 majira ya saa 09:45 asubuhi huko mtaa wa Chapwa, kata na tarafa ya Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya. 

  Inadaiwa kuwa, marehemu ambaye alikuwa abiria kwenye gari hilo aliruka toka ndani ya gari baada ya kuona gari limeshindwa kupanda mlima na kuanza kurudi nyuma. Mwili wa marehemu umehifadhiwa kituo cha afya Tunduma. Dereva alikimbia baada ya tukio. Upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na kumtafuta mtuhumiwa.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi  anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa wa tukio hili azitoe katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za kisheria. 

  Imesainiwa na:
  [Ahmed Z. Msangi – SACP]
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya.

  0 0

  A key report of the oversight activity of EAC Institutions with regards to governance, project performance was today adopted by the Assembly.

  The Report presented to the House by Chair of the Accounts Committee, Hon Jeremie Ngendakumana emanates from oversight activities carried out by the Accounts Committee last month (February 2016) following queries obtained from the EAC Audited Financial Statements for the year ended 30th June 2014. 

  It also set to establish the adherence to the extent of status of implementation of the Assembly’s recommendations. The Committee visited the Lake Victoria Fisheries Organisation (LVFO) and the EAC Civil Aviation Safety and Security Oversight Agency (CASSOA) in Jinja and Entebbe respectively.  

  The Committee reported that the oversight activity at the Inter-University Council of East Africa (IUCEA) which was envisaged was not undertaken as the heads of the institution were away as at time of the activity.  The Committee however received information on governance and its adherence to the Assembly’s recommendations sent by the IUCEA.
  Hon ShyRose Bhanji during debate on the Report. She called for additional funding for the EAC Institutions.

  The objectives of the assessment were to assess whether governance and management systems of the institutions are good enough to guarantee performance and proper discharge of duties.    It further sought to establish the implementation of the Assembly’s recommendations, strengthen governance and management systems of EAC Institutions and to establish extent to which the said institutions apply modern governance and management of applied technologies.

  At the LVFO, the Committee reported the need for Council of Ministers to fast track accession of other Partner States to the LVFO  as well as the need to urge the Council of Ministers to avail current data of fish to LVFO for updates.  This the Committee ascertains, arises from the fact that the quality of fish is declining despite achievements and initiatives by LVFO. Therefore, the Committee informed the House that it was vital to carry out comprehensive sensitisation, provide all amenities and other facilities to fish farmers to spur increase in numbers.
  Hon Yves Nsabimana makes his contribution on the floor of the House today.

  The Committee generally noted progress with regards to the status of implementation of the Assembly’s recommendations at the Jinja- based LVFO.  The Assembly however calls on the Audit Commission to report during the next audit on a number of areas including the unclaimed Value Added Tax and other outstanding areas such as the persisting overdue receivables. Other thematic areas include need to harmonise guidelines for development of fish cages, setting of regional standards for fish-feed and evidence of a disaster recovery plan.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akimuuliza jambo Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame, mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ajili ya ziara ya kikazi Zanzibar. Kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Sururu.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akikagua gadi maalumu iliyoandaliwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi Zanzibar alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, mjini Magharibi Zanzibar.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar, Makamanda wa Polisi, Wakuu wa Upelelezi pamoja na Maafisa Wanadhimu wa mikoa mitatu ya Unguja. Kulia meza kuu ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akipewa maelezo na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omari Makame (kulia) wakati wa kikao chake na Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar, Makamanda wa Polisi, Wakuu wa Upelelezi na Maafisa Wanadhimu wa mikoa mitatu ya Unguja. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa kikao cha bodi ya barabara Mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze akifafanua jambo katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.


  NA VICTOR MASANGU, PWANI  

  IMEELEWA kwamba kutokana  na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini zimeweza kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya barabara  na madaraja katika baadhi ya maeneo ya mkoani Pwani hali ambayo imekuwa ni kero kubwa  kwa wananchi kutokana  na magari kukwama hivyo  kutokupitika kwa urahisi.

  Hayo yamesemwa  na  Mhandisi mkuu wa kitengo  cha mipango kutoka Wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Zuhura Amani wakati akiwakilisha taarifa ya utekelezaji  wa kazi za matengenezo na miradi ya maendeleo kwa wajumbe  wa kikao cha bodi ya barabara cha Mkoa, ambapo amesema kuwa kuharibika kwa miundombinu hiyo  kunarudisha nyuma jitihada za serikai katika kuleta huduma kwa jamii.

  Zuhura alisema    kuwa jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 20.9 zilipangwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2014 hadi 2015 lakini kutokana na kuwepo kwa ufinyu wa bajeti zoezi hilo halikuweza kufanikiwa kwa wakati uliopangwa.

  Meneja wa wakala wa barabara Tanroad Mkoa wa Pwani Tumaini Salakikye akitolea ufafanuai na kujibu maswali yalioulizwa na wajumbe wa kikao hicho juu ya miundombinu ya barabara.

  Kwa upande wao wajumbe waliohudhuria  katika kikao hicho  akiwemo Mwenyekiti wa CCM  katika Wilaya ya Kibaha Mji,Maulid Bundala  pamoja na Katibu msaidizi wa Mkoa wa Pwani  Shangwe Twamala walisema hai hiyo ya ubovu wa barabara inachangia kwa kiasi kikubwa kukwama kwa magari hivyo kupelekea usumnufu mkubwa hasa katika kipindi cha mvua.


  0 0  0 0

  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa dini wakati alipowasili katika kambi ya Rumasi-Lukole iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera,kambi hiyo hutumika kupokea wakimbizi wanaotoka nchini Burundi ambapo baadae hupelekwa katika makambi ya Nyarugusu yaliyopo mkoani Kigoma.Waziri Mkuu yupo mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,akizungumza na raia wa Tanzania pamoja na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi ya Rumasi-Lukole(hawapo pichani), Waziri Mkuu alitembelea kambi hiyo iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera na kuwaasa wakimbizi hao kuishi kwa kufuata sheria za nchi pasipo kuvunja amani iliyopo nchini.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akizungumza na wakimbizi wanaoishi katika kambi ya Rumasi-Lukole(hawapo pichani),wakati ya ziara aliyoongozana na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.Kambi hiyo iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera hupokea wakimbizi kutoka nchi ya Burundi kabla ya kuwapeleka kwenye makambi ya wakimbizi ya Nyarugusu,mkoani Kigoma.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Veronica Simba

  Serikali ya Tanzania imeendelea kupokea maombi ya wawekezaji hususani katika miradi mbalimbali ya uzalishaji na usambazaji umeme. Hivi karibuni, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alikutana na kuzungumza na Ujumbe kutoka Kampuni ya NARI Group Corporation ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Gridi ya Taifa la China, ambao walimweleza Waziri kuwa, pamoja na madhumuni mengine, wana nia ya kuzalisha umeme.

  Makamu Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Bao Tianhua alimweleza Waziri Muhongo kuwa, Kampuni yake inao mtaji wa kutosha pamoja na teknolojia ya kisasa katika uzalishaji umeme. Aliongeza kuwa Kampuni ya NARI ina uzoefu mkubwa katika kutekeleza miradi ya umeme kwani ilianza kufanya kazi kutoka miaka ya 1960.

  Akijibu swali la Waziri kuhusu kiwango cha umeme ambacho Kampuni yake imejipanga kuzalisha endapo itakubaliwa maombi yake, Tianhua alisema wamejipanga kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 300 hadi 400 kwa kuanzia.

  Akieleza zaidi kuhusu nia ya Kampuni yake kuwekeza katika uzalishaji wa umeme nchini, Tianhua alisema kuwa wangependa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) katika mradi huo ambapo NARI watawezesha masuala yote ya kiuchumi katika mradi.

  Vilevile, alisema kuwa lengo lao ni kuzalisha umeme kwa kutumia gesi kupitia teknolojia ijulikanayo kitaalam kama ‘combined cycle’.

  Akitoa mwongozo kuhusu maombi yaliyowasilishwa, Profesa Muhongo aliwataka wawekezaji hao kukutana na kuzungumza na TANESCO pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) ili kujadili kwa kina kuhusu mapendekezo husika na kwamba, iwapo maombi yao yatakubaliwa, ndani ya kipindi cha mwezi mmoja (Aprili 15 mwaka huu), NARI wanatakiwa wawe wamethibitisha iwapo watafanya uwekezaji huo ama la.

  “Muda tunaotoa kwa sasa si zaidi ya mwezi mmoja, hivyo ndani ya mwezi mmoja, iwapo maombi yenu yatakuwa yamekubaliwa, mtapaswa kuwa mmewasilisha jibu lenu.”

  Aidha, Waziri Muhongo aliwataka NARI kuwasilisha kwa TANESCO na EWURA mapendekezo mengine waliyowasilisha kwake kuhusu nia ya kuwekeza katika miradi ya umeme vijijini kwa kutumia teknolojia ya makontena maalumu pamoja na miradi ya umeme jua. Aliwataka kuzungumzia hayo katika kikao kilichopangwa kufanyika baina yao.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kushoto), akimsikiliza Meneja wa Kanda ya Ulaya na Afrika wa Kampuni ya NARI Group, Chen Chao wakati alipokutana na Ujumbe kutoka Kampuni hiyo hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo pamoja na Viongozi na Maofisa waandamizi wa Wizara. NARI wameonyesha nia kuwekeza katika uzalishaji umeme.
  Makamu Meneja Mkuu wa Kampuni ya NARI Group, Bao Tianhua (Kushoto), akimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia) zawadi ya picha ya mmoja wa miji maarufu ya China. Anayeshuhudia ni Meneja wa Kampuni hiyo kwa Kanda za Ulaya na Afrika, Chen Chao. Ujumbe kutoka Kampuni ya NARI Group ulikutana na Waziri Muhongo hivi karibuni Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam na kuonyesha nia ya kuwekeza katika uzalishaji wa umeme.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa pili – kushoto), akizungumza jambo na Meneja wa Kampuni ya NARI Group kutoka China, Chen Chao (Kulia) mara baada ya kikao baina yao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ambapo walionesha nia ya kuwekeza katika uzalishaji wa umeme.

  0 0  0 0

  Could I be totally honest with you?
  Now is the great time to build wealth and fortune in Tanzania’s gas by taking advantages of opportunities brought about by weak oil price
  Yes, if you don’t act now, you are missing huge opportunities and you’ll hate yourself in the future.

  While many people are worrying about bad oil price, is the excellent opportunities to tap  opportunity in gas business and reap reward from it
  With a Stock market crash, people lose jobs and oil firms shut down projects.
  One might think I have lost my marble when I say now is the best time to launch gas business.

  Right, I know it sounds crazy, but it’s true.
  let’s dive in and you’ll see why you must go into gas business right now.
  Angel investors want to fund you
  In these tough times, investors find alternative sources of income, They look for new possibilities to make a living. Investors move out money from the stock market and they will subsidize you if your prospects are promising

  Gas industries need Innovation
  And when I say innovation is anything running from technology, material or procedure. Not necessarily to bring new products in oil market you can improve the existing one.Have a technology that will help operation run better and safer?
  Do you have an idea that will help to deliver a product better, cheaper and quicker? In this time of low price, Oil firm will pay attention to you than usual.

  Oil and gas companies want to save money
  At this moment, Clients are stressing over their cash. They are searching for less expensive options.
  Your capacity to offer quality products and solution at sensible costs. You’ll draw in numerous clients and keep them when the prices show signs of improvement
  Most Talented Tanzanians are Looking for new jobs
  Finding highly qualified employees is overwhelmed task. But in response to low oil prices, experienced engineers have got laid off.
  Many fresh graduates struggling with tightening jobs market and More Accountants are looking for next positions. Think what would happen if you launch oil and gas business right now? You find the right staff.

  Low Competition
  At the point oil prices are great, everyone wants to start the gas business in the hope of instant gratification. But under the current atmosphere, many Tanzanians have less certainty to get into the new gas venture.
  And they have less access to finance. As long as you have fund it is the perfect time to start gas business

  Many companies are looking for new partnership
  It troublesome for stand all alone, oil companies search for new organizations that have distinctive approaches to convey items and solution to unite and adjust the low prices
  Other segments of oil industry are booming
  Downstream sector of the oil industry is booming and benefit access to oil slump.They buy a lot of products and solutions.

  Are You Ready To act Now?
  In essence is rarely to encounter all of these opportunities when there are strong oil prices. Now is the better time to tap oil and gas business opportunities, If you procrastinate, You will hate yourself.
  Now go out and do it.

   Hussein Boffu
  Graduate In Petroleum Geoscience
  Hussein.Boffu@Tanzaniapetroleum.com
  0655 37 65 43

  0 0

  Benki ya NMB imetambulisha mkopo mpya kwaajili ya wanachama wapya wa mfuko wa pensheni wa LAPF, mkopo huu unaitwa Anza Maisha.

  Wanachama wapya wa LAPF watapata fursa ya mkopo wa kuanzia maisha kipindi ambacho bado hawana sifa za kupata mikopo ya maendeleo kupitia benki mbalimbali angalau kwa miezi sita ya mwanzo toka kuwa wanachama wa mfuko wa LAPF.

  Mkopo huo utatolewa na NMB kwa kushirikiana na LAPF ambapo sifa ya kwanza ya kupata mkopo huu ni kuwa na akaunti ya NMB pamoja na kuwa mwanachama wa mfuko wa LAPF na mwanachama awe ameshachangia angalau mara tatu (miezi mitatu).

  NMB imetambua changamoto ambazo mfanyakazi anazipata pale tu anapoanza kazi mpya hivyo mkopo wa Anza Maisha utawanufaisha wanachama wa mfuko wa LAPF kujiendeleza pale walipokwama kwasababu ya kukosa fedha za kuanzia maisha.

  Mkopo wa Anza Maisha ulitambulishwa rasmi kwenye mkutano mkuu wa 8 wa mwaka wa wanachama wa LAPF uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.
  Kaimu afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja Wadogo (Chief Retail Banking) - Abdulmajid Nsekela akitoa wasilisho juu ya huduma mbali mbali zitolewazo na NMB kwa wateja kutoka kwenye taasisi katika mkutano mkuu wa 8 wa Mwaka wa wanachama wa mfuko wa LAPF jijini Arusha.

  0 0

  Kamanda wa Polisi Wilaya ya ilemala , Sweetbert Kisha akikata utembe kuzindua duka jipya la Airtel Airtel lililopo ndani ya Rockcity shopping Mall jijini Mwanza, akishuhudia Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel, Adriana Lyamba.
  Kamanda wa Polisi Wilaya ya ilemala , Sweetbert Kisha na Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel, Adriana Lyamba wakikata keki kwa pamoja wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel lililopo ndani ya Rockcity shopping Mall jijini Mwanza, akishuhudia (kuli) ni wakala Mkuu wa Airtel Money Mwanza, Mohamed Gichani.
  Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel, Adriana Lyamba akitoa maelezo kwa Kamanda wa Polisi Wilaya ya ilemala , Sweetbert Kisha kuhusu huduma ya Airtel Money inayotelewa katika duka jipya la Airtel wakati uzinduzi wa duka jipya la Airtel lililopo ndani ya Rockcity shopping Mall jijini Mwanza.


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam CCM, Ramadhan Madabida, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Nishati na Madini Dkt. Juliana Palangyo wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka Meneja wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi I Mhandisi John Mageni kuhusu utendaji kazi wa kituo hicho.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa Japan Nchini Masaharu Yoshida, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda , Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi  wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini mama mmoja alijitokeza kumpongeza kutokana na utendaji kazi mzuri wa Serikali yake ya awamu ya tano mara baada ya uzinduzi rasmi ujenzi wa wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

  0 0


  0 0


  0 0
 • 03/16/16--13:30: Article 21


older | 1 | .... | 1160 | 1161 | (Page 1162) | 1163 | 1164 | .... | 3348 | newer