Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

GSM FOUNDATION YAIPIGA JEKI TIMU YA TAIFA YA RIADHA ILIYOKO KAMBINI WEST KILIMANJARO

$
0
0
 Kocha wa timu ya taifa ya riadha Fracis John (kulia) akiwa na wanariadha wanaounda timu ya taifa ya riadha wakitizama msaada wa Track Suit ulitolewa na GSM Foundation kwa ajili ya wanariadha hao. 
 Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akitizama msaada wa track suit zilizotolewa na kampuni ya GSM Foundation. 

 Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akikabidhi msaada wa track Suit zilizotolewa na GSM Foundation . 


HAWA NDIO WALIOWAHI KUWA WAKUU WA MKOA WA IRINGA KUANZIA MWAKA 1964 MPAKA HIVI SASA

Airtel FURSA yaingia Dodoma yatoa msaada wa shs milioni 9

$
0
0
Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA umeendelea na utekelezaji wa  ahadi yake ya kuwawezesha wajasiliamali wawili kila wiki nchini kwa kutoa misaada yenye thamani ya hadi shilingi milioni 10 kwa kikundi au kijana atakaeotoa mchanganuo na kusimamia biashara itakayoweza kusaidia kuongezea kipato na kupunguza umasikini katika jamii .

Wiki hii Airtel FURSA imeingia mkoani Dodoma na kukabidhi vitendea kazi vyenye dhamani ya shilingi milioni 9 kwa  kijana mjasiliamali Fikiri Chinji anaeishi katika kijiji cha Ng”ong”ona ili aweze kuendeleza shughuli zake za useremala na kuweza kuajiri vijana wengine wanaomzunguka.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano katika kijiji cha Ng”ong”ona Dodoma  Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Dangio Kaniki alisema “vifaa alivyoomba ndio tunavyomkabidhi ni pamoja na mashine yakupiga msasa, mashine kwaajili ya kutobolea na kutengeneza urembo pamoja na nyingine yakuranda mbao. Pia tumejenga kalakana yake hapa kijijini ili apate mazingira mazuri ya kufanyia kazi zake kwa ustadi  na kufundisha vijana wengine kujiajiri kupitia mradi huu”

“Airtel Fursa tumeona ni muhimu kumuwezesha kijana huyu  aweze pia kuongeza thamani ya vitu anavyotengeneza na  kuviuza kwa bei nzuri, vile vile tumejipanga kuja tena Dodoma hivi karibuni na tutasaidia kikundi cha ujasiliamali kiitwacho PAMBANA cha Dodoma Mjini chenye jumla ya vijana 30 ambapo wasichana ni 20 na wavulana 10 na kinajishughulisha na usafi wa mazingira na kutengeneza sabuni” alieleza Dangio
  
Akipokea Vifaa hivyo huku akishangiliwa na wanakijiji wenzake, kijana Fikiri  ameishukuru Airtel fursa kwa kuona umuhimu wa  kumpiga jeki kwa kumwezesha vifaa na sehemu ya kufanyia shughuli zake,

“Sasa nitafanya kazi zangu kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na kutengeneza bidhaa zitakazokubalika sokoni, naishukuru sana Airtel Fursa kwa kunishika mkono” Alisema Fikiri

Mradi wa Airtel FURSA uko katika msimu wa pili ambapo tokea kuanzishwa kwake umefanikiwa kuandaa na kufanya semina za ujasiliamali 17 na kukutana na vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 zaidi ya 3000, pia hadi sasa imeweza kutoa misaada kwa vijana na makundi ya vijana  hao wajasiliamali zaidi ya  108 kwa lengo kuwaongezea uzalishaji na kipato.
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (katikati), akijaribisha moja ya mashine mashine walizomkabidhi kijana Fikiri Chinji (kushoto), anayejishughulisha na ufundi seremala, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye karakana yake iliyojengwa na Airtel katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma mwishoni mwa wiki hii. Anayeshuhudia (kulia) ni Meneja mauzo manispaa ya Dododma Hendrick Bruno.
Kijana Fikiri Chinji anayejishughulisha na ufundi seremala, akionyesha jinsi mashine yake mpya aliyokabidhiwa na Airtel Tanzania, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, inavyofanyakazi katika hafla fupi iliyofanyika kwenye karakana yake iliyojengwa na Airtel katika Mtaa wa Ng’ong’o na manispaa Dodoma mwishoni mwa wiki hii. Anayeshuhudia ni Meneja masoko manispaa ya Dodoma Saidimu Ngalesoni (kulia) akifuatiwa na Meneja mauzo manispaa ya Dodoma, Hendrick Bruno (wa pili kulia)
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa nne kulia), akimkabidhi kijana Fikiri Chinji (wa tano kushoto), anayejishughulisha na ufundi seremala, msaada wa vifaa mbali mbali vya ufundi na kujengewa karakana mpya kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye karakana yake iliyojengwa na Airtel katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma mwishoni mwa wiki hii. Wanaoshuhudia ni wanakijiji wa Ng’ong’ona na wafanyakazi wa Airtel waliofika kushuhudia tukio hilo.
Wanakijiji wa Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma wakiangalia banda alilokabidhiwa Kijana Fikiri Chinji (hayupo pichani) anayejishughulisha na ufundi seremala, pamoja na msaada wa vifaa mbali mbali vya ufundi kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, mwishoni mwa wiki hii.

BEI YA MADAFU LEO

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKABIDHIWA TUNZO YA MSANII BORA AFRIKA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wasanii wa Film wa hapa Nchini baada ya kukabidhiwa Tunzo ya mshindi Bora wa Film ya Kiswahili East Afrika (AMVCA) na Tunzo ya Kiswahili Afrika iliyofanyika Nchini Nigeria, hafla hiyo iliyofanyika leo March 14,2016 Oysterbay Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Tunzo ya mshindi Bora wa Film ya Kiswahili East Afrika (AMVCA) iliyofanyika Nchini Nigeria kutoka kwa mshindi wa Film hiyo Msanii Elizabeth Michael (Lulu) wakati wa hafla fupi iliyofanyika Oysterbay Dar es salaam leo March 14,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Tunzo ya mshindi Bora wa Film ya Kiswahili Afrika iliyofanyika Nchini Nigeria kutoka kwa mshindi wa Film hiyo Msanii Single Mtambalike (RICHIE) wakati wa hafla fupi iliyofanyika Oysterbay Dar es salaam leo March 14,2016.

MWAKYEMBE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UNICEF

$
0
0
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) Bi. Maniza Zaman akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipomtembelea ofisini kwake mapema leo (14/3/2016) jijini Dar Es Salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Bi. Maniza Zaman alipomtembelea ofisini kwake leo (14/3/2016) jijini Dar Es Salaam.

WAZIRI NAPE NNAUYE KUFUNGUA KIKAO CHA KAZI CHA MAAFISA HABARI WA SERIKALI LEO MKOANI MOROGORO.

$
0
0
Maafisa habari na Mawasiliano Serikalini wakijitambulisha muda huu mbele ya Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo mhe Nape Nnauye ambae atafungua kikao chao cha kazi cha mwaka ukumbi wa VETA Morogoro.

BAKITA yampongeza Rais Dkt. Magufuli kwa matumizi ya Lugha ya Kiswahili.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA), Prof.Martha Qorro(Kulia) akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari ambapo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa uzalendo wake wa kuitumia lugha ya Kiswahili katika mikutano mikubwa ya kitaifa ikiwemo mkutano wa 17 wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki , katikati ni Katibu Mtendaji wa BAKITA Dkt. Seleman Sewangi na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bi.Lorietha Laurence.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA),Dkt. Seleman Sewangi akionyesha kamusi Kuu  ya Kiswahili kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa uzalendo wake wa kuitumia lugha ya Kiswahili katika mikutano mikubwa ya kitaifa ukiwemo mkutano wa 17 wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,katikati  ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Kiswahili la Taifa(BAKITA), Prof.Martha Qorro na kulia ni wake Mkurugenzi,Taasisi ya Taaluma za Kiswahili chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Ernesta Mosha .(Picha na Eliphace Marwa-maelezo).


Na Lorietha Laurence-Maelezo.

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli kwa uzalendo wake wa kuitumia lugha ya Kiswahili katika mikutano mikubwa na hafla mbalimbali za kitaifa na kimataifa.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi BAKITA, Prof. Martha Qorro ameeleza msimamo huo wa Rais Dkt.Magufuli  umewasidia Watanzania kupata taarifa moja kwa moja kutoka tukio husika.

“Uamuzi na msimamo wa Rais Magufuli wa kutumia lugha ya Kiswahili katika mikutano mikubwa ikiwemo  mkutano mkuu wa 17 wa viongozi wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umepokelewa kwa furaha kubwa na wananchi na wadau wengi wa Kiswahili ndani na nje ya Tanzania” alisema Prof.Martha.

Aliongeza kuwa kupitia msimamo huo wa Mhe. Rais Magufuli,   Baraza linaamini kwamba hatua hiyo itasaidia kukuza lugha ya Kiswahili na kutoa fursa ya ajira kwa Watanzania kupitia tafsiri na ukalimani na hivyo kuwapelekea maendeleo wananchi wote wa Afrika Mashariki.

Naye Katibu Mtendaji wa BAKITA Dkt. Seleman Sewangi ametoa wito kwa viongozi wengine wa ngazi mbalimbali za Kitaifa kufuata nyao za Mhe.Rais Magufuli kwa kuipa kipaumbele lugha ya Kiswahili ili kufikisha ujumbe kwa Watanzania walio wengi.

“Natoa wito kwa viongozi wetu wa ngazi mbalimbali za kitaifa kuitumia lugha ya Kiswahili katika mikutano mikubwa na hafla mbalimbali za kitaifa na kuachana na dhana ya kutumia lugha ya kigeni yenye lengo la kuwafurahisha wageni wachache” alisema Dkt. Sewangi.

Aidha, aliongeza kuwa katika kuhakikisha kuwa lugha ya kiswahili inatumiwa vizuri, Baraza hilo linaendelea kutekeleza mkakati wa kukamilisha kanuni zitakazopelekwa bungeni ili kumuwezesha Waziri mwenye dhamana kuwa na mamlaka ya kusimamia sheria ya lugha ya Kiswahili ya mwaka 1961 iliyorekebishwa mwaka 1985 ili kuipa nguvu ya kumshitaki mtu yeyote kwa matumizi mabaya ya lugha hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi,Taasisi ya Taaluma za Kiswahili chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Ernesta Mosha ameziomba ofisi za Serikali hususani mahakama kutumia lugha ya Kiswahili kwa kuwa ni lugha inayoeleweka na Watanzania wengi ikizingatiwa kuwa sio wote wanajua kutumia lugha ya kiingereza.
 


NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT KIGWANGALLA AZINDUA KONGAMANO LA TATU LA WANASAYANSI WA UGONJWA WA KISUKARI LEO JIJINI DAR

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Dkt Hamisi Kigwangalla katika ufunguzi wa Kongamano la tatu la Kisanyansi na Utafiti wa ugonjwa wa kisukari Africa, lililozinduliwa leo katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC),Kongamano hilo ambalo litamalizika tarehe 16 March 2016, linaendeshwa na Asasi inayojihusisha na Masuala ya Ugonjwa wa kisukari Afika Mashariki na Kusini,asasi inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica diabetes study group.Asas hii ilianzishwa mwaka 2011 ili kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa huo na kuutafiti pamoja na kutafuta tiba.Kushoto kwake ni Mratibu wa Kongamano hilo Doctor Kaushik Ramaiya,na baadhi ya wageni kutoka Mfuko wa kusaidia Kisukari Duniani (NCD Symposium),kutoka Denmark.
 
Kongamano la tatu la Wanasanyansi wa ugonjwa wa kisukari limezinduliwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Dkt Hamisi Kigwangalla katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere (JNICC)

Kongamano hilo ambalo litamalizika tarehe 16 March 2016, linaendeshwa na Asasi inayojihusisha na Masuala ya Ugonjwa wa kisukari Afika Mashariki,asasi inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica diabetes study group.Asas hii ilianzishwa mwaka 2011 ili kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa huo na kuutafiti pamoja na kutafuta tiba.

Akiongea na waandishi wa Habari, Mratibu wa Kongamano hilo Doctor Kaushik Ramalya, Kongamano hilo limekaribisha wageni kutoka nchi nyingine za Afrika ya Mashariki na kusini kushiriki katika majadiliano na uchunguzi huo wa Kisayansi, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa namana ya kutua matatizo yatokanayo na ugonjwa huo.

Alisema kongamano hilo ambalo linahusisha East African Diabetes study Group (EADSG) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, litafuatiwa na mkutano Maalum wa wadau wa kisukari duniani utakaofanyika, Machi 17 hadi 18 2016 katika ukumbi huo huo wa Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar Es Salaam, Tanzania.

Mkutano huo ulioandaliwa na Mfuko wa kusaidia Kisukari Duniani (NCD Symposium),kutoka Denmark kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto nchini Tanzania, pamoja na Shirika la Afya Duniani Ofisi za Mikoa kwa Afrika pamoja na Shirikisho la Kisukari duniani utajadili mambo mbali kuhusu namna ya kusaidia wagonjwa wa ishio na Kisukari kwa kuwa gharama zake ni kubwa mno.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SUBASH PATEL WA M.M.I STEEL AMKABIDHI MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, MABATI YENYE THAMANI YA SH.MILIONI 200 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel (wa pili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (wa kwanza kushoto), mabati yenye thamni ya sh.milioni 200 Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule mbalimbali jijini Dar es Salaam. Wengine wanaoshuhudia makabidhiano hayo kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa M.M.I Steel, S.K. Modi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Issaya, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymund Mushi na kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, 
 Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel (kulia), akizungumza katika makabidhiano hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik (katikati), akitoa shukurani kwa msaada huo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumuzia changamoto ya madarasa katika wilaya yake.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akitoa shukurani baada ya kupokea msaada huo.

Picha ya pamoja baada ya makabidhiano.

Na Dotto Mwaibale
UMOJA wa Viwanda vinavyoshughulika na utengenezaji wa vifaa vya ujenzi nchini umemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mabati yenye thamani ya sh.milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi msaada huo Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa M.M.I Steel, Subash Patel alisema waliguswa mno na changamoto hiyo inayowakabili wanafunzi ndio maana akawaomba wenzake wasaidie.
"Kampuni yangu imetoa vifaa vyenye thamani ya sh. milioni 100 na Kampuni ya Ujenzi ya Estim imetoa sh.milioni 50 wakati Export Trading imetoa sh. milioni 50" alisema Patel.
Patel alitumia fursa hiyo kuyaomba makampuni mengine kujitoa kusaidia shughuli za maendeleo nchini hasa katika sekta ya elimu yenye changamoto za uhaba wa madarasa na madawati.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadik amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya vyumba vya madarasa jijini Dar es Salaam hasa katika Wilaya ya Temeke na Ilala ambapo katika shule moja kuna zaidi ya wanafunzi kuanzia 3000 hadi 5000.
Sadiki alisema msaada huo utasaidia kupunguza changamoto hiyo katika jiji la Dar es Salaam.
Hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo ilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema,  Ilala, Raymond Mushi na Mkurugenzi wake.

HARAMBEE YA KUMCHANGIA MDAU MARIAM HUSSEIN YAFANYIKA DMV

$
0
0
Mariamu Hussein akihudhuria harambe ya kumchangia iliyofanyika siku ya Jumamosi Silver Spring, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na WanaDMV na marafiki zao. Mariam Hussein anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani.


Vitu mbalimbali vilivyoletwa na WanaDMV kwa ajili ya kuvipiga mnada kwenye harambee iliyofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.

WanaDMV na marafiki zao waliohudhuria harambee ya Mariam Hussein (wanne toka kushoto) iliyofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.
Mariam Hussein (kati) akiwa na familia yake kwenye harambee ya kumchangia fedha za matibabu ya saratani iliyofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016
Mnada ukiendelea 

WAZIRI Mkuu Majaliwa atembelea Kambi ya utenganisho ya wakimbizi ya Mwisa inayosimamiwa na Jeshi la Magereza

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(MB) alipotembelea Kambi Maalum ya Mwisa inayohifadhi Wakimbizi kutoka nchini Burundi leo Machi 14, 2016. 
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(MB)akitoa hotuba yake fupi kwa Maafisa na askari wa  wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kutoka vituo mbalimbali vya Magereza yaliyopo Mkoa wa Kagera alipotembelea Kambi ya Utenganisho ya Mwisa leo Machi 14, 2016.
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini mkubwa hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(hayupo pichani).
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni akitoa neno fupi kabla ya kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kutoa hotuba yake fupi.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa taarifa fupi ya Hali ya Magereza nchini mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(hayupo pichani).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiongea na Wakimbizi(walioketi chini) katika Kambi ya Mwisa inayosimamiwa na Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Shirika la kuwahudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR). 
Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

AFISA MIFUGO ANUSURIKA KUTUMBULIWA JIPU NA WAZIRI MKUU

$
0
0
AFISA MIFUGO wa kata ya Kakunyu, wilayani Misenyi mkoani Kagera, Bw. Eric Kagoro amenusurika kutumbuliwa jipu kwenye mkutano wa hadhara kuhusiana na sakata la kuruhusu ng'ombe 291 waje kulishwa kwenye ranchi ya mifugo ya Misenyi. 
 Tukio hilo limetokea leo mchana (Jumatatu, Machi 14, 2016) wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na mamia ya wananchi waishio jirani na ranchi hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye makao makuu ya ranchi hiyo. 
 Waziri Mkuu alimuibua Bw. Kagoro katikati ya mkutano kwa kumtaja jina na tuhuma zinazomhusu kuhusu mifugo iliyokamatwa. "Afisa Mifugo wa kata yupo hapa? Aliuliza Waziri Mkuu. Wewe ndiyo Eric?" 
Alipojibu ndiyo akaulizwa tena:"Nimekujuaje?""Nimeambiwa wale ng'ombe waliokamatwa ni wa rafiki yako na wewe ndiye ulitoa libali waje kulishwa kwenye ranchi hii. Siyo kazi yako kuruhusu mifugo ya nje ije kulishwa hapa kwenye ranchi. Kuanzia sasa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingiza mifugo kwenye ranchi ili ipate malisho " 
 "Leo Nimekusamehe .Kazi yako ni kuhakikisha mifugo ya kwenye kata hii iko salama. Kazi yako ni kuwasaidia wafugaji wa kata hii wafuge vizuri na uhakikishe mifugo yao inakuwa na tija." alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa. 
 Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaasa watendaji wa kata na vijiji kutotumia nafasi zao kuleta migogoro baina ya watu wa nje na wananchi wanaowaongoza. "Mwenyekiti wa kijiji huna ruhusa ya kugawa kitalu cha ranchi au kuruhusu mtu yeyote akalime ndani ya ranchi", alisema. 
 Aliwataka pia maafisa uhamiaji wawe makini na vyeti vya kuandikisha uraia wanavyovitoa kwa wananchi wanaoishi mipakani kwani imekuwa ni mianya ya kuleta migogoro ya ardhi. "Watu wa uhamiaji kuweni makini na CN mnazotoa (CN=Certificate of Naturalisation). 
Wote wanaoomba CN wanataka blocks tu" Alitoa agizo kuwa watafutwe watu wote walioingia nchini kwa mgongo wa CN, wakamatwe na kurejeshwa makwao. 
"Kuna watu wamekuja hapa nchini wakaomba CN lakini wakikaa wanaleta wenzao waje kununua ardhi kwa kutumia mgongo wa CN zao." 
 Alisema kuna watu wametoja wilaya ya Karagwe ambako pia kuna tatizo kama la Misenyi na kuwataka wahusika wajiandae kuchujwa na kuchukuliwa ardhi zao kama watakuwa hawajaziendeleza ili wapewe Watanzania wenye uhitaji wa kulima na kufuga.

Ujumbe wa JWTZ watembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC

$
0
0
Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC alikutana na Ujumbe wa JWTZ ulioongozwa na Mkuu wa Tiba Jeshini, Brigedia Jenerali (Dkt.) Denis Raphael Janga, aliyekuwa amefuatana na Mkuu wa Chuo cha Kijeshi cha Tiba - Lugalo, Brigedia Jenerali (Dkt) Robinson Mboni Mwanjela. 
Wengine ni Mkurugenzi wa Kinga Jeshini, Luteni Kanali Charles Emilio Mwanziva pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wauguzi, Luteni Kanali Lawrence Tia Banda. Ujumbe huo ulikwa na ziara ya Kikazi ya wiki moja hapa Marekani, katika kuendeleza mahusiano baina na JWTZ na majeshi ya Marekani.
 Pichani kutoka kushoto: Col. Adolph Mutta (DA), Brig. Gen. (Dkt) Denis R. Janga, Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi, Brig. Gen. (Dkt) Robinson M. Mwanjela, Lt. Col. (Dkt) Charles E. Mwanziva na Lt. Col. Lawerence T. Banda

MSAGA SUMU NDANI YA DANGA CHEE YA MICHUZI TV


TEASER JOTO LA ASUBUHI JUMANNE MARCH 15, 2016

Kampuni ya Total yamhakikishia Rais Magufuli ujenzi wa bomba la mafuta haraka iwezekanvyo

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki,    Javier  Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa wajumbe walioambatana na  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki,    Javier  Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki,    Javier  Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki,    Javier  Rielo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki,    Javier  Rielo  aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU.

Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo amemuhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha Mafuta kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga hapa Tanzania haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.
Bw. Javier Rielo ametoa ahadi hiyo leo tarehe 14 Machi, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam.Mradi huo utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga na utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.
Katika Mazungumzo hayo Bw. Javier amemueleza Rais Magufuli kuwa Kampuni yake inatarajia kutumia dola za kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari zimeshaandaliwa.Pamoja na kuukaribisha uwekezaji huo mkubwa kwa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka kampuni hiyo kuharakisha mchakato wa kuanza kwa mradi, na ameshauri muda wa miaka mitatu uliopangwa kuukamilisha mradi huo upunguzwe, ili manufaa yake yaanze kupatikana mapema.
Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, amesema Wizara yake ipo tayari kuhakikisha mradi huo unafanikiwa, na itatoa ushirikiano wa kutosha kuharakisha utekelezaji wake.

Prof. Muhongo amebainisha kuwa licha ya kwamba hali ya kijiografia, hali ya hewa na bandari ya Tanga vinatoa mazingira bora ya kufanikiwa kwa mradi huo, Tanzania pia inatarajia kunufaika na bomba hilo, kwa kuwa kuna tafiti mbili za mafuta zinazoendelea katika ziwa Tanganyika na katikati mwa Tanzania, ambazo zikikamilika kwa mafanikio inatarajiwa bomba hilo litasaidia kusafirisha mafuta yake.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
14 Machi, 2016.

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: Sifai - Q Jay ft Joslin

KUMBUKUMBU YA STEPHEN JONATHAN STEPHEN

$
0
0
Leo tarehe 15 Machi 2016 ni miaka 16 tangu utwaliwe kutoka duniani. 

Tulikupenda sana kaka na bado tunakumbuka uchangamfu wako, utani na kutoa msaada wako kwetu bila kuchoka.

Unakumbukwa na dada zako, wajomba, baba, jamaa na rafiki zako.

Tunaamini ya kuwa kimwili hauko nasi ila kiroho tuko pamoja tukitegemea kuwa siku moja tutajaonana.

Tutaendeleza yale uliyokuwa ukiyafanya wakati wa uhai wako.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihidimiiwe.

MAKALA YA SHERIA: KUENDELEZA SHAURI ALILOACHA MAREHEMU ILI KUPATA ALICHOKUWA AKIDAI

$
0
0
Na Bashir Yakub. 

 Makala haya yanaeleza wakati ambapo ndugu anafariki huku akiacha shauri mahakamani ambalo alikuwa akidai kitu fulani kama haki yake. Yaweza kuwa alifungua kesi kudai ardhi, nyumba, mirathi, mgogoro wa kimkataba, fidia, na madai mengine yote. 

Makala yatatizama uwezekano wa ndugu kuendeleza madai haya ili kuona namna ya kupata kile alichokuwa akidai marehemu. 

 1.ISEMAVYO SHERIA. 

Amri ya 22 kanuni ya 1 – 12 Sheria ya mwenendo wa mashauri ya madai ndiyo inayozungumzia jambo hili. Katika kanuni hizo si tu imezungumzwa haki ya marehemu mlalamikaji bali pia haki ya marehemu mlalamikiwa/mdaiwa. 

 Kanuni ya 1 inasema kuwa kifo cha mlalamikaji/mdai au mlalamikiwa/mdaiwa hakiui shauri ikiwa haki ya kulalamika bado haijafa. Maana yake ni kuwa kuna wakati mdai anakufa lakini haki yake ya kuendelea kudai alichokuwa akidai inaendelea kuishi na kuna wakati akifa anakufa na haki yake ya kudai. Ni wakati gani akifa anakufa na haki yake ya kudai na ni wakati gani akifa haki yake inaendelea kuishi tutaona hapa chini. 

2. KUENDELEA KUISHI KWA HAKI YA MADAI NA KUFA KWA HAKI YA MADAI. 

Kuendelea kuishi kwa haki ya madai maana yake ni kuwa ndugu wa marehemu hasa msimamizi wa mirathi anapata haki ya kuendeleza shauri na kudai kilekile alichokuwa akidai marehemu. Na kufa kwa haki hiyo maana yake ni kuwa hakuna ndugu yoyote kutoka upande wa marehemu akiwemo msimamizi wa mirathi atayekuwa na haki ya kudai au kuendeleza shauri ili kupata kile alichokuwa akidai marehemu. 

 Hali ni hiyohiyo kwa upande wa mlalamikiwa/mdaiwa aliyefariki. Kwani kuna wakati ndugu watalazimika kurithi shauri ambalo alikuwa ameshitakiwa nalo na kuna wakati hawatalazimika.

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images