Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1159 | 1160 | (Page 1161) | 1162 | 1163 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shehena ya sukari wakati alipotembelea ghala la kiwanda cha Sukari cha Kagera akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mpaka kati ya Tanzania na Uganda kwenye Ranchi ya Missenyi mkoani Kagera Machi 14, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi,Festo Kiswaga.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Uganda waishio kwenye mpakani waliovuka mpaka ili kumuona wakati alipotembelea kijiji cha Benkoma wialyani Missenyi akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kudhibiti uagizaji wa sukari kutoka nje ili kulinda soko la ndani.

  Ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Machi 14, 2016) wakati akizungumza na uongozi wa kiwanda cha sukari cha Kagera pamoja na uongozi wa mkoa wa Kagera alipotembelea kiwanda hicho ambapo alisema wamezuia sukari kutoka nje ili kuhakikisha sukari inaisha katika maghala yao.

  Akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Kagera, Waziri Mkuu ameviagiza viwanda kuzalisha sukari nchini vizalishe sukari ya kutosha ili kukidhi mahitaji ya soko.

  Alisema mahitaji halisi ya sukari hapa nchini ni tani 420,000 huku uwezo wa viwanda vya ndani ni kuzalisha tani 300,000 hivyo alitoa wito kwa viwanda hivyo kuongeza uzalishaji.

  "Tunahitaji viwanda vya ndani vizalishe sukari ya kutosha na mahitaji yawe yamefikiwa kama tulivyokubaliana, lengo ni kuzuia uagizaji wa sukari kutoka nje ambao ukiendelea utavivuruga viwanda vya ndani," alisema.

  Pia alivitaka viwanda hivyo viwe vimefikia malengo ya kuzalisha sukari ya kutosha katika kipindi cha kuanzia miaka mitatu hadi minne kama walivyokubaliana katika kikao cha wadau wa sukari nchini kilichofanyika hivi karibuni.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika mashamba ya miwa, ununuzi wa mitambo pamoja na kuajiri idadi kubwa ya watumishi ambao ni Watanzania.

  Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Ash Rana alisema kwa sasa wanazalisha tani 60,000 za sukari na kwamba wana lengo la kuzalisha tani 120,000 katika kipindi cha miaka minne ijayo.

  Alisema uzalishaji wa sukari kiwandani hapo umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo mwaka wa fedha wa 2011/2012 walizalisha tani 35,362 na mwaka 2015/2016 wamezalisha tani 60,000.

  Ofisa huyo aliiomba Serikali ipunguze riba ya mikopo ya kwenye uwekezaji wa sekta ya kilimo ambapo kwa sasa wanatozwa asilimia 20 kiwango ambacho alisema ni kikubwa sana.

  Alisema wana mipango ya kukiboresha na kukipanua zaidi kiwanda hicho na hivi sasa wako katika hatua za mwisho za kupata mkopo wa Dola za Marekani milioni 68 ambao kati ya hizo, dola milioni 10 zitapelewa katika uboreshaji wa umwagiliaji na zilizobaki katika kuimarisha miundombinu ya kiwanda hicho.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu ( Mb) akitoa hutuba kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW).Mkutano huu wa wiki mbili unawakusanya wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia ambapo hujadiliana na kubalishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua mbalimbali ambazo serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya mwanamke na mtoto wa kike.
  Waziri wa Malawi akimpongeza Waziri Ummy Mwalimu mara baada ya hotuba yake aliyoitoa kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika.
  Mhe. Waziri Mwalimu akichangia majadiliano ya Mawaziri yaliyofanyika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni kuhusu hali ya Wanawake. Majadiliano hayo ya Mawaziri yalihusu uimarishaji wa mfumo ya kisheria na kisera kwaajili na utekelezaji wa usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake.
  Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huo.

  BOFYA HAPA KUSOMA HABARI KAMILI

  0 0

   
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga akimsikiliza Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jassem Alnajem wakati alipomtembelea ofisini kwake Machi 14, 2016. ambapo aliahidi nchi yake kuimarisha zaidi uhusiano na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga akimuelezea Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jassem Alnajem kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara hiyo wakati balozi huyo alipomtembelea Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Machi 14, 2016..
  Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jassem Alnajem akimkabidhi zawadi ya kumbukumbu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga wakati balozi huyo alipomtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake Machi 14, 2016.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jassem Alnajem wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Kitwanga ofisini kwake leo. Kulia ni Mwambata wa Ubalozi huo hapa nchini Bw. Mishal Achamidi.

  0 0


  0 0

  Ikiwa ni tunzo ya 4 tangu kuanza kwa zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi ambapo zoezi hili lilianzishwa mwezi Septemba, 2015 likiwa na dhumuni la kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri.

  Mshambuliaji Ibrahim Ajibu ameshinda kwa mara ya pili tuzo ya mchezaji bora mwezi Januari, 2016 baada ya kupigiwa kura kwa wingi na wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba na soka la Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News pamoja na kwenye mitandao rasmi ya kijamii ya Simba.

  Facebook www.facebook.com/simbatanzania Twitter na Instagram @simbasctanzania.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Rais wa Simba Evans Aveva amesema, “sisi kama uongozi wa klabu yetu ya Simba tunaamini katika kuwapa motisha

  wachezaji wetu kila iitwapo leo na hii ni katika kuongeza chachu ya maendeleo si tu kwa mchezaji bali kwa klabu nzima kwa ujumla, Ajib anashinda tunzo hii kwa mara ya pili mfululizo. Wote mtakubaliana nami kuwa kwa kiwango anachoonesha mshambuliaji Ajib ni kweli mshabiki, wanachama na wapenzi wa Simba hawajakosea kumchagua tena mchezaji huyu”Napenda kutoa wito kwa wachezaji wetu wote kuendelea kujituma zaidi kwani mashabiki wao wakiongozwa na uongozi mzima tunamatumaini makubwa msimu huu 2015/2016, tukiamini kwenye falsafa yetu ya SIMBA NGUVU MOJA, aliongeza Rais Evans Aveva.

  Akizungumza na simbasports.co.tz Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Imani Kajula amesema, “EAG Group inapenda kusisitiza kuendelea kuongeza utayari wake katika kushirikiana na klabu ya Simba kwenye kutoa motisha kwa wachezaji wa Simba ambapo italeta chachu ya kufanya vizuri zaidi na hivyo kuweza kutengeneza mfumo mzuri wa kuongeza vyanzo vya mapato na hatimaye faida kubwa kwa wachezaji na timu kwa ujumla”.

  Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba. Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 kisha utaletewa ujumbe jibu kwa kutuma neno “OK” na hapo utakuwa umejiunga rasmi, Huduma hii ni maalum kwa Tigo na Vodacom.

  0 0

  Serikali imewapongeza wadau kwa kutoa huduma za chanjo ya ugonjwa wa Kisukari ikiwemo kusaidia vijana wadogo wanaosomea masomo mbalimbali ya kisayansi hapa nchini.


  Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la tatu la ugonjwa wa Kisukari kwa nchi za Afrika Mashariki,Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla, amebainisha kuwa Serikali kupitia wizara hiyo ina mpango kabambe wa kuhakikisha inapambana na tatizo la ugonjwa wa Kisukari hapa nchini ambapo pia amewataka wadau wasichoke kushirikiana katika mapambano hayo.

  Aidha, amewapongeza vijana walio katika vyuo vikuu hapa nchini licha ya kupata tiba ya ugonjwa wa Kisukari, lakini kwa hali yao hiyo bado wana moyo wa kusoma kuhakikisha wanafika mbali hivyo Serikali inajisikia faraja na kuwataka wadau kuwa na moyo huo huo wa kusaidiana na Serikali.
  Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba maalum ya uzinduzi wa kongamano hilo 
  Kwa upande wao baadhi ya washiriki wakiwemo vijana wanafunzi na wengine wakiwemo waliotoa igizo namna ya ugonjwa Kisukari jamii unavyouweka kando, wameeleza kuwa kitendo cha dozi ya Kisukari kuuzwa kinawapa shida watu wengi kwani wapo wanaopoteza maisha kwa kukosa pesa za kutumikia dozi hiyo.

  Hata hivyo, walimuomba Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kuhakikisha Serikali wanaliangalia hilo ili dozi ya Kisukari yaani Insulini, ipatikane bure kwa watumiaji wake.

  Kongamano hilo lililozinduliwa jana Machi 14.2016, ni la siku tatu na linatarajiwa kufikia tamati, kesho Machi 16.2016. Ambapo linajumlisha wataalaam wa utafiti wanasayansi katika ugonjwa wa Kisukari ( pre – congress training – applied research in diebetes) na kuandaliwa na asasi inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica diabetes study group. 
  Baadhi ya wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu ambao ni wadau wakubwa katika mapambano dhidi ya Kisukari wakiwa tayari kutoa ujumbe kwa Serikali kuona namna ya kusaidia jamiii katika mapambano ya ugonjwa wa kisukari.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge akielekeza jambo kuhusu wavu uliowekwa kwa ajili ya kuzuia mashabiki wasirukie na kuharibu miundombinu katika maeneo ya vyoo vya uwanja wa Uhuru jana wakati wa kikao cha ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.
  Msanifu wa Majengo na mbunifu wa Mchoro wa Uwanja wa Taifa Aloyce Peter Mushi akifafanua jambo wakati wa kikao cha ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Bibi. Cecilia Kasongo, Mhandisi wa Uwanja wa Taifa Yusuf, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge, Muhandisi wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa Uhuru E. Mwamakunga na Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
  Meneja wa Ujenzi wa Kampuni ya BCEG inayojenga uwanja wa Uhuru Zhang Jiawei akifafanua jambo wakati wa kikao cha ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge, Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio, Msanifu wa Majengo na mbunifu wa Mchoro wa Uwanja wa Taifa Aloyce Peter Mushi Muhandisi wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa Uhuru E. Mwamakunga.


  0 0


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkulu akiongea na waaandishi jinsi alivyotapelewa shilingi milioni kumi na wezi wa mitandao.
  Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu akiwa anaonyesha ujumbe mfupia wa maneno ambao matapeli hao walikuwa wanatuma kwa watu

  Na Woinde Shizza ,Arusha.

  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu ameibiwa kiasi cha shilingi milioni 10 na wezi wa mtandao ambao waliteka mawasiliano yake ya simu za mkononi kwa muda wa saa 3 na kutumia namba hizo kuomba fedha kwa watu wa karibu na kiongozi huyo.

  Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake ,Nkulu amesema kuwa jana majira ya saa 10:00 alasiri simu zake zilikua hazipatikani hewani mpaka majira ya saa 3:00 usiku ndipo aliposhtuka na kuanza kufuatilia na kugundua kuwa mawasiliano yake yalitekwa kwa muda.

  Mkuu huyo wa Wilaya amelaani vitendo vya wizi wa mtandao vinavyofanywa na watu wenye nia ovu huku akiwataka wananchi na wamiliki wa makampuni ya simu kuwa makini juu ya wizi huo wa kimtandao ambao umeshamiri miaka ya hivi karibuni.

  Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa Yoitham Ndembeka ambaye alitumiwa ujumbe wa kumtaka atume fedha kupitia namba ya mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa baada ya kusumbuliwa na matapeli hao ambao hawakutaka kupokea simu aliamua kuachana nao huku akitafuta namna ya kuonana ana kwa ana na Mkuu huyo wa Wilaya.

  Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel kanda ya Kaskazini alipotafutwa kujibu madai hayo simu yake haikupatikana hewani.

  Wizi wa mitandao umeshamiri na kushika kasi hasa katika kipindi hiki ambacho teknolojia imekua kwa kiasi kikubwa ,hivyo makapuni ya simu,mamlaka za kusimamia teknolojia ya mawasiliano TCRA pamoja na polisi wanapaswa kuchukua hatua kupambana na uhalifu huo.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aende Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kufanya upya tathmini na kukagua ugawaji wa viwanja 843 kwenye manispaa hiyo.

  Waziri Mkuu Majaliwa alitoa agizo hilo jana (Jumapili, Machi 14, 2016) wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Mayunga mjini Bukoba.

  Alifikia hatua hiyo baada ya wananchi kubeba bango lenye ujumbe kuelezea kutopewa viwanja hivyo vilivyopimwa na Manispaa ya Bukoba. Viwanja hivyo vilipimwa na kugawiwa kwa wananchi ambao baadhi yao baada ya kulipa fedha, hawajapewa viwanja hivyo ikiwa ni takriban miaka zaidi ya 10.

  Akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Kagera, Waziri Mkuu alilazimika kumpandisha jukwaani Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Bw. Wallace Karia ili atoe maelezo ya nini kimekwamisha wananchi kupewa viwanja hivyo.

  Katika maelezo yake, Bw. Karia alisema mwaka 2003, vilitengwa viwanja 843, kati ya hivyo 352 vilikuwa eneo la Kyabitembe, 137 Ihungo na Rwome na vingine 132.

  Bw. Karia ambaye hana muda mrefu tangu ahamishiwe katika manispaa hiyo, alisema kumbukumbu za ofisi zinaonesha kuwa viwanja 182 ndio wahusika hawajapewa, na viwanja vingine 85 vilikuwa havijapimwa eneo la Kilimahewa na Kashai, huku kukiwa na vingine 5,000 vya mradi.

  Aliongeza kuwa walitarajiwa kuwalipa wananchi hao katika mwaka wa fedha 2016/17; kauli ambayo ilisababisha kelele kutoka kwa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa Waziri Mkuu.

  Kutokana na hilo, Waziri Mkuu aliingilia kati na kumueleza Mkurugenzi huyo kuwa kelele hizo zinaashiria kuwa watu hao hawajaridhishwa na majibu yake.

  Alisema anafahamu kuwa mkurugenzi huyo na meya ni wapya, lakini akawaagiza ndani ya mwezi mmoja, kufanya mapitio ya viwanja hivyo 843, na hasa watu 182 ambao hawajapatiwa viwanja wahakikishe wanawapatia kwa sababu viwanja vipo.

  “Rais mstaafu alikuja hapa na kupewa kilio cha kupunjwa fedha. Najua wakati huo mtasema ninyi hamkuwepo. Wewe (MD) na Meya wako mkae na kupitia mikataba na mafaili. Nyie na mkoa mkae pamoja na kujua vile viwanja vilivyochukuliwa na JWTZ. Nitamleta CAG hapa, ndani ya mwezi mmoja afanye mapitio ya viwanja tu,” alieleza Waziri Mkuu na kushangiliwa na maelfu ya wananchi.

  Katika mkutano huo, Waziri Mkuu pia aliwahakikishia wakazi wa Manispaa ya Bukoba kuwa watalipwa fidia zao baada ya kukubali kupisha ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh. bilioni 31.

  Waziri Mkuu aliendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa kutembelea wilaya za Misenyi na Karagwe na leo atakuwa wilayani Ngara.

  0 0

  Na Veronica Simba

  Serikali imetoa ridhaa kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kufanya uchimbaji wa madini hayo kwa njia ya chini kwa chini (underground mining), sambamba na njia waliyokuwa wakitumia awali ya uchimbaji wa wazi (Open Pit).

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesaini Kibali kinachoruhusu Mgodi wa GGM kufanya uchimbaji huo wa chini kwa chini, leo Machi 15 katika Ofisi za Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na Uongozi wa GGM kabla ya kusaini Kibali husika, Waziri Muhongo alimwambia Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi huo, Terry MulPeter kuhakikisha wanatumia utaratibu wa wazi katika kulipa ushuru wa huduma (service levy).

  Alisema, wananchi, hususan wanavijiji wanaoishi jirani na Mgodi huo wanayo haki kujua ni kiasi gani kinalipwa na GGM kama ushuru wa huduma kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika vijiji vyao.

  “Mtapaswa kuwasilisha Mfano wa Hundi ya malipo, yenye kiasi cha fedha mlichotoa kwa jamii kila mnapolipa ushuru wa huduma ili wananchi wajue ni kiasi gani mmelipa,” alisisitiza.

  Vilevile, Profesa Muhongo aliongeza kuwa, wakati wa kukabidhi Hundi hiyo ya mfano, Naibu Waziri wa Nishati na Madini ni lazima awepo kushuhudia zoezi hilo na kama sio yeye basi atawakilishwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini.

  Alisema, kiongozi mwingine anayepaswa kushuhudia zoezi hilo la kukabidhi hundi ya mfano ya malipo ya ushuru wa huduma kutoka kwenye Mgodi kwenda kwa jamii ni mmoja wa viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Mtaa husika.

  Kabla ya kusaini Kibali hicho, Profesa Muhongo aliwauliza Kaimu Kamishna wa Madini, Julius Sarota na Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Ziwa Viktoria Mashariki, David Mulabwa kama Mgodi huo umekamilisha taratibu zote zinazopaswa ikiwa ni pamoja na kulipa kodi na tozo mbalimbali za madini kwa wakati, ambapo viongozi hao waliafiki.

  “Taratibu zote za kisheria ikiwa ni pamoja na masuala ya uhifadhi wa mazingira zimefuatwa kikamilifu,” alisema Sarota. Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Mulabwa alimhakikishia Waziri kuwa amejiridhisha na sababu zilizotolewa na Mgodi huo kuomba kibali cha kuchimba chini kwa chini na hivyo hana pingamizi kuhusu ridhaa hiyo kutolewa kwao.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa GGM, MulPeter, akijibu swali la Waziri kuhusu ulipaji wao wa kodi na tozo mbalimbali kwa Serikali, alisema kuwa Mgodi huo umekuwa ukilipa kodi zote stahiki kwa wakati.

  “Kwa mwaka huu wa 2016 kwa mfano, tumelipa Dola za Kimarekani Milioni 21.6 kama mrabaha, tumelipa Dola za Kimarekani Milioni 1.6 kama ushuru wa huduma na makadirio ya malipo ya kodi ya mapato kwa mwaka huu ni Dola za Kimarekani Milioni 37,” alisisitiza.

  Aidha, Waziri Muhongo alitumia fursa hiyo kuutaka Uongozi wa Mgodi huo kufanya zoezi la utafiti wa madini (exploration) na kubainisha maeneo ambayo yako ndani ya leseni yao lakini hawatayatumia kwa shughuli za uchimbaji ili wapewe wananchi wenye uhitaji kwa ajili ya kufanyia shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

  Waziri Muhongo alisaini Kibali kinachotoa ridhaa kwa Mgodi wa GGM kufanya shughuli za uchimbaji wa chini kwa chini kupitia Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, kifungu cha 48 (3) kinachompa mamlaka hayo Waziri mwenye dhamana na Wizara husika.

  Kibali hicho cha kuchimba chini kwa chini kwa Mgodi wa Geita kitatumika katika Mashimo (Pit) ya Star na Comet.

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia), akisaini Kibali cha kuuruhusu Mgodi wa Dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine – GGM) kufanya uchimbaji wa madini wa chini kwa chini (underground mining) badala ya uchimbaji wa wazi (Open pit) uliokuwa ukifanywa awali. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa GGM, Terry MulPeter. Kwa kibali hicho, sasa GGM watafanya uchimbaji kwa njia zote mbili. Waziri Muhongo amesaini Kibali hicho  Machi 15, 2016 Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam.

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine – GGM) Terry MulPeter, Kibali cha Mgodi huo kufanya uchimbaji wa madini wa chini kwa chini (underground mining). Awali, GGM walikuwa wakifanya uchimbaji wa wazi pekee. Kibali hicho kimetolewa, Machi 15, 2016 Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa GGM, Terry MulPeter (Kulia), akimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kushoto) wakati wa kikao baina yake na Uongozi wa GGM, kabla ya kusaini Kibali kinachouruhusu Mgodi huo kufanya uchimbaji wa chini kwa chini (Underground mining). Tukio hilo limefanyika Machi 15, 2016 Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni baadhi ya Viongozi na Maofisa Waandamizi wa Wizara.

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akizungumza na Uongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine – GGM) (Kushoto), kabla ya kusaini Kibali kinachouruhusu Mgodi huo kufanya uchimbaji wa chini kwa chini (Underground mining). Kulia ni baadhi ya Viongozi na Maofisa Waandamizi wa Wizara. Waziri amesaini Kibali hicho  Machi 15, 2016 Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  Marehemu  atakapokuwa   ameacha  shauri  mahakamani  ambalo  alikuwa  anashtakiwa nalo  kabla  ya  kufa  kwake  basi  hukumu  itakapotoka  itatakiwa  kutekelezwa.  Hapa  tunaongelea  hukumu  itokanayo na mashauri  ya  madai. Sambamba na  hilo makala  yataangalia  pia mambo  kadhaa  yanayohusu  kifo  cha  mtu  ambaye  alikuwa  akishitakiwa/akilalamikiwa  mahakamani kabla  ya  kifo  chake. Amri  ya  xxii  kanuni  ya  1 – 12  ya  sheria  ya  mwenendo  wa  mashauri ya madai  ndiyo  itakayotuongoza.

  1.JE MSHITAKIWA  AKIFA  NA  KESI  ITAKUFA.

  Kanuni  za  jumla (general rule)   ni  kwamba  shauri  hutakiwa  kufunguliwa  na  mtu  aliye  hai  dhidi/akimshitaki  mtu  aliyehai. Hii  ni  kanuni  ya  jumla  yenye  kumaanisha kuwa  mtu  aliyekufa  hawezi  kushtaki  wala  kushtakiwa. Hata  hivyo  kwenye  kanuni  za  sheria  pale  penye  kanuni  ya  jumla( general rule)  huwa  kuna  vinginevyo( exception).  Hii  ina  maana  yapo  mazingira  ambapo  mshitakiwa  atakufa  lakini  kesi  yake  haitakufa  itaendelea. 

  2. KESI KUENDELEA HATA  BAADA  YA  KIFO  CHA  MSHITAKIWA/MLALAMIKIWA.

  Ikiwa  marehemu  alikuwa  ameshtakiwa/amelalamikiwa   katika  kesi  ambazo  zinahusu  mali  kama  nyumba, gari, kiwanja  na  mali  nyinginezo   na  akafa kabla  ya  kesi  hiyo  kuisha  basi  kesi  hiyo  itaendela.  Pia  ikiwa  alishitakiwa  katika  mashtaka yanayohusu   masuala  ya  mikataba  pia  kesi  hiyo nayo  itaendelea.


  0 0

  Na Mwandishi wetu

  Akizungumzia maadhimisho hayo Dr Asser Mchomvu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki anasema kuwa uongozi wa KH unapenda kuwashukuru wadau wote walioshirikiana nao katika kuiwezesha KH kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa wote.
  indexMkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki,Dk.Asser Mchomvu .
  Dr Mchomvu anaongeza kuwa katika kutambua mchango wa wadau mbalimbali kwa kufikisha miaka 29, KH itafanya maadhimisho yake kwa kutoa msaada kwa vituo vya afya pia kufanya upimaji wa kinywa na meno bure.“Madhimisho haya yataambatana na utoaji wa vifaa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha, ambapo KH itatoa msaada wa vitanda vya hospitali na magodoro siku ya Alhamis tarehe 17.03.2016,” alisema Dr MchomvuAlisisitiza kuwa pamoja na hilo, KH itatoa pia huduma ya upimaji na ushauri wa afya ya kinywa na meno kwa wananchi kwa siku mbili bure ( siku ya Jumatano na Alhamis tarehe 16 na 17, Machi 2016) kuanzia saa 2 asubuhi, pale pale Hospitali ya KAIRUKI, Mikocheni, Dar es Salaam.
  KAI1 KAI2
  Dr Mchomvu anaeleza kuwa, kutakuwa na ghafla fupi ambapo Mkurugenzi atatoa salamu baada ya kukata keki na watoto waliozaliwa KH mwaka 1987. Watu wote wanakaribishwa katika ghafla hiyo itakayofanyika hapo KH siku hiyo ya Alhamisi tarehe 17.03.2016 saa 10 jioni.

  Kwa upande mwingine KH imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma zake huku ikizingatia ufanisi na ubora katika utowaji wa huduma zake kwani inatumia vifaa vya kisasa ambavyo vina ubora wa hali ya juu.

  0 0


  SIMU.tv: Jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kushirikiana na raia wema limefanikisha kuua watu wawili kati ya 4 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakati wakitaka kuvamia kituo cha utafiti wa kilimo. https://youtu.be/kLBUrUL9Cu4
   SIMU.tv: Hospitali ya Butiama iliyoko mkoani Mara yaelezwa kukabiliwa na hali mbaya ya utoaji huduma za afya kufuatia uchakavu wa miundombinu pamoja na ukosefu wa vifaa tiba. https://youtu.be/w061iu0qI-4
   SIMU.tv: Jumla ya watoto 30 wenye matatizo ya vicha vikubwa venye kujaa maji pamoja na migongo wazi wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es salaam. https://youtu.be/CZz3UPkesOA
   SIMU.tv: Rais Magufuli atoa siku 15 kwa mawaziri na wakuu wa mikoa kuhakikisha majina yote ya watumishi hewa yanaondolewa katika malipo.https://youtu.be/XoPeFVIa99Y
   SIMU.tv: Jeshi la polisi visiwani Zanzibar lathibitisha kutokea kwa mlipuko wa bomu katika nyumba ya kamishina wa polisi Zanzibar na kusababisha athari kubwa.https://youtu.be/T08XsrYLe8o
   SIMU.tv: Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu yakanusha taarifa zilizochapishwa na gazeti la Jamb leo kwamba serikali ya awamu ya 5 imewapunguzia Maraisi wastaafu ulinzi na kulitaka gazeti hilo kuomba radhi. https://youtu.be/xmT3EI-zJs0
   SIMU.tv: Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo abainisha Tanzania kugundua rasilimali nyingine ya gesi asilia katika bonde la mto Ruvu mkoani Pwani.https://youtu.be/l_R8oTcKQlw
   SIMU.tv: Waziri mkuu Kassim Majaliwa atoa siku 5 kwa uongozi wa mkoa wa Kagera kutoa maelezo kuhusiana na matumizi ya fedha za mradi wa ukimwi pamoja utekelezaji wa ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali CAG.https://youtu.be/MaBAtXUqMe8
   SIMU.tv: Waziri wa ujenzi Prof. Mkame Mbarawa afanya ziara katika daraja la Kigamboni jijini Dar es salaam kujiridhisha kuwa liko katika hatua za mwisho kwa kubainisha kuwa litazinduliwa mwezi wa 4 mwaka huu.https://youtu.be/JQFqEpCGTXU
   SIMU.tv: Kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii imekutana na kujadili majukumu na utekelezaji wa taasisi ambazo ziko chini ya wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo. https://youtu.be/c-Bv2BF5KeM

  0 0

     Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad Mselle  akimfanyia  usafi wa nywele  mmoja wa watoto wanao lelewa katika Kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi waliopo Buhangija Mkoani shinyanga walipofika katika kituo hicho kwa mwendelezo wa Wiki ya Afya ya Kinywa na Meno ambapo kilele chake ni Machi 20, Mkoani Morogoro. 
    Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Conrad Mselle  akimfanyia uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno Mwanafunzi wa Darasa la pili  Lucia  Eliasi wa Kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi kilichopo Mkoani Shinyanga, Buhangija   ambapo ni mwendelezo wa wiki ya kinywa na meno duniani na kwa leo wameonwa  watoto157 na kesho ni mwendelezo wawale waliokutwa na matatizo.

   Daktari bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno  Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Dk. Nuru Mpuya  na akimwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga  Dk. Ntuli Kapologwe, akizungumza jambo, kushoto ni Kiongozi wa Msafara Dk.  Arnold Mtenga
    msimamizi wa Kituo cha Buhangija na Mwalimu wa Elimu Maalum na watoto wasioona,  Sasu Nyanga , akiwakaribisha Madaktari bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno.
  Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Simba akihutubia washiriki wa semina hawapo pichani wakati akifunga semina, siku ya watumiaji wa huduma Ulimwenguni. 
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, akihutubia kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika ufunguzi wa semina ya siku ya haki za watumiaji wa huduma Ulimwenguni.
   Baadhi ya washiriki wa semina wakimsikiliza mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo hayupo pichani siku ya watumiaji wa huduma Ulimwenguni  inayoadhimishwa tarehe 15 Machi, ya kila Mwaka.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano upande wa sekta ya Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Ally Simba (kushoto) siku ya watumiaji wa huduma Ulimwenguni.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiweka jiwe la msingi la usimikaji mtambo mpya wa kufua umeme wa Ngara akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2016. Kushoto ni Naibu Waziriwa Nishati na Madini Dkt. Kalemani.
   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akiweka jiwe la msingi la usimikaji mtambo mpya wa kufua umeme wa Ngara akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2016. Kushoto ni Naibu Waziriwa Nishati na Madini Dkt. Kalemani. 
   aziri Mkuu, Kassim Majliwa kizungumza na wakimbizi wa Burundi walioko katika kambi ya  Lumasi  iliyopo wilayni Ngara. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15 2016.
   Baadhi ya wakimbizi wa Burundi walioko kwenye kambi ya Lumasi iliyopo wilayani Ngara wakimsikilza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 15, 2916.


  0 0

    Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi (aliyesimama), akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Mamlaka hiyo wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa alipofanya ziara ya siku moja Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
  Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) pamoja na Viongozi Waandamizi wa Mamlaka hiyo, wakiwa katika kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani), alipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. 
   Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati  na Maji (EWURA), Omary Bendera (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa Vitabu mbalimbali vyenye maelezo kuhusu Mamlaka hiyo, wakati alipotembelea Makao 
  Makuu ya EWURA hivi karibuni.
   Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Omary Bendera (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa Vitabu mbalimbali vyenye maelezo kuhusu Mamlaka hiyo, wakati alipotembelea Makao Makuu ya EWURA hivi karibuni.
  Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Omary Bendera (kulia) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo Vitabu mbalimbali vyenye maelezo kuhusu Mamlaka hiyo, wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa Justin Ntalikwa Makao Makuu ya EWURA hivi karibuni.

older | 1 | .... | 1159 | 1160 | (Page 1161) | 1162 | 1163 | .... | 3284 | newer