Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1157 | 1158 | (Page 1159) | 1160 | 1161 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inatoa siku 60 kuanzia tarehe 14 Machi, 2016 kwa wanufaika wote wa mikopo wanaodaiwa na HESLB kujitokeza na kuanza kulipa madeni yao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Aidha, katika muda huu wa siku 60 waajiri pia wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao wa kisheria wa kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao waliohitimu katika vyuo vya elimu ya juu ndani na nje ya nchi. Taarifa zinazopaswa kuwasilishwa zijumuishe majina kamili ya waajiriwa, vyuo na mwaka waliohitimu.

  Itakumbukwa kuwa Sheria iliyoanzisha HESLB (Sura 178) (kama ilivyorekebishwa) inatoa wajibu kwa mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu na pia wajibu kwa mwajiri.

  Wajibu wa Mwajiri
  Hivyo basi, taarifa hii inalenga kuwakumbusha waajiri ambao bado hawatimizi wajibu wao kisheria (kifungu cha 20) wa kuwasilisha majina ya waajiriwa wao wote ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu kwa HESLB ndani ya siku 28 tangu waajiriwe. Adhabu ya kutotekeleza wajibu huu kwa mwajiri ni faini ya shilingi milioni saba (Tshs milioni 7) au kifungo au vyote kwa pamoja.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Bendi maarufu ya Inafrika band aka Wazee wa Indege wanatarajiwa kuruka wakati wowote ule kuelekea nchini marekani kushiriki katika maoyesho makubwa ya kimataifa ya Festival of nations, yatakayo fanyika Dollywood Theme Park. Bendi hii kutoka Tanzania ndio bendi pekee iliyoteuliwa kuliwakilisha bara la Afrika katika maonyesho hayo ya kimataifa.

  Inafrika band itakuwepo nchini marekani katika ziara ya kikazi kwa muda wa miezi mitatu kuzikonga nyoyo za washabiki wa kimataifa nchini marekani.Kuchaguliwa kwa Inafrika band kushiriki maonyesho hayo makubwa kunatokana na mvuto wa muziki wa bendi hiyo kukubalika zaidi kimataifa. Muziki ambao una maadili ya kitanzania ambako nje ya mipaka umewateka washabiki wengi wa kimataifa.

  Bendi hiyo yenye makao jijini Dar-es-salaam imejikuta haina muda wa kupumzika kutokana na wingi Tour za kimataifa kwa muda wa miaka 10 sasa.
  Ni kama wiki mbili tu bendi hiyo imerudi kutoka safari ya nchi 19 za bara la ulaya. Tunawatakia kila la heri Inafrika Band aka Wazee wa Indege katika kutuwakilisha huko Marekani. 

  Bendi hiyo ilikuwapo Dollywood Marekani mwaka 2014 na kuwanasa washabiki wengi na muziki wao wa kitanzania watupie jicho at http://www.inafrikaband.co.tz au http://www.facebook.com/inafrikaband.wazeewaindege


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kwanda  cha maji cha Bunena Spring Water akiwa akika ziara ya mkoa wa Kageza Machi 13, 2016.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mradi mkubwa wa maji wa Bunena mjini Bukoba ulio chini ya mamlaka ya maji ya mji huo BUWASA  akiwa katika siku ya kwanza  ya ziara ya mkoa wa Kagera machi 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mlkuu)
     Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua  kiwanda cha Maji   ya Bunena Spring Water  kilichopo mjini Bukoba Machi 13, 2016. Alikuwa katika sik ya kwanza ya ziara ya mkoa wa Kagera.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua uzalishaji wa maji ya  kiwanda cha maji ya Bunena Spring Water cha Bukoba mjini akiwa aktika siku ya kwanza ya ziara ya mkoa waKagera Machi, 13, 2016.  Kulia kwake ni Askofu wa jimbo la Bukoba,Method Kilaini. (Picha na Ofisi ya waziri Mkluu)
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo mafupi kuhusiana na maji hayo ya  kiwanda cha maji ya Bunena Spring Water cha Bukoba mjini akiwa aktika siku ya kwanza ya ziara ya mkoa waKagera Machi, 13, 2016.  Kulia kwake ni Askofu wa jimbo la  Bukoba,Method Kilaini.  (Picha na Ofisi ya waziri Mkluu)

  0 0

  Huduma  ya usafiri  wa reli ya Kati iliyokuwa imesimama kwa takribani miezi miwili sasa imerejea kufuatia  kukamilika kwa ukarabati wa reli  hiyo katika eneo la kidete wilayani kilosa, mkoani Morogoro.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa  amesema  hayo baada ya kukagua na kuridhika na ukarabati uliofanywa katika maeneo ya Magulu, Munisagara, Mzaganza na kidete Wilayani Kilosa.

  “Hakikisheni mnailinda reli hii kwa manufaa yenu na ya Taifa, leo hii reli iko  vizuri na treni ya kwanza kutoka Dar Es Salam  kwenda bara itapita na kumaliza changamoto ya usafiri iliyokuwa inawakabili wananchi wanaotumiia reli hii”.Amesema Profesa Mbarawa.

  Profesa Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo ya Kilosa, Magulu, Munisagara, Mzaganza, Kidete, Godegodena Gulwe ambao maeneo yao yanakabiliwa na mafuriko ya mto Mkondoa kuacha Kilimo cha kuelekeza Maji kwenye reli bali washirikiane na Serikali kudhibiti maji hayo kwenda kwenye  hifadhi ya reli.

  Amesema Shirika la Reli Tanzania ( TRL) linaendelea kuhakikisha  kuwa treni  inayopita  kwenye reli ya Kati  inapata mzigo mwingi wa kusafirisha kutoka bandarini za Tanga na Dar Es Salaam kuelekea mikoa ya Mwanza, Kigoma na Mpanda, hivyo wafanyabiashara watumie fursa hiyo ili kupunguza mzigo unaosafirishwa kwa Nadia ya barabara.

  Waziri Profesa Mbarawa ameteembelea bwawa la Kidete linaloelezwa kuwa chanzo cha mafuriko pindi linapojaa wakati wa mvua za Vuli  na Masika katika mikoa ya Dodoma na Iringa.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa John Henjewele amemhakikishia Waziri Profesa Mbarawa kuwa ofisi yake itafuatilia kwa karibu malalamiko ya wananchi wanaoishi karibu na reli  ya Kati ili kuyapatia ufumbuzi na kuwataka wananchi hao kuitumia fursa ya kuwa karibu na reli kunufaika kiuchumi.

  Takribani Shilingi millions 926 zimetumika katika ukarabati wa reli hiyo kufuatia uharibifu uliotokea mwezi  Januari na kukata Mawasiliano ya reli Kati ya mikoa ya  Dodoma na Morogoro na kusababisha Safari za treni kutoka bara kuishia Dodoma.

  Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi,, Uchukuzi na Mawasiliano Serikalini.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.

  Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.

  Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
  1.Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
  2.Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga - Mkuu wa Mkoa wa Geita.
  3.Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu - Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
  4.Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga - Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
  5.Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga - Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
  6.Mh. Godfrey Zambi - Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
  7.Dkt. Steven Kebwe - Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
  8.Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
  9.Mh. Anna Malecela Kilango - Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
  10. Mhandisi Methew Mtigumwe - Mkuu wa Mkoa wa Singida.
  11. Mh. Antony Mataka - Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
  12. Mh. Aggrey Mwanri - Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
  13. Mh. Martine Shigela - Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
  14.Mh. Jordan Mungire Rugimbana - Mkuu wa Mkoa Dodoma.
  15.Mh. Said Meck Sadick - Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
  16.Mh. Magesa Mulongo - Mkuu wa Mkoa Mara.
  17.Mh. Amos Gabriel Makalla - Mkuu wa Mkoa Mbeya.
  18.Mh. John Vianey Mongella - Mkuu wa Mkoa Mwanza.
  19.Mh. Daudi Felix Ntibenda - Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
  20.Mh. Amina Juma Masenza - Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
  21.Mh. Joel Nkaya Bendera - Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
  22.Mh. Halima Omary Dendegu - Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
  23.Dkt. Rehema Nchimbi - Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
  24.Mhandisi Evarist Ndikilo - Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
  25.Mh. Said Thabit Mwambungu - Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
  26.Luteni Mstaafu Chiku Galawa - Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).

  Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa, wataapishwa Jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaam.

  Gerson Msigwa
  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
  Dar es salaam
  13 Machi, 2016

  0 0


  Wakazi wa kata ya Kibirizi katika manispaa ya Kigoma ujiji wagoma kupokea notice ya kupisha ujenzi wa bandari kavu kwa madai ya kulipwa fedha ndogo ukilinganisha na thamani ya mali zao https://youtu.be/lsEW21hKctM
   Watu watu wafariki dunia na wengine 6 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya SAIBABA kugonga uso kwa uso na lori mkoani Arusha.https://youtu.be/CFJC9j1tY8Q
   Familia moja katika maeneo ya Magomeni jijini Dar es salaam yanusurika kuteketea kwa moto baada ya nyumba yao kuungua yote na kuzua taharuki katika mtaa huo. https://youtu.be/0LhWj-lSaJY
   Serikali yaifunga shule ya sekondari ya ufindi IYUNGA ya jijini Mbeya hadi mwezi wa 4 ili kupisha ujenzi wa mabweni mawili na ukarabati wa majengo yaliyoungua moto wiki kadhaa zilizopita. https://youtu.be/c05R7gZn9NM
   Maafisa wa mamlaka ya mapato nchini TRA yawatia mbaroni Wachina 2 eneo la Tabata jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kukwepa kodi kupitia mauzo.https://youtu.be/-9WYOu9Eb6E
   Kazi ya uopoaji wa miili 3 ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite waliofariki dunia kwa kufukiwa na kifusi imeendelea huku miili miwili ikifanikiwa kuopolewa. https://youtu.be/Q9ZpsKzmB60
   Askari wa hifadhi ya Selous walalamikiwa kwa vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na askari kwa wananchi wa Liwale mkoani Lindi.https://youtu.be/b2Xr01aHCgI
   Siku mbili baada ya wizara afya kufunga chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Tumbi mkoani Pwani, leo hii hospitali hiyo yafungua kituo hicho baada ya ukarabati kukamilika. https://youtu.be/y2e93Bk5_88
   Waziri mkuu Kassim Majaliwa awasili mkoani Kagera kwa ziara ya siku 3 kikazi huku akitoa tahadhali kwa idara ya uhamiaji mkoani humo.https://youtu.be/8R3U5t3ZKUM
   Wafanyakazi 276 wa kampuni ya ujenzi ya CRG ya mjini Dodoma wafanya mgomo kushinikiza kulipwa malimbikizo yao yaliyodumu kwa zaidi ya miaka 3.https://youtu.be/zutWTnAeoxs
   Hatimaye huduma ya usafiri wa treni kupitia reli ya kati iliyokuwa imesimama kwa muda kufuatia mafuriko kuharibu miundombinu ya reli mkoani Morogoro, yarejea tena baada ya matengenezo kukamilika. https://youtu.be/pf_bs1unZU0
   Aliyekuwa mkuu wa Brigedia ya JWTZ Tabora Brigedia Jenerali Sukambi, awataka maafisa na askari wa jeshi hilo kulinda kiapo chao na kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kupambana na ubadhilifu.https://youtu.be/zic2E_1ZsnM
   Baadhi ya wananchi washauriwa kutumia nguvu zao binafsi kuiunga mkono serikali katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ili kujiletea maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla. https://youtu.be/Foqj3YtPY1A

  0 0


  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba akikabidhi msaada wa Mabati 64 kwa ajli ya Ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari ya Bazo iliyopo kata ya Vuga Wilayani Lushoto mkoa wa Tanga.
  Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba akizungumza na Wananchi wa Kata Mponde katika Mkutano hadhara, ambapo Mbunge huyo ameeleza Mikakati mbalimbali ya kuwasaidia wananchi wa Kata hiyo ambao wengi wao hujishughulisha na masuala ya Kilimo.
  Gari ikiwa imebeba Rola 70 za Mabomba ya kusafirishia Maji, ambayo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba kwa wananchi wa Kata ua Usambara ili kupunguza Kero ya muda mrefu ya wananchi hao katika Suala la Upatikanaji wa maji safi na salama.( Picha na Imani Nsamila ).


  0 0

  Ndugu watanzania na wote wanaofuatilia kazi zangu nasikitika kuwajulisha kuwa kuna Jennifer Mgendi feki kaibuka Facebook kafungua akaunti kwa jina langu kachukua na picha zangu ambazo zinapatikana mtandaoni kaziweka kwenye akaunti yake ili kuwaaminisha watu kuwa ni Jennifer Mgendi.

  Mtu huyu ambaye naamini hana lengo lingine zaidi ya kunichafua amekuwa akipost vitu anavyojua mwenyewe na kuwasiliana na watu mbalimbali ambao baadhi wamekuwa wakinipigia kufuatilia mambo ''tuliyoongea facebook''!! 

  Cha ajabu amekuwa akiwapa namba yangu ya simu ambayo ipo kwenye cd zangu ili kufanya watu wazidi kuamini kuwa wanachat na Mimi.

  Napenda kuujulisha umma kuwa sipo Facebook wala sichat na mtu yoyote Facebook. Mawasiliano ninayotumia ni ya simu ya mkononi na email kama zinavyoonekana kwenye dvd zangu.

  Kwa ujumbe huu natoa onyo kwa mtu huyo kuacha mara moja kwani mamlaka husika inalifanyia kazi jambo hili na hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

  0 0

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) Antony Mavunde ametaka kuondolewa kwa changamoto maeneo ya kazi ili kazi isaidie maendeleo ya binadamu badala ya kujikimu.Naibu Waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua ripoti ya maendeleo ya binadamu ya mwaka 2015 inayoelezea kazi kwa maendeleo ya binadamu.

  Alisema kwa sasa kuna figisu kubwa katika kazi nchini hasa kutokana na waajiri wengi kugeuza kazi kama sehemu ya kujikimu kwa wafanyakazi wao kwa kutowapa stahiki husika ikiwamo mikataba ya ajira.

  Alisema kazi inapokuwa ni ya kujikimu kunakuwa na migogoro mingi na kuvurugika kwa uzalishaji na kutishia maendeleo ya taasisi husika na maendeleo ya mtu binafsi.Alisema Tanzania imefurahishwa na yaliyomo katika ripoti hiyo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kutokana na kuzungumzia jinsi kazi zinavyoweza kusaidia upatikanaji wa maendeleo.
  UNDP HUMAN DEVELOPMENT REPORT 2015 LAUNCH
  Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) akizindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Machi 11, 2016.
  Anthony Mavunde
  Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde akionyesha ripoti hiyo kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari (hawapo pichani).
  IMG_6200
  Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo kwa pamoja wakiwa wameshikilia ripoti hiyo.


  0 0

   Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael akiwa ameongozana na Mkuu wa usalama wa uwanja huo Macmilan Matili kuangalia maeneo mbalimbali ya uwanja huo. 
   Meneja wa uwanja mdogo wa ndege Moshi,Fredrick Kimaro akimuonesha Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael eneo la maegesho ya ndege katika uwanja huo. 
   Eneo la kukimbilia ndege katika uwanja mdogo wa ndege Moshi likionekana katika hali hii.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0


  Mariamu Hussein akihudhuria harambe ya kumchangia iliyofanyika siku ya Jumamosi Silver Spring, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na WanaDMV na marafiki zao. Mariam Hussein nasumbuliwa na ugonjwa wa saratani.
  Vitu mbalimbali vilivyoletwa na WanaDMV kwa ajili ya kuvipiga mnada kwenye harambee iliyofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, Maryland nchini Marekani.

  Vitu mbalimbali vilivyoletwa katika mnada wa harambee ya Mariam Hussein uliofanyika siku ya Jumamosi March 12, 2016 Silver Spring, maryland nchini Marekani.
   

  0 0

  Bango Sangho - Kibugumo
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) akimpima uzito mtoto Shafii Haji (mwaka mmoja na nusu) mkazi wa Kibugumo Darajani, kama ishara ya kuzindua kambi ya huduma za upimaji afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu wa kambi hiyo kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk. Ali Mzige, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile (wa kwanza kulia) pamoja na Muuguzi wa Zahanati ya Kibugumo, Agnes Mokiwa (wa pili kulia) wakishuhudia tukio hilo.
  Bango Sangho- kibugumo Primary School
  Meza kuu kwenye uzinduzi wa kambi ya upimaji afya kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mratibu wa kambi hiyo ya upimaji kutoka Kliniki ya Al Hilal, Dk.Ali Mzige, Mwenyekiti wa Umoja wa Jamii ya watu kutoka India, Bengali waliopo Tanzania (Bango Sangho), Kunal Banerjee, Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kibugumo, Mzamilo Ally, Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
  Bango Sangho Kibugumo
  Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile akisisitiza jambo kwenye uzinduzi huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema kutoa nasaha katika ufunguzi wa kambi hiyo.
  Bango Sangho - Kibugumo
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akitoa neno la ufunguzi wa kambi ya upimaji afya kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano iliyofadhiliwa na Umoja wa Watu kutoka Bengali, India wanaoishi Tanzania (Bango Sangho) katika shule ya Msingi Kibugumo iliyopo Kigamboni jana jijini Dar es Salaam.


  0 0

  mssoga

  Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiongozwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Msoga, Dk. Juliet Lema wakati wa ukaguzi huo. Kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Dkt. Beatrice Jane Byalugaba.(Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipa hadhi ya kuwa Hospitali Wilaya iliyokuwa Zahanati ya Msoga ambayo tayari imekamilisha jengo lake jipya la Hospitali hiyo inayotarajia kuanza kuanzia Mwezi Aprili mwaka huu.

  Akitoa maagizo hayo baada ya ukaguzi wa timu ya wataalam kutoka Wizara hiyo ya Afya pamoja na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla waliofanya hivi karibuni katika Hospitali hiyo, ameeleza kuwa kuanzia Mwezi Aprili ianze kazi kwa kuanza na huduma za wagonjwa wa nje na baada ya miezi mitatu itaendeshwa na huduma zote muhimu ikiwemo kulaza wagonjwa.

  “Naagiza ndani ya mwezi mmoja ianze kazi na huduma za kawaida. Baada ya miezi mitatu itaendelea na huduma muhimu zote katika Hospitali hii mpya ya Wilaya” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa hitimisho lake kwa wasimamizi wa Zahanati hiyo ya Msoga.
  Dk. Kigwangalla na timu yake waliweza kukagua majengo ya Hospitali hiyo mpya ambapo na kuona inakidhi vigezo ya kuwa Hospitali ya Wilaya.

  Majengo ya Hospitali hiyo yapo katika Kituo cha afya cha Msoga, kata ya Msoga, Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani, Ni miongoni mwa Hospitali itakayokuwa ya kisasa na kubwa.Aidha, kutokana na matukio mengi ikiwemo ya ajali nyingi zinazotokea mara kwa mara katika barabara ya Chalinze-Segera, Hospitali hiyo ya Wilaya itakuwa msaada na itawezesha kupunguza mzigo wa vituo vya afya vya vya jirani ikiwemo Lugoba, Chalinze na vinginevyo ndani ya Halmashauri hiyo yaa mji mdogo wa Chalinze.
  msoga
  Jengo hilo la Hospitali ya Wilaya inavyoonekana kwa nje
  msoga 55
  Waziri Dk. Kigwangalla akiwa na timu yake wakikagua eneo hilo la Hospitali ya Wilaya. Jengo linaloonekana nyuma awali lilipangiwa kuwa sehemu ya kuhifadhia maiti (Mochwari) hata hivyo wamebadilisha matumizi yake na Mochwari itajengwa mbali kidogo na hapo ilikutoa naafasi kubwa kwa kujengwa mochwari ya kisasa.
  msoga 22
  Dk. Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni katika Zahanati ya Msoga mara baada ya kufanya ukaguzi na kuagizia majengo mapya ya Hospitali hiyo kuanzia mwezi ujao wa Aprili yaanze kutumika kama Hospitali ya Wilaya ambapo Madawa na vifaa vinatarajiwa kupelekwa muda wowote kuanzia sasa.

  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York
  Wajumbe wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, ( UNSC)  wamekubaliana  juu ya mfumo ambao utatumika kupima utekelezaji  wa  Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ( Agenda 2030)
  Makubaliano hayo yamefikiwa mwishoni mwa wiki wakati wajumbe  24 wanaounda Kamisheni ya  Takwimu ya Umoja wa Mataifa,  pamoja na wadau wengine walipokutana kwa mkutano wao wa 47 uliodumu kwa wiki moja.
  Mkurugenzi Mkuu wa  Ofisi ya Taifa ya  Takwimu, Dr. Albina Chuwa aliongoza ujumbe wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika mkutano huu, ambapo  Tanzania ilishiriki kama  Mjumbe wa Kundi la Waatalamu kuhusu Viashiria   vya Mendeleo Endelevu (Inter-Agency Expert on  Indicators  of Sustainable  Development Goals).
  Pamoja na kujadiliana kuhusu  viashiria  na umuhimu wake katika kupima utekelezaji wa Agenda-2030, washiriki wa mkutano huu pia walijadili   ajenda nyingine  zilizohusu  takwimu  za wakimbizi,, program ya  ulinganifu wa kimataifa wa  data,  na misaada  ya kitakwimu katika utekelezaji wa Agenda  2030.
  Agenda  2030  ina malengo    malengo 17  yakiwa pia na viambatisho  169 na  ilipitishwa    rasmi na  Viongozi Wakuu wa  Nchi na Serikali mwezi Septemba  mwaka  jana na utekelezaji wake umeanza mwezi Januari  mwaka huu.
  Ajenda  imebeba maudhui ya  “kubadili dunia yetu: ajenda ya mwaka 2030 kwa maendeleo endelevu”. Ni ya   kihistoria ikijumuisha  masuala  yote muhimu  yanayowahusu na kugusa maisha ya kila mtu na ikiwakilisha matarajio   makubwa ya maendeleo ya dunia nzima.
  Inaelezwa  pia kwamba ni  ajenda ya watu, ambayo imesheheni mipango ya kutokomeza umaskini wa aina zote, bila kumwacha mtu yeyote nyuma. Ikilenga pia kuhakikisha Amani na usalama, kuongeza ufanisi katika shughuli za maendeleo na kubuni ubia unaojali binadamu na sayari Dunia.
   
  Pichani  Dr. Albina Chuwa ,  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (mstari wa mwisho) katika siku ya mwisho ya  Mkutano wa  47 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa,  mkutano  uliopitisha mfumo wa  viashiria vya kupitia utekelezaji wa  Malengo ya  Endelevu ya Maendeleo ( agenda 2030) aliyeketi nyuma na Mkurugenzi  Mkuu, ni Afisa Mwandamizi wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bw. Songelael Shilla.
   Sehemu ya  Wajumbe wa Mkutano wa 47 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa wakifuatilia  majumuisho ya mkutano wao wa wiki mmoja uliomalizika mwishoni mwa wiki.

  0 0

  WALIMU 447 wa shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida hawajapandishwa madaraja yao mbalimbali kutoka mwaka 2014/2015 mpaka sasa hali ambayo imepunguza ari ya utendaji wao wa kazi za kila siku.
  Katibu wa Chama Cha Walimu (CWT) Wilaya ya Manyoni, Nelea Nyang’uye aliyasema hayo kwenye taarifa ya kamati ya utendaji ya chama hicho aliyotoa kwa Naibu katibu mkuu CWT,Ezekiah Oluoch aliyekuwa na ziara ya siku moja wilayani Manyoni iliyolenga kusikiliza kero pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
  Aidha Nelea alifafanua kwamba kati ya walimu hao,walimu 390 ni walimu wa shule za msingi na kwamba walimu 276 licha ya kuwa na sifa za kupandishwa madaraja lakini mpaka wamefikia hatua ya kugota na bila kupandishwa na walimu 114 wanastahili kupandishwa kwa utaratibu wa kawaida.
  Kwa mujibu wa katibu huyo wa CWT,kwa upande wa idara ya elimu sekondari kuna walimu 9 waliogota na walimu 50 wanastahili kupandishwa kwa utaratibu wa kawaida lakini mamlaka zinazohusika zimeshindwa kushughulikia wilayani hapa.
  Kuhusu malipo ya fedha za likizo,Nyang’uye aliweka bayana kuwa kwa kipindi cha mwezi disemba,mwaka jana Halmashauri ya wilaya ya Manyoni ilitarajia kupokea shilingi milioni 30 lakini fedha walizopokea ni shilingi milioni 21 na hivyo kuwa na upungufu wa shilingi milioni saba.
  Hata hivyo msemaji huyo wa chama alisisitiza kwamba fedha hizo za nauli ya likizo hupelekwa kidogo sana na kibaya zaidi fedha hizo hupelekwa wakati likizo ikiwa imeshaanza au inakaribia kwisha,jambo ambalo linapelekea walimu wwenye haki ya kulipwa kuanza kukopa.
  “Nauli za likizo kuletwa kidogo mno na zinaletwa wakati likizo ikiwa imeanza au inakaribia kwisha,jambo ambalo linapelekea walimu wenye haki ya kulipwa kuanza kukopa,kwa mfano nauli ya mwezi disemba,mwaka jana iliyoletwa kwa idara ya elimu ya msingi ni shilingi 23,000,000/= na idara ya elimu sekondari ni shilingi milioni saba”alisisitiza katibu huyo wa CWT.
  Nyang’uye hata hivyo alionyesha masikitiko yake kutokana na Tume ya Utumishi wa Walimu(TSD) wilaya ya Manyoni kushindwa kushughulikia mashauri ya kinidhamu kwa wakati na hivyo kuchukua muda mrefu sana na kutoa mfano wa shauri moja la walimu wawili waliosimamishwa kazi tangu mwaka 2013 mpaka sasa hawajuia hatma yao.

  Ni Katibu wa TSD Mkoa wa Singida,Bwana Samweli Ole Saitabau(aliyesimama) akitoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa haki za walimu wa wilaya ya Manyoni ambao bado haapandishwa madaraja yao.

  Ni Baadhi ya wanachama wa CWT Wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida wakiwa katika mkutano wa pamoja na Naibu Katibu Muu wa CWT,Bwana Ezekiah Oluoch


  0 0

  Taasisi mpya ya Kijamii ijulikanayo Madam Sophy Charity Events yenye malengo ya kusaidia jamii hasa ile yenye uhitaji maalum ikiwemo watu wasiojiweza imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam sambamba na kutoa misaada mbalimbali kwa watu na watoto wenye uhitaji huo maalum.

  Tukio hilo la kipekee lililoandaliwa na kuratibiwa na Mwanadada, Sophia Mbeyela pia lilijumuisha wadau na marafiki mbalimbali walioungana na Madam Sophy katika kufanikisha tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu ambayo ilishirikisha watoto wanafunzi wa kituo cha Matumaini wenye Ulemavu wa viungo na ngozi.

  Madam Sophy na marafiki zake kwa pamoja waliweza kutoa misaada ya vitu mbalimbali kwa watoto hao ambapo pia walipata wasaha wa kuzindua taasisi hiyo huku mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni ambaye aliwakilishwa na Mbunge Kibaha Vijijini, Mh. Amoud Abduul Jumaa ambaye aliahidi kufikisha kilio cha walemavu na watu wenye mahitaji maalum Serikalini paamoja na kwenda kuwasilisha Bungeni ilikuona utekelezaji wake kwa ukaribu.

  “Madam Sophy Charity. ni taasisi ambayo zaidi ni kuona wenzetu wenye uhitaji maalum hasa walemavu wanapata nafuu katika kuendana na majukumu ya nchi hii kwani sote tuna haki sawa kama wengine na ulemavu wetu usitutenganishe. Tunahitaji Serikali kuhakikisha inashusha bei vifaa vyote vya walemavu ikwemo viungo vya bandia ikiwemo mikono na miguu ambayo kwa kiungo mimoja pekee yake kinakaribia hadi milioni moja” alieleza Madam Sophy.

  Madam Sophy aliongeza kuwa, Serikali inayo wajibu wa kujenga shule nyingi zaidi za watu wenye ulemavu kwani zilizopo sasa bado ni chache na watu wenye ulemavu wamehamasika kujitokeza kusoma hivyo jukumu lililopo ni kuhakikisha wanaongeza shule za watu hao pamoja na kutengeneza miundombinu ambayo inakuwa rafiki kwa walemavu kuanzia mashuleni na hata maeneo muhimu.

  Aidha, Kwa upande wake, mgeni rasmi huyo aliweza kuchangia kiasi cha Sh Laki tano kwa ajili ya kuunga mkono juhudi na harakati za Madam Sophy ambapo alieleza kuwa, licha ya ulemvu wake ameweza kuonesha njia ya kujikwamua pamoja na kuwasaidia wenzake.

  Madam Sophy ambaye kitaaluma ni Mwalimu, ni miongoni mwa wanafunzi waliopata kusoma katika shule hiyo na kumaliza hapo darasa la saba mwaka 2002 ambapo pia aliendelea na shule mbalimbali ikiwemo Sekondari ya Jangwani na baadae chuo, ameomba wadau kujitokeza kuungana naye katika kuhakikisha wanasaidia watu na jamii yenye uhitaji maalum kwani kutoa ni moyo.
  mada wote
  Baadhi ya wadau wakitoa zawadi na vitu mbalimbali kwa Madam Sophy ambavyo vitagawiwa kwa wanafunzi wa shule hiyo ya Jeshi la Wokovu na wale wa Makumbusho Sekondari.
  madae
  Wanafunzi wenye ulemavu wa viungo na ngozi wakiwa katika tukio hilo.
  madass
  Wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wakitoa burudani kwa mgeni rasmi (hayupo pichani).


  0 0  It’s been a one year without you, but we know we must go on, for you would want us too. Thank you for all the wonderful memories we have of you and for being the best dad any person could have.

   I know you smiling down on us from heaven, because we can feel your love all around us, but not forgotten in the 14 March, 2015 by Mama Mchanga, Ernest Mchanga, Eng. 

  MaluguMchanga, Tabitha  Christopher, MalumeMchanga, YohanaMchanga, Paul Mchanga. We keep you in hearth always.  We love and miss you,your grandchildren send their love and blessings too.
                MCHANGA’S FAMILY

  0 0
 • 03/13/16--23:39: DONDOO ZA MAGAZETI

 • 0 0

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kimewaagiza wenyeviti wa chama wa wilaya zote Mkoani Singida kuunda kamati za kufuatilia mali za chama za wilaya zao pamoja na miradi yake yote iliyopo kwenye maeneo yao na taarifa za kamati hizo zitumwe makao makuu ya mkoa.

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,Marther Mosses Mlata alitoa agizo hilo alipokuwa aakiongea na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Manyoni,uliokuwa na lengo la kuwashukuru kwa kumchagua kwa kishindo kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

  Akizungumza na wanachama wa chama hichco,wa wilaya ya Manyoni,Mwenyekiti huyo alisema kwamba iwapo miradi ya chama hicho itafahamika na kutambulika kikamilifu uzalishaji wake,utasaidia kuondokana na tabia ya kuwategemea madiwani kusaidia kwa kila jambo linalojitokeza kwenye maeneo yao.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata akisisitiza jambo kwenye mkutano wa kuwashukuru wajumbe wa wilaya ya Manyoni.

  “Mwenyekiti ninaomba uunde kamati maana mimi nitaunda hivi leo ninamalizia halafu nitatangaza kamati yangu,hivyo unda kamati itakayofuatilia mali za chama za wilaya na miradi yake yote ije pale makao makuu ya mkoa”alisisitiza huku akishangiliwa na wanachama wa chama hicho waliohudhuria mkutano huo.

  “Nimesema mali za wilaya,mali si mnazo,miradi mnayo,mapatoo,mapatoo… mnasomewa,mwenyekiti wenu anasema?alihoji mwenyekiti huyo mbele ya wanachama hao ambao kwa kauli moja walipinga kutosomewa taarifa za mapato na matumizi ya chama chao.

  Kwa mujibu wa Mlata hata hivyo alitumia mkutano huo pia kuwaagiza watendaji wa ngazi za matawi na kata kwenda kuunda kamati hizo kwa madhumuni kama hayo ya kutambua mali za wanachama wa chama hicho na kutuma taarifa zao wilayani na kusisitiza pia kwamba kwa kata na matawi yasiyokuwa na miradi ikabuni haraka ili vyanzo vya mapato viweze kuwepo kwenye maeneo husika.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata akivishwa skafu muda mfpi tu mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za chama mjini Manyoni.

  Naye Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki(CCM), Emanueli Mtuka alisema kuwa ili fedha zilizoahidiwa na Rais wa serikali ya awamu ya tano,Dk.John Pombe Magufuli kwa kila Kijiji kupatiwa shilingi milioni hamsini,ni vyema vikundi vyote vilivyoundwa wilayani hapa kutosubiri fedha hizo na badala yake vifungue akaunti benki,kuchagua viongozi pamoja na kuanza kufanyakazi mara moja na hiyo ndiyo sifa pekee ya kupata fedha hizo.

  “Tuliimba sana kipindi kile kuna milioni hamsini inakuja kweli si kweli…ile milioni hamsini haitagawiwa kama njugu,bali ni kwenye vikundi kama vile kikundi cha Kaloleni kimekaa vizuri nadhani mama atakisemea vizuri sana sitaki kukisemea”alifafanua Mtuka.

  Kwa mujibu wa mbunge Mtuka kikundi cha Kaloleni kimekaa kisayansi,kina viongozi,kina mikakati na wameshaanza kazi kwa kufungua akaunti,kuchagua viongozi na waanze kufanyakazi mara moja hata kama kwa kuchechemea.

  Mbunge wa jimbo la Manyoni mashariki,Bwana Emmanueli Mtuka akifafanua juu ya upatikanaji wa shilingi milioni 50 za JPM.


  Hata hivyo mbunge huyo alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa vikundi vya vijana pamoja na akina mama vya Manyoni waige mfano ulioonyeshwa na kikundi cha Kaloleni ili navyo visisubiri kuwezeshwa na badala yake vianze kufanyakazi haraka iwezekanavyo kwani ndiyo sifa pekee ya kupata fedha hizo.

  Awali katika taarifa ya wanakikundi cha umoja wa vijana wa CCM(UVCCM) ilieleza mafanikio waliyopata kuwa ni pamoja na cherehani nne,jora tano za vitambaa na mashsine mbili za kufyatulia matofali na akiba benki ya shilingi 150,000/=.
  Kuhusu changamoto wanakikundi hao walisema kwamba licha ya mafanikio hayo lakini kikundi hicho kinakabiliwa pia na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa fedha za kununulia vitendeakazi  vya kikundi hicho.

older | 1 | .... | 1157 | 1158 | (Page 1159) | 1160 | 1161 | .... | 3272 | newer