Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

WAFANYAKAZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WATOA MSAADA HOSPITALI YA MWANANYAMALA KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

$
0
0
Meneja wa PPF Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa (katikati) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali Caroline Hanne Van, Raia wa Denmark kwa niaba ya watoto wawili (kitandani) waliodaiwa kuokotwa jana maeneo ya Mbezi Beach na kufikishwa hospitalini hapo leo asubuhi, wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo Machi 8, 2016. Kushoto ni Emel Kudahl Christensen na wa tatu (kulia aliyekaa) ni Emma Nikoline Wennberg, wauguzi wa kujitolea kutoka nchini Denmark. Picha na Mafoto Blog
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya Watoto wachanga/Njiti, wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakigawa vitu mbalimbali kwa wagonjwa wazazi waliolazwa kwenye Wodi ya Watoto wachanga/Njiti, wakati Wafanyakazi wa Mfuko huo walipofika Hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Wazazi na watoto ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo.

WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI PAMOJA NA WAFANYABISHARA WADOGO WATAKIWA KUSHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA MADINI MERERANI

$
0
0
kamishina wa madini kanda ya kaskazini Elius Kayandabila akiwa anaongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya maandalizi ya maonyesho ya madini na vito yanayotarajiwa kuanza hapo kesho ndani ya mji mdogo wa mererani

Na Woinde Shizza,Arusha
WACHIMBAJI wa madini ya vito nchini wametakiwa kushiriki katika maonyesho ya wachimbaji wadogo wa madini ili kuweza kutumia fursa hiyo ya kuuza na kupanua wigo wa kupata masoko ya ndani na nje ili kuweza kukuza uchumi wao na pato la taaifa.

Hayo yameelezwa leo na kamishina wa madini kanda ya kaskazini Elius Kayandabila wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya maonyesho hayo yanayotarajiwa kuanza kesho march 9 hadi kumi katika mji mdogo wa mererani uliopo mkoani Manyara.

Hata hivyo amesema kuwa lengo haswa ni kuonyesha madini hayo ya wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kupata fursa mbalimbali ikiwemo kuwakutanisha na wafanyabiashara wakubwa wa ndani ya nchi ambapo maonyesho hayo yatawasaidia pia kupata masoko kwa urahisi.

Aidha ameongeza kuwa wachimbaji zaidi ya 50 watashiriki maonyesho hayo ya madini katika mji mdogo wa marerani ambapo hii ni kwa mara ya kwanza maonyesho hayo kufanyika eneo hilo ,ambapo alifafanua kuwa maonyesho haya pia ni moja ya maandalizi ya maonyesho makubwa ya kimataifa ya vito na madini ambayo hufanyika kila mwaka mjini Arusha .

Kayanda bila aliwataka wachimbaji hao kuweza kutumia fursa hiyo ya maonyesho haya ili kuweza kujifunza na kupata masoko ya ndani na nje kwa uhakika huku akiwasihi wakazi wa jiji la arusha pamoja na mkoa wa manyara kujitokeza kwa wingi kuangalia aina mbalimbali za madini zinazopatikana hapa nchini.

Aidha pia alitumia fursa hiyo kuwasihi wafanya biashara wadogo na wakubwa ambao wanafanya biashara ya madini kujitokeza kwa wingi katika maonyesho haya ili kuweza kupata madini hayo kwa bei nafuu na kuweza kufaamiana zaidi na wachimbaji wadogo pamoja na wafanyabiashara wadogo wa madini.

Wakinamama Jijini Arusha watoa msaada Gereza la Kisongo

$
0
0
Sehemu ya wakinamama wakazi wa Jiji la Arusha, walipotembelea Gereza kuu la kisongo Mkoani humo, wakiwa na mahitaji mbalimbali ikiwa ni zawadi kwa ajili ya Wafungwa waliopo kwenye Gereza hilo, wakati wa kusherehekea Maadhimisho ya siku ya Wanawake Dunia wakiongozwana Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Viola Lazaro. Picha zote na Mahmoud Ahmad, Arusha.

Ninawatakia wanawake wenzangu‎ Ulimwenguni kote, Heri ya Siku ya Mwanamke-MJ.

$
0
0
Monica Joseph
 Mmiliki wa  Kampuni ya Monfinance Investment
 Group na Muwakilishi  wa Philips Tanzania.
"Wanawake Tunapashwa Kuona Jinsia yetu kama rasilimali na sio Dhima". ( Women should view their gender as a resource rather than a liability) - MJ.

Ningependa kutumia fursa hii kama Dada, Mke, Mama, mfanyakazi, Mwanaharakati na mjasiliamali kuwapongeza wanawake wote kwa kuadhimisha siku hii muhimu ya kuwaenzi wanawake wote ulimwenguni. 

Historia ya Maisha yangu, ni kielelezo cha maisha ya wanawake wengi ulimwenguni wanaopitia changamoto mbalimbali.‎ Nililelewa katika mazingira kandamizi ya Jinsia ya kike-kwenye jamii ambayo mtoto wa kiume alipewa nafasi ya kipekee katika masuala mbalimbali dhidi ya mtoto wa kike...Kwa mfano kipaumbele cha kupata elimu walipewa watoto wa kiume wakati watoto wa kike wakitarajiwa kushughulika na kazi za nyumbani, kupika,kuchota maji na kusaidia shughuli za kilimo na hatimaye kuolewa. 

Bibi yangu (Apumzike kwa Amani) alikuwa mhanga wa mfumo huo kandamizi. Kwa taabu alizopita Bibi yangu alijiwekea nadhiri kwamba Mjuu wake, hatopitia shida alizopitia yeye...na hivyo siku zote alikuwa akiniasa kwamba "Niyu (jina langu la nyumbani),Unaweza kila kitu kinachofanywa na mtoto wa Kiume". Aliniimarisha kifikra na kiakili. 

Na siku zote alikuwa na msemo wake "Niyu Kasome, Ukasome umshinde Babu yako, Usije kuwa unanyanyasika kama sisi"- ushauri wake ndio ulikuwa dira yangu ya maisha ambapo nilisoma kwa bidii na kufanikiwa kuhitimu shahada ya uzamili katika masuala ya fedha kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Uingereza. 

Hadi hivi leo, sauti ya Bibi haijakoma masikioni mwangu, sijaacha kutafuta elimu na maarifa ya masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo katika jamii...ni kwa sababu hiyo nilipata mafunzo ya muda mfupi ya uongozi na majadiliano kutoka Chuo kikuu cha Harvard cha nchini Marekani. Nitaendelea kuitafuta Elimu na pia kusaidia wenzangu, sababu naamini moja ya njia ya Mwanamke kujikomboa katika ukandamizaji wa kijinsia ni kuongeza kiwango cha elimu kwake mwenyewe na kwa wanawake wenzake. 

 Waswahili wana msemo usemao maisha ni shule.....msemo huu nimeuishi katika maisha yangu ya baada ya masomo. Nimefanya kazi katika mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi. nimefanya kazi na taasisi ya ISHI iliyokuwa inashughulikia masuala ya Ukimwi, baada ya hapo nimefanya pia katika kampuni‎ ya Philips Medical Systems ya Uholanzi na baadaye nimefanya kazi kampuni ya mawasiliano ya Maktech. Kwote nilipopita nimekumbana na changamoto mbalimbali zilizohusiana na jinsia yangu.

 Utekelezaji wa majukumu yangu ulinilazimu kuwa na mikutano na watu mbalimbali Serikalini na kwenye taasisi za fedha ambapo watu niliokuwa nakutana nao ni wanaume ambao baadhi yao wamekuwa na mawazo ya mfumo dume yaliyojaa dharau na manyanyaso. Wengine kwenye fikra zao wanadhani mwanamke yeyote mwenye mafanikio, iwe kwenye biashara, siasa, ajira, lazima anabebwa na wanaume.‎ Wakiona mwanamke amefanikiwa tu, utasikia..huyu 'hawala wa fulani'. hii ni dhana potofu na inayolenga kumdhalilisha na kumnyanyasa mwanamke. Mimi binafsi sikukubali kuyumbishwa na watu wenye mawazo ya aina hiyo. 

Kila nilipokumbana na changamoto za aina hiyo nilipata hamasa ya kufanya kazi kwa bidii zaidi na kuwadhihirishia kwamba NINAWEZA, ilee sauti ya bibi ndioa ilikuwa ikinitia hamasa zaidi na zaidi na hatimaye kuniwezesha kufanya vizuri hadi kufikia kuaminiwa kupewa majukumu makubwa zaidi kama vile Mkurugenzi Mkuu katika kampuni ya Mokasi Medical Systems ambayo ni wakala wa kampuni ya Philips ya Uholanzi. Hasama hiyo iliniwezesha pia kuanzisha kampuni yangu inayotoa Huduma za kifedha - Monfinance Investment Group Ltd. 

Mbali na shughuli hizo nimeweza pia kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya FINCA Microfinance Tanzania. Kwa ujumla siku zote za maisha yangu nimejihusisha na harakati za kupigania haki za wenye shida na mahitaji katika jamii kutokana na msingi niliojengewa na bibi yangu wa kukataa unyonge na kusaidia wanyonge. Hurka hiyo ndio ilipelekea ajira yangu ya kwanza kuwa kwenye taasisi ya uhamasishaji wa masuala ya ukimwi ya ISHI. Niliguswa kujihusisha na kampeni hizo kwasababu binafsi nimepoteza ndugu, jamaa na marafiki kutokana na ugonjwa huo. Mbali na ISHI,nimekuwa nikijihusisha na kampeni ya kuzuia mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) iitwayo IMETOSHA.

 Ni jambo la udhalilishaji uliopitiliza kuwakata binadamu wenzetu viongo vyao kwa imani za kishirikina. Pia nimeshiriki kwenye uhamasishaji wa magonjwa yasiyojulikana (Rare diseases).‎ Tunaposherehekea siku ya Mwanamke duniani rai yangu kwa wanawake wenzangu, tushirikiane, tusaidiane, tupeane moyo na tuwezeshana ili tufikie lengo letu la usawa 50/50 kufikia mwaka 2030. Kila mwanamke atimize wajibu wake kwa kujitambua na kuhakikisha haki yake hainyongwi. ‎‎

Mimi nimejitambua, ninasimamia haki yangu, na wala siipiganii, ni yangu, Jinsia yangu hainitofautishi kiutendaji na jinsia ya kiume. Ninachoangalia ni Mchango wangu katika maendeleo ya Uchumi, jamii na familia na sio Jinsia yangu. Ninachotambua katika jinsia yangu ni kuwa mimi ni Dada, Mama, rafiki, na Mke. Mengine yote,nipo sawa na wote, wanaume na wanawake.‎ Happy Women's Day 2016.
a7caeb96fbdcd21385508290de4f359f"Wanawake Tunapashwa Kuona Jinsia yetu kama rasilimali na sio Dhima".  Women should view their gender as a resource rather than a liability) - MJ. 


WAZIRI MBARAWA AWATAKA TBA KUZINGATIA THAMANI YA FEDHA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiongea na Menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania - TBA (hawapo pichani) wakati alipotembelea Ofisi za Wakala huo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiongea na Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania –TBA kutoka mkoa wa Pwani na Dar es salaam katika mkutano wa Wakala huo uliofanyika Karimjee jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia), akiongea na wafanyakazi wa TBA kutoka mkoa wa Pwani na Dar es salaam katika mkutano wa Wakala huo uliofanyika jijini Dar es salaam. Katikati ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifuatilia.

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA TANO WA BUNGE LA AFRIKA YA MASHARIKI.

$
0
0
  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashriki, Kanda na Kimataifa, Balozi Augustino Mahiga akiapa kuwa Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki katika Mkutano wa Tano wa Bunge hilo uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim majliwa kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Machi 8, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akihutubia Mkutano wa  Tano wa Bunge la Afrika ya Mashariki kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Machi 8,2016
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge Job Ndugai wakiwa katika picha ya pamoja na Spikia wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Daniel Fredrick Kadega (katikati) baada ya kuhutubia Mkutano wa  Tano wa Bunge la Afrika ya Mashariki kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es salaam Machi 8,2016.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema tatizo la rushwa barani Afrika limesababisha bara hilo lipoteze dola za Marekani bilioni 150 kila mwaka.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Machi 8, 2016) wakati akihutubia wajumbe wa mkutano wa tano wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linaloendesha vikao vyake jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulioanza Machi 6, utamalizika Machi 18, mwaka huu.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema rushwa imechangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya Jumuiya hiyo. "Rushwa yaweza kuwa kwa njia kuhonga fedha, kupata fedha kwa kula njama, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, ama kwa njia za vitisho," alisema.

"Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Afrika (AU), rushwa na urasimu vimeainishwa kuwa ni vikwazo vikubwa vinavyochangia kuchelewesha ufanyaji wa biashara kwenye mipaka ya nchi za Jumuiya yetu," alisema.

Amesema sekta binafsi inachukuliwa kama injini ya maendeleo na ukuaji wa uchumi na akatumia fursa hiyo kuipongeza jumuiya ya wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kwa kuandaa kanuni za kiutendaji  ambazo zimelenga kuhamasisha uadilifu kwenye ufanyaji biashara unaozingatia haki za binadamu, sheria za kazi, utunzaji mazingira na vita dhidi ya rushwa.

Akizungumzia kuhusu uondoaji wa vikwazo visivyohusisha kodi (non-tariff barriers) kama njia mojawapo ya kuimarisha biashara kwenye jumuiya hiyo, Waziri Mkuu alisema kwa upande wa Tanzania, vizuizi vya barabarani kwenye barabara kuu ya Kaskazini vimepunguzwa kutoka 50 hadi vitano.

Alivitaja vizuizi vitano vilivyobakia kuwa ni vile vilivyopo kwenye mizni ya Mikese (Morogoro), Nala (Dodoma), Njuki (Singida), Mwendakulima (Shinyanga) na Nyakahura (Kagera).

"Sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya uondoaji wa vikwazo visivyohusisha kodi ilipitishwa Machi 2015 na sasa hivi inaendelea kusainiwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pamoja na mambo mengie, nia ya sheria hii ni kuondoa vikwazo vinavyosababisha uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, kurahisisha sheria za biashara ndani ya Jumuiya yetu," alisema.

Akizungumzia kuhusu miradi ya uwekezaji ya Jumuiya hiyo, Waziri Mkuu alisema miradi ya ujenzi wa barabara inahitaji kiasi cha dola za marekani bilioni 20; ukarabati na upanuzi wa njia za reli unahitaji dola za marekani bilioni 30; uendeshaji wa mashirika ya ndege na viwanja vya ndege unahitaji dola za marekani bilioni 15; uendelezaji bandari na usafiri wa majini unahitaji dola za marekani bilioni 10; utekelezaji wa miundombinu ya nishati inahitaji dola bilioni 5 ambavyo kwa pamoja vinahitaji dola marekani bilioni 80.


Alisema kuwepo kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi ndani ya jumuiya hiyo, kunaifanya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhesabika kuwa ni jumuiya yenye nguvu kubwa ya kiuchumi barani Afrika.

tahadhari ya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini kuanzia usiku wa tarehe 08-03-2016 hadi 09-03-2016: warning information on heavy rain over some areas of the country from tonight 08-03-2016 to 09-03-2016.

TIZA JOTO LA ASUBUHI JUMATANO MARCH 9


SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Balozi Seif aweka jiwe la msingi ujenzi wa skuli ya ghorofa kwarara

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Skuli ya Ghorofa na Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Tumaini hapo Kwarara Wilaya ya Magharibi.
Msimamizi wa Ujenzi wa Skuli mpya ya Ghorofa ya Kwarara Mhandisi Ali Mrabouk akimfahamisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ramani ya ujenzi wa majengo ya Skuli ya Ghorofa ya Kwarara pamoja na Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Tumaini.
Mandhari ya eneo linalojengwa Skuli ya Ghorofa kwarara pamoja na Kituo cha Habari na Mawasliniano cha Tumaini Wilaya ya Magharibi “B” unaofadhiliwa kwa pamoja kati ya mashirikia matatu ya Good Neighbors, Shirika la Habari la Korea Kusini {SBS } pamoja na Shirika la Maendeleo ya Korea Kusini KOICA.
Balozi wa Korea ya Kusini Nchini Tanzania Bwana Songo akitoa salamu kwenye hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Skuli ya Ghorofa pamoja na Kituo cha Habari na Mawasiliano zinazojengwa kwa msaada wa mashirika ya Nchi hiyo. Picha na – OMPR – ZNZ.

MGODI WA BULYANHULU WAALIKA WANAWAKE KUJIONEA UCHIMBAJI MADINI YA DHAHABU CHINI YA ARDHI

$
0
0
Mfanyakazi wa mgodi wa kuchimba dhahabu wa Bulyanhulu, unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, akiwa na baadhi ya akina mama sehemu ya uchimbaji chini ya ardhi (underground mining), wakati akina mama wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo na wafanyakazi wa kike walipotembelea ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake Duniani, leo Machi 8, 2016. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

KATIKA kuadhimisha kilele  cha siku ya Wanawake Duniani leo Machi 8, 2016, akina mama wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, unaomilikiwa na kampuni ya Acacia,huko wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga, wao walitembelea na kuona shughuli za uchimbaji madini chini ya ardhi (Underground operations).

Akina mama hao kutka kada mbalimbali za vikundi vya wajasiriamali, wakulima, na viongozi wa dini, walifanya ziara ya kutembeela na kujionea shughuli za uchimbaji madini chini ya ardhi kiasi cha kilomita 2 kutoka uso wa ardhi, walieleza kufurahishwa kwao na kusema hata wao wanaweza.

Pamoja na maeneo waliyoyatembelea, walijionea mashine za kuchironga miamba, pamoja na karakana (gereji) ya kutengeneza magar na mashine zinazotumika kwenye eneo hilo. Ziara hiyo iliwachukua takriban masaa matatu (3), na bila kuchoka walikamilisha  ziara hiyo na wote walikuwa katika hali nzur nay a furaha.

Katika tukio linguine, Mgodi huo ulimpatia kila mshiriki wa ziara hiyo, mche moja wa matunda ili wakapande kwenye maeneo wanayoishi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya mgodi kuhifadhi mazingira kwenye maeneo jirani na mgodi huo.

Siku ya wanawake Duniani, huadimishwa Machi 8 ya kila mwaka ili kuelezea changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake na kutafuta majawabu yake.
 Mama huyu ambaye ni sister wa kanisa Katoliki, alikuwa miongoni mwa wanawake waliotembelea mgodi huo chini ya ardhi.
 Ramadhani Chura, (kulia), mchimbaji wa madini chini ya ardhi, akiwapa maelezo akina mama hao umbali wa kilomita 2 kutoka uso wa ardhi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAKALA YA SHERIA: SHERIA HAIKATAZI KUFUNGA NDOA IWAPO MMOJA WA WANANDOA HAYUPO

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.

Mtu  mmoja  aliyeko  Zurich  alipiga  simu  akiuliza  swali  ambalo  ni  kichwa  cha  haya  makala .   Yeye  yuko  zurich  lakini  anataka  kufunga  ndoa  na  mwanamke  aliyeko  Tanzania  bila  kulazimika  kurudi  nchini. Anataka  afunge  ndoa  akiwa  hukohuko zurich  na  mwanamke  akiwa  Tanzania .

 Alisema  huko  aliko  jambo hilo linaruhusiwa  kisheria  ila  wasiwasi  wake  ni  kama  hata  Tanzania  jambo  hilo linaruhusiwa.  Kabla  ya  kutizama jambo  hilo  kisheria upo  umuhimu  pia wa  kutizama  baadhi  ya  mambo  kuhusu  ndoa.

1.NINI  MAANA  YA  NDOA.

Kwa  mujibu  wa  kifungu  cha  9( 1 )  cha  sheria  ya  ndoa  sura  ya  29,  ndoa imetafsiriwa  kama  muungano  wa  hiari  kati  ya  mwanamke  na  mwanaume   wenye  lengo  la  kudumu  maisha  yao  yote. 

2.  SHERIA  INASEMAJE  KUHUSU WAZAZI   KUCHAGUA  WACHUMBA. 

Katika  maana  ya  ndoa  kuna  neno  hiari. Hili  ni  jambo  la  kwanza  katika  ndoa. Maana  yake  ni kuwa kusiwe  na  kulazimisha,  ulaghai,  udanganyifu n.k. Hata  kurubuni  kunakolenga  kuondoa  hiari  ya  mtu   nako  ni  kulazimishwa. Pia   wazazi  kuwachagulia  vijana  wao  wachumba  na  kuwashinikiza  kuwaoa  au  kuolewa  nao  nako  ni kuondoa  hiari  ya  wahusika.

 Si  kosa  mzazi  kuona mchumba  kwa ajili  ya kijana  wake isipokuwa  ni  kosa akitumia  nafasi hiyo   kulazimisha/kushinikiza  kufungwa  ndoa. Haya  ni  kwa  mujibu  wa  kifungu  cha  16  cha  sheria  ya  ndoa.

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI JUMANNE MACHI 8, 2015

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: FM Academia - Dunia kigeugeu

RAIS WA VIETNAM, MHE. TRUONG TAN SANG AWASILI TANZANIA

$
0
0



Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe wakiwapungia mkono viongozi mbalimbali waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akimkaribisha Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (katikati) mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere akiongozana na mkewe 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na baadhi ya viongozi waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa

Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akiwasalimia baadhi ya Watanzania na Wavietnam waliokuja kumpokea mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere 8 Machi, 2016 Jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa .


TAASISI YA TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) YAANDAA KONGAMANO LA KUTOA AHADI YA UWIANO SAWA WA KIJINSIA

$
0
0
Mgeni Rasmi ,Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk .Ashatu Kijaji akitoa hotuba yake katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia.
Mwenyekiti wa Tanzania Women of Achievement , Sadaka Gandi akiongea na washiriki wa kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili.Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia. 
Rais wa Tanzania Women of Achievement Irene Kiwia akitoa hotuba ya ufunguzi katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili.Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) yenye kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia. 
Mmoja wa wazungumzaji wakuu Prof Slyvia Kaaya akichangia mada katika mjadala wa uwiano sawa wa kijinsia pembeni yake ni Bi Mary Rusimbi aliyekuwa mkurungezi mtendaji wa BOT ,na kulia kwake ni Mwenyekiti wa TAWLA Aisha Bade ,anayefuatia ni Mtendaji Mkuu wa WOMEN FUND TANZANIA Mary Rusimbi katika kongamano la shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake dunia Tarehe 8 Machi lililofanyika jijini katika hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam mapema jumapili iliyopita .Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Tanzania women of Achievement(TWA) kukiwa na kauli mbiu ya Kutoa uwiano sawa kijinsia .

Waandishi wa habari wameaswa kuandika habari zenye tija kwa taifa.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali kifungua semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuandika na kutoa habari za sekta za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.
  Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Victoria Msina akimkaribisha Mkurugenzi wa BoT, Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali wakati wa ufunguzi wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika na kutoa habari za za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.

 Baadhi ya washiriki wa semina wakimskiliza Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali wakati wa ufunguzi wa semina inayofanyika mjini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika na kutoa habari za za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa semina inayofanyika mjini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi hao kuandika na kutoa habari za za uchumi, biashara na fedha maendeleo yenye tija kwa taifa.


Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Wanahabari nchini wameaswa kutumia taaluma yao vema katika kuhabarisha umma kuhusu masuala ya uchumi, biashara na fedha kwa lugha ambayo wananchi wa ngazi mbalimbali wataweza kuelewa kirahisi ili waweze kuchangia katika maendeleo yenye tija kwa taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali alipokuwa akifungua semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kuandika na kutoa habari za sekta ya uchumi na fedha.

“Benki Kuu ya Tanzania inatambua na inathamini sana mchango mkubwa unaofanywa na magazeti, vituo vya televisheni na radio kwa kutenga nafasi maalum kwa ajili ya habari za fedha na uchumi na hasa zinatolewa na Benki Kuu” alisema Bw. Richard.

Katika kuhakikisha vyombo vya habari vinatoa elimu katika masuala ya fedha na uchumi, Bw. Richard amesema kuwa BoT imechukua jukumu la kuwajengea uwezo wanahabari kila mwaka ili kuwaongezea uelewa wao kuhusu majukumu na kazi za Benki hiyo na mchango wake katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Malengo mengine ya semina hiyo ni kuchochea na kukuza ari ya wanahabari katika kuandika habari za uchumi  na fedha, kutafsiri   na kuchambua taarifa mbalimbali za uchumi na fedha zinazotolewa na taasisi mbalimbali, kuwafahamisha wanahabari   masuala yanayoendelea katika uchumi wa Tanzania na wa dunia, mwelekeo wa uchumi na masuala ya fedha katika siku zijazo na kuimarisha uhusiano mzuri wa kikazi uliopo baina ya vyombo vya habari,  wanahabari na Benki Kuu.

Zaidi ya hayo, Bw. Richard ameongeza kuwa Benki Kuu kama taasisi, inajukumu la kujifunza namna vyombo vya habari vinavyofanya kazi na mahitaji yao katika kuandaa na kuwasilisha taarifa na habari za uchumi na fedha.

Aidha, Bw. Richard amesema kuwa ukuaji wa uchumi nchini unaoendelea sasa unatokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali na BoT katika kutekeleza sera za uchumi na fedha pamoja na usimamizi wa uhakika wa sera hizo.

“Kadiri uchumi unavyokua na kadiri mazingira ya biashara yanavyoendelea kuvutia wawekezaji, mahitaji ya taarifa na habari sahihi na kwa wakati kuhusu uchumi wa nchi yetu ikiwa ni pamoja na masoko ya fedha, uchumi wa kanda na dunia kwa ujumla yanaongezeka sambamba na umuhimu wake” alisisitiza Bw. Richard.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa semina hiyo kwa niaba ya wanahabari hao Ezekiel Kimwaga kutoka gazeti la Raia Mwema ameupongeza uongozi wa BoT kwa kufikisha miaka 50 na kuishukuru benki hiyo kuthamini na kutoa fursa ya semina hiyo kwa wanahabari kila mwaka ambayo inawaongezea uelewa katika masuala ya uchumi na fedha.

Semina hiyo ya siku nne inajumuisha mada mbalimbali zinazowasilishwa na wataalam kutoka BoT ni pamoja na kuzijua kurugenzi ambazo zinazohusika na masuala ya uchumi, biashara na fedha ambazo ni Utafiti na Sera za Uchumi, Masoko ya Fedha, Usimamizi wa Mabenki, Bodi ya Bima na Amana, Mifumo ya Malipo ya Taifa na Huduma za Kibenki.

Mada nyingine katka semina hiyo ni kuzijua alama za usalama zilizopo katika fedha, dawati la malalamiko ya wateja wa mabenki pamoja na kuzijua kazi za matawi ya Benki Kuu ya Tanzania.
Mwisho.

PROF. MBARAWA; TUMIENI DATA CENTRE KUTUNZA TAARIFA ZENU

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akionesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mfumo wa ufatiliaji wa kielektroniki katika jengo la kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili mwaka huu jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitizama kwa karibu mtambo wa kuratibu usalama katika kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) jijini Dar es Salaam. Kituo hicho cha kwanza kujengwa nchini kitatunza taarifa za Serikali na sekta binafsi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda wakati akikagua kituo cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka sekta ya Mawasiliano Eng. Peter Mwasalyanda wakati akikagua kituo hicho cha kutunza taarifa mbalimbali (data centre) kitakachoanza kazi rasmi mwezi Aprili jijini Dar es Salaam.

……………………………………………
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amezitaka taasisi za Serikali na binafsi kukitumia kituo cha kisasa cha kuhifadhi taarifa (data centre) kutunza taarifa zao ili kuzihakikishia usalama na uhakika wa kuzitumia wakati wote.

Akizungumza baada ya kukagua kituo hicho kinachosimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sekta ya Mawasiliano amesema asilimia 75 imetengwa kwa ajili ya kutunza taarifa kutoka sekta binafsi na asilimia 25 itatunza taarifa za Serikali.

Waziri Mbarawa amezitaka taasisi za Benki, Simu, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala wa Serikali Mtandao (e-GA) kutembelea kituo hicho kujifunza mifumo ya uhifadhi taarifa na kujiunga ili kunufaika na huduma za kituo hicho.

Amesema huduma ya mtandao katika kituo hicho imeimarishwa kutokana na kuunganishwa na mkongo wa taifa na hivyo itawarahisishia wateja wake kuweka na kuchukua taarifa kwa haraka.

Kituo hicho ambacho ni cha kwanza kujengwa katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ni fursa mpya kwa wafanyabiashara na wadau mbalimbali wenye taarifa nyingi kuzihifadhi na kuzitumia wanapozihitaji kinalimikiwa na Serikali.

DONDOO ZA HABARI MAGAZETI LEO.

MKUU WA MKOA WA MTWARA MH. HALIMA DENDEGU AZINDUA RASMI SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2016 KATIKA UWANJA WA MASHUJAA.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendegu akitoa Hotuba yake kwa wakazi wa Mtwara na Kuzindua Rasmi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2016 linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la  OXFAM Tanzania .
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh. Fatma Ally akizungumza na wakazi wa Mtwara,wageni mbalimbali na wadau pia kufungua rasmi sherehe hizo wakati wa Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani na Uzinduzi wa Shindano la Mama wa Chakula kwa Mwaka 2016
 Meneja wa Programu ya Uwazi na Utawala Bora kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Bi. Betty Mlaki akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkazi wa Shirika Hilo Jane Foster wakati wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani na uzinduzi rasmi wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2016.Mamia ya wakazi wa Mtwara wakiwa katika Sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani na uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwa mwaka 2016, katika Uwanja wa Mashujaa.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>