Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MWAKILISHI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI UNHCR ANAYEMALIZA MUDA WAKE BI. JOYCE MENDS-COLE IKULU JIJINI DAR LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR anayemaliza muda wake Bi. Joyce Mends-Cole Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UNHCR anayemaliza muda wake Bi. Joyce Mends-Cole Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

GLOBAL PEACE FOUNDATION TANZANIA celebrates International Women’s Day

$
0
0
The International Women's Day is celebrated in many countries around the world. It is a day when women are recognized for their achievements without regard to divisions, whether national, ethnic, linguistic, cultural, economic or political. International Women's Day first emerged from the activities of labour movements at the turn of the twentieth century in North America and across Europe. 
Since those early years, International Women's Day has assumed a new global dimension for women in developed and developing countries alike. The growing international women's movement, which has been strengthened by four global United Nations women's conferences, has helped make the commemoration a rallying point to build support for women's rights and participation in the political and economic arenas.

 International Women’s Day (IWD) is now an official holiday in countries throughout the world from Afghanistan to Armenia and Uzbekistan and Zambia. The tradition sees men honouring their mothers, wives, girlfriends, colleagues, etc with flowers and small gifts. In some countries IWD has the equivalent status of Mother’s Day where children give small presents to their mothers and grandmothers. 
On 6th March 2016, Global Peace Foundation Tanzania participated the IWD   celebrations at Serena Hotel, Dar Salaam, the event was organized by Vital Voices Global Partnership,  the Country Director, Martha Nghambi was one of the speaker during the event.

Global Peace Foundation Tanzania,  a non-profit organization dedicated to promoting an innovative and values based approach to peace building,  its  a chapter of a premier international non-profit, Global Peace Foundation (GPF), headquartered in Washington, D.C. 
GPF engages a global network of public and private sector partners in more than 20 countries across Africa, Asia, Europe and the Americas to implement programs and activities that transform education, build youth leadership, strengthen community-based development efforts, and foster a culture of service and volunteerism. 
With chapters in Kenya, Nigeria, Uganda and Tanzania, GPF maintains a strong presence in Africa and has a successful track record of promoting peaceful coexistence and mitigating extremist and sectarian violence. 
During the 2015 general elections, GPF Tanzania in collaboration with Inter Religious Council For Peace Tanzania (IRCPT), conducted Peace Dialogue and a successful pre-election Social media campaign, Amani Kwanza, to encourage peaceful participation of youth, and also In July 2015,  GPF Tanzania gathered about 200+ Leaders and Former African Presidents to the Global Peace Leadership Conference held at Melia Hotel, Zanzibar,  and about 800+ Youth from East Africa including  Colleges and Universities’ Presidents,  for  the East African Youth Summit  that held at Zanzibar Beach Resort, the theme was “Promoting Peace, Security and Sustainable Development in the East Africa Region: A Call to Moral and Innovative Leadership “


 Country Director, Global Peace Foundation Tanzania Martha Nghambi speaks out during the International Women's Day held at the Serena Hotel in Dar es salaam over the weekend.

 GPF Tanzania representatives posed with their partners, Tanzania Women Interfaith Network (TWIN)

 Masked participants celebrate the day  during the International Women's Day held at the Serena Hotel in Dar es salaam over the weekend.
 A cross-section of participants  during the International Women's Day held at the Serena Hotel in Dar es salaam over the weekend.
 Super model Tausi Likokola was one of the high profile participants  during the International Women's Day held at the Serena Hotel in Dar es salaam over the weekend.
 Country Director, Global Peace Foundation Tanzania Martha Nghambi (left) pose with stakeholders during the International Women's Day held at the Serena Hotel in Dar es salaam over the weekend.

TEASER JOTO LA ASUBUHI LA EFM 93.7 MARCH 8 JUMANNE

Msaada kwa ndugu yetu Ahmed Albaity

MABALOZI NA UPASUAJI WA MOYO WATEMBELEA Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam

$
0
0
Naibu Balozi wa Ujerumani, John Reyels, (kulia) akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Katika hoapitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam, Profesa Mohamed Janabi (kushoto) baada ya naibu balozi huyo kuwatembelea watoto waliofanyiwa upasuaji wa moyo jana. Katikati ni Rais wa Rotary Club  Dar es Salaam, Zainul Dossa.
 Naibu Balozi wa Israel, Nadar Peldman akizungumza na madaktari, wauguzi na wadau mbalimbali wa sekta ya afya baada ya kuwatembelea watoto waliofanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Muhimbili. Jana watoto wanne walifanyiwa upasuaji na leo watoto sita wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji kwenye taasisi hiyo.  
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi, akishukuru mabalozi, wawakilishi wa BAPS Charities, madaktari kutoka Israel na wadau wengine kwa misaada mbalimbali ambao wamekuwa wakisadia kufanikisha shughuli za upasuaji wa moyo kwenye taasisi hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa  shirika lisilo la kiserikali la Save  Child’s  Heart (SACH), Simon Fisher kutoka nchini Israel akizungumza leo baada ya kufuatilia shughuli ya upasuaji wa watoto ambayo imeanza jana katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Muhimbili. Kushoto ni Rais wa Rotary Club nchini Tanzania, Sharmila Bhatt. 

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Bakari akiwashukuru wadau hao wakiwamo mabalozi kutoka Israel na Ujerumani na wadau wengine kwa misaada mbalimbali wanayoitoa katika taasisi hiyo. Leo Profesa Bakari amewataka madaktari na wauguzi wa taasisi hiyo kutumia vizuri nafasi mbalimbali za mafunzo kutoka kwa wadau hao wa afya.

EAC SECRETARY GENERAL UNVEILS MOBILE APPLICATION TO SCALE-UP OUTREACH AND SENSITIZATION ON EAC INTEGRATION

$
0
0

The Secretary General of the East African Community, Amb. Dr. Richard Sezibera, has unveiled an EAC Mobile Application whose main aim is to disseminate news, information and reports on a timely basis about the current state of affairs and development in the EAC. 
Unveiling the mobile application version 3.2  at the 4th EAC Secretary General’s Forum in Dar es Salaam, Tanzania, Amb. Sezibera hailed the EAC Youth Ambassadors’ Platform, the architect of the application, for the brilliant innovation. 
The Secretary General singled out Otim Brian Joseph, Jacob Eyeru, Leku Dennis and Esemu Herbert from the EAC Youth Ambassadors Platform-Uganda Chapter for developing the first-ever EAC mobile application product and making accessible globally. 
The Secretary General disclosed that the application, also known as EAC in the Palm,was free, open and easily accessed mobile platform dedicated to easing sharing and disseminating EAC related information as well as tracking reports on development programs in the region. “This will increase information outreach and sensitization on the EAC integration process in real time,” said Amb. Sezibera. 
At the launch ceremony, Mr. Otim, the Head of the EAC Mobile Application Project at the EAC Youth Platform, outlined some of the benefits of the product, which include; prompt information outreach to all citizens of the Community and the rest of the world through individual smartphones thus advancing the “one to one” sensitization efforts of the Community; rebranding EAC on the social global network where information on EAC activities as updated on the website is made available to the public on a real time basis through the application; enhanced people-centred integration motive through the interactive chat module embedded in the application, and; increasing the involvement of citizens to informative capacity building discussions regardless of nationality, age, ethnicity, tribe and religion.

The Head of the Corporate Communications and Public Affairs at the EAC Headquarters, Mr. Owora Richard Othieno, is excited that the Secretariat has endorsed the application because “the world today has high-tech information dissemination channels to fast-track market and stakeholder interactions. To this end, technological innovations are being adopted at an unprecedented scale and speed, particularly by over-the-top players and this should be no exception for the EAC Secretariat.” 
Present at the ceremony were; Dr. Ramadhan Mwinyi, Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs, East African, Regional and International Cooperation,Tanzania; Hon. Jesca Eriyo, the Deputy Secretary General (Productive and Social Sectors) at the EAC Secretariat; the German Ambassador to Tanzania and EAC, Amb. Egon Kochanke, and; Mr. Charles Njoroge, Deputy Secretary General (Political Federation).
Mr. Otim Brian Joseph joins Amb. Sezibera, Hon. Jesca Eriyo, German Ambassador to Tanzania and EAC, Amb. Egon Kochanke, and Mr. Charles Njoroge take time out for a photo opportunity.

Zitto Kabwe ndani ya Mikasi na Salama Jabir

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MHE. BALOZI ENG. JOHN WILLIAM KIJAZI KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Eng. John William Herbert Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu jijini Dar es Salaam. Balozi Kijazi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi wakwanza kushoto na Wamwisho kulia ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue pamoja na viongozi Wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Hafla ya kuapishwa Balozi Kijazi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu wakuu na Naibu Katibu Wakuu.
Balozi Kijazi ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India, anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John  Pombe Magufuli ameagana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) anayemaliza muda wake Bi. Joyce Mends-Cole Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amemshukuru kwa kazi kubwa ya kuhudumia wakimbizi kwa kipindi chote alichokuwepo hapa nchini.
Kwa upande wake Bi. Joyce Mends-Cole amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri inayofanywa na Tanzania kuzisaidia nchi zenye matatizo, hususani migogoro ya kisiasa ambayo husababisha watu wake kuwa wakimbizi.
Pia amepongeza kuteuliwa kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, kusaidia usuluhishi wa mgogoro wa Burundi ambao umesababisha idadi kubwa ya wakimbizi kukimbilia Tanzania.
Hata hivyo amesema idadi ya wakimbizi wanaokimbilia Tanzania imepungua kutoka wakimbizi 3,000 waliokuwa wakiingia hapa nchini kwa wiki, wakati Mgogoro wa Burundi ulipoanza hadi kufikia wakimbizi takribani 1,000 wanaingia hapa nchini kwa wiki hivi sasa.
Aidha, Bi. Joyce Mends-Cole amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano alioupata kwa kipindi cha miaka mitatu aliyofanya kazi hapa nchini, na ameahidi kuwa Balozi wa kuitangaza vyema Tanzania.

Gerson Msigwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam


07 Machi, 2016

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, WAKUU WA WILAYA YA ILALA NA TEMEKE WATEMBELEA SHULE ZA MSINGI.

$
0
0
 Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha wamiliki wa Maroli Tanzania(TATOA) na Menejimenti leo iliungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Wakuu wa Wilaya wa Ilala na Temeke kutembelea shule za Msingi za Majimatitu, Mbande na kisongola ili kujionea hali halisi ya shule hizo na kujua changamoto mbalimbali wanazopitia.
 Hii ni katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kuwa watoto wote wanapewa elimu ya msingi bure. Wanachama wataendelea kupatiwa utaratibu wa namna ya kushiriki kuchangia juhudi hizi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha wamiliki wa Maroli Tanzania(TATOA) Mhe. Emmanuel J. Kakuyu akiwa katika picha na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Mbande wakati ujumbe mzito wa TATOA ulipotembelea shule kadhaa za Dar es salaam ili kujionea hali halisi ya shule hizo na kujua changamoto mbalimbali wanazopitia na kujua nini cha kusaidia katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Tano katika Elimu.


Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha wamiliki wa Maroli Tanzania(TATOA) na Menejimenti leo iliungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick na Wakuu wa Wilaya wa Ilala, Raimond Mushi na Mkuu wa Wilaya ya Temeke walipotembelea shule za Msingi za Majimatitu, Mbande na kisongola ili kujionea hali halisi ya shule hizo na kujua changamoto mbalimbali wanazopitia.

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: Samba Mapangala "Marina"

KUMBUKUMBU YA MIAKA MINNE TANGU KUTWALIWA

$
0
0
MAREHEMU JUDICA STEPHANO TERI

22.06.1946  hadi  08.03.2012


Ni miaka minne leo tangu utwaliwe na Bwana.

Kila siku zinapopita tangu utangulie, mkeo mpendwa Janeth, watoto Joan, Linda, Davis na Hillary pamoja na wenzi wao na wajukuu tunakumbuka na kuenzi sana ucheshi, upendo na busara zako.

Ndugu, dada na marafiki wote pia tunakukumbuka kwa mengi mazuri. Kwetu sote utaendelea kuwa nasi milele kiroho na kifkra.
Mungu aendelee kuilaza roho yako mahali pema peponi.


Tunafarijika kuwa baada ya maisha haya kuna ufufuo wa mwili usioharibika (1Wakor. 15: 50 -52)

NIDA YASITISHA MIKATABA YOTE YA WAFANYAKAZI WA MKATABA WALIOKO KATIKA OFISI ZAKE ZOTE

SHUGHULI YA MAWLID YA KUMSIFU MTUME WETU MUHAMMAD (S.A.W) SIKU YA 19/03/2016 SEGEREA MWISHO,DAR

$
0
0
 ASSALAAM ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKATU
Al Madrasat Rahman iliyopo Segerea mwisho,Dar-es-Salaam
.
INAWAALIKA KATIKA SHUGHULI YA MAWLID YA KUMSIFU
MTUME WETU MUHAMMAD (S.A.W) siku 19/03/2016 JItokezi kwa wingi!

Ndugu zetu watukufu wa kiislam Uongozi wa Al Masjid Qubbah na  Madrasat Rahman ya Tabata Segerea Mwisho,Dar-es-salam inawaalika waislamu wote waume kwa wanawake,Masheikh,na Madrasat mbalimbali kuwa siku ya jumamosi ya tarehe 19/3/2016 kutakua na Maulid ya kumswifu bwana Mtume Muhammad (S.A.W) katika viwanja vya madrasat Rahman segerea mwisho. 
 
Kama ilivyoada kuanzia saa nne asubuhi kutakua na maulid ya kina mama mpaka saa kumi alasiri, na baada ya swalatul inshai kutakua na maulid ya jumuiya waume kwa wanawake.Jitokezeni kwa wingi katika shughuli hii,tuuzaje uwanja wa shughuli hii ,kushiriki kwenu ndio mafanikio na baraka ya shughuli hii ya Maulid ya Mtume Muhammad(S.W.A)
 Karibuni sana.INSHAALLAH

WABILLAH TAUFIQIH mawasiliano Simu 0777 000036, au 0712 840 960

SERIKALI YAZISHAURI TAASISI ZA KIBENKI NCHINI KUWA NA VILABU VYA MICHEZO NA MASHINDANO

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imezishauri Taasisi za Kibenki zilizopo nchini kuanzisha timu na vilabu vya michezo ili kukuza michezo pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa vijana walio wengi ambao wana vipaji lakini hawana timu za kuwaendeleza.

Hayo yamebainishwa kupitia kwa Waziri mwenye dhamana, Mh. Nape Nnauye mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali ikiwemo tuzo za wachezaji bora walioshinda katika michezo maalum ya BRAZUKA KIBENKI iliyoandaliwa na benki ya Barclays na wadau wengine.

Waziri Nape amebainisha kuwa, Nia ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inakuza michezo na kuwa na fursa za kiuchumi kupitia michezo hivyo taasisi hizo zinazo fursa ya kuongeza ajira na ustawi mzuri wa michezo endapo zitaanzisha timu za michezo na kimashindano kwani zinaweza na zinao wajibu huo.

Kwa mujibu wa Mratibu wa michuano hiyo, Nasikiwa Berya alieleza kuwa, jumla ya timu 16 zilishiriki huku ikianza 28 Novemba 2015 na kufikia tamati 20 Februari 2016 ilikuwa ni ya aina yake na kutoa mwangaza wa kimaendeleo wa kimichezo ambapo pia imesaidia kuimarisha afya, ushikamano na undugu kwa baina ya wachezaji na washangiliaji ambao wengi wao walitoka katika mabenki shiriki 15 ikiwemo matawi yao ya Tanzania Bara na Visiwani.

Katika tukio hilo, washindi mbalimbali walipatiwa vyeti vya shukrani hii ni pamoja na wadhamini wa mashindano hayo ikiwemo kutoka mabenki, kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) na makampuni mengine walipewa vyeti vya shukrani katika kufanikisha michuano hiyo.Nao
Mwakilishi kutoka MeTL Group, Bw.Zainul Mzige (kulia) akikabidhi cheti cha ushindi kwa Mchezaji Nuhu Mkuchu kutoka benki ya NMB.
nape bora
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akikabidhi tuzo ya golikipa bora, Gabriel Bernard.
Nape boraa
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akikabidhi tuzo ya mfungaji bora mchezaji kutoka benki ya NMB, Ahmed Nassoro.


KIPINDI CHA DIIRA YA DUNIA

MAKALA YA SHERIA;JE KUKATAA KUPOKEA SUMMONS KUNA MADHARA GANI KISHERIA ?.

$
0
0


Na  BashirYakub.
Summons  ndio wito maalum wa mahakama. Mara  zote unapofuguliwa mashtaka (unaposhtakiwa) hasa mashtaka ya madai basi ili uweze kufika mahakamani na kujua mashtaka yanayo kukabili yaipasa mahakama kutuma wito maalum ambao kwa jina  la kitaalam ndio huitwa  “summons”. 

1.KWANINI  WATU  HUKATAA  KUPOKEA/KUSAINI   WITO   HUU.
Mara  nyingi wito huu unapotumwa baadhi ya watu hukataa kabisa kuupokea na wengine huupokea lakini hukataa kuusaini.  Zipo sababu ambazo huwafanya watu wasipokee wito huu :  

( a ) Kwanza  ni imani kuwa usipopokea wito basi shauri ulilofunguliwa haliwezi kuendelea. 

( b )Sababu nyingine ni kuamini kuwa ukikataa kupokea wito utakuwa umejitoa katika hatia(liability)  ya kutambua chochote kinachoendelea hivyo chochote kilichopo mahakamani kitakuwa hakikuhusu.  
           
( c )Pia wengine hukataa kupokea wito kwa kuamini kuwa kupokea wito ndio kukubali shitaka na hivyo ni  bora  kuukataa kwa kuwa kufanya hivyo itakuwa ni kukana shitaka. Tutaona hapa chini kama imani hizo zina ukweli wowote.


UNDP WAFANYA KONGAMANO LA VIJANA, LENGO NI KUWASAIDIA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI

$
0
0
Hawa Dabo

Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la vijana na maendeleo, kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).


Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam limefanya kongamano la vijana na maendeleo kujadili jinsi vijana wanavyoweza kutumika kusaidia kuleta maendeleo nchini na kubadili mfumo wa vijana katika kufanya maamuzi yaliyo sahihi.

Akizungumzia kongamano hilo limelofanyika siku ambayo UNDP imetiza miaka 50 tangu kuanzishwa, Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP nchini, Amon Manyama alisema kuwa vijana wana nafasi kubwa katika jamii na kama wakitumika vizuri wanaweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo na hivyo kupitia kongamano hilo wanataraji kuwapa mbinu mpya.

Alisema mbali ya kuangala jinsi wanavyoweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo pia wanajadili kwa pamoja ili kuona jinsi gani wanaweza kubadili mfumo wa vijana wa kufanya maamuzi ambao wengi wao wamekuwa wakifanya maamuzi ambayo baadae yanaonekana kutokuwa sahihi.

“Tunafanya kongamano hili na vijana kutoka vyuo mbalimbali ili kuona mustakabali wa vijana wa Tanzania, kuona jinsi gani wanaweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo Tanzania na hata kubadili mfumo wao wa kufanya maamuzi,” alisema Manyama.
Youth and Development Symposium UNDP, Tanzania
IMG_5271
Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP nchini na mshereheshaji wa kongamano hilo, Amon Manyama akizungumza katika kongamano la vijana na maendeleo.

Nae Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo alisema vijana wana nafasi kubwa kusaidia uapatikanaji wa maendeleo nchini na wao kama UNDP wamekuwa wakisaidia na serikali ili kuwasaidia vijana kwa kuwapa mbinu ambazo wanaweza kutumia ili kufikia malengo waliyonayo.

Alisema licha ya kuwepo changamoto zilizopo katika sera ya vijana lakini pia vijana wamepoteza udhubutu wa kufanya maamuzi na hivyo kongamano hilo wanaweza kukuza uwezo wao wa kujiamini na kufanya maamuzi ambayo yanakuwa ni sahihi.

“Vijana wanatakiwa kuwa na malengo na kukuza uwezo wa kujiamini … vijana wanaweza kusaidia kupatikana maendeleo Tanzania na wana hamasa ya kusaidia kupatikana maendeleo hivyo wanatakiwa kupewa nafasi katika kufanya maamuzi,” alisema Bi. Dabo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

BENKI YA CRDB TAWI LA WATER FRONT WASHEREKEA SIKU YA WANAWAKE KWA KUMTEMBELEA MGONJWA WA SARATANI BI. SAKINA

$
0
0
Keki ya wanawake waliofungua akaunti ya MALKIA katika benki ya CRDB tawi la water Front, kwaajili ya kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.
Mstaafu wa Benki ya CRDB tawi la Water Front jijini Dar es Salaam, Adelaida Bishagazi akikata keki kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.
---------------------------------------- 
Mara baada ya kusherekea siku ya wanawake Duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8, wafanyakazi wa benki ya CRDB tawi la water front jijini Dar es Salaam wameenda mali zaidi kumsaidia Mgonjwa wa ugonjwa wa Saratani kutoka mkoani Kigoma, Bi Sakina ambaye alikuwa akipewa matibabu katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.
Meneja  huduma kwa wateja wa benki ya CRDB tawi la Water Front, Mary Ngowi akimkabidhi Dawa pamoja na Sindano za Saratani Bi Sakina (kulia)mkazi wa mkoani Kigoma ambaye alikuja kwaajili ya matibabu jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Watanzania watakiwa kuthamini miundombinu ya michezo.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Maendeleo ya Michezo aliyepo katika Uwanja wa Taifa, Nsajigwa Gordon,  kuhusu viti vilivyobadilishwa baada ya kuharibiwa na mashabiki, wakati wa ziara Uwanjani hapo leo jijini Dar es Salaam.

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akiwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Afisa Maendeleo ya Michezo anayesimamia Uwanja wa Taifa Nsajigwa Gordon
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James akikagua Koki ya bomba la  sink la kunawia katika moja ya choo cha Uwanja wa Taifa alipofanya ziara ya kushitukiza Uwanjani hapo leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images