Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

TANZANIA NA UIGEREZA KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA KIUCHUMI

0
0
 Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige akimueleza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), tarehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimueleza jambo Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige (hsyupo pichani), tarehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige (wa kwanza kulia) akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), (hayupo pichani) alipokutana naye Ofisini kwake, tarehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa  Idara ya uratibu wa shughuli za serikali Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery (kushoto) alipotembelea ofisi hiyo, tarehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es Salaam.

Tanzania na Uingereza zinatarajia kuendelelea kushirikiana katika masuala ya Uchumi kupitia Mpango wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Tanzania na Uingereza “UK partnership in Prosperity” ambao unajikita katika maeneo makubwa ya ushirikiano ya Mafuta na Gesi, Nishati Jadidifu; Kilimo; na Uboreshaji Mazingira ya Biashara.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa kufanya mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige, leo jioni, terehe 08 Machi, 2016, Jijini Dar es salaam.
Tunatarajia mpango huu ukishafanyiwa maboresho utaimarisha uchumi wa nchi zote mbili, tunatarajia baada ya maboresho hayo makampuni mengi kutoka uingereza kuja kufanya biashara nchini kuwekeza .Tunaelewa nia ya serikali ya Uingereza kuwekeza  katika miundo mbinu iliyopo vijijini hasa katika sekta ya maji na kilimo hii itasaidia kuinua maisha ya wananchi wanaoishi vijijini hasa wanawake , hii ni kutokana na kuwa asilimia 80 ya wananchi nchini wanaishi vijijini na wengi wao ni wananawake na leo ukizingatia ni siku ya wanawake Duniani” Alisema Mhagama.

Aliongeza kuwa mpango huo umekuja muda muafaka wakati serikali inaendelea na juhudi za kuishirikisha sekta binafsi katika kukuza uchumi nchini kwa kuwa serikali inatambua sekta binafsi ndio chachu ya maendeleo nchini.

“Tunahitaji ushirikiano wenu ili muweze kutujengea uwezo wa kuwavutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa kwa msingi wa kuendeleza viwanda nchini na hatimaye tunaweza kufanya kwa ubora  biashara kimataifa ” alisistiza.

Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Mhe. James Duddrige ali fika ofisini hapo kwa lengo la kuonana na Waziri Mkuu kwa ajili ya kumueleza ushirikiano wao watakaoendelea kuutoa kwa serikali ya awamu ya tano katika masuala ya Dawa za kulevya na biashara haramu ya pembe za ndovu nchini pamoja na uboreshaji wa Mpango wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Tanzania na Uingereza “UK partnership in Prosperity”  .

Mpango huo wa Ushirikiano wa Ushirikiano Kati ya Tanzania na Uingereza ulizinduliwa rasmi Novemba 2015 na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda.

Imetolewa na
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU
O8 MACHI 2016


BREAKING NYUUUZZZ......: WATU WATATU WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE ZAIDI YA 16 WAJERUHIWA VIBAYA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MATATU, JIJINI DAR ASUBUHI HII

0
0
Ajali mbaya iliyohusisha Magari matatu likiwemo Daraladal ya abiria linalofanya safari zake kati ya Gongo la Mboto kwenda Ubungo, imetokea mapema leo asubuhi katika barabara ya Mandela eneo la Tabara Matumbi, Jijini Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 16 kujeruhuwa vibaya sana na kukimbizwa hospitali ya Amana, Ilala kwa Matibabu.

Inaelezwa kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma, hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugonga na Lori lingine lililokuwa limepakia Ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu Mnadani.

Jitihada za kuyatoa magari hayo zinafanyika sasa. Kama unaweza kutoitumia barabara hiyo asubuhi hii ni vema kuepuka msongamano
Muonekano wa Daladala hilo baada ya kugongana uso kwa uso la Lori lililokuwa limepakia Ng'ombe, eneo la Tabata Matumbi, Jijini Dar es salaam leo.
Askari wa Usalama Barabarani na baadhi ya mashuhuda wakiwa eneo la tukio.
Baadhi ya Ng'ombe walikuwemo kwenye Lori hilo, wakiwa wamewekwa kando baada ya kuokolewa.
Kichwa cha Lori hilo, kikiwa Chini baada ya Ajali.

WAZIRI MBARAWA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA FLOW METER

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa Meneja ujenzi wa kampuni ya BQ Bw. Neven Slavujevic inayojenga mtambo wa kupima mafuta bandarini (flow meter ) kwenye kituo cha kupakulia mafuta kilichopo Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akipanda juu ya mtambo wa kupima mafuta bandarini (flow meter) kwa ajili ya kuukagua kwenye kituo cha kupakulia mafuta kilichopo Mji Mwema Kigamboni jijini Dar es salaam.
Meneja ujenzi wa kampuni ya BQ Bw. Neven Slavujevic inayojenga mtambo wa kupima mafuta bandarini (flow meter )akifafafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa alipokagua mtambo huo.

MR NICE ARUDI NA KIOO

JPM AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI MAALIM SEIF

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea na kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Shariff Hamad, katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam, ambako anapata mapumziko baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Hindu Mandal alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Airtel yazindua usajili mpya katika huduma ya Wazazi Nipendeni

0
0
Airtel Tanzania kwa kushirikiana na mHealth Tanzania washerehekea kuanza kwa mwaka wanne wa ushirikiano wao wa kutoa taarifa za afya kwa wa mama wajawazito na watoto kwa njia ya  ujumbe mfupi kupitia program ijulikanayo kama “Wazazi Nipendeni”  kwa  kuzindua namba maalumu (USSD) itakayowawezesha watoa  huduma za afya  kuongezea ufanisi katika kutoa na huduma kwa mama na watoto.

Airtel Tanzania imekuwa kampuni ya kwanza kushirikiana na mHealth Tanzania katika kuwawezesha wateja wake nchi nzima kupata tarifa za afya bila gharama zozote.

Katika mwendelezo wa kuboresha huduma hii, Airtel inayofuraha kutangaza teknokalogia mpya  itayowawezesha watoa  huduma za afya kuandikisha kina mama wajawazito na watoto  kwenye huduma ya “Wazazi Nipendeni” kupitia  namba maalumu (USSD code) kwa haraka na urahisi zaidi.

Namba hiyo maalumu itawawezesha maelfu ya watoa huduma za afya katika vituo mbalimbali kuwasadia wamama wajawazito, wa mama wenye watoto wadogo, watoto wadogo pamoja na wasaidizi wao kujiandikisha na huduma ya bure ya ujumbe mfupi wa taarifa za afya na kuwakumbusha tarehe za kuhudhuria kliniki.

Akiongea kwa niaba ya Airtel,  Meneja Huduma za Jamii, Hawa Bayumi alisema “Tunajivunia kuwa sehemu ya mpango huu kwani tunaamini upatikanaji wa taarifa za afya ni muhimu  hivyo tunawawezesha kinamama  wajawazito na wenye watoto wadogo kupata taarifa hizi kupitia simu zao za mkononi wakiwa majumbani kwao bila gharama zozote.  katika kuhakikisha idadi kubwa ya  kila mama wanajiandikisha kwenye huduma ya Wazazi Nipendeni  leo tunazindua rasmi namba maalumu kwa watoa huduma za afya kufanya usajili,  lengo letu nikuhakikisha tunajenga utamaduni wa watu kufatilia afya zao.

huduma hii ya “ Wazazi Nipendeni” itawawezesha watakao jiunga kupata ujumbe mfupi wenye taarifa za afya 4  kwa wiki,  tunaamini kwa kufanya hivyo tutawawezesha wamama wajawazito na watoto kuzingatia afya bora wakati wote. aliongeza Singano.

Naye Mtoa huduma za afya  wa kituo cha afya Vingunguti, Mosi Mohamed alisema” sasa anaweza kutumia namba hiyo maalumu  kusaidia jamii inayomzunduka kujiunga na huduma ya ujumbe mfupi wa bure ya Wazazi Nipendeni kwa urahisi akiwa mahali popote.

Akiongea kwa niaba ya Wizara ya Afya, Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani alisisitiza umuhimu wa kutumia teknologia ya mawasiliano  katika kupunguza vifo vya wamama  wajawazito “ utoaji wa taarifa muhimu za afya na kutoa ushauri kwa kina mama wajawazito na wenye watoto wadogo kunasaidia kujenga jamii yenye afya bora.  Huduma hii mpya ya namba maalumu itaboresha na kuongeza ufanisi mkubwa kwa watoa huduma wa afya nchi” alisema.

Huduma ya Wazazi Nipendeni inashirikisha washirika wengine zaidi ya 30 katika maeno mbalimbali  wakiongozwa na Wizara ya Afya, Ripoti inaonyesha  tangu kuanzishwa kwa huduma hii zaidi ya watu million 1.25 wamejiunga na huduma hii ya Wazazi Nipendeni kutoka katika mitandao mbalimbali. Kati yao zaidi ya 250,000 ni watumiaji wa Mtandao wa Airtel wamepokea ujumbe mfupi wa bure zaidi ya million 18 wenye ushari wa kiafya.
Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani ( kulia) na Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi (katikati) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC) Tanzania, Dr Maestro Evans wakipongezana baada ya kuzindua namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayowapa taarifa mbalimbali za afya bure ijulikanayo kama “Wazazi Nipende”. mradi wenye lengo la kupunguza idadi ya vifo vya kina mama wajawazito na watoto.
Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati uzinduzi wa namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayowapatia taarifa mbalimbali za afya bure ijulikanayo kama “Wazazi Nipende” inayotolewa na Airtel pamoja na mHealth Tanzania chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya. Katikati ni Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi akifatiwa Mkurugenzi Msaidi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC) Tanzania, Dr Maestro Evans
Meneja Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi(katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa namba maalumu itakayowawezesha watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto kwenye huduma itakayo wapatia taarifa mbalimbali za afya ijulikanayo kama “Wazazi Nipende” inayotolewa na Airtel pamoja na mHealth Tanzania na washirika wengine chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya. Kulia ni Mratibu wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani na kushoto ni Mkurugenzi Msaidi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC)Tanzania, Dr Maestro Evans.

TEASER YA JOTO LA ASUBUHI ALHAMISI MARCH 10

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: DDC MLIMANI PARK


MAOMBI MAALUM YA KUMWOMBEA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI NA SERIKALI YAKE YAFANYIKA JIJINI MBEYA.

0
0

Baadhi ya maaskofu kutoka makanisa mbalimbali Mkoani Mbeya wakiwa wamshika Picha ya Rais na ramani ya Tanzania wakati wa maombi maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya.
Askofu Dkt Charles Gadi wa kanisa la The City of Refuge Church yenye makao makuu jijini Dar es salaam akizungumza na waumini walioshiriki katika maombi ya kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya March 8 mwaka huu. . 
Baadhi ya waumini walioshiriki Maombi Maalum ya Kumwombea Rais Dkt John Pombe Magufuli na serikali yake yaliyoandaliwa na Jukwaa la wakristo Mkoani Mbeya kwa kushirikiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la The City of refuge Church Dkt Charles Gadi katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya March 8 mwaka huu.

DIRA JUMATANO 09.03.2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI MAALIMU SEIF SHARIF HAMAD.

0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif aliruhusiwa kutoka hospitalini jana na hali yake inaendelea vizuri.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumjulia hali  na kusema kuwa hali yake ya kiafya inaimarika siku baada ya siku.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam mara baada ya kumjulia hali jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU







DKT SHEIN AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI MAALIM SEIF LEO JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiambatana na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Ikulu na Utawalabora Mheshimiwa Dkt. Mwinyihaji Makame, amemtembelea kumjulia hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar  Maalim Seif Shariff Hamad ambaye yuko hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko baada ya kutolewa hospitali. Amesema afya yake inazidi kuimarika siku hadi siku. Dkt. Shein alifika hotelini hapo mnamo majira ya saa mbili usiku. (Picha na Salmin Said, OMKR)
 Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akimjulia  hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar  Maalim Seif Shariff Hamad hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akimjulia  hali Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanibar  Maalim Seif Shariff Hamad hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Picha na OMKR

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

RAIS WA VIETNAM, MHE. TRUONG TAN SANG AKARIBISHWA IKULU, JIJINI DAR LEO

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kushoto) akimkaribisha mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.
 Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye koti la drafti) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Kulia niRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli
 Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (wa tatu kushoto) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Wa pili kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakipanda jukwaani kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za Taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakiwa katika jukwaa kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za Taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (mwenye tai nyekundu) akikagua gwaride la heshima katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi,
 2016.
 Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akipokea zawadi ya ua toka kwa mtoto mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 akiwa amefuatana na mmewe kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.

 Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe mamaMai Thi Hanh wakiwasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbalikati ya Tanzania na Vietnam.

(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO)

No Country for Cartoonists – The Exit of GADO Mwapembwa.

0
0
Godfrey Mwapembwa, better known to Kenyans and followers of his work around the world as GADO (pictured), talks of this moment with shades of disbelief on his face.
They seem to have endured the months between the November 2015 meeting between him and Nation Media Group’s Editor-In-Chief, Tom Mshindi, and our evening meeting early this March. 
It is the disbelief, perhaps, of a man whose stature as an editorial cartoonist isn’t just renowned locally, but globally. Every few minutes, he returns to one statement that perhaps sums up what feeling filled up that blankness he was initially confronted by; betrayal. During
that meeting, GADO found out that the Nation Media Group would not be renewing his contract.“ It wasn’t that it happened – rather, how it all happened that I am disappointed in,” he says.
It’s hard not to see why GADO’s look back on what led to the end of one of the longest running editorial cartoon partnerships that the Nation has ever had would be wistful.GADO’s being pushed towards the exit of the Nation Media Group began on different dates, depending on who you speak to within the organization. 
He tells me that some senior editors think that his fate was sealed in March of 2013, the month that the Jubilee Government was elected. Others, who wouldn’t speak on the record, think that the change of guard at the senior level of management had more to do with his exit than anything else. Specifically, Tom Mshindi’s alleged pedantic, almost over-bearing order that he sees every editorial cartoon before it goes to print. 

TEASER JOTO LA ASUBUHI LA EFM 93.7 ALHAMISI MARCH 10, 2016

HOJA YA HAJA : Muda wa kufanya kazi kwa mazoea umekwisha Tanzania.

0
0
 Na Mdau Ughaibuni
Tangu JPM aingie madarakani amekuwa akifanya maamuzi ya haraka kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wanyonge wa Tanzania. Naamini amekuwa akifanya hivyo ili kuwaonyesha  njia   viongozi wengine wa chini yake  ili nao  wawe wabunifu, wenye uthubutu,  na waweze kufanya maamuzi ya  haraka ili kuwapunguzia shida watanzania wanyonge.
Swali ninalojiuliza, Je viongozi wa chini yake wanaliona hilo na kufuata mfano wake. Tumewaona wachache wanaojitahidi lakini wengine  sina uhakika  kama watafikia matakwa ya Rais wetu mpendwa. Nachelea kusema haya kwani viongozi wasio wabunifu, wanaofanya kazi kwa mazoea na wasio na uthubutu wataendelea kumchosha Rais na Waziri mkuu wetu na kuchukua muda wake mwingi kufanya maamuzi ambayo yangefanywa nao katika ngazi zao. Ni vyema Rais na Waziri mkuu   waachwe  wafanye mambo makubwa zaidi  katika ngazi yao.
Je, Viongozi wa Wizara ya Afya walikuwa hawaoni kuwa wakina Mama wanalala chini mpaka Magufuli aje? Kama waliona walichukua hatua gani?  Ni jambo la wazi Kwamba hali ilivyo kuwa Muhimbili ni hivyo ilivyo katika   hospitali nyingine mikoani na wilayani na viongozi wapo. Unategemea Rais au Waziri mkuu  watembelea  hospitali za wilaya  zote ndio  mambo yabadilike.   Ni vyema viongozi wa ngazi hizo  waende na spidi ya JPM na kama hawawezi basi , ameshasema mwenyewe kwamba wampishe.
Muda wa kufanya kazi kwa mazoea umekwisha. Mfano mzuri  ni kuhusu  askari wa usalama barabarani, wanaona dhahiri  vijana  wa bodaboda wanavunja  sheria kwa kuvuka taa nyekundu, hawafuati  miongozo ya taa za barabarani  na mara nyingi wanasababisha ajali. Akari polisi wanasubiri mpaka ajali itokee na sio kuzuia ajali isitokee. Kuna siku moja niliwauliza askari wa usalama barani kwa nini hawawakamati waendesha bodaboda wanaovunja sheria kwa kuvuka kwenye taa nyekundu? Kwa mshangao askari huu alinijibu hawa hatuwawezi labda tuwapige risasi. Utaona kabisa  ubunifu katika utendaji kazi wake hakuna kabisa. Siku moja nilitembelea chuo kikuu kimoja jjini DSM katika idara inayoshughulikia maji na mazingira. Idara hii ndio unayofundisha wahandisi wa maji na mazingira, Lakini cha kushangaza  katika ofisi yao hakuna maji ya bomba wana weka maji kwenye ndoo kwa ajili ya  chai na kutumia maliwatoni. Kwa kweli kilinishangaza kidogo, hawa ndio wataalam wenyewe wanaofudisha taaluma  za maji  lakini wenyewe wanashindwa kujiwekea maji  ya bomba  yanayofanya kazi ndani za ofisi zao, sasa wanafundisha nini? Utaona hapa ni kufanya kazi kwa mazoea na kukosa ubunifu. Mifano ni mingi. Mheshimiwa JPM  una kazi kubwa sana ya kubadilisha  mfumo. Ikiwezekana baadhi ya wafanyakazi wa serikali wastaafishwe mapema ili uweke damu mpya  yenye ubunifu na uthubutu. Kuna watanzania wengi wako nje wameajiriwa na mashirika ya kimataifa wako tayari kuja kuijenga nchi chini ya uongozi wako imara. Ikiwezekana  nao warudishe nyumbani waje wachangie uchumi wa taifa. Naamini ukijenga mfumo wa uwajibikaji na ukaweka damu mpya katika ngazi zote ma DC, RC, Wakurugenxzi wa wilaya na idara za serikali utaivusha Tanzania   haraka kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Mungu ibariki Tanzania

UNFINISHED HOUSE FOR SALE

0
0
The plot on which the house exists is located at Tegeta - Mivumoni via Madale road, Five kilometers (5 kms) from Wazo Cement Factory over a gravel road all time accessible by any means of transport.
The plot is Eight hundred square meters (800m2) in size, with lots of space left for car park, garden and even a servant quarter. The building comprises of 4 bedrooms of which 2 are self contained, spacious lounge, dinning, kitchen, public toilet and bathroom, 2 verandas. It has reached roofing stage.

Property is legally owned by one person with Purchase (Ownership) documents witnessed and approved by Local Government. Most of the neighbouring plots are surveyed.
The area is quite ideal for residencial and commercial use with facilities like Electricity and Tap water accessible. Neighbouring landmarks are residencial houses, St. Patrick secondary school, vocational training college, Mivumoni dispensary and TAG church.
For more details; Call, Sms or WhatsApp: +255715902270 or Email: philipbenedict88@yahoo.com

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL: NIMEKUCHAGUA WEWE - BOB RUDALA

Watanzania wameaswa kuwa na tabia kuweka akiba benki.

0
0
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.
Watanzania wameaswa kujenga tabia ya kujiwekea akiba kupitia mabenki kwa manufaa yao na taifa kwa kwa ujumla ikiwa ni mchango wao katika kutekeleza kaulimbiu ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kufikia malengo waliojiwekea katika kujiletea maendeleo endelevu.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Fedha na Utawala kutoka Bodi ya Bima na Amana (DIB) iliyo chini ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Richard Malisa wakati akitoa mada juu ya bodi hiyo katika semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi hao katika kuandika, kutoa na kusambaza habari za sekta ya uchumi biashara na fedha.

“Pesa zinapowekwa na kuwa benki hutumika kuchangia kuinua na kuimarisha usalama wa akiba ya mtu binafsi na kwa upande wa nchi zinatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuinua sekta ya elimu, afya, maji,  ujenzi wa barabara na kilimo” alisema Malisa.

Katika kuonesha umuhimu wa bodi hiyo nchini, Malisa alisema kuwa taasisi ama mtu binafsi anapoweka pesa zake benki, hiyo ni amana kubwa na muhimu kwa kuwa tabia hiyo ya uwekaji pesa ina tija na inaongeza usalama wa pesa ambayo ni njia salama ikilinganishwa na kutumia njia za zamani za watu kuweka pesa kwenye godoro ambayo sio salama.

Faida nyingine za mtu binafsi ama taasisi kuweka pesa zao benki ni kuongeza mtaji wake kwa kupata riba kulingana na muda pesa hizo zinapokuwa benki na mteja anauhakika pesa yake ipo salama kwa kuwa ipo mikononi mwa Bodi ya Bima na Amana endapo litatokea tatizo lolote kwenye benki alipoweka pesa zake.

Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images