Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 113 | 114 | (Page 115) | 116 | 117 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Namtumbo,Abdula Lutavi akitoa matone ya chanjo kwa mtoto wa Bi.Hilda Berth wa kijiji cha Luhimba wilaya ya Songea ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya chanjo.Picha na Ofisi ya Mkuu qa Mkoa wa Ruvuma.

  0 0
 • 04/26/13--09:35: mdau akikata kiu
 • Kamera ya Globu ya Jamii leo imemnasa Mdau huyu akikata kiu kwa kunywa maji kutoka kwenye bomba lililokuwa nikimwagilia maua kwenye moja ya bustani katikati ya jiji la Mwanza mchana wa leo.

  0 0

   Ukiwa unaingia kwenye kituo cha Daladala cha Mwaloni Jijini Mwanza,kuna Shimo hili ambalo limekuwa ni kero kwa Daladala zinazoingia kupaki kwenye kituo hicho.Shimo hili linawezekana kabisa kuzibika kwani linatakiwa kuwekwa karavati tu.
   Mtoto akijiandaa kuvuka barabara.
   Mwendesha bodaboda akiwa katika chombo chake huku akiwa kapakia abiria,bila ya kuvaa helment ambayo kaining'iniza kwenye usukani.
   Hapa ndio wamepaki wenyewe.
  Sambusa
   Barabara ya kuelekea Chuo Kikuu cha Mt. Augustine.

  0 0


  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Mh. Baraka Konisaga (kushoto) akisalimiana na Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) jijini Mwanza,Andrew Mbwambo wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Furahisha tayari kwa Hafla ya kutoa Baraka zake wa Bia ya Safari Lager iliyoshinda Tuzo ya Bia Bora Barani Afrika.Kulia ni Meneja Matukio wa TBL kanda ya Ziwa,Erick Mwayela na wa Pili kushoto ni Mdau Deodatus Katambi.
  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Mh. Baraka Konisaga akipokea Kombe la Ushindi wa Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager kutoka kwa Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo ikiwa ni kutoa Baraka zake kwa Kombe hilo kuwepo jijini Mwanza,katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo.
  Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza,Mh. Baraka Konisaga akinyanyua Juu Kombe la Bia Bora Barani Afrika ulioupata Bia ya Safari Lager wakati wa kutoa baraka zake kwa ziara ya Kombe hilo jijini Mwanza.  

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZINGINE

  0 0


  Watanzania wanaoishi New Jersey na New York City. Wanasikitika kutangaza kifo cha Mtanzania mwenzao Adolph aka Brian aka Thadeo Lwakajende kilichotokea tarehe 24 mwezi wa 4, 2013 hapa New Jersey, USA. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu inaendelea huko New Jersey. Ili kufanikisha mipango hiyo wanawaomba watanzania wote popote pale walipo wajiunge nao kusaidia kuchangisha hela za shughuli hiyo. Unaweza kutuma hela kwa kutumia paypal adolffuneralcost@gmail.com au katika site hii ya Adolf sending home fund http://dt.tl/adolfsendhomecost


  Kwa mawasiliano ya shughuli hizi wasiliana na 

  Peter Luangisa (917) 681-6971

  Rashidi Kamugisha (973) 703-4596

  Bernard Kivugo (973) 580-7166

  William Vedasto (973) 551-2916

  Tunatanguliza shukurani zetu za dhati.

  0 0

  Na Mahmoud Ahmad, Arusha
    Jeshi la polisi mkoani hapa limemtia mbaroni mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mhe Godless Lema kwa tuhuma za uchochezi kwa wanafunzi kwenye chuo cha uhasibu mwanzoni mwa wiki katika vurugu zilizotokea chuoni hapo baada ya mwenzao kuuwawa juzi usiku huko maeneo ya njiro jijini hapa
  Kamanda wa polisi mkoani hapa kamishna msaidizi wa polisi Liberatus Sabas alisema kuwa Mhe Lema  alikamatwa huko nyumbani kwake Njiro majira ya saa 9 usiku. 
  Afande  Sabas alisema jeshi hilo linaendelea na mahojiano na mtuhumiwa na kuwa katika tukio hilo zaidi ya watuhumiwa 14 walifikishwa mahakamani jana na kuwa hao hawezi kuwaongelea kwani kesi yao ipo kwenye chombo hicho cha sheria. 
   Pia kamanda Sabas alisema kuwa Mh Lema anashikiliwa kutokana na vurugu zilizotokea juzi kwenye chuo cha uhasibu na kuwa atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu. 
   Kwa upande mwengine Kamanda Sabas  alisema kuwa zaidi ya hao watu 14 na Mhe. Lema hakuna mtuhumiwa mwingine aliyakamatwa. Awali ilisemakana wakili wake Albert Msando nae amekamatwa.
   Mnamo siku ya Jumatatu mwanafunzi mmoja aliuwawa kwenye mitaa ya Njiro jijini Arusha na watu wasiojulikana hali iliyoleta tafrani hadi wanafunzi hao walipoleta vurugu chuoni hapo na polisi kutumia mabomo ya machozi kuwatawanya.
  Sekeseke hilo lilimalizwa na jeshi la polisi baada ya wanafunzi kutotii amri ya mkuu wa mkoa huo Magessa Mulongo na kuanza kuingia barabarani kuandamana.

  0 0
 • 04/26/13--20:00: Ngoma azipendazo ankal
 • WESTERN JAZZ BAND NA NGOMA YAO YA 'VIGELEGELE' WALIKUWA HAWANA MSHINDANI

  0 0

   Nguna katika mnuso wa harusi Kigamboni mwaka 1990
   Dah! Hatua mbona kubwa ndugu mwandaazi...
  Hii nguna itafika kweli huku...????

  0 0
 • 04/26/13--20:00: Ngoma azipendazo ankal
 • Bi Shakila na 'Kifo cha Mahaba' anaweza kuliza wengi

  0 0

  NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI GEORGE M. MASAJU AFUNGA MAFUNZO YA SIKU TANO YA MAJADILIANO YA MIKATABA YA KIMATAIFA. MAFUNZO HAYO YALIWAHUSISHA MAWAKILI WA SERIKALI NA WANASHERIA WA WIZARA NA TAASISI MBALIMBALI ZA SERIKALI.
  NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI GEORGE M. MASAJU AKITOA ZAWADI KWA MMOJA YA WAKUFUNZI WA MAJADILIANO YA MIKATABA YA KIMATAIFA KUTOKA DLA PIPER WAKATI WA KUFUNGA MAFUNZO HAYO
  NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI GEORGE M. MASAJU AKIBADILISHANA MAWAZO NA WAKUFUNZI WA MAFUNZO YA MAJADILIANO YA MIKATABA YA KIMATAIFA KUTOKA DLA PIPER
  NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI (WALIOKAA MWENYE SUTI) GEORGE M. MASAJU KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WAKUFUNZI NA WAHITIMU WA MAFUNZO YA MAJADILIANO YA MIKATABA YA KIMATAIFA. MAFUNZO HAYO YAMEFANYIKA KATIKA SHULE YA SHERIA TANZANIA

  0 0

   Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Rais Dkt  Jakaya Mrisho Kikwete (katikati, mbeke)  akiwa katika picha ya pamoja na askari 30 aliowatunuku nishani mbalimbali, ikiwa ni moja ya shamrashamra ya kuadhimiasha miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Ikulu, Dar es Salaam 
   Rais Kikwete  akiwa na askari waliotunukiwa Nishani ya Utumishi Mrefu Tanzania
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja na askari waliotunukiwa Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema
   Rais Kikwete katika picha ya pamoja na askari waliotunukiwa Nishani ya Utumishi Mrefu
   JK akiwa katika ya pamoja na askari waliotunukiwa Nishani ya Ushupavu
   Rais Kikwete akiwa na wajumbe wa kamati ya Nishani 

  0 0

  Mwakilishi wa Kudumu  wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa,  Mhe Tuvako Manongi, Akizungumza  wakati Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa lilipojadili Utatuaji wa Migororo katika Afrika kwa njia ya Amani,  majadiliano hayo yalifanyika  hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni sehemu pia ya  Kuadhimisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwa Muungano wa Afrika.  Majadiliano hayo yalihitimishwa kwa kupitishwa bila kupingwa Tamko la Kisiasa kuhusu  utatuaji wa Migogoro Afrika  kwa    njia wa amani. Tamko hilo liliandaliwa na Kundi  la Nchi za Afrika katika Umoja wa Mataifa. Akichangia majadiliano hayo,  Mwakilishi wa Kudumu Umoja wa mataifa Mhe Tuvako Manongi pamoja na kuzungumzia sababu na vyanzo vya migogoro isiyo  kwisha  Barani Afrika, pia alitoa wito  kwa Afrika kukataa kugawanywa, kudharauliwa na kunyonywa. Pembeni ya Balozi ni  Afisa wa Ubalozi , Bw. Noel Kaganda


  Na Mwandishi Maalumu
  Baraza  Kuu la  Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja  Tamko la Kisiasa kuhusu Utatuzi wa  Migogoro  Barani Afrika kwa njia ya  Amani.
  Tamko hilo  ambalo ndani yake  linaainsha  na kutambua mchango mkubwa wa   Muungano wa Nchi Huru za Afrika  (OAU) na sasa Muungano wa Afrika ( AU)  katika kuchagiza  na kusimamia  pamoja na mambo mengine, maendeleo ya nchi za Afrika na watu wake,  kupiga vita  umaskini, ujenzi wa utawala bora, demokrasia , haki za  binadamu na utatuzi wa migororo kwa njia za amani.
  Kabla ya kupitishwa kwa Tamko hilo,  Baraza Kuu la Umoja wa  Mataifa,  kwa siku nzima ya Alhamisi na ijumaa asubuhi lilijikita katika  majadiliano  ya mada iliyohusu ‘utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani barani afrika’, ikiwa pia ni sehemu na  Baraza hilo kuadhimisha miaka  50   tangu kuanzishwa kwa OAU na baadaye AU.
  Miongozi wa viongozi wakuu walioshirikia majadilaino hayo, na ambayo yaliandaliwa na Bw. Vuk Jeremic,   Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon,   Rais wa  Equatoria Guinea Theodore Obiang Nguema Mbasogo, Rais Mstaafu wa Burundi Jean Pierre Buyoya  ambaye pia     Mwakilishi  maalum wa Muungano wa Afrika  huko Mali na Sahel,  wakiwamo pia mawaziri  kadhaa wa  Mambo ya Nchi za Nje.
  Akiungana na wazungumzaji wengine katika mkutano huo, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi, pamoja na kuainisha sababu na vyanzo vya migogoro Barani Afrika, alisema, Afrika lazima ifikie mahali ikatae kugawanywa.
  “Bara la Afrika lina fursa  nyingi,  Afrika inapanda chati. Afrika lazima ikatae kugawanywa, ikatae kudharauliwa na ikatae  kunyonywa” akasema Mwakilishi wa Kudumu, Tuvako Manongi.
  Na kubainisha kwamba,  Afrika lazima pia ikatae kutambuliwa kama bara ambalo limejaa migogoro  . “  Huu ni wakati wa  kufufua  upya pan africanism,  hiki ni kipindi cha mwamko mpya wa Afrika. Lazima tufanye kazi kwa pamoja  ili kuwapa matumaini watu wetu” akasisitiza Manongi.
  Akasema    wakati tukisherehekea maadhimisho ya miaka 50 wa OAU,  ni  vema kila mmoja wetu akaahidi  upya  kuimarisha ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika  kama ilivyoainishwa  katika  Sura ya Saba ya Katima ya Umoja  wa Mataifa.
  Akatoa mfano kwa kusema  uhusiano huo unapashwa kuendelezwa katika nyanja zote za  usalama na  maendeleo.  Kama ambavyo imeshashuhudiwa  katika   uundwaji wa Jeshi la  Mseto  kati ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika   katika Jimbo la Darfur ( UNAMID),  Misheni ya  Muungano wa Afrika huko Somalia, (AMISOM0  na tukio la hivi karibuni la kurejewa na  kuongozewa uwezo mpya Misheni ya Kutuliza Amani katika DRC ( MONUSCO) kulikoendana na kuridhiwa  upelekaji wa Brigedi Maalum inayoundwa na wanajeshi kutoka Tanzania, Afrika ya Kusini na Malawi.
  Aidha akasema majadiliano hayo  ya Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa, yamefanyika ikiwa  ni siku chache tu,   tangu kufanyika kwa Mkutano wa Baraza la Usalama la Afrika katika ngazi ya Mawaziri nchini Tanzania,  mkutano ambao pia ulijadili kwa kina pamoja na mambo mengine  hali ya usalama  barani afrika , vyanzo vya migogoro na ufumbuzi wake.
  Karibu wazungumzaji wote  wakiwamo wawakilishi wa Marekani na Jumuiya ya Ulaya waliochangia majadialiano hayo ya utanzuaji wa migogoro kwa njia ya amani, licha ya  kutambua, kusifu na kupongeza kazi kubwa ambayo imefanywa na inaendelea kufanywa na   Muungano wa  Afrika na Taasisi za Kikanda katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, walisisitiza haja na  umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa kuendeleza ushirikiano wake na Muungano wa Afrika.
  Aidha wazungumzaji huo walitambua na kukiri kwamba  Bara la Afrika licha ya  changamoto mbalimbali zikiwamo za migogoro inayoibuka hapa na pale,  imepiga hatua kuubwa za kimaendeleo, kiuchumi na kijamii na kwamba   Bara hilo linastahili kupongezwa na kuendelea kusaidiwa.


  0 0

  Baadhi ya wageni wakiwa wanapata chakula baada ya kuzunguka na kuanggalia wanyama na ndege katika  mbuga ya wanyama ya Serengeti kama walivyokutwa na kamera yetu mbugani hapo
  Picha na Mahmoud Ahmad wa Globu ya Jamii.

  0 0
 • 04/27/13--01:19: Article 0


 • 0 0

  Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.
   
  Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Rosemary Aloyce (kulia) na Mshindi wa Tatu Tarchisic Mtui mara baada ya warembo hao kutawazwa kuwa ndio washindi wa Shindano hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo. Kupata picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  Na Mwandishi Wetu
  Jumla ya warembo 16 wametemwa katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Redds Miss Tabata ambao utafanyika Mei 31 Dar West Park.
  Mratibu wa shindano hilo, Godfrey Kalinga, alisema jana kuwa warembo hao wametemwa kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo utoro, kukosa sifa za kushiriki na utovu wa nidhamu.
  Kalinga aliwataja warembo waliyotemwa kuwa ni Sophia Claud (21), Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rachel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Ray Issa (22), Shamim Abass (22), Shan Abass (22), Amina Ally (18), Magdalena Bhoke (21)  na Zilpha Christopher (19)
  Kalinga aliwataja warembo wanoendelea na mazoezi katika umbumbi wa Dar West Park, Tabata kila siku kuwa ni Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19),  Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20) and  Glory Jigge (18).
  Wengine ni Rachel Mushi (20), Caroline Sadiki (20), Kabula Juma Kibogoti (20), Blath Chambia (23), Suzzane Daniel Gingo (18), Upendo Lema (22), Pasilida Mandari (21) na Martha Gewe (19).
  Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Redds Miss Ilala baadaye mwaka huu.
  Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
  Redds Miss Tabata inaandaliwa na  Bob Entertainment na Keen Arts na chini ya Udhamini wa Redds, CXC Africa, Fredito Entertainment, Brake Point, Michuzi Media Group na Saluti5.


  0 0

   Keki maalum ilyoandaliwa kwenye maandimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanzania
   Balozi Philip Marmo akiteta jambo na mmoja wa wageni walialikwa kwenye sherehe hiyo.
  Wanakikundi cha Ngoma toka Tanzania Sisi Tambala wakitumbuiza kwa wimbo wao maarufu wa 'Katope' kwenye sherehe ya Muungaano.
  Picha na mdau Leah Mushi wa TBC1

  0 0
 • 04/27/13--02:06: Article 17


 • 0 0

  LIGI Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam hatua ya sita bora, inamalizika rasmi leo ambapo timu tatu zitakata tiketi ya kucheza hatua ya Kanda ili kupata nafasi ya kusaka nafasi ya kucheza Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara. 
  Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Mohamed Mharizo, amezitaja mechi zitakazochezwa leo kuwa ni Red Coast itakayomenyana na Day Break kwenye uwanja wa Kinesi, wakati kwenye Uwanja wa Makurumla, Friends Rangers wao watakuwa wakichuana vikali na Sharif Stars, huku kwenye Uwanja wa Airwing, Boom FC itakuwa ikikabiliana na Abajalo. 
   Hadi sasa Red Coast inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 8, ikifuatiwa na Abajalo yenye pointi 7, wakati Sharif Stars inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 6. Friends Rangers wao wanashika nafasi ya nne wakiwa na pointi 5 huku Day Break wakiwa na pointi 3 na Boom FC ikishika mkia kwa kujikusanyia pointi 2.

  Beki wa timu ya Red Coast, Rashid Juma (jezi ya njano), akijaribu kumdhibiti mchezaji wa Boom FC, Barnabas Kanji, wakati wa mechi ya Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam, hatua ya sita bora, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Makurumla, Aprili 24. Timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.


older | 1 | .... | 113 | 114 | (Page 115) | 116 | 117 | .... | 3272 | newer