Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 112 | 113 | (Page 114) | 115 | 116 | .... | 3285 | newer

  0 0

   Mdau akila kichwa mbele ya Sanamu ya Samaki iliopo kwenye kipita shoto cha Barabara ya Nyerere,jijini Mwanza mapema leo.Watu wengi kutoka maeneo mbali mbali,hupenda kufika katika eneo hili na kujipatia taswira za ukumbusho.
   Mdau akimuelekeza mteja wake namna ya kuweka pozi ili kupata taswira iliyo bora,
   Wapiga picha wakisubiri wateja katika kipita shoto hicho kama walivyonaswana Kamera ya Globu ya Jamii,mapema leo hii.

  0 0

  5th Economic women conference and business expo brought by Dare to Dream Foundation with Vodacom.

  Dare to Dream Foundation will be hosting another women’s business conference and exhibition on the 11th May 2013 from 8:00am to 5:30 pm at the Golden Jubilee tower, 5th floor.

  The Dare to Dream Business Expo & Conference is for all women including emerging female entrepreneurs who are operating their own small to medium sized businesses. If you have not gone into business for yourself you'll benefit by listening to accomplished and well-learned panelist, and gain marketable tools by attending workshops on how to turn your passion into a thriving business that in years to come you can be proud of. Discovering ways to turn your business into a power house and gaining strategies that you can implement immediately has never been so fun, so come join us as we empower each other!

  Tanzanian women are determined to stay competitive despite a harsh economic environment and they aim to build businesses that endure. More than 250 entrepreneurs, professionals, and others who are dreaming of starting their own ventures will be attending the Dare to Dream Conference + Expo hosted by Vodacom. 

  Attendees will listen to several renowned speakers, including author and motivational speaker from Uganda, Ms. Rehmah Kasule, founder and President of CEDA International ; H.E ambassador (rtd) Mwanaidi Sinare Maajar, Partner and advocate of REX attorneys, Joy Nyabongo of Service Excellence and others

  The conference also will feature industry leaders who will talk about global opportunities, business technology, marketing, and financing. Some of the topics will include, “ Tips to turn a Small company into a marketable Business, Learn ways women owned businesses gain financing, Building Your customer Base by Tapping Into Growth Communities with Buying Power attracting the perfect customers, and Creating loyal customers, Branding a business how it works & Why it’s important among many other topics.

  Other sponsors for this event include PSPF, CRDB bank, Umoja water and A1 oudoor.

  The Business Beyond Tomorrow day is open to the public and includes access to the conference and exhbition. Early ticket purchasing is advised as there is a limit of 250 tickets only. Each ticket is priced at Tshs 50,000/= For those who will need to showcase their products contact Virginia Ndlovu on 0684867752 or email at Virginia.d2d@gmail.com.

  Registration for attendants begins at 8 a.m. with talks scheduled throughout the day until 5 p.m. The day's activities include breakfast, lunch, snacks and a networking mocktail. In addition to providing information on successful sustainable initiatives, this conference will be entirely empowering.

  0 0


  Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Zanzibar, Mhe Haroun Ali Suleiman,akimkabidhi fedha taslima zaidi ya  shilingi Milioni tatu, mmoja wa viongozi wa shehia ya Mzuri kwa ajili ya mashindano ya kumuenzi aliyekuwa kiongozi wa siku nyingi nchini marehemu Hasnou Makame   Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi naUshirika Mhe Haroun Ali Suleiman akizungumza na Balozi mdogo wa India hapa nchini Mhe Pawal Kumar ofisini kwakwe Mwanakwerekwe mjini Zanzibar, jinsi India itakavyoweza kuisaidia Zanzibar juu ya kuanzishwa kwa Benki ya Jamii.

  Wanahabari  wa vyombo mbalimbali vya habari wakipata maelezo kwa Mshauri Mkuu wa Msafara wa wakandarasi kutoka India Bw. Ummashan Kar Misra juu ya kukifanyia matengenezo kiwanda cha sukari Mahonda 
  Mfanyakazi wa Idara ya Usafiri barabarani (kushoto) kwa kushirikiana na Askari wa Usalama barabarani wakiwa katika operesheni ya kukagua vyombo vya moto barabani katika kuadhimisha wiki ya usalama barabarani 

  Kondakta wa gari ya abiria ya Chwaka akiondoa marembo ya mbele ambayo yanamzua dereva kuona mbele baada ya kuamriwa kufanya hivyo na Askari wa Usalama Barabarani katika uperesheni wa ukaguzi wa Magari ulioandaliwa na Idara ya Usafiri na Lesseni kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani. 
  Picha zote na Khamisuu Abdallah wa Globu ya Jamii, Unguja


  0 0

  TAREHE 23 - 24 APRILI 2013 Tarehe 23 - 24/04/2013, Mhe. Begum K. Taji, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa alifanya ziara ya kikazi Lyon, mji wa pili kwa utajiri baada ya Paris. Akiwa Lyon, Balozi Taji alihudhuria mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Wintech Global na washirika wake. 
   Madhumuni ya mkutano huu ambao kauli mbiu yake ni ‘Clear Vision of the Crude Oil Market’ ni kuwafahamisha wadau wa sekta ya mafuta kuhusu kipimo maalum kinachotarajiwa kuzinduliwa na kampuni hii kwa ajili ya kupima kiwango cha tindikali kinachopatikana kwenye mafuta mazito (crude oil). Kiwango cha tindikali ndicho kinachoamua bei ya mafuta haya katika soko la dunia. 
  Kwa mujibu wa Wintech mpaka hivi sasa hakuna kipimo maalum kwa ajili ya kupima tindikali katika mafuta haya. Washiriki wa mkutano huu walikuwa ni wadau wa sekta hii ikiwa ni pamoja na makampuni ya mafuta, nchi zinazozalisha mafuta na zile zinazotegemea kuchimba mafuta katika siku za usoni. 
  Baadhi ya mabalozi kutoka nchi za Afrika hususan nchi za Afrika Mashariki walialikwa kuhudhuria mkutano huu. Pamoja na kuhudhuria mkutano huo, Mhe. Balozi Taji alipata fursa ya kukutana na watu mbalimbali kwa ajili ya kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii, biashara na uwekezaji. 
  Baadhi ya watu aliokutana nao ni Bw. Philippe Grillot, Rais wa Chama cha wafanyabiashara na wenye viwanda wa Lyon. 
  Katika mazungumzo yao walikubaliana kuandaa mkakati maalum utakaofanyika Lyon kwa ajili ya kuelezea fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana Tanzania na kuyakaribisha makampuni hayo kuwekeza katika sekta za kilimo; nishati; miundombinu; utalii na madini. Vile vile, Mhe. Balozi Taji alifanya mahojiano na ‘radiopluriel’ na kutumia fursa hii pia kuitangaza Tanzania.

  Mhe. Balozi Begum K. Taji akiwa na wakuu wa kampuni ya WINTECH GLOBAL ambao ni waandaaji wa mkutano huo uliofana sana.


  Balozi Begum K. Taji akiwa na baadhi ya washiriki. Kulia kwa Balozi Taji ni Balozi wa Msumbiji anayewakilishia nchi yake Ufaransa.  Balozi Begum K. Taji akiwa pamoja na Bw. Juvenal Noel, mtangazaji wa Radio Pluriel. Kituo hicho ni moja ya vituo vikubwa sana nchini Ufaransa na Balozi alipata fursa nzuri kuitangaza Tanzania na vivutio vyake 


  0 0  Na. ELIPHACE MARWA 
  na FRANK SHIJA - MAELEZO

  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar kaushiria Muungano uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania miaka 49 iliyopita.

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi kesho katika maadhimisho ya miaka 49 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

  Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wahabari kuzungumzia maadhimisho hayo  yatakayofanyika kesho katika uwanjwa wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

  Amesema kuwa kesho ni siku muhimu kwa Watanzania kuenzi na kuudumisha Muungano kwa  kuwa umesababisha Tanzania kupata heshima kubwa Afrika na duniani kote.

   “Ninatoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wetu, kwani hakuna asiyejua kuwa Muungano huu umetuletea heshima kubwa kimataifa, hivyo ni wajibu wetu kuulinda na kuudumisha” amesema Mh. Samia.

  Aidha  Waziri huyo amesema kuwa pamoja na changamoto zilizopo Muungano umeendelea kuimarika kwa kuwa wananchi wana imani kubwa na Muungano huu na Serikali imeendelea kushughulikia kero mbalimbali za Muungano.

  Mh. Samia ameongeza kuwa katika kushughukia kero zilizopo katika Muungano , Serikali ya awamu ya tatu mwaka 2004 iliunda kamati yenye wajumbe kutoka pande mbili za Muungano ya kushughulikia kero hizo.

  Aidha,mwaka 2006 kamati hiyo  ilianza kushughulikia kero hizo mpaka sasa jumla ya hoja tisa kati ya hoja 13 za Muungano zimekwisha kamilika na kupatiwa ufumbuzi.

  Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa na  Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume tangu tarehe 26/04/1964  ambapo kesho unatimiza  miaka 49.


  0 0

  Kijana  Masha  Yusuph mkazi wa  Iringa akiwa  ofisi ya mwanasheria  wa Halmashauri ya  manispaa ya  Iringa Bw Innocent Kihaga  (kulia) baada ya  kukamatwa  na mgambo  wa Manispaa hiyo akichafua ukuta  wa bustani ya Manispaa kwa kubandika matangazo yake  bila  kibali
  Mgambo  wa Manispaa ya  Iringa  wakiwa  wamemweka  chini ya ulinzi kijana Masha  Yusuph  kwa  kuchafua mji
  Hapa   wakimtaka  kijana  huyo kuokota takataka  alivyokuwa akizitupa ovyo baada ya  kubandika matangazo yake
  Hapa  akipelekwa  ofisi  za Mwanasheria  na kupigwa faini ya  shilingi 50,000 kwa  uchafuzi  wa mazingira  Hapa  akiingizwa katika  ofisi  za Mwanasheria.
  Picha na Francis Godwin

  0 0  Mahmoud Ahmad, Arusha
  Jumla ya  dola za Kimarekani million 177,238,966 zimetengwa kwenye bajeti ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa mwaka wa fedha 2013-14 na kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo kwenye kikao chao cha 26 dharura kilichoisha leo  jijini hapa.
  Mbali ya bajeti hiyo mkutano huo ulioanza mnamo April 22, 2013  kwa ngazi ya wataalamu na kufuatiwa na mkutano wa makatibu wakuu wa nchi wanachama na kupokea hatua zilizofikiwa katika majadiliano ya itifaki ya umoja wa fedha wa jumuiya ya Afrika ya mashariki ambao unatarajiwa kutiwa saini na wakuu wa jumuiya hiyo katika mkutano wao wa 15 mwezi Novemba mwaka huu.
  Aidha mkutano huo utajadili pia pendekezo la kuongeza wigo wa mamlaka ya mahakama ya Afrika ya Mashariki kwa kupitia mapendekezo yaliojadiliwa kwenye vikao vya wataalamu na makatibu wakuu wa jumuiya hiyo.
  Katika hatua nyingine mkutano huu wa dharura wa 26 wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambao umeisha  leo kwa kuwakutanisha wataalamu na makatibu wakuu kutoka nchi wanachama wa jumuiya hiyo,  umejadili mambo matatu makuu yatakayopelekwa kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa jumuiya kwa ajili ya kutia saini.
  Kwa upande mwingine mkutano huu umejadili pia hatua iliyofikiwa katika uandaaji wa itifaki ya hadhi na kinga kwa watumishi wa jumuiya na taasisi zake zote.

  0 0

  Ulifika wakati wa wageni waalikwa mbalimbali kuserebuka na muziki mzuri uliokuwa ukiporomoshwa na bendi ya B Band,kwenye hafla ya "Marketer's Night Out ",ambapo msemaji mkuu alikuwa ni Dkt.Wale Akinyemi kutoka nchini Nigeria.Usiku huo ulidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker Lite.
  Msemaji mkuu wa hafla ya "Marketer's Night Out " Dkt.Wale Akinyemi kutoka nchini Nigeria akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani) waliofika kwenye hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa chini ya udhamini mkubwa wa kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker Lite.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Steve Gannon akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali kwenye hafla hiyo ya "Marketer's Night Out " ndani hotel ya Golden Tulip usiku huu jijini Dar.
  Mkurugenzi Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Ephrahim Mafuru akizungmza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya Usiku wa maafisa masoko (Marketer's Night Out),uliofanyika ndani ya hoteli Golden Tulip,Masaki jijin Dar.Usiku huo umedhaminiwa na kampuni ya  bia ya Serengeti kipitia kinywaji chake cha Tusker Lite.
   Mmoja wa watangazaji mahiri kutoka kituo cha redio, Eastafrica Radio atambulikae haswa kwa jina la Zembwela akijitambulisha mbele ya hafla maalum ya Usiku wa Maafisa Masoko kutoka makampuni mbalimbali,ndani ya Golden Tulip,Masaki jijin Dar.
   Pichani shoto ni Meneja Masoko wa Multchoice-Tanzania, Furaha Samalu akiwa na msemaji mkuu wa hafla ya  Marketer's Night Out,Dkt.Wale Akinyemi kutoka nchini Nigeria.
  Pichani kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Tusker Lite,Anitha Msangi akiwa na mdogo wake wakifurahia jambo.
  Baadhi ya Wanamuziki wa bendi ya B Band inayoongozwa na Banana Zorro wakitumbuiza usiku huu wenye hafla fupi ya Usiku wa Maafisa Masoko (Marketer's Night Out),iliyofanyika  kwenye moja ya ukumbi wa mikutano wa hotel ya Golden Tulip,Masaki jijini Dar.Usiku huo umedhaminiwa na kampuni ya  bia ya Serengeti kipitia kinywaji chake cha Tusker Lite.KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 04/25/13--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Sipho "Hotstix" Mabuse anaungana nasi kusherehekea Mungano kwa ngoma ya 'Zanzibar'

  0 0
 • 04/25/13--21:00: IN LOVING MEMORY

 • Dear Dad - Adolf IsariaMkony

  Remembering You on your Birthday.

  Born 26/4/1948 passed on 26/12/2002

  We know that today was his Special day!

  a celebration of his birthday,

  It's always hard to face this day

  now that he is gone ten year ago,

  But the memories that he left behind

  Lives on in our heart,

  And will always serve to give comfort

  when the tears begin to flow,

  and we are missing him.

  He know's you are thinking of him,

  so just say .... Happy Birthday Dad!


  Missed by your loving wife, sons, daughters, grandchildren, brothers,sisters, friends and relatives.


  The lord giveth, the Lord taketh

  His name be Glorified.  Amen.


  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya vinywaji baridi ya PEPSI kwa Bara la Asia, Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Saad Abdul Latif, hivi karibuni alifanya ziara nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya ziara ya kuzitembelea nchi za ukanda wa Afrika Mashariki (Kenya, Tanzania na Uganda). 
  Katika ziara hiyo, Bw. Latif, aliambatana na Rais wa Kampuni hiyo ya PEPSI kwa bara la Asia, Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Sanjeev Chadha, ambapo waliweza kukutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo. 
  “Ni furaha kubwa kuwa hapa nchini Tanzania. Kubwa ninaomba muwe na uhaikika ya kwamba Kampuni ya PEPSI, imedhamiria kuhakikisha kwamba wateja wake wanafurahia bidhaa zenye ubora wa kimataifa katika bei nafuu zilizo za kirafiki,” alisema Bw. Latif. 
  Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Bi. Mapunjo aliishukuru Kampuni hiyo ya PEPSI kutokana na ahadi yake iliyojiwekea ya kusaidia katika suala zima la maendeleo ya kiuchumi hasa katika juhudi zake za kuboresha viwanda, masoko, miundombinu na usambazaji. 
  “Kampuni ya PEPSI nchini (SBC Tanzania) inazalisha na kutengeneza nafasi za ajira nchini Tanzania,” aliongeza Bi. Mapunjo. 
   Hivi karibuni Kampuni ya SBC imeanzisha kiwanda cha kisasa cha PEPSI katika jiji la Nairobi, ambapo matokeo yake yamekuwa mazuri naya kutia moyo kutoka kwa wateja. SBC si tu inatoa chaguo la ziada kwa wateja wake kwenye vinywaji vyake, lakini pia inatoa thamani ya ziada kwa fedha. 
  Vinywaji hivi vya PEPSI venye ujazo wa 350 ML kwenye glasi kinauzwa bei ya kawaida ambayo ni sawa na bei ya chupa yenye ujazo wa 300 ML. Ni pamoja na Pepsi, Mirinda, Mountain Dew na aina tofauti za Evervess 
  Kampuni ya SBC Tanzania, ni kampuni pekee inayozalisha bidhaa mbalimbali za PEPSI nchini Tanzania.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa  PepsiCo, Asia, Mashariki ya Kati na Africa Bw. Saad Abdul-Latif (shoto) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa SBC Tanzania Bw. Ziad El Khalil.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Joyce Mapunjo akifurahia jambo na Bw. Saad Adbul-Latif.

  0 0


  Bendi ya muziki wa dansi "Ngoma Africa Band" a.k.a FFU UGHAIBUNI  yenye maskani nchini  Ujerumani inawatakia kila la heri na fanaka ya MIAKA 49 YA MUUNGANO wa jamuhuri ya TANZANIA, watanzania wote popote walipo. Muungano wetu wa bara na visiwani ni muungano wa undugu wa damu.
  Mungu Ibariki Tanzania,
  Mungu Ubariki Muungano wetu.

  Usikose kupata burudani kamili at http://www.ngoma-africa.com  au

  0 0
  0 0


  Blog ya Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini, Washington, DC, Marekani na Jumuiya ya Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia wanapanga kusheherekea miaka 3 ya Vijimambo na kukuletea tamasha ni kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ili watoto wanaoishi huku waweze kuendeleza matumizi ya lugha hii na utamaduni wake kizazi hadi kizazi. 

  Siku ya July 6, 2013  hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center lililopo 
  207 w Hampton Pl, 
  Capitol Height, MD

  Mambo mengi yatakuwepo, Vikundi mbalimbali vya utamaduni, Mitindo ya mavazi kutoka Tanzania na hapa Marekani, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani na hapa Marekani yote ni kudumisha utamaduni wetu wa kiswahili

  TEGA SIKIO, HABARI ZAIDI ZITAFUATA
  -------------------------------------------------------
  kwa wajasiliamali ambao wangepenga kudhamini na kuijipatia meza ya kutangaza bidhaa au shughuli wazifanyazo tafadhali wasiliana 301 613 5165, 301 661 6696 na 301 792 8562 mwisho ni June 1, 2013 Asante


  NO COVER CHARGE, FREE DINNER  0 0

   Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiingia uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam leo kuongoza Watanzania kusherehekea miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Pamoja naye kwenye gari hilo la wazi ni Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange
   Nyomi si ya kawaida hata pa kutema mate hakuna
   Msafara wa Rais Kikwete ukizunguka uwanja wa Uhuru
  Nyomi ya leo. Taswira zingine na kumwaga baadaye.


  0 0
  0 0


  NduguWaTanzania,

  Kwa Niaba ya TAWI la Chama Cha Mapinduzi Uingereza ,na kwa niaba yangu binafsi, Napenda kutoa salamu za dhati kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein, kwa Serikali ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania,na kwa WaTanzania wote kwa ujumla kwa kutimiza miaka 49 ya Muungano wa nchi yetu, TANZANIA.

  Pamoja na salamu hizo, binafsi na kwaniaba ya wana CCM UK ,napenda kuwaomba na kuwakumbusha WaTanzania wenzangu, tuendelee kuuenzi na kuulinda Muungano wetu kwa kudumisha AMANI, UPENDO, UMOJA, UTULIVU na MSHIKAMANO. Hizi ndizo silaha zilizoweza kuulinda Muungano huu ambao umetuletea Heshima ya kipekee Duniani kote, kwa takriban nusu karne sasa.

  Ndugu WaTanzania,  nawasihi kamwe tusichezee amani tuliyonayo. Tujifunze kutoka nch mbalimbali duniani ambazo wamechezea amani yao na sasa wamo ndani ya dimbwi kubwa la machafuko, mauaji ya halaiki na yanayoendelea kila kukicha.  Maelfu ya raia wasio na hatia wamepoteza maisha yao katika Nchi mbalimbali, wengine kupata ulemavu wa kudumu, kupoteza makazi na kuharibikiwa na mwenendo mzima wa mfumo wa maisha yao, milipuko ya mabomu isiyoisha na raia kukosa amani na utulivu. WaTanzania kamwe tusikubali  kuipoteza amani yetu kwa uchochezi wa watu wachache, na ambao kwa sababu zao binafsi hawatutakii mema , na mpaka wako tayari kutumia visingizio kama vya siasa na dini ili watusambaratishe.  Aidha, WaTanzania wa Nje ya Nchi (Diaspora)tunajivunia na kutambua kwamba tuna nafasi ya pekee ya kuchangia katika maendeleo ya Nchi yetu Tanzania katika Nyanja tofauti . Mojawapo ya Mchango wetu Mkubwa kwa Taifa ni kufuatilia kwa ukaribu mambo yanayoendelea nyumbani ,nakutoa mchango wetu wa kimawazo pale inapobidi.

  CCM-UK tutaendelea kutoa shukrani za dhati kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhur iya Muunganowa Tanzania Dr.JakayaMrishoKikwete , pamoja na Serikali yake anayoiongoza kwa kuona umuhimu wa kutushirikisha WanaDiaspora na kuthamini mchango wetu.Tunafarijika sana na kuahidi siku zote kwamba tutaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Tanzania, kama inavyowezekana kwa raia wengine

  Weng Ulimwenguni wanaoishi nje ya Nchi zao na wanachangia kukuza uchumi na kuendeleza jamii zao kwa kutumia ujuzi na ufanisi waliojifunza ughaibuni.

  MWISHO WaTanzania wenzangu, tusherehekee sikukuu ya Muungano wetu kwa Amani na Utulivu, tuvumiliane na sote tutie nia ya kudumisha na kuulinda Muungano wetu na kuwapuuza wale wote wasioutakia wema Muungano wetu.

  Tuwaenzi waasisi wetu Baba waTaifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwa kuulinda Muungano, kudumisha amani na utulivu, aidha kufanya kazi kwa juhudi na kuinua uchumi wa nchi yetu hadi kufikia azma ya - MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, SI NDOTO YANAWEZEKANA.

  Kwa Niabaya CCM UK– Nawatakia WaTanzania wote popote pale walipo Dunian iMaadhimisho na Sherehe njema za siku hii adhimu.


  MUNGU IBARIKI AFRIKA - MUNGU IBARIKI TANZANIA

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

  -----------------------------------------------------

  Mariam A. Mungula

  KATIBU

  CHAMA CHA MAPINDUZI – UINGEREZA


  IMETOLEWA NA IDARA YA ITIKADI, SIASA NA UENEZI – CCM-UK 


  0 0


  0 0


  0 0

   Picha ya mchoro ya kivuko cha  Dar es Salaam – Bagamoyo kitakavyokuwa.

   Mtendaji Mkuu wa TEMESA Mhandisi Marceline Magesa (mwanamke) , na mwakilishi wa kampuni ya  JOHS GRAM HANSSEN A/S ya  Denmark  Andreas Gottrup wakiweka  saini mkataba wa ujenzi wa Kivuko  cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo jijini Dar es Salaam, katika hafla iliyoshuhudiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (aliesimama katikati) Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick(alie vaa  shati la kitenge) Balozi wa Denmark nchini Tanzania  Mh, Johnny Flinto (mzungu aliesimama  mstari wa nyuma). Pamoja na watendaji wakuu wa  Wizara ya Ujenzi. 
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadick Mecky (kulia) akizungumza wakati wa  hafla ya uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa  Kivuko cha Dar es salaam – Bagamoyo. Kivuko hicho kitagharimu shilingi 7.91 bilioni za kitanzania. Mwengine ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli. 
  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (kulia) akiongea na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mh. Johnny Flinto,katika  sherehe ya uwekaji  saini mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaa- Bagamoyo (April 25, 2013).
   baadhi ya viongozi wakiwa katika meza kuu
  Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya TEMESA, Prof. Idrisa Mshoro (kulia) akimueleza  jambo  Mwakilishi wa  kampuni ya JOHS GRAM HANSSEN A/S ya Danmark , Andreas Gottrup wakati wa sherehe za uwekaji saini mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo jijini Dar es  Salaam(April,25,2013). 
   baadhi ya wadau wa wizara ya ujenzi wakishuhudia tukio hilo.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Marceline Magesa (kulia) akizungumza  katika hafla ya uwekaji saini  mkataba wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaam- Bagamoyo leo jijini . Kivuko hicho  kitakuwa na uwezo wa  kubeba watu 300 , kitagharimu  shilingi7.91 bilioni.(bilioni7.91 za tz).Pichani  kutoka kulia ni Waziri wa Uchukuzi Dkt,John Magufuli,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam  Mecky Sadick, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi , Balozi Herbert Mrango.Picha zote na Mwanakombo Jumaa.


older | 1 | .... | 112 | 113 | (Page 114) | 115 | 116 | .... | 3285 | newer