Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live

DAR ES SALAAM CINEMA GALORE UPDATES

0
0

CENTURY CINEMAX MLIMANI CITY | NOW SHOWING:
(26 APRIL – 02 MAY 2013)

[OBLIVION [PG-13]*Tom Cruise
[- 12 pm*/ 2:30 pm / 5 pm / 7:30 pm & 10 pm]

[A HAUNTED HOUSE [R]* Marlon Wayans- 6 pm / 8 pm & 10 pm ]

[OLYMPUS HAS FALLEN [PG-13]*Gerard Butler, Morgan Freeman

-5pm / 7:30 pm & 10 pm]

[G.I. JOE RETALIATION 3D [ALL AGES]*Dwayne Johnson
12 pm*& 2:30 pm]

 [THE CROODS 2D [ALL AGES]*2D ANIMATIONS12 pm*/ 2 pm & 4 pm ]

(*12 pm / 12:30)-Shown on SUN & P-HOLIDAY
(*) - ALL 3D & 2D movies price per ticket tsh 10,000
except Tuesdays & Thursdays Tshs 8,000 per ticket(not applicable on public holidays)
 CENTURY CINEMAX - MWENGE BRANCH | NOW SHOWING:
(26 APRIL – 02 MAY 2013)
[NEW WORLD CINEMAS - MWENGE]
*All Shows-Everyday -Price per ticket Tshs 7000 only

[EK THI DAAYAN [ALL AGES] *Emraan Hashmi
 – 2:30 pm / 5 pm / 7:30 pm & 10 pm]

 [COMMANDO – ONE MAN ARMY [ALL AGES] *Vidyut Jamwal
 – 2:30 pm / 5 pm & 7:30 pm]

*Mondays closed, except public holiday

FOR FORTHCOMING MOVIES STARTING  FRIDAY 03RD MAY 2013:

ECOBANK TANZANIA KUKUZA BIASHARA KATI YA TANZANIA AND CHINA

0
0
Ecobank Tanzania Limited, ambayo ni mojawapo ya benki katika kundi la Ecobank jana imezindua rasmi kitengo cha China kiitwacho ‘China Desk’ katika hafla ya Chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Great Wall Masaki, Dar es Salaam. Benki hiyo pia imezindua ununuzi wa moja kwa moja wa sarafu ya kiChina RMB ambayo imewalenga wafanyabiashara wanao nunua bidhaa kati ya China na Tanzania. Hafla hii iliwavutia watu wapatao 180 hasa wawekezaji wa kichina na Tanzania pamoja na wana habari.

“Kundi la Ecobank limeweka mkakati wa ushirikiano na benki ya China ili kusaidia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China. Katika mwaka uliopita, biashara kati ya nchi hizi mbili ilifikia $2.5 billioni. Sio ajabu kwamba Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza Africa kutembelewa na Rais Mhe. Xi Jinping. Ndani ya mwaka uliopita, biashara kati ya nchi hizi mbili imeongezeka kwa asilimia 15%! Ni wakati mwafaka sisi kuzindua kitengo cha China hapa Tanzania kama ilivyo katika Ecobank nchini zingine barani Africa” Alisema Bw. Enoch Osei-Safo Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania.

Pamoja na uzoefu wa miaka 25 katika nchi 32 za Afrika, Kundi la Ecobank lina rekodi ya mafanikio katika huduma za benki kwa wafanyabiashara wa Kichina katika Afrika. Hakika, Ecobank kupitia muundo wa kimataifa wa usimamizi wa akaunti iliyopo nchini China imesaidia biashara nyingi za kiChina kuendesha biashara na uwekezaji katika nchi tofauti barani Afrika.

Katika mwaka wa 2012, Ecobank ilifungua ofisi wakilishi Beijing, ambayo inasimamia uhusiano kati ya Ecobank na biashara za kiChina barani Africa na Kampuni zilizopo Afrika zinazofanya biashara nchini China. Kupitia kitengo hicho kilichopo Beijing na mtandao wa Ecobank barani Africa, benki hii imejitokeza kama njia ya kukuza bishara kati ya China na Afrika.

Uwekezaji wa China katika Afrika umeongezeka kutoka $ 900 milioni katika mwaka 2000 hadi $ 68 bilioni katika 2010 ambayo ilisaidiwa na sera ya 'Chinafrique' inayoendeleza biashara bila vikwazo. “Uwekezaji kutoka China unazidi kukua na ofisi yetu Beijing inapokea maombi mengi sana ya ushauri wa uwekezaji Afrika.” anasema Lu Xiaoning, Meneja wa ofisi wakilishi Beijing. Hivi karibuni, Mheshimiwa Zhou Yi, mmiliki wa Hengxu ambalo ni Kundi la Makampuni iliyo na makao makuu katika Mkoa wa China Sichual, aliweka wazi mipango ya kuwekeza $ 700 milioni katika ujenzi wa hoteli ya kifahari katika mbuga ya Serengeti, Tanzania.

"Kwa wawekezaji kama Mr Yi, thamani yetu ni rahisi kwa huduma mbalimbali tunazotoa kwa soko hili la kipekee". Anasema Mr.Enoch Osei-SAFO. "Tunazidi kusaidia kukuza uwezo wa jumuiya ya biashara ya Tanzania katika kuchukua fursa zilizopo kukuza uchumi, kwa njia ya mafunzo pamoja na washirika wetu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Benki Kuu ya Tanzania na vyombo vya habari. Hii yote inafanyika katika utekelezaji wa kauli mbiu yetu, Ecobank Inatuwezesha ampayo ina lengo la kujenga uwezo kwa Tanzania kuongeza fursa za kiuchumi, “aliongeza.

Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.ecobank.com

 Bw. Enoch, Bi. Lu Xiaoning ambaye ni Meneja wa Ofisi wakilishi ya Ecobank mjini Beijing pamoja na Bw. Erick Mushi wakifurahia habari za uendeshwaji mzuri wa biashara kati ya Ecobank Tanzania na Ofisi wakilishi Beijing.

Virginia Cortavitare na Eric Tirabassi kutoka Tanzania Invest pamoja na MkurugenziMtendaji wa Ecobank Tanzzania Bw. Enoch Osei-Safo na Mshauri wa PR nchini Daisy Mumbi wakijadiliana swala kwenye hafla ya chakula cha jioni katika hoteli ya Great Wall Masaki

Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Bw. Enoch Osei Safo akihojiwa na wanahabari kuhusu uhusiano wa Ecobank na wafanyabiashara kati ya Tanzania na China

BE THE FIRST TO KNOW...

0
0

KFC will open to the public on WEDNESDAY 1 MAY at 11h00! The joint is  located on  MWAI KIBAKI road (former Old Bagamoyo road), opposite FEZA School in Mikocheni, Dar es salaam.




GOLDEN BUSH YAWALAMBA WAHENGA BAO 2-1

0
0
Jana Wazee wa kazi Golden Bush walikutana na wazee wenzao Wahenga katika mechi ya kirafi ikiwa na sehemu ya kusherekea siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mechi lichezwa uwanja wa TP Tandale jijini Dar es salaam ambapo wapenzi wa soka walishuhudia Wahenga wakikubali kipigo cha goli 2-1. 
Magoli yote yalifungwa katika kipindi cha pili huku Golden Bush wakianza kufumania nyavu kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Athuman Machuppa alieunganisha pasi safi kutoka kwa Shaban Kisiga “Maloni”. Golden bush walifunga goli la pili kupitia kwa Shaban Kisiga aliyepiga chenga ngome yote ya Wahenga na kutumbukiza mpira wavuni. Wahenga walijipatia goli la kufutia machozi katika dakika ya za lala salama kwa njia ya mkwaju wa Penalty ikiwekwa wavuni na Macocha Tembele. 
 Hadi mwisho wa mchezo Golden Bush chini ya Mwalimu wao Maradaraka Seleman “Mzee wa Kiminyio” waliibuka kidedea na kushehekea sikukuu ya mapinduzi kwa furaha kabisa. 
 Golden bush Veterans wako katika maandalizi ya mwisho kabisa kuelekea Tanga kwa ajili ya mechi za kirafiki na veterans ya huko. Imetolewa na msemaji wa na mchezaji mwandamizi wa golden bush Fc bwana Onesmo Waziri “Ticotico”
Golden Bush FC
Wahenga FC
Mchezo ukiendelea kwa nguvu katikati ya uwanja

Wake-Up Motivational Talks Series DVD

Mdau alex kusaga wa Clouds Media Group auaga rasmi ukapera jioni ya leo.

0
0
 Bibi harusi,Evelyne Julla akitoa tabasamu la nguvu na lenye furaha mara baada ya kuikamilisha ndoto yake ya kumpta mwenza wake wa maisha,Bwa.Alex Kusaga wa Clouds Media Group.
 Maharusi wakizifurahia pete zao za ndoa mara baada ya mapumziko mafupi kabla ya kuingia mnusoni jioni ya leo ndani ya hotel ya Serena jijini dar.
 Wakishoo love na mdogo wake Alex Kusaga,ambaye ni wifi ya bibi harusi.
 Maharusi wakionesha   vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufunga harusi ndani ya kanisa la St.Immaculata,Upanga jijini Dar.
 Maharusi wakila kiapo cha ndoa 
Maharusi wakiwa katika sura za furaha kabisa wakitoka nje ya kanisa mara baada ya kutimiza ndoto yao ya kuishi pamoja,baada ya hapo usiku huu mnuso uko ndani ya Serena hotel.

JK amkaribisha Rais Uhuru Kenyatta Arusha

0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais wa Kenya Mhe Uhuru Kenyatta katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro wakati alipowasili leo jioni kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki unaofanyika jijini Arusha.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Mkewe Margareth Kenyatta wakifurahia ngoma za utamaduni muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijijini Arusha. Picha na Freddy Maro

Red Carpet Swagga @ Bongo Black Ball - celebrating Tanzanian Music held at Mlimani City Dar

0
0
Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House (TMH) Khadija Mwanamboka (kushoto) ambaye pia ndio Mwandaaji wa Bongo Black Ball Party iliyobeba Theme " Celebrating Tanzania Music" kupitia kampuni yake ya Vitu vya Khadija Events & Clothing akiwa na wadau mbalimbali kwenye mnuso wa nguvu uliowakutanisha Masupastaa wa Bongo wadau waliopo kwenye Fashion Industry katika usiku uliopambwa na msanii Mkongwe wa muziki nchini King Kiki a.k.a mzee wa kitambaa cheupe pamoja na burudani kutoka kwa wasanii wa Bongo Flava Linex na Mwasiti. Pichani Bi. Khadija Mwanamboka akiwa na wageni mbalimbali kwenye Red Carpet ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
Designer Ally Rehmtullah ndani ya nyumba.
Blogger Missie Popular aliwakilisha kikazi zaidi.
Gyver Meena and Salma Msangi a.k.a Kimora Lee looking Gorgeous (I think these two Girls rock the night).
Mama Mia....Wow.....!
Kwa picha zaidi Bofya hapa

WANAFUNZI WA VYUO VIKUU 13 WASHIRIKI KWENYE WARSHA YA MAANDALIZI YA AJIRA PINDI WAMALIZAPO MASOMO YAO

0
0
 Rais wa chama cha wanafunzi wa vyuo vikuu(AIESEC)Bw.Frank Mushi,akiongea katika warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira pindi wanapomaliza masomo ya vyuo vikuuwarsha hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
 Wanafunzi wa vyuo vikuu 13 walioshiriki katika warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira pindi wanapomaliza masomo yao ya  vyuo vikuu,warsha hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
 Ofisa raslimali watu wa Vodacom Tanzania,Bw.Stephen Kisanko,akiongea na waandishi wa habari juu ya udhamini wa warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira pindi wanapomaliza masomo yao ya  vyuo vikuu warsha hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Masoko wa chama cha wanafunzi wa vyuo vikuu(AISEC)Bw.Elvis Kashaija,akiongea na waandishi wa habari juu ya maandalizi na umuhimu wa vijana kushiriki katika warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira pindi wanapomaliza masomo yao ya  vyuo vikuu warsha hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
 Ofisa raslimali watu wa Vodacom Tanzania,Bw.Stephen Kisanko,akitoa mada kwa wanafunzi  juu ya maandalizi na umuhimu wa vijana kujiandaa katika kuingia kwenye ajira pindi wamalizapo masomo yao ya vyuo vikuu,wakati wa warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira warsha hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania .iliyofanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Wanafunzi wa vyuo vikuu 13 walioshiriki katika warsha ya 14 inayohamasisha vijana kujianda katika ajira pindi wanapomaliza masomo yao ya  vyuo vikuu,warsha hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa Nkuruma,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Red Coast, Abajalo, Friends Rangers zafuzu hatua ya Kanda

0
0

Ligi Daraja la Pili mkoa wa Dar es Salaam hatua ya sita bora imemalizika leo kwa timu tatu za Red Coast,  Abajalo na Friends Rangers zimefuzu kucheza hatua ya Kanda.
Katika mechi iliyochezwa Makurumla, Friends Rangers iliifunga Sharif Stars mabao 2-0. Mabao hayo yamefungwa na Khatib Kuduku katika dakika ya 12 na Mwenda Athuman katika dakika ya 57.Kwa matokeo hayo Rangers imefikisha pointi 8.
Kwenye uwanja wa Kinesi Red Coast wameibuka na  ushindi wa bao 1-0.Bao hilo limefungwa dakika ya 32 na Rafael Mapunda. Kwa matokeo hayo Red Coast wamefuzu hatua hiyo kwa kujikusanyia pointi 11 wakiwa vinara wa ligi hiyo.
Abajalo nao wamefuzu hatua hiyo baada ya kuichapacha Boom FC mabao 2-0. Hata hivyo mechi hiyo ilivunjika kutokana na wachezaji watatu wa Boom FC kutolewa kwa kadi nyekundu.Abajalo imeweza kufuzu baada ya kujikusanyia pointi 10.
Imetolewa na Ofisa Habari wa DRFA
MOHAMED MHARIZO

KENYA YAIMWAGIA SIFA KEMKEM KAMPUNI YA MCDONALD LIVE LINE TECHNOLOGY YA TANZANIA

0
0
 Mmiliki wa Kampuni ya McDonald Live Line Technology, McDonald Mwakamele (kulia) akiwaonesha maofisa kutoka Kampuni ya Umeme ya Kenya (KPCL), vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengeneza umeme bila kuuzima walipotembelea chuo cha kampuni hiyo, mwanzoni mwa wiki, wilayani Mvomero, Morogoro. Kenya iko mbioni kuingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya mafundi wao kufundishwa teknolojia hiyo ya kisasa. Kutoka kushoto ni maofisa wa KPCL, Meneja Uendeshaji, Noah Ogano, Peter Waweru na Mhandisi Charles Mwaura ambaye ni Naibu Meneja Huduma za Kawaida.
 Mwakamele akiwaonesha maofisa wa KPCL, baadhi ya vifaa vinavyotumika katika kazi hiyo. (PICHA ZOTE KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mwakamele akiwaonesha maofisa wa KPCL kifaa kinachotumika kubebea nguzo.
 Mwakamele akiwaonesha gari maalumu linalotumika kumpeleka fundi kutengeneza nyaya na vikombe juu ya nguzo.
 Mwakamele akionesha jinsi ya kutengeneza vikombe vya umeme
 Mwakamele akiwa juu ya nguzo akionesha jinsi ya kutengeneza umeme bila kuukata. (PICHA ZOTE KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Naibu Meneja wa KPCL, Mhandisi Charles Mwaura akikabidhiwa na Mwakamele mavazi maalumu ya kazi yasiyopisha umeme.
 Mhandisi Mwaura wa KPCL, akivishwa na Mwakamele moja ya mavazi hayo
Mhandisi Mwaura akimshukuru Mwakamele


Na Mwandishi Wetu, Morogoro

UONGOZI wa Shirika la Umeme nchini Kenya(KPLC), umesema kuwa unaangalia namna ya kuingia makubaliano ya wataalamu wake kuja nchini Tanzania ili kujifunza kutumia teknolojia ya kufanya matengenezo ya umeme bila kuukata.
 
Uamuzi huo unatokana na kile ambacho uongozi huo umeeleza wananchi wa Kenya wamechoshwa na tabia ya kukatiwa umeme wakati yanapofanyika matengenezo wakati wa kubadili nguzo au vikombe  na sasa wameamua kutafuta dawa ya tatizo hilo.

Wakizungumzia wiki hii mkoani Morogoro walipotembelea kampuni pekee Afrika Mashariki na Kati inayoweza kutengeneza umeme bila kuukata ya McDonald Liveline Technology, walisema wamefurahishwa na teknolojia hiyo na imebaki kwao kuamua ni wataalamu wangapi wajifunze kwa maslahi ya nchi yao.
Walisema kuwa wamefika mkoani hapa kwa sababu tu ya kuridhishwa na utendaji kazi wa kampuni ya McDonald Liveline Technology na kwamba wakiwa nchi jirani wana haki ya kupata utaalamu huo na ndio maana wamefunga safari ili kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Donald Mwakamele.
Akizungumza zaidi akiwa katika eneo ambalo Kampuni ya McDonald imefunga mitambo yake kwa ajili ya kutoa mafunzo 'Liveline' Meneja wa Operesheni na Huduma wa KPLC Noah Omondi, alisema kuwa Tanzania imepata bahati ya kuwa na mtaalamu huyo na wao watamtumia kwa ajili ya kufanikisha malengo ya nchi yao ya kutokata umeme ovyo wakati wa matengenezo.
Omondi aliyekuwa ameambatana na Mwalimu wa matengenezo ya mtandao wa ugavi wa umeme Peter Waweru na Meneja msaidizi wa huduma na matengenezo wa mkoa wa Nairobi Charles Mwaura alisema kuwa kikubwa ambacho wao wanakitazama sasa ni kutafuta ufumbuzi wa umeme nchini mwao na kwamba hawatarudi nyuma.
Akizungumza zaidi kuhusu kampuni yake Mwakamele alisema teknolojia hiyo ni muhimu kwa nchi mbalimbali na kwamba kuifahamu kwake teknolojia hiyo ameweza kufanya kazi katika mataifa makubwa duniani ikiwemo Marekani na nchi nyingine za Afrika.

Alisema hakuna sababu ya kukata umeme wakati unapoamua kutengeneza kwani teknolojia ambayo inaweza kutumika kufanya matengenezo bila kukata umeme ipo na kwake inapatikana muda wote.

Aliongeza kukata umeme wakati wa matengenezo ni kusababisha hasara ambayo inaweza kuepukika kwa kutumia teknolojia ambayo yeye anaifahamu na anaifundisha.
"Hakuna sababu ya kukata umeme,  njia mbadala ipo ambayo unaweza kuitumia kwa kufanya matengenezo bila kuukata.Tunaifanya teknolojia hii katika nchi mbalimbali.Nipo tayari kuifanya popote na wakati wowote ninapohitajika,"alisema Mwakamele.
Alisisitiza endapo teknolojia hiyo ya matengenezo bila kukata umeme itatumika, Tanzania itaweza kuokoa fedha na muda ambavyo vimekuwa vikipotea kila umeme unapokatwa kwa ajili ya matengenezo kama ya kubadilisha nguzo au kukata miti iliyo karibu na nyaya za umeme.
Hata hivyo alisema anaguswa na uzalendo wa nchi yake, na ndio maana kila mara amekuwa akiwataka watalaamu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kufika chuoni kwake kujifunza teknolojia hiyo ambayo ni muhimu katika kipindi hiki kwa maslahi ya taifa.

ngoma azipendazo ankal

0
0
John Lissu pamoja na kundi lake zima la nyimbo za Injili wamezidi kufanya vizuri kwa kutoa nyimbo na video bora kwa viwango vya juu. Tutazame video hii iliyofanyiwa kazi jijini Dar-es-Salaam, Tanzania. Tuwaunge mkono kwa kununua kazi zao original.

TOKA MAKTABA YA GLOBU YA JAMII

0
0
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa na Rais wa Cuba, Fidel Alejandro Castro Ruz, Rais wa Zaire, Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Za Banga na Rais wa Zambia Dkt Kenneth David Kaunda katika maongezi ya pembeni ya mkutano wa kimataifa

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA LA TZ METHODIST MSASANI NA KUZINDUA CD YA KWAYA YA WATOTO WANAOFADHILIWA NA COMPASSION INTERNATIONAL TZ

0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya maua kutoka kwa watoto wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, wakati alipowasili katika kituo hicho leo kwa ajili ya kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili katika Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, leo kwa ajili ya kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, Joseph Mayala, leo  wakati wa hafla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo. Kulia ni Askofu wa Kanisa hilo, Dkt. Mathew Byamungu. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia waumini wa dini ya Kikristo wa Kituo cha Kanisa la Tanzania Methodist la Msasani, wakati alipowasili katika kituo hicho leo kwa ajili ya kuhudhuria harambee ya kuchangia ujenzi wa Kituo cha Kanisa hilo iliyofanyika sambamba na Ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya Shirika la Compassion International Tanzania kwa kuingia Ushirika wenza na Makanisa ya Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua Cd ya Kwaya ya Watoto wanaofadhiliwa na Shirika hilo.
 Baadhi ya waumini waliohudhuria harambee hiyo.
 Watoto wa Kwaya inayofadhiliwa na Shirika la Compassion International Tanzania, wakitoa burudani ya kuimba moja ya wimbo wao ulio katika Albam yao iliyozinduliwa katika hafla hiyo.Picha na OMR.

WARATIBU WA MIKOA WAKITATHMINI MCHAKATO WA UCHAGUZI WA WAJUMBE WA MABARAZA YA KATIBA YA WILAYA

0
0
Mratibu wa Mkoa wa Pwani katika mchakato wa upatikanaji wa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, Mohamed Magati akizungumza katika kikao cha tathimini baina yao na Wajumbe wa Sekreatarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kilichofanyika katika Ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam leo jumamosi (April 27, 2013).
Mratibu wa Mkoa wa Ruvuma katika mchakato wa upatikanaji wa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, Christina Kumwenda akizungumza katika kikao cha tathimini baina yao na Wajumbe wa Sekreatarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kilichofanyika katika Ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam jumamosi April 27, 2013.
Mratibu wa Mkoa wa Shinyanga katika mchakato wa upatikanaji wa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, Godfrey Kajia akizungumza katika kikao cha tathimini baina yao na Wajumbe wa Sekreatarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kilichofanyika katika Ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam jumamosi April 27, 2013.
Waratibu wa mchakato wa upatikanaji wa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya katika mikoa 30 ya Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Uratibu katika Tume, Joseph Ndunguru (wa pili kulia, mstari wa mbele) mara baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika katika ofisi za Tume Jijini Da re s Salaam Jumamosi April 27, 2013. PICHA NA TUME YA KATIBA.

UZINDUZI RASMI WA SHINDANO LA "REDD'S MISS TABORA 2013" WAFAANA NDANI YA UKUMBI WA FRANK MAN PALACE HOTEL

0
0
AFISA UTAMADUNI MKOA WA TABORA BW. KATUNZI KATIKA UZINDUZI WA SHINDANO LA MISS TABORA 2013, NDANI YA UKUMBI WA FRANKMAN PALACE HOTEL.
MKALA FUNDIKIRA AMBAYE NI MWENYEKITI  WA KAMATI MAANDALIZI YA SHINDANO, AKIELEZEA UFAAFU NA TASWIRA YA MABADILIKO YA HALI YA JUU YA SHINDANO LA MISS TABORA 2013
NASSOR WAZAMBI, MJUMBE WA KAMATI YA MAANDALIZI YA MISS TABORA 2013 AKIKAZIA MIPANGO YA MABORESHO YA SHINDANO LA UREMBO MKOANI TABORA
DADAZZZ WAKIPIGA KWITO MWANZO MWISHO
AFISA UTAMADUNI MKOA WA TABORA, BW. KATUNZI AKIZINDUA SHINDANO KWA KUKABIDHI FOMU KWA MOJA YA WASHIRIKI 
BAADHI YA WASHIRIKI WALIOJICHUKULIA FOMU ZA USHIRIKI
KUSHOTO: DIANA, ZENNA (MISS SINGIDA 2012) NA KALUNDE

WAREMBO NDANI YA UKUMBI WA FRANKMAN PALACE  HOTEL

(PICHA NA: AloySonBlog)
== == ==
BW. KATUNZI ALIPONGEZA JITIHADA ZILIZOFANYIKA KUHAKIKISHA MKOA SASA UNAJIKITA KATIKA FURSA NZURI ZA KUWAWEKA SAWA VIJANA HAPO MKOANI NA ZAIDI KUNUFAISHA JAMII YA WANATABORA.

AMETOA WITO KWA JAMII KULIPOKEA SHINDANO HILO VYEMA NA KUTOA USHIRIKIANO WOWOTE UNAPOHITAJIKA, IKIWA YEYE MWENYEWE AMESEMA ATAKUWA MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA SHINDANO LINAFANYIKA KWA UFASAHA WA HALI YA JUU.

AKIONGEZEA, AMESEMA KUWA WAZAZI WANATAKIWA KUWA NA MWITIKIO MZURI KWA WATOTO WAO WAKITAKA KUONESHA VIPAJI VYAO KWENYE FURSA MBALIMBALI ZITAKAZO WANUFAISHA KIMAISHA WATOTO WAO.

PONGEZI KUBWA ZILITOLEWA PIA KWA WATU, MAKAMPUNI NA YEYOTE AFANIKISHIE KUTOA MCHANGO WAKE WA HALI NA MALI KUFANIKISHA MASHINDANO HAYO KUFANYIKA.

Gari litalopiganiwa na mabondia Thomas Mashali na Fransic Cheka siku ya Mei Mosi mwaka huu

0
0

Yasini Abdallah 'Ustadhi', Msemaji wa mbambano wa Thomasi Mashali na Fransic Cheka akiwa akiwaonesha wana habari gari  litagombaniwa kama zawadi na mabondia hao

JK AOMBOLEZA KIFO CHA MJUMBE WA BARAZA LA SENETI LA KENYA MAREHEMU MUTULA KILONZO

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kuomboleza kifo cha Mjumbe wa Baraza la Seneti na Waziri muhimu wa zamani wa nchi hiyo, Mheshimiwa Mutula Kilonzo (pichani), aliyefariki dunia juzi, Ijumaa, mjini Nairobi.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kikwete amemwambia Rais Kenyatta kuwa amepokea habari za kifo cha ghafla cha mwanasiasa huyo kwa mshtuko na huzuni na kuwa kifo chake kimeipokonya nchi hiyo mmoja wa viongozi waliokuwa wanajali na kutanguliza maslahi ya Kenya na wananchi wake.

“Kwa hakika, kifo cha Mheshimiwa Mutula Kilonzo kimeipokonya Kenya kiongozi muhimu. Mchango mkubwa aliuotoa katika kipindi cha kuivusha Kenya kutoka kwenye changamoto za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 hadi sasa ambako nchi imetulia na inasonga mbele, kamwe hautasahaulika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Katika nafasi zote za Uwaziri alizozishikilia katika kipindi hicho, kwanza kama Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba na baadaye kama Waziri wa Elimu, alijithibitisha na kujipambanua kama Mzalendo wa kweli kweli wa Kenya na mpenzi halisi wa nchi yake.”

Ameongeza Rais: “Nakutumia Mheshimiwa Rais salamu zangu za rambirambi na zile za Serikali yangu kufuatia msiba huu. Aidha, kupitia kwako naomba unifikishie salamu zangu kwa familia ya Mheshimiwa Kilonzo. Nataka wajue kuwa niko nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na naungana nao kuomboleza na kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mutula Kilonzo.Amin.”


Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

IKULU,

DAR ES SALAAM

 28 Aprili, 2013

RATIBA YA MAZISHI YA NDUGU ADOLPH BRIAN THADEO LWAKAJENDE SIKU YA MEI MOSI

0
0

Adolph, Brian au Thadeo Lwakajende
 Enzi ya uhai wake

TUNAPENDA KUWATANGAZIA KWAMBA ILE HARAMBE YA ADOLPH BRIAN ILIYOKUWA IFANYIKE LEO JUMAPILI SAA 10 JIONI NEW YORK, HAITAFANYIKA TENA BAADA YA KUJITOKEZA WAFADHILI KUTOKA BUKOBA NA NEW YORK WATAKAO GHARAMIA GHARAMA ZA MAZISHI YA MAREHEMU YATAKAYOFANYIKA JUMATANO MAY 1, 2013

       RATIBA YA MAZISHI NI KAMA IFUATAVYO

     VIEWING:            LEE.O.WOOD FUNERAL HOME
                                      23 EAST 2ND STREET
                                     MT.VERNON,NY,10552   
                                    TIME:  10:00 AM/ 4 ASUBUHI

     MAZISHI :                  MT.PLEASANT CEMETERY 
                                      80 COMMERCE STREET
                                       HAWTHORNE,NY,10532 
                                       TIME: 1:00PM/7 MCHANA

KWA MAELEKEZO ZAIDI WASILIANA NA:

   RAHMA ADAM.........617 818 7657
  PETER LUANGISA...917 681 6971
  RASHIDI KAMUGISHA...973 703 4596
  BERNARD KIVUGO.......973 580 7166
  WILLIAM VEDASTO......973 551 2916

TAFADHALI MTAARIFU MTANZANIA MENZAKO UKIPATA UJUMBE HUU.  

JK, UHURU KENYATTA NA PIERRE NKURUNZINZA JIJINI ARUSHA LEO

0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi na Rais Mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta wakiwaaga wajumbe waliohudhuria mkutano wa Wakuu wa  nchi za Jumuiya ya Umoja wa Afrika ya Mashariki uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo. 
Picha  na Freddy Maro
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live




Latest Images