Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1142 | 1143 | (Page 1144) | 1145 | 1146 | .... | 3283 | newer

  0 0
 • 02/29/16--12:38: TAARIFA YA MSIBA
 • Mrs Elipina Kisamo Mlaki na Linda Kisamo wanasikitika kutangaza kifo cha baba yao mpendwa Dr Michael Kisamo aliyefariki Jumapili 28/2/2016. 

  Mipango ya Mazishi inafanyika Nyumbani kwake Kinondoni Mkwajuni/Sokoni Magengeni. na Mazishi yanataraji kufanyika Usangi Jumatano 2.03.2016.

  Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe

  Ahsante kwa Ushirikiano.

  0 0
 • 02/29/16--13:04: Article 4
 • Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge amezindua mradi wa maji wa Longuo, katika Kijiji cha Longuo, Wilaya ya Moshi mwishoni mwa wiki katika ziara yake mkoani Kilimanjaro. Mradi huo unaohudumia vijiji vya Longuo na Kariwa, umekuwa faraja kubwa kwa wananchi, ambao kwa muda mrefu walikuwa na tatizo la kupata huduma ya majisafi na salama na kusababisha hatari ya magonjwa ya milipuko kwa wananchi.

  Mhe. Lwenge, amefurahishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao umechukua siku themanini tu kukamilika, na kuipongeza Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Moshi (MUWSA) kwa usimamizi mzuri wa mradi huo. Pia, alitembelea chanzo cha maji, chemchemi ya Kisimeni iliyopo Kata ya Uru Kusini ambayo inachangia uzalishaji wa maji katika Wilaya ya Moshi.

  Vilevile, Mhe. Lwenge alitembelea miradi ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA). Katika ziara yake hiyo mkoani Arusha, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, aliweza kufika kwenye chanzo cha maji cha Midawe, kilichopo kwenye Mto Nduruma, katika Kijiji cha Bangata, kilichopo Kata ya Bangata, Wilayani Arumeru ambao unachangia asilimia ishirini ya uzalishaji maji kwa Jiji la Arusha. 

  Pia, alifika kwenye chanzo cha maji cha chemchemi ya Machare, iliyopo Kata ya Moshono, Wilayani Arumeru iliyovamiwa na wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu kinyume na sheria na kuhatarisha uzalishaji wa maji ya kutosha kwa ajili ya kuhudumia mji wa Arusha.
  Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akizungumza mbele ya Waziri wa Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge, viongozi na wananchi wa Longuo, Wilayani Moshi.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Inj. Gerson Lwenge akimtwika maji mama katika Kijiji cha Longuo, Wilayani Moshi mara baada ya kuzindua mradi wa maji kijijini hapo.
  Jiwe la msingi likiashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Longuo, Wilayani Moshi.


  0 0

  Na  Bashir  Yakub.

  Tunapoongelea  upimaji   ifahamike  kuwa  upimaji  upo  wa  aina  nyingi.Kutokana na hilo upimaji  unaoongelewa  hapa  ni  upimaji  miliki. Lakini  pia  tunaongelea   upimaji miliki wa  ardhi  mijini na  sio vijijini. Upimaji wa  ardhi miliki ni  upimaji  ambao  lengo  lake  ni  kummilikisha  mtu  ardhi. 

  Kummilikisha  mtu  ardhi  sio  kumuuzia  ardhi.  Kummilikisha  mtu  ardhi  ni  kutambua  ardhi  yake  kimipaka  na  kumpatia  nyaraka  mahsusi(specific)  inayohusiana  na  umiliki( hati).  

  Kwa  maana  hii  wanaomiliki  ardhi  ambazo  hazijapimwa   hatuwezi  kusema  wamemilikishwa  ardhi . Haijalishi  ardhi  hizo  ni  za  kwao na  wamezinunua  kwa  pesa zao. Kwa  kusema  hivyo  haimaniishi  kuwa  ambao  hawana  hati  au  hawajapima  ardhi  zao  basi  sio  wamiliki,  hapana  isipokuwa  ni  kuwa  tu kwamba hawajamilikishwa  kisheria  na  mamlaka    za  serikali. 

  Kutokana  na  hilo   ardhi  iliyopimwa  na  ile  ambayo  haikupimwa  hutofautiana  hadhi na thamani kwa  kiasi  kikubwa.

  1.NYARAKA  ZINAZOHITAJIKA   ILI  UPIMIWE  ARDHI.

  ( a )  Barua  kwenda  kwa  mkurugenzi.  Anayetaka  kupimiwa  ardhi   anatakiwa  kuandika  barua  kwenda  kwa mkurugenzi  wa  halmashauri  husika. Barua  ni  nyaraka  ya  kwanza  kabisa  ambayo unatakiwa  kuwa  nayo.  Ni katika  barua  hiyo  ambamo  utaeleza   nia  yako  ya  kutaka   kupimiwa  ardhi na  matumizi  ya  ardhi  yako kama  ni  makazi,kiwanda n.k.

  ( b ) Kuambatanisha  mkataba  wa  mauziano.  Katika  hatua  hii  mkataba  wa  mauziano utatambuliwa kama nyaraka  ya  umiliki. Mkataba  huu  ndio  utakaokutambulisha  kama  mmiliki  wa  ardhi  husika. Huu  unaambatanishwa  kwasababu  mmiliki  wa  ardhi  ndiye  mwenye  jukumu  la  kuomba  kupimiwa.  

  Hivyo  kuambatanishwa  kwa  mkataba  kunathibitisha  kuwa  mmiliki  ndiye  anayeomba  kupimiwa  kwa  mujibu  wa  sheria. Ni  vema  mkataba  wa  umiliki  ukawa  ni  ule   mkataba  wa  kisheria   ulioandaliwa  na  kushuhudiwa  na  mwanasheria.

  ( c ) Barua  iliyotajwa  hapo  juu  katika  “A”  hakikisha  ina  muhuri  wa  mwen yekiti  wa  serikali  za  mtaa,  sahihi  pamoja  na mhuri  wa  mtendaji. Mwenyekiti  na  mtendaji  atakayetumika  sio  wa  pale  unapoishi    bali  pale  lilipo  eneo  unalotaka  kupima.  Kama  eneo  lipo  unapoishi  basi  utamtumia  huyohuyo  wa  eneo  unaloishi.


  0 0

  The Committee on the Elimination of all Forms of Discrimination Against Women considered the Tanzania's 7th and 8th Consolidated reports on the Implementation of the Provisions of the Convention for a period from 2008 to 2014 in Geneva on 26 February 2016.

  In his opening remarks,  head of Tanzania delegation, Amb. Modest J. Mero, Tanzania Permanent Representative to UN, Geneva  presented that Tanzania had undertaken over the years initiatives geared towards cultivating the rights of Women through development of policies, legal and institution frameworks. 

  He highlighed that Tanzania had achieved progress in addressing trafficking in Persons including women through publishing the Regulations 27 and 28 of January 2015, which among others implement the National Anti- Trafficking in Person. In its efforts to end Child Marriage, the government enacted the Law of the Child Act in 2009, which amended the Law of Marriage Act, 1971 by replacing the age of a child stating that "a child is any person under 18 years". 

  In combating discrimination against People with Albism, Ambassador said Tanzania has undertaken numerous measures and actions to address the situation such as expediting investigation, arresting and prosecuting the perpetrators along with media outreach and information campaigns. In combating halmful practices of Female Genital Mutilation (FGM), Ambassador reported measures undertaken including criminalizing the offence under the Penal Code and implementing a National Plan of Action to Accelerate Eradication of FGM.

  During interactive discussion, Tanzania was commended for establishment of the Tanzania Women's Bank, 2009 to empower women both economically and socially. Specific efforts to enhance women access to finance through Saving and Credit Cooperatives (SACCOS) was hailed by the Committee. 

  In the Health Sector,  the Committe commended Tanzania's progress made to ensure reduction of infant, children and maternal mortality rates.  Tanzania's efforts to combat Violence Against Women by undertaking several measures including establishement of a National Multi-sectoral Committees to prevent and respond to violence against Women and Children in Tanzania Mainland and Zanzibar was also commended by the Committee members. 

  The Committee welcomed various measures undertaken by Tanzania to promote women's full and equal participation in decision making in all areas of public and professional life. The Committe conglaturated Tanzania for increasing a number of Women participation in Parliament and Zanzibar House of Representative and women judges at different levels.

  Couple of recommendations was offered by the Committee for Tanzania's consideration in its efforts to promoting and protecting the rights of Women in the country including taking necessary steps to repeal or amend customary laws that indirectly discriminate Women. Intensify its efforts to amend or modify domestic laws and bring them in line with the provisions of the Convention.

  0 0


  0 0


  0 0

  Ratiba kamili ya kuaga mwili wa mpendwa Da Jessie ni kama ifuatavyo.
  1. Kuanzia Jumatatu tutaendelea kujumuika nyumbani kwa marehemu, 44 Fleetwood Ave, Mt. Vernon, NY, 10552

  2. Jumatano, Machi 2, 2016
  Flynn Memorial Home,
  1652 Central Park Avenue,
  Yonkers, NY 10710.
  Tel: 914-963-5178

  Heshima za mwisho (Viewing): 4pm-7pm

  Ibada (Service): 7pm-8pm
  Baada ya shughuli kumalizika, tutatoa tangazo la wapi pa kukusanyika usiku huo kwa wale ambao watataka kujumuika na wafiwa.

  Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuondoka New York kwenda Dar es Salaam, Tanzania asubuhi ya Alhamisi Machi 3, 2016.

  Mwenyezi Mungu akipenda Jessie atapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele siku ya weekendi mara baada ya kuwasili Dar es Salaam siku ya Ijumaa, Machi 4. Taarifa zaidi zitafuata.

  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mpendwa wetu Da Jessie Wayasa Mgeni Chiume mahala pema Peponi. Ameen.

  Link ya kutoa rambirambi ni:
  www.gofundme.com/daMgeni

  Kwa taarifa zaidi:
  Michael Chiume: 6466626999
  Chris Litunwa: 6145926231
  Nathan Chiume: 6465526347
  Hajji Khamis: 3476238965

  Uongozi,
  New York Tanzanian Community.

  0 0

   Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya Afisa mtendaji mkuu wa Benki ya Barclays Afrika , Maria Ramos na waandishi hao kwa njia ya simu ya mezani akiwaAfrika Kusini kuhusiana na benki hiyo kuongeza wateja wake wa bara la Afrika hasa katika nchi za Afrika Kusini, Botswana, Ghana na Zambia ikiwa benki hiyo inawateza zaidi ya 885,000 kwa bara la Afrika na kuongeza mapato yake kwa asilimia 10, Ikiwa kwa bara la Afrika  Maria amesema kuwa inakabiliwa na changamoto nyingi katika ufanyaji wa biashara hasa katika kutokupatawafanyakazi wachapakazi, umasikini na kutokua na usawa katika ufanyaji wa  biashara ya benki.
  Kutoka kulia ni Afisa Masoko wa benki ya Barclays Tanzania, Joe Bendela akisikiliza kwa ukaribu katika simu ya mezani ambayo ilitumika kuongea na Afisa mtendaji mkuu wa Benki ya Barclays Afrika, Maria Ramos akiwa afrika Kusini leo wakati wakiongea na waandishi wa habari wa jijini Dar es Salaam. Aidha Maria amesema kuwa Benki hiyo barani Afrika imeongeza mapato yake kwa asilimia 10 .
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

   Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji (TIC), Julieth Kairuki akizungumza katika mkutano wa SADC uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya wawakilishi wa nchi mwanachama wa SADC wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji (TIC), Julieth Kairuki akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika mkutano wa wadau wa SADC uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.


  Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii
  SERIKALI imesema itaendelea kuboresha miundombinu ili kuweza kuvutia uwekezaji wa viwanda ili nchi iweze kukua kiuchumi.  Hayo ameyasema leo Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji, Adolff Mkenda katika Mkutano wa w tano Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SADC),amesema kuwa katika kuhamasisha uwekezaji wa ndani nje serikali imejikita katika kujenga miundombinu ya barabara.


  Amesema kuwa uchumi unakua kwa asilimia saba na nguvu kazi kubwa iko vijiji kwa theluthi mbili hivyo lazima kuweka mazingira uwekezaji katika nguvu kazi hiyo.


  Mkenda amesema wakati inaanzishwa SADC ikiwa ni kujikomboa kisiasa lakini kwa sasa ni nchi kujikomboa katika uchumi katika sekta ya viwanda.


  Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC),Julieth Kairuki amesema kuwa mkutano huo kufanyika nchini mafanikio ya kujifunza kwa nchi zingine zinavyofanya uwekezaji.


  Amesema nchi 14 ziko nchini ambapo zitaweza kukubaliana ukuzaji wa uwekezaji wa viwanda katika mapinduzi ya kiuchumi kwa nchi zilizo katika jumuiya hiyo.

  Julieth amesema TIC imeweka mazingira ya mazuri kwa wawekezaji wa ndani na nje na sio kugawa maeneo ya vijiji kwa wawekezaji huku wakiwa na hekta 122000.

  0 0

  Walemavu wakishangilia kwa pamoja na viongozi wa kampuni ya GAPCO ambao walikuwa ndiyo wadhamini mbio za kilomita 10, za Kilimanjaro Marathon 2016 zilizofanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita. 
   Walemavu wakianza kutimua mbio za kilomita 10, za Kilimanjaro Marathon 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Mmoja ya walemavu Vosta Peter (30) kutokea Dar es Salam akiongoza katika mbio za Kilometa 10 za Kilimanjaro Marathoni 2016 zilizokuwa zimedhaminiwa na kampuni ya GAPCO na kufanyika mjini Kilimanjaro mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Picha zote na Cathbert wa Kajunason Blog.

  Na Cathbert Kajuna - Kilimanjaro. 
  MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya GAPCO Afrika Mashariki, Macharia Irungu amewataka wanamichezo kujibidishe kwa kufanya mazoezi mara kwa mara ili waweze kufanya vizuri katika mashindano wanayoshiriki. 

  Akizungumza mwishoni mwa wiki mjini Kilimanjaro wakati wa Mashindano ya Kilimanjaro Marathoni 2016, ambapo GAPCO ndiyo waliodhamini upande wa Walemavu, alisema kuwa wanamichezo wengi walemavu na hata wasiowalemavu hujisahau sana kufanya mazoezi ya kutosha jambo linalowafanya wengi wao kutoweza kufanikiwa kushinda kwenye mashindano. 

  Aliongeza kuwa wao kampuni ya GAPCO waliweza kujitolea kuwasaidia walemavu ili waweze kuonyesha vipaji vyao japo mwanzo waliweza kuwasisitiza wafanye mazoezi na ndiyo maana wameweza kufanya vyema. "Napenda kuwaasa wanamichezo wale walemavu na wasio walemavu, wapende kujitoa kufanya mazoezi ya kutosha maana siri ya ushindi ni mazoezi wala hakuna muujiza unaoweza kukupa ushindi kama haujajitoa kufanya mazoezi ya kutosha," alisema Irungu. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya GAPCO Tanzania, Vijay Nair alisema wamefurahishwa na mahudhurio ya watu wenye ulemavu waliojitoa kushiriki mashindano hayo, na wao hawatawatupa wataendelea kuwa nao bega kwa bega. Bw. Nair aliwaasa walemavu wawe na moyo wa upendo na mshikamano ili waonyeshe mfano bora hata wanapojitokeza kusaidiwa wafaidike kwa pamoja. 

  Mashindano ya mbio za Kilimanjaro marathon za 10KM kwa walemavu zilidhaminiwa na GAPCO ambapo shindano lilijumuisha baiskeli za walemavu zenye matairi matatu zenye viwango vya kimataifa wapatao 60 kutoka Dar es Salaam, Arusha, Moshi na Zanzibar.

  0 0

  Benki ya NMB imeendelea kuimarisha uhusiano wake na Chama Cha Wanasheria nchini (Tanganyika Law Society) kwa kuudhamini  mkutano wa mwaka kwa kiasi cha Tsh 10M kwaajili ya maandalizi na shughuli za mkutano huo uliyofanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
   Ofisa mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo Benki ya NMB PLC Abdulmajid Nsekela akiongea na wanasheria waliohudhuria Mkutano wa Mwaka wa Wanasheria uliyofanyika AICC mjini Arusha.


   Chama Cha Wanasheria nchini (Tanganyika Law Society) waliohudhuria Mkutano mkuu wa mwaka katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.

  0 0

  Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi Dawasa Mhandisi Romamus Mwang’ingo (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Kulia) juu ya ufanyaji kazi wa mitambo ya Ruvu chini.
  Mafundi wakiwa katika harakati za kulaza bomba litakalotumika kuleta maji kwenye tanki kubwa lililopo kibamba toka Ruvu chini na juu kwa ajili ya uhifadhi na usambazaji maji katika Jiji la Dar es salaam.
  Mafundi wakikarabati bomba kuu la kusambaza maji toka Ruvu juu katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo jirani.
  Mkuu wa msafara wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi (Katikati) akisikiliza maelezo juu ya ufanyaji wa kazi wa mitambo inayotumika kusambaza maji toka Ruvu juu kutoka kwa Meneja Mradi toka kampuni ya WABAG Mr. Pintu Dutta wakati wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Dar es Salaam ilipotembelea mitambo hiyo.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

   Viongozi meza kuu.

   Meneja Masoko na Mawasiliano Mfuko wa Pensheni wa LAPF  James Mlowe (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,  kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa kufanyika machi 10 na 11 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti.
   Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.

  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

  Na Dotto Mwaibale
  MFUKO wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kuwa na sh.trioni moja  na bilioni 87 za thamani ya uwekezaji kutoka mwezi juni mwaka jana.

  Hayo yalibainishwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF James Mlowe wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mkutano mkuu wa nane wa mfuko huo unaotarajiwa kufanyika Machi 10 na 11 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.

  Alisema LAPF imeendelea kupiga hatua kila mwaka ukilinganisha na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii hapa nchini.

  " LAPF imeweza kutoa mikopo ya masomo kwa watu 800 katika maeneo mbalimbali nchini yenye thami ya sh.bilioni 1.2 jambo ambalo tunajivunia" alisema Mlowe.

  Akizungumzia kuhusu mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa LAPF, Valerian Mablangeti alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika  kwa wadau wa mfuko huo kupatiwa barua za mualiko.

  Alisema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene na kuwa mawaziri wengine wakaoshiriki kwenye mkutano huo ni  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Jafo Selemani .

  Alisema katika mkutano huo Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali atatoa taarifa ya hesabu za mfuko huo na pia kutakuwa na mada inayohusu afya kutoka kwa Daktari wa  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
  (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa, Hiiti  Sillo akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kukamatwa kwa kiwanda bubu cha kutengeneza perfumes bandia  aina SAME.leo  jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti  Sillo akiwaonesha wandishi wahabari (hawapo  pichani) mitambo ya kutengenezea perfumes bandia zinazoitwa kwa jina la SAME   leo jijini Dar es Salaam. 
  Wandishi wakimsilkiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa, Hiiti  Sillo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA), Hiiti  Sillo akiwaonesha wandishi wa habari perfumes bandia zinazoitwa kwa jina la SAME   leo jijini Dar es Salaam.


   Na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii

  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ,Kanda ya Mashariki kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imekamata  vipodozi vya manukato ‘Perfume’  katika nyumba  inayomilikiwa na Mwanaidi iliyopo eneo la Tuangoma,  Wilayani Temeke Mkoani Dar es Salaam.

  Akizungumzna na wandishi wa habari  jijini Dar es Salaam leo ,Mkurugenzi Mkuu wa TFDA,Hiiti Sillo amesema kuwa walipata taarifa juu ya utengenezaji wa mafuta ya manukato na ndipo wakafanyia kazi na kwenda kukamata.

   Amesema katika nyumba hiyo  ina vifaa vya kimaabara, malighafi na kemikali mbalimbali  za kutengeneza manukato yenye alama ya kibiashara  SAME huku mafuta yakionyeshwa stika kuwa inatengenezwa nchini Uturuki

  Sillo amesema wangalizi wa nyumba hiyo Fatuma Selemani anashikiliwa na Jeshi la Polisi ili kusaidia upelelezi na jalada la Polisi na MBL/IR/1998/2016 limefunguliwa katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Mbagala, Temeke.

  Amesema vielelezo vyote ikiwa ni chupa 5,350 za perfumes zilizokamatwa dukani pamoja na vifaa, malighafi, kemikali na stika mbalimbali zilizokamatwa dukani vinashikiliwa.

  Sllo  amewaomba wananchi wote ambao wanazo majumbani kwao perfumes aina ya SAME waache kuzitumia na wazirudishe katika ofisi za TFDA zilizopo hapa nchini kwa sababu perfumes hizo hazijasajiliwa na TFDA na hivyo ubora na usalama wake haufahamiki.

  Aidha amesema wananchi waendelee kutoa taarifa kuhusu mtu au makundi ya watu mbalimbali wanaojihusisha na biashara haramu za utengenezaji, uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba katika maduka au majumbani mwao.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , Magesa Mulongo baada ya kuwasili kwenye uwanja  wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo baada ya kuwasili  kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa mkoa wa Mwanza baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1,2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi, Angelina Mabulla baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimu wananchi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo
   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitazama ngoma  ya nyoka baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza Machi 1, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Magessa Mulongo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  Wanafuzi 106 wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Namabengo wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameandamana kwenda kumwona mkuu wa mkoa Said Mwambungu kumpelekea malalamiko dhidi ya vitendo vya udharirishaji wanavyofanyiwa na makamu mkuu wa shule hiyo Shaibu Champunga. Ebu wasikilize kupitia RUVUMA TV on Line.

  0 0
 • 03/01/16--12:00: DIRA YA DUNIA 01.03.2016

 • 0 0
  0 0older | 1 | .... | 1142 | 1143 | (Page 1144) | 1145 | 1146 | .... | 3283 | newer