Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1141 | 1142 | (Page 1143) | 1144 | 1145 | .... | 3285 | newer

  0 0

  WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (pichani) anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka jijini Mwanza Machi 27.
  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maaandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Waziri Nape amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo litaanzia Geita Machi 26 na kumalizia Kahama Machi 28.
  Msama alisema kamati yake inaendelea na maandalizi ya kuelekea tamasha hilo ambalo litashirikisha waimbaji mbalimbali hapa nchini.
  “Maandalizi kuelekea Tamasha la Pasaka yanaendelea vema, hivyo wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wajiandae kupokea ujumbe wa neno la Mungu kupitia viongozi wa dini na waimbaji wa muziki wa Injili,” alisema Msama.
  Msama alisema baadhi ya waimbaji  waliothibitisha kushiriki tamasha hilo ambao ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Christopher Mwahangila, Joshua Mlelwa, Sifael Mwabuka, Jenipher Mgendi, Kwaya ya AIC Makongoro na Kwaya ya Wakorintho Wapili.
  Aidha Msama alisema viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na kwa watoto shilingi 2000.

  0 0


  0 0

  Askari wa Kikosi cha Zimamoto Jijini Mbeya, akiendelea na jitihada za kuuzima moto unaoendelea kuwaka na kuteketeza Mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga jijini humo, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa, na jitihada za kuuzima zinaendelea.
  Kikosi cha Zimamoto Jijini Mbeya, kikiendelea na jitihada za kuusima moto huo.
  Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya, wakiwa wakiwa nje ya Shule yao wakiangalia bila kujua cha kufanya wakati Mabweni yao yakiteketea kwa moto. Picha na habari kamili itawajia baadae kidogo.

  0 0


  0 0

  Wadau hao wakinyoosha mikono juu kuonesha umuhimu wa kuadhimishwa kwa siku hiyo ya Magonjwa Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii ndani ya jamii.
  Mratibu wa tukio hilo Bibi Sharifa Mbaraka akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye moja ya ukumbi wa hoteli ya Serena leo jijini Dar,Bi.Sharifa alisema kuwa tukio hilo limedhamiria kujumuisha  vyombo vya habari na wadau wengine ili kujenga uelewa kuhusu magonjwa hayo. 

  “Yapo magonjwa tofauti yanayowasibu watu wachache takribani 7000 ambayo yameshabainishwa duniani hadi leo na Tanzania haiwezi kujitoa kwenye  hili. Hata hivyo watu wengi hapa Tanzania hawana uelewa  kuhusu magonjwa hayo”,alisema Bi Sharifa ambaye watoto wake wawili Ali Mohammed Kimara 5, na Nasreem Mohammed 3, wanasumbuliwa na magonjwa hayo.

  Alifafanua kuwa kutokana na uzoefu wake, amepata msukumo  na kuamua kuwaunganisha wazazi, wagonjwa walio na magonjwa hayo na raia wenye mapenzi mema ili kujenga uelewa muhimu na kutoa wito kwa jamii kuchukua hatua.

  Pichani wa pili kulia ni Mdau mkubwa wa sekta ya afya Monica Joseph kutoka Philips Medical Systems , akifafanua zaidi kuhusiana na huadhimishwa kwa Siku ya 'Rare Disease' Duniani ambayo inaadhimishwa leo.Monica amesema kuwa ni wakati mwafaka kwa Watanzania kuwa na tahadhari ya kuelewa kuhusu magonjwa hayo ili wanajamii waweze kufahamu mbinu za kuyadhibiti iwapo watayakuta ndani ya jamii. pichani kulia ni Dkt.Mariam Nooram kutoka hospital ya Aghakhan.
   
  Kauli mbiu ya Siku ya Magonjwa Yanayotokea kwa kundi dogo la jamii Mwaka 2016 ni ‘Sauti za Wagonjwa’ na inamaanisha kutambua mchango muhimu unatolewa na wagonjwa katika kutaka mahitaji yao na kuchochea mabadiliko ambayo yataboresha maisha yao na masiha ya familia zao na maisha ya wale wanaowahudumia. 

  Kauli mbiu ya Siku ya Magonjwa yanayotokea kwa kundi dogo la wanajamii ambayo ni, “Ungana nasi kuzifanya sauti za waathirika zisikike” ikitaka jamii kwa jumla, wale wanaishi bila magonjwa hayo au wanaothirika nayo moja kwa moja kuungana na jamii ya waathirika katika kuelewa athari za magonjwa hayo. Watu wanaoishi na magonjwa hayo na familia zao mara kadhaa hutengwa. Jamii inaweza kuwaunganisha kutoka kwenye kutengwa huko. 


  Lengo la jumla la Siku ya Magonjwa yanayotokea kwa kundi dogo la jamii ni kuhamasisha uelewa miongoni wa umma kwa jumla kuhusu magonwa hayo na athari zake kwa maisha ya wagonjwa ili kuyapa kipaumbele kwenye afya ya jamii ya Tanzania na kwenye bajeti ya serikali kupitia Wizara husika.
  PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Muonekano wa Barabara ya Moshi - Arusha inayoendelea na Upanuzi wake kuwa njia sita, kama ionekanavyo.


  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akiongea na menejimenti ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kuzitambua taasisi zilizopo chini ya wizara yake.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani (Kushoto) akifafanua jambo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Mhandisi.Julius Mamilo(kulia) wakati ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo leo jinini Dar es Salaam.


  0 0

  SHIRKA la ndege la Etihad limepokea tuzo ya heshima katika mabadiliko ya kifedha kwa mwaka 2015 kutoka kwa kampuni ya kimarekani ya Innovation Enterprise inayoongoza kwenye masuala ya uvumbuzi katika sekta uwekezaji.

  Tuzo hiyo ilitolewa kwa Shirika la Ndege la Etihad ambalo lilifanikiwa kuzishinda kampuni nyingine kupitia kituo chake cha nje cha mpango wa Mabadiliko ya kifedha. Programu hiyo iliundwa mahususi  kwa ajili ya shughuli za utendaji na uendeshaji wa shirika hilo katika mazingira ya gharama nafuu.

  James Rigney, Afisa Mkuu wa fedha wa shirika la ndege la Etihad alisema…”Tunajisikia fahari kupokea tuzo hii kwa kazi kubwa iliyofanywa na Timu yetu ya mipango ya fedha. Tulikuwa na muda mfupi tu wa miezi sita katika kuhakikisha tunatekeleza mabadiliko ya mpango wetu, na juhudi yao kwenye kazi hii ulitufanya tuweze kupunguza nguvu kazi kifedha, kuanza kusonga mbele na muundo wa kikanda uliopunguza gharama na kukuza kipato hadi kufikisha dola za kimarekani milioni 28 kama akiba huku lengo likiwa kufikia dola za kimarekani milioni 50 milioni hadi mwisho wa mwaka huu.”

  Awamu ya kwanza ya kituo cha nje cha mpango wa Mabadiliko ya kifedha kilihitaji kuundwa kwa kituo kimoja chenye ubora kitakachoshughulikia miamala yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1 kutoka nchi zaidi ya hamsini. 

  Awamu ya pili ilitazamia shirika la ndege la Etihad kupitisha mipango ya kuboresha michakato muhimu na kuondoa vikwazo, ili kuhakikisha shughuli hizo zinafanyika kituoni hapo bila kukiuka viwango vya juu vya kuongoza ndege Shirika la Innovation Enterprise ndio linaongoza katika kukuza ubunifu katika mipango ya fedha na taaluma ya uchambuzi, na ni mratibu mkubwa wa matukio katika sekta ya Mipango ya fedha na uchambuzi.

  0 0

  BUNGE la Afrika Mashariki limesema kuwa changamoto zilizokuwepo katika Bandari ya Dar es Salaam zimeweza kufanyiwa kazi na Rais Dk.John Pombe Magufuli na kufanya Bandari hiyo kutoa huduma kwa ufanisi.

  Hayo ameyasema leo Mwakilishi Bunge hilo, Shy Rose Bhanji wakati Wabunge wa Afrika Mashariki Tanzania walipokutana na Spika Bunge, Job Ndugai kwa ajili ya kufahamiana kutokana wabunge hao wanatokana na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Amesema kuwa Bunge la Afrika Mashariki lilikuwa walikuwa wakizungumzia juu ya bandari ya Dar es Salaam katika utoaji uwa huduma lakini sasa Rais Dk.John Pombe Magufuli ameweza kufanyia kazi.
  Shyrose amesema wataendelea kutoa ushirikino kwa Rais katika kutumia farsa yake ya Hapa Kazi Tu katika kuwahudumia watanzania.

  Nae Mwakilishi wa Spika Owen Mwandumbimbya ambaye ni Afisa Habari wa Bunge amesema kuwa Spika atatoa ushirikiano kwa wabunge kupitia kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
   Spika wa Bunge, Job Ndugai akiwatambulisha wabunge wa bunge la Afrika Mashariki waliofika ofisini kwake leo katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam kwaajili ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa serikali ya awamu ya tano.
  Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Shy-Rose Banji akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufika katika ofisi  ndogo za bunge kwaajili ya kumpongeza Spika wa Bunge, Job Ndugai na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mbunge wa Bunge la Afrika, Mhe. Shy-Rose Banji jijini Dar es Salaam leo katika Ofisi ndogo za Bunge.
  Picha na Avila kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

  Mwanafunzi wa chuo cha St. Joseph kampasi ya Dar es Salaam akiwa miguuni wa Askari leo mara baada ya kuishiwa nguvu wakati wakitawanywa na Askari hao jijini Dar es Salaam leo walipokuwa wakiandamanda kuelekea wizara wizara ya elimu, Sayansi na mafunzo ya Ufundi.
    Wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph tawi la jijini Dar es Salaam wakitawanywa na askali wa kutuliza Ghasia (FFU) leo wakati wanafunzi hao wakiandamana wanaelekea wizara ya elimu, Sayansi na mafunzo ya Ufundi kudai kushinikiza chuo hicho (Kampasi)tawi la Arusha kifunguliwe.
  baada ya tawi hilo kufungiwa na TCU wiki iliyopita.
  Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

  0 0

  Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, Rajai Ayoub, aliyepata pointi 95 kwa upande wa Tajweed, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. . Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar.
  Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kumtafuta mwakilishi wa Nchi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Kimataifa ya Qur'aan Tukufu, Abubakar Mohamed, aliyepata pointi 86 kwa upande wa washindani wa Juzuu 30, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, jana Feb 28, 2016. Mashindano hayo yameandaliwa na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake, Saleh Omary. Kushoto ni Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mahd Aghajafar. 
  Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu, waliohudhuria mashindano hayo, wakimsikiliza Dkt. Bilal, wakati akihutubia.

  0 0

   Wamawake wakiwa wametandika khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari 29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini hapo.
   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016.
   Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao hospitalini hapo Februari 29, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa kujenga zahanati na nyumba ya mganga kwenye kijiji cha Nandagala, wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. 

  Msaada huo wenye thamani ya dola za Marekani 55,000 (sawa na sh. Milioni 119.35)   umetolewa na kampuni ya Huawei Technologies yenye makao yake jijini Dar es Salaam.  Pia wametoa kompyuta za mezani (desktop) 25 pamoja na UPS  25 kwa ajili ya shule tano za sekondari wilayani humo. 


  Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo jana (Jumapili, Februari 28, 2016) Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei, Bw. Bruce Zhang alisema kampuni yake imetoa msaada huo ikiwa ni mwitikio wa sera ya Wizara ya Afya inayotaka kila kijiji kiwe na zahanati na kila kata iwe na kituo cha afya.


  Wakati huohuo, kampuni ya mtandao wa simu ya Halotel ilimkabidhi  Waziri Mkuu hundi ya sh. Milioni 9/- ambazo ni mchango wao wa kumsaidia  Waziri Mkuu ambaye pia ni mbungewa jimbo la Ruangwa ili zisaidie kulipia familia zisizo na uwezo kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).


  Akizungumza na wanakijiji hao kabla ya kukabidhi hundi hiyo, Meneja Mkuu Msaidizi wa Biashara wa Mkoa wa Lindi, Bw. Sebastian Innocent alisema: "Mchango huu utazihusu kaya 900 ambazo zinalipiwa sh. 10,000 kila moja. Kila kaya inatakiwa kulipia watu sita, hivyo tutaweza kuwafikia watu 5,400 kupitia mchango huu.


  Alisema kampuni yao imejenga minara 50 katika mkoa wa Lindi ambapo 40 inafanya kazi na minara 22 kati ya 40 imeunganishwa na inatoa huduma ya 3G.  


  Akitoa shukrani kwa misaada yote,  Waziri Mkuu alisema anaishukuru kampuni ya Halotel kwa kumsaidia kulipia sh. Milioni 9/- kwa ajili ya CHF ambazo alisema zimegawanywa katika vijiji 90 vya wilaya nzima ya Ruangwa na kwa kaya 10 za watu sita sita.


  Aliwashukuru kwa kuweka minara katika wilaya hiyo jambo ambalo alisema litasaidia wananchi kupata mawasiliano ya simu kwa urahisi zaidi.


  Kuhusu zahanati,  Waziri Mkuu Majaliwa aliishukuru kampuni ya Huawei Technologies kwa msaada huo ambao alisema utakapokamilika, utawapunguzia wananchi adha ya kwenda kijiji cha jirani kupata huduma ya matibabu. 


  Alisema ana mpango wa kuweka nguvu ya umeme jua (solar power systems) kwenye shule zote za msingi, shule zote za sekondari  na zahanati zote kwenye wilaya ya Ruangwa ambayo ndiyo jimbo lake ili asiwepo mtoto wa kushindwa kusoma au mtu kupata matibabu kwa sababu ya kukosa umeme. Wilaya ya Ruangwa ina shule za msingi 82, shule za sekondari 15, vituo vya afya vitatu na zahanati 28.  Waziri Mkuu alirejea Mtwara jana hiyo hiyo na leo hii amerejea Jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Tanga katika kikao maalum kilichoangaliwa kwa ajili yake kilichofanyika Ikulu ndogo mjini Tanga jana jioni Februari 28, 2016. 
  (Picha na OMR)

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016.

  • Ni baada ya kudai rushwa ya sh. 100,000/- kumfanyia upasuaji mgonjwa.
  • Mama alilazimika kuuza shamba ili apate fedha za kumtibia baba yake
  • Aagiza maduka ya dawa nje ya hospitali hiyo yafungwe leo hii
  • Amwagiza RAS aitishe kikao cha watumishi wote leo saa 9 alasiri

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza kusimamishwa kazi kwa Dk. Fortunatus Namahala wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Ligula ambayo ni hospitali mkoa wa Mtwara kutokana na tuhuma za kumdai mgonjwa rushwa ya sh. 100,000/-.


  Pia ametoa agizo la kufungwa kwa maduka yote ya dawa yaliyo nje ya hospitali hiyo kuanzia leo na kumtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw. Alfred Luanda asimamie zoezi hilo mara moja.  Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Februari 29, 2016) kwenye kikao cha watumishi wa hospitali hiyo alichokiitisha baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya hospitali hiyo na kupokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa na ndugu wenye wagonjwa waliolazwa.  Mara baada ya kuwasili, Waziri Mkuu aliamua kwenda mojamoja mapokezi badala ya wodini kama alivyopangiwa na kuuliza maswali ni kwa nini wana dirisha moja la kupokelea wagonjwa wote. "Dirisha la wazee lipo?" akajibiwa hakuna. "Dirisha wa watu wa Bima ya Afya (NHIF) lipo" nalo pia akajibiwa halipo. "Je wazee wana daktari wao", hakupata jibu.


  "Mganga Mkuu ni kwa nini hujatenga dirisha la wazee wakati haya maelekezo yalishatolewa siku nyingi? Tengeni dirisha la wazee  na uhakikishe wana daktari wao. Siyo kuwaleta huku ili waje kusukumana na wagonjwa vijana,"  alisema wakati akimwagiza Mgaga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Shaibu Maarifa.

  Akiwa njiani kuelekea wodi aliyopangiwa kuiona, Waziri Mkuu alikutana na kundi la wagonjwa waliokuwa wakiimba "tuna jambo, tuna jambo" wakiashiria kutaka kusikilizwa. Kati ya wauguzaji watatu aliowasikiliza, Waziri Mkuu alipokea kero za kuuziwa dawa kwa bei za juu kwenye maduka ya dawa binafsi, lugha mbaya za madaktari na wauguzi, uchafu wa vyoo na uhaba wa maji.

  Lakini kero ya Bi. Tatu Abdallah aliyelazimika kuuza shamba la baba yake ekari 2.5 ili apate fedha za kulipa gharama za kufanya upasuaji kwenye hospitali binafsi baada ya baba huyo kutimuliwa kutoka hospitali ya Ligula ndiyo ilimgusa zaidi Waziri Mkuu.


  "Februari mosi nilimleta baba yangu hapa nikaambiwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji. Nikaandikiwa ninunuue dawa za sh. 85,000/- hapo nje (pharmacy haikumbuki jina) pia uzi wa kushonea kwa sh. 25,000/-. Lakini pia daktari akasema anataka sh. 100,000/- ya kwake. Lakini hadi Februari 7 hakufanyiwa huo upasuaji."  "Tarehe 12 Februari  baba alitolewa wodini na kuambiwa arudi tarehe 16 Februari. Niliumia sababu kijiji tunachotoka ni mbali na hali ya baba ilizidi kuzorota. Ndipo baba akaniambia nirudi kijijini kwetu Kilomba nikauze ekari 2.5 za shamba lake ili tulipie matibabu. Niliuza na kumpeleka baba katika zahanati ya Sajora. Huko nililipa sh. 560,000/- na baba akafanyiwa upasuaji sasa hivi yuko nyumbani".  "Leo nataka huyu daktari aje achukue boksi hili la dawa alizoniandikia na pia anirudishie hela yangu iliyopotea bure. Mie sijazitumia, ni kwa nini aliniandikia wakati baba hajampa huduma yoyote?" Alipoulizwa kama anaweza kumtambua akimuona, mama huyo alikiri kuwa anaweza.   Waziri Mkuu alitembelea pia wodi ya akinamama waliojifungua na kukuta wakiwa wametandikiwa shuka moja na wagonjwa kulazimika kuweka khanga juu ya mipira wanayolalia wodini ambayo pia wanaambiwa wajinunulie kabla ya kwenda hospitali kujifungua.  Akiwa njiani kuelekea theatre, Waziri Mkuu alipata kilio cha wagonjwa wengine ambao walisema hospitali hiyo haina maji, choo kinachotumika ni kimoja na kwamba usafi umefanyika leo waliposikia kuwa atatembelea hospitali hiyo.   Akiwa katika kikao na watumishi hao, Waziri Mkuu aliwainua madaktari wote ili wajitambulishe ndipo akamuomba mama aliyedaiwa rushwa aende kumshika mkono daktari mhusika.  "Gwaride la utambuzi ni jambo la kawaida. RPC hakikisha huyu mama hasumbuliwi. Lakini leo nitaanza na huyu Daktari kwa sababu rushwa haivumiliki. RAS simamia suala lake lakini pia shirikiana na TAKUKURU na Polisi kufanya uchunguzi wa jambo hili hadi mwisho," alisema.   Kuhusu madai na stahili za watumishi, Waziri Mkuu amemwagiza RAS, RMO na Afisa Utumishi wa mkoa wafanye kikao na watumishi wote wa hospitali hiyo leo saa 9 alasiri na kisha wamletee taarifa.


  Kabla ya kufikia uamuzi wa kumsimamisha Dk. Namahala, Waziri Mkuu alitumia muda mwingi kuwaelezea watumishi hao jinsi walivyo na umuhimu katika huduma zao na kwamba nafasi yao ni nyeti kwa maisha ya binadamu hivyo wanapaswa kuwa na huruma na siyo kuwaumiza wananchi wa kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

  Aliwataka waache tabia ya kuwatoza fedha watoto wanaolazwa hospitalini hapo na wanawake wanaojifungua kwani wanapaswa kutibiwa bure kwa mujibu wa sera ya Serikali.
  Sakata la hospitali ya Ligula lilianza juzi (Jumamosi, Februari 27, 2016) wakati Waziri Mkuu akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa ambapo baadhi yao walikuwa wakichomekea kuwa aende hospitalini hapo kwa kuwa kuna majipu ya kutumbua.

  Waziri Mkuu aliwajibu kuwa amesikia ujumbe wao na ataenda huko lakini alishindwa kutokana na ratiba za siku hiyo kumalizika jioni sana.
  Waziri Mkuu amerejea Jijini Dar es Salaam mchana huu.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Cheti Judith Mwambela mmoja kati ya washiriki Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya pili ya Kimataifa inayojadili kuhusu Bayoanuwai  katika hifadhi ya kupunguza umaskini na uhifadhi ya viumbe hai na maendeleo endelevu kusini mwa Jangwa la Sahara. Warsha hiyo imefunguliwa leo Februari 29, 2016 katika ukumbi wa Hoteli ya  Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
  (Picha na OMR).

  0 0

   Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA akisalimiana na Mama Othman Chande alipowasili katika Shule ya Sekondari Tambaza kuhudhuriaWorld Thinking Day iliyoandaliwa na Tanzania Girl Guide Association.
   Wanachama wa Girl Guide wakiwasili katika Shule ya Sekondari Tambaza  katika kusherekea World Thinking Day  ambao walipokelewa na Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete.
   Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi  na baadhi ya wanafunzi Wanachama na viongozi wa  Girl Guide.
  PICHA NA YUSUPH BADI.  Na Philomena Marijani- Meneja Uraghbishi na Mawasiliano, WAMA

  CHAMA cha Girl Guide Tanzania kimetakiwa kuweka mikakati ya kuhakikisha inaongeza wanachama watakaojiunga na chama hicho ili vijana wengi waweze kunufaika.


  Rai hiyo imetolewa mwishoni wa wiki na Mke wa Rais Mstaafu na  Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mama Salma Kikwete wakati wa maadhimisho  ya kilele cha  siku ya  World Thinking Day yenye kauli mbiu ya Ungana, Shirikiana, Sherekea  iliyoadhimishwa na Tanzania Girl Guides Association. Sherehe hizo zilianza kwa maandamano ya wanafunzi Wanachama kutoka Upanga katika Makao Makuu ya Girl Guide Tanzania na kumalizikia  katika Shule ya Sekondari Tambaza ambapo  sherehe rasmi ilifanyika hapo.


  Akiongea katika sherehe hizo Mama Salma Kikwete  alipongeza uongozi wa Girl Guide  kwa kufikia mikoa 19 ambapo  mpaka sasa chama kina  wanachama 97,143 na aliongeza kuwa changamoto kubwa waliyonayo ni kuongeza Wanachama zaidi kwani Tanzania ina watu wengi sana.


  “Wito wangu kwenu ni kuongeza juhudi ya kuwafikia vijana wengi zaidi kwani sote tunajua umuhimu wa TGGA katika kuwasaidia vijana kujiepusha na changamoto mbalimbali katika makuzi yao. Ni lazima tuweke malengo ya muda mfupi, kati na mrefu ndani ya miaka mitatu ili ifikapo  mwaka 2018 tuwe tumeingiza wanachama zaidi ya 100,000/= Tumieni vizuri shule za msingi na sekondari , nina hakika mtafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana. ” Alisema Mama Kikwete

  Mama Kikwete pia alishauri uongozi wa Girl Guide Tanzania kubunimbinu za kukabiliana na changamoto kwa kutumia rasilimali walizonazo.


  “Kwa kuwa TGGA ni chama kikongwe, chenye rasilimali kama ardhi ambazo ziko sehemu nzuri kibiashara  naamini kwamba ikitayarishwa mipango mizuri  mnaweza kupata wabia wenye tija au mkawekeza kama chama kwa kushirikiana na mabenki. Mtakusanya kodi ambazo zitasaidia uendeshaji na kuongeza uwekezaji. ”Alisema Mama Kikwete.


  Akielezea maana ya World Thinking Day Mkufunzi wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association, Mama Magreth Olumbe alisema kuwa sherehe hii ilianza rasmi mwaka 1926 ambayo ni siku ya; kuwakumbuka Girl Guide wote duniani na hasa wale walio kwenye mazingira magumu;kuongelea mambo yanayowagusa wasichana kwa mfano mimba za utotoni, kuolewa katika umri mdogo; na kukumbuka mwanzilishi wa Chama Lord Baden Powell na mke wake Olave Baden Powell.  


  Akisoma risala kwa Mgeni Rasmi, Kamishna Mkuu wa  Tanzania Girl Guides Association, Mama Symphorosa Hangi alisema kuwa katika kuadhimisha  World  Thinking Day walikuwa na wiki mbili za kutoa huduma kwa jamii ikiwemo kuwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Ocean Road na kutoa chakula, mavazi   na nauli za kuwarudishwa makwao wale waliokuwa wameruhusiwa baada ya matibabu. Aliongeza pia walitumia muda huo kuhamasisha wasichana wengine kujiunga na chama cha Tanzania Girl Guides ili nao waweze kupata fursa ya kujikwamua kifikra kwa kupitia mafunzo yanayotolewa na chama.


  Chama cha Girl Guides Tanzania (TGGA) kilianzishwa hapa nchini mwaka 1928. TGGA ni chama kisicho cha serikali na ni cha kujitolea chenye lengo la kuwaendeleza watoto wa kike na wanawake kwa ujumla kushiriki katika maswala ya kijamii na kiuchumi kwa kupitia elimu na mafunzo yanayotolewa kwa kuzingatia kanuni za Girl Guides pamoja na kuwajenga kimaadili.

  0 0

  NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa kwa Duka la dawa za binadamu la Shine Care Pharmacy lililopo Temeke, baada ya kubainika kuendeshwa kinyume cha sharia ikiwemo kutokuwa na kibali cha uendeshaji na mfamasia husika.

  Dk. Kigwangalla ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Mfamasia Mkuu wa Serikali pamoja na msajili wa Baraza la famasia nchini na maafisa wengine, ambapo katika tukio hilo mapema leo Februari 29.2016, walikuta madawa mbalimbali yaliyokwisha muda wake na yale ambayo hayatakiwi kuuzwa katika duka kama hilo.

  Aidha, Dk. Kigwangalla akitoa agizo la kufungwa kwa duka hilo, ameagiza kuchukuliwa hatua ikiwemo kupelekwa Mahakamani mara moja il iwe fundishi na kwa maduka mengine yenye kufanya hivyo.

  Kwa upande wake, Mfamasia wa Serikali, Bw. Henry Irunde amebainisha kuwa, dawa hiza za binadamu zilizokutwa hazifai kuuzwa katika maduka hayo na pia duka ambalo linaendeshwa bila kuwa na Mfamasia ni kinyume na sharia kwani watumiaji wakitumia dawa bila kuwa na maelezo ya kutosha kutoka kwa mtaalam wa dawa zinaweza kusababisha usugu kwa mwili wa binadamu n ahata kumsababishia matatizo.

  Duka hilo la dawa ambalo lipo hatua chacche kutoka Hospitali ya Temeke, ni miongoni mwa maduka makubwa ya dawa za binadamu ambapo pia wachunguzi ha wa madawa ya binadamu walibaini kuwa milango mingi zaidi kinyume na ile inayotakiwa kuwa kwa maduka ya dawa hali ambayo walitilia mashaka huenda vitendo vingine vya kutoa huduma vinatumika licha ya kuwa milango hiyo ilifungwa kwa kile kilichoelezwa kuwa wahusika hawakuwapo.

  Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, zoezi hilo la kukagua maduka ya dawa ni la nchi nzima na watazunguka nchi nzima kufanya ukaguzi huo bila kutoa taarifa hivyo kwa yeyote atakaekutwa anaendesha kinyume cha sharia atachukuliwa hatua stahiki.

  Tazama  tv, Kuona video hiyo hapa: 
  Imeandaliwa na Andrew Chale.
  Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akitoa maagizo hayo ya kufungwa kwa duka hilo.
  Baadhi ya maafisa walioambatana na Naibu Waziri wa Afya. Dk Kigwangalla wakimsikiliza kwa makini, Dk. Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa tukio hilo.
  Mfamasia Mkuu wa Serikali Henri Irunde, akitoa taarifa yake ya ukaguzi katika duka hilo kwa wanahabari na Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
  (Picha zote na Andrew Chale.)

  0 0


  BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imekuwa ikifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kufuatia video iliyotumwa katika YouTube https://www.youtube.com/watch?=iveX49WE7fw na imekuwa ikisambazwa kupitia njia mbalimbali za habari ikimuonesha mtu mmoja kutoka nchi jirani akisema kuwa Olduvai Gorge ambayo kimsingi iko Tanzania kwamba iko Kenya.

  Video hii imeibua majadiliano katika mitandao ya kijamii baina ya watanzania na watu wengine ambao wanaitakia mema Tanzania na wanaoelewa vizuri kuwa Olduvai Gorge iko Tanzania.

  Bodi ya Utalii Tanzania kama taasisi ya Umma yenye jukumu la kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii imeshtushwa na video hii iliyojaa upotoshwaji mkubwa ambao tunaamini mbali ya malengo mengine inalenga kuchafua kazi nzuri ambayo imekuwa ikifanywa na Bodi kwa kushirikiana na wadau wengine katika kutamgaza vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo Olduvai Gorge.

  Tunapenda kuchukua fursa hii kupinga vikali upotoshwaji huu uliofanywa na mtu huyo wakati akihutubia mkutano amabao tumeambiwa ulikuwa ni wa Vijana wa Umoja wa Mataifa uliofanyika Amerika mwezi Agosti mwaka jana. Tunapenda dunia ifahamu kuwa kama ilivyo kwa Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Zanzibar n.k Olduvai Gorge mahali panapoaminika kuwa ndipo binadamu wa kwanza duniani aliishi na ambako Dr. Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la binadamu huyo wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 2 iliyopita iko pia Tanzania na si mahali pengine popote duniani. Eneo hili la Olduvai Gorge liko katika bonde la ufa katikati ya bonde la Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Manyara nchini Tanzania.

  Tunatoa wito kwa watanzania mahali popote walipo kuendelea kuunga mkono juhudi za Bodi ya Utalii Tanzania za kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii kwa kujibu na kusahihisha papo hapo bila woga mara tu taarifa ya upotoshaji kuhusu nchi yetu inapotolewa iwe ni kwenye mikutano ya ndani ya nchi au ya Kimataifa. Tunaamini kuwa ni jukumu la kila mtanzania kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya Utalii badala ya kuiachia TTB kazi hii peke yake. 

  Yawezekana katika mkutano huo wa vijana ambao mjumbe huyo wa nchi jirani alipata fursa ya kuzungumza na kufanya upotoshaji huzo, wajumbe wa Tanzania pia walikuwepo ambao wangweza kukosoa upotoshaji huo papo hapo na kuelezea ukweli na usahihi wa mahali ilipo Olduvai Gorge.

  Imetolewa na:
  Ofisi ya Uhusiano
  BODI YA UTALII TANZANIA.

  0 0

  Mfululizo mpya wa makala zilizochapishwa na The Lancet unatoa ushahidi kuwa kuboresha unyonyeshaji wa maziwa ya mama kunaweza kuokoa maisha ya zaidi ya watoto 820,000 kila mwaka duniani na Dola za Kimarekani bilioni 300 kila mwaka. 

  “Katika kipindi cha miaka iliyopita kumekuwa na maendeleo katika kupunguza vifo vya watoto na utapiamlo nchini Tanzania. Hata hivyo, watoto 270 chini ya miaka mitano wanakufa kila siku na karibu asilimia 40 ya watoto hao wanakufa ndani ya mwezi mmoja wa kuishi. Kati ya watoto wanaonusurika, mtoto mmoja kati ya watatu wanadumaa kwa sababu ya utapiamlo sugu. 

  Watoto hawa wanakosa fursa zao katika maisha. Hali duni ya lishe inaathiri uwezo wa mtoto kujifunza na pia uwezekano wa mtoto huyo kutengeneza kipato akiwa mtu mzima. Lakini kuna afua zinazojulikana zinazoweza kusababisha mabadiliko makubwa na kuhamasisha kunyonyesha maziwa ya mama. ” amesema Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania, Bibi Maniza Zaman, wakati akiongea na vyombo vya habari Dar es Salaam. “Mfululizo wa makala ya “The Lancet” unatoa ushahidi wenye ushawishi kuhusu faida mbalimbali za kunyonyesha. Uwekezaji kwenye kulinda, kukuza, na kusaidia unyonyeshaji maziwa ya mama kunaweza kuokoa maisha ya watoto wa Tanzania, na hatimaye, kusaidia kukuza uchumi.” 


  0 0

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Yono Auction Mart pamoja na Jeshi la Polisi imefanya ukaguzi wa stempu za kodi katika kazi za wasanii na imefanikiwa kukamata CD na DVD za Muziki na Filamu takribani 7,780 ambazo hazina stempu za kodi kutoka kwa wasambazaji mbalimbali jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Bw. Richard Kayombo alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu ofisini kwake.

  Bw. Kayombo alisema msako huo ulioanza tarehe 26/02/2016 katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam umebaini ukiukwaji wa Sheria kutoka kwa wasambazaji wa kazi za wasanii zikiwemo CD na DVD za nyimbo na Filamu.

  Aidha, aliongeza kuwa sambamba na hilo kumebainika udanganyifu kutoka kwa baadhi ya wasambazaji kutumia stempu kinyume na sheria, “Kuna baadhi ya wasambazaji huweka CD ama DVD mbili kwenye kasha moja huku nakala moja ya CD/DVD ikiwa imebandikwa stempu halali ya kodi na nakala nyingine ikiwa haina stempu,” alisema.

  Wakati huo huo baadhi ya CD na DVD zilikamatwa zikiwa zimedurufiwa pamoja na stepu ya kodi.

  Kwa upande wa kazi zinazoingizwa kutoka nje ya nchi, baadhi ya kazi zilikamatwa kutoka nje ya nchi zikiwa hazina stempu ya kodi jambo ambalo ni kinyume cha sheria na pia hupoteza mapato ya nchi kwa ujumla.

  Bw. Kayombo ametoa wito kwa wasambazaji wa kazi za wasanii kutumia stempu za kodi kwa mijibu wa sheria na kusisitiza kwamba ni sharti wahusika wanaoingiza kazi za wasanii kutoka nje ya nchi wapate kibali kutoka Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) ili wapate kibali cha kubandika stempu kwenye kazi hizo na si vinginevyo.

older | 1 | .... | 1141 | 1142 | (Page 1143) | 1144 | 1145 | .... | 3285 | newer