Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1140 | 1141 | (Page 1142) | 1143 | 1144 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

   Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  DK. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumzana na wadau mbilimbali wa mpira wa kikapu (NBA) juu ya Timu bora nane kutoka kila kundi zitakazofuzu kushiriki kweye ngazi ya mitoano  Oktoba 2016. Timu bora mbili kutoka kila kundi zitakutana kwenye michezo kuwania ubingwa ili kumpata Bingwa wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana,  katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
   Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana (Junior NBA) jijini Dar es Salaam Jumamosi kwa ku-shoot kikapu kwa ustadi. 
   Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali baada ya kuzindua  Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana (Junior NBA) jijini Dar es Salaam Jumamosi   
   Rais Mstaafu DKT. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mchezaji Mwandamizi wa (WNBA) Allison Feaster katika uzinduzi huo  jijini Dar es Salaam
  Sehemu ya mashabiki wa  Mpira wa kikapu   waliofika katika uzinduzi wa Ligi ya Mpira wa kikapu ya vijana,leo jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

  0 0

   Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitembelea bandari ya Mtwara Februari 27, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na wafanyakazi wa  kampuni ya TPDC baada ya kuwasili kwenye mtambo wa kuchakata  gesi wa Madimba, Mtwara Vijijini kukagua shughuli za gesi Februari 27, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na viongozi wengine akikagua mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, Mtwara Vijijini Februari 27, 2016. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Naibu Waziri Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Medadi Kalemani na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio,  na  Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Halima Dendego.
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TPDC baada ya kutembelea mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, Mtwara Vijijini Februari 27, 2016
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na walimu na wakufunzi wa Chuo cha Elimu cha Mtwara baada ya kuzungumza nao  chuoni hapo , Februari 27, 2016. 

  0 0

   Kikao cha halmashauri kuu ya tawi la CCM Diaspora London kimefanyika Jumamosi jioni jijini London ili kupanga mikakati ya kuimarisha uhai wa chama na wanachama wake nchini Uingereza. Kikao hicho kilichofana sana kilifanyika chini ya Mwenyekiti Tinno Msei
  Kikao hicho cha halmashauri kuu ya tawi la CCM Diaspora London kilichofanyika fanyika Jumamosi jioni jijini London kilimchagua Ndg. Chris Lukosi (katikati) kuwa Mkuu wa propaganda na uhamasishaji wa tawi hilo

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga kiasi cha sh. bilioni 1.65/- kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwenye vyuo vya walimu hapa nchini.

  Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Februari 27, 2016), wakati akizungumza na walimu na watumishi wa sekta ya elimu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mtwara uliofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara.

  "Serikali inatambua uhumimu wa mafunzo kwa vitendo katika vyuo vya ualimu ni kwa sababu hiyo mwezi huu wa Februari tumetoa sh. bilioni 1.65/- kwa vyuo vya ualimu 35 vya umma nchini ili kuwezesha wakufunzi na walimu wanafunzi kushiriki kikamilifu mafunzo kwa vitendo (Block Teaching Practice)," alisema huku akishangiliwa.

  Alisema fedha hizo zinapaswa zitumike kulipia posho za kujikimu, nauli na ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia.

  Mapema, akizungumza na mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kuimarisha elimu na akawaonya wote wanaowaharibia elimu watoto wa kike.

  "Tunataka watoto wa kike wasome wa Kitanzania wasome hadi elimu ya juu waje wawe watumishi wa umma hapo baadaye. Kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake tukikumbuka kaulimbiu ya Mama Salma Kikwete ya kwamba 'Mtoto wa Mwenzio ni wako'," alisema.

  "Yeyote atakayemharibia mtoto wa kike masomo kwa kumrubuni na chips au pipi ajiandae kwenda Lilungu, (gereza la mkoa wa Mtwara)", alisema.

  0 0  0 0

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nape Nnauye akiwa anakazia jambo kwa wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya serikali ya TSN kuhusu kuboresha kazi zao na kuandika habari zinazofichua maovu katika jamii na kusimamia haki bila kumuonea mtu.
  Mhariri wa magazeti ya Daily News Bw.Charles Masele akimweleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nape Nnauye(hayupo pichani) mapungufu mbalimbali ya kampuni ya TSN na kumwomba waziri uyo awasaidie kuiboresha kampuni hiyo.
  Mwenyekiti wa RAAWU tawi la Tanzania Standard Newspaper(TSN) Bw.Oscar Mbuza akimweleza waziri Nape(kulia) changamoto mbalimbali ya wafanyakazi.
  Sehemu ya wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya serikali(TSN) wakimskiliza Mhe. Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye(hayupo pichani).
  Waziri Nape nnauye akipiga “Selfie” na mfanyakazi wa magazeti ya kampuni ya serikali ya TSN baada ya mkutano na wafanyakazi hao katika ofisi za kampuni hiyo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya Serikali(TSN) wakifurahia picha ya pamoja na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nape Nnauye.Picha na Daudi Manongi.
  ……………………………………..

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye amewaasa wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya serikali ya Habari Leo,Daily News,SpotiLeo na Sunday News kuwa mstari wa mbele katika kufichua maovu katika jamii,kwani kwa kufanya ivyo watajijengea heshima katika jamii na kuongeza idadi ya watu kuwaletea kazi zao kwa ukaribu zaidi.

  Waziri nape ameyasema hayo leo hii jijini Dar es Salaam katika ofisi za magazeti ya serikali(TSN) kwenye kikao na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

  “Acheni kumumunya maneno,msaidieni Rais katika kufichua maovu ya nchi yetu ila tu msimuonee mtu bali mtende haki na hasa mkosoe ili kujenga na kwa namna hiyo mtajijengea heshima kubwa katika jamii”.

  Waziri nape pia aliitaka menejimenti ya kampuni iyo kubadilisha fikara zao kwa kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara ili kampuni iyo ijitegemee vyema katika mambo yake.

  Pia aliitaka menejiment ya kampuni iyo kukaa chini na RAAWU ili wahakikishe wafanyakazi wanafata taratibu za kazi na kuwaasa kushughulikia vipaumbele vya wafanyakazi hao ambavyo ni vifaa vya kazi ambavyo kutokuwa navyo inapelekea kushuka kwa morali ya kazi na pia madai ya wafanyakazi yashughulikiwe ndani ya mwezi mmoja.

  Nae Mwenyekiti wa RAAWU katika kampuni iyo Bw.Oscar Mbuza alimweleza waziri nape kuwa wanatambua haki na wajibu wa kila mfanyakazi na kwamba kumekuwa na ukiukwaji wa sheria,taratibu na kanuni kwa mtizamo wao na ivyo wanaomba yafanyiwe kazi ili kurudisha imani yao kwa viongozi wao.

  Nao wafanyakazi mbalimbali wa kampuni iyo walieleza changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo kutokuwepo kwa bima ya afya,hawapandishwi cheo na kulipwa malimbikizo mbali mbali wanayoidai kampuni hiyo.

  Mhe.Nape pia amehaidi kufanya vikao vya mara kwa mara na wafanyakazi wa kampuni iyo ili kuboresha mambo mbalimbali ya kampuni hiyo.

  Story na Daudi Manongi.

  0 0

  Bondia Mtanzania Francis Cheka (kulia) akichapana na mpinzani wake bondia kutoka nchini Serbia, Geard Ajetovic, wakati wa pambano lao la raundi 12 la ubingwa wa Mabara , uzito wa Super Midle wa WBF lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Katika raundi ya kwanza bondia Cheka alionekana kuanza kwa woga na kumfanya mpinzani wake kumshambilia kwa ngumi za kushitukiza na kumpeleka chini, jambo lililomfanya Cheka kuchanganyikiwa na kuhesabiwa na mwamuzi na kisha kuendelea na pambano.

  Baada ya kwenda chini katika raundi ya kwanza raundi ya pili cheka alionekana kucheza kwa tahadhari kubwa kwa kupiga na kukimbia huku mpinzani wake akionekana kujigadi muda wote na kupiga ngumi za kushitukiza zilizokuwa na madhara kwa Cheka.

  Katika pambano hilo Bondia Francs Cheka, aliibuka na ushindi kwa pointi.
   
  Cheka akijitahidi kupangua konde la mpinzani wake....

  Cheka, alichanika katika raundi ya nane baada ya mpinzani wake kumbananisha kwenye kona iliyokuwa na utelezi ambapo aliteleza na kupoteza mwelekeo na kushambuliwa mfululizo. 


  0 0

  Beki Shomari Kapombe wa timu ya Azam FC ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Januari 2016.

  Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Kapombe alicheza dakika zote 180 za mechi mbili za timu yake dhidi ya African Sports na Mgambo Shooting. Mechi ya tatu ya Azam FC katika raundi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons ilikuwa kiporo, na ilichezwa Februari24, 2016.

  Kapombe alifunga mabao yote mawili kwenye ushindi wa mabao 2-1 wa timu yake dhidi ya Mgambo Shooting. Pia alisaidia kupatikana bao la Azam kwenye mechi dhidi ya African Sports iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1, na mara nyingi mashambulizi ya timu yake yalianzia upande wake.

  Washindani wa Kapombe kwenye kinyang'anyiro hicho katika mwezi huo walikuwa mshambuliaji wa Tanzania Prisons ya Mbeya, Jeremiah Juma na beki wa Coastal Union ya Tanga, Miraji Adam.

  Kwa kutwaa tuzo hiyo, Kapombe atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Limited.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Vodashop lilipo uhindini jijini Mbeya, kulia Msimamizi mkuu wa kanda ya Nyasa wa Vodacom Tanzania Macfadyne Minja .
  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akikata keki wakati wa uzinduzi wa Voda shop Mbeya.
  Wafanyakazi wa Vodacom katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa mwenye suti ya kaki wakati wa uzinduzi wa Vodashop Mbeya.


  0 0

  Ifikapo saa mbili na nusu usiku wa leo usikose kuangalia kipindi cha mizani ya wiki kupitia television yako ya AZAM TWO ambapo utamsikia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumzia mikakati ya serikali ya awamu ya Tano katika kupambana na Dawa za Kulevya hapa nchini pamoja na kueleza athari za matumizi ya dawa hizo .Katika kipindi hicho Msanii Ray C, naye atashiriki pamoja na kuipongeza serikali kutoa matibabu ya bure kwa waathirika wa dawa za kulevya, awaonya wenzake kwa kuachana na dawa hizo kabisa

  usikose usikose.....

  0 0


   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na wakazi wa mji wa Moshi waliojitokeza kwa wingi kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo mwaka huu zaidi ya watu elfu 8 walishiriki kutoka nchi mbali mbali ambapo kati ya hao 200 walitoka nchini Kenya. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikimbia kwenye riadha ya Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo alikimbia kilomita 5 pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Anthony Mtaka, mashindano hayo ya riadha yameshirikisha zaidi ya nchi 40.
   Mshindi wa kwanza wa kilometa 42.2 Kiprotich Kirui akiinua mikono juu kama ishara ya kushangilia ushindi wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisoma risala mara baada ya kuhitimisha mbio za Kilimanjaro Marathon ambapo aliwapongeza wahiriki wote, wadhamini na kuwataka Watanzania kutumia mbio hizo kama fursa ya kuutangaza utalii uliopo nchini.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Tanga baada ya kupokea Taarifa ya Mkoa huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza leo Februari 28, 2016. Makamu wa Rais yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantumu Mahiza leo Februari 28, 2016. Makamu wa Rais yupo Mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili.(Picha na OMR).
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Mwantum Mahiza alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku Mbili Mkoani humo leo Februari 28, 2016.
  Chipukizi wa Umoija wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga akimvisha Skafu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani hum oleo Februari 28,2016.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Vijana wa Chipkizi wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa Tanga alipowasili uwanja wa ndege wa Tanga kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani humo leo Februari 28,2016.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam leo wakati alipozungumzia mpango wa kuwasafirishwa walimu bure jijini Dar es salaam wakati wa kwenda na kurudi kazini huku akiwa ameongozana na viongozi wa vyama vya usafirishaji wa abiria jijini Dar es salaam pamoja na viongozi wa Madereva wa Daladala jijini Dar es salaam.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
  Mwenyekiti wa Chama Chama Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es salaam, Said Mabrouk(wa kwanza kushoto) akizungumzia mwitikio wa wamiliki hao kuhusu kuwasafirisha walimu ili kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Wilaya ya Konondoni Mh. Paul makonda na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kutoa elimu bure hapa nchini, kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Madereva, Shabani Mdemu, wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji abiria Dar es Salaam, (UWADAR),William Masanja.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji abiria Dar es Salaam, (UWADAR),William Masanja akizungumza na waandishi wa habari leo jijinni Dar es Salaam.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  WALIMU wa Shule ya Msingi na Sekondari Mkoa wa Dar es Salaam watasafiri na Daladala bure kuanzia Machi  7 mwaka huu.

  Akizungumza na waadishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema kuwa kutokana na changamoto za walimu ameona kuna umuhimu wao kusafiri bure waweze kupunguza makali ya nauli za kila siku wanapopanda daladala hizo.

  Amesema kuwa walimu watasafiri kwa  usafiri huo kuanzia saa 11:30 hadi saa 2 kwa muda wa asubuhi na baada ya muda huo kupita watalipa nauli zao na nyakati za jioni watarudi majumbani mwao kwa kupanda daladala hizo kuanzia saa 9 hadi saa 12.Makonda amesema kuanzia kesho watatengeneza vitambulisho vya walimu wote wa serikali wa mkoa wa Dar es Salaam ambavyo wataonyesha kwa makondakta wa daladala vikiwa na saini ya mkuu mkuu wa Wilaya.

  Amesema utaratibu huo utakuwa ukitumika kwa siku za kazi tu kwa walimu kupanda bure na sio vinginevyo na walimu wanaoishi mikoa mingine na wanafundisha Dar es Salaam watalipa nauli zao kufika katika vituo vyao vya kazi.

  Aidha amesema kuwa walimu wataingia katika Daladala wasiopungua wawili na wengine watasubiri daladala zingingine kutokana na maoni ya wamliki wa vyombo vya usafiri.Nae Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam, Sabri Mabroock amesema kuwa wanaunga mkono sera ya elimu ya Rais  Dk.John Pombe Magufuli.

  Amesema walimu wamekuwa na changamoto wakati mwingine wanashindwa kulipa hata nauli hivyo kupanda  bure watakuwa wamerahisisha maisha.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea misaada mbalimbali kwa ajili ya wakazi wa vijiji vya Mtondo na Nanjaru wilayani Ruangwa mkoani Lindi ambao nyumba zao ziliezuliwa na upepo Januari mwaka huu.

  Akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo leo (Jumapili, Februari 28, 2016), Waziri Mkuu alisema maafa huwa yanakuja bila kutarajiwa na akatumia fursa hiyo kuwashukuru wadau waliotoa misaada ya chakula, magodoro, mashuka, vitenge, mabati na mbegu za mazao.

  Aliwataja wadau hao kuwa ni benki ya NMB, NSSF, wakazi wa Ruangwa na marafiki wa Ruangwa waishio Dar es Salaam ambao walifika kukabidhi misaada hiyo.
   
  Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku mbili katika mikoa ya Mtwara na Lindi  kukagua athari za mafuriko, hatua zinzochukuliwa za utoaji misaada kwa waathirika na kuwapa pole wananchi walioathirika na mafuriko hayo, alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi waishio mabondeni wahame kwa sababu mvua kubwa bado zinakuja.

  "Jambo hili si mipango ya mtu binafsi na sote tunajua kwamba tunahitaji mvua kwa ajili ya mazao lakini safari hii zimekuja zaidi ya kiwango cha kawaida. Mamlaka ya hali ya hewa imeshasema kuwa mvua kubwa zaidi zinakuja ifikapo Machi mwaka huu", alisema.

  Ili kuepusha maafa zaidi, kuanzia sasa, wale waliojenga mabondeni wanapaswa wahame. Pia nawasihi wananchi wachukue tahadhari wakiona mvua inakuja na upepo mkali wasikae ndani ya nyumba sababu hapa kijijini tumempoteza mzee wetu mmoja ambaye aliangukiwa na nyumba baada ya nyumba yake kuangukiwa na mti kutokana na mvua hizo," aliongeza.

  Kwa mujibu taarifa ya maafa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Bi. Mariam Mtima, mvua zilizonyesha kati ya Januari na Februari mwaka huu zilisababisha nyumba 393 kuezuliwa na nyingine kubomoka na kuacha wakazi wa vijiji hivyo bila makazi.

  "Zahanati ya kijiji cha Mtondo iliezuliwa paa, daraja la mto Muhuru limebomoka na halipitiki kabisa na ekari 1,186 za mashamba ya wananchi zimesombwa na maji. Mazao yaliyoathirika ni mahindi, muhogo, mikorosho, mtama, ufuta, kunde, mpunga na mbaazi," alisema Mkuu huyo wa wilaya katika taarifa yake.

  Alivitaja vijiji vingine ambavyo mafuriko hayo yaliharibu mashamba ya wananchi kuwa ni Nambilanje, Mkaranga, Namkatila, Chinongwe A, Likwachu, Nauname na Mbekenyera.

  Alisema hali hiyo imesababisha upungufu mkubwa wa chakula wilayani humo na sasa hivi wanahitaji tani 1,133 za chakula aina wanga ambazo anataraji zitatosheleza mahitaji kwa mwezi Machi 2016.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, FEBRUARI 28, 2016.

  0 0

  Kila mwaka Siku ya mwisho ya Mwezi Wa Pili huadhimishwa Siku ya 'Rare Disease Duniani. Mwaka huu itakuwa Kesho tarehe 29 Feb 2016. Sharifa Mbarak ni mama mwenye watoto wawili ambao waliathirika na magonjwa hayo yasiyotambulika. Kesho ataongea na Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wakiwamo na madaktari wa watoto Dr. Mariam wa Agakhan na Professor Kareem wa Muhimbili pamoja na Monica Joseph , mdau kutoka Philips Medical Systems katika hotel ya Serena Dar es Salaam,Saa 4 asubuhi katika kampeni ya kuhamasisha magonjwa yasiyotambulika. Tunaomba ushiriki wako katika siku hii muhimu kwa Watoto wa Sharifa na watoto wote duniani wanaoteseka na magonjwa haya.

  0 0


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na  Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Arusha Mhe. Lekule Laizer baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.

  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Msshariki Mhe Joshua Nassari aliyekuwa mmoja wa viongozi  na wananchi waliojitokeza kwa wingi kumpokea alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utofanyika jijini Arusha.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Amos Makalla  baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi zaJumuiya ya Afrika Mashariki leo February 28, 2016.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasili Mkoani Arusha ambako pamoja na mambo mengine ataongoza Mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Jumatano tarehe 02 Machi, 2016 Mjini Arusha.

  Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Magufuli amelakiwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali pamoja na vikundi vya burudani za ngoma kabla ya kuelekea Arusha Mjini.

  Rais Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.Kabla ya kuongoza kikao hicho Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na viongozi wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Tarehe 03 Machi, 2016 Rais Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya, wataweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha - Holili - Taveta - Voi inayoziunganisha nchi za Tanzania na Kenya.

  Barabara hiyo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotekelezwa na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.


  Gerson Msigwa

  Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.

  Dar es salaam

  28 Februari 2016
  0 0

  Na Woinde Shizza,Same

  Wananachi wa vijiji vya Vumari na Muheza wilayani Same mkoani Kilimanjaro wamenufaika na miradi mbalimbali inayotekelezwa na hifadhi ya taifa ya Mkomazi iliyopo wilayani humo ambayo imegharimu zaidi ya kiasi cha sh,150 milioni kupitia kitengo cha ujirani mwema.

  Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa bweni la washichana katika shule ya sekondari ya Vumari sanjari na zahanati iliyopo ndani ya kata ya Mahole iliyopo kilomita 51 kutoka Makao makuu ya wilayani ya Same.

  Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea miradi hiyo mkuu wa shule ya sekondari ya Vumari ,Phillip Mzava alisema kwamba shule yake ni miongoni mwa shule zilizonufaika na miradi ya ujirani mwema inayotekelezwa na hifadhi ya taifa ya Mkomazi.

  Alisema ya kwamba shule yao ilipokea jumla ya kiasi cha sh,50 milioni kutoka hifadhi hiyo na wao kuchangia jumla ya zaidi y ash,21 milioni kwa kuwashirikisha wananchi kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wasichana shuleni hapo.

  Alisema kwamba mradi huo umesaidia kuinua ufaulu wa wananfunzi na kuongeza idadi ya mahudhurio kwa kuwa hapo awali wanafunzi walilazimika kut embea zaidi ya kilomita 15 hadi shuleni hapo.

  Hatahivyo,alisema kwamba mradi huo umesaidia kuokoa tatizo la mimba za utotoni kwa wanafunzi wa kike ambao walikuwa wakipata vishawishi njiani wakati wakija shuleni hapo huku akisema kwamba shule hiyo pamoja na kuwa kijijini lakini mwaka juzi ilishika nafasi ya kwanza katika ngaziya wilaya na mwaka jana kushika nafasi ya kwanza.

  “Mwaka 2012 kidato cha wasichana 12 walipata ujauzito na hawakufanya mtihani,mwaka 2013 wasichana 8 walipata ujauzito na hawakufanya mtihani,mwaka 2014 walikuwa 4 waliopata ujauzito hawakufanya mtihani lakini 2015 hakuna hata mmoja kutokana na ujenzi wa mabweni haya”alisema Mzava

  Naye,Afisa tatibu kiongozi wa zahanati ya Mahole iliyopo ndani ya kijiji cha Muheza,Chambua Mbwambo akizungumzia mradi wa zahanati hiyo alisema kwamba walipokea kiasi cha sh,56 milioni na kisha wananchi kuchnangia kiasi cha sh,24 milioni kwa ajili ya ujenzi huo.

  Mbwambo,alisema kwamba mradi huo umesaidia kuwahudumia wakazi 10,000 wa kijiji hicho kwa huduma za mama na mtoto pamoja na maabara na kuwaondolea usumbufu waliokuwa wakiupata hapo awali wa kwenda umbali mrefu kusaka huduma za matibabu.

  “Awali kabla ya kujenga zahanati kijijini hapa wakina mama walikuwa wakijifungulia njiani na wengine walifariki lakini kwa sasa wanapata huduma hapa hapa tunaishukuru Tanapa”alisema Mbwambo

  Naye,mhifadhi wa ujirani mwema katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi,Deogratius Nicholaus alisema kwamba lengo kuu la kufadhili miradi hiyo ni kupunguza kero na changamoto zinazowakabili wakazi wanaozunguka hifadhi hiyo sanjari na kujenga mahusiano mazuri na wakazi hao.
  Afisa utalii mwandamizi wa hifadhi ya taifa ya Mkomazi iliyopo mkoani Kilimanjaro,Pellagy Marandu wa kwanza kushoto akifafanua aina ya kobe waliomo ndani ya hifadhi hiyo jana wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo kujifunza na kutangaza vivutio vya utalii hapa nchini.

  0 0  BOFYA HAPA KUONA HABARI ZAIDI

older | 1 | .... | 1140 | 1141 | (Page 1142) | 1143 | 1144 | .... | 3272 | newer