Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1143 | 1144 | (Page 1145) | 1146 | 1147 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Click link to Sign the Petition!

  OLDUVAI GORGE IS IN TANZANIA
  Tanzania Tourist Board (TTB) has been following up the ongoing discussions on social media following a video clip being posted on YouTube (https://www.youtube.com/watch?v=iveX49WE7fw) which has been circulating through various media channels showing a person claiming that Oldupai Gorge, a site in Tanzania that holds evidence of the earliest existence of mankind is in Kenya.

  This video clip has triggered a lot of discussions on the different social media among Tanzanians and other people who have good wishes for Tanzania tourism who know very well that Oldupai Gorge is in Tanzania and NOT in Kenya.
  As a public institution, responsible for marketing and promotion of Tanzania tourist attractions, Tanzania Tourist Board is also dismayed by this misleading information which intends to distort the good work the Board has been doing in promoting Tanzania tourist attractions including the Oldupai Gorge.

  The Board would like to take this opportunity to strongly refute this statement delivered by the said person from a neighboring country while addressing one of the sessions of the International Young Leaders Assembly (IYLA) in USA, August 2015.

  We would like to inform the world that as it is the case for Mt. Kilimanjaro, Serengeti National Park, Zanzibar to mention just a few, Olduvai Gorge which is referred to as the Cradle of Mankind, where Dr. Louis and Mary Leakey discovered important hominid remains of the nutcracker ‘Australopithecus bosel’, who lived nearly two years ago, is also in Tanzania and not elsewhere in the world. 
  It is located in the eastern Serengeti Plains in the Arusha Region and about 45 km, from Laetoli, another important archaeological site of early human occupation. The paleoanthropologist-archeologist team Mary and Louis Leakey established and developed the excavation and research programs at Olduvai Gorge which achieved great advances of human knowledge and world-renown status. Olduvai Gorge is one of the key tourist attractions for Tanzania. 
  We call upon Tanzanians and those with good wishes for Tanzania wherever they are to continue supporting the effort’s undertaken by TTB in marketing Tanzania and her all tourism attractions. We believe that it is the role of every single Tanzanian to promote Tanzania as Africa’s best destination and ask them to join and support Tanzania Tourist Board in its efforts to promote destination Tanzania.

  We would like to applaud the reaction made by Tanzanians and non-Tanzanian s alike within and out of Tanzania, who through this incident were able to stand up as ‘one voice’ and tell the world that OLDUPAI GORGE is INDEED IN TANZANIA!

                                                 
                                                           Issued by:


  Public Relations Office


  TANZANIA TOURIST BOARD

  0 0

  Baada ya kutangaza Olduvai Gorge na Mlima Kilimanjaro upo kwao, Watani wetu wa Jadi  sasa wamehamia katika kutumia jina la mlima huo mrefu kuliko yote barani Afrika kwenye ndege zao. Tujadili hili. Mdau unazungumziaje hili na maudhi mengine hayo?


  0 0  0 0


  0 0  0 0
 • 03/01/16--13:34: Sauti za Busara 2017
 • Sauti za Busara resumes at the Old Fort in Stone Town, Zanzibar during 9th – 12th February 2017.
  During four days, East Africa’s favourite festival will feature:
  • Live Music: World-class performances with 400 artists (40 groups) on 3 stages, 100% live!
  • Carnival Parade: Bringing more buzz to Zanzibar Town and outlying areas
  • Swahili Encounters: Local and visiting artists meet, exchange and create collaborations
  • Movers & Shakers: Local and global industry professionals meet, network and exchange
  • Busara Xtra: Fringe events across the island, as organised by local communities

  0 0

  Na  Bashir  Yakub.  

  Kazi  kubwa  ya  sheria  zote  zinazoshughulika  na  masuala   ya  ardhi   ni kuratibu  na  kutoa  mwongozo  katika   miamala  mbalimbali  ya masuala ya ardhi  katika  maisha  ya  kila  siku. 

  Miamala  hiyo  ni  kama  uuzaji  na  ununuzi  wa  ardhi, masuala  ya  mikopo  na  rehani, upangaji  na  upangishaji, masuala  ya  fidia, kuhamisha  umiliki, haki  na  wajibu wa  mmiliki ardhi, haki  na  wajibu  wa  serikali  katika  ardhi  yote, upimaji  na  ramani, namna ya kutatua  migogoro  ya  ardhi, n.k. 

  Makala  yatagusa  kwa  mtindo  wa  dondoo  baadhi  ya  mambo  ya  msingi  yaliyo  katika  sheria  ya ardhi namba  4 ya  1999  sura  ya  113.

  1.SHERIA  NAMBA  4  YA MWAKA 1999.

  Sheria  hii  ilipitishwa  na  bunge  la  Jamhuri  ya  Muungano  mwaka 1999.  Hata  hivyo  ilianza  kutumika  rasmi  mwezi  mei  mwaka  2001.

  ( a ) MDHAMINI  WA  ARDHI  YOTE NI  RAIS. 

  Sehemu  ya  pili  ya  kifungu  cha  3  cha  sheria  hii  inaanza  kwa  kueleza  sera  ya  taifa  ya  ardhi. Kubwa  linalotajwa  ni  kuwa  ardhi  yote  ni  mali  ya  umma  ambayo  mdhamini  wake    ni  rais  wa  Jamhuri  ya  Muuungano  wa  Tanzania. Huu  ndio  msingi  mkuu  wa  ardhi  yetu.

  ( b ) WASIMAMIZI   WAKUU   WA  ARDHI.

  Sehemu  ya  iv  kifungu  cha  8  mpaka  18  kinaeleza   watumishi  wakuu  na  wasimamizi  wa  ardhi  kitaifa. Waziri  wa  ardhi  ndiye  mwenye  dhamana  kuu  akifuatiwa  na  kamishna  mkuu  wa  ardhi  kabla  ya   kutajwa  kamishna  msaidizi  na  baadae maafisa  ardhi . Wajibu,  kazi  na  majukumu  yao  yameainishwa  katika  vifungu  hivyo. Sambamba  na  hilo  mipaka  katika  utekelezaji  wa  majukumu  yao  ni  jambo  jingine lililoainishwa.

  ( c ) KUMILIKI   HATI.

  Sehemu  ya vi  kifungu  cha  24 mpaka  30  yameelezwa  masuala  ya  hakimiliki.  Taratibu  za  kupata  hakimiliki  na  umilikishwaji .  Wakati  huohuo  vifungu  vya 31  mpaka  35  vimeeleza  vyema  masharti  yanayoambatana    na  hakimiliki ,muda  wa  hakimiliki  pamoja  na  kodi  za ardhi.

  Kifungu  cha  76  mpaka  78  kimeongelea  uuzaji  wa  ardhi   hasa  zenye  hati miliki.


  0 0

   Mercedes Benz(2004) - Kompressor (Sports - Lorinser)
  Features: Leather Seats (Power), 
  Sun Roof (Power), Transmission-Manual/Auto, 
  Central Locking, Alloy Wheels(Lorinser), 
  Auto Climatization
  Price: 38m
  Contact: 0754-942125
   Interior
  Front and side

  0 0


  0 0   
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na akifafanua jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha leo Machi 1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Pichani kulia ni Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni.
   Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni akiongea na wanahabari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha leo Machi 1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.Pichani shoto ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza kwa makini 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni wakifanya mazungumzo kwenye Ikulu Ndogo ya Arusha jijini Arusha leo Machi 1, 2016 mara tu baada ya Kiongozi huyo wa Uganda kuwasili jijini humo kuhudhuria Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  0 0
 • 03/01/16--20:00: WELCAB VEHICLE FOR SALE.
 •   


  We sell the welcab Vehicle (see Photo).  This is also can be used for the handicapped person (Someone who is difficult to walk without help, he/she will sit in the passenger’s seat and can go anywhere without having some assistance by other person). This car can store the wheel chair in the back.  The lift of this wheel chair is installed in the trunk area.


  The following are the details of the car; Toyota Ractis, 2009y model 51,000km, at,ac,ps,pw,cl,Navi, radio/CD, air bags, Special seat, lift in the trunk. Blue color Grade 4.0.  Price - CIF us $ 7,000.


  For More details contact +255 754 400606 or +255 658 856351      


  0 0

   NAIBU WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Bw. Luhaga Mpina amesema mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa nane hapa nchini ambayo inakabiliwa na tishio la kugeuka jangwa kutokana na tatizo la ukataji miti hovyo.

  Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Simiyu, Mwanza, Mara, Singida na Arusha. Mingine ni Kilimanjaro, Dodoma na Manyara.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Machi 2, 2016) alipopewa nafasi na waziri Mkuu Kassim Majaliwa awasalimie wananchi waliofika kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kwenye jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

  Alisema kila wilaya imepewa agizo la kupanda miche milioni 1.5 kwa mwaka na kwa sababu hiyo watawapima wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurudenzi wa halmashauri na Manispaa ambao hawatafikisha idadi hiyo ya miche na kuwasilisha majina yao kwa Waziri Mkuu.

  "Ilani ya Chama cha Mapinduzi imeagiza kila wilaya ipade miche milioni 1.5 kwa mwaka. Kwa hiyo kuanzia Machi 3, mwaka ambayo ni siku ya upandaji miti, tutawamoniter Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wote ili kubaini ni nani hajatekeleza agizo hili. Tutakuletea mezani kwako majina ya wale ambao watashindwa kutekeleza agizo hili ambalo liko kwenye Ilana ya CCM," alisema.

  Kwa upande wake, Naibu Waziri huyo alisema amekuja na miche 7,000 ya matunda aina ya miembe, michungwa na mifenesi ambayo ameahidi kuigawa kwa kila wilaya. "Tunataka katika ziara yako hii tusambaze miche 5,000 kwa kila jimbo la mkoa huu na wakati unamaliza ziara yako tutakuwa tumesambaza miche 35,000," alisema.

  Naibu waziri Mpina alisema kupandwa kwa miti mbalimbali ya matunda, kutawasaidia wananchi kupata matunda ya kula, ya kuuza na kupata fedha lakini pia itawasaidia kuwa chanzo cha mali ghafi kwenye viwanda vya kusindika matunda.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, MACHI 2, 2016.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.


  0 0

  WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Ally Mwalimu leo Machi 2.2016, amepokea msaada wa fedha kwa ajili ya kuwezesha matibabu ya wagonjwa wa moyo katika taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo kwa msaada huo, jumla ya watoto 101, wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika taasisi hiyo kwa gharama za fedha hizo zilizotolewa na Jumuiya ya Kihindu waishio Dar es Salaam ijulikanayo kama BAPS Charity, kwa kuguswa kwao na kutoa msaada mkubwa na upendo waliouonyesha kwa watanzania wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo.

  Wiziri Ummy amebainisha kuwa, kiasi cha msaada unaotolewa utawezesha wagonjwa wapato hao kupatiwa matibabu ya moyo hivyo kuwa, faraja kubwa kwa wagonjwa waliokuwa wakisubiria huduma hizo kwa muda mrefu kutokana na kushindwa gharama za matibabu yake.

  Aidha, kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amepongeza kwa msaada huo kwani utasaidia kutoa matibabu kwa watoto hao 101, huku pia taaisi yake ikikabiliwa na changamoto ya wagonjwa wengi ambapo amezitaka taasisi na wadau wengine kujitokeza kuchangia ilikupunguza wagonjwa wanaosubiria kupatiwa matibabu hasa upasuaji.

  Prof. Janabi ameeleza kuwa, matibabu ya wagonjwa wa moyo yana gharama kubwa kwani kwa mtoto mmoja ndani ya nchi yanafikia hadi Milioni nne (Mil 4) huku kwa nje ya nchi matibabu hayo yakifikia hadi Milioni 16, gharama hizo ni kubwa hivyo wadau na taasisi binafsi zimeombwa kujitokeza ilikuokoa maisha ya wagonjwa wengi hasa watoto ambao wapo katika taasisi hiyo na mikoa mingine.
  Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi akisoma taarifa fupi juu ya magonjwa wagonjwa wa moyo wanaopatiwa matibabu katika taasisi hiyo na namna walivyojipanga kutoa matibabu ya upasuaji kwa watoto hao 101, waliolipiwa gharama za matibabu kutoka BAPS Charity. Wengine ni Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wa BAPS Charity.
  Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akipata kumjulia hali mtoto Zahara Seleman Muna (10) ambaye anasumbuliwa na magonjwa ya moyo. Hata hivyo Waziri Ummy Mwalimu amejitolea kama Waziri kuhakikisha atawasaidia watoto hao katika kutimiza ndoto zao ikiwemo kuwasomesha na masuala mengine kupitia Wizara yake ambayo yenye dhamana, Waziri Ummy aliguswa na watoto hao kutokana na ndoto zao walizokuwa nazo ikiwemo kusoma zaidi.
  .Waziri Ummy Mwalimu akiwa akipeana mkono na kushikiria hundi ya sh. Mil 220, iliyotolewa na taasisi ya BAPS Charity kwa ajili ya kusaidia matibabu ya watoto 101, wa magonjwa ya moyo waliopo katika taasisi ya JKCI. .

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba  (kulia), akizungumza na wajumbe wapya wa kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknojia ya kisasa wakati akiizindua rasmi Dar es Salaam leo katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI). Kushoto ni Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Utafiti na Maendeleo, Hussein Mansour.
   Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru (kushoto), akitoa mada kuhusu zao la muhogo na changamoto za magonjwa yanayolishambulia.
   Baadhi ya wanakamati hao wakiwa ukumbini katika hafla 
  hiyo ya uzinduzi.

  Na Dotto Mwaibale

  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba ameitaka kamati ya kitaifa ya matumizi salama ya bioteknojia ya kisasa kutengeneza mpango kazi utakaosaidia kuharakisha shughuli zao na kuisaidia serikali.

  Makamba alitoa mwito huo wakati akizindua kamati hiyo mpya katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI) jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

  "Tengenezeni mpango kazi wenu ili serikali iufahamu na kuweza kuwasaidia kifedha endapo utakwama badala ya kukaa bila ya kuwa na dira na kusubiri kufanya mikutano yenu ya kupitisha jambo fulani mara tatu katika kipindi cha miaka nane" alisema Makamba.

  Alisema kamati hiyo ni ya muhimu sana katika utoaji wa maamuzi kuhusu masuala ya matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa na kukuza uelewa kwa wajumbe wa kamati hiyo na wananchi kwa ujumla.

  Alisema Tanzania ni nchi mwanachama wa mkataba wa bioanuai wenye malengo makuu matatu,  Hifadhi ya bioanuai, matumizi endelevu ya bioanuai na mgawanyo sahihi wa faida zitokanazo na matumizi yake.

  Alisema Tanzania iliridhia mkataba huo mwezi Machi, 1996 ili kushirikiana na Jumuia ya Kimataifa katika kutekeleza malengo yaliyotajwa.

  Alisema alisema changamoto kubwa ya teknolojia hiyo ya bioteknolojia ya kisasa bado kuna wasiwasi kuhusu athari zinazoweza kutokea ambazo ni mzio, kujitokeza kwa magugu sugu, saratani, usugu wa dawa kwa matibabu ya magonjwa, wakulima kutegemea mbegu za kununua kila na madhara mengine ambayo kwa sasa hayajawa bayana.

  Msimamizi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mikocheni (MARI), Dk. Joseph Ndunguru alisema wamejipanga kujenga kituo kikubwa cha utafiti kitakacho gharimu dola za Marekani 556,000.

  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda alisema ili wakulima waweze kufanikiwa katika kilimo chao ni vizuri wakawa wanazingatia ushauri wa wataalamu ambao wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali ambazo huwapelekea wao kwa matumizi ya kilimo.

  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Bi. Zaynab Matitu akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu kushiriki katika michezo itayofanyika Machi 5 mwaka huu ili kuadhimisha siku  ya  Wanawake Duniani  katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kushoto ni Mwenyekiti wa wa Baraza hilo Bw. Diomiz Malinzi.
  Mwenyekiti wa wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Bw. Diomiz Malinzi akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu kushiriki katika michezo itayofanyika Machi 5 mwaka huu ili kuadhimisha siku  ya  Wanawake Duniani  katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam kulia ni Makamu Mwenyekiti Bi. Zaynab Matitu.Picha zote na Ally Daud – Maelezo


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano nchini (TCRA), Dk.Ally Simba akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) juu hatua mbalimbali walizochukua kwa kampuni za simu za mikononi leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu watendaji wa TCRA na waandishi habari wakisikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Ally Simba (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii).


  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  KAMPUNI za Mawasiliano ya Simu za Mkononi zimepigwaa faini ya Sh.Milioni 90 kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya kanuni za ubora wa huduma.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jijini leo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA), Dk.Ally Simba amesema kuwa kampuni hizo zimepigwa faini tofauti kutokana na makosa mbalimbali ya utoaji huduma ya mawasiliano kwa wananchi.

  Dk.Simba amesema kampuni ziliitwa na mamlaka ambapo zilikiri kufanya hivyo na kukubali na kosa na maamuzi yaliyofikiwa kuwapiga faini kwa mujibu wa sharia za nchi.Mkurugenzi Mkuu huyo alizitaja kampuni hizo na faini zake kuwa ni Aitel sh.milioni 22.5 ,Smart sh.milioni 12.5, Tigo sh.milioni 25,Vodacom sh.milioni 27.5 pamoja na Zantel sh.milioni 25.

  Amesema kuwa kutokana kampuni hizo kushindwa kutimiza masharti TCRA itaendelea na utekelezaji wa sheria na maamuzi mengine kwao kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.Amesema baadhi ya makosa ni simu iliyopiga kudai kuwa inatumika wakati sivyo, wakati mwingine simu unapiga mwito wake unadai simu hiyo haipatikani wakati simu hiyo iko hewani.


  Aidha amesema kuwa watoa huduma wote wa simu za mkononi kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa na kuzingatia vigezo vilivyoanishwa.Dk.Simba amesema kuwa kampuni za simu za mikononi zimejikita katika kujitangaza kwa njia mbalimbali katika kuweza kupata wateja wapya lakini hazifanyi uwekezaji wa huduma bora kwa wananchi wanaotangazia.

  Hata hivyo TCRA imeipiga faini kampuni ya Azam Marine Sh.Milioni Tano kutokana na kufanya usafirishaji wa vifurushi kutoka Dar es Salaam na Zanzibar bila kuwa na leseni ya utoaji wa huduma hiyo.Amesema kuwa ni kosa kwa Azam Marine kufanya huduma ya posta bila kuwa leseni huku wakikri kufanya biashara ya kusafirisha vifurushi.

  Kampuni ya Lifalo imepigwa faini sh.10 kutokana na kufanya masafa ya ujumbe mfupi bila kuwa na kibali cha TCRA na lifalo ilikiri kufanya hivyo.Dk.Simba amesema kuwa walipewa namba mara ya kwanza kwa muda na baada ya kuisha hawakuweza kuendelea huku wakiendelea kutoa huduma ya ujumbe mfupi.

  0 0


  In this photo taken Wednesday March 2, 2016 at Tanzania’s Dar es Salaam Port, Handler from Tanzania Police Force leads the trained canine from the U.S Customs and Border Protection (CBE), as the Canine sniffs illegal items from one of these boxes during the handing over ceremony of four canines trained at CBE’s world class facility in El Paso Texas in the U.S. The U.S Government through it’s Embassy in Dar es Salaam has equipped police working at Julius Nyerere International Airport and the Port of Dar es Salaam with capability to detect a variety of illegally trafficked items, including wildlife products and drugs. U.S Embassy Deputy Chief of Mission, Virginia Blaser has Said. (PHOTOS; K-VIS MEDIA/Khalfan Said).
  The bravery canine snatch a suspected illegal item
  Canines line-up with their handlers, during the parade
  U.S deputy chief of mission in Tanzania, Virginia Blaser, makes her remarks during the event .

  BY K-VIS MEDIA/Khalfan Said

  THE U.S Government through it’s Embassy in Dar es Salaam has equipped police working at Julius Nyerere International Airport and the Port of Dar es Salaam with capability to detect a variety of illegally trafficked items, including wildlife products and drugs.

  Presenting four canines at a ceremony held at Dar es Salaam Port, Wednesday March 2, 2016. U.S Embassy Deputy Chief of Mission, Virginia Blaser, said, Wildlife and narcotics trafficking are serious crimes with devastating consequences for Tanzania’s natural resource, economy, and security, these are the rezones led to the U.S Government to support Tanzania Government to curb the vice.

  Four Police Officers, from Tanzania Police’s Dog and Horse Unit, who were specially selected for the canine detection program Tanzania, by the Office of the Inspector General of Police were trained together with their canines and certified in 2015 at CBE’s world class facility in El Paso, Texas in the U.S, said Blasser.

  In February 2016, CBE trainers arrived in the country to conduct on-the-job training at the Airport and Port.
  The Canine Detection Program is a model of what can be achieved when partners work together, stopping the poaching crisis and illicit narcotics trafficking requires everyone to contribute, she said.

  In his part. The Minister for Tourism and Natural Resources, Professor Jumanne Maghembe, who received the canines on behalf of the government, thanks the U.S Government for their endeavor support.

  He warned that, the country is facing serious threats on poaching and other crimes, “This support came timely and we promised to use this expertise to confront the hardcore criminals.

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Museven baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC,(kulia) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC.
  Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki wakisimama wakati wimbo wa umoja wa nchi hizo ukipigwa katika mkutano wa 17 wa EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto mkoani Arusha.
  Miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania walioalikwa katika mkutano wa 17 wa Viongozi wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto Hotel Mkoani Arusha,(katikati) Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini,akiwa na Mawaaziri wa Nchi za Jumuiya hiyo,{Picha na Ikulu.]

  0 0

   Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Trumark Tanzania, Agnes Mgongo akizungumza na waandishi wa habari jijiniDar es Salaam leo kuhusiana na kufanyika kwa tamasha la pamoja tunafanikisha linanaloandaliwa na kampuni ya Trumark litakalo fanyika Machi 5, mwaka huu katika ukumbi wa Kingsolomon Namanga jijini Dar es Salaam. Agnes amesema kuwa kutakuwa na burudani zitakazotolewa na Barnaba na Classic Band, Bi. Patricia Hillary na mchekeshaji maarufu MC Pilipili, wakisindikizwa na wasanii chipukizi.
  Aidha TruMark inawashukuru wahamasishaji na wadhamini wa maadhimisho haya, ambao ni Vayle Springs, Mummy’s Exclusive Shop, Flexible Entertainment, Marie Stopes Tanzania, King Solomon Hall, King Solomon Events, Mono Accessories, CSI Tanzania, MagicFM na Channel Ten.  
  Mwanamziki wa zamani wa Taarabu, Patricia Hilary akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa katika tamasha la Pamoja tunafanikisha linaloandaliwa na Kampuni ya TruMark kuwa atatumbuiza kwa nyimbo zake za zamani za Taarabu kama wimbo wa ewe njiwa utaimbwa laivu na mwanamziki huyo. Kulia ni Mratibu wa Tamasha la pamoja tunafanikisha wa kampuni ya TruMark, Azavery Phares.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  KAMPUNI ya TruMark yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam imeandaa tamasha la kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani la Pamoja Tunafanikisha, litakalofanyika Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa King Solomon, Namanga, Machi5,2016ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ndiye atakayekuwa mgeni rasmi tamasha hiyo litawashirikisha wanaume na wanawake ili kufurahia mafanikio ya wanawake.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa TruMark, Agnes Mgongo, amesema kampuni yake imeandaa tamasha hilo kwa kuwa kumekuwa na matukio mengi ya mafanikio kwa wanawake nchini Tanzania, ambayo bado wanaume hawajashirikishwa ipasavyo kuyatambua na kuyafurahia mafanikio hayo kwa kiwango kinachoridhisha.

  “Ni kweli, wapo wanawake wengi wenye mafanikio hapa nchini, lakini bado kuna changamoto nyingi, mojawapo ikiwa uchache wa ushiriki wa wanaume katika, kwanza, kufanikisha mafanikio hayo na, pili, kufungua fursa nyingi zaidi ili wanawake wengi zaidi waweze kuwa sehemu ya mafanikio hayo, kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii, kama vile sekta za fedha, elimu, sayansi, teknolojia, kilimo, viwanda, taaluma na biashara,” amesema.

  Kwa kutambua hilo, Agnesy amesema yeye na timu yake kabambe ya TruMark wameamua kuandaa adhimisho la kusheherekea Siku ya Wanawake Duniani ambapo mwaka huu, adhimisho hilo linaambatana na kaulimbiu ya kimataifa linalotutaka watu wote, wanaume na wanaume, kushirikiana kuharakisha harakati za kumwezesha msichana na mwanamke kufikia malengo na mafanikio yake, linalosema "PamojaTunafanikisha".

  Mwaka huu, maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, chini ya mwamvuli wa 'PamojaTunafanikisha' kampuni ya TruMark inaona fahari kubwa kuandaa sherehe hii ambayo ni jukwaa muhimu kwa taifa letu, katika kuhakikisha wanawake wanakuwa sehemu mojawapo ya kuchangia pato la taifa na maendeleo ya nchi.

  “Kila mtu mahali alipo kwa nafasi yake ni kiongozi wa kuleta chachu ya Maendeleo, hivyo basi, haina budi kila mtu, mahali popote, ashiriki vyema na kutimiza wajibu wake huo, huku tukisaidiana kwa pamoja kuanzia ngazi ya familia hadi taifa,” amesema.

  Agnesy amewashukuru Marie Stopes Tanzania ambao, kwa ushiriki wao, wameamua kutoa huduma ya bure ya upimaji na ushauri wa njia zote za uzazi wa mpango, upimaji wa saratani ya mlango wa uzazi kwa washiriki wote watakaofika kuhudhuria adhimisho hilo la Pamoja Tunafanikisha.

   Amewaomba wanaume kushiriki kwenye tamasha hili la Pamoja Tunafanikisha ili kwa pamoja jamii nzima iweze kufanikisha, sio tu mafanikio ya wanawake, lakini pia kuwawezesha kupata fursa zote za mafanikio, ikiwa ni pamoja na kutafuta fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.

  Adhimisho hilo, ambalo litafanyika kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga, Dar es Salaam, Jumamosi, tarehe 5 Machi 2016, litakuwa na burudani zitakazotolewa na Barnaba na Classic Band, Bi. Patricia Hillary na mchekeshaji maarufu MC Pilipili, wakisindikizwa na wasanii chipukizi.

  TruMark inawashukuru wahamasishaji na wadhamini wa maadhimisho haya, ambao ni Vayle Springs, Mummy’s Exclusive Shop, Flexible Entertainment, Marie Stopes Tanzania, King Solomon Hall, King Solomon Events, Mono Accessories, CSI Tanzania, MagicFM na Channel Ten.
  Imetolewa na TruMark Limited | +255-718-969 731 | +255-716-676 665 | info@trumark.co.tz.

older | 1 | .... | 1143 | 1144 | (Page 1145) | 1146 | 1147 | .... | 3270 | newer