Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

KATIBU WA BUNGE AFANYA UKAGUZI WA UKARABATI WA UKUMBI WA BUNGE UNAOENDELEA MJINI DODOMA.

$
0
0
 Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah (aliyesimama katikati) akikagua ukarabati wa ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma. Ukarabati huo unahusisha urekebishaji wa paa la ukumbi huo pamoja na urekebishaji wa Viti na mifumo ya Umeme.
  Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah (wa kwanza kulia) akikagua ukarabati wa ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma.
 Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah akikagua taa za Umeme ambazo zinatakiwa kubadilishwa wakati wa ukarabati wa ukumbi wa Bunge.

Picha na Ofisi ya Bunge.

TFF, KTA WAZINDUA PROGRAMU YA MAENDELEO YA SOKA KWA WANAWAKE.

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na Taasisi binafasi ya Karibu Tanzania Association (KTA) kwa pamoja wamezindua programu ya maendeleo ya soka kwa wanawake vijana ili kuhamasisha usawa wa kijinsia, uwezeshaji kijamii na kiuchumi kwa wanawake nchini itakayofadhiliwa na Shirika la Forum Syd kutoka nchini Sweden.
Uwekaji saini wa mkataba huo wa ushirikiano umefanywa na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mia Mjengwa Bergdahl, Mratibu wa Programu hiyo kutoka taasisi ya Karibu Tanzania Sweden katika ofisi za TFF zilizopo Karume.
Programu hiyo ni ya aina yake ambayo haijapata kufanyika nchini inalenga kujenga mfumo utakaotumiwa nchi nzima katika kutoa elimu na mafunzo kwa soka la wanawake kwenye maeneo ya ufundi (makocha), waamuzi (refarii), uongozi na tiba kwenye michezo.
Pia itawezesha kuendeleza vipaji kwa wachezaji wanawake vijana na kuongeza hali ya kujitambua na kujiamini kwa walengwa. Lengo ni kuongeza idadi ya wachezaji wenye ubora na viwango kwa soka la wanawake vijana katika ngazi zote, hivyo kuifanya programu hii kuwa nyenzo katika kuwawezesha wanawake.  
Kwa kuanzia kozi 20 za soka la wanawake vijana kwenye Vyuo 20 vya maendeleo ya wananchi zitaanzishwa kwenye kanda saba.  Jumla ya wanawake vijana 600 ikiwamo 30 kutoka katika kila chuo cha Maendeleo ya Wananchi watashiriki.
Katika programu hii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wanashiriki kikamilifu kwa kuwezesha wanafunzi na miundo mbinu ya vyuo vya maendeleo ya wananchi vilivyo chini ya wizara hiyo kutumika katika kufanikisha programu hii.
Mafunzo yatatolewa sambamba na mafunzo mengine ya kawaida yanayotolewa kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi, kama vile maarifa ya jumla na mafunzo ya ufundi. 

KAMPUNI YA KICHINA MATATANI KWA KUTENGENEZA VIBAO VYA NAMBA ZA MAGARI KINYUME CHA SHERIA

$
0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya msako wa kushtukiza katika kampuni ya Tanzania China Trade and Tourism Development Ltd iliyoko Barabara ya Nyerere Dar es salaam baada ya kupata taarifa kutoka kwa msamaria mwema na kukamata vifaa pamoja na malighafi za kutengeneza na kutoa vibao vya namba za pikipiki kinyume na sheria.

Katika msako huo uliofanyika tarehe 19 Februari 2016 katika kampuni hiyo, Maofisa wa TRA waliweza kukamata na kutaifisha vibao vyenye namba za pikipiki 2,500 na vibao 5,600 ambavyo havikuwa na namba. Pia maofisa wa TRA walikamata malighafi za rangi ya vibao katoni tatu, pamoja na mashine ya kupaka vibao rangi yenye uzito wa kilo 155.

Mashine nyingine iliyokamatwa katika msako huo ni ya kutengeneza namba za magari yenye uzito wa kilo 902 ambayo imezuiwa isihamishwe kutoka katika kampuni hiyo pamoja na kompyuta mpakato ambayo imepelekwa katika maabara ya uchunguzi TRA kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Taarifa za kuwepo kwa utengenezaji wa vibao vya magari kinyume na taratibu na sheria zilitolewa na msamaria mwema ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni husika Donglinh Guo, Meneja wa Kiwanda Yong Qing Cheng na Meneja wa ghala Peng Zhan walikamatwa baada ya kutokea fujo wakati wa msako na kufikishwa katika kituo cha Polisi Changombe.

Kampuni ya Tanzania China Trade and Tourism Development LTd ndio waingizaji pekee wa pikipiki za Falcon tangu mwaka 2008 ambapo inatuhumiwa kutoa vibao vya namba za pikipiki kwa wateja wake kwa shilingi 5,000 kinyume na sheria.
Uchunguzi wa thamani ya kodi iliyopotea bado unaendelea.

Vibao vya magari na pikipiki hutolewa na kampuni ambazo zinatambuliwa na TRA baada ya kupewa idhini. Kampuni hizo ni Masasi Sign, Auto Zone, Sign Industry, Kiboko, Budda Auto works, Parkinson Ltd na Next Telecom.

Ili kujiridhisha kuwa kadi za pikipiki zinazotolewa kwa wateja wa kampuni hiyo ni halali, TRA ilifanya uchunguzi na kugundua kuwa kadi hizo zinatolewa kihalali.

TRA inawatahadharisha wananchi kufuata taratibu na sheria ili kuepuka usumbufu unaoweza kutokea endapo watagundulika kujihusisha na vitendo ambavyo ni kinyume na sheria.

BENKI M YAZINDUA HUDUMA YA “MONEY MOJA KWA MOJA”

$
0
0
Katika kuendeleza utamaduni wake wa kuendana na wakati kwa kutoa huduma za kiwango cha juu, Benki M imezindua huduma mpya inayojulikana kama Money.Moja Kwa Moja ambayo itakuwa ikitumiwa na wateja wake kutuma hundi kwenda benki kutoka mahali walipo bila wao kwenda benki. Huduma hii ni ya kipekee kabisa kutokea barani Africa.

Akiongea katika uzinduzi wa huduma hiyo, naibu mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Bi. Jacqueline Woiso alieleza kuwa katika huduma hii wateja hawatahitaji kwenda benki kwa lengo la kuweka hundi zinazotoka katika mabenki mengine. “Huduma itahusu hundi zile ambazo wateja wetu wamelipwa na wateja wao kutoka benki zingine ambao huzileta kwetu kwa ajili ya kupelekwa kwenye benki hizo ili ziweze kulipwa”, alisema.

Hii imekuja baada ya Benki kuu ya Tanzania kuboresha mfumo wa malipo kwa njia ya hundi za ndani kwa lengo la kuufanya mfumo huo kuwa salama zaidi na wa haraka, mfumo huo mpya unajulikana kwa jina la TACH na umeanza kufanya kazi hivi karibuni.

“Kupitia huduma hii ya Money.Moja Kwa Moja wateja wataepukana na foleni za barabarani pindi watakapokuwa wakielekea kwenye matawi yetu, watapunguza mahitaji ya nguvu kazi na pia hawatakuwa na haja ya kuharakisha kuwahi benki pindi muda wa benki kufungwa unapokaribia. Wateja wetu wataweza kufanya miamala ya hundi wakati wowote watakaopenda na mahali popote na kuzituma kupitia mtandao na fedha hizo zitaingizwa kwenye akaunti zao bila wasiwasi wowote. Hivyo huduma hii itawawezesha wateja wetu kupata huduma ya kibenki mahali popote walipo” alieleza Jaqueline.

“Money.Moja Kwa Moja ni huduma yenye usalama zaidi inayotumia mtandao wa intaneti ambapo mteja wetu ataweza kuweka hundi kwenye akaunti yake kwa kutumia kifaa maalum kitakachochukua taswira ya hundi hiyo na kuituma benki na pia kuihifadhi taswira hiyo endapo itahitajika baadaye. Yote haya yatafanyika hapohapo ulipo bila wewe kutoka kwenda benki”, aliendelea Bi Woiso.

Benki M ilianzishwa mnamo mwaka 2007 kwa lengo la kutoa huduma ya kiwango cha juu hapa Afrika kwa kupitia huduma zake mbalimbali. Imekuwa ni benki ya kwanza kutoa huduma masaa 12 kila siku kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa mbili usiku, siku 7 za wiki yaani Jumapili hadi Jumapili. “Pia tunatoa Garantii endapo tutazidisha muda tuliokubaliana kufanikisha miamala ya wateja, huduma hii inajulikana kama SSG (Service Standard Guarantee), huduma ambayo mpaka sasa hamna benki ingine imeweza kuwa nayo hapa nchini” alimalizia.
Mkuu wa bidhaa wa Benki M, Johnbrighton Ngowi akifafanulia jambo kwa waandishi wa habari kuhusu huduma mpya iliyozinduliwa na Benki hiyo ijulikanayo kama “Money.Moja Kwa Moja”ambayo itatumiwa na wateja wa benki hiyo kuweka taswira ya hundi na kuituma benki kutoka mahali popote walipo bila ya kwenda benki, uzinduzi huo ulifanyika jijini dare s salaam hivi karibuni. Mwingine ni naibu mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Bi. Jacqueline Woiso.
Baadhi ya wageni waalikwa walikohudhuria uzinduzi wa huduma mpya ya benki M ijulikanayo kama “Money.Moja Kwa Moja” ambayo itamwezesha mteja wa Benki M kuweka taswira ya hundi na kuituma benki kutoka mahali popote walipo bila ya kwenda benki.

PROF. MBARAWA ATOA MWEZI MMOJA KWA MAKANDARASI.

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kuhusu ukusanyaji madeni ambayo Wakala wa Majengo nchini (TBA) inadai wapangaji wake. 
 Muonekano wa barabara ya Sakina-Tengeru Km 14.1 inayojengwa kwa njia nne kwa kiwango cha lami ili kupunguza msongamano wa magari kuingia na kutoka katikati ya jiji la Arusha. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Fadhili Nkurlu jijini Arusha.

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa makandarasi wote nchini kuhakikisha wanasaini mikataba ya ajira na wafanyakazi katika miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea nchini kote.

Akizungumza jijini Arusha mara baada ya kufanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa Km 14.1 na barabara ya mchepuo ya kusini (Arusha bypass) yenye urefu wa Km 42.4, Prof. Mbarawa amesema mkandarasi atakayeshindwa kutoa mikataba kwa mujibu wa sheria za Tanzania, atanyang’anywa kazi ya ujenzi kwa kuvunja sheria.

“Barabara zinajengwa kwa kodi za wananchi hivyo wajenzi wa barabara nao ni lazima wafuate sheria za nchi ili kuhakikisha Serikali inapata kodi stahili na wafanyakazi wazawa nao wanapata haki stahili kwa mujibu wa ajira zao", amesema Waziri Prof. Mbarawa. 

Amezitaka taasisi za TRA, NSSF na nyingine zinazosimamia ajira za wafanyakazi kufuatilia miradi ya ujenzi ili kuona fursa za mapato ambazo serikali inaweza kupata na kusajili wafanyakazi katika hifadhi ya mifuko ya jamii.

Waziri Prof. Mbarawa amewataka mameneja wa tanroads na maafisa kazi kukagua mikataba ya ajira za ujenzi katika maeneo yao ili kuona haki inatendeka kwa makandarasi na kwa wafanyakazi ili ujenzi wa barabara ukamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amefungua mkutano wa Sita wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na kuwataka kuweka mikakati itakayowezesha kulinda hifadhi ya barabara, kudhibiti magari yanayozidisha uzito na kusimamia kasi katika miradi ya ujenzi wa barabara.

“Mmekua mkifanya kazi nzuri, endeleeni kufanya kazi kwa uadilifu, uwazi, weledi na kujiwekea malengo ya kujipima mwaka hadi mwaka ili muendelee kuwa tassisi ambayo watu watakuja kujifunza kwenu”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa TANROADS imejipanga kuhakikisha miradi ipatayo 90 ya ujenzi wa barabara inayoendelea nchini kote inakamilika katika ubora unaotakiwa na unao uwiana na thamani ya fedha.

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amemuagiza Meneja wa Wakala wa Majengo nchini (TBA), mkoa wa Arusha, Bw. Victor Baltazar kukusanya madeni yote kwa haraka ili kukamilisha miradi ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na za biashara inayosimamiwa na Wakala huo mjini Arusha kukamilika kwa wakati.

Prof. Mbarawa ambaye yuko katika ziara ya mikoa ya kanda ya kaskazini amezitaka taasisi zilizo chini wa wizara hiyo kuhakikisha zinafanya kazi kibiashara ili kuboresha mapato ya Serikali na hivyo kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi.

WAFUMBUZI WA MIFUMO YA TEKNOLOJIA KUNUFAIKA NA M-PESA.

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha mifumo ya kiteknolojia ya biashara wa Vodacom Tanzania, Josephat Kyando (kushoto)”Head of VAS & M-Commerce Technology” na Meneja wa huduma za M-Pesa wa kampuni hiyo, Polycarp Ndekana wakiangalia moja ya mifumo ya Kiteknolojia inayotumika kutoa huduma za kifedha wakati wa semina ya  siku moja ya wafumbuzi wa mifumo mbalimbali ya Kiteknolojia  iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa makampuni binafsi ili kujua jinsi gani wanaweza kutumia huduma ya M-Pesa kuboresha biashara zao jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya wafumbuzi wa mifumo mbalimbali ya Kiteknolojia  wa makampuni binafsi wakiwa kwenye semina ya  siku moja ya wafumbuzi wa mifumo hiyo  iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ili kujua jinsi gani wanaweza kutumia huduma ya M-Pesa kuboresha biashara zao jijini Dar es Salaam jana.

WAFUMBUZI wa mifumo mbalimbali ya Kiteknolojia  kutoka  makampuni binafsi jijini Dar es Salaam wamenufaika na mafunzo ya jinsi gani wanaweza kutumia huduma ya M-Pesa kuboresha biashara zao katika Warsha  ya siku moja iliyofanyika  jijini Dar es Salaam jana.


Akiongea kuhusiana na mafunzo hayo  Mkuu wa kitengo cha mifumo ya kiteknolojia ya biashara wa Vodacom Tanzania, Josephat Kyando alisema mafunzo haya   ni mafunzo ya kwanza bora yanayoendana na teknolojia ya kisasa ambayo hayajawahi kutokea hapa nchini yanayohusiana na huduma za M-Pesa ambayo kampuni imeanza kuyatoa sasa.


Kyando pia alisema kuwa washiriki wameweza kujua Programu za utekelezaji shughuli za kibiashara ambazo inaendelea kuzibuni na jinsi zitakavyotumika kuboresha uendeshaji wa biashara za sekta mbalimbali kupitia huduma ya M-Pesa.


“Hivi sasa huduma ya M-Pesa imekuwa na inaendelea kutumika katika huduma nyingi za malipo na kurahishisha biashara na kuwezesha watumiaji wake kuwa  na usalama wa maisha yao na fedha zao hivyo ndio maana tumekuwa na utaratibu wa kukutana na wadau mbalimbali na kuwaelimisha ni kwa jinsi gani wataboresha biashara zao kupitia huduma hii”.Alisema.


Alisema kuwa makampuni mengi binafsi hususani yanayomilikiwa na kuongozwa na vijana wameonyesha mwamko mkubwa wa kuhudhuria mafunzo haya ambapo pia wanapata fursa ya kutoa maoni yao kuhusiana na jinsi unavyoweza kuboreshwa zaidi.


Katika semina hiyo ilibainishwa kuwa huduma ya M-Pesa inaweza kurahisisha na kuyapunguzia gharama wafanyabiashara na taasisi mbalimbali  katika kulipa mishahara ambapo badala ya kutumia muda mrefu kwenda kwenye mabenki wakawa wanalipwa kwa kutumia huduma hii ambayo inaongoza kuwa na watumiaji wengi nchini.


Kyando alisema kuwa Vodacom kupitia kampeni yake ya Life is Better imedhamiria kubuni huduma mbalimbali za kutumia mtandao kurahisisha maisha ya watanzania ikiwemo kuwapatia mawasiliano ya gharama nafuu.

WAZIRI MUHONGO ATAKA MAKAMPUNI KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA KATIKA UTAFITI WA MAFUTA, GESI.

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mbele) akiongoza kikao kati yake na kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa vifaa na teknolojia katika utafutaji wa mafuta na gesi ya  Schlumberger. Pia kikao hicho kilihusisha watendaji kutoka Wizara hiyo pamoja na  taasisi zake  likiwemo  Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) na Mamlaka  ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Masoko  kutoka kampuni  ya Schlumberger, Abdul Adeshina (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Meneja Masoko  kutoka kampuni  ya Schlumberger, Abdul Adeshina akielezea shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaza vifaa na teknolojia kwa ajili ya utafiti wa mafuta na  gesi nchini.

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ametaka makampuni yanayojishughulisha na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa  gesi na mafuta nchini kuongeza kasi ya utafiti kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili sekta ya  gesi na mafuta iweze kukua na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.


Profesa Muhongo alitoa kauli hiyo alipokutana na kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa vifaa na teknolojia katika utafutaji wa mafuta na gesi ya  Schlumberger yenye makazi  yake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili  utendaji kazi wa  kampuni hiyo.


Kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam kilihusisha watendaji kutoka Wizara hiyo pamoja na  taasisi zake  likiwemo  Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) na Mamlaka  ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).


Alisema  Tanzania kwa sasa ina utajiri mkubwa wa  rasilimali ya  gesi ambayo  itachochea katika  ukuaji wa uchumi wa nchi  kupitia umeme wa uhakika utakaotumika katika viwanda na kuongeza  ajira kwa  vijana wa kitanzania.


Aliendelea kusema kuwa ili  sekta ya gesi na mafuta iweze kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi, Tanzania inahitaji wawekezaji  watakaowekeza kwa kasi kwa kutumia  teknolojia ya kisasa.


Alisisitiza kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na mwekezaji  yeyote mwenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya gesi na mafuta kwa kutumia  teknolojia ya kisasa.


“ Kama serikali  tumedhamiria kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi zenye utajiri unaotokana na rasilimali za gesi na mafuta, hivyo  tunapenda kushirikiana  na wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kutumia  teknolojia  ya kisasa,” alisema  Profesa Muhongo


Profesa Muhongo aliihakikishia kampuni ya Schlumberger kuwa  serikali itafanya kazi kwa karibu nayo na kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika ili sekta ya  gesi na mafuta iweze kukua kwa kasi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.


Awali akizungumza katika kikao hicho Meneja Masoko  kutoka kampuni  ya Schlumberger, Abdul Adeshina alisema  kampuni  yake  imekuwa imekuwa  ikitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kitanzania asilimia  80 wanaofanya kazi katika kampuni  hiyo.


Aliongeza kuwa kampuni hiyo imekuwa  ikishirikiana kwa karibu na  Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) katika shughuli za utafiti wa mafuta na gesi nchini  na kusisitiza kuwa kampuni hiyo  ipo tayari kutumia teknolojia na  vifaa vyake katika kuboresha shughuli za utafutaji wa mafuta na  gesi nchini.

Serikali yatoa wito wafanyabiashara wa Mauritius kuwekeza nchini

$
0
0
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akipokea maelekezo ya bidhaa kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya SLK Gold Taste wakati wa Mkutano na Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius jana Jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa huduma za kibiashara wa Tantrade, Fidelis Mugenyi (kushoto) na Balozi wa heshima wa Mauritius, Abbas Rizvi. 
Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Mkutano na Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius jana Jijini Dar es Salaam. Wengine ni Balozi wa heshima wa Mauritius, Abbas Rizvi (kulia) na Meneja wa kampuni ya Enterprise Mauritius, Rajen Subbamah.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano huo.
Washiriki wa maonyesho wakitembelea baadhi ya wafanyabiashara.
Serikali imeahidi kuendelea kuboresha mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kuongeza miradi ya uwekezaji ili kufikia lengo na Dira ya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Charles Mwijage wakati wa ufunguzi wa Mkutano na Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius yakilenga kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina ya mataifa haya mawili jana Jijini Dar es Salaam.

Alisema moja kati ya jitihada zinazofanywa na serikali ni pamoja na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kufanya baadhi ya mambo ambapo sasa usajili wa kampuni unaweza kufanywa mtandaoni.

“Natoa wito kwa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Mauritius kuwekeza nchini kutokana na uwepo wa rasilimali za kutosha, bandari pamoja na soko la uhakika kwani nchi yetu inapakana na nchi saba ambazo muwekezaji anaweza kuuza bidhaa huko kwa urahisi,” alisema Mh. Mwijage katika hotuba yake iliyosomwa naMkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo.

Maonyesho hayo yanaandaliwa na kampuni ya Talemwa Investment Consulting Company (TICC) pamoja na Enterprise Mauritius kwa ushirikiano na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA).

Awali akiongea wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi wa TICC, Bw. David Lutabana alisema maonyesho hayo ni fursa ya kipekee inayowakutanisha wafanyabiashara kutoka nchi hizi mbili ili kuweza kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili fursa mbalimbali zilizopo katika nchi hizo.

Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Meneja wa kampuni ya Enterprise Mauritius, Rajen Subbamah, alisema sekta zinazoshiriki kutoka Mauritius ni pamoja na sekta ya ukandarasi, bidhaa za kilimo, kemikali, viwanda vya utengenezaji nguo na vidani, pamoja na sekta zingine.

“Nchi yetu ina uhaba mkubwa wa malighafi na kwa upande mwingine Tanzania imebarikiwa kwa kiasi kikubwa kuwa na rasilimali mbalimbali. Kupitia mkutano huu tunatizamia kujenga mahusiano na wafanyabiashara wa hapa Tanzania ili tuweze kufanya biashara zitakazonufaisha pande zote mbili,” alisema Bw. Subbamah.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

BEI YA MADAFU HII LEO.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA MABALOZI OFISINI KWAKE LEO.

$
0
0
WAZIRI MKUU Kasim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi watatu kutoka nchi za Uturuki, Ireland na Uswisi pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na mabalozi hao leo (Jumanne, Februari 23, 2016), ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amewashukuru mabalozi hao kwa kuja kujitambulisha rasmi na kwa pongezi walizokuja kumpatia na kuahidi ushirikiano zaidi pamoja na nchi hizo.

Mapema leo, Waziri Mkuu amekutana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez ambaye amemweleza jinsi UNDP imekuwa ikisaidia programu za kukabiliana na maafa (resilience), ukuaji wa uchumi, utawala bora na masuala ya jinsia.

Amesisitiza haja ya Tanzania kuendeleza kampeni ya kupambana na ujangili na kusisitiza kuwa Umoja huo una nia ya kusaidia utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Naye Balozi wa Uturuki, Bibi Yesemin Eralp alimweleza Waziri Mku nia ya nchi kuleta wawekezaji katika nyanja za kilimo, nishati, afya na ujenzi na kusisitiza kuwa kuna haja ya kufungua ubalozi wa Tanzania nchini kwao ili kuimarisha uhusiano uliopo.

“Tunao uwezo wa kifedha na tunao uwezo wa kitaalamu na kiteknolojia. Tukifungua viwanda hapa nchini, tunaweza kuongeza ajira kwa Watanzania,” alisema.

Naye Balozi wa Ireland nchini, Bibi Fionnuala Gilsenan alimweleza Waziri Mkuu jinsi ambavyo nchi yake imekuwa ikisaidia sekta za kilimo kupitia mpango wa ASDP, bajeti ya Serikali na suala la lishe na urutubishaji wa vyakula (food nutrition and fortification).

“Tulianza na suala la kilimo na bajeti ya Serikali. Hivi sasa tunataka kusaidia kwenye uelimishaji juu ya haki za wanawake, masuala ya uzazi wa mpango, pamoja na kupambana na ndoa za utotoni,” alisema.

“Tumeamua kupigia kelele suala la lishe na urutubishaji wa vyakula kwa sababu lishe duni imechangia kwa kiasi kikubwa udumavu wa watoto wengi. Tulipoanza tatizo hili lilikuwa limeenea kwa asilimia 46 kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano lakini sasa limepungua na kufikia asilimia 36 hadi 38,” aliongeza.

Amemuomba Waziri Mkuu Majaliwa alishikie bango suala hilo kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kote nchini kwani mtoto akishadumaa kimakuzi hata akili yake pia inadumaa na tatizo lake haliwezi kurekebishwa kwa tiba yoyote ile.

Naye Balozi wa Uswisi nchini, Bibi Florence Mattli alimweleza Waziri Mkuu nia ya nchi yake kudumisha ushirikiano na Tanzania ambao umedumu kwa miaka 50 ili kukuza viwango vya uchumi na kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Alimweleza Waziri Mkuu jinsi nchi yake imekuwa ikisaidia kundeleza nyanja za kupambana na rushwa kupitia TAKUKURU na kampeni ya kusaidia kujenga uelewa wa wananchi kupitia vyombo vya habari nchini.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza  na  Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez  Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 23, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Yosemin Eralp kabla ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 23, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HUDUMA YA MAJISAFI YAREJEA JIJINI DAR

$
0
0
SHIRIKA LA Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imerejesha  huduma ya upatikanaji wa Maji katika maeneo yote yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu chini  jijini Dar es salaam, pamoja na maeneo ya mji wa Bagamoyo mkoani Pwani kutokana na mtambo huo kuzimwa kwa wastani wa saa 36 kuanzia siku ya Alhamisi 18/02/201.

Akizungumzia kurejea kwa huduma hiyo, Meneja uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amesema kuwa huduma ya Maji katika jiji la Dar es salaam na miji ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa sasa yameanza kwenda kwa wananchi, na maeneo mengi ya jiji ambayo yalikosa huduma ya Maji kutokana na uzimwaji wa mtambo wa Ruvu chini.

“Napenda kuwaambia wateja wetu kuwa huduma ya Maji kwa sasa imerejea kwenye maeneo mengi ya jiji baada ya matengenezo kukamilika na mtambo kuwashwa siku ya Jumapili saa 9:30 alasiri” alisema Bi. Lyaro.

Alibainisha kuwa Kuna maeneo mengine yatachelewa kupata Maji kwani mara nyingi kwa kitaalamu huwa mtambo ukizimwa kwa zaidiya saa 24 ndani ya mabomba ya kupitisha Maji hujaa hewa hivyo baadhi ya maeneo kazi ya utoaji hewa kwenye mabomba unaendelea, hivyo tuwahakikishie wananchi kuwa huduma imerejea na wataipata ndani ya muda tuliotarajia.

Awali, mtambo wa Ruvu Chini ulizimwa ili kuwaruhusu wakandarasi kutoka kampuni ya sino Hydro na mafundi kutoka DAWASCO kukarabati bomba la Maji lenye inchi 54 linalosafirisha Maji kutoka Bagamoyo mpaka matenki ya Chuo kikuu cha ardhi, Bomba lililokuwa likivuja maeneo ya Makongo Jeshini, na kusababisha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kukosa huduma ya Maji, Mji wa Bagamoyo vijiji vya Zinga, Kerege na Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach na Kawe.

Maeneo mengine ni pamoja na Maeneo ya Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City centre, Ilala,, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya Rufaa Muhimbili, Buguruni, Chang’ombe na Keko.

ZUHURA YUNUS WA BBC AFANYA MAHOJIANO NA RAIS MUSEVENI WA UGANDA

BREAKING NEWZZZ: WAZIRI KITWANGA AAGIZA MABADILIKO MAKUBWA IDARA YA UHAMIAJI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga ameagiza yafanywe mabadiliko makubwa katika Vitengo mbalimbali vya Idara ya Uhamiaji ili kuboresha huduma na kuimarisha uadilifu katika Vitengo hivyo.

Mheshimiwa Kitwanga ametoa maagizo hayo leo wakati alipofanya kikao na Viongozi wa Idara ya Uhamiaji ambapo pia kilihudhuriwa na Viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwemo Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara.  Kikao hicho kilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Katika kikao hicho, Mheshimiwa Kitwanga ameagiza watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji walioko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, wahamishwe na kupelekwa maeneo mengine nchini, wakiwemo wale wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Wengine watakaohamishwa ni kutoka Kitengo cha Pasipoti, Uhasibu, Hati za Ukaazi na Kitengo cha Upelelezi, vyote vya Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.



Aidha ameagiza pia kuwa Wakuu wote wa Vitengo vya Upelelezi vya wilaya zilizopo jijini Dar es Salaam, na pia wale wa Vituo vya Tunduma, Mtukula, Holili na Kasumulo, wahamishiwe maeneo mengine, na pia watumishi wote waliokaa kwa zaidi ya miaka mitatu katika Vituo hivyo.



Amesema hatua hii inayochukuliwa sasa  ni mwanzo tu wa mabadiliko makubwa yatakayofanywa katika Idara ya Uhamiaji ili kuboresha huduma zinazotolewa na Idara hii ambayo ni moja ya Idara muhimu za Serikali.

Amesema katika kuisafisha Idara hii, uangalifu mkubwa utachukuliwa ili kuhakikisha kuwa hakuna mtumishi anayeonewa wala kupendelewa, lakini lengo kubwa ni kuvunja mtandao wa wapokea rushwa na wale wasiowajibika.



Amesema kufuatana na utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa matatizo ya rushwa katika Idara ya Uhamiaji yanashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na asilimia 30, asilimia 20 ni uongozi mbovu na asilimia 20 ni matumizi mabaya ya madaraka. Asilimia 15 inahusisha vitendea kazi wa mifumo hafifu ya kufanya kazi, asilimia 10 huduma mbovu na asilimia 5 ukabila na upendeleo.



Amewataka Viongozi na watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya kazi na waepuke vitendo vya kupokea rushwa na kusaidia wahamiaji haramu na wauza madawa ya kulevya.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

23 Februari, 2016
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni (kulia meza kuu) wakifurahi jambo pamoja na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji (kushoto) na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (kulia), wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi ndani ya Idara hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wakwanza upande wa kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MKAZI WA MAFINGA APORWA SH.MILIONI 12 DAR.

$
0
0
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MKAZI wa Mafinga,  David Isack ( 32) alivamiwa na majambazi na kuporwa sh.milioni 12 ambazo alikuwa akipeleka katika Benki ya  DTB, ambapo alivamiwa na  watu  watano wanatuhumiwa kuwa ni majambazi wakiwa na usafiri wa pikipiki  mbili aina ya boxer.

Akizungumza na waandishi wa habari ijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro amesema kuwa tukio hilo lilitokea Februari 12 mwaka huu katika eneo la Uwanja Ndege , katika kurupushani za kutaka kuchukua fedha hizo walitokea askari na kuwazingira na kisha kuanza kukimbia na kuweza kudondosha bunduki aina ya SMG pamoja na risasi 24 ambazo zilitakiwa kutumika katika tukio hilo.

Amesema askari walipowakamata wananchi walikusanyika katika tukio hilo na kuanza kuwapiga watu wanaodaiwa kuwa majambazi mpaka kupoteza maisha kutokana kushambuliwa huko na wengine watatu waliweza kukimbia na kiasi hicho cha fedha.

Kamishna Sirro amesema Isac alikuwa akitokea benki ya NMB na kwenda kupeleka fedha hizo katika benki ya DTB iliyopo Quality Plaza.

Katika operesheni nyingine imefanikiwa kukamata bastola moja ambayo ilipatikana  Februari 19 mwaka huu maeneo ya Kiwalani Kwa Gude kutokana na polisi kupata taarifa juu ya watu kujificha katika kichaka kwa ajili ya kufanya uhalifu  na baada ya kugundua polisi wapo eneo hilo walikimbia na kuacha silaha hiyo na jeshi la polisi linafanyia kazi mmiliki wa silaha.

Hata hivyo Jedhi la Polisi Kanda Maalumu linawashikilia watu wane wanaodaiwa kuwa ni majambazi sugu waliowakamata eneo la  Buguruni kwa Mnyamani ambao ni Mohamed Hassan maarufu kwa jina Kidali (21)Mkazi wa Vingunguti Speco,Hamis Alli (20) Mkazi wa Buguruni kwa Mnyamani, Adam Salum (23) Mkazi wa Buguruni  kwa Madenge, Bakari Hamis (19) Mkazi wa Buguruni.

Aidha amesema katika taarifa usalama Barabarani wameweza kukusanya zaidi ya Sh. Bilioni moja ya ni fedha iliyotokana na makosa ya magari kuanzia Januari 02 hadi Februari 22 mwaka huu.

MAJALIWA AKUTANA NAWADAU WA SUKARI.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa sukari nchini, ofisini kwake jijini Dar es salaam leo, Februari 23, 2016. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAJASIRIAMALI WAKULIMA NA WAFUGAJI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MIKOPO YA MASHINE BILA DHAMANA.

$
0
0
Bango la matangazo la Kampuni ya EFTA LTD ilikiwa kwenye mzunguko wa Mnara wa Mwenge likiwakaribisha kwenye maonyesho ya siku tatu ya mashine na mikopo kama lilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha

Mahmoud Ahmad Arusha.
WAJASIAMALI kote nchini wakiwamo pia wakulima na wafugaji nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya mikopo ya vifaa ikiwemo trekta na mashine mbali mbali za kilimo na ufugaji sambamba na vifaa mbali mbali lengo likiwa ni kukuza kipato kwa wananchi.

Akizungumza na waanahabari meneja mikopo wa kampuni ya Wasambazaji wa vifaa kutoa mikopo kwa wajasiriamali bila dhamana yeyote (EFTA)yenye makao makuu yake Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Peter Temu amesema kuwa wanawakaribisha wananchi kwenye maonyesho hayo ya siku tatu yakatayofanyika mkoani hapa.

Amesema kuwa kwenye maonyesho hayo zaidi ya wauzaji na wasambazaji wa mashine 25 watakuwa wakionyesha bihdaa na mashine walizonazo kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wananchi watakaoudhuria ili wajue matumizi bora ya mashine aina,mashine halisi,waranti na mabo mengine mbali mbali bila ya kiingilio.

Alisema kuwa mbali na maonyesho hayo ya EFTA pia wamejianda kuwafanya watembeleaji wa mabanda ya maonyesho hayo kuona na kupata mambo mengi ya ziada ikiwemo kupata semina na mafunzo kwa wajasiriamali toka kwa wataalamu mbali mbali bila malipo.

“Mafunzo haya yatatolewa bure na wataalamu wenye uzoefu na masuala ya ujasiriamali na kilimo ili wakulima na wajasiriamali wapate faida ya shughili wanazofanya kama kuongeza thamani katika bidhaa wanazozalisha na vifungashio vya kilimo na viwandani”alisema Temu

Alisema hiyo itakuwa fursa muhimu nay a kipekee kwa watanzania watakaobahatika kufika kwenye viwanja vya makumbusho kwa siku tatu kuanzia Alhamisi hadi yatakapofungwa jumamosi huku wakitarajia wakazi wengi kutoka mikoa ya kaskazini ikiwemo Kilimanjaro,Tanga,Arusha na Manyara kuchangamkia na kufika kukutana na wauzaji na was am,bazaji hawa huku wakijua kuwa EFTA LTD inafanya nn kwa ajili yao katika shughuli nzima ya utoaji wa mikopo bila dhamana na kutoa huduma ya mikopo moja kwa moja kwa wajasiriamali na wakulima wote watakaofika katika maonyesho hayo.

“Tunaposema mashine za kila Aina tunamaanisha anazohitaji mteja na sio kuwa tunamchagulia mteja,mfano mashine na vifaa vya kilimo,mashine za kufyatulia matofali,mashine za kukamulia alizeti vifaa vya maabara mashine za kutengeneza chakula cha mifugo na kutotolea vifaranga pamoja kilimo cha umwagiliaji na green house na nyingine nyingi’’Alisema Temu

The Ultimate Guide On How To Start Petro Filling Station In Tanzania

$
0
0
We all know Tanzanian oil and gas sector is the industry with amazing opportunities. Unfortunately, only a few have access to information regarding emerging opportunities in the gas sector.

And the sad reality is this, people having this information are unwilling to share with others.
I wonder why there is restricted information in this sector.

Okay, that is the talk of another day. The topic at hand is how to set up petrol station in Tanzania.
Article explains how to start petrol station with detailed requirements on initial capital needed to start this business, profit potential you make in this business and tips to succeed in this investment.

Let’s get started
Despite the fact that Tanzania has not recent oil discovery but we are the largest consumer of petroleum products.According to international energy agency, Tanzania consumes 35,000 barrel of oil refined products in 2013.Is for this reasons petrol station is lucrative business in Tanzania.

Why petrol station is the fantastic business
In business sense, An outstanding business is the one which offers products or solutions that are in serious requirement by people
This is true for this investment. Why? because everyone is in contact with oil-related products(diesel kerosene and gasoline)

Thousands of automobile, vehicle, and motorbike in Tanzanian run by oil product, Factories, organizations, medical centers, educational institutions, media house all have generators powered by diesel fuel. Not to mention Media house, and town halls.

BIBI ABIOLA DELUPE MWAKILISHI WA UBALOZI WA NIGERIA ATEMBELEA EFM.

$
0
0
Mwakilishi wa ubalozi wa Nigeria, bibi Abiola Delupe aitembelea Efm Radio leo  katika vitengo tofauti na  kuona utendaji kazi wa radio. Huku akikutana na baadhi ya watangaziji  kujadili mambo tofauti tofauti na jinsi watakavyo weza kuendeleza kazi zoa nje ya mipaka ya Tanzania.
  Meneja mkuu Dennis Ssebbo akijadili mambo tofauti kuhusiana na ufanisi wa kazi katika radio hiyo.
Bibi Abiola Delupe (Kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi  wa Efm radio Francis Ciza. 
Baadhi ya viogozi wa Efm Radio katika mazungumzo na Bibi Abiola Delupe.
 Bibi Abiola Delupe akizungumza jambo na Mkurugenzi  wa Efm radio Francis Ciza.

RAIS DKT. MAGUFULI AHAKIKISHIWA KUWA HALI YA BURUNDI NI SHWARI.

TEASER JOTO LA ASUBUHI JUMATANO FEBRUARY 24, 2016

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images