Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109604 articles
Browse latest View live

JK AZINDUA OFISI YA CCM WILAYA YA KIBAHA MJINI LEO

0
0

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizindua Ofisi ya CCM Wilaya ya Kibaha mjini mkoani Pwani leo. Ofisi hiyo imejengwa na familia ya Mbunge wa Kibaha mjini Slyvester Koka (kulia). (Picha na Bashir Nkoromo).

BARAZA LA WATOTO RUANGWA LAPATA VIONGOZI.

0
0

Mwandishi wetu Lindi
BARAZA la watoto mkoani  Mkoani Lindi  limefanya uchaguzi wa Viongozi wataliongoza  kwa muda wa miaka miwili kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 baada ya   viongozi waliokuwapo madarakani kumaliza muda wake kwa mujibu wa katiba.

Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa  
 Uliofadhiliwa na  shirika lisilo la kiserikali la Save the Children International  ambapo nafasi zilizogombewa ni pamoja na  Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti,Katibu,Katibu Msaidizi  Mtunza Hazina wajumbe kamati ya utendaji na  kundi maalumu.

 Msimamizi wa uchaguzi  Afisa maendeleo mkoa Lindi, Anna Maro alimtangaza Aziza Ahmad   kutoka wilaya Ruangwa kuwa Mwenyekiti  baada ya kupata  kura 9 na kuwashinda wapizani  wake Salamu Mwinja kutokaWilaya Kilwa aliyepata kura 6 na siwafu mpende kutoka Lindi aliyepata kura 5 huku Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikichukuliwa na Shaibu Peleu  kutoka wilaya Liwale badaa ya kupata kura 8 kati ya 18 zilizopigwa na kuwaacha wapizani  wake  wa wili  wakigawanya kura sita sita kila moja.

 Nafasi ya Katibu wa baraza hilo  ilichukuliwa na Abdul Selema kutoka wilaya ya kilwa  ambaye alipata kura 13 baada ya kumshinda mpizani wake Saidi Mohamedi kutoka Lindi mjini aliyepata kura 7 na  Katibu Msaidizi alipata  Swaumu Juma  aliyepata  kura 8 kati ya kura zote zilizopigwa.

Anna maro  alimtangaza Sadamu Hamidu kutoka Kilwa  kuwa Mhazini wa baraza hilo ambaye alipata kura 9 wakati Siwatu mpende  kutoka Lindi Mjini alipata nafasi ya Mhazini Msaidizi kwa kupata kura 9

kwenye Uchaguzi huyo  pia walichaguliwa wajumbe wawakilishi kundi maalumu wa baraza la Mkoa wa Lindi ambapo wajumbe   ambapoArkama Kihaku  kutoka wilaya ya Liwale alipata kura 17 na Nasoro isa kutoka Lindi Mjini alipata kura 2  

Akizungumzia majukumu ya baraza la watoto Daudi Busweli Afisa Maendeleo ya jamii kutoka shirika lisilo la kiserikali la save the children  ambalo linafadhili mabaraza ya watoto mkoa wa Lindi  na shughuli za na kusimamia haki za watoto kwa kushirikiana na asasi za kijamii  za  Kingonet, Ropa na Lingonet  alisema kuwa baraza la watoto linajukumu la kutambua haki za watoto na kuzisimamia haki hizo na kutafuta njia za kuondoa changamoto zinazosababisha watoto kutotendewa haki zao na jamii.
 Akizungumza kwa niaba ya viongozi waliochaguliwa kwenye uchaguzi huyo Mwenyekiti wa baraza hilo  Aziza Ahmadi    amesema kuwa baraza la watoto wilaya humo aliwavumilia wazazi, walezi na wananchi atakaye nyanyasa na  kuvunja  haki ya mtoto ya kupata elimu , Kulindwa kwa kumsababishia Mtoto wa kike hasa wanafunzi akwa  kumpa ujauzito ,kushindwa kumpeleka  shule kwa visingizio visivyo vya msingi.

Aidha Aziza Ahmadi  amewashauri watoto  hasa wa kike kuacha tamaa ambazo zinawaingiza kwenye matatizo yanayosababisha kupata mimba za utotoni ambazo zinaharibu malengo yao ,pia amewataka wazazi kuwalinda watoto wao ili wasiingie kwenye vishawishi hasa wanapokuwa shuleni kwani vishawishi hivyo ndivyo vinapelekea wao kushindwa kuendelea na masomo,

Aziza  amevitaja vishawishi hivyo kuwa ni pamoja na simu za Mkononi ambazo zinajenga uhusiano wa karibu wa wanaume au wanawake wenye tabia za kuwaingiza watoto kwenye matendo yanayokwenda kinyume na haki za watoto na maadili

Aidha ameiomba jamii kutoa ushirikiano kwa baraza la watoto ili liweze kufanya kazi yake bila vikwazo kwa maendeleo ya watoto ambao ni taifa tegemewa la kesho.

Bodi TSN yamsimamisha kazi Mhariri Mtendaji.

0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo jinsi gazeti linavyotengenezwa kutoka kwa mchapaji msaidizi wa magazeti ya serikali (TSN) Bw.Paul Kasele alipofanya ziara katika shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitembezwa kuonyeswa mazingira ya kampuni ya magazeti ya serikali(TSN) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni mhariri mtendaji wa kampuni hiyo ya magazeti ya serikali Bw.Gabriel Nderumaki ambaye amesimamishwa kazi kutokana na utendaji usiorizisha na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Prof Moses Warioba. Picha na Daudi Manongi.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo mhe Nape Nnauye akiongea na vyombo vya Habari kuhusu maagizo aliyoyatoa kwa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya serikali TSN ikiwemo sababu za wafanyakazi wengi kuacha kazi katika shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya magazeti ya serikali (TSN) Prof Moses Warioba(wa kwanza kushoto) akitoa tamko la kumsimamisha kazi Mhariri mtendaji wa kampuni ya magazeti ya serikali Bw.Gabriel Nderumaki(hayupo pichani) kutokana na utendaji usiorizisha.Wengine pichani ni wajumbe wa Bodi hiyo Dkt Evelyn Richard na Bw.Alfred Nchimbi
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea kampuni ya magazeti ya serikali TSN leo jijini Dar es Salaam.

BODI ya wakurugenzi wa magazeti ya Serikali,(TSN) imemsimashisha kazi Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo Bw Gabrieli Nderumaki kupisha uchunguzi kutokana na utendaji usioridhisha ndani ya kampuni hiyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Prof Moses Warioba amesema hatua za kumsimamisha kazi Mhariri Mtendaji huyo umetokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambapo nafasi yake itachukuliwa na Naibu Mhariri Bi Tumma Abdalah.

“Kumekuwa na mambo mengi yanayofanyika bila kufuata utaratibu ndani ya kampuni hii ikiwemo wafanyakazi kutoelewana na menejimenti katika kulipwa stahili zao, pamoja na wafanyakazi kupewa majukumu ambayo hawana uwezo wa kuyatekeleza”.Alisema Prof Warioba.

Aidha Prof Warioba ametengua uteuzi wa Bw Felix Mushi aliyekuwa Meneja mauzo na masoko katika kiwanda cha uzalishaji kwa kukosa sifa na utendaji mbovu uliopelekea kampuni kushuka katika uzalishaji.

Hatua hiyo ya kuwawajibisha watendaji hao imetokana na Ziara ya Mhe. Nape Nnauye Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika Kampuni hiyo ambapo pia hakuridhiswa na utendaji mbovu uliopelekea wafanyakazi 21 kuacha kazi.

“Nataka Bodi itafakari juu ya malalamiko yaliopo kwa wafanyakazi na wachukue hatua kabla mimi sijakutana na wafanyakazi hao wiki ijayo ili kujua mapungufu yako wapi.”Alisema Mhe Nape.Hata hivyo Bodi hiyo ya wakurugenzi inaendelea kutafuta namna ya kuboresha utendaji ndani ya kampuni ili iendane na kasi iliyopo katika uzalisahaji wa magazeti kwa kiwango kikubwa.

UKAGUZI WA SERIKALI KUU,IDARA,TAASISI MASHIRIKA YA UMMA HAUJAKAMILIKA -CAG.

0
0
 Naibu Mkazi Mkuu  wa Hesabu za Serikali , Idara  na Mashirika ya Umma,  Benjamin Mashauri, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu  ukaguzi  kwa Serikali Kuu, Mashirika ya mma na Serikali za Mitaa kwa mwaka 2014/15, Dar es Salaam, jana. Kulia ni  Sarah Reubeni, Msemaji wa ofisi ya  Taifa ya Ukaguzi. 

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),imesema kuwa ukaguzi wa mwaka 2014/2015  kwa serikali kuu haujakamilika hivyo kutumia rasimu hiyo ni makosa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Naibu Mkaguzi wa Mashirika ya Umma, Benjamin Mashauri amesema kuwa taarifa ya mkaguzi inakamilika ni baada ya kuiwasilisha kwa Rais kwa mujibu wa katiba inatakiwa iwasilishwe mwishoni mwa machi mwaka huu.

Mashauri amesema kuwa taarifa zinatolewa baadhi ya  vyombo vya habari na kunukuu ripoti ya CAG  kwa mwaka wa fedha 2014/2015 ni batili  kutokana na taarifa hiyo haijakamilika na wananchi wanatakiwa kupuuza taarifa hizo.

Amesema rasmu hiyo inayotumika baadhi  vyombo vya habari wakati taarifa hiyo haijakamilika na kukamilika kwake ni mara ya kuwasilishwa kwa Rais na kupeleka katika bunge na hapo inakuwa imekamilika kwa kutumia kwa ajili ya wananchi juu ya fedha ya umma ilivyotumika.

"Kuendelea kutumia rasmu hiyo wakati haijakamilika ni kupotosha watanzania na kukiuka maadili ya kiutendaji na taaluma yake kwa kuwapa taarifa zisizo na uhakika"amesema Mashauri.

Amesema kuwa ofisi hiyo itaendelea na kutekeleza majukumu yake yote kwa kuzingatia misingi na uwazi na uwajibikaji usiokiuka taratibu za kisheria katika kukusanya na kutumia rasilimali za umma.

WADAU WA FILAMU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTUNISHA MFUKO WA MAENDELEO YA FILAMU

0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na mdau wa filamu Bi.Khadija Seif (Didas) wakati alipomtembelea ofisini kwake kujadili jinsi gani ya kutunisha mfuko wa maendeleo ya filamu.Bi Khadija anategemea kuchangisha milioni 200 katika mfuko huo.mwingine pichani ni Bi.Joyce Fissoo ambae ni Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania.

mwanahabari Fred Mosha azikwa leo kwenye Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar

0
0
Sehemu ya waombolezaji, walioshiriki Mazishi ya mwanahabari wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa  Mtangazaji wa  Redio Tumaini, marehemu Fred Mosha makaburi ya Kinondoni baada ya ibada katika Kanisa la Katoliki  la Chang'ombe Parokia ya Mtakatifu Francis Xavier, Temeke, Dar es Salaam 
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Fred Mosha likiwekwa sawa tayari kwa Mazishi.
Ibada ya Mazishi ikiendelea kwenye Makaburi ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam jioni hii.

'Empty Space' contemporary art exhibition at The French Alliance of Dar es Salaam

0
0
Dear Art lovers, 
 It is a pleasure to announce 'Empty Space', a contemporary art exhibition of mix media, painting, engraving, drawing & photography. The opening event will take place at The French Alliance of Dar es Salaam, (Tanzania) on the Tuesday 5th of April at 6:30pm.

ZAIDI YA TRILIONI ZAKUSANYWA KWA MWEZI FEBRUARI - DKT.LIKWELILE

0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa wizara hiyo imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na katika kipindi cha mwezi Februari mwaka huu zimekusanywa zaidi ya Sh. trilioni 1 tofauti na mwanzo ambapo zilikuwa zkikusanywa Sh.bil 850. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Waziri wa Afya, Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee Mpoki Ulusubisya.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akifafanua kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam jinsi Mamlaka hiyo ilivyofanikiwa kukusanya mapato kutoka trilioni 1.2 kwa mwezi Disemba mpaka trilioni 1 na bilioni 79 kwa mwezi Januari na kwa mwezi Februari wanatarajia kukusanya trilioni 1.013 na tayari wamefikia nusu ya malengo waliyojiwekea.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknologia na Ufundi Tarishi Kibenga amesema Wizara yake itazitumia fedha walizopewa mwezi huu kulingana na malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Diploma na wanafunzi wa chuo kikuu. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata.
Katibu Mkuu Wizara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee akifafanua namna Wizara yake ilivyojipanga kuzitumia fedha walizopata mwezi huu ambapo amesema zitatumika kulingana na malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za mradi wa ujenzi wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Walimu wa shule za msingi binafsi za jijini Dar es Salaam jana wameanza mafunzo kuhusiana na mitaala mipya ya masomo

0
0
Na Mugishagwe Zablon

Walimu wa shule za msingi binafsi za jijini Dar es Salaam jana wameanza mafunzo kuhusiana na mitaala mipya ya masomo kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na serikali hivi karibuni ambayo sasa yanafanya elimu hiyo iwe hadi darasa la 10 badala ya la saba la awali.

Akizungumza  wakati wa kufungua mafunzo ya ufundishaji kwa walimu kwa kutumia mtaala ulioboreshwa kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na pili kwa shule binafsi, Kamishna wa Elimu katika Wizara ya Elimu, Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balalusesa alisema lengo ni kuboresha kiwango cha elimu nchini.

Kamishna huyo alisema mtaala huo uliofanyhiwa maboresho umeanza kutumika katika shule za msingi nchini na kinachofanyika hivi sasa ni mafunzo kwa walimu hao ambayo alisema kuwa ingawa yamechelewa lakini bado yanahitajika.

Alisema ingawa walimu wa shule za msingi za serikali wamepata mafunzo hayo lakini wale wa binafsi walikuwa bado na sasa ndio wakati wao lengo kuhakikisha kunakuwa na uwiano wa viwango vya elimu baina ya shule na pia kuwa na mtaala mmoja.

Kamishna huyo alibainisha kuwa licha ya mitaala hiyo ya la kwanza na la pili kukamilika pia imeandaliwa ambayo imetayarishwa kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili ili kukidhi mahitaji ya shule zote iwe za serikali au za binafsi.

Alisema pia kulingana na mabadiliko hayo, pia kutakuwa na mitihani ya kuwapima wanafunzi wa darasa la pili ili kuzuia uwezekano wa kuwa na darasa la tatu wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu ili kujua uwezo wa watoto kitaaluma na kuwasaidia wale ambao uwezo wao mdogo katika eneo hilo.

Pia vitabu vyote vya kiada kwa shule za msingi vitachapisha na kusambazwa na TIE “Msingi wa utungaji, uchapaji na usambazaji wa vitabu vya kiada kwa shule za msingi nchini unatokana na kauli ya Rais John Magufuli ya kutaka vitabu vya masomo msingi nchini kuchapwa na taasisi hiyo  ili kudhibiti upotoshaji na kuhuisha elimu nchini” alisema.

Profesa Balalusesa alisema kinachofanyika sasa sio kuandika mtaala mpya isipokuwa kuufanyia maboresho ule wa mwaka 2005 ili uendane na mabadiliko ya sasa ambayo yanataka elimu msingi iwe hadi darasa la 10 badala ya la saba

Alibainisha kuwa awali ulikamilika mtaala wa darasa la kwanza na pili na hivi karibuni wa la tatu na nne na itaendelea hivyo hadi kufikia kulikokusudiwa ambako ni kuwa na mtaala ambao utaunganisha elimu ya msingi na sekondari kabla ya kuelekea hatua zaidi.

Awali akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Ofisa Eimu Wilaya ya Ilala, Elizabeth Thomas alisema wilaya ya Ilala imeamua kuwashirikisha waimu wa sule binafsi pia kutokana na ukweli kuwa ni wadau wakubwa wa elimu hususan jijini Dar es Salaam.

 Ofisa Eimu Wilaya ya Ilala, Elizabeth Thomas akizungumza wakati wa semina ya mafunzo kwa walimu ya jinsi ya kufundisha kwa kutumia mtaala ulioboreshwa  kwa shule za msingi kutokana na mabadiliko ya sasa ambako wanafunzi watasoma hadi darasa la 10 badala ya la saba kama ilivyokuwa awali ambayo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wawekezaji Binafsi katika Elimu (TAPIA), Albert Katagira akizungumza akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo kwa walimu wa shule binafsi,  jinsi ya kufundisha kwa kutumia mtaala ulioboreshwa  wa shule za msingi kutokana na mabadiliko ya sasa ambako wanafunzi watasoma hadi darasa la 10 badala ya la saba, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 
 Walimu wa shule za sekondari za binafsi, wakifuatilia semina ya mafunzo kwa walimu jinsi ya kufundisha kwa kutumia mtaala ulioboreshwa  wa shule za msingi kutokana na mabadiliko ya sasa ambako wanafunzi watasoma hadi darasa la 10 badala ya la saba, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. 
Kamishna wa Elimu katika Wizara ya Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balalusesa akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo kwa walimu wa shule binafsi, jinsi ya kufundisha kwa kutumia mtaala ulioboreshwa  wa shule za msingi kutokana na mabadiliko ya sasa ambako wanafunzi watasoma hadi darasa la 10 badala ya la saba, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Picha zote na Mugishagwe Zablon

TMF OUTRECH TO JOURNALISTS IN DAR ES SALAAM

"EXCLUSIVE VIDEO: YAMOTO BAND - MAMA"

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAFURIKO IRINGA, APOKEA MISAADA YA MAAFA YA SH. MILIONI 86/-

0
0






 Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa akiwapa pole wanawake na watoto wakati alipotembelea makazi ya dharura  waliyojengewa na serikali katika kijiji cha Kasanga  wanapohifadhiwa waathirika wa mafuriko yaliyozikumba tarafa za Pawaga na Idodi , Iringa Februari 22, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua baadhi ya nyumba za dharura wanazoishi wananchi wa katika kijiji cha Kasanga baada ya maeneo yao kukumbwa na mafuriko kwenye tarafa za Pawaga na Idodi, Iringa  Februari 22, 2016. Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipokea taarifa ya msaada  kutoka kwa meneja uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mangele katika mkutano wa kuwapa pole wananchi wa tarafa za Pawaga na Idodi uliohutubiwa na Waziri Mkuu katika Kijiji cha Kasanga, Iringa Februari 22, 2016. Mfuko huo umetoa mabati 200 na saruji mifuko 200 vyote vikiwa na thamani ya sh. 6,600,000/=.
  Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa akiwapa pole kinamama na watoto wakati alipotembelea makazi ya dharura  waliyojengewa na serikali katika kijiji cha Kasanga  wanapohifadhiwa waathirika wa mafuriko yaliyozikumba tarafa za Pawaga na Idodi , Iringa Februari 22, 2016.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea misaada mbalimbali yenye thamani ya sh. milioni 85.88/- kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko kwenye vijiji vya kata ya Mlenge, tarafa ya Pawaga,  wilaya ya Iringa vijijini mkoa wa Iringa. 
Misaada hiyo imetolewa na wadau mbalimbali kutokana na mafuriko ambayo yalibomoa nyumba 82 katika kitongoji cha Kilala, kijiji cha Kisanga na kuwaacha wananchi wake bila makazi. 
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kasanga ambako alikwenda kukagua athari za mafuriko  na kuwapa pole wananchi hao leo mchana (Jumatatu, Februari 22, 2016), Waziri Mkuu aliwashukuru wadau wote waliojitolea kuwachangia watu waliopata maafa kutokana na mafuriko hayo.
Wadau waliotoa misaada hiyo ni Benki ya NMB mabati 500, mifuko ya saruji 500, kilo 820 za maharage, kilo 750 za unga wa mahindi na lita 250 za mafuta ya kupikia vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 20/-. Wengine ni Mfuko wa Pensheni wa PPF uliotoa mabati 200 na mifuko ya saruji 200  vyenye thamani ya sh. milioni 6.6/-.
Wengine ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) waliotoa mabati 200 na mifuko ya saruji 160 vyenye thamani ya sh. milioni 4.5/-; Kiwanda cha kusindika nyanya cha RedGold kimetoa mifuko ya saruji 100 na mabati 50 vyenye thamani ya sh. Milioni 3/-; mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Bi. Susan Chogisasa na wenzake wametoa mabati 150, mifuko 23 ya saruji, kilo 100 za  maharage, kilo 50 za chumvi na nguo mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 1.3/-.

Madiwani wa Iringa Vijijini walitoa sh. 380,000/-, Wabunge wa Viti Maalum kupitia CCM walitoa vifaa vya sh. Milioni 1.7/-; ofisi ya CCM Mkoa wametoa vifaa vya sh. milioni 6.1/-, Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Iringa,  Bw. Salim Abri aliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Iringa sh. milioni 5/- ili wanunue vyakula vya waliopatwa na maafa.
Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mbunge wa Isimani, Bw. William Lukuvi alitoa fedha taslim sh. milioni  20/- kati ya hizo sh. milioni  15 zikiwa ni zake na milioni 5/- ni za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Bw. George Simbachawene.  Pia alikabidhi seti 251 za mashuka zenye thamani ya sh. milioni 4/- zikiwa ni mchango kutoka Benki ya CRDB.

Waziri Lukuvi ambaye alishatoa mabati 250, aliahidi kuongeza mabati mengine 250 (yote yana thamani ya sh. milioni 8), pia alikabidhi sh. milioni 1.5/- kwa diwani wa Mlenge ili ziwasaidie kukodi gari la kukarabati barabara yao ambayo imeharibika sana kutokana na mafuriko hayo. 
Mapema, akitoa taarifa ya maafa kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Amina Masenza alisema jumla ya kaya 82 zilikosa makazi kutokana na mvua zilizonyesha Februari 12 na kusababisha mafuriko. Kabla ya hapo, kaya nyingine 75 zenye wakazi 377ziliathirika kutokana na mvua zilizoanza Februari 3, mwaka huu. 
Alisema miundombinu ya barabara na ya maji safi iliharibiwa vibaya na kusababisha hasara ya zaidi ya sh, milioni 250/-. Pia wakazi hao walikubwa na uginjwa wa kipindupindu kutokana na mto Mapogoro kufurika na kusomba baadhi ya vyoo vya wakazi hao. 
“Tangu Februari mosi, wamekkkwishapokea waginjwa wa kipindupinda 351 llakini walioko wodini hivi sasa ni wagonjwa 25 tu,“ alisema Mkuu huyo wa mkoa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 22, 2016.





Libeneke la MODEWJIBLOG lapata kwikwi ya kiufundi, kurudi hewani hivi punde..tupo pamoja

0
0
WADAU WA MTANDAO WA HABARI WA MODEWJIBLOG TUMEPATA TATIZO LA KWIKWI YA KIUFUNDI KUANZIA ASUBUHI YA LEO HIVYO TUNALIFANYIA KAZI HARAKA KWA KADIRI INAVYOWEZEKANA ILI TUWEZE KURUDI HEWANI.
TUNAOMBA RADHI KWA WADAU WETU  WOTE PAMOJA NA WATEMBELEAJI WETU POPOTE WALIPO KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA.
Endelea kuperuzi nasi wakati wote kwa habari mbalimbali: www.modewjiblog.com

IMETOLEWA NA UONGOZI WA MODEWJIBLOG.COM

TANZIA: MAMA WILLELMINA KASIMBALA AFARIKI DUNIA

0
0
Bw. Prosper  Manase Mwakale anasikitika kutangaza kifo cha mama yake mzazi,  Willelmina Kasimbala (pichani, kilichotokea Leo ghafla jijini Dar es Salaam. 


Maandalizi ya mazishi yanafanyika nyumbani Kwa marehemu kimara stop Over jijini Dar es salam. Habari ziwafikie ukoo wa Kasimbala , Rutataza, Na waliokuwa wafanyakazi wenzake Air Tanzania!



MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA WILLELMINA MAHALI PEMA PEPONI 
- AMEN

MCHAMBUZI WA MUZIKI MASHUHURI NCHINI ZOMBOKA AMLILIA MWANAHABARI MAHILI MAREHEMU FRED MOSHA

0
0
Waombolezaji wakiingiza jeneza lenye mwili wa aliyekuwa  Mtangazaji wa  Redio Tumaini, marehemu Fred Mosha katika Kanisa la Katoliki  la Chang'ombe Parokia ya Mtakatifu Francis Xavier, Temeke, Dar es Salaam  leo , kwa ajili ya kuombewa. Mazishi yalifanyika kwenye makaburi ya Kinondoni.

TEASER JOTO LA ASUBUHI JUMANNE FEBRUARY 23, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI LEO

MHE. RAIS JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA MABALOZI WA DRC NA NAMIBIA

0
0


Mhe. Balozi Mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini, Mhe. Balozi Jean Pierre Tshampanga Mutamba akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu tarehe 22 February, 2016. 


Rais Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa DRC mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.


Mhe. Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini, Mhe. Theresia Samaria akikabidhi Hati za Utambulisho kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu tarehe 22 February, 2016. 




Rais Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Namibia mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. 

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mhe. Balozi Mteule wa Namibia wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa na maafisa wa Ubalozi wa Namibia hapa Nchini. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA.




MAKALA YA SHERIA: KUPATA LESENI YA KUTAFUTA MADINI TANZANIA.

0
0
Na  Bashir  Yakub

1.LESENI  HUTOLEWA  KWA  NAMNA  MBILI.

Unapohitaji  leseni  ya  kutafuta madini  unapaswa  kujua  kuwa  leseni  hizi  hutafutwa  kwa  namna  mbili  tofauti. Kwanza  kwa  maombi  maalum  na  pili  kupitia  zabuni. Sheria  mpya  ya  madini  sheria  namba  14  ya  2010 ndiyo  kiini  cha  makala  haya.


2.LESENI  KWA  MAOMBI  MAALUM.

Kwa  maombi  maalum  ni  hatua  ya  kawaida  ya  kuomba  kama ambavyo  unaweza  kuomba  kazi  au  tenda  yoyote  ambayo haijatangazwa na  serikali. Hatua  hii  huja  baada  ya  mjasiriamali  kuliona  eneo  la  madini   na  kuamini  kuwa  anaweza  kuwa  sehemu  ya  biashara  ya  eneo  hilo. 

Maombi  hufanywa  katika  fomu  maalum  ambazo   hupatikana  kwa  kamishna  wa  madini.  Makamishna  wa  madini  hupatikana  hata  wilayani  au  mikoani  hivyo  inategemea  ni  sehemu  ipi unataka  kutafuta  hayo  madini.

 Kubwa  ni  kuwa  utatakiwa  kutumia  wilaya  au  mkoa  husika  katika  kupata  fomu   hiyo  kwa  ajili  ya  kutuma  hayo  maombi.


DIRA YA DUNIA JUMATATU 22.02.2016

Viewing all 109604 articles
Browse latest View live




Latest Images