Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110087 articles
Browse latest View live

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

$
0
0

Hospitali ya mkoa Tabora Kitete yazidiwa na wagonjwa kutokana na ukosefu wa huduma bora za afya katika baadhi ya wilaya za mkoa huo.https://youtu.be/UgnG1W5wLCM  


Rais wa Burundi Piere Nkurunzinza amemuhakikishia Rais Magufuli kuwa hali ya Burundi ni shwari huku akibainisha kupokea ugeni mkubwa wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bw. Ban Ki-moon.https://youtu.be/GfZxnTqJt-s  

Shule ya msingi Majimatitu iliyoko Mbagala wilayani Temeke inayokabiliwa na msongamano mkubwa wa wananfunzi imepata wafadhili watakao jenga madarasa 5 na shule mpya ya ghorofa.https://youtu.be/7WYPLzwY7hc  

Serikali yatakiwa kuchukua hatua madhubuti za kuzuia uhamaji holela wa wafugaji kutoka eneo moja kwenda jingine ili kuzuia migogoro kati ya wakulima na wafugaji isiyo ya lazima. https://youtu.be/FM-S4CH6X6E  

Kufuatia kufungiwa kwa chuo cha St. Joseph tawi la Songea, sintofahamu yatanda kwa wanafunzi wa chuo hicho campas ya Arusha na kupelekea wanafunzi wa chuo hicho kufanya mgomo kushinikiza uongozi wa chuo hicho kuwathibitishia kama chuo hicho hakitafungiwa. https://youtu.be/Wf1BGlDUpPw

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amhakikishia Rais John Magufuli kuwa hali ya nchini Burundi inaendelea vizuri;https://youtu.be/azoU02jZvfA  

Serikali ya Tanzania yasema itandelea kudumisha  ushirikiano wake na nchi za Uturuki, Ireland na Uswisi; https://youtu.be/8EnW3lRd3vY
  
Inaelezwa kuwa hali ya uchafu yarejea tena katika jiji la Dar es Salaam ikiwa imepita takribani miezi ya kampeni ya usafi iliyoendeshwa na Rais John Magufuli; https://youtu.be/a_RiO7GBkzw  

Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais Mhe. Seleman Jaffo  avitaka vituo vya afya mkoani Dodoma kukopa pesa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya vituo vya afya; https://youtu.be/XLJ4rMBMfYU   

Wanafunzi wa shule za misingi na sekondari mkoani Mara waanza kunufaika na mradi wa kujifunza masomo kwa njia ya teknolojia ya habari na mawasiliano TEHAMA; https://youtu.be/EcAnr04eZxc  

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam lafanikiwa kuwa kamata watuhumiwa mbali mbali wa ujambazi wa kutumia silaha;https://youtu.be/cZpl7KLZO7Q  

Inaelezwa kuwa kampuni ya Lithos Spices itanunua tani mia tano za viuongo toka nchini; https://youtu.be/Pcldm5wgkHQ  

Bodi ya wataalamu wa ununuzi wa ugavi nchini TSPTB yatunukiwa cheti cha ubora; https://youtu.be/dbiEWeI_s5Y  

Mfuko wa maendeleo nchi TASAF wagawa ruzuku ya shilingi milioni 26 kwa kaya masikini kwa wakazi wa Tandale jijini Dar es Salaam;https://youtu.be/HBhqFG_fcUs  

Inaelezwa kuwa maonesho ya siku nne ya viwango yanatarajiwa kuanza kesho jijini Dar es Salaam; https://youtu.be/4a3BU7hLc_w  

Rais wa shirikisho la soka nchini TFF, Jamal Malinzi azungumzia sakata la upangaji wa matokeo kwa  baadhi ya timu zinazoshiriki ligi daraja la kwanza; https://youtu.be/pFZ1TlT_f6o  

Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF laingia mkataba na shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Association KTA kwa ajili ya kuinua soka la wanawake nchini; https://youtu.be/41KdhMJ4SL8



Will you attend on 11 & 12 March?

INTRODUCING: SHEAR MODULAS x WISE MAN-MATUSI(official video)

DIRA YA DUNIA JUMANNE 23.02.2016

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA ZIMBABWE NCHINI MHE JUDITH KANGOMA-KAPIJIMPANGA LEO IKULU

$
0
0
Balozi wa Zimbabwe nchini Mhe Judith Kangoma-kapijimpanga akimsalimia kwa unyenyekevu wa wanawake wa Kiafrika Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam  Jumanne February 23, 2016

RAIS WA ZANZIBAR AKUTANA BALOZI MTEULE WA KUWAIT.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait Mahadhi Juma Maalim leo alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait Mahadhi Juma Maalim leo alipofika Ikulu Mjini Unguja kujitambulisha.
[Picha na Ikulu.]

TUME YA MIPANGO YATEMEBELEA SHIRIKA LA MAENDELEO YA VIWANDA VIDOGOVIDOGO (SIDO)

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO), Omar Jumanne Bakari (wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa timu ya wataalam kutoka Tume ya Mipango ikiongozwa na Bibi. Florence Mwanri Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kuhusu ufanisi wa mashine ya kutengenezea sabuni katika kiwanda kidogo cha sabuni ambazo soko lake linapatikana jijini Dar es Saalam na mikoa ya jirani.
 Viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa Bw. Abdallah Kayumbi (wa kwanza kulia) kuhusu uzalishaji wa vifaa vinavyotumika kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia upepo (wind Turbines).
 Viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango na SIDO wakiangalia mashine ya kuzalisha nyuzi kwa ajili ya kutengeneza nguo inavyofanya kazi katika kiwanda cha Fruitful Goshen, Matengenezo Textile. 
Picha na Tume ya Mipango.

SERIKALI NA AKDN WAJADILIANA KUBORESHA MKATABA WA USHIRIKIANO

$
0
0
Maafisa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika kikao cha pamoja na Taasisi ya Maendeleo ya Aga Khan (The Aga Khan Development Network- AKDN). Wa tatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine ambaye alifungua rasmi kikao hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz P. Mlima. Kushoto kwa Balozi Sokoine ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Baraka H. Luvanda ambaye aliongoza mazungumzo kwa upande wa Serikali ya Tanzania. Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kilipitia upya Mkataba wa Ushirikiano wa Kimaendeleo kati ya Serikali na AKDN ambao ulisainiwa mwaka 2001. 
Kiongozi wa Ujumbe wa Mtandao wa Maendeleo wa Agakhan Dkt. Shakif Sachedina wa kwanza kushoto ambaye aliongoza mazungumzo kwa upande wa AKDN akiwa na baadhi ya wajumbe wakifuatilia mazungumzo ya kikao. 
Sehemu nyingine ya wajumbe wa AKDN wakifuatilia kikao. 
Wajumbe wa Serikali ya Tanzania walioshiriki kikao hicho ambapo Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa ilikuwa mwenyeji. Ujumbe wa Serikali ulihusisha Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU); Mamlaka ya Mapato Tanzania; Ofisi ya Rais Ikulu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Wizara ya Sera na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu; Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 
Balozi Joseph Sokoine akiagana na wajumbe wa AKDN baada ya kukamilisha zoezi la ufunguzi wa kikao hicho. 

SEKRETARIATI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE, USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, KIKANDA NA KIMATAIFA

TAARIFA MUHIMU KWA UMMA

Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imetangaza nafasi kumi (10) za kazi kupitia mtandao wake www.eac.int tarehe 19/02/2016. Kati ya nafasi hizo, nafasi tano (5) ni za kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na nafasi tano (5) ni kutoka Tume ya Ushindani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (The EAC Competition Authority).

Maombi ya kazi hizo yanatakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo tarehe ya mwisho kuwasilisha maombi hayo kwa nafasi za Registrar, Deputy Registrar, Mergers and Acquisitions,Deputy Registrar, Monopolies and Cartels, Accounts Assistant na Senior Personal Secretary ni tarehe 13/03/2016. Kazi hizi ni za mkataba kwa kipindi cha miaka mitano (5) na kurudiwa mara moja kwa kipindi kingine cha miaka mitano kutegemea utendaji kazi wa mtumishi husika. Aidha tarehe ya mwisho ya kuwasilishwa maombi ya na nafasi za Accounts Assistant,Principal Research Fellow,Research Assistant, Senior Research Fellow na EAC Quality Management System (QMS) Focal Officer ni tarehe 18/03/2016. Nafasi hizi za mkataba kwa muda wa mwaka mmoja (1) na utarudiwa kutokana na utendaji kazi wa mtumishi pamoja na upatikanaji wa fedha.

Kwa maelekezo zaidi kuhusu utaratibu wa kuomba, kuwasilisha maombi na maelezo ya ziada tafadhali tembelea tovuti ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki : www.eac.int. au kupitia link; bofya hapa

Wizara inapenda kuwaarifu na kuwahamasisha Watanzania wenye sifa stahiki waweze kuomba kazi hizi ili kuongeza ushiriki na uwakilishi wa Tanzania katika Ajira za Jumuiya na hivyo kushiriki ipasavyo katika maamuzi mbalimbali yanayohusu nchi yetu katika Jumuiya.

Watanzania watakaopenda kuwasilisha maombi ya kazi hizo wawasiliane na Wizara hii kupitia Idara ya Utawala kwa maelekezo zaidi kabla hawajatuma maombi yao.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Februari 24, 2016.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkaribisha Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipomtembelea waziri Mkuu ofisini kwake Magogoni Dar es salaam kwamazungumzo ya kikazi 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiongea na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd alipofika ofisini kwa waziri Mkuu jijini Dar es salaam kwamazungumzo ya kikazi .
Picha na Chris Mfinanga

MTOTO APOTEA, ANATAFUTWA NA WAZAZI WAKE

$
0
0
Kijana Eric Filipi Mzee mwenye umri wa miaka 16 ametoroshwa na watu wasiojulikana nyumbani kwa Walezi wake Mr & Mrs Noel Ngallo Mbezi Beach, eneo la samaki wabichi karibu na hospitali ya Massana. Kwa taarifa tunaomba sana yeyote atakayemuona awasiliane kwa simu namba 0719 308383, 0754 308383, 0715 284951, 0754 284951 au kituo cha chochote cha polisi hususan Kawe na Osyterbay.

MAN CITY, DYNAMO KYIV KUKIPIGA LEO

$
0
0
Na Bakari Issa Madjeshi

Klabu ya Soka ya Manchester City ya nchini Uingereza leo itakuwa na kibarua kigumu cha kupambana na Klabu ya Dynamo Kyiv ya nchini Ukraine katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA CHAMPIONS LEAGUE).

Manchester City ikiwa chini ya Manuel Pellegrini itaingia katika kipute hicho ikiwa na kumbukumbu ya  kupoteza mchezo wake wa Kombe la FA dhidi ya Chelsea kwa kukubali kichapo cha mabao 5-1, siku ya Jumapili.
Hata hivyo,Kocha wa Kikosi hicho Pellegrini alitetea uamuzi wake wa kutowapanga wachezaji wake muhimu akiwa na haya yakusema ”Ilitubidi kufanya maamuzi magumu dhidi ya Chelsea lakini ndio uamuzi pekee tuliokuwa nao kwa wakati ule”

“Tulikuwa na wachezaji 13 kwa hiyo lilikuwa ni kusudi letu kuendelea katika michuano yote na hatukuweza kufanya hivyo”

“Kitu cha muhimu ni ufanisi wa wachezaji wetu muhimu. Ni dakika 90 za mwanzo za michezo miwili,chochote kitakachotokea ,sio mwisho wa mchezo wa mkondo wa kwanza”,alieleza  Pellegrini

Pia, Pellegrini atamtumia mlinzi wa kushoto, Eliaquim Mangala alierejea uwanjani baada ya kuwa majeruhi tangu Januari 6 ya mwaka huu,wakati huohuo Kocha huyo atawakosa Winga Kevin de Bruyne na Jesus Navas,viungo Samir Nasri na Fabian Delph na Mshambuliaji Wilfred Bony.
Kwa upande wa Dynamo Kyiv ambayo haikucheza mchezo wowote wa kiushindani tangu ilipokumbana na Maccabi Tel Aviv katika hatua ya makundi ya Ligi hiyo ya Mabingwa Ulaya,Desemba 9 mwaka jana.

Hata hivyo,Kocha wa Kikosi hicho cha Ukraine, Sergei Rebrov anahofu ya kumkosa winga wake machachari, Andriy Yarmolenko ambaye alikua anasumbuliwa na maumivu ya goti aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Maccabi

Je? tuone ndani ya dakika 90 nani atacheka na nani atalia...

TWO TANZANIAN BOOM TOWNS FOR OIL AND GAS INVESTMENT

$
0
0
Are you seeking where to invest in Tanzanian oil and gas sector?
Do you wonder which town is best to invest in Tanzanian oil and gas sector?
Don’t worries.What if I told you some Tanzanian towns are booming thanks to natural gas discovery?
And these gas discoveries make some towns in Tanzania offering enormous investment opportunities to make health payoff
If you’re looking where to invest for the next coming month or year in Tanzanian oil and gas sector here are 2 hotspots for investment that I would explain.
1:Mtwara
Is rapidly becoming hub region for business with increasing population marketplace.
The immense discovery of natural gas offers huge potential rewards.And many foreign investors has been attracted to the region.

Ever ask yourself why African billionaire Dangote choose to invest in Mtwara.The logic simple. He has already eyeing opportunities in the region.
With Mtwara port plus good infrastructure and logistics, Mtwara is the hottest spot for establishing  vocational training institution recruitment firms because there many clients in the area.

However, Mtwara is the better place for building training institution related to oil and gas.
Like vocational training institution to help get local technicians which are in the dire demand in oil and gas sector.
2:Lindi
With little gas production in Songo songo field since 2004, plus plan to build the Liquefied natural gas plant (LNG) in the area on the horizon, would make Lindi potential market for business.
Because people should travel in this area. There would be significant demand in real estate, hotels and transportation

Final Words
In the last decades, Mtwara and Lindi have appeared as sleeping regions. But the discovery of natural gas has been transforming the regions in the hub town for investment In the country.

Hussein Boffu
Graduate in Petroleum Geoscience
 Hussen.boffu@Tanzaniapetroleum.com
0655 37 65 43/0689 95 57 11

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA KATIBU MTENDAJI WA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Richard Sezibera Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine Rais Magufuli amepokea taarifa ya maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 02 Machi, 2016 Katika Jiji la Arusha, Nchini Tanzania. 

Rais Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi tano wanachama ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. 

Akizungumza mara baada ya mazungumzo hayo Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Dkt. Richard Sezibera, amesema maandalizi kuhusiana na mkutano huo yanakwenda vizuri. 

Amesema pamoja na mambo mengine mkutano huo, utajadili masuala kadhaa yakiwemo mpango wa kuanzisha viwanda vya magari ndani ya Jumuiya ili kupunguza uingizaji wa magari kutoka nje ya nchi na Marais kuzindua pasi ya kusafiria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Kuhusu hali ya Jumuiya, Dkt. Sezibera amesema inaendelea vizuri na ametaja baadhi ya mambo ambayo yamefanyika kuwa ni kutiwa saini kwa mkataba wa umoja wa forodha, makubaliano ya soko la pamoja na makubaliano ya sarafu moja. 

Mengine ni kuwepo kwa mazungumzo kuhusu uimarishaji wa miundombinu kama vile reli na umeme ndani ya Jumuiya, na mazungumzo kuhusu umoja wa kisiasa. 

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga, amesema Tanzania ikiwa ni mwenyeji wa kikao hicho ipo tayari kupokea ugeni na kwamba pamoja na kufanyika kwa kikao hicho, marais wa Tanzania na Kenya watafungua barabara inayounganisha Tanzania na Kenya katika Mpaka wa Holili na kutakuwa na shughuli ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha pamoja cha mpakani kwa ajili ya kuwezesha upitaji wa mizigo na watu yaani "One Stop Boarder Post" 

Gerson Msigwa 
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU. 
Dar es salaam.
24 Februari, 2016.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU MGENI RASMI KATIKA TAMASHA LA PAMOJA TUNAFANIKISHA.

$
0
0
Na M wandishi wetu.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan (Pichani) mgeni rasmi Tamasha la Pamoja Tunafanikisha litakaloandaliwa na kampuni ya Trumark katika kusherehekea maadhimisho ya siku ya mwanamke Dunia.

Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo ambaye ndie mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo amesema mama Samia pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya wanawake watakutana siku ya Machi tano ili kusheherekea mafanikio ya mwanamke pamoja na kuziangalia changamoto zinazomzunguka na kuzibadili kuwa fursa.

“Kwa kweli tamasha hili litakuwa la aina yake ikizingatiwa hii ni mara ya kwanza kwa nchi yetu kuwa na makamu wa Rais mwanamke tangu kupatikana kwa uhuru, hii itatoa fursa kwa wanawake kuamini kuwa tunaweza kutimiza ndoto zetu kwenye safari ya mafanikio”alisema Agnes.

Agnes amesema Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inalenga katika kuwaleta pamoja wanawake na wanaume na kutoa ahadi zao za kuwa mabalozi wa kuharakisha harakati za usawa wa kijinsia katika maeneo yanayowazunguka.

Ameongeza kuwa tamasha hilo litakuwa jukwaa la kukutanisha wanawake kutoka fani na kada tofauti ili kutengeneza mtandao ambao utakuwa chachu muhimu kwa ustawi wao ambapo tamasha hilo litaenda sambamba na watoa mada kutoka nyanja mbalimbali kama vile uchumi na fedha, ujasiliamali na masuala ya afya maonyesho ya biashara ya bidhaa za ubinifu kutoka kwa wanawake, chakula cha usiku na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii wa hapa nchini akiwemo Elias Barnaba na bendi yake ya Clasicc ,mkogwe wa muziki wa taarab Mama Patricia Hillary na Misoji Mikwabi ambao wataongozwa na mchekeshanji maarufu MC Pilipili.

Agnes aliwashkuru wadau mbalimbali wakiwemo King Solomon Hall, Valleys Spring, Mummys Exclusive Shop, Flexible Entertainment, Channel Ten na Magic Fm. Pia aliwakaribisha wadau wote kuungana pamoja katika siku hii muhimu.

ZAKIA MEGHJI AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI MOI JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)  Zakia Meghji (wa kwanza kulia) akifungua Baraza la tatu la Wafanyakazi Taasisi hiyo sambamba na utoaji vteti kwa wafanyakazi bora na pesa taslimu kwa kila mfanyakazi, Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa NIMR. wa katikati ni  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi  Dkt, Othman Kiloloma na anayefatia ni Katibu wa Baraza la wafanyakazi hilo Dkt. Clement Mugisha
 (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

Goodluck Gosbert kuzindua albamu Tamasha la Pasaka

$
0
0
MUIMBAJI nguli wa muziki wa Injili jijini Mwanza, Goodluck Gosbert anatarajia kuzindua albamu yake ya Ip[o siku yenye nyimbo nane kwenye Tamasha la Pasaka jijini Mwanza linalotarajia kufanyika Machi 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Alex Msama  tamasha hilo linatarajia kuanza Machi 26 mkoani Geita kwenye ukumbvi wa Desire kabla ya kumalizia uwanja wa Taifa Wilayani Kahama ambalo litafanyika Machi 28.

Msama alisema albamu hiyo ni moto wa kuotea mbali, hivyo wakazi wa mikao ya Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ambalo litashi8rikisha waimbajki mbalimbali wa Tanzania.Msama alizitaja nyimbo zilizoko kwenye albamu hiyo ni pamoja na Ipo siku, Acha waambiane, Haohao, Nisamehe, Pendo langu, Ndiwe Mungu, Moyo tulia na Surprise.Aidha Msama alitumia fursa hiyo kueleza kwamba viingilio katika tamashja hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na watoto shilingi 2000.

"Tamasha la Pasaka ni sehemu ya kusaidia wenye uhitaji maalum ambao ni pamoja na walemavu, yatima na wajane ambao wanahitaji msaada kutoka kwa wadau kama kampuni ya Msama Promotions," alisema Msama.

Msama aliwataja waimbaji waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Bonny Mwaitege, Upendo Nkone, Jesca BM Honore, Jennifer Mgendi, Sifael Mwabuka, Joshua Mlelwa, Martha Baraka, Christopher Mwahangila, Anastazia Mukabwa, Kwaya ya AIC Makongoro, Kwaya ya Wakorintho wapili, Faustine Munishi, Solomon Mukubwa.

MSAJILI WA HAZINA AKAGUA UJENZI WA MRADI WA ECO RESIDENCE UNAOJENGWA NA NHC KINONDONI HANANASIFU

$
0
0
1
Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru  akishuka kwenye gari wakati alipowasili kwenye mradi wa Eco Residence ulioko Kinondoni Hananasifu unaojengwa na shirika la Nyumba la Taifa NHC huku akiongozwa na Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu tayari kwa ukaguzi wa jengo hilo ambalo nyumba zake zote zimeshauzwa na linatarajiwa kukabidhiwa hivi karibuni kwa Shirika hilo.

Akizungumza na Vyombo vya habari mara baada ya ukaguzi wa jeno hilo Msajiri wa Hazina Bw. Lawrence Mafuru amepongeza uongozi wa NHC kwa kazi kubwa wanayoifanya ambapo wamefanikiwa kujenga majengo yenye tahami ya shilingi Trilioni 3.5 kutoka umiliki wa mwanzo ambapo kulikuwa na majengo yenye thamani ya shilingi trilioni 1.
Mkopo uliotumika kugharamia ujenzi wa majengo hayo mapya kutoka mabenki mbalimbali ni jumla ya shilingi Bilioni 300 ambazo kiasi cha shilingi Bilioni 100 zimeshalipwa tayari katika mabenki hayo na kiasi cha shilingi bilioni 200 zinaendelea kulipwa
Naye Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu amesema shirika hilo linao mpango mkubwa wa ujenzi wa nyumba 500 za gharama nafuu kwa ajili ya watanzania wenye kipato cha chini ambazo zitaanza kujengwa mwaka huu huko Luguruni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam..(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru  akimsikiliza Violet Mafuwe Msanifu wa majengo kutoka kampuni ya CPI Iternational ambaye pia ni Meneja Mradi wa Eco Residence wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.
3
 Msajili wa Hazina, Bw. Lawrence Mafuru akimuuliza jambo Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu mambo mbalimbali kuhusu miradi ya shirika hilo wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.

MICHUANO YA KOMBE LA FA: YANGA YAIPIGISHA KWATA JKT MLALE KWA BAO 2-1

$
0
0
Mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya akimtoka beke wa JKT Mlale, Lucas Chapanga katika mchezo wa Kombe la FA uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.  Yanga ilishinda 2-1. Kwa matokeo hayo Yanga imeingia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. (Picha na Habari Mseto Blog)
Lucas Chapanga akichuana na  Geofrey Mwashiuya.

Salum Telela akichuana na Said Ngapa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KLABU YA KIMATAIFA LIONS CLUB INTERNATIONAL YATOA MSAADA WA MADAWATI YA CHUMA SHINYANGA

$
0
0
Leo Februari 24,2016 ,Chama cha Kimataifa kinachotoa misaada mbalimbali ya Kijamii cha Lions Club International chenye makao yake makuu nchini Marekani kimetoa msaada wa madawati 165 yenye thamani ya shilingi milioni 18 katika shule ya msingi Town na Mwenge zilizopo katika manispaa ya Shinyanga ili kumaliza changamoto ya wanafunzi kukaa chini.

Pichani viongozi wa wilaya ya Shinyanga,wazazi na maafisa kutoka Lions Club International wakiongozwa na Gavana wa Lions Club katika nchi ya Tanzania, Uganda na Sudani ya Kusini bwana Hyderali Gangji wakiwa katika shule ya msingi Town...Madawati hayo 165 yametolewa na Lions Club ya mkoa wa Mwanza.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama  Malunde ametuletea picha 30 kilichojiri mwanzo hadi mwisho.Gavana wa Lions Club International katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji alisema wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali mkoani Shinyanga ambapo mwaka jana walitoa msaada wa chakula kwa wahanga wa mvua ya Mwakata wilayani Kahama,pia chakula katika kituo cha walemavu wa ngozi cha Buhangija,kutoa madawati katika shule ya msingi Town na Mwenge  Miongoni mwa madawati ya chuma 165 yaliyotolewa na Lions Club International katika shule ya msingi Town na Mwenge katika manispaa ya Shinyanga.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 
Viewing all 110087 articles
Browse latest View live




Latest Images