Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Dkt. Kalemani aagiza wadaiwa sugu wa umeme ‘washughulikiwe’

$
0
0
Na Veronica Simba - Nzega

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuwachukulia hatua kali ikiwemo kuwafikisha Mahakamani wadaiwa wake sugu hususan Kampuni na watu binafsi.

Dkt Kalemani alitoa agizo hilo jana wilayani Nzega, akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Tabora kukagua miradi mbalimbali ya sekta za nishati na madini inayotekelezwa chini ya Wizara yake.

Alisema, Serikali ilikwishaanza kulipa madeni yake kwa TANESCO, hivyo hakuna budi Kampuni na watu binafsi wanaodaiwa na Shirika hilo kulipa madeni yao pia.

“Meneja wa TANESCO, Sheria ya Umeme inakuruhusu kuwachukulia hatua wadaiwa waliogoma kulipa madeni yao. Wapeleke Mahakamani.” Katika kuhakikisha agizo lake linapewa uzito unaostahili, Naibu Waziri aliwaagiza Mameneja wa TANESCO wa Mkoa wa Tabora kumpatia orodha ya majina ya wale wote wanaodaiwa na Shirika hilo mkoani humo ifikapo kesho Ijumaa, Februari 19 mwaka huu.

“Mnipatie orodha hiyo ifikapo Ijumaa, iwe ni kampuni ya mtu mzito au mtu mwingine yeyote,” alisisitiza. Aliongeza kuwa, ni lazima hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya waliokaidi kulipa kwani kitendo hicho ni kuihujumu TANESCO.

Naibu Waziri alisema Serikali imedhamiria kukusanya mapato yote stahiki kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wake, hivyo alimwambia Meneja wa TANESCO Mkoa wa Tabora kuwa asipochukua hatua kama alivyomwagiza, hatasita kumuwajibisha yeye mwenyewe.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kalemani ameagiza kuwa Makandarasi wote wanaojihusisha na shughuli za kutandaza waya na vifaa vingine kwa ajili ya kuunganisha umeme majumbani na katika majengo mbalimbali (wiring), kujisajili katika Ofisi za Wilaya za TANESCO.

Alisema, agizo hilo linafuatia kuwepo na wimbi la matapeli maarufu kama vishoka ambao hufanya kazi hiyo ya kuunganisha umeme pasipo kuwa na utaalam husika.

Aidha, aliwataka wananchi kutofautisha kazi zinazofanywa na TANESCO na zile zinazofanywa na Makandarasi binafsi katika zoezi zima la kuunganisha umeme.

Alisema, kazi ya TANESCO ni kusimika nguzo za umeme na kuunganisha Waya unaoingiza umeme katika nyumba au jengo husika lakini si kazi ya Shirika hilo kufunga Waya na Vifaa vya umeme ndani ya nyumba au jengo.

“Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika sana kwamba wanatapeliwa kwa kutozwa fedha nyingi na/au kufungiwa vifaa vya umeme visivyo na ubora kwenye nyumba zao. Mara nyingi lawama hizo huelekezwa TANESCO.”

Dkt Kalemani alisema, ndiyo maana Serikali kupitia Wizara yake, imeamua kuwa Makandarasi wote wanaojihusisha na shughuli hizo wasajiliwe katika Ofisi za TANESCO za Wilaya ili wafahamike na hivyo kuwaepushia wananchi adha ya kutapeliwa.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ishihimulwa, Kata ya Bukumbi, wilaya ya Nzega hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora.
Nyaya za umeme katika Kijiji cha Mambali, Wilaya ya Nzega. Kijiji hiki ni miongoni mwa vijiji vilivyounganishiwa umeme kupitia Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Awamu ya Pili ya REA.

Prof. Muhongo na Wawekezaji

$
0
0
Waziri wa nishati na madini, Prof.Sospeter Muhongo amekuwa na vikao na wawekezaji zaidi ya 300 kutoka pande zote za dunia ikiwemo tanzania amnao wanahitaji kuwekeza katika sekta ya nishati. Katika kikao cha mwisho kilicho fanyika ferbruari 18 amewaaeleza wawekezaji hao kuwa kwa sasa Serikali kwa sasa inatumia mwezi mmoja tangua kuanza mazungumzo hadi kufukia muafaka wa kumruhusu mwekezaji huo kuwekeza au laa tofauti na ilivyokuwa hapo awali zoezi hilo lilikuwa likitumia miezi sita na zaidi. Prof. Muhongo amesema watanzania walionesha nia ya kuwekeza kutumia fursa hiyo na kwa wale waliongia ubia na wageni kutoka nje wahahikishe wanatimiza lengo walilolikusudia kwa kuiwezesha Tanzania kupata umeme wa uhakika ili kutimiza azma ya Srikali ya kufikia uchumi wa kati mwaka 2025. aidha amewatoa hofu wawekezaji na kuwahidi kuwa Serikali itawaunga mkono kwa kila hatua watakayokuwa wamepia.​ 

Mjasiriamali wa Bucha la Nyama Akabidhiwa Vifaa vya kisasa na Airtel FURSA

$
0
0
 Baada ya kufanya semina ya ujasiriamali na kutoa elimu ya kuboresha mtaji kwa vijana takribani vijana 300 mkoani Morogoro, Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel kupitia Mpango wa Airtel Fursa  imeendeleza na dhamira yake ya kuboresha maisha ya watanzania na kuwawezesha kuzifikia ndoto zao.
Kwa kuthibitisha dhamira  Airtel FURSA imemkabidhi mjasiliamali  wa bucha la nyama  wa  mji mdogo wa Ngerengere, wilayani Morogoro, Hashim Mikidadi , vifaa vya kisasa vinavyotumika katika kazi yake, jokofu,  pamoja nakukarabati bucha,  vyenye jumla ya thamani ya shilingi  milioni tisa.
Hashim Mikidadi ni kijana mwenye umri wa miaka 23 aliyejikita katika shughuli za ujasiliama wakati akiendelea na elimu ya Sekondari ili kukidhi mahitaji ya shule na chakula pamoja na kusaidia wazazi wake ambao ni wazee. Akiwa Katika umri wa miaka 17 alianza kuweka akiba ya Ths. 300,000 iliyopatikana kutokana na kazi ya kufyatua na kuuza matofali.  Aliamua kuzitumia pesa hizo na kuwekeza katika kilimo cha Ufuta ambapo baada ya  misimu miwili ya kilimo , Hashimu alifanikiwa kupata shilingi laki Tsh 800,000 ambazo alianzisha biashara ya bucha ambayo anaendelea nayo hadi sasa.
Akiongea kwa furaha mara baada ya kukabithiwa vifaa hivyoMjasiriamali  Mikidadi , aliishukuru mungu kwa kupata msaada huu kupitia  Airtel Fursa na kusema “ nilianza biashara nikiwa na mtaji mdogo ambao haukidhi mahitaji ya biashara yangu. Sikuwa na vifaa vya kuniwezesha kufanya biashara yangu kwa ufanisi lakini leo Airtel kupitia Airtel FURSA imeniwezesha na sasa naamini ntawawezesha kuendesha biashara hii na kuisadia familia yangu pamoja na jamii inayonizunguka”
“ napenda kutoa shukrani pia  kwa wafanyakazi wa Airtel kwa kushiriki katika  ukarabati mkubwa wa bucha langu kwani uwepo wa vifaa hivi  vya kisasa katika bucha yangu ni  kuhamasisha wateja wangu na wale ambao si  wateja wangu wavutiwe kupata huduma  kutoka katika hii” alisema Mikidadi.
Akiongea wakati wa kumkabithi vifaa hivyo, Meneja wa Huduma za Jamii wa  Airtel Tanzania, Hawa Bayumi alisema Airtel inaijali jamii inayowazunguka na kuzielewa changamoto nyingi ambazo vijana wamekuwa wakikutana zao ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira na ukosefu wa mitaji wa kuanzisha biashara zao  na mpango wa Airtel Fursa ni njia moja wapo  ya kubadirisha maisha yao.
Leo unayofuraha kumpatia msaada wenye thamani ya shilingi milioni 9 ikiwa vifaa, ni pamoja  na gharama za ukarabati mkubwa uliofanyika kwenye  bucha hiyo  ambayo  kwa sasa imekuwani ya viwango vya juu katika mji wa Ngeregere .
 “Airtel FURSA”  ni mradi endelevu unaowalenga vijana nchi nzima kwa kuwapatia vifaa  ,mafunzo ya biashara na mafunzo mbalimbali kupitia mtandao ili kufikia malengo yao. Kutuma maombi tuma ujumbe mfupi kwenda namba 15626 ikiwa na taarifa zifatazo Jina, umri, aina ya biashara unayoifanya, mahali na namba za simu. Unaweza pia kutuma maombi yako kwa kupitia barua pepe ya: 
airtelfursa@tz.airtel.com. Au tembelea tovuti yetu ya  www.airtel.com  na ujaze fomu yako ya maombi

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA TAASISI YA SEKTA BINAFSI NCHINI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania  (TPSF) ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

Serikali yasema kukamilika kwa daraja la Kigamboni kutasaidia kupungua kwa msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam;https://youtu.be/GC9Lc3qke7k

Mkuu wa mkoa wa Arusha amuagiza mkuregenzi wa halmashauri ya Karatu kumsimamisha mtendaji wa wa kijiji Dofa kwa tuhuma ya ubadhilifu wa fedha za umma; https://youtu.be/xvKArzLIaWU

Serikali mkoani Iringa yaanza kubaini makazi ya kudumu kwa ajili ya wananchi waliokumbwa na mafuriko;https://youtu.be/6Nhw14N2gKw

Mifuko ya hifadhi ya jamii kwa nchi za Afrika Mashariki yatakiwa kuwainua kiuchumi watu waliojiajiri katika sekta zisizo rasmi;https://youtu.be/5NSqRN6mpr4

Benki ya Stanbic Tanzania yailipa benki kuu Tanzania faini ya bilioni tatu kwa tuhuma ya kujihusisha katika malipo ya kampuni ya EGMA kinyume na taratibu za kibenki; https://youtu.be/_xALcw23MFw

Rais John Magufuli aigiza mamlaka ya mapato nchini TRA kukamata kazi za wasanii zisizo na alama maalum ya TRA;https://youtu.be/SA5RfSTiiwU

Bodi ya filamu nchini yazitaka kampuni zinazohusika na utengenezaji wa filamu nchini kutumia watalaamu wazawa katika kazi zao ili kukuza wigo wa ajira kwa vijana wa kitanzania;https://youtu.be/U25Lnb-lYho
Waziri wa nishati Prof.Sospeter Muhongo awataka wawekezaji wa ndani kushirikiana na wakezaji wa kimataifa kuwekeza katika nishati ya umeme; https://youtu.be/zikgy8AzQ8o

Baadhi ya shule za misingi mkoani Dodoma zafanya  vibaya katika mitihani ya taifa kutokana na kusitishwa kwa mpango wa ugawaji wa vyakula shuleni; https://youtu.be/UkSAp7N6qMA

Jeshi la polisi nchini latakiwa kujenga uhusiano mzuri na wananchi ili kusaidia upatikanaji wa taarifa zenye kuhatarisha hali ya usalama nchini; https://youtu.be/YrwWWNVlr1k  

Baraza la mitihani Tanzania NECTA latangaza matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2015; https://youtu.be/bxPrUzfMLeA
Umoja wa wafanyabiashara wa mafuta nchini waiomba EWURA kutazama upya upangaji wa bei ya nishati ya mafuta mikoani;https://youtu.be/aHs1blNtves
Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga alitaka jeshi la polisi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kujiepusha na vitendo vya rushwa pamoja na tuhuma za uonevu dhidi ya raia.https://youtu.be/S1y6lnKzekE

Waendesha pikipiki maarufu kama boda boda mkoani Kilimanjaro watakiwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kufichua wahalifu kwani baadhi ya wahalifu ni wateja wao.https://youtu.be/ei3hyzLRt_M

Halmashauri ya wilaya ya Kilwa yapiga marufuku uvuvi haramu wa kutumia mabomu unaofanywa katika kisiwa cha Nyuni kilichoko katika kata ya Songosongo. https://youtu.be/_ZGz5zhTEz8

Serikali ya Tanzania inatarajia kuzindua program ya kieletroniki ya masuala ya ardhi kuanzia upangaji, upimaji hadi utolewaji wa hati ndani ya miaka 5. https://youtu.be/lqnv5b4sywo

Wanakijiji wa kijiji cha Mhunze mkoani Simiyu wamkataa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Peter Marando kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za ruzuku za elimu mashuleni.https://youtu.be/RqKjZTtn2wM

Shirika la umeme nchini TANESCO limewahakikishia wateja wake kuwa kukamilika kwa vituo 3 vya kufua umeme mwishoni mwa mwezi wa 6 mwaka huu vitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la kukatika umeme katika mikoa ya Pwani na Dar es salaam.https://youtu.be/jiSHQfJxs3Y

Wasanii kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Filamu nchini

$
0
0
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ndogo ya wasanii iliyoundwa kwa ajili ya kufuatilia uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa DIDAS Entertainment Bi. Khadija Seif (katikati) ambaye pia ndiye mratibu wa zoezi hilo kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu, akifafanua jambo wakati wa kikao cha Kamati ndogo ya wasanii iliyoundwa kwa ajili ya kufuatilia uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
 Msanii Single Mtambalike (Richie) akielezea jambo wakati wa kikao cha Kamati ndogo ya wasanii iliyoundwa kwa ajili ya kufuatilia uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ndogo iliyoundwa kwa ajili ya kufuatilia uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Filamu Tanzania wakiwa ndani ya kikao leo jijini Dar es Salaam. Picha na: Kitengo cha Mawasiliano, WHUSM.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 18.02.2016

VIJANA NCHINI WASHAURIWA KUWA NA MOYO WA KUJITOLEA KABLA YA KUPATA AJIRA RASMI

$
0
0
Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.

Vijana nchini hususani wanaomaliza masomo ya vyuo wametakiwa kujijengea tabia ya kufanya kazi zinazokuwepo pindi wamalizapo masomo yao na isiwe mpaka kazi inayoanza na maslahi makubwa.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika warsha iliyozikutanisha taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa kujitolea za vijana.

Bi Ledama, alisema kumekuwepo na kundi kubwa la vijana ambao wamekuwa wakihitimu masomo yao lakini hawajishughulishi na kazi yoyote lakini kuna wanaweza kutumia fursa zilizopo hata kwa kuanza kwa kujitolea na kupitia kwenye kazi hiyo akajifungulia milango ya mafanikio.

Ameongeza kuwa, Vijana wengi wamekuwa wakihitaji kazi ambazo zina maslahi makubwa pindi tu wanapoanza kazi kwa kipindi kifupi wapate maisha mazuri bila kutambua kuwa wanahitaji kufanya kazi kwa bidii na maisha mazuri ndiyo yanafuata.

“Ukitaka maisha mazuri lazima ufanye kazi kwa bidii sio unataka uanze kazi upange nyumba ya vyumba vitatu na ipo sehemu nzuri, ununue gari Mark X na mengine mazuri lakini lazima ufanye kwanza kazi,

“Vijana mnatakiwa kutambua kuwa ajira ni ngumu kupatikana hata kwa kuanza kufanya kazi kwa kujitolea bila malipo unaweza kuwa na juhudi na mwisho wa siku unakuwa na maisha mazuri,” alieleza Bi Usia Nkhoma Ledama.

Mwenyekitiwa BMT amteua Mohamed Kiganja kuwa Katibu Mtendaji

$
0
0
Na Lilian Lundo – Maelezo

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania Deonis Malinzi amemteua Mohamed Kiganja kuwa Katibu Mtendaji mpya wa baraza hilo baada ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo Bw. Henry Lihaya kutenguliwa.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti Malinzi ameeleza kuwa uteuzi huo umekuja baada ya kuona mapungufu ya utendaji kwa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.“Baraza la Michezo Tanzania limefikia maamuzi haya baada ya kutoridhishwa na utendaji wa Bw. Lihaya na hivyo Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye kufanya maamuzi ya kumtengua” alisema Bw. Malinzi

Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya BMT namba 12 ya mwaka 1967 kifungu namba 5(1) ambacho kinampa mamlaka Mwenyekiti wa BMT kuteua Katibu Mtendaji baada ya kupata idhini ya Waziri mwenye dhamana.

Aidha kabla ya uteuzi huo Kiganja alikuwani Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuanzia mwaka 2015 mpaka uteuzi wake ulivyofanyika.

Pia aliwahi kufanya kazi kama Afisa Mwandamizi Michezo wa Baraza la Michezo Tanzania na Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi wa Waziri Mkuu, anashahada ya kwanza ya Elimu katika masuala ya Michezo na Utamaduni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Airtel yachezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Airtel Mkwanjika.

$
0
0

 Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akizungumza na wateja wakati wa kuchezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Airtel Mkwanjika ambapo wateja 40 walichaguliwa kuwa washindi wa promosheni hiyo. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha,
Bakari Majid na Afisa masoko wa Airtel Nasoro Abdulbakari (kulia).
Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akimkabithi mshindi wa Airtel Mkwanjika Diana Samwel na mkazi wa Dar es Saalam pesa taslimu mara baada ya kujinyakulia shilingi 480,000 kupitia boksi la Airtel Mkwanjika. 

·Zaidi ya wateja 212 wajishindia pesa taslimi
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Airtel Mkwanjika nakupata washindi 40 ambapo kila mmoja atajishindia pesa taslimu hadi shilingi milioni 1 kupitia boksi la Airtel Mkwanjika

Promosheni ya Airtel Mkwanjika ilizinduliwa mwishoni mwa mwezi Disemba na kuwazawadia wateja wanne watakaojiunga na vifurushi vya yatosha au kuongeza muda wa maongezi kupitia vocha au Airtel Money kila siku. Jumla ya washindi 28 walipatikana kupitia droo kila wiki na kuzawadiwa pesa taslimu.

Akiongea wakati wa kuchezesha droo ya mwisho, Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema” Leo tumefikia mwisho wa promosheni yetu ya Airtel Mkwanjika , promosheni ambayo imeweza kuwazawadia wateja zaidi ya 212

nchi nzima. Tunajisikia furaha kuona mwitikio mkubwa kutoka kwa wateja wetu na tunapenda kuwahakikishia kuwa Airtel itaendelea kutoa huduma bora za kibunifu zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu yanayoendelea kubadilika na kukua kila siku na huku tukiendelea kuwazawadia kupitia promosheni kama hii ya Airtel Mkwanjika”

“Tunaamini kupitia Airtel Mkwanjika tumetoa zawadi ambazo zimewawezesha wateja wetu kukabiliana na changamoto walizonazo na kuwasaidia kuongeza mitaji ya biashara zao na kuongeza ufanisi katika shughuli zao mbalimbali za kiuchumi na za kijamii. Tunaamini washindi wetu watakuwa ni ushuhuda tosha wa namna gani Airtel kupitia promosheni hii imeweza kubadili maisha yao na ya jamii zao kwa ujumla. Aliongeza Matinde

Promosheni ya Airtel Mkwanjika imefikia mwisho, Airtel bado itaendelea kuwawezesha washindi kutoka katika mikoa mbalimbali nchini ambao bado hawajaingia kwenye boksi la Airtel Mkwanjika kupata nafasi ya kufanya hivyo ili kuweza kujiokotea pesa na kukabithiwa zawadi zao.

DDCA YACHIMBA VISIMA 52 NA MABWAWA 3 SIKU 100 ZA RAIS DKT. MAGUFULI.

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa Bw. Egwaga Nungu akiongea na waandishi wa habari (Hawapo Pichani) na kuwaeleza kuhusu Mafanikio waliyoyapata Katika Siku 100 za uongozi wa Rais John Pombe Magufuli ikiwamo kuchimba visima 52 na Mabwana 3 sehemu mbalimbali nchini, wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Saalam, Kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari-MAELEZO Bi. Lilian Lundo
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
WAKALA wa Uchimbaji Visima na Mabwawa (DDCA) wamefanikiwa kuchimba visima 52 na Mabwana 3 sehemu mbalimbali nchini Katika Siku 100 za uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano kutoka Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa Bw. Egwaga Nungu wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.

“Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa (DDCA) katika kipindi cha kuanzia Novemba hadi februari tumeweza kufanikiwa kuchimba visima 52 zitakavyowezesha kupataikana kwa maji safi kwa watanzania katika maeneo mbalimbali na pia wakala umefanikiwa kuchimba mabwawa 3” Alisema Bw. Egwaga.

Akiongelea Matarajio na mipango ya wakala Katika mwaka wa fedha 2015/2016 Bw. Egwaga amesema kuwa wakala unatarajia kuchimba visima 400, kupima wingi wa maji katika maeneo 420, kusafisha visima 500, pumping installation visima 400 na kukarabati visima 100.


Katika kipindi cha miaka kumi wakala wamefanikiwa kuongeza cha maji kwa jamii kwa wastani wa 53,823m3 za maji kwa siku na kufikia wastani wa asilimia 86 na kuwawezesha wananchi kupata vyanzo vya maji safi na salama kupitia uchimbaji wa visima.

BEI YA MADAFU LEO.

KESHO MTOTO HATUMWI DUKANI MTANANGE KATI YA YANGA NA SIMBA.

$
0
0
Vituo vinavyotumika kuuza tiketi za mchezo huo ni ofisi za TFF – Karume, Buguruni Oilcom, Ubungo Oilcom, Uwanja wa Taifa Temeke, Mavuno House - Posta, Dar Live Mbagala, Breakpoint – Kinondoni, Kidongo Chekundu – Mnazi Mmmoja, Mwenge na Kivukoni Ferry.
Kiingilio cha juu cha mchezo huo ni shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa viti vya rangi ya machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.
Milango ya Uwanja wa Taifa itafunguliwa kuanzia saa 5 kamili asubuhi, huku barabara ya Chang,ombe ikifungwa kuanzia asubuhi, na magari maalumu yenye stika maalumu ndiyo yatakayoruhushiwa kuingia eneo la uwanja wa Taifa kwa kupitia barabara ya Mandela na uwanja wa Uhuru.
Upande wa ulinzi, Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama watakuwepo kuhakikisha usalama wa wapenzi wa mpira watakaokuja kushuhudi mchezo huo, vitu kama silaha, vilevi, mabegi na vitu vyenye ncha havitaruhusiwa kuingia ndani ya uwanja.
Shirikisho linawaomba wapenzi, wadau na washabiki wa mpira wa miguu nchini kununua tiketi katika magari ya kuuzia tiketi katika vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizo halali kwa mchezo huo.
Mchezo huo utachezeshwa na mwaamuzi Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na mwamuzi Josephat Bulali (Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha) wote wakiwa wakiwa waaamuzi wenye beji za FIFA, mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) na Kamisaa wa mchezo huo atakua Khalid Bitebo (Mwanza). 

WAFANYABIASHARA WA MBAO NA MAGOGO KANDA YA KUSINI WAKUTANA MJINI LINDI KUJADILI FURSA NA CHANGAMOTO ZA BIASHARA YA MAZAO YA MISITU

$
0
0
Ili kueneza shughuli za Usimamizi Shirikishi wa Misitu Nchini Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) pamoja na washirika wake; Shirika la Kuhifadhi Mpingo na Maendeleo-MCDI, Mtandao wa Jamii wa Usiamizi wa Misitu Tanzania-MJUMITA, Shirika la WWF Tanzania pamoja na Kampeni ya Mama Misitu.

Lengo la Warsha hiyo ya wafanyabiashara ni pamoja na kuongeza nguvu katika jitihada za kuimarisha mijadala kwa wafanyabiashara wa mbao/magogo juu ya mambo muhimu yanayosibu biashara ya mazao ya misitu ikiwemo kuoanisha baadhi ya Changamoto na Mafanikio

Warsha hiyo imelenga katika kuwasilisha fursa zilizopo za kufanya uvunaji katika misitu ya hifadhi za vijiji ikilinganishwa na uvunaji katika misitu ya wazi ikiwa pamoja na kutoa ufafanuzi wa mambo ya kitaalam yahusuyo upimaji na ukadiriaji wa ujazo wa mbao.

Sambamba na utekelezaji wa shughuli za mradi wa washirika WWF Tanzania na Jumuiko la Maliasili Tanzania unaohusu mambo ya uwekezaji katika misitu na ardhi (unaofadhiliwa na WWF Finland kupitia ofisi za WWF Tanzania) pamoja na shughuli za Kampeni ya Mama Misitu (inayofadhiliwa na Serikali ya Finland). Miradi hii miwili ndiyo itakayogharimia warsha hiyo.

Warsha Hiyo Imehusisha wafanyabiashara toka wilaya za Liwale,Tunduru,Masasi,Nachingwea,Ruangwa,Kilwa ,Lindi na Rufiji
Mshauri wa Kampeni ya Mama Misitu,Bw Cassian Sianga akipitia baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na wafanya biashara wa Mazao ya Misitu katika warsha inayoendela Mjini Lindi
Meneja wa Wakala wa Misitu(TFS)Kanda ya Kusini akitoa mada kuhusiana na Taratibu na sheria za Uvunaji wa mazao ya Misitu

MAGUGU MAJI YATISHIA HUDUMA ZA USAFIRI ENEO LA KAMANGA FERRY JIJINI MWANZA.

$
0
0
Vita ya Kupambaza na Uwepo wa Magugu Maji katika Maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria, bado haijazaa matunda Chanya. 

SUALA la kupambana na magugu maji katika ziwa hilo bado ni changamoto, licha ya kuwepo kwa Miradi mbalimbali ikiwemo ile ya Uhifadhi wa Mazingira ya Bonde la Ziwa Victoria (LIVEMPT I & II) iliyolenga kuokoa uwepo wa Ziwa Victoria ambayo pia ililenga kupambana na magugu maji.

Mara kadhaa huduma za usafirishaji katika Kivuko cha Busisi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, zimekuwa zikitatizwa na uwepo wa Magugu maji ambayo hutanda katika eneo la ferry la kivuko.

Usumbufu kama huo unahofiwa huenda ukajitokeza katika eneo la Kamanga Ferry Jijini Mwanza, baada ya Magugu Maji kugonga hodi na kuanza kutanda katika eneo hilo.

Kumbuka Magugu maji yanaweza kutambaa kutoka eneo moja hadi jingine kulingana na upepo unavyovuma na yanaweza kuleta athari ya usafirishaji majini ikiwa chombo cha usafiri (Meli/Ferry) kitanasa katika Magugu maji.

Suala kubwa ni kuhakikisha mapambazo zaidi dhidi ya magugu maji yanaendelea ikiwemo kuvitumia vikundi vya Kusimamia Rasilimali za Uvuvi katika Ziwa Victoria (Beach Management Unit-BMU) ambavyo mara moja moja pale vinapowezeshwa, vimekuwa vikifanya shughuli ya kutoa magugu maji Ziwani.

Hata hivyo jitihada za vikundi hivyo zimekuwa zikikwama kuleta suluhisho maana magugu maji yanapotolewa majini, ni vyema yakachomwa moto jambo ambalo huwa ni nadra kufanyika na matokeo yake magugu maji hayo hurudi ziwani kwa njia moja ama nyingine, ikiwemo kwa njia ya shughuli za kilimo katika maeneo ya kandokando mwa ziwa Victoria.
Shughuli za Kupambana na Magugu Maji zikifanyika eneo la Nera Jijini Mwanza mwishoni mwa Mwaka jana
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group.

Mbunge wa Chalinze atoa Vitabu 3438 kwa Shule za Msingi na Sekondari jimboni kwake

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akikabidhi vitabu 3438 vya shule za Msingi 105 na Sekondari 17 vyenye thamani ya Shilingi Milioni 68,760,000, kwa Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Mkoani Pwani. Makabidhiani hayo yamefanyika mapema leo asubuhi kwenye Shule ya Sekondari ya Mdaula.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akizungumza mara baada ya kukabidhi vitabu hivyo. kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mdaula, Mwalimu Komba.
Mratibu wa Taasisi ya Kulea Village, Bw. Kombo (wa pili kulia) akizungumza machache wakati wa hafla ya kukabidhiwa Vitabu kwa Shule za Msingi na Sekondari, vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete (mwenye skafu shingoni). 

UKARABATI WA BOMBA LA DAWASCO ENEO LA MAKONGO WAENDELEA

$
0
0
Mafundi wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam(Dawasco) wakiwa na Wakandarasi kutoka kampuni ya Sino Hydro wakikarabati bomba la Maji lenye inchi 54, lililokuwa likivuja maeneo ya Makongo jeshini na kusababisha kukosekana kwa huduma ya Maji maeneo mbalimbali ya jiji kwa Saa 36, huduma hiyo inatarajia kurejea katika hali yake ya kawaida leo ambapo bomba hilo ni tegemeo la kuleta Maji kutoka Ruvu chini na kupeleka katika matenki yaliyopo Chuo kikuu cha Ardhi, Jijini Dar es Salaam.

DKT. KOLIMBA AKUTANA NA UJUMBE WA BUNGE LA SWEDEN

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb) akiukaribisha ujumbe wa wabunge wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Bunge la Sweden walipomtembelea leo ofisini kwake.Wabunge hao wapo nchini kwa madhumuni ya kutathmini na kukagua miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Sweden kwa Tanzania ili kubaini utaratibu bora zaidi wa kusaidia Tanzania katika kipindi kijacho. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb) (kulia) akizungumza na kiongozi wa ujumbe huo, Mhe. Kenneth G. Forslund anbaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Sweden. Katika mazungumzo hayo, Dkt. Kolimba alishukuru Serikali ya Sweden kwa misaada yake katika sekta ya elimu ya juu na Bajeti ya Maendeleo. Aidha, Mhe. Naibu Waziri alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden hususan katika masuala ya kiuchumi na biashara. 

Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine, Bi. Tunsume Mwangolombe, Bw. Adam Issara na Bw. Ally Kondo.

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA UJUMBE WA WABUNGE KUTOKA MAREKANI NA SWEDEN

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wabunge wa Bunge la Marekani (Congress) waliomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Febuari, 2016.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Wabunge wa Bunge la Marekani (Congress) waliomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge akiagana na Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Sweden mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake jijini Dar es salaam.

Ukataji wa Tikect kwa ajili ya kuangalia mechi Uwanja wa Taifa kwa njia ya Elekroniki waiva

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza katika kikao baina yake na uongozi kutoka TFF na BMT ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujadili suala la matumizi ya mashine za Elekroniki katika kukusanya mapato yatokanayo na mauzo ya Tiketi wakati wa mechi kwenye Uwanja wa Taifa.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Dioniz Malinzi na kulia ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
Katibu Mkuu wa TFF Celestine Mwesiga (kushoto) na Muhasibu Mwandamizi wa TFF Bw. Daniel Msangi wakifuatilia kwa makini wakati wa kikao baina yao na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) akizungumza katika kikao baina ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (katikati) na uongozi kutoka TFF na BMT leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja akizungumza wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (katikati) na uongozi kutoka TFF na BMT leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura ((wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa TFF, BMT na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mara baada ya kumaliza wa kikao kilichofanyika ofisinii kwake leo jijini Dar es Salaam.Kikao hicho kimefanyika ili ya kujadili suala la matumizi ya mashine za Elekroniki katika kukusanya mapato yatokanayo na mauzo ya Tiketi wakati wa mechi kwenye uwanja wa Taifa. Picha na: Frank Shija, WHUSM
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images