Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1128 | 1129 | (Page 1130) | 1131 | 1132 | .... | 3285 | newer

  0 0

  . Washabiki wawili wa soka nchini, watapata nafasi kushuhudia bila malipo mechi ya ligi kuu ya soka ya nchini Hispania baina ya Barcelona na Deportivo la Coruna itakayofanyika April mwaka huu, nchini humo kupitia promosheni ya pamoja baina ya tigo, LigaBBVA na Azam Media.

  Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. 
  Meneja Masoko na Mauzo wa Azam Media, Mgope Kiwanga alisema washindi watapatikana kipindi hiki cha promosheni  ambayo imeanza rasmi jana 17 Februari na itaendelea hadi Machi mwaka huu 2016.

  Kiwanga alisema kinachotakiwa ni anayetaka kuwania nafasi hiyo kuhakikisha kimoja kati ya kifurushi vikuu vya Azam televisheni kipo hewani iwapo ni cha Pure, Plus au Play na anakuwa ameingia katiika droo moja kwa moja na wateja wa tigo pesa nao watakuwa na fursa hiyo pia wakinunua kifurushi kupitia tigopesa.

  Meneja huyo alisema kampuni yake itagharamia malazi, chakula na pesa ya kujikimu kwa washindi hao kipindi chote ambacho watakuwa nchini humo pia watazamaji wa Azam televisheni watakua na fursa ya kushiriki kwa kupiga simu kabla ya mechi na wakati wa mapumziko.

  “Mteja akipiga simu ataulizwa maswali na akijibu vizuri anakuwa katika nafasi ya kushinda tuzo hiyo ya kwenda kuangalia mechi hiyo” alisema na kuongeza kuwa kuna zawadi zingine nyingi ambazo zitatolewa kwa washindi.

  Alisema zawadi hizo ni kutoka LigaBBVA ambazo ni t-shirt za Barcelona, mipira na zingine na meneja wa Promosheni wa Tigopesa, Mary Rutta alisema hiyo ni fursa muhimu kwa wateja wa kampuni hiyo kuweza kunufaika na fursa zinazojitokeza.

  Rutta alisema wateja wa kampuni hiyo wana fursa nzuri ya kuweza kujishindia nafasi hizo kupitia ununuzi wa vifurushi vya Azam kupitia tigopesa na alibainisha kuwa kinachofanyika ni kuwawezesha wateja Zaidi ya milioni 5 nchini kunufaika na huduma za kidigitali.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Rhys Torrington akizungumza kuhusiana na promosheni ya Kampuni ya Azam Televisheni kuwasafirisha bila malipo kwenda nchini Hispania washabiki wa soka jijini Dar es Salaam jana. Wa kwanza kulia ni Meneja Mauzo na Masoko Wa Azam, Mgope Kiwanga na Meneja Promosheni wa Tigo, Mary Rutta. Picha na Mugishagwe Zablon

  Meneja Mauzo na Masoko Wa Azam, Mgope akizungumza kuhusiana na promosheni ya Kampuni ya Azam Televisheni kuwasafirisha bila malipo kwenda nchini Hispania washabiki wa soka nchini, wakati wa mkutano na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Rhys Torrington na Meneja Mauzo na Masoko Wa Azam, Mgope Kiwanga. Picha na Mugishagwe Zablon


  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipata maelezo kuhusu michoro ya viwanja vya ndani vinavyotarajiwa kujengwa pembeni mwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kutoka wa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ( watatu kulshoto) na katibu Mkuu wake Profesa Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) wakati alipozungumza na wadau wa michezo kwenye uwanja wa Taifa leo Februari 17, 2016
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa michezo nchini kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo Februari 17, 2016.
   Baadhi ya wapenzi na viongozi wa michezo nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza na wadau wa michezo nchini kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam leo Februari 17, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa michezo nchini baada ya kuzungumza ao kwenye uwanja wa taifa jijini dar es salaam leo Februari 17, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na wadau wa michezo nchini baada ya kuzungumza nao kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Februari 17, 2016

  0 0

   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni alipowasili katika shule ya Msingi ya Mbuyuni, Oysterbay, jijini Dar es salaam kwa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 
   Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Oysterbay, jijini Dar es salaam katika sherehe hiyo fupi ya Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisikiliza risala toka kwa mwanafunzi wa shule ya Msingi ya Mbuyuni Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi ya saa toka kwa mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo. 
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wasiojiweza katika shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu
  KWAYA mbili za nyimbo za Injili zimethibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa kuanzia Machi 26 hadi 28.

  Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama tamasha hilo linaanza Geita katika ukumbi wa Desire ambalo litafanyika Machi 26, Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba litafanyika Machi 27 na Kahama Machi 28 kwenye uwanja wa Taifa.

  Msama alizitaja kwaya hizo zinazotarajia kupanda jukwaani katika mikoa hiyo ni pamoja na AIC Makongoro Vijana ya jijini Mwanza sambamba na Wakorintho Wapili ya Mafinga ya Iringa.

  Msama alitoa wito kwa wakazi wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ambalo malengo yake ni kusaidia wenye uhitaji maalum ambao ni walemavu, yatima na wajane.

  “Nawaomba wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi ili tuwasaidie wenzetu wenye uhitaji maalum ambao ili wafikie malengo wanahitaji kutoka kwetu,” alisema Msama.

  Aidha Msama alisema bado wanaendelea kufanya mawasiliano na waimbaji mbalimbali wa Tanzania ambao kwa pamoja watafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.

  0 0
 • 02/18/16--02:12: BEI YA MADAFU HII LEO.


 • 0 0

  Akizungumza na baadhi ya wakurugenzi na mameneja wa benki hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya miaka 20 ya utendaji wa benki hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Charles Kimei alisema wamefanikiwa kuifanya taasisi hiyo kuwa kinara wa kutoa huduma bora.

  Alisema amana za wateja wa benki hiyo zimeongezeka zaidi ya mara 100 kutoka sh. bilioni 40 walizoanza nazo mwaka 1996 hadi sh. trilioni 4.2 iliyokuwepo Desemba 31 mwaka jana.“Safari ya miaka 20 ilikuwa na misukosuko ikiwemo kupata hasara y ash. bilioni 1.8 mwaka 1997 lakini tunajivunia kusema tumepita salama na sasa tumekuwa taasisi bora ya fedha hapa Tanzania.

  “Idadi ya bidhaa zetu, wateja na hata thamani ya benki pia imeongezeka… tunao waajiriwa 2,682 wenye nidhamu,” alisema Dk. Kimei huku akibainisha kwamba katika kampeni hizo watawekeza zaidi kwenye elimu.Alisema maadhimisho ya kuelekea kilele cha miaka 20 ya CRDB yatakayohitimishwa Juni mwaka huu yamepewa kauli mbiu ya ‘Benki inayokua na kuboresha maisha ya watu.
  Mkurugenzi wa Masoko, Utafitti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sherehe za miaka 20 ya benki ya utendaji wa benki hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sherehe za miaka 20 ya benki hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
  Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Dk. Charles Kimei (kushoto).

  0 0

  Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper Ltd (TSN) wakimskiliza Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kuzungumzia changamoto mbali mbali za kampuni hiyo.kutoka kulia ni Dkt Consolatha Ishebabi,Dkt Evelyn Richard na Bw,Alfred Nchimbi.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizungumza jambo na mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper Ltd (TSN) Bw.Prof Moses Warioba (kushoto).
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (wa kwanza kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspaper Ltd (TSN) kuhusu changamoto mbalimbali za kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwa katibu mkuu ni Prof Moses Warioba ambaye ni mwenyekiti wa bodi hiyo.
  Picha na Daudi Manongi-WHUSM.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa michezo nchini kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Februari 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya wapenzi na viongozi wa michezo nchini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza na wadau wa michezo nchini kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Februari 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipata maelezo kuhusu michoro ya viwanja vya ndani vinavyotarajiwa kujengwa pembeni mwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kutoka wa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ( watatu kulshoto) na katibu Mkuu wake Profesa Elisante Ole Gabriel (wapili kushoto) wakati alipozungumza na wadau wa michezo kwenye uwanja wa taifa Februari 17, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa michezo nchini baada ya kuzungumza ao kwenye uwanja wa taifa jijini dar es salaam Februari 17, 2016.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wadau wa michezo nchini baada ya kuzungumza nao kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Februari 17, 2016.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi cheti katika Mkutano wa Nane wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika Mashariki na Kati. Makamu wa Rais amefungua rasmi mkutano huo leo katika Ukumbi wa Benki Kuu.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kulia) akiteta jambo na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama katika ufunguzi wa Mkutano wa nane wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika Mashariki na Kati. Mkutano huo wa siku mbili umefunguliwa leo na unafanyika jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na Vyombo mbalimbali vya Habari mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa nane wa Mifuko ya Jamii Afrika Mashariki na Kati. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Halima Maulid Salum akifungua warsha ya uzinduzi wa Mradi wa Afya bora ya mama na mtoto katika Hoteli ya Mzson Shangani Mjini Zanzibar.
   Mkurugenzi Idara ya Kinga na elimu ya afya Dkt. Mohd Dahoma akizungumza na washiriki waliohudhuria katika warsha ya uzinduzi wa mradi wa Afya bora ya Mama na Mtoto katika ukumbi wa Hoteli ya mazson Shangani mjini Zanzibar.
   Baadhi ya washiriki katika uzinduzi wa Mradi wa Afya ya mama na mtoto uliofanyika Hoteli ya Mzson Shangani wakifuatilia uzinduzi huo.
  PICHA NA ABDALLA OMARA/MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

   Rais John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
  Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na kundi la sanaa la Tanzania One Theatre baada ya kuongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016
  Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wataalamu wa TEHAMA baada ya  kuongea  na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016
  Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo Fleva  baada ya  kuongea  na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
  Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo Movie   baada ya  kuongea  na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.
  Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na sehemu ya wanahabari  aliokuwa nao katika kampeni baada ya kuongea  na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016
  Rais John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na watendaji kutoka CCM Makao Makuu  baada ya  kuongea  na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Bharti Airtel ya India, Sunil Bharti Mittal kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaaam Februari 18, 2016.
  Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Airtel Afrika, Christian Defaria (kulia) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Bharti Airtel ya India, Sunil Bharti Mittal (katikati) kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaaam Februari 18, 2016. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One, Joyce Mhaville, (kulia) akiwafafanulia jambo wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakati walipotembelea kituo hicho  kwa ajili ya kujifunza  mbalimbali na kuelendeleza Mahusiano mazuri ya kibiashara,Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, Meneja Uhusiano Matina Nkurlu,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia  wakati  uongozi wa kampuni hiyo ulipotembelea  ITV na Redio One jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara kituoni hapo.
   Maofisa wa Vodacom Tanzania ,wakiongozwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ian Ferrao(wapili kushoto) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa  Rosalynn Mworia (aliyekaa)   Meneja Uhusiano Matina Nkurlu, (kushoto)na Meneja biashara,Grace Lyon  wakioneshwa jinsi taarifa ya habari inavyoenda hewani na  na mtangaziji wa kituo cha ITV Abdallah Mwaipaya, Wakati  Uongozi wa kampuni hiyo ulipotembelea kituo hicho  jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara kituoni hapo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(wapili kulia)  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia ( kushoto)  na Kaimu mkuu wa Masoko na Mawasiliano,Yvonne Maruma wakimsikliza kwa makini  Mhariri wa  ITV na Redio One,Stephen  Chuwa alipokuwa akiwafafanulia jambo kuhusiana na utendaji wa wa kituo hicho,Wakati  Uongozi wa kampuni hiyo ulipotembelea  kituo hicho  jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara kituoni hapo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kushoto) akimsikiliza matangazaji wa kituo cha EATV, Deo alipoongoza  Uongozi wa kampuni yake kutembelea  kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na kituo hicho na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara  kituni hapo jana.
   Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao na   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia , wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa  East Africa Redio na EATV,wakati  Uongozi huo ulipotembelea  kituo hicho  jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na kituo hicho na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara  kituni hapo jana.

  0 0

  KUMEKUWA na hoja iliyowasilishwa na mtu mmoja kwenye mitandao ya kijamii kuhusu matumizi ya NAPTHA kwa kurusharusha mwanga kidogo kwa uzalishaji wa hii NAPTHA.

   NAPTHA huzalishwa kwa wingi kutokana na usafishaji mafuta ghafi (crude oil) ambapo, crude oil hutiwa katika kinu cha moto au joto kali inayopelekea kuzalisha mafuta na gesi tofauti katika layers tofauti.

  Layers hizi hutofautisha mafuta na gesi tofauti yaani PETROL, KEROSENE (mafuta ya taa) na DIESEL mpaka chini kabisa kunapatikana LAMI.

  Hali kadhalika gesi aina tofauti kama butane, propane, nakadhalika hupatikana hapa, nivyema pia  na kuwajuza Watanzania kuwa hii gesi ya kupikia majumbani, iitwayo Liquefid Petroleum Gas au LPG, inayosambazwa katika mitungi kama ORYX, MIHAN, CAM GAS, LAKE GAS nakadhalika hutokana na mchanganyiko wa PROPANE NA BUTANE kupata LPG. 

  Huingizwa nchini kutoka nchi zinazozalisha mafuta na kusambazwa hapa nchini katika mitungi ya gesi ya kilo 3, 6, 15, 38, na hadi mitungi mikubwa ya kilo 500, 1000 nakadhalika.

  Sasa tofauti za mafuta haya huja kwenye parameters tofauti kama boiling points, flammability rates, viscocity, density nakadhalika nakadhalika.
  Refineries tofauti duniani huenda wakazalisha bidhaa Fulani na Fulani zaidi kulingana na mikakati yao , mfano huenda akaseti kupata petro zaidi.

  Ama ikirudi kwenye NAPTHA, hii imeegemea zaidi katika PETROLI na tofauti zinakuja kwenye parameters kama ilivyitajwa hapo juu. 

  Kutoka uchimbaji wa mafuta ghafi (crude oil) na usafishaji wa mafuta yaani petroleum refinery, ifahamike kwa Watanzania refinery tuliyokuwa nayo ya TIPER ambayo kwa leo ni mali ya kampuni ya ORYX. Refinery hii ilitumika miaka ya nyuma kusafisha mafuta, kwa maana mafuta ghafi yaliingizwa nchini, na uzalishaji au usafishaji wa mafuta kama nilivyoeleza awali ulifanyika hapa nchini. Refinery hii ilikufa kifo cha mende, ingawaje ki uchumi ilikuwa na faida.
                                                                                            
  Katika uchimbaji wa NATURAL GAS, pia hupitia hatua kama ya hapo juu, ila hapa huingizwa kwenye mtungi mkubwa kwanza wa High Pressure Separator, ambapo GAS ASILIA huchujwa, ikielea juu kwa sababu ya wepesi wake (density), na chini yake kubaki CONDENSATE. 

  Hii condensate, hukamuliwa maji (water) na kutolewa na ilibaki kuingizwa tena katika Low Pressure Separator. Hali kadhalika hupatikana maji na mabaki kuwa aina tofauti za kinachofanana na mafuta ghafi, Zao hili sasa, huwekwa katika treatment tofauti kupata kitu gani mzalishaji anataka….ambapo, pamoja na mengineyo hupatikana NAPTHA.
  Hii NAPTHA sasa hupitia pia michakato tofauti kama vile kuiondolea sulfur na treatments nyinginezo zinazoweza kukupatia PETROL.
  Vile vile, kutokana na NAPTHA, tunaweza pata SOLVENTS, sabuni za maji au cleaning fluids, diluents (nimekosa neno la Kiswahili hapa) za rangi, varnish, asphalt, pamoja na bidhaa kama solvents katika makampuni ya mpira (rubber) , viberiti vya gesi, hata mali ghafi katika dry cleaners na kutengeneza mbolea.
  Sasa basi, Watanzania tunapotezwa sana katika propaganda kuliko kuelewa vitu, na kuchangamkia Fursa Kuliko kumshambulia OILCOM, hapa naona fursa nyingi, nyingi, na nyingi ambazo OILCOM aliona baadhi, na sio kwa U-HASI BALI KWA U- CHANYA.
  Zipo sheria za OSHA zinazosimamia athari au maelekezo ya viwango vya matumizi ya NAPTHA. Na sheria nyingine nyingi katika hili.

  TPDC ilitengaza tenda ya kuuza CONDESATE. Wadau mbalimbali waliomba na aliyeshinda akapewa. 

  0 0

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo  akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo.

  Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
   WANAUME wameshauriwa kushiriki na kufurahia mafanikio ya wanawake kwa kuwa na usawa wa kijinsia na kusaidia kufanikisha malengo na ndoto za wanawake wanaowazunguka katika maeneo yao.


  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo wakati akizungumza na wandishi wetu jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa wanaume wana nafasi kubwa ya kumsaidia mwanamke kujikwamua katika nyanja za kiuchumi, kiafya hata kijamii kwani ndiye baba, kaka, au kiongozi wa familia.


  Agnes amesema Kuwa kutambua umuhimu wa mwanaume katika suala hili, Trumark katika kuadhimisha siku ya wanawake dunianin wameandaa tamasha la Pamoja Tunafanikisha ambalo litahusisha wanaume ili nao waelewe kuwa wana umuhimu mkubwa katika maisha ya mama, dada, Binti na wake zao.


  Tamasha la Pamoja Tunafanikisha litafanyika Machi 5, mwaka huu katika Ukumbi wa King Solomoni, eneo la Namanga jijini Dar es salaam ambapo wanaume na wanawake wataungana kusherekea mafanikio ya wanawake na  kutambua changamoto nyingi zinazomkabili mwanamke,  katika kuadhimisha siku hiyo  kutakuwa na  wadau mbalimbali  kutoka nyanja tofauti ili kujadiliana namna ya kuzikabili changamoto hizo  na kuzifanya  kuwa fursa na pia kuwapongeza wanawake ambao wameonyesha njia kwa kujikwamua kiuchumi, jamii na kiafya.


  Kampuni ya Trumark imekua ikiadhimisha siku ya wanawake Kwa takribani miaka mitano sasa na tumekuwa na mafanikio makubwa kwani washiriki wengi wamekuwa na mrejesho chanya, nakuongeza mtandao katika shuguli zao mbalimbali.


  Agnes amesema maadhimisho yataambatana na burudani kutoka kwa wasanii wa bendi ya mapacha watatu pamoja na chakula cha usiku katika kusheherekea mafanikio ya wanawake,pia anawakaribisha  wanawake pamoja na wanaume kujitokeza kwa wingi ili maadhimisho hayo yalete mafanikio zaidi  katika siku hii muhimu kwa jamii yetu. 
  Kwa mawasiliano

  Daria Erasto

  Afisa Uhusiano

  Trumark

  +255 716 676665/ 754 095017


  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati), akiongozwa na baadhi ya viongozi wa Machimbo ya Dhahabu ya Matinje yaliyopo katika Kijiji cha Matinje Kata ya Mwashiku wilayani Igunga. Naibu Waziri alitembelea Machimbo hayo hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani (Mwenye Suti-katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Machimbo ya Matinje yaliyopo Kata ya Mwashiku wilayani Igunga, Charles Nogu, wakati alipotembelea Machimbo hayo akiwa katika ziara ya kazi hivi karibuni. 
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini (katikati) akikagua machimbo ya Matinje yaliyopo Kata ya Mwashiku wilayani Igunga, alipotembelea Machimbo hayo hivi karibuni. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mbunge wa Manonga, wilaya ya Igunga, Seif Gulamali. Wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa Machimbo hayo, wataalamu kutoka Wizarani, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

  Na Veronica Simba - Nzega
  SERIKALI imetoa siku tano kwa mwekezaji wa madini ambaye ni Kampuni ya NMDC Limited kutoka India, kushughulikia utaratibu wa kuwalipa fidia wananchi wa Kata ya Ntobo iliyopo wilayani Igunga, mkoa wa Tabora, walioachia ardhi yao kumpisha mwekezaji huyo.

  Agizo hilo lilitolewa juzi, Februari 17 na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani, wilayani Nzega alipokutana na viongozi wa Kampuni hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tabora kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya wizara yake.

  Akiwa wilayani Igunga, Naibu Waziri alipokea taarifa kuwa mwekezaji huyo alipewa leseni nne za uchimbaji madini wa kati mwaka 2012 lakini mpaka sasa hajaanza shughuli za uzalishaji kutokana na kutolipa fidia za maeneo ya wakazi wa eneo hilo.

  Kutokana na taarifa hiyo, Naibu Waziri aliagiza kukutana na Mwekezaji huyo ambapo walikutana naye juzi akiwa wilayani Nzega akiendelea na ziara yake. 

  Katika kikao hicho, ilibainika kuwa, kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 20.7 zinadaiwa kama fidia kwa wananchi waliopisha eneo husika.

  Ilielezwa kuwa, ulipaji huo wa fidia umekwama kutokana na mwekezaji huyo kutotaka kulipa fidia yote kwa wakati mmoja bali anataka alipe fidia kidogo kwa kuanzia na eneo dogo kati ya lile analomiliki ambalo anadai ndilo atakaloanza kufanyia kazi.

  Aidha, alidai kwamba atakuwa analipa fidia kwa eneo lililobaki kulingana na atakavyokuwa akilitumia.

  Akizungumza katika kikao hicho, Kamishna Msaidizi wa Madini wa Kanda ya Kati-Magharibi, Humphrey Mmbando alimweleza Naibu Waziri kuwa, wananchi wa eneo husika wanalalamika kuwa tangia eneo lao lichukuliwe na mwekezaji huyo, shughuli zao zilizokuwa zikifanyika katika eneo hilo zimesimama na hivyo wanahitaji kulipwa fidia stahiki.

  Kamishna Mmbando aliongeza kuwa, kufuatia malalamiko ya wananchi, Ofisi yake ilimtaka mwekezaji huyo awe ametoa majibu ya namna atakavyoshughulikia madai ya wananchi ndani ya siku 10 ambayo ilikuwa ni juzi, Februari 17, wakati kikao hicho kikikaa.

  Kutokana na maelezo hayo, Naibu Waziri alitoa siku tano zaidi kwa mwekezaji huyo ili ashughulikie mambo kadhaa katika kutatua mgogoro huo.

  Ndani ya siku hizo tano, Naibu Waziri alimtaka mwekezaji huyo, atoe taarifa rasmi ya kimaandishi kwa Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Magharibi kuwa anakusudia kufanya uzalishaji kwa kuanzia na eneo dogo ndani ya leseni yake.

  Pia, alimtaka mwekezaji huyo kumwomba Mthaminishaji wa Serikali kufanya uthamini kwa kujikita katika eneo lile tu ambalo anakusudia kuanza kulifanyia kazi.

  Vilevile, Naibu Waziri alimtaka mwekezaji huyo kuzungumza na wananchi husika ili wakubaliane kiasi cha fidia atakachotoa kwao kwa kuzuia shughuli zao za kujipatia kipato katika eneo hilo kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

  Mbali na maagizo hayo, Naibu Waziri alimtaka mwekezaji huyo awaruhusu wananchi kuendelea na shughuli za uzalishaji katika eneo ambalo atakuwa hajaanza kulifanyia kazi.

  “Nimewapa siku tano zaidi, mfanyie kazi maagizo niliyoyatoa vinginevyo, tutachukua hatua nyingine stahiki za kisheria dhidi yenu.”

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Kalemani ameagiza kufutwa kwa leseni zote za madini ambazo hazifanyiwi kazi na maeneo hayo kugawiwa kwa wachimbaji wadogowadogo ili wayafanyie kazi na kulipa mrabaha kwa Serikali.

  “Kwa kuanzia, katika eneo hili, nimeagiza leseni za utafutaji wa madini za kampuni za Kilimanjaro Mine na Mabangu Resources ziandikiwe taarifa ya kufutwa na tutaendelea na maeneo mengine,” alisema.

  Alisema kuwa kuna wawekezaji wengi ambao wamekuwa wakishikilia maeneo kwa muda mrefu pasipo kuyafanyia kazi na hivyo kuikosesha Serikali mapato yatokanayo na kodi, pia kuwakosesha wananchi maeneo ya kufanyia kazi.

  Awali, Naibu Waziri alitembelea Machimbo ya Madini katika Kijiji cha Matinje B, Kata ya Mwashiku wilayani Nzega ambapo mbali na kumpongeza mmiliki wa machimbo hayo, Jason Shinyanga, kwa kulipa mrabaha wa Serikali, alimtaka kuboresha mazingira ya uchimbaji katika eneo hilo.

  Meneo aliyoagizwa kuboresha ni pamoja na kujenga nyumba za kulala watumishi wake pamoja na vyoo bora. “Tunakupa taarifa ya siku 60 urekebishe dosari hiyo, usiporekebisha, tutasahau kama umelipa mrabaha au la,” alisisitiza Naibu Waziri.

  Aidha, Naibu Waziri aliwashauri wananchi wanaojishughulisha na uchimbaji kuhakikisha wanapata ushauri wa kitaalamu kutoka ofisi za madini katika maeneo yao kabla hawajaanza shughuli hizo.

  Pia, aliwataka kuhakikisha wanakuwa na leseni halali za kuendeshea shughuli hizo za uchimbaji ili pamoja na mambo mengine kuongeza thamani ya maeneo yao pindi wanapotaka kuyauza au kuingia ubia na wawekezaji wa kati na wakubwa.

  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia) akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale wakati Naibu Waziri huyo alipowatembelea katika ofisi Makao Makuu ya TANROADS leo Jijini Dar es Salaam. 
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wakifuatilia taarifa toka kwa Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale wakati alipopata ugeni wa Naibu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Edwin Ngonyani katika Makao Makuu ya ofisi hizo Jijini Dar es Salaam.
  (Picha na TANROADS)

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Bharti Airtel ya India, Bw. Sunil Bhartri Mittal kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwake jijini Dar es salaam, Februari 18, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Airtel Africa, Bw. Christian Defaria (kulia) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Bharti Airtel ya India, Bw. Sunil Bhartri Mittal (katikati) kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwake jijini Dar es salaam, Februari 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa pili kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tarehe 18/02/2016 juu ya ripoti ya Utafiti wa Watalii walioingia nchini mwaka 2014. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bw. Jonhson Nyella na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Zahoro Kimwaga kulia.
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wa Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
  ................................................................................

  Sekta ya utalii Tanzania ambayo mchango wake katika mauzo ya nje ya nchi ni takribani  asilimia 24.0 iliendelea kukua katika mwaka 2014 kama inavyodhihirishwa na ongezeko la idadi ya watalii wa kimataifa kutoka 1,095,885 mwaka 2013 hadi 1,140,156 mwaka 2014.  Matokeo ya utafiti wa mwaka 2014 yanaonyesha ongezeko kubwa la mapato ya utalii ambayo yanatokana na ongezeko la idadi ya watatii.  Wageni wengi wanaiona Tanzania kama kivutio pekee chenye watu marafiki na mandhari ya kuvutia.


  Utafiti huu umefanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT) kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Idara ya Uhamiaji na Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT). 


  Matokeo muhimu ya utafiti ni kama ifuatavyo:


  1)   Mapato yatokanayo na Utalii yaliongezeka kwa asilimia 8.2 hadi  kufikia Dola za Kimarekani 2,006.3 milioni katika mwaka 2014, ikilinganishwa na Dola za Kimarekani  milioni 1,853.3 zilizopatikana mwaka 2013;


  2)   Zanzibar ilipata Dola za Kimarekani 269.3 mwaka 2014 ikilinganishwa na dola za Kimarekani milioni 210.5 mwaka 2013;


  3)    Wastani wa matumizi yote ya mtalii kwa usiku ilikuwa Dola za Kimarekani 221 chini kidogo ya Dola za Kimarekani 284 zilizoripotiwa mwaka 2013.


  4)    Wageni waliofika chini ya mpango mfuko ziara walitumia wastani wa Dola za kimarekani 326.9 kwa mtu kwa usiku wakati wale waliokuja kwa kujitegemea walitumia wastani wa Dola za kimarekani 147.8;


  5)   Masoko makuu 15 ya utalii nchini yanachangia asilimia 82 ya watalii wote wa kimataifa. Zimbabwe, Uholanzi na China ni masoko mapya katika masoko makuu 15 katika mwaka 2014; ambayo yamechukua nafasi ya Sweden, Uswisi na India katika masoko Makuu 15 yaliyopatikana mwaka 2013;


  6)   Utalii wa wanyamapori - uliendelea kuwa shughuli kuu ya utalii katika Tanzania Bara ulichangia kwa asilimia 43.5. Idadi kubwa ya watalii waliokujai kutembelea wanyamapori walikuja kutoka Marekani, Uingereza, Ufaransa na Italia. Kwa upande Zanzibar, shughuli mashuhuri ilikuwa utalii wa ufukweni na kiutamaduni;


  7)    Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa asilimia 54.1 ya wageni wanatumia kati ya siku nane hadi 28. Wageni kutoka Ujerumani, Uholanzi, Italia, Ufaransa na Hispania walikaa muda mrefu zaidi na wale waliotoka Zimbabwe walikaa siku chache zaidi;


  8)    Kama ilivyoonekana katika tafiti zilizopita, watalii hawakufurahishwa na kutokuwa na huduma ya credit cards katika maeneo yanayotoa huduma za kitalii. Asilimia 87 ya watalii walilipia huduma mbalimbali za kitalii kwa kutumia fedha taslimu.
  Nakala ya ripoti hii inapatikana katika tovuti ya taasisi washirika ambazo: www.mnrt.go.tz, www.bot.go.tz, www.zanzibartourism.net, www.nbs.go.tz na www. moha.go.tz. 

  (Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Maliasili na Utalii)

  0 0

  Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania na Mkufunzi wa Mafunzo ya Bioteknolojia , Dk.Emmarold Mneney (kulia), akiwafundisha wanachuo wa Chuo cha Ualimu cha Bunda (BUNDA TTC), kuhusu matumizi ya bioteknolojia na uhandisi jeni Wilaya ya Bunda mkoani Mara leo asubuhi.
  Mtafiti Kiongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akizungumza na wanachuo hao katika mafunzo hayo.
  Wanachuo hao wakifuatilia mafunzo hayo. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 1128 | 1129 | (Page 1130) | 1131 | 1132 | .... | 3285 | newer