Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1130 | 1131 | (Page 1132) | 1133 | 1134 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Shirika la Ndege la RwandAir limetangaza kuwepo kwa punguzo la bei zake kwa kuelekea sehemu zifuatazo: Kigali, Nairobi, Mombasa, Entebbe, Bujumbura, Kamembe, Lusaka, Johannesburg, Dubai, Accra, Lagos, Douala, Juba, Libreville, Brazzaville.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mkazi wa Shirika hilo, Ibrahim Bukenya amesema wameamua kutoa punguzo hilo ili kuwawezesha wateja wao kusafiri katika maeneo hayo tajwa kadri wawezavyo na kwa gharama nafuu.

  Pia amesema kwa sasa Shirika hilo lina Ndege kubwa nane 8 na linataraji kuongeza Ndege mpya mbili aina ya Airbus A330-300 na mbili aina ya Boeing 737-800 kufikisha jumla ya Ndege kumi na mbili 12, kufikia mwisho wa mwaka huu.

  Shirika la Ndege la Rwanda litaanzisha safari zake mpya kuelekea, Guangzhou,Lilongwe,Cotonou, Khartoum, Paris,London, Harare na Mumbai na kufanya jumla ya safari zake kuwa  23.

  Bukenya ameongeza kwa kusema kuwa niwakati sasa kwa Mtanzania kutumia Shirika la RwandAir kwani wako na bei nafuu, Kusafiri kwa raha na Ndege mpya, Kupata huduma bora kuanzia wakati wa kupata tiketi hadi mwisho wa safari. Kwa huduma zaidi tembelea wakala wa RwandAir aliyeko jirani yako au nenda ofisi zao zilizoko jengo la Viva Towers ghorofa ya pili na unaweza kuwapata kwa namba za simu 0782 039152 au 022 2103435 na barua pepe sales.dar@rwandair.com
  Meneja Mkazi wa Shirika la Ndege la RwandAir, Ibrahim Bukenya akiwa ofisini kwake.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo kaburini katika kaburi la Baba Mzazi wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia ,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Mzee Ali Mwalimu katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu eneo la Mchukuuni mjini Tanga Februari 19, 2016
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati aliposhiriki mazishi ya baba mzazi wa waziri huyo mzee Ali Mwalimu, nyumbani kwa marehemu eneo la Mchukuuni mjini Tanga Februari 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kulia) pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga(watatu kulia) alipokuwa akiwafafanulia jambo juu ya studio ya kurushia vipindi vinavyofanywa na kituo hicho, wakati wa ziara maalum iliyofanywa na Uongozi wa kampuni hiyo kwa ajili ya mafunzo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao( kushoto ) alipotembelea makao makuu ya kituo hicho jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho,katikati Materi Mushi.
  Mkuu wa Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Sebo(kushoto)akiwafafanulia jambo juu ya studio ya kisasa ya EFM, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia (katikati) Wakati wa ziara maalum ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam,kulia ni Mfanyakazi wa radio hiyo Kasampaida.
  Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kulia) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Redio ya EFM,Francis Ciza (Majey) baada ya Uongozi wa Vodacom Tanzania kutembelea ofisi hizo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali na kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara na kituo hicho kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam.


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo jioni (Ijumaa, Februari 19, 2016) amekagua bandari ya Tanga na kumtaka Mkuu wa Bandari ya Tanga (Port Master), Bw. Henry Arika amletee maelezo juu ya ukiukwaji wa manunuzi ya tishari ifikapo kesho (Jumamosi) saa 6 mchana.

  Waziri Mkuu ambaye aliwasili Tanga leo mchana ili kushiriki mazishi ya baba mzazi wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mchukuuni, Tanga, aliamua kuzuru bandari hiyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege akiwa njia njiani kurejea Dar es Salaam.

  Katika ziara hiyo fupi, Waziri Mkuu alikataa kuingia ofisini (bandarini) na akataka apelekwe mahali tishari tatu za bandari hiyo zilipo. Katika maswali aliyoulizwa na Waziri Mkuu, Bw. Arika alikiri kuwa matishari hayo hayafanyi kazi kama inavyotakiwa kwa sababu yanasubiri kusukumwa na tugboat  (meli ndogo).

  "Nataka kesho saa 6 mchana uniletee barua yenye maelezo ni kwa nini mlinunua tishari tatu ndogo badala ya mbiili kubwa wakati mnajua Serikali ilitenga Dola za Marekani milioni 10.113 kwa ajili ya kununua tishari mbili zenye uwezo wa kujiendesha zenyewe  (self propelled) "

  “Nataka maelezo ni kwa nini mlizinunua tangu mwaka 2011 lakini zimekaa bila kufanya kazi hadi Novemba mwaka jana? Na kwa nini mnaendelea kutumia hela ya Serikali kwa kukodisha tishari kutoka Mombasa badala ya kutengeneza za kwenu au kufundisha vijana wa Kitanzania? Kwani tunao wahitimu wangapi wa fani hii?" alihoji Waziri Mkuu.

  "Taarifa nilizonazo ni kwamba moja ya tishari lilidondoka baharini mkaenda kutafuta huko na kulivuta hadi hapa ndiyo maana yameshindwa kufanya kazi inavyotakiwa," aliongeza.

  Katika majibu yake, Bw. Arika alisema wao waliagiza tishari hizo kupitia ofisi ya Bandari makao makuu ambayo iko Dar es Salaam. "Pia wakati zinaagizwa sikuwepo hapa Tanga. Nimekuja mwishoni mwa mwaka jana," alisema Mkuu huyo wa Bandari ambaye inaelezwa alitokea Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bibi Mwantumu Mahiza awaite watu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Bandari na Jeshi la Polisi wakae na kutafuta mbinu za kudhibiti njia za panya zinazotumika kupitisha sukari ya magendo.

  "Mkuu wa Mkoa simamia hawa watu, msaidiane kudhibiti uingizaji wa sukari kwa njia za panya. Kuna majahazi yanaleta sukari kutoka Brazil. Mheshimiwa Rais amepiga marufuku uingizaji wa sukari kutoka nje ili viwanda vyetu vya ndani viweze kuongeza uzalishaji. Dhibitini bandari zote ndogondogo hadi Pangani," alisema Waziri Mkuu.

  Alisema changamoto inayoikabili Serikali ni kwamba hata Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  au Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) hawawezi kuzikagua sukari hizo na hazijulikani ubora wake licha ya kuwa zinafika kwa walaji.

  Waziri Mkuu amerejea jijini leo jioni.
  Waziri Mkuu, Kssim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Bandari ya Tanga , Henry Arika (kulia kwake) kukagua bandari hiyo Februari 19, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa bandari ya Tanga, Henry Arika (kulia kwake ) na Mhandisi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Felix Mahangwa wakati alipotembelea bandari ya Tanga Februari 19, 2017.
  Matishari matatu ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametaka apewe maelezo kwa maandishi kuwa ni nani aliyeidhinisha mchakato wa manunuzi yake bila kuzingatia viwango na ubora uliokusudiwa na serikali. mheshimiwa Majaliwa alifanya ziara katika bandari ya Tanga Februari 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akiwahutubia wajumbe wa Baraza kuu la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakati akifungua kikao cha tatu cha Baraza hilo kilichofanyika leo katika ukumbi wa TAFORI mkoani Morogoro.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Fedha na Mipango Prof. Isaya Jairo akisoma hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa kikao cha tatu cha Baraza Kuu la Pili la wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kilichofanyika leo katika ukumbi wa TAFORI mkoani Morogoro.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza kuu la Pili la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kikao cha tatu cha Baraza hilo kilichofanyika leo katika ukumbi wa TAFORI mkoani Morogoro.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza na Wabunge kutoka nchini Sweden (hawapo pichani) leo jijini Da es salaam wakati wa mkutano uliofanyika Wizarani hapo, kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya Tanzania na Sweden. Kulia ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumzia vipaumbele vya Serikali wakati wa mkutano na Wabunge kutoka nchini Sweden leo jijini Dar es salaam kwa ziara ya kikazi nchini.

  Waziri wa Fedha na Mipango,Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na Wabunge wa Sweden katika ukumbi wa Wizara hiyo, kuzungumzia ushirikiano baina Tanzania na Sweden.

  Katika mazungumzo yake na wabunge hao ambao wamewasili nchini kwa  ziara ya kikazi, Dkt. Mpango amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo makini na inafanyakazi kwa ufanisi ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma stahiki kutokana na rasilimali zilizopo nchini.

  Amesema Serikali imejipanga kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani ili kuiwezesha nchi kujiendesha yenyewe na kuacha kutegemea misaada ya wahisani.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amefanya ziara ya Kikazi Nchi Rwanda na kuonana na Rais wanchi hiyo Mhe. Paul Kagame. 
  Waziri Mahiga alifanya ziara hiyo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Waziri Mahiga akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere mara baada ya kuwasili, amesema ziara hiyo ya kikazi nchini Rwanda ililenga kuonana na Rais wanchi hiyo Mhe. Paul Kagame kwakuwa ni jirani na ni mmoja wa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo pia walitumia fursa hiyo kujadili masuala mbambali kuhusu Jumuiya.
  Aidha katika mazungumzo hayo walijadili suala la mgogoro wa kisiasa wa nchini Burundi na kwa pomoja kuangalia namna bora zaidi ya kurejesha amani ya kudumu katika nchi hiyo.
   Pia Mhe. Waziri alipata fursa ya kuzungumza na wafanyabishara wa Nchini Rwanda ambapo wamesifu utendaji wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli. Wafanyabiashara hao wamesifu utendaji wa Serikali kwa hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kuboresha utendaji wa taasisi zake ikiwamo Bandari. “Nimepewa salamu za pongezi na wafanyabiashara wa Rwanda nizilete kwa Serikali ya Tanzania kwa kazi nzuri iliyofanywa na Serikali na wameahidi kuongeza ushirikiano wa kibishara baina ya nchi hizi mbili” alisema Waziri Mahiga.  
  Vilevile Rais Mhe. Paul Kagame katika mazungumzo hayo amesisitiza ujenzi wa mradi wa reli ya ukanda wa kati ambayo itasaidia kukuza biashara zaidi baina ya nchi hizi mbili na kuongeza fursa za uwekezaji.

  Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga, akiwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere akitokea Nchini Rwanda ambako alienda kumuwakilisha Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
  Mhe. Waziri akijadili jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kasiga.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kasiga akimkaribisha Mhe. Waziri kuongea na waandishi wa habari juu ya lengo la safari ya kwenda nchini Rwanda na manufaa yake kwa Taifa, kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Mhe. Balozi Samuel Shelukindo.
  Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.
  Mhe. Waziri akiongea na waandishi wa habari na kuwaeleza safari ilikuwa na lengo la kuonana na Mhe. Rais Paul Kagame kama jirani na mwanachama wa Jumuiya ya Afrika mashariki na kufanya mazungumzo naye juu ya hali ya kisiasa nchini Burundi pia aliweza kuzungumza na wafanyabiashara nchini Rwanda ambao walieleza kuridhishwa na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano. 
  Wakizungumza mara baada ya kumaliza Mkutano na vyombo vya habari.

  0 0


  0 0


  Wizara imepata taarifa zisizo na ukweli zinazoenezwa na kusambazwa na watu wasiokuwa na nia njema kwa Wizara na Serikali kwa ujumla, kuwa Wizara iliyokuwa ya Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliendesha zoezi la kukusanya wasifu(CV) za Wafanyakazi wake kwa lengo la kuwafukuza kazi.

   Wizara imesikitishwa na inalaani vikali uvumi wa taarifa hizi na  inakanusha kuwa taarifa hizi hazina ukweli wowote.


  Zoezi la kukusanya CV za watumishi ni zoezi la kawaida kwa waajiri na hufanyika Mara kwa mara kwa lengo la kuhuisha sifa na uzoefu wa watumishi wanazopata wakiwa kazini ambapo hatimaye huwekwa kwenye majalada yao binafsi, mwajiri anapaswa kuhakikisha jalada la kila mtumishi lina taarifa zinazoeenda na wakati, hivyo zoezi hili lilifanyika kwa lengo la kuhuisha taarifa za watumishi wa Wizara kama ilivyoelekezwa na mwajiri na si vinginevyo. 
  Wizara inapenda kutoa ufafanuzi kuwa CV si miongoni mwa nyaraka zinazohitajika katika kumfukuza kazi mtumishi bali mtumishi anafukuzwa kazi kwa kukiuka sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi ambapo taratibu maalumu za kinidhamu hufuatwa. Katika kipindi husika Wizara haina mtumishi anayetuhumiwa kwa kosa la kinidhamu linaloweza kupelekea kufukuzwa kazi, hivyo taarifa hizi hazina ukweli wowote.


  Aidha, Wizara inakemea vikali watu wenye tabia ya kutoa taarifa zisizo na ukweli na zenye kupotosha umma. Vilevile Wizara inapenda kuwaasa wananchi kuheshimu sheria na taratibu za Nchi sambamba na kutoeneza taarifa zinazotokana na vyanzo visivyokuwa rasmi au zisizothibishwa na mamlaka husika, kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria na taratibu za Nchi.


   Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

  Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.


  19 Februari, 2016


  0 0  0 0

  \
  Serikali yaiomba jamii ya kimasai kuendelea kudumisha amani na utulivu ulipo nchini; https://youtu.be/mdBojN2LoWk  

  Spika wa bunge Job Ndugai amesema Tanzania na nchi ya Sweden zitaendelea kushirikiana katika nyaja mbali mbali ili kuleta maendeleo; https://youtu.be/lJqfHv3j9M8  

  Wanafunzi 16 wa chuo kikuu cha Mtakatifu Joseph kilichopo mkoani Ruvuma wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kufanya fujo;https://youtu.be/NTRkhZ4kC28  

  Serikali ya Tanzania na Rwanda zimekubaliana kushirikiana katika kutatua mgogoro wa kisiasa katika nchi ya Burundi;https://youtu.be/uc0uiTAAKbI  

  Sensa ya kilimo, uvuvi na ufugaji nchini inatarajiwa kuanza Februari 23 mwaka huu; https://youtu.be/8UufjeT2o5w   

  Benki M yaanzisha huduma ya mpya ya Money moja kwa moja kuwarahisishia wateja wake pindi watakapohitaji kutoa pesa katika akaunti zao; https://youtu.be/U4qx4EFmsXY  

  Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Mhe Nape Nnauye amsimamsisha kazi katibu mtendaji wa baraza la michezo Tanzania kwa kutoridhishwa na utendaji kazi wake;https://youtu.be/BIlxnR9npOE  

  Tiketi kwa ajili ya mchezo  wa watani wa jadi baina ya Simba SC na Yanga zaanza kuuzwa hii leo; https://youtu.be/Ae_KWLGrKJg  

  Shirikisho la vyuo vya elimu ya juu CCM visiwani Zanzibar limeitaka tume ya uchaguzi ZEC kuwa makini na uwepo wa makamishina wa chama cha wananchi CUF katika vikao vya tume ya uchaguzi Zanzibar; https://youtu.be/BUyqUC93RtI  

  Mkuu wa mkoa wa Kaskazin Pemba,Mhe.Omary Khamis Othman achukuizwa na kitendo cha watendaji wa wizara ya kilimo visiwani humo kuuza mashamba ya serikali; https://youtu.be/ODaORN-b2Xw

  Wananchi mkoani Tabora wametakiwa kufuata sheria na taratibu wakati wa ununuzi wa maeneo ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima; https://youtu.be/xevgvUP4f68

  Wafanyakazi wa taasisi ya uhasibu nchini TIA wametakiwa kufanya kazi kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa;https://youtu.be/n1gCzlJKLgs  

  Tume ya vyuo vikuu nchini TCU yafuta  kibali cha usajili wa vyuo vikuu vishiriki viwili; https://youtu.be/93fRBknYuRQ

  Mwanamke mmoja huko mkoani Geita achinjwa na kufariki dunia huku mumewe akijeruhiwa kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kukopa fedha. https://youtu.be/nKX0-ZRLB2A  

  Tume ya vyuo vikuu nchini TCU, yavifutilia mbali vyuo vikuu vitatu nchini kwa kushindwa kusimamia ubora, na taaluma pia kukiuka sheria ya uendeshaji wa vyuo. https://youtu.be/kOOP7D00Yag  

  Serikali yaingilia kati mgogoro mkubwa ulioibuka baina ya wafugaji wa jamii ya kimasai na wale wa kibarbaig waliokuwa wakituhumiana kuibiana ngombe na kuupatia utatuzi.https://youtu.be/OEArqoc1WAA  

  Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa afanya ziara ya kushitukiza katika bandari ya Tanga na kumuagiza meneja wa banadari hiyo kuandika barua ya kujieleza kufuatia ukiukwaji wa taratibu za manunuzi. https://youtu.be/y5UxC7uyyNc  

  Wachimbaji wa madini ya dhahabu mkoani Shinyanga huenda wakaanza kuzalisha kwa tija baada ya kutengenezewa mashine itakayo rahisisha kuvuta udongo wenye madini kutoka ardhini.https://youtu.be/U9ZCiV4_cqs  

  Siku chache baada ya naibu waziri Suleiman Jaffo kuipa maagizo hospitali ya Zakheim, wananchi wakiri kuwepo kwa mabadiliko makubwa ukilinganisha na hapo awali. https://youtu.be/6VG3NaEA-14  

  Baadhi ya wanafunzi, wazazi na walimu watoa mtazamo tofauti juu ya matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa hapo jana.https://youtu.be/ENEaqif5rRs
  Attachments area  0 0  0 0
  0 0

  Lady Jaydee
  Mkongwe wa muziki wa bongo fleva Lady Jaydee ametangaza rasmi kurudi tena kwenye gemu  baada ya ukimya wa muda mrefu.  Lady Jaydee ameweka wazi ujio wake mpya kwenye muziki ikiwa leo ni siku ya 29 kuelekea uzinduzi wa #NaamkaTena. Tazama promo ya siku ya 29 ambapo Mh. Nape Nnauye kamzungumzia Lady Jaydee hivi.
  "Mimi Kama kiongozi wa Sanaa nchini, Nitahakikisha natetea muziki wa Tanzania. Lady JayDee anaamka tena", amesema Mh.Nape Nnauye.
  #LadyJayDeeOfficialCountDown #NaamkaTena

  0 0

  Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi (kulia), akizungumza na wakulima na Washiriki wa Mafunzo ya kutumia simu za mkononi kupashana habari za kilimo yaliyofanyika Kijiji cha Kisamwene wilayani Butiama mkoani Mara leo mchana.
  Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi (kulia), akiwaonesha wakulima wa Wilaya ya Butiama mkoani Mara zao la mhogo uliotokana na mbegu aina ya ukombozi iliyofanyiwa utafiti nchini. Nyinondi alikuwa akiwaonesha wakulima jinsi unavyoweza kupiga picha zao hilo na kulitafutia soko wakati akitoa mafunzo ya kutumia simu jinsi kupashana habari za kilimo katika mafunzo yaliyofanyika juzi wilayani humo.

  Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel Otunge akiwa katika shamba la mkulima wa mfano lililopo kijijini hapo.
  Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel Otunge akimpiga picha mmoja wa wakulima katika mafunzo hayo.
  Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa Wilaya mpya ya Buhigwe, Mary Tesha akiwasilisha taarifa kuhusu kero na changamoto mbalimbali kuhusu sekta ya nishati, zinazowakabili wananchi wake mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia), alipofanya ziara wilayani humo hivi karibuni.

  Na Veronica Simba - Buhigwe

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani amekataa kupokea Taarifa ya utendaji kazi kwa Wilaya mpya ya Buhigwe mkoani Kigoma, kutoka kwa Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa Wilaya hiyo, Ntungwa Njegelo. Dk Kalemani alikataa kupokea taarifa hiyo juzi Februari 19, alipokutana na Uongozi wa Wilaya hiyo mpya, kwenye Ofisi ya muda iliyopo wilayani humo, akiwa pamoja na watendaji mbalimbali kutoka wizarani, Tanesco na Wakala wa Umeme Vijijini (REA)

  Akizungumzia sababu za kukataa kupokea taarifa hiyo, Naibu Waziri alisema haijitoshelezi kwani haijaeleza kwa kina masuala mbalimbali muhimu ya kiutendaji katika wilaya hiyo.


  “Kwa mfano, taarifa hii inaeleza vijiji 12 vimepata umeme lakini haielezi idadi hiyo ni kati ya vijiji vingapi. Pia, haielezi ni asilimia ngapi ya umeme imepatikana. Taarifa hii haiwezi kunisaidia maana nataka kutatua kero hivyo ni lazima nijue ukubwa wa tatizo.”
  Kufuatia hatua hiyo, Naibu Waziri Kalemani alimwagiza Meneja huyo aandae taarifa mpya, yenye maelezo ya kina kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme hususani mradi wa REA (Umeme Vijijini) Awamu ya pili na kuiwasilisha kwake Jumatatu, Februari 22 mwaka huu.


  0 0

  Mtanange wa watani wa jadi kati ya Wekundu wa Msimbazi (Simba) dhini ya Vijana wa Mtaa wa Twiga na Jangwani (Yanga) unaotaraji kupigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, huku homa ya mchezo huo ikizidi kupanga kwa mashabiki wa pande zote mbili. Je nani ataibuka kidedea leo??

  0 0

  Kulia ni Mtanzania Allan Kyariga jina la kisanii Allan Kingdom siku ya Jumatatu Feb 15, 2016 alikua nominated kwenye Grammys Awards zilizofanyika Los Angeles, California katika wimbo wa All Day aliyeimba akishirikiana na Kanye West. Allan Kingdom alikua nominated kwenye Best Rap Song na Best Rap Performance kushoto kwenye picha ni mama yake mzazi Lau Kyariga akiwa amemsindikiza mwanae wote wanaishi Minnesota.

  Video: Allan Kingdom akifanyiwa mahaojiano 
  kwenye zulia jekund siku ya Grammys Awards.

  Wimbo wa All Day Allan Kingdom na Kanye West alipofanya show Live jijini London mwaka jana
  Lau Kyariga akiwa kwenye zuria jekundu kwenye
  Gammys  Awards Los Angeles, California

  0 0
 • 02/20/16--01:19: Article 16


 • 0 0

  Mkuu wa Wilaya mpya ya Buhigwe, Mary Tesha akiwasilisha taarifa kuhusu kero na changamoto mbalimbali kuhusu sekta ya nishati, zinazowakabili wananchi wake mbele ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (wa pili kutoka kulia), alipofanya ziara wilayani humo hivi karibuni. 

  Na Veronica Simba - Buhigwe
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani amekataa kupokea Taarifa ya utendaji kazi kwa Wilaya mpya ya Buhigwe mkoani Kigoma, kutoka kwa Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wa Wilaya hiyo, Ntungwa Njegelo.

  Dk Kalemani alikataa kupokea taarifa hiyo juzi Februari 19, alipokutana na Uongozi wa Wilaya hiyo mpya, kwenye Ofisi ya muda iliyopo wilayani humo, akiwa pamoja na watendaji mbalimbali kutoka wizarani, Tanesco na Wakala wa Umeme Vijijini (REA)

  Akizungumzia sababu za kukataa kupokea taarifa hiyo, Naibu Waziri alisema haijitoshelezi kwani haijaeleza kwa kina masuala mbalimbali muhimu ya kiutendaji katika wilaya hiyo.

  “Kwa mfano, taarifa hii inaeleza vijiji 12 vimepata umeme lakini haielezi idadi hiyo ni kati ya vijiji vingapi. Pia, haielezi ni asilimia ngapi ya umeme imepatikana. Taarifa hii haiwezi kunisaidia maana nataka kutatua kero hivyo ni lazima nijue ukubwa wa tatizo.”

  Kufuatia hatua hiyo, Naibu Waziri Kalemani alimwagiza Meneja huyo aandae taarifa mpya, yenye maelezo ya kina kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme hususani mradi wa REA (Umeme Vijijini) Awamu ya pili na kuiwasilisha kwake Jumatatu, Februari 22 mwaka huu.

  Aidha, Dk Kalemani alimwagiza Meneja huyo kufuatilia na kufanyia kazi malalamiko ya wananchi katika eneo lake, kuhusu kuwepo na mashimo yaliyochimbwa kwa ajili ya kusimika nguzo za umeme katika mashamba yao lakini yameachwa wazi kwa muda mrefu pasipo zoezi hilo kufanyika hivyo kuwazuia kuendelea na shughuli zao za kilimo.

  Awali, akiwasilisha taarifa kwa niaba ya wananchi wake kuhusu kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili kuhusiana na sekta ya nishati, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mary Tesha alimwomba Naibu Waziri kusaidia ili mashimo yaliyochimbwa katika baadhi ya vijiji kwa ahadi ya kusimika nguzo za umeme, yafanyiwe kazi mapema ili wananchi waendelee na shughuli za kilimo katika mashamba yao.

  Vilevile, Dk Kalemani alisema pamoja na mapungufu kadhaa, Tanesco wamejitahidi kufanya kazi nzuri ya kuwaunganishia wananchi wa vijijini umeme kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

  Alimpongeza Mkandarasi mzalendo anayeunganisha umeme wa REA Awamu ya pili mkoani Kigoma, Wilbroad Mutabuzi kupitia kampuni yake ya JV State Grid Electrical and Trchnical Works Ltd kwa kazi nzuri anayoifanya.

  “Kuna baadhi ya maeneo tumekutana na matatizo ya wakandarasi kufanya kazi chini ya kiwango hivyo kuturudisha nyuma. Huyu Mkandarazi mzawa anayefanya kazi hiyo hapa Kigoma anajitahidi sana na namtaka aendelee hivyo.”

  Alisema ameagiza zoezi la kuunganisha umeme wa REA Awamu ya pili likamilike ifikapo Mwezi Aprili mwishoni, hivyo wale wote waliopangwa kuunganishiwa umeme katika awamu hiyo, wanapaswa kuwa wamepatiwa huduma hiyo ndani wa kipindi hicho.


  Naibu Waziri Kalemani yupo katika ziara ya kikazi kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya wizara yake. Alianza ziara hiyo mkoani Tabora, sasa yupo Kigoma na anatarajia kumalizia ziara hiyo ya siku 10 mkoani Geita.


older | 1 | .... | 1130 | 1131 | (Page 1132) | 1133 | 1134 | .... | 3348 | newer