Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

SHUKRANI YA FAMILIA YA GOGADI NA MBUGUNI.

$
0
0
SHUKRANI 
FAMILIA YA GOGADI NA MBUGUNI INATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA KUTUFARIJI HADI MAZISHI YA BABA YETU MPENDWA MAREHEMU DEUSDEDIT GOGADI ALIYEFARIKI GHAFLA TAREHE 31 DECEMBER, KWA KUWA SIYO RAHISI KUMSHUKURU MMOJA MMOJA TUNAOMBA SHUKRANI ZETU ZIWAFIKIE WOTE.  

MKESHA WA KUOMWOMBEA MAREHEMU BABA YETU UTAFANYIKA NYUMBANI KWAKE KIJITONYAMA TAREHE 12 IJUMAA NA KUFUATIWA NA IBADA YA SHUKRANI KATIKA KANISA LA MWENGE ROMAN CATHOLIC TAREHE 13 SAA 12.30 ASUBUHI. RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA NURU YA DAIMA IMWANGAZE APUMZIKE KWA AMANI AMEN.

KAMUSOKO ACHAGULIWA KUWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI DISEMBA

$
0
0

MCHEZAJI Thaban Kamusoko amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Disemba, 2015 baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa Yanga (Amissi Tambwe).

Kamusoko ameisaidia timu yake ya Yanga katika michezo iliyochezwa mwezi Disemba kwa kushiriki dakika zote katika michezo mitatu iliyochezwa mwezi wa Disemba.

Kwa kuchaguliwa kwake kuwa mchezaji bora wa wa mwezi Disemba, Kamusoko atakabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa ligi Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

23RD MEETING OF THE SECTORAL COUNCIL OF MINISTERS RESPONSIBLE FOR EAC AFFAIRS AND PLANNING KICKS OFF IN ARUSHA

$
0
0
The 23rd Meeting of the Sectoral Council of Ministers Responsible for EAC Affairs and Planning (SCMEACP) kicked off in Arusha, Tanzania today.

The five day meeting started with the Session of Senior Officials which will run from February 8th – 10th, 2016, followed by the Session of Permanent/Principal Secretaries that will take place from February 10th – 11th, 2016. The meeting will be capped by the Ministerial Session which will take place on Friday, February 12th, 2016.

Among the items on the agenda of the meeting are:
Consideration of the report on the Implementation of previous decisions of the SCMEACP;
Consideration of a Progress Report on the Status of Implementation of the EAC Common Market;
Consideration of a Progress Report on the Elimination of Non-tariff Barriers;
Consideration of a Progress Report on COMESA-EAC-SADC Tripartite Arrangement;
Consideration of Declaration on the Establishment of the EAC Common Higher Education Area, and;
Progress Report on the Study on Equitable Sharing of Benefits and Costs of EAC Integration.
The Session of Senior Officials is being chaired by Mr. Eliabi Chidota from the Ministry of Foreign Affairs, Regional and International Cooperation in the United Republic of Tanzania. Tanzania is the current Chair of the Community.

The Session was officially opened by the EAC's Deputy Secretary General for Planning and Infrastructure, Dr Enos Bukuku. Also present at the official opening was the Deputy Secretary General (Productive and Social Sectors), Hon. Jesca Eriyo.

Rais Magufuli ampa pole mama Tunu Pinda

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za pole Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda aliyepatwa na ajali ya gari, iliyotokea jana tarehe 08 Februai, 2016 akiwa safarini kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam.


Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkundi lililopo katika Manispaa ya Morogoro ambapo gari aliyokuwa akisafiria Mama Tunu Pinda, ilipinduka baada ya kumgonga mwendesha pikipiki aliyeingia ghafla barabarani.


Katika salamu hizo alizozituma kupitia kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko taarifa za kutokea kwa ajali hiyo na amemuombea Mama Pinda na Majeruhi wengine kupona haraka.


"Kupitia kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda, naomba unifikishie pole nyingi kwa mkeo Mama Pinda kwa kuumia katika ajali hii, na namuomba Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi wote ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku"alisema Rais Magufuli.


Mama Tunu Pinda anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es salaam, na hali yake inaendelea vizuri.



Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dodoma

09 Februari, 2016

BENKI YA POSTA TANZANIA, TPB, YAZINDUA HUDUMA ZA KIFEDHA TAWI LAKE LA BABATI MKOANI MANYARA

$
0
0
Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru (katikati), akikata tepe kikiwa ni ishara ya uzinduzi wa huduma za kifedha kwenye tawi la Benki ya Posta Babati mkoani Manyara leo Februari 9, 2016. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi, na kushoto ni Menyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB, Profesa Lettice Rutashobya
Msajili wa hazina, Lawrence Mafuru (wapili kushoto), akimpa zawadi mmoja wa wateja wa Benki ya Posta tawi la Babati, Theofil Muhale Tsaghayo baada ya kufungua rasmi huduma za kibenki katika tawi la Babati, mkoaniManyara Februari 9, 2016. kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo Prof. Lettice Rutashobya.

Na Mwandishi wa K-VIS MEDIA, Babati.
BENKI ya Posta Tanzania (TPB) imezindua huduma za Kibenki kwa kufungua tawi lake jipya kwenye mji wa Babati mkoani Manyara. Akizungumza kwenye uzinduzi huo Februari 9, 2016, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB, Lettice Rutashobya alisema tawi lililokuwepo hapo awali halikuweza kutosheleza mahitaji ya wakazi wa Mji wa Babati na vitongoji vyake kutokana na udogo wake.

‘’Tawi hili limefunguliwa ili kutimiza dhamira ya Benki yetu ya kupeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wateja wake, na sasa Tawi hili litatoa huduma bora na za kisasa ikiwemo ile ya ATM kwa wafanyabiashara, wafanyakazi na wananchi kwa ujumla katika wilaya hii ya Babati”, aliwahakikishia Profesa Rutashobya.

Profesa Rutashobya aliwashukuru wateja wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake kwa kutumia huduma wa TPB wa Wilaya ya Babati na vitongoji vyake kwa kutumia huduma za Benki hiyo kwa wingi, na kulifanya tawi hilo kuwa ni mojawapo ya matawi yanayofanya vizuri kifaida.

Naye Msajili wa Hazina, Lawrence N. Mafuru, ambaye ndiye aliyezindua huduma za kibenki za tawi hilo, aliipongeza Benki ya Posta kwa kuleta maendeleo ya kuninua maisha ya Mtanzania ya hali ya chini kwa kuongeza huduma za kibenki karibu na jamii hiyo, na kwa kubuni huduma mbalimbali hususan za mikopo, zenye lengo la kumuinua kimapata mwananchi wa chini.

Msajili huyo wa Hazina, alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wakazi wa Babati kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki ya Posta, kwa kufungua akaunti na kwenda kuomba mikopo ambayo oinatolewa kwa riba nafuu na benki hiyo.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta, Sabasaba Moshingi amesema uamuzi wa kujenga tawi hilo ambalo linatoa huduma zote zinapatikana kwenye matawi mengine ya Benki ya Posta Tanzania nchi nzima.

“Azma ya Benki ya Posta, ni kuwafikia na kutoa huduma za kibenki kwa wananchi wote (financial Inclusion), alisema Moshingi.

CHANGIA DAMU OKOA MAISHA HOSPITALI YA MUHIMBILI

$
0
0
DAMU2 Maadhimisho ya miaka 6 ya utoaji wa Huduma ya Damu Hospitali ya Muhimbili Tarehe 25-27 Februari 2016 kuanzia Asubuhi mpaka Jioni.

Serikali kuendelea kutafuta fedha kwa ajili ya wawekezaji wa Umeme- Profesa Muhongo

$
0
0
Na Teresia Mhagama, Mtera

Imeelezwa kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kutafuta fedha  kwa   ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ambayo wananchi  wameamua kuiendeleza  ikiwemo miradi ya uzalishaji umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali kama maji,upepo, jua, nishati  jadidifu, makaa ya mawe na mawimbi ya bahari. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa kikao chake na wazalishaji wa umeme wa maji na wale wanaotaka kuzalisha umeme huo chini ya megawati 20 kilichofanyika katika Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Mtera. 

“Serikali lazima iwe Msemaji wa wawekezaji hawa ili kuhakikisha wanapata fedha na teknolojia za kuendesha miradi yao na hii itapelekea Taifa kuwa na nishati ya kutosha kwani wawekezaji hawa sasa watakuwa na uwezo wa  kuzalisha umeme,” alisema Profesa Muhongo. 

Ili kufanikisha suala, Profesa Muhongo  aliwataka wadau hao wanaotaka kuzalisha umeme wa maji chini ya megawati 20 kuhakikisha kuwa wanaandika na kuwasilisha wizarani mapendekezo yanayochanganua  miradi  wanayotaka  kuanzisha kabla ya mwisho wa mwezi huu ili litengenezwe kalabrasha moja litakalotumika katika kuombea fedha kwa wafadhili mbalimbali na Taasisi za Kifedha. 

“Ifikapo tarehe 28 mwezi huu mchanganuo wa mapendekezo yenu yawe yamemfikia Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati ili serikali iangalie namna ya kutafuta fedha zitakazowawezehsa  kuendeleza miradi yenu ya  umeme badala ya  mtu mmoja mmoja kuanza kuzunguka na maombi yake binafsi  ya kutafuta fedha kutoka Taasisi mbalimbali jambo linalochelewesha upatikanaji wa fedha hizo, “ alisema Profesa Muhongo. 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

$
0
0


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016.
           Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa VICOBA, Devota             Likokola (wapili kulia ) wakati alipotembelea banda la Benki ya Posta         Tanzania katika Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi        alioufungua kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha walimu Julius         Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016.
                                                 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Airtel fursa yawafikia vijana mkoani Morogoro

$
0
0
Wafanyakazi wa Airtel wakifanya ukarabati bucha la kijana Hashim Mikidadi, kijana aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel fursa Tunakuwezesha, wakiongozwa na Asisa mauzo wa Airtel Aminata Keita (katikati) Mwishoni mwa wiki .Hashim ni kijana mjasiriamali anayejihusisha na kuuza bucha la nyama lililopo standi ya mabasi Ngerengere mjini Morogoro.
Afisa mauzo wa Airtel Aminata Keita (kushoto) akiongea na kijana Hashim mkazi wa Ngerengere mjini Morogoro aliyewezeshwa na Airtel Kupitia mpango wake wa Airtel Fursa walipoungana nae katika ukarabati wa bucha lake kabla ya kukabidhiwa vitendea kazi mwanzoni mwa wiki ijayo.

Katika jitihada za kusaidia vijana wajasiriamali, wafanyakazi wa  Airtel wameungana na shirika lao kupitia mpango wake wa Airtel FURSA kuwafikia vijana mkoani Morogoro. Mwishoni mwa wiki hii wafanyakazi hao walijitokeza kumsaidia kijana Hashim Mikidadi, kijana mjasiriamali  anayejihusisha na kuuza bucha la nyama kwa kukarabati duka lake  lililopo standi ya mabasi Ngerengere mjini Morogoro.

Akizungumza wakati wa zoezi la ukarabati wa bucha hilo Afisa mauzo wa Airtel, Aminata Keita alisema "Airtel tunajali sana jamii yetu inayotuzunguka hivyo tunaelewa changamoto nyingi ambazo vijana wamekuwa wakikutana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira, ukosefu wa mtaji wa kuanzisha biashara zao na mambo mengine mengi. Msaada wetu kama wafanyakazi wa Airtel ni kuunga mkono mpango wa kampuni yetu ya kusaidia vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel Fursa  katika kusaidia vijana wetu kwa kuwaonyesha njia ili waweze kuinua jamii inayowazunguka na kufikia ndoto zao."

"Leo tunafuraha kubwa kuona kwamba tumeweza kumfikia na kumuwezesha kijana huyu mjasiriamali aliyewezeshwa na Airtel FURSA, ambaye Airtel Fursa imebadilisha maisha yake kwa kukarabati paa la bucha lake, kutengeneza sakafu kwa kuweka tiles za kisasa, na matengenezo mengine mengi ambayo imeipa duka hilo mtazamo mpya kabisa . Mapema wiki ijayo Airtel FURSA itamalizia kwa kumuwekea vifaa vya kisasa  kabisa  vikiwemo vifaa vya  kukatia nyama, jokofu la kisasa la kuhifadhia nyama na vifaa vingine vnavyohitajika kwa kazi za bucha. Vifaa hivyo na gharama za utengenezaji vimegharimu kiasi cha sh. milioni 9, alisisitiza Aminata.

Wakati wa shughuli hiyo ya makabidhiano, wafanyakazi wa Airtel walijiunga na wakazi wa  Ngerengere ambao walijitokeza kumuunga mkono  Hashim kwa kuwa na nidhamu kwa jamii inayomzunguka na ni mfano wa kuigwa na vijana wenzie.

Kwa upande wake Hashim aliwashukuru sana Airtel kwa kuweza kumpatia  fursa hii kwani ni vijana wengi sana wanaohitaji msaada huu lakini leo hii nafasi hii imemdondokea yeye.

“Bila kuwasahau nawashukuru sana wafanyakazi wa Airtel kwa kusaidia ukarabati wa bucha langu kwani mtazamo huu mpya  na vifaa vya kisasa utasaidia kuhamasisha wateja wangu na wale ambao hawakuwa wateja wangu.”.
“Nilianza nikiwa sina kitu. Lakini leo Airtel imeinua maisha yangu na kuniwezesha kuwapatia ajira vijana wenzangu waliokuwa mtaani bila kazi. ".

Airtel Fursa uwezeshaji ilizinduliwa mwezi Mei mwaka jana na ina tarehe kufikiwa vijana zaidi ya 3000 na mafunzo ya ujasiriamali na misaada ya biashara kwa karibu na 100 wajasiriamali bora vijana wote mmoja mmoja na katika vikundi vya vijana na hatimaye kukua kujenga fursa na jamii inayowazunguka. Katika msimu wa pili Airtel imeahidi kutumia zaidi ya sh. bilioni 1 katika mpango wa kuwawezesha vijana wa Tanzania kufikia uwezo wao katika ulimwengu wa biashara.

Airtel Fursa awamu ya kwanza ulianza mwaka jana mwezi wa tano na mpaka sasa umeshaweza kufikia vijana zaidi ya 3000 kwa kuwapatia mafunzo ya biashara ya ujasiriamali na wengine wapatao 100 wameweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi vya kuendelezea biashara zao za ujasiriamali. 

Katika awamu ya pili Airtel Fursa imeahidi kutumia zaidi ya sh. bilioni 1 ukiwa na lengo la kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za biashara na vifaa vitakavyowawezesha kukuza biashara zao.

Wasichana kunufaika na kampeni maalumu ya Afya.

$
0
0
-Kupitia ujumbe wa simu za mkononi
WASICHANA Nchini kuanzia leo wataanza kunufaika na kampeni maalumu ya kutumia ujumbe mfupi wa maneno kwa njia ya simu za mkononi kwa ajili ya kutoa elimu kwa wasichana kuhusiana na hedhi na jinsi ya kujistiri wanapokuwa kwenye kipindi hicho.

Kampeni hiyo ambayo Taasisi ya Vodacom Foundation kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la T-MARC imewalenga wasichana wenye umri wa kuanzia miaka 18-40  wanaotumia simu za mkononi pia inahamasisha jamii kuacha kuonea aibu mijadala kuhusiana na changamoto za kipindi cha hedhi ambazo zinawakumba wasichana wengi na pia kutoa elimu ni jinsi gani ya kujistiri vizuri ili waendelee na majukumu yao ya kila siku.

Vodacom Foundation imewezesha mradi huu kwa kutoa fursa ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye thamani ya shilingi milioni 100 na utatekelezwa na Shirika la T-MARC Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya  PUSH Mobile kwa kipindi cha miezi sita.

Ushirikiano wa Vodacom Foundation na T-MARC unaendelea kutekeleza mradi wa Hakuna Wasichoweza unaondelea katika mikoa ya Lindi a Mtwara ambao kwa kiasi kikubwa meanza kuonyesha mafanikio kwa kupunguza uoro wa wasichana mashuleni wanapokuwa katika vipindi vya hedhi.Mradi huu pia unatarajiwa kuwafikia wasichana  Zaidi ya 10,000 katika mikoa hiyo.

Akiongea kuhusu mradi wakati wa uzinduzi,Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Ian Ferrao,alisema Vodacom inajivunia kushirikiana na T-MARC kusaidia  afya za wanawake kwa kuwa moja ya dhamira ya kampuni ni kutumia ubunifu wa teknolojia kuboresha maisha ya watu kwenye jamii kama ambavyo imefana kutumia mtandao wake kutoa elimu ya afya na uzazi.

Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Dk.Moshi Kimizi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa  kampeni hii alipongeza Vodacom Foundation na T-MARC kwa kuona umuhimu wa kuelimisha jamii kuhusiana na changamoto za hedhi ambazo zinachangia  wanawake kubaki nyuma.

“Napenda kuungana na kauli mbiu ya kampeni hii,ambayo ni Hedhi sio ikwazo cha kupata elimu kwa wasichana na nawaomba watanzania wote waungane na mimi kuhakikisha kuwa wanashiriki katika kampeni hii kwa kutuma neon MSICHANA kwenda namba 15077 ili kupata taarifa sahihi kuhusiana masuala haya”.Alisema Dk.Kimizi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la T-MARC,Diana Monica Kisaka ameshukuru Vodacom kwa kutoa msaada huu na kudai kuwa utasaidia wasichana wengi kupata elimu ya afya hususani kuhusiana na suala la hedhi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zake pia utaweza kupata taarifa Zaidi kuhusiana na ukubwa wa tatizo hili ambalo liko nchini pote.
Takwimu zilizopo juu ya tatizo hili kutokana na utafiti uliofanyika  mwaka 2010 zinabainisha kuwa wasichana wapatao 68,538 wamekatiza masomo yao kutokana na  changamoto za hedhi ambao ni asilimia 75 ya  wanafunzi watoro mashuleni.

Mbali na msaada huu,Vodacom Foundation imeishatumia Zaidi ya shilingi 378 katika mradi wa Hakuna Wasichoweza kati ya mwaka 2014-2015 ambao unaendelea katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco,Dkt Moshi Kimizi(katikati)na Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania,Diana Kisaka(kushoto) wakimsikiliza Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehimbiza(kulia) wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo(hawapo pichani)katika hafla ya Uzinduzi wa kampeni ya Ujumbe Mfupi(SMS) kwa Njia ya Simu za mkononi kupitia mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaotoa elimu bora ya kujisitiri kwa wasichana wakati wa hedhi na Usafi kwa mtoto wa kike ambayo huwafanya wasichana kukosa masomo yao mara kwa mara.
 Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania,Diana Kisaka(kushoto)na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehimbiza(kulia) wakimshuhudia Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco,Dkt Moshi Kimizi(katikati)akibofya kitufe cha kompyuta kuashiria Uzinduzi rasmi wa kampeni ya Ujumbe Mfupi(SMS) kwa Njia ya Simu za mkononi kupitia mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaotoa elimu bora ya kujisitiri kwa wasichana wakati wa hedhi na Usafi kwa mtoto wa kike ambayo huwafanya wasichana kukosa masomo yao mara kwa mara.Hafla hiyo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam. 
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco,Dkt Moshi Kimizi(katikati)akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile,Freddie Manento(wapili kushoto) wakati wa hafla ya Uzinduzi wa kampeni ya Ujumbe Mfupi(SMS) kwa Njia ya Simu za mkononi kupitia mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaotoa elimu bora ya kujisitiri kwa wasichana wakati wa hedhi na Usafi kwa mtoto wa kike ambayo huwafanya wasichana kukosa masomo yao mara kwa mara,Wanaoshuhudia kushoto Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania,Diana Kisaka na  Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehimbiza(kulia)
Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu, Afya, wafanyakazi wa T-Marc Tanzania na Vodacom wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Uzinduzi wa kampeni ya Ujumbe Mfupi(SMS) kwa Njia ya Simu za mkononi kupitia mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaotoa elimu bora ya kujisitiri kwa wasichana wakati wa hedhi na Usafi kwa mtoto wa kike ambayo huwafanya wasichana kukosa masomo yao mara kwa mara.

WAZIRI, MPANGO, MWAKYEMBE, JAJI MKUU OTHMAN CHANDE WAIKALIA KIDETE FEDHA YA MAHAKAMA YA SH.BILIONI 12.3 YA AHADI RAIS DK. JPM

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Fedha na Mipango,Dk.Philip Mpango,Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe pamoja na Jaji Mkuu, Othman Chande wamekutana kwa ajili ya fedha ya Sh.bilioni 12.3 iliyotolewa na Rais John Pombe Magufuli juu ya uendelezaji wa miundombinu ya mahakama nchini pamoja na uendeshaji wa kesi mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Jaji Mkuu Othman Chande mbele ya mawaziri wa wawili, amesema fedha hiyon itakwenda katika maeneo ya utengenezaji wa miundombinu ya mahakama ili wanannchi waweze kupata haki katika vyombo vya sheria.

Jaji Mkuu, Chande amesema kuwa michoro ipo tayari kwa ajili ya ujenzi wa mahakama za mwanzo na wilaya ambazo hazina pamoja na mikoa ambayo hazina mahakama kuu.

Amesema adhima ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha wananchi wanapata haki pale wanapotaka katika vyombo vya sheria isiwe kikwazo cha kukosekana kwa mahakama katika eneo husika.

Nae Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema kuwa hundi iliyotolewa jana tayari fedha hiyo imeingizwa katika akaunti ya mahakama ziweze kuanza kazi yake iliyokusudiwa.

Kwa upande wa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwan fedha hiyo itasukuma ujenzi wa miundombinu ya mahakama ili wananchi waweze kupata haki.

Amesema hatua za ujenzi wa Mahakama ya Wahujumu Uchumi na Wala Rushwa nao uko katika hatua nzuri lakini kwa fedha hiyo ni kwa ajili uboreshaji wa miundombinu ya mahakama.
 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kuipatia Mahakama kiasi cha shilingi Bilioni 12.3 zitakazotumika  katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya Mahakama na ujenzi wa Mahakama mpya katika maeneo mbalimbali nchini. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto).
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu Serikali kuendelea kushirikiana na Mahakama ya Tanzania ili kuwezesha ufanisi wa shughuli zake.

Mzungu Kichaa releases ‘RELAX YOUR MIND’ new East African reggae video

$
0
0
The Tanzanian based singer, Mzungu Kichaa, has released a bonafide reggae tune: RELAX YOUR MIND. The new video features his Tanzanian band Bongo Beat in true show for their renowned eclectic high-energy African style that has become their signature.

Mzungu Kichaa says, “It was important for me to get some of the magic that has developed during live-concerts onto a recorded track and I think we managed to do that on this song. The bridge, which goes “set the night on fire” was developed on stage during a late night performance at Operaen in Christiania during one of our tours in Denmark. 

The song was recorded in a studio in Denmark while we were on tour. So I guess this process really represents our journey as a band and the positive energy we have received from our audience. An energy that we want to share with the world through this video….”

Relax Your Mind was shot on location in Dar es Salaam and features a number of Mzungu Kichaa´s long standing crew, some of which are family. They include Director of Photography (DOP) Adam Juma, Video Director Rita Wachera, Artistic Director Jessica Olsen and Producer Louise Kamin.

MBUNIFU WA MAVAZI AMINA DESIGN ATOA MADA KUHUSU FAIDA ZA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA ZANZIBAR

$
0
0
Mbunifu wa Mavazi Amina  Plummer Akitoa Mada kwenye Semiana ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Zanzibar yenye Lengo la Kuwafundisha Mbinu Mbalimbali za Biashara pamoja na Matumizi Sahihi ya Vipodozi Pendwa vya Luvtouch.

Mbunifu wa mavazi Amina Plummer amewaasa wanawake wa zanzibar kujikita kwenye ujasiriamali kwa kuwa ndio njia pekee ya kumkomboa mwanamke.amesema ajira nyingi zimekuwa na ubaguzi na pili ni nafasi chache sana zinatolewa kwa wanawake hivyo basi wanawake hawana budi kujikomboa kwa njia ya ujasiriamali.mama amina alisema hayo wakati akitoa mada alipowatembelea wanawake wa zanzibar walioniufaika na mradi wa manjano dream makers ulio chini ya taasisi ya manjano foundation yaliomalizika kwenye hotel ya mtoni marine zanzibar.
Mbunifu wa mavazi Amina Design akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser Pamoja wa Baadhi ya wasaidizi Kutoka Taasisi ya Manjano Foundation.

Akieleza Zaidi Mama Amina Plummer Ambaye  ni Mbunifu wa Mavazi amewaomba wanawake wa Zanzibar Kupenda Ujasiriamali kwa Kuwa ni Kazi Pekee ambayo kadiri Unavyoifanya kwa Juhudi na Maarifa Pia  inasaidia Kuongezeka kwa Kipato cahako.Hivyo wakina mama wa Zanzibar hawana Budi Kuchangamkia nafasi hiyo ya kujifunza Ujasiriamali Kutoka Taasisi Ya Manjano Foundation.
Washiriki wa Semina Hiyo kutoka  Visiwani Zanzibar wakisikiliza kwa Makini Mda zilizokuwa zikitolewa kwenye Mafunzo hayo.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII PROF. JUMANNE MAGHEMBE AZUNGUMZIA TUKIO LA KUSHAMBULIWA HELKOPTA YA DORIA ILIYOPELEKEA KIFO CHA RUBANI WAKE.

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo tarehe 09/02/2016 katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu ya Wizara hiyo kuzungungumzia tukio la hivi karibuni (tarehe 29 Januari 2016) la kushambuliwa kwa helkopta ya doria na kuuawa Rubani Rogers Gowel Raia wa Uingereza. Katikati ni Naibu Waziri Maliasili na Utalii Eng. Ramo Makani na Katibu Mkuu Wizara hiyo Maja Gen. Gaudence Milanzi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, INSPEKTA Jenerali (IGP), Ernest Mangu, kulia akifafanua moja ya jambo katika Mkutano huo. Kulia ni Waziri wa  Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe.
 Baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Maliasili walioshiriki mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Bw. Herman Keraryo. 
Waandishi wa habari wakichukua matukio ya mkutano huo na baadhi ya washiriki wakifuatilia.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
(Picha na Hamza Temba - Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii)

NMB Yawafikia wakazi wa Turiani, Yakabidhi madawati kwa shule ya Msingi Mtibwa

$
0
0
Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati 60 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa shule ya Msingi Mtibwa iliyo katika kata ya Turiani – Mvomelo mkoani Morogoro. Huu ni mwendelezo wa benki kujali wateja na jamii inayozunguka matawi yake huku ikiamini kuwa ni kupitia jamii ndipo wateja wake wengi wanapotoka, kwa hiyo kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ni utamaduni waliojiwekea.

Kwa mwaka huu – 2016 NMB imepanga kutumia zaidi ya Shilingi Bilioni 1 kusaidia jamii katika Nyanja za elimu na afya pamoja na kusaidia vipaumbele vilivyowekwa na serikali kwenye elimu ikiwa ni pamoja na Tehama na maabara kwa shule za msingi na sekondari.
Meneja wa Tawi la NMB Turiani akikabidhi madawati kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Mtibwa - Enock Kagonji huku Mwanafunzi wa darasa la sita Nasma Seif akishuhudia tukio hilo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtibwa wakiwa wamekalia madawati waliyopewa na NMB


ASILIMIA 10 YA WATANZANIA WANAMILIKI UCHUMI WA NCHI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji ili kufikia lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi. 

“Taarifa zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa nchi na sera hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujenga na kufaidika na uchumi wa mchi yao,” alisema.

Waziri Mkuu amesema maeneo yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya haraka na yanayogusa maisha ya wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu, ujenzi, biashara, utalii, madini, viwanda na usafirishaji.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Alisema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe. Waziri Mkuu pia alizindua Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu, Bibi Jenista Mhagama alisema hadi sasa mikoa 20 imekwishatenga maeneo ya uwekezaji kwenye halamhashauri zake  na imeanza kuweka miundombinu ya kuvutia wawekezaji.

Naye Mweyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Prof. Omari Issa alisema katika dunia ya sasa imebainika kuwa haina maana kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia masoko au kumuunganisha wadau wa masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia Watanzania kwa kuwaunganisha na masoko.

MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YAZUKA TENA WILAYANI MVOMERO,MBUZI ZAIDI YA 70 ZAKATWA KATWA MAPANGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati ya drafti),ikiwemo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro sambamba na wananchi wakishuhudia tukio la mgogoro wa Wakulima na Wafugaji,ambapo takribani mbuzi zaidi ya 70 wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba ametembelea Kijiji cha Kigurukwa mjini Morogoro kulikotokea mapigano ya Wakulima na Wafugaji yaliyosababisha kuuawa kwa mbuzi  na Kondoo zaidi ya 70.Waziri Mwigulu ameagiza Kamati ya Ulinzi ya Mkoa kuhakikisha wote waliohusika katikla tukio hilo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Pia ameagiza kutekelezwa haraka hukumu ya mahakama iliyotolewa mwaka 2005 iliyoagiza kuwekwa kwa mipaka kati ya eneo la wafugaji na wakulima.

 Baadhi ya Mbuzi waliokatwa katwa na mapanga .
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba akiongozwa na wafugaji kabila la Wamasai kufuatia mgogoro wao na Wakulima na kupelekea uharibifu mkubwa wa kuuwawa kwa wanyama zikiwemo mbuzi zaidi ya 70.  
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba sambamba na Mbunge wa jimbo la Mvomero Mh Sadick Murad (mwenye shati la drafti),wakiwemo na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mvomero na wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio la kuuwawa kwa mbuzi zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana,ambapo Waziri huyo ameahidi sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvui Mh.Mwigulu Nchemba akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero katika kijiji cha Kigurukwa mkoani Morogoro kufuatia mgogoro mkubwa kuzuka kati ya Wakulima na wafugaji,ambapo inaelezwa kuwa katika tukio hilo mbuzi  na kandoo zaidi ya 70 wakiwa wamekatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana.Waziri Mwigulu Nchema ameahidi  kuwa sheria na hatua za kudumu za tatizo hilo kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

UONGOZI WA KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL) LASITISHA HUDUMA YA TRENI YA JIJI MAARUFU KAMA TRENI YA MWAKYEMBE.

$
0
0
Shimo katika tuta la reli  eneo la Buguruni kwa Mnyamani  ambalo limesababishwa na mvua inayoendelea kunyesha hapa nchini ambapo ukarabati wa eneo hilo unaendelea ili kufanikisha usafiri kurejea hapo kesho.


KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL)
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa huduma ya treni ya jiji maarufu kama Treni ya Mwakyembe awamu ya jioni ya leo Februari 09, 2016. 

Taarifa imefafanua kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na maji ya mvua kuchimba shimo kubwa katika tuta la reli karibu na stesheni ya Buguruni kwa Mnyamani.

Uharibifu huo uligundulika leo asubuhi mara baada ya treni kupita eneo hilo ikielekea stesheni ya Dar es Salaam.wakati wa safari yake ya kwanza kutoka Kituo cha Ubungo Maziwa.

Tayari mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio wakiendelea na kazi ya ukarabati na kwamba inatarajiwa huduma hiyo itarejea tena hapo kesho kama kawaida.

Atakayesoma taarifa hii amuarifu mwenziye.
Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,



Nd Masanja Kungu Kadogosa
Dar es Salaam,
Februari 09, 2016.

Rais Magufuli ampa pole mama Tunu Pinda

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425



OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za pole Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda aliyepatwa na ajali ya gari, iliyotokea jana tarehe 08 Februai, 2016 akiwa safarini kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkundi lililopo katika Manispaa ya Morogoro ambapo gari aliyokuwa akisafiria Mama Tunu Pinda, ilipinduka baada ya kumgonga mwendesha pikipiki aliyeingia ghafla barabarani.

Katika salamu hizo alizozituma kupitia kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko taarifa za kutokea kwa ajali hiyo na amemuombea Mama Pinda na Majeruhi wengine kupona haraka.

"Kupitia kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda, naomba unifikishie pole nyingi kwa mkeo Mama Pinda kwa kuumia katika ajali hii, na namuomba Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi wote ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku" alisema Rais Magufuli.

Mama Tunu Pinda anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es salaam, na hali yake inaendelea vizuri.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
09 Februari, 2016

TPDC yakanusha taarifa iiliyochapishwa kwenye Gazeti la Mtanzania la Jumapili tarehe 7 Februari 2016

$
0
0
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), linapenda kuchukua fursa hii kukanusha taarifa iiliyochapishwa kwenye Gazeti la Mtanzania la Jumapili tarehe 7 Februari 2016 Toleo Na: 8087 lenye kichwa cha habari ‘TPDC kwafukuta’.  Taarifa hii si sahihi na ina lengo la kulichafua Shirika na kuupotosha umma wa Watanzania.

TPDC ni Shirika la Umma, linalomilikiwa kwa asilimia mia moja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo taratibu za kuliendesha Shirika hufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi. 

Hii ina maana kwamba, taratibu za kupata Kampuni ya kufanya Utafiti wa Vitalu vya mafuta na gesi kwa kutumia teknolojia ya ‘Airborne Gravity Gradiometry’   ilifuata sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 pamoja na kanuni za manunuzi ya umma za mwaka 2013. 

Aidha, tungependa kuwafahamisha watanzania kwamba taarifa iliyotolewa na gazeti la Mtanzania zilikuwa zina lengo la kupotosha umma kwani zoezi zima la kutafuta mkandarisi lilikuwa la wazi na lilihusisha kampuni tatu ambazo ni Bell Geospace ya Marekani, CGG ya Ufaransa na ARKEX ya Uingereza ambazo ndizo kampuni pekee zenye uwezo wa kutumia teknolojia tajwa hapo juu. 

Kutokana na kuwepo kwa kampuni tatu tu hapa dunia zenye utaalamu uliohitajika, Shirika liliwasiliana na kampuni husika kwa mujibu wa kanuni ya manunuzi  ya umma ya mwaka 2013 namba 152(1) (b) ili kuwasilisha taarifa za kiufundi na kifedha  kwa TPDC.

Baada ya taratibu hizo za manunuzi kufanyika, ndipo kutokana na tathimini iliyofanyika, Kampuni ya CGG ndiyo iliyopewa kazi ya kufanya utafiti maeneo yafutayo; Eyasi – Wembere iliyopo Manyara, na Mandawa Mkoani Lindi wakati Lake Tanganyika North iliyopo Kigoma, ilifanywa na kampuni ya Bell Geospace. 

“Airbone Gravity Gradiometry” ina gharama nafuu, inachukua eneo kubwa la utafutaji na kwa kipindi kifupi sana. Ni aina ya teknolojia inayotafiti maeneo mapya ya utafutaji na yale ambayo tayari yameshaonyesha dalili nzuri za utafutaji wa hapo awali. Imechukua miezi mitatu tu kwenye maeneo tajwa hapa nchini kukamilisha kazi ya kukusanya data.

TPDC inakanusha vikali kuwepo kwa shinikizo toka kwa Mtu au Taasisi yoyote katika kufanikisha zoezi hili, aidha Shirika linasisitiza kuzingatiwa kwa utaratibu wa sheria za manunuzi na hivyo kuwataka Watanzania kupuuza taarifa hizi zilizotolewa na gazeti la Mtanzania kwani ni za uzushi na upotoshaji mkubwa.

Tunawaomba wadau wote wa sekta ndogo ya mafuta kuendelea kufanya kazi za utafiti, utafutaji na uendelezaji wa sekta nzima ya gesi asilia.

“Gesi Asilia kwa Maendeleo ya Taifa”

Imetolewa na:
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji
Shirika la Maendeleo ya Petroli ya Tanzania
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images