Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1119 | 1120 | (Page 1121) | 1122 | 1123 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Hatimaye Alikiba ametoa wimbo wake “Lupela” uliokuwa ukisubiriwa na mashabiki wake Afrika Mashariki kwa wiki kadhaa sasa. Wimbo huo ni sehemu ya kampeni ya “Ujangili Unatuumiza Sote” iliyozinduliwa mwaka jana na WildAid na African Wildlife Foundation mashirikia yanayofanya kazi pamoja barani Afrika na Asia kupunguza mahitaji ya bidhaa zitokanazo na wanyamapori na kuongeza uelewa wa janga la ujangili linaloikabili Afrika. Video ya wimbo huo imerekodiwa jijini Los Angeles Marekani ambapo Alikiba alikuwa mgeni rasmi kweye hafla maalum iliyoandaliwa na shirika la uhifadhi wanyamapori la kimataifa la WildAid. Chini ya kauli mbiu “Ujangili Unatuumiza Sote”, Alikiba amefanya kazi na WildAid kuongeza uelewa wa Watanzania kuhusu tatizo la ujangili wa tembo ambao wamechinjwa kwa maelfu miaka ya hivi karibuni kwa ajili ya meno yao.
  Katika uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es salaam, wageni mbalimbali na waandishi wa habari walipata fursa ya kuusikiliza wimbo na kuangalia video yake kwa mara ya kwanza. "Tunaona fahari sana kuwa na Alikiba kama Balozi wa WildaAid”, alisema Salome Gasabile Meneja wa WildAid Tanzania. “Katika mwaka mmoja uliopita, yeye na meneja wake Seven wamefanya kazi bila kuchoka kupinga ujangili wa tembo na tunaamini wimbo huu utakuwa na faida kubwa katika vita dhidi ya ujangili”. “Nina furaha kubwa kuwa sehemu ya mradi huu. Naamini kila mara watu wakisikiliza wimbo huu watakumbuka faida ya tembo kwa urithi na uchumi wa bara la Afrika. Wanaingiza pesa nyingi kupitia utalii na fedha hizo zinaweza kusaidia kuleta ajira, kujenga shule na hospitali kwenye jamii zinazozunguka hifadhi za taifa,” alisema Aleya Aleya Janell ambaye ameshiriki kwenye video ya wimbo huo kama Lupela.
  Asha Franklin, aliyeshiriki kama tembo wanaocheza muziki amefanya kazi na Rihanna na Ciara katika video mbalimbali amesema “Hii video ni nzuri kwani imechanganya burudani ya muziki na jambo zuri kwa jamii” Ushiriki wetu kama tembo wananocheza muziki ilikuwa ni ubunifu wa hali ya juu lakini pamoja na kwamba ni burudani bado unaweza kuona faida ya kubwa ya wimbo huu.” Video hiyo iliongozwa na Kevin Donovan, huku ikirekodiwa na kutengenezwa na muandaaji filamu maarufu wa Hollywood Brian Rumsey ikiwa ni mchango wake kwa kampeni hiyo. Oththan Burnside, ambaye ameishafanya kazi na wanamuziki wengi maarufu kama Rihanna na Sean Paul alihusika kuandaa wimbo huu na staili ya uchezaji wa tembo.
  “Tuufanye mwaka 2016 mwaka wa tembo – mwaka ambao hatimaye tutakumbuka kuwa hatimaye tuikomesha ujangii wa tembo na kuwapa tembo nafasi ya kuishi” alisema Burnside. “Tusaidie kuokoa maisha ya wanyama hawa wazuri,” alisema Burnside. Kwa mujibu wa shirika la WildAid wimbo huo hautatumika kibiashara na unapatikana bure kwa mashabiki kupakua au kusikiliza kweye mtandao wa www.yearoftheelephant.org Uzinduzi wa wimbo huo umeenda sambamba na kampeni ya #jointheherd inayofanyika kupiti mitandao ya kijamii ikiongozwa na wau maarufu mbalimbali wakiwemo muigizaji Lupita Nyong’o, Jackie Chan na Jacqueline Mengi ambao wanaendelea kuhamasisha watu kupitia www.yearofthelephant.org ambapo watu huweza kujitengenezea picha zao na kuzitumia kwenye mitandao ya jamii.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa barabara za mzunguko (ring roads) zenye lengo la kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji la Dar es Salaam utakamilika baadae Mwezi Juni mwaka huu.

  Amesema kufuatia Serikali kuanza kulipa madeni ya makandarasi amewataka makandarasi wote kurudi kazini ili kufikia lengo la Serikali la kukamilisha barabara hizo mwezi juni sambamba na ulipaji wa madeni yote.

  “Tunawaomba wale wenye nyumba pembeni mwa barabara za mzunguko ambao wapo kwenye orodha ya kulipwa fidia waondoke maeneo hayo ili kuruhusu kazi ya ujenzi wa barabara kuendelea”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa.

  Waziri Prof. Mbarawa amekagua barabara za Tankibovu - Goba (km9), Goba – Mbezi Mwisho (Km7), Kimara Baruti – Msewe - Chuo Kikuu (km2.6), Mbezi Mwisho – Malambamawili – Kifuru - Kinyerezi (km14), na Tabata Dampo - Kigogo (km1.6).

  Barabara hizo zenye urefu wa Km 27.2 zimejengwa kwa gharama ya takriban sh. bilioni 56.3 ikiwa ni gharama za ujenzi na fidia ambazo zote zinalipwa na fedha za mfuko wa barabara.

  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale amewataka madereva kulinda barabara hizo kwa kutoegesha magari katika maeneo yasiyoruhusiwa na kukemea vitendo vya uchimbaji mchanga pembeni mwa madaraja.

  Waziri Prof. Mbarawa pia amekagua ujenzi wa daraja la Kinyerezi lenye urefu wa mita 40 lililojengwa kwa gharama ya sh. Bilioni 2.3 ambao ujenzi wake umekamilika.

  Barabara za mzunguko jijini Dar es Salaam zinajengwa kwa kiwango cha lami ili kuvutia magari mengi kutumia barabara hizo na kupunguza msongamano katikati ya jiji ambapo hadi sasa Km 27 zimekamilika na Km 28 zinaedelea kujengwa.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, 
  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia), akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (wa tatu kulia), huku Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es Salaam Eng. Julius Ndyamukama akifatatilia maelezo hayo.

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akifafanua hatua za Serikali za kuhakikisha ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dar es Salaam unakamilika mwezi juni mwaka huu.

   Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Dar es Salaam Eng. Julius Ndyamukama akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Kimara - Baruti – Msewe – Chuo Kikuu yenye urefu wa Km 2.6.

   Muonekano wa daraja la kinyerezi lenye urefu wa mita 40 ambao ujenzi wake umekamilika

  Muonekano wa Barabara ya Tankibovu-Goba inayojengwa kwa kiwango cha Lami kama ilivyokutwa leo mchana.


  0 0

   Mjumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe Prosper Mbene (MB) akifafanua jambo wakati wa Kikao cha Mafunzo cha Kamati hiyo ilipokutana na Sekta inayosimamiwa na wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti Mhe Hawa Ghasia (MB) akiongoza kikao cha Kamati hiyo wakati wa mafunzo ya wiki moja kwa kamati hiyo jijini Dar es Salaam.
   Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara Mhe. Vicky Kamata (MB) akiongoza kikao cha Kamati hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia  kwake ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Charles Mwijage (MB).
   Naibu waziri wa TAMISEMI Mhe Selemain Jaffo (MB) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Hesabu za serikali wakati wa kikao cha Kamati ilipokutana kwa ajili ya mafunzo kuhusu majukumu ya wizara ya TAMISEMI jijini Dar es Salaam.
  Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt Tulia Ackson (MB) akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea Kamati za Kudumu za Bunge ambazo zipo katika mafunzo kuhusu maeneo yao ya kazi jijini Dar es Salaam.
  Picha na Ofisi ya Bunge


  0 0

  Greetingz Everybody!
  All good?
  Well, tuanze na hii  “WALK IT OFF ” ya FID Q feat TAZ.....
  Sio kawaida ya kuwatumia ngoma ambayo haijafanyika TONGWE RECORDS lakini naomba nifanye hivi kwa mara ya kwanza kwa kuwa huyu jamaa ni mvivu mno wa kufanya Video.....Na pia ni  Swahiba wangu sanaa...
  WALK IT OFF.. 

  Sincerely
  Jay-murder .a.k.a Mkombozi wa Hip-hop

  0 0
 • 02/09/16--08:52: SYDS Bariadi Albinism Report
 • 0 0
 • 02/09/16--08:55: Article 2


 • 0 0

  Hello, 
  My name is Andrea and I was born 1963 in Magdeburg, GDR. My birth name was Andrea Uhlig, daugther of Roland and Inge-Lore, sister of Ralf-Michael. when I was a school-child, in the mid seventies, our family often visited by a woman from Dar es salaam/ Tanzania. 
  Her name was Ndeana Mamkwe.
  She was there in the GDR to continuing education as teacher I think. .... Now I am looking for the woman and I found the name of Ndeana Mamkwe in your blog. 
  Is she your mother or another related person from you ??
  As I could see, were you in Germany, maybe can speak/ write german and you know something about Ndeana and can help me to greet her. 

   Thank you very much!! 
   Andrea Klug 
   jamklug@aol.com

  0 0


  0 0

  Balozi wa Cuba nchini, Copez Tomo, akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akirekodi mambo muhimu kwenye 'diary' yake wakati wa mazungumzo na Balozi wa Cuba nchini, Copez Tomo aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Uturuki nchini, Bi. Yasemin Fralp (katikati) akizungumza jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alipomtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo yenye lengo la kuboresha mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki.

  0 0

  MWIMBAJI nguli wa nyimbo za Injili hapa nchini, Upendo Nkone pia amethibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi mwaka huu katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

  Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex Msama Nkone ameungana na wenzake waliothibitisha kushiriki tamasha hilo, Rose Muhando na Bonny Mwaitege waliothibitisha wiki iliyopita.

  Msama alisema hivi sasa kamati yake inaendelea na mchakato wa maandalizi ya tamasha hilo ambalo linatarajia kuanzia Geita (Machi 26), Mwanza (Machi 27) na Kahama (Machi 28).

  "Tunaendelea na mchakato wa kufanikisha Tamasha la Pasaka 2016 ambalo litakuwa ni la aina yake kwa sababu linatarajia kutoa ujumbe wa neno la Mungu kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa hasa mauaji ya walemavu wa ngozi 'albino'," alisema Msama.

  Aidha Msama alisema Tamasha la Pasaka lina malengo ya kufanikisha kuwasaidia wenye uhitaji maalum ambao ni pamoja na yatima, walemavu na yatima ambao husaidiwa kupitia tamasha hilo.

  Msama alitumia fursa hiyo kuwataka wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi kwa lengo la kufanikisha matakwa ya wenyer uhitaji maalum.

  0 0

   Lori la Mizigo lenye namba za usalili T 493 DBR limepiga mweleka na kuangukia basi la abiria aina ya Toyota DCM lenye namba za usajili T 104 BCT lifanyalo safari zake kati ya Gongo la Mboto mpaka Simu 2000 mapema leo asubuhi katika makutano ya barabara ya Tabara na Mandela, jijini Dar es salaam. Hakuna aliepoteza maisha kwenye ajali hii ila kuna watu kadhaa wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa matibabu.
   Linavyoonekana Lori hilo baada ya kupiga mweleka leo.
   Lionekavyo Daladala hilo baada ya kungukiwa na Lori hilo.
  Sehemu ya Mashuguda.

  0 0
 • 02/10/16--02:14: BEI YA MADAFU LEO


 • 0 0

  Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitambulisha mpambano wao utakaopigwa siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa katikati ni kiongozi wa ngumi Antony Rutta.
  Kiongozi wa mchezo wa masumbwi nchini Antony Rutta katikati akiwainua mikono juu kuwatambulisha mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa pasaka katiku uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
  Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli mbele ya waandishi wa habari katikati ni kiongozi Antony Ruta wa pili kushoto ni Dei Miyeyusho na mwingine ni kocha Cristopher Mzazi wakati wa kutangaza mpambano wa mabondia hawo siku ya Pasaka .

  MABONDIA Fransic Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wamesaini mkataba wa makubaliano wa kuzipiga siku ya sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam

  akizungumzia mpambano uho mratibu wa mabambano hayo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa amewasainisha mabondia hawo kwa kuwa viwango vyao vipo juu sana katika kipindi hiki na ndio mpambano utakaokuwa kama ndio mkali wa kufungua mwaka 2016

  aliongeza kwa kusema mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo mabondia mbalimbali watazipiga siku ya pasaka

  Mohamed Matumla atavaana na Cosmas Cheka wakati mabondia Mada Maugo atavaana na Abdalla Pazi katika mpambano wa nani zaidi kati yao pia bondia Vicent Mbilinyi atavaana na Mwinyi Mzengela na Pius Kazaula wa Morogoro atamenyana na Seba Temba

  Super D amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuja kwa wingi kushudia mpambano uho ambao utakuwa na msisimko wa aina yake vilevile wamepanga kuanza ngumi hizo mapema ili wapenzi wawai kurudi majumbani kwa na kujumuika na familia zao katika sikukuu hiyo hivyo ameomba mashabiki kufika mapema ili ngumi nazo zianze kwa wakati na kumalizika kwa wakati.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii.
  Naibu Waziri Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) akiwa katika mkutano wa wafanyabiashara nchini jijini Dar es salaam kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii. Kushoto ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alfayo Kidata.
  Makamu Mwenyekiti wa TPSF Salum Shamte (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na wafanyabiashara nchini kuhusu Serikali inavyoshirikiana na sekta binafsi katika kuinua uchumi wa nchi ili kuweza kuwahudumia wananchi katika kupata huduma za jamii. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.


  0 0

  Ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) imetolewa leo, ambapo jumla ya timu 16 zinakutana katika hatua hiyo (16 bora) itakayoanza kutimua vumbi wikiendi ya Februari 26-1 Machi 2015 katika viwanja mbalimbali nchini.

  Michuano hiyo iliyoshirikisha jumla ya timu 64 kutoka ngazi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili, inaingia katika mzunguko wa nne huku kukiwa na timu kutoka katika ngazi zote za ligi za TFF nchini.

  Ijumaa tarehe 26 Februari kutachezwa michezo miwili ambapo, Ndanda FC watawakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, huku Coastal Union wakiwa wenyeji wa wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

  Jumamosi, Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex - Shinyanga, Jijini Mbeya Tanzania Prisons watacheza na mshindi kati ya Mbeya City/Wenda FC kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

  Februari 28, michezo mitatu itachezwa, Simba SC watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Panone FC watacheza dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto African wakicheza na wachimba madini wa Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  Raundi hiyo itamalizika Machi 01, 2015 kwa mchezo mmoja kuchezwa ambapo Young Africans watawakaribisha JKT Mlale katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

  Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) mwaka huu ataiwakilisha Tanzania kwenye Mashindano ya kombe la Shirikisho Barani Africa (CAF CC) mwakani 2017.

  0 0


  NA K-VIS MEDIA Na Mashirikaya Habari

  HILARY Clincton, (Pichani juu), ambaye anaomba kuteuliwa na chama chake cha Democrat, kuwania kiti cha rais wa Marekani kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini humo, ameshindwa kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo na New Hamshire.

  Pia Mgombea wa chama cha Republican, “mbaguzi” Donald Trump, ameshinda kwenye mchujo wa uteuzi katika jimbo hilo la New Hamshire uliofanyika sambamba Jumanne usiku.
  Seneta wa Vermont Bernie Sanders, ndiye aliyemshinda Hillary Clinton, huku Trump, tajiri mkubwa kutoka New York, na ambaye amekuwa akiwashutumu wageni hususan Waislamu kuwa wanaleta “shobo” nchini humo yeye amewabwaga mahasimu wake wa karibu Gavana wa Ohio, John Kasich aliyeshika nafasi ya pili, Gavana wa Florida, Jeb Bush, Seneta wa Texas, Ted Cruz na Seneta wa Florida, Marco Rubio.

  Trump na Seneta Sanders wote wawili wamekuwa wakiwataka watu wapige kura dhidi ya watu ambao tayari wamekuwa kwenye mfumo wa utawala wa nchi hiyo.
  Clinton ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kwenye utawala wa sasa wa Obama, tayari amempongeza Bw Sanders, lakini akasema ataendelea kupigania kila kura kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumtafuta mgombea urais wa chama cha Democratic.
  Seneta Bernie Sanders (kushoto) na Tajiri Donald Trump

  0 0

  This year marks the 50th anniversary of bilateral relations between Switzerland and Tanzania. As part of the planned year-long anniversary events and celebrations, the Embassy of Switzerland is today hosting an Open Debate on Youth Employability at the Coral Beach Hotel in Dar es Salaam. 

  Nearly two thirds of Tanzania’s population is under 25 years of age. This presents a tremendous opportunity for human capital. To fully exploit this potential, it is essential to invest in the skills and education of youth. A recent study by International Labour Organization (ILO) reveals that 21.1% of youth (15 - 29 years) in the labour force in Tanzania are unemployed, a rate higher than in most sub-Saharan countries. 

  More than 800,000 young Tanzanians enter the job market each year, but only about 40,000 find formal jobs. The job market outlook for Tanzania is still negative, mainly because of the lack of skilled workers and the mismatch between skills supply and demand. Therefore, job creation is increasingly seen as a priority by all stakeholders.
  The debate looks at youth unemployment challenges and potential solutions in round table and plenary discussions with about 80 representatives from public and private sector, youth, civil society and international partners. 

  It also discusses key factors of successful labour market measures, including the Swiss dual system of education VPET (Swiss Vocational and Professional Education and Training). The Swiss VPET system – based on a close collaboration between private and public sector - enables two to four year apprentice trainings to young people, combining work experience at an enterprise together with practical and theoretical learning at vocational training colleges. 

  The debate is moderated by Aidan Eyakuze, Executive Director at Twaweza. Notable panelists include Mr. Hassan Mshinda, Director General at COSTECH; Ms. Mary Kawar, ILO Country Director and Mr. Mr. Thomas Katebalirwe, Ag. Director TVET, Ministry of Education, Science, Technology and Vocational Training. Other panelists include representatives from public and private institutions, NGOs and international actors. 
  The Embassy of Switzerland through its Development Cooperation already contributes together with the MasterCard Foundation to the SNV project “Opportunities for Youth Employment” (OYE), which aims at sustainably increasing youth employment and income through tailored technical, vocational and life skills trainings.

  Prior to the open debate, a Swiss delegation of Swiss Ambassadors and Heads of Cooperation from Southern and Eastern African countries have visited various places to learn more about the situation of youth employment in Tanzania. The delegation got introduced to the Buni Innovation Hub at COSTECH, a private sector employer that recruits VETA (Vocational Education and Training Authority) graduates, and participated in a youth meeting at the University of Dar es Salaam.

  0 0


  0 0

  Wagonjwa anaotibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) hivi sasa wanapata dawa kwa zaidi ya asilimia 96 kutoka kwenye maduka ya dawa yaliopo hospitali hapa.

  Mafanikio hayo yamekuja baada ya uongozi wa hospitali hiyo kuboresha mfumo wa Tehama katika utoaji na uagizaji dawa.

  “Wagonjwa wanaokosa dawa kwenye maduka yetu, hospitali inanunua haraka ili mgonjwa apate dawa kwa wakati. Kwa sasa ukosekanaji wa dawa hospitalini umepungua kwa kiasi kikubwa sana kutokana na kuimarisha utendaji ndani ya hospitali,” amesema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru.

  Hayo yamesemwa leo na Profesa Museru wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya hospitali hiyo katika siku 100 za Rais John Pombe Magufuli tangu alipochaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
  Profesa Museru amesema kwamba Katika muda wa kipindi cha miezi miwili Disemba 2015 na Januari 2016, hospitali imefanikiwa kulipa wafanyakazi malimbikizo ya madai yao ambayo walikuwa wakiidai hospitali hiyo kwa kipindi kirefu.

  Malipo hayo ni malipo ya on call, malipo ya wauguzi ya usiku, malipo ya posho mbalimbali hasa kwa madaktari pamoja na kada nyingine za afya ambazo zinashughulika moja kwa moja na wagonjwa.

  Amesema kwamba kutolipwa kwa malipo hayo kulishusha morali ya wafanyakazi kwa kiwango kikubwa na kupunguza kasi ya ufanyaji kazi na hivyo kusababisha kukosekana kwa tija katika utoaji wa huduma kwenye hospitali hiyo.

  Katika hatua nyingine, Profesa Museru amesema kwamba mapato kwenye hospitali hiyo yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 60 baada ya Disemba hospitali hiyo kuzalisha Shilingi bilioni 3.3 kutoka wastani wa shilingi 2.7 zilizokusanywa miezi mitano (Julai 2015 hadi Novemba 2015).

  “Mwezi  Disemba mwaka jana  tulizalisha shilingi bilioni 3.3 na Januari 2016 tulizalisha shilingi bilioni 4.3,” amesema mkurugenzi huyo.
  Akizungumzia mashine za CT-Scan na MRI, Profesa Museru amesema kwamba Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli ilinunulia Hospitali hiyo mashine mpya ya CT-Scan yenye uwezo wa 126 slices.

  “Uwapo wa mashine hii mpya umeongeza uwezo kwa kiwango kikubwa wa kupima wagonjwa wengi kwa wakati mmoja. Sasa tunaweza  kumpima mgonjwa mmoja tumbo na kifua kwa sekunde sita. Awali  tulikuwa tunapima wastani wa wagonjwa 20, lakini sasa tunapima wagonjwa wastani wa 50 ndani ya saa 24.

  “Baada ya kuwapo kwa mashine hizi mbili za CT-Scan, Hospitali haitegemei tena kukosekana kwa vipimo vinavyohitaji mashine hizi. Aidha mashine hii mpya ambayo ni ya kisasa zaidi na yenye nguvu kubwa imewezesha kufanya vipimo vya kiutalaamu zaidi hasa kwa upande wa viungo vya ndani kama moyo, utumbo, ubongo na hivyo kupata majibu sahihi ya chunguzi na uhakika zaidi. Mashine hii mpya tangu ilipofungwa Novemba 26, 2015 hadi Februari 9, 2016 imepima wagonjwa 863,” amesema Profesa Museru.

  Amesema kwamba baada ya mashine ya MRI kutengenezwa wagonjwa zaidi ya 2,200 wamepimwa na kwamba baada ya mashine ya CT-SCAN kutengenezwa wagonjwa zaidi 1,000 wamepatiwa vipimo.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mafanikio ya hospitali hiyo katika siku 100 za Rais John Pombe Magufuli tangu alipochaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
  Baadhi ya madaktari na waandishi wa habari wakimsikiliza Profesa Lawrence Museru leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku 100 za Rais Magufuli.

  0 0

  Na Lorietha Laurence-Maelezo
  SERIKANI imebaini wizi wa takribani shilingi Milioni 700 katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kupitia kampuni ya Wakala wa ukatishaji tiketi ya Salama World Travel iliyopo visiwa vya Komoro.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ,Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa ameeleza kuwa wizi huo umefanywa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa shirika hilo.

  “Kufuatia upotevu huo Serikali imechukua hatua thabiti ikiwemo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL Bw.Steven Kasubi ili kupisha uchunguzi utakaofanywa na kikosi cha polisi kitengo cha usalama mtandaoni ili kubaini mtandao mzima uliohusika ” alisema Prof.Mbarawa.

  Aidha aliongeza kuwa kwa utaratibu wa kawaida wa shirika hilo wakala anapewa ruhusa ya kuuza tiketi za ndege kuanzia kiasi cha shilingi milioni 15 tu na pale anapomaliza mauzo anarudisha fedha kwa shirika na baadaye kupewa ruhusa tena.

  Prof.Mbarawa anasema kwa sasa wameanza na shirika la Ndege la Tanzania kwa kwa lengo la kulifufua kwa kununua ndege mpya na kuwa na wafanyakazi wachapakazi na waadilifu.

  “Siku mbili zilizopita nilifanikiwa kukutana na menejimenti ya ATCL na kubaini mapungufu mengi na hivyo kuamua kuyafanyia kazi kwa kuhakikisha shirika hii linarudi kutenda kazi kwa udhabiti kwa kuwashughuikia wale wote wanaoenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma” alisema Prof.Mbarawa.

  Vilevile aliongeza kuwa Serikali imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kufanya uchunguzi kwa mawakala wengine wote wa Shirika hilo kubaini kama fedha za uuzaji wa tiketi hizo zinarudishwa kama inavyotakiwa.

  Prof.Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kuachana na wizi kwa njia ya mtandao kwa kuwa sheria ya mtandao iliyoanzishwa mwaka jana inatumika katika kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafikishwa katika mkondo wa sheria na kuchukuliwa hatua stahiki.

older | 1 | .... | 1119 | 1120 | (Page 1121) | 1122 | 1123 | .... | 3286 | newer