Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

HALMSHAURI YA WILAYA YA BUTIAMA YATOA UFAFANUZI WA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI MWIBAGI KUKOSA MAHALI PA KUSOMEA.

$
0
0
Na Nyakongo Manyama
Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Mkoani Mara imesema imepata ufumbuzi wa changamoto ya wanafunzi wa darasa la kwanza na awali Shule ya Msingi Mwibagi wilayani waliokosa mahali pa kusomea kwa kuwagawa wanafunzi hao kwa awamu mbili.

Hayo yamebainishwa leo (Alhamisi 04, Februari 2016), Afisa Elimu wa Wilaya hiyo, Hans Mgaya, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii, ambapo alikiri kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa madarasa shuleni kutokana na ongezeko la wanafanuzi walioandikishwa kuanza darasa la kwanza mwaka huu, ambapo hata hivyo tayari wameshachukua hatua mbalimbali za kukabiliana na tatizo hilo.

Aidha, Mgaya amesema kuwa jitihada za muda mfupi walizozifanya ni kuwagawa wanafunzi hao katika mikondo miwili ili waweze kubadilishana madarasa , mkondo mmoja utaingia asubuhi na mkondo mwingine mchana. 

Kwa mujibu wa Mgaya alisema jitihada za muda mrefu ni kujenga shule nyingine mpya ili kusaidia kuchukua wanafunzi wengi kwa wakati mmoja, ujenzi wa shule hiyo ulishaanza kabla ya tamko la elimu bure na tupo katika hatua ya awali ya ujenzi wa msingi wa madarasa hayo alisema Mgaya.

“wanafunzi walioandikishwa kujiunga na shule ya msingi kwa mwaka huu 2016 imeongezeka kwa kiasi kikubwa hivyo kusababisha idadi ya wanafunzi kuwa kubwa” alisema Mgaya.

Idadi ya wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza walioandikishwa kwa mwaka 2016 katika shule ya msingi Butiama kuanza masomo, ambapo hata hivyo zaidi ya wanafunzi 240 wa shule hiyo wanasomea katika chumba kimoja.

TASWIRA MBALI MBALI ZA HALI YA MAFURIKO KATIKA ENEO LA KIBAIGWA MKOANI DODOMA

$
0
0
 Kutoka na Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini, imepeleka kujaa maji katika eneo hili la Kibaigwa Mkoani Dodoma na kufanya magari kupita kwa shida katika Barabara kuu itokayo Morogoro kwenda Dodoma, kama ionekanavyo pichani.Picha na Othman Michuzi.
 Askari Polisi kwa kikosi cha Usalama Barabarani wakisimamia zoezi la upishanaji wa Magari katika eneo hilo, kutokana na uwingi wa maji yanayotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
 Magari yakilazimika kupita upande mmoja wa barabara.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI





Adjustment to the passenger train running schedules

RAIS MAGUFULI AZINDUA MWAKA MPYA WA KIMAHAKAMA KATIKA SIKU YA SHERIA DUNIANI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Mahakama katika Siku ya Sheria Duniani katika uwanja wa Mahakama mtaa wa Chimala eneo la Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 4, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Mahakama katika Siku ya Sheria Duniani katika uwanja wa Mahakama mtaa wa Chimala eneo la Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 4, 2016. PICHA NA IKULU.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI TAMISEMI, SIMBACHAWENE ATEMBELEA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF MJINI DODOMA LEO.

$
0
0
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene ametembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma Leo. Katika ziara hiyo mh. Waziri amepongeza jitihada za Mfuko kuongeza Wanachana kila mwaka pamoja na huduma bora zinazotolewa kwa wanachama hasa katika kulipa mapema madai ya wananchama.

Akiongea na watumishi wa Mfuko wa LAPF amepongeza jitihada za watumishi kwa utendaji wao mzuri unaopelekea utendaji bora wa Mfuko. Mh. waziri amepongeza uwekezaji unaofanywa na LAPF katika kuhakikisha Mfuko unakuwa endelevu . 

Pia ameahidi kushirikiana na Mfuko ili kuhakikisha unaendelea kufanya 
vizuri zaidi.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akisalimiana na kiongozi wa LAPF leo alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akisaini kitabu cha wageni leo alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pension wa LAPF  wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene alipotembelea ofisi za Mfuko huo mjini Dodoma.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chaweneakizungumza na wafanyakazi wa mfuko huo leo alipotembelea ofisi za Mfuko wa Pension wa LAPF mjini Dodoma.

SERIKALI YALAANI KITENDO CHA KUDHALILISHWA KWA MTANZANIA NCHINI INDIA

$
0
0

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali juu ya kitendo cha kushambuliwa na kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa kike wa Kitanzania nchini India. Hatua hizo ni pamoja na kikao chake na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sandeep Arya ambapo Serikali ilimtaka Balozi huyo kufikisha ujumbe nchini kwake wa kuwahakikishia ulinzi raia wa Tanzania waliopo India na kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo. Mkutano ulifanyika Wizarani tarehe 04 Februari, 2016.
Sehemu ya Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo. 
Mkutano ukiendelea.

Serikali ya Tanzania imesikitishwa na inalaani vikali kitendo cha udhalilishwaji alichofanyiwa mwanafunzi wa kike wa Kitanzania na Kundi la watu katika jimbo la Bangalore nchini India.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi alipokutana na Wandishi wa Habari kwa ajili ya kuwaeleza hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia kitendo hicho cha kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa Kitanzania nchini India.

Balozi Mwinyi alisema kuwa, hatua zilizochukuliwa ni pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini India kuiandikia Serikali ya nchi hiyo kuomba maelezo kamili kuhusu tukio hilo pamoja na kuitaka Serikali ya India kuwachukulia hatua za kisheria watu wote waliohusika pamoja na kuimarisha usalama katika maeneo wanayoishi wanafunzi wa Kitanzania. 

Aidha, Balozi Mwinyi alieleza kuwa amemwita Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Sandeep Arya na kumweleza masikitiko ya Serikali ya Tanzania kufuatia kitendo hicho cha kushambuliwa na kudhalilishwa kwa mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania.

Katika mazungumzo yao, Balozi Arya alieleza bayana kuwa Serikali ya India imesikitishwa na tukio hilo la udhalilishaji na kwamba Serikali imeahidi kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kutekeleza uovu huo.

Alisema kuwa Waziri Mkuu wa Jimbo la Bangalore aliongea na umma kuelezea masikitiko yake kuhusu uovu huo na kuahidi kuwa mamlaka za jimbo hilo zitaimarisha usalama katika maeneo yote wanayoishi wanafunzi wa Tanzania na raia wengine kutoka nje.

Balozi Arya aliihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa India inaheshimu ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na nchi yake, hivyo itashughulikia suala hilo kwa ukamilifu na hadi wakati huu tayari watu watano wanashikiliwa na vyombo vya usalama wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo. 

Sanjari na taarifa hiyo, Balozi Mwinyi aliwaomba Watanzania kutohusisha tukio hili la uhalifu na ajali ya Mtanzania, Bw. Christian Benjamin Mlyansi iliyotokea nchini India jana usiku na kusababisha kifo chake. Alisema kuwa Bw. Mlyansi alipata ajali ya kawaida alipokuwa anaendesha pikipiki ambapo ilipoteza mwelekeo na kugonga ukingo wa kati wa barabara.

SPECIAL OFFERS TO DAR AND MOMBASA FROM THE UK

$
0
0
DDC Global Logistics
    
KAZI NI KIPIMO CHA UTU

AIR CARGO TO DAR £4.00 INCLUSIVE CLEARANCE
AIR CARGO TO DAR £2.00 EXCLUSIVE CLARANCE

SEA CARGO TO DAR £2.00 INCLUSIVE CLERANACE

4X4 CARS TO DAR/MBS £820
SALOON CARS TO DAR/MBS  £720

40' CONTAINER TO DAR/MBS £1,600
20' CONTAINERS TO DAR/MBS £1,100

WE HERE TO MAKE CHANGES ON SHIPPING INDUSTRY

QUALITY SERVICES AT AFFORDABLE RATES

CALL US TODAY AT +44 1708524200  MOBILE +44 7913376799

UNIT 2 HARBOUR HOUSE, COLDHARBOUR LANE, RAINHAM. RM13 9YB

Factoring Promotion Conference Tanzania 2016


Tamko la Mtandao Wa Mabadiliko Ya Tabianchi Kuhusu Mapendekezo Ya Mpango Wa Maendeleo 2016-17.

JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA DAR ES SALAAM LASITISHA ULINZI SHIRIKISHI MJINI.

$
0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lasitisha shughuli za ulinzi shirikishi kwa muda usiojulikana katika vituo vya Polisi vya mjini kati kutokana na malalamiko na utendaji kazi ambao hauna tija kwa jamii.

Kauli hiyo imekuja baada ya kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam kuona mapungufu mbalimbali ikiwa na matendo yenye harufu ya rushwa, vikundi hivyo kutokufuata sheria na taratibu za ukamataji kwa kutumia nguvu kupita kiasi hata pale isipohitajika pamoja na utendaji mbovu.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Katazo hilo limesababisha kufungiwa kwa vikundi vya ulinzi shirikishi kwa muda usiojulikana  mpaka pale Jeshi la polisi litakapo lidhishwa na kuwapa mafunzo maalumu ya ukamataji wa bodaboda zinazovunja sheria za barabarani.

Pia Kamanda Sirro amesema kuwa limefanikiwa kukamata magari mawili yanayosadikiwa  kubeba vitu vilivyoibwa kwenye ofisi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)  magari hayo ni Toyota Noah yenye namba za usajili T 989 CNV  na Mitubish Pajero yenye namba za usajili T 386 CVV na kuwakamata walinzi wawili waliokuwa zamu kulinda siku hiyo katika jengo hilo.

"Katika wizi huo vitu vilivyoibwa ni Compyuta mbili, aina ya Dell pamoja na CPU, Monitor zake na Televisheni moja aina ya Sumsung inchi 40" Alisema Sirro.

Katika tukio jingine Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuokoa Tumbaku boksi 71 yenye thamani ya shilingi 150,000,000 mali ya Ahmed Huwel miaka 36 mfanyabiashara na mkazi wa Msasani Regent.

Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kukamatwa kwa magari mawili yaliyohusika katika wizi ofisi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

JUMUIYA YA MARADHI YA SARATANI ZANZIBAR YAAADHIMISHA SIKU YA SARATANI DUNIANI

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya maradhi ya saratani Zanzibar Dkt. Msafiri Marijani akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ya Jumuiya hiyo Mpendae ikiwa ni maadhimisho ya siku ya saratani duniani, kushotoni kwake ni Mkurugenzi wa Utumishi na uendeshaji Wizaraya ya Afya.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya maradhi ya saratani Zanzibar kwenye maadhimisho ya siku ya saratani Zanzibar.
Mkurugenzi wa Utumishi na uendeshaji Wizaraya ya Afya Zanzibar ndugu Omar Mwinyi Kondo akizungumza na waandishi katika maadhimisho ya siku ya saratani duniani yaliyofanyika Ofisi ya Jumuiya Mpendae, (kulia).

Billioni 60 zatengwa kufufua General Tyres Arusha

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO

Shillingi Billioni 60 zinategemea kutumika kufufua kiwanda ya matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha ambacho kimesharudi mikononi mwa Serikali, na fedha hizo zitatumila kurekebisha mitambo ya umeme ya kiwanda hicho na kupata mitambo mipya itakayoendana na teknolojia ya utengenezaji wa matairi duniani.

Akijibu swali la Mhe. Joshua Nassari Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) lililouliza ni lini serikali itafufua kiwanda cha matairi cha General Tyres kilichopo Jijini Arusha kwani ni tegemeo kwa ajira kwa wananchi wa Jijini la Arusha,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles John Mwijage amesema kiwanda hicho kimesharudi mikononi mwa Serikali na wako mbioni kukifufua ili kianze kufanya kazi ya kuzalisha matairi nchini.

“ Tumeanzisha viwanda nchi ili kuzalisha bidhaa na kutoa ajira kwa watanzania na sio kuwatesa wananchi kwa kukosa ajira au kuagiza bidhaa ambazo tunaweza kuzalisha hapa hapa nchini, hivyo basi Serikali kupitia Wizara yangu tutatenga fedha kwa ajili ya kufufua kiwanda hiki ili kianze kufanya kazi mara moja”

“ Sio tu tutafufua kiwanda cha General Tyres pekee bali tunafatilia viwanda vyote ambavyo vimekiuka sheria na kanuni kwa kutoviendeleza viwanda hivyo ili kuvirudisha mikononi mwa Serikali au kuwatafuta wawekezaji wengine watakaoweza kuviendesha viwanda hivyo” Alisema Mhe. Mwijage.

Aidha Mhe. Charles  John Mwijage amesema ni kweli makampuni mengi yaliyobinafsishwa hayakufanya vizuri katika uendeshaji wake ukiacha mifano ya makampuni machache yanayofanya vizuri yakiwemo Tanzania Breweries Limited (TBL),Morogoro Polyester 21st Century na Tanzania Cigarette Company Limited (TCC), hivyo Wizara yangu ikishirikiana na Msajili wa Hazina juu ya Viwanda ilifanya tathmini iliyoonesha kuwa mashirika mengi yaliyobinafsishwa hawakutekeleza mikataba ya mauziano kikamilifu.

Ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha makampuni yote haya yanazalisha kwa tija ili tupate bidhaa,kodi ya Serikali na ajira kwa wananchi wa Tanzania ili kutimiza adhma ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ya kuwa na Tanzania yenye viwanda kwa maendeleo ya taifa.

Serikali kupitia Wizara yetu inaboresha mazingira ya uwekezaji hali itakayowajengea imani kwa wawekezaji na kupelekea kupanua zaidi shughuli zao za kibiashara na pia kuendeleza mpango wa Viwanda vidogo na vya kati unaoshirikisha SIDO na Halmashauri za Wilaya na Mikoa ili kuanzisha Viwanda vya Mkoa vya kuongeza thamani ya bidhaa za Kilimo,Uvuvi na ufugaji kupitia njia hii ajira nyingi zitaongezeka na kupunguza tatizo la ajira nchini.

ORODHA YA MAWAZIRI VIVULI

$
0
0
ORODHA YA MAWAZIRI VIVULI;

1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI - Mhe. Jaffar Michael. 

2. Waziri wa Nchi Utumishi - Mhe. Ruth Molel. 

3. Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira - Mhe. Ally Saleh (Alberto).

4. Waziri wa Nchi, Sera na Bunge - Mhe. Ester Bulaya.

5. Waziri wa Fedha na Mipango - Mhe. Halima James Mdee.

6. Waziri wa Ujenzi - Mhe. James Francis Mbatia.

7. Waziri wa Nishati na Madini - Mhe. John John Mnyika.

8. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda - Mhe. Peter Msigwa.

9. Waziri wa Mifugo na Uvuvi - Mhe. Magdalena Sakaya. 

10. Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Mhe. Juma Hamad Omar. 

11. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi - Mh Godbless Jonathan Lema.

12. Waziri wa Ardhi - Mhe. Wilfred Lwakatare.

13. Waziri wa Maliasili na Utalii - Mhe. Ester Matiko. 

14. Waziri wa Viwanda na Biashara - Mhe. Anthony Calist Komu.

15. Waziri wa Elimu - Mhe. Suzan Limo. 

16. Waziri wa Afya - Mhe. Godwin Molel.

17. Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo - Mhe. Joseph Mbilinyi.

18. Waziri wa Maji na Umwagiliaji - Mhe. Hamidu Bobali.

19. Waziri wa Katiba na Sheria - Mhe. Tundu Antiphas Lissu.

Hapa hawajajumuishwa Manaibu Mawaziri Vivuli!

Imetangazwa na kiongozi rasmi wa upinzani bungeni hii leo.

TASWIRA MBALI MBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0


Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson akiongoza kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Naibu wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Ashatu Kijaji wakatiakitoa Taarifa ya Utendaji wa Soko la Bima Nchini kwa kipindi cha Mwaka unaoishia tarehe 31 Desemba,2014 wakati wa kikao cha 9 cha Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma.
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula kwenye jengo la Utalwala la Bunge mjini Dodoma Februari 5, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mbunge wa Simanjiro , James Ole Millya (kulia)kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 5, 2016. Katikati ni Mbunge wa longido, Onesmo Ole Nangole.

AFISA UHAMIAJI MKOA WA DAR ES SALAAM AKAMATWA KWA RUSHWA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA

Mkuu wa TAKUKURU (M) Ilala,

S.L.P 6420, Kinondoni

Simu : (022)2861088 Nukushi 2150047 

Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ilala imemkamata afisa wa ofisi ya uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma ya kuomba shilingi milioni 1 na kupokea Shilingi laki 5 kutoka kwa mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali mnamo tarehe 4 Februari, 2016.

Bw.Kiangwike Ngumba mwenye cheo cha afisa mkaguzi wa uhamiaji alikamatwa baada TAKUKURU kupokea taarifa kutoka kwa Bw.Bille Mohamed kuwa mtuhumiwa na maafisa wengine walifika katika eneo lake la biashara na kuchukua hati ya kusafiria ya ndugu yake kwa madai kuwa wanakwenda kuifanyia ukaguzi. Hata hivyo, baadaye afisa huyo alimtaka mtoa taarifa kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kama sharti la kurejesha hati hiyo.

Uchunguzi wa tuhuma hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwafuatilia na kuwachunguza maafisa wengine waliohusika ili wafikishwe mahakamani. Afisa huyo na wenzake wanakabiliwa na tuhuma ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007. 

Tunatoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kuripoti vitendo au viashiria vyovyote vya rushwa dhidi ya watumishi wasio waadilifu katika ofisi za TAKUKURU ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

IMETOLEWA NA RAPHAEL MBWAMBO- MKUU WA TAKUKURU MKOA WA ILALA 05/2/2016 


LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA RAUNDI YA 18 KUENDELEA WIKIENDI HII

$
0
0
Ligi Kuu ya Vodacoma Tanzania bara raundi ya 18 inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, Jumamosi ukichezwa mchezo mmoja na Jumapili kuchezwa kwa michezo saba.

Jumamosi ligi ya kuu ya Vodacom itaendelea kwa mchezo mmoja tu, ambapo katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, African Sports watawakaribisha Stand United kutoka mkoani Shinyanga.

Michezo saba itachezwa siku ya Jumapili ambapo maafande wa JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Young Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, na Ndanda FC watawakaribisha Mtibwa Sugar katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Kagera Sugar watacheza dhidi ya Simba SC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Azam FC watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa Chamazi, Majimaji dhidi ya Mgambo uwanja wa Majimaji mjini Songea na Toto Africans watawakaribisha Coastal Union uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA ASHIRIKI KUJADILI JINSI YA UDHIBITI WA MADAWA YA KULEVYA.

$
0
0

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. John Haule (Kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Mashariki mwa Afrika wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu, Bw. Jose Vila De-Castillo, alipotembelea Ubalozini, jijini Nairobi, jana. Bw. De-Castillo aliomba Ubalozi uwe kiungo kati ya Taasisi yake na Serikali ya Tanzania. 

Taasisi hiyo inaendesha mpango wa miaka mitano wa udhibiti wa rushwa, mitandao ya uhalifu, biashara na matumizi ya madawa ya kulevya, ujangili na biashara ya binadamu kwa nchi za Tanzania, Burundi,Comoro, 
Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Seychelles na Somalia. Kulia ni Ofisa wa Ubalozi, Bw. Mussa Haji.

MANISPAA YA ILALA KUJADILI BAJETI YA SH.BIL 55 KWA MWAKA 2015/2016

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

BAJETI ya Manispaa ya Ilala kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ni sh.bilioni 55 kutoka sh.bilioni 30 ya mwaka wa fedha 2014/2015.

Akizungumza katika baraza la madiwani katibu wa baraza hilo na Mkurgenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi amesema kuwa kutokana na bajeti hiyo kuwa juu madiwani wanatakiwa kufanya kazi katika kubuni vyanzo vya mapato.

Amesema kuwa baraza ndilo linaweza kufanya bajeti hiyo ikatimia katika makusanyo kutokana na vyanzo vya mapato vilivyopo au kuongeza vyanzo vingine.

Mngurumi amesema katika kuanza kufanya kazi kwa baraza la madiwani lazima kamati zipatikane ambapo hilo limefanyika kwa kufanya uchaguzi.

Aidha amesema kuendana na bajeti hizo kamati ziweze kujadili bajeti jinsi ya kuweza kupata bajeti itakayosaidia kuendesha na kutoa huduma kwa wananchi wa manispaa ya Ilala.

Meya wa Manispa kwa ya Ilala, Charles Kuyeko amewataka madiwani kujadili kwa kina bajeti hiyo katika kamati.
 Katibu wa Karaza Madiwani na Mkurgenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi akizungumza katika Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo, lililofanyika kwenye Ukumbi Arnatoglou, Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.
 Sehemu ya Madiwani wa Manispaa ya Ilala.

VIDEO YA LUPEZA YA ALI KIBA YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
VIDEO ya Lupeza ya msanii wa kizazi kipya, Ali kiba ambaye pia ni 

balozi wa WILD AID Afrika yazinduliwa jijini Dar es Salaam leo ikiwa wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya nchi walijitokeza kwa 
 wingi katika kumuunga mkono msanii na  balozi wa WILD AID Afrika, 


katika uzinduzi wa video yake hiyo.


Video hiyo iliyofanyiwa nchini marekani imezinduliwa katika Hoteli ya
Slipway jiji Dar es Salaam huku kiba akiwataka watanzania na walimwengu
kuachana na kujihusisha na ujangili wa kuuwa wanyama pori.


Baadhi ya wasanii waliojitokeza ni AT,  MwanaFA, Aika, Nahreel,

Vanessa, Jux,  Joh Makini, Wema Sepetu, Baraka Da Prince na wengine
wengi.
 Msanii na  balozi wa WILD AID Afrika, Ali Saleh ‘Ali Kiba’ akizungumza na wadau mbalimbali  (hawapo pichani) juu ya  uzinduzi wa video yake mpya ya Lupeza jijini Dar es Salaam.

 Wadu mbalimbali wakimsikiliza  Msanii na  Balozi wa WILD AID Afrika,Ali Saleh ‘Ali Kiba’katika uzinduzi wa video yake mpya ya Lupeza.jana jijini Dar es Salaam.

 Msanii na  Balozi wa WILD AID Afrika, Ali Saleh ‘Ali Kiba’akiwakabidhi CD wasanii mbalimbali na wanau wa muziki mara baada ya uzinduzi huo.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.

RAIS DKT. MAGUFULI AWATAKA WATU WALIOTELEKEZA MASHAMBA NA VIWANDA WALIVYOUZIWA NA SERIKALI WAVIFUFUE HARAKA IWEZEKANAVYO.

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images